Sio kweli chakula cha Rais lazima kipimwe kabla ya kuliwa

Taasisi ya Rais wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA nzito sana tusiichukulie poa kwa chuki zetu binafsi mkuu.
Kuna uwezekano uwezekano mkubwa sana hata ungekuwa Wewe katika nafasi ya bwana Humphrey Polepole ungefanya zaidi ya kumshikia Dafu Mh. Rais wa JMT.
Mkuu ule ni umbea na kujipendekeza kulikotukuka mwanaadamu anaefanana na ngedere huwa na tabu sana.
 
Mkuu ule ni umbea na kujipendekeza kulikotukuka mwanaadamu anaefanana na ngedere huwa na tabu sana.
Huo ni mtazamo wako mkuu.
Inawezekana wewe ungekuwa katika nafasi ya Polepole ungefanya zaidi ya huo umbea na kujipendekeza kulikotukuka. Kumbukeni makamanda mlipiga/walipiga Deki barabara ili mgombea Urais 2015 kupitia upinzani asafiri kwa wepesi. Kimtazamo wangu ule ndio Umbea na Kujipendekeza kulikotukuka mkuu. Ni hayo tu.
 
Vitu ambavyo Rais kabla ya kula lazima vipimwe Ni vile vya kupikwa kwa Mazingira Kama ya hotel Au event maalum kuepuka sumu Ila sio Kila anachokula lazima kipimwe



Mie kilichonifurahisha sio Rais kula dafu bali kiherehere Cha Humphrey Polepole kushikilia dafu wakati Rais anakunywa Maji ya dafu!


Watu tunajua Sana kuji pendekeza kwa Kweli

Na Gerson Msigwa kaiweka Kwenye page yake ya Instagram kuonesha maana ya Unyenyekevu kwa Mkuu wa Dola

Ila Pia Nimejifunza kitu Kuwa Ndugu Rais Magufuli huwa anatembea Na Fedha Mfukoni tofauti Na Jakaya ambae kuna Siku 2006 nusura adhalilike ambae akiwa Mtaa wa Samora ilipo NBC Samora akiwa Kwenye Ziara ya kutembelea zilizokuwa ofisi Za Idara ya Misitu alikatiza Ombaomba ambae akamuomba Fedha Na Jk bila ya hiyana akazama mfukoni akajipiga 'sachi' Sana akakosa pesa ndipo Mpambe wake akaokoa Jahazi kwa kutoa Za kwake Na kumpa Rais amabe akamkabidhi pale pale.
Vitu ambavyo Rais kabla ya kula lazima vipimwe Ni vile vya kupikwa kwa Mazingira Kama ya hotel Au event maalum kuepuka sumu Ila sio Kila anachokula lazima kipimwe.Hakipimwi mkuu wanaonjeshwa wapishi waliopika
Huu ndio ukweli mkuu,wanaobisha wabishe,niliona kipindi cha jakaya kule kigamboni kambi ya navy alikuwa anakuja breakfast na lunch,ikateuliwa kampuni ya catering kupika kwenye ile event,Kila mara usalama wanapita pita,muda wa chakula kupelekwa sehemu ya kulia chakula ulipofika maana haikuwa kiinaliwa mahali kilipopikiwa,wakati kinawekwa kwenye vyombo maalum vya buffet usalama walikuwa wanamuonjesha mkuu wa ile catering company kila chakula kilichopikwa.Ikafika Lunch utaratibu ukawa ule ule wakuonjeshwa!
 
lengo la kupima ni nini?

ilo dafu nani alijua atalila raisi hadi lipimwe ama kufanyiwa figisu za kumdhuru raisi.

oooh dafu hukaa siku 2 ivyo kusababisha tumbo kuuma, unaumwa wewe.

chakula kilicho andaliwa kwa ajili ya raisi ndio hupimwa sio kila alacho hupimwa
 
Huo ni mtazamo wako mkuu.
Inawezekana wewe ungekuwa katika nafasi ya Polepole ungefanya zaidi ya huo umbea na kujipendekeza kulikotukuka. Kumbukeni makamanda mlipiga/walipiga Deki barabara ili mgombea Urais 2015 kupitia upinzani asafiri kwa wepesi. Kimtazamo wangu ule ndio Umbea na Kujipendekeza kulikotukuka mkuu. Ni hayo tu.
Hapo ndo mnapokosea mimi sio kamanda wala mgambo.Huo ni umbea ha maofisini wapo wengi sana.Mimi sio kamanda wala hii mada sio ya polepole ila umbea wake umemponza halafu mimi siwezi kumnyenyekea binaadamu.
 
Kulikuwa na urongo unaenezwa chakula cha mh Rais lazima kipimwe tena lazima ale MTU mwingine kabla yake..

Magufuli amethibitisha sio kweli,km mnakumbuka alikula kwenye mgahawa mwanza,Jana kala dafu adharani bila kutest MTU wala kupimwa.

Mi najua madafu uwa yanakaaga wiku3 hayajauzwa na kwavile hayajakomaa maji yake yanavunda hivyo ni raisi kuumwa tumbo..ila mh hakujali ilo wala hakuwaza madafu ni ya lini..

Tuache kudanganyana acheni urongo urongo....

Sent using Jamii Forums mobile app
Usichukulie poa maswala ya ulinzi na usalama.
Kuna uzi humu JF kuhusua muuza madafu.. na pia kuhusu yule muuza mahindi aliyekujagundulika ni mlinzi wa Naibu Rais wa Kenya Bw. Rutto.
Uzi wa muuza madafu una hizi picha.
Majibu utajaza mwenyewe.
tapatalk_1546964640678.jpeg
tapatalk_1546964630131.jpeg
 
Hapo ndo mnapokosea mimi sio kamanda wala mgambo.Huo ni umbea ha maofisini wapo wengi sana.Mimi sio kamanda wala hii mada sio ya polepole ila umbea wake umemponza halafu mimi siwezi kumnyenyekea binaadamu.
Umbea wa Polepole ni nini hapo!?
Unyenyekevu wa binadamu ni moja ya nguzo bora sana maishani. Mwanadamu aliyekosa Unyenyekevu mara nyingi huwa amejawa na kutawaliwa na Kiburi, Ujuaji, Uzandiki, Unafiki, Ushirikina, Chuki, Wizi/Uporaji, Uzinzi n.k. Na Dini zote zinatufundisha tuwe WANYENYEKEVU.
 
Mdau aliyesema hicho kilikuwa hakijaandaliwa kwa ajili ya raisi yupo sahihi, kinachopimwa huwa ni kile kilichoandaliwa kwa ajili yake maana ndo rahisi kutumika kama njia ya kumdhuru lakini hichi cha mtaani hawezi wekwa chochote kwa sababu kinatumika na wote we unafikiri nani angejua kuwa atanunua dafu? Na hata kama atanunua atachagua lipi? Na kwa muuzaji yupi? So tutumie tu common sense

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taasisi ya Rais wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA nzito sana tusiichukulie poa kwa chuki zetu binafsi mkuu.
Kuna uwezekano uwezekano mkubwa sana hata ungekuwa Wewe katika nafasi ya bwana Humphrey Polepole ungefanya zaidi ya kumshikia Dafu Mh. Rais wa JMT.

Ni Kweli Hata Mie ningemshikia dafu Au Hata ku brush viatu Na sijaandika kwa Chuki Kama ulivyodhani nimeandika kuonesha modern mode of Slavery

Sio ngazi ya Rais Hata Ngazi ya Ukurugenzi wapo wanapokea Mabosi wao Mabegi wakishashuka Kwenye Magari japo sio Madereva wala wahudumu wa Ofisi

Bila ya Unafiki Maisha hayaendi vyema
 
Usilolijua ni kama usiku wa Giza ndugu.
Yule muuza madafu unafikiri ni hawa wauza madafu wa mtaani!? Rais wa JMT hawezi kula mtaani hovyo...system iko hivyo tokea kwa Rais wa Awamu ya kwanza.

Kuna picha zilishawahi zunguka humu JF zikimuonyesha jamaa mmoja aliyekuwa akiuza madafu mjini kumbe alikuwa ni mwanakitengo na sasa hivi anahudumu katika Chama tawala.
Kuna picha nyingine ilimuonyesha Makamu wa Rais Kenya Mh. W. Rutto akila mahindi ya kuchoma barabarani, yule muuza mahindi kumbe alikuwa ni mmoja wa walinzi wa Mh. Rutto na picha ziliwekwa akiwa kazini na Makamu wa Rais.
Umemaliza kabisa... kuna watu wanafikiri kuwa amri jeshi wa nchi ni mzaha.
 
Back
Top Bottom