Sio kosa kuoa wake zaidi ya mmoja

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Na. Robert Heriel.

Huwaga sipendi kutoa makala laini laini. Makala zenye Maneno matamu. Siku zote natoa mada ngumu zenye ukweli mchungu. Haijalishi nani inamgusa au vipi atajisikia. Ukweli mchungu ndio dawa ya magonjwa sugu.

Dini zenye asili ya abrahamu ambazo ni Ukristo, Judaism na Uislamu zote hazipingi Ndoa ya wake wengi ikiwa mtu atataka kuoa wake wengi.

Wapo baadhi ya watu huwafanya watu watumwa kwa sheria wanazojitungia wao wenyewe. Wanawaonea watu wanaopenda kuoa wake wengi kwa kuwaambia dini hairuhusu.

Ukiwaambia wakupe sheria isemayo hivyo wanambwela mbwela. Hawawezi kukupa na hawatakupa hata siku moja. Na hata wakikupa watakupa sheria isiyokuhusu wewe.

Sheria za ndoa hasa dini za kikristo inamzuia mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja. Hoja kubwa wanaoitumia ni kuwa Adamu aliumbiwa mwanamke mmoja hivyo Mungu alitaka watu waoe mke mmoja. Hii hoja ni mfu. Kamwe mtu mwenye akili hawezi kuitaja na kumuelekeza mtu mwenye nia ya kuoa wake wengi.

Mtu anayetaka kuoa wake wengi atakachohitaji ni kupewa sheria ya Mungu aliyosema usioe wake wengi. Ni sawa na mlevi wa pombe atataka umpe sheria aliyoitoa Mungu kuwa Usinywe pombe.

Kumbuka Biblia inavitabu kadhaa lakini kitabu pekee ambacho ndicho msingi wa neno la Mungu ni Sheria au torati. Vitabu vya Torari ni Kutoka, Kumbukumbu la Torati ba Mambo ya Walawi. Hizo ndio torati. Hivyo mtu akikutaza jambo kimsingi anapaswa atoe nukuu kutoka katika vitabu hivyo vitatu.

Vitabu vya mafundisho, Historia na unabii sio sheria wala haviwezitumika kumzuia mtu asifanye jambo na wala sio lazima mtu afanye mambo hayo. Kwa mfano kubatizwa sio sheria wala torati kumaanisha ni fundisho tuu ambalo mtu huweza kufanya au asifanye.

Kucheza kanisani sio dhambi wala sio sheria kwamba ni lazima. Hayo ni mapokeo tuu.

Tukirudi kwenye mada yetu. Kwenye Torati au sheria ambapo ni vitabu vitatu ambavyo ni Kitabu cha Kutoka. Kumbukumbu la torati na Mambo ya Walawi havimzuii mtu kuoa wake wengi.

Mtu wa kawaida anaouwezo wa kuoa wanawake anaowataka kwa kufuata taratibu maalumu tuu.

Mtu pekee anayeruhusiwa kuoa mke Mmoja ni Mchungaji, Askofu, Kuhani na watu wote wanaosimama kwa ajili ya kuongoza watu kwa Mungu.

Sheria inamtaka mchungaji au kuhani au Askofu awe na sifa hizi
1. Aoe mwanamke Bikra.
Mchungaji au Askofu ili akamilike na aeleweka kwa Mungu lazima aoe mwanamke bikra. Tofauti na hapo hana la maana wala la ziada. Ni kama mtu wa kawaida tuu. Mtu wa kawaida huweza amua aoe mwanamke yeyote bikra au asiwe na bikra.

2. Asioe mjane wala mtu aliyezalishwa.
Ndio maana akaambiwa aoe mwanamke bikra.

3. Awe mume wa mke mmoja.

Torati ya Musa aliyopewa na Mungu ndio inatanabaisha hivyo.

Hakuna Torati inayomzuia Mwanaume kuoa mke zaidi ya mmmoja. Ila zipo sheria zinazoelekeza namna mtu aliyeoa wake wengi atakavyoishi na wake zake. Kumaanisha inaruhusiwa.

Askofu na jamii za makuhani ndio wamelazimishwa kuoa mke mmoja tena sio hawa wanawake wa kawaida ambao hawana bikra bali awe na bikra.
Nanukuu hapo chini kwa habari ya Makuhani.
Mambo ya walawi 21;
13 Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.

14 Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.

15 Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye.

Kwa habari za mtu wa kawaida kuoa wake wengi biblia haijakataza. Bali imetoa ufafanuzi kwa watakao hitaji kuoa wanawake zaidi ya mmoja. Imetoa sheria ambapo kama imetoa sheria ni kwamba inaruhusu jambo hilo.

Nanukuu Kumbukumbu la torati 21;
15 Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa;

16 ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu;

17 lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.

Kuna mtu atasema kuwa Mpango wa Mungu ulikuwa mtu awe na mwanamke mmoja na sio wawili ndio maana alimuumba Hawa/Eva peke yake. Mtu huyo huyo akasahau kuwa Pia haikuwa mpango wa Mungu kumuumba mwanamke bali yeye alipanga kumuumba Mtu ambaye ni Adamu. Baadaye ndio akaona sio vyema Adamu awe peke yake atatafuta wa kumsaidia.

Mwanaume kama mfano wa Mungu anaouwezo wa kusema sio vyema mke huyu awe peke yake. Nitamtafutia wa kumsaidia ingawaje hakuwa na mpango huo. Mwanamke ili asiongezewe mke mwenzake lazima awajibike lazima awe na adabu na nidhamu. Lazima aonyeshe anajua kumudu kazi za nyumbani. Sio kusema hataki mke wa pili alafu hana anachojua. Kazi kupiga umbea vibarazani. Kazi kukifanya anamdomo kwa mume wake. Kazi kujifanya anataka haki sawa. Kazi anajifanya yeye ni mrembo kuliko watu wote hivyo anaweza kuleta ujeuri.

Mwanamke wa hivyo. Kuongezee mwenzake au fukuza aende kwao. Kama alivyofanya Mfalme Ahasuero kwa Malikia Vashti. Kisha akamchukua Malikia Esta.

Isaya anasema
Isaya 4;
Mlango 4
1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.

Aya hiyo ni unabii wa Isaya sio torati wala sheria. Isaya anabashiri kuwa zama zinakuja ambazo bila shaka ndio hizi kuwa wanawake mafungu mafungu watagombania mwanaume mmoja.

Yule mwenye kisu kikali ndiye mla nyama. Yule aliyemtiifu ndiye atakayekula nyama. Ukizingua unawekwa Sabu wenzako waendelee.

Andiko hili lisije likawa ndio kigezo cha baadhi ya wanaume wajinga kujiolea olea wanawake bila kuwa na akili wala uwezo wa kuwahudumia kimwili na kifedha.

Ni bora kuoa mke zaidi ya mmoja kuliko kufanya uzinzi wa kuchepuka chepuka kama Mbwa au nguruwe.

Wanawake na ninyi muwe na akili. Kuliko uwekwe makando kando ati mchepuko ukakosa haki na heshima kwa Jamii na Kwa Mungu ni Heri ulazimishe akuoe wala hakuna atakayekushangaa kutaka kuolewa mke wa pili.

Lakini watu wanakushangaa kuwa mchepuko ukiliwa kiporo na kufanywa kama kahaba. Kama mtu anakutaka na ameoa. Mwambie bila hofu kuwa nioe. Nipo tayari juwa mke wa pili lakini sio kuishi kama mtumwa.

Mara mke wangu yupo. Mara usinitumie text saa mbili. Yaani hata Kuku hawezi fanya huo upumbavu.

Ni wakati wa kubadilika. Sheria hazikatazi. Kama yupo anayesema zinakataza mwambie akufunulie torati akuonyeshe hiyo sheria.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
0693322300
 
Hupendi kutoa maneno malaini laini? Sasa haya ni magumu? Mi nayaona malaini tu. Yaani kama mashavu ya K.
 
Yaan nyuchi hizi sijui zina nini Yaan kuta kuchwa watu wanazipambania...
 
Mimi nadhani haya mambo ni utaratibu tu tumejiwekea kama wakristu. Siyo amri ya mungu. Kwa hiyo ni vyema kutofautisha amri na utaratibu..sheria na kanuni tunazojitungia hapa duniani.

Pale unapoona hukubaliani na kanuni fulani iwe kwenye kundi fulani, basi unajitoa. Hivyo wale wote ambao hawakubaliani na kanuni hii ya kikristo wanaweza kujitoa kuanzisha makundi yao au kujiunga na makundi yanayokubaliana na hicho wakitakacho
 
Back
Top Bottom