Sio kila mahusiano ni ya ndoa

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
Unapoingia katika mahusiano ya kimapenzi sio lazima yaishie kwenye ndoa. Mahusiano mengine yapo uli ujifunze jambo.Kuna migogoro, tabia mbaya, kila aina ya ubaya, uongo, kutoendana tabia. Haya yote yapo katika mahusiano. Kwaiyo ukiona uhusiano umevunjika jua kuna jambo unajifunza. Na lirekebishe ili uhusiano unaokuja uende vizuri.

Ukiwa kwenye mahusiano hata yakiisha usiumie sana. Huwezi kujua umeepuka na jambo gani.Kumbuka sio kila mwanamke niwa kuoa au kuolewa. Kuna wanawake wapo kwa ajili ya kuchezewa. Hawa ni wale dizaini ya wanawake ambao hata akimpata mwanaume mpole kiasi gani. Ataharibu na kwenda kwa mwanaume mwingine ba huko pia hata dumu.

Pia kuna wanaume sio waoaji hawa ni wale hit and run. Anakuja kustuka ana miaka 40 hana mtoto anaishi kisela. Pia hawa ni wanaume wa kuepuka. Mwanaume hajui kesho yake. Unajikosesha sokoo wakat kuna walio serious na wako tayari kuwa na wewe.
 
Nadhani kila anayeanza mahusiano awe na malengo na wakubaliane wote wawili, nje ya hapo ni kupotezeana na muda.
 
Ila katika kila mahusiano lazima muahidiane kuoana ndo yananoga.
Wengine wanaitana mume wangu na mke wangu kabisa… . very funy
 
Mahusiano ni kama maji hivyo wewe mwenyewe angali hii ladha yanirdhisha niendelee kunywa itanikata kiu au imetiwa chumvi hivyo bora niyaache mapema. By z way hakuna palipoandikwa kuoa na kuolewa ni lzm bali "'nendeni mkaijaze nchi na kuitiisha" na kuijaza sio mpk kuzaa hata uwepo wako wewe na kufa kwako kaburi lako limeijaza nchi
 
Sikuhizi hakuna waoaji wala waolewaji, Wote chenga tuu... Mapenzi yalikuwa Tanganyika Sio Tanzania...
 
Mahusiano ni kama maji hivyo wewe mwenyewe angali hii ladha yanirdhisha niendelee kunywa itanikata kiu au imetiwa chumvi hivyo bora niyaache mapema. By z way hakuna palipoandikwa kuoa na kuolewa ni lzm bali "'nendeni mkaijaze nchi na kuitiisha" na kuijaza sio mpk kuzaa hata uwepo wako wewe na kufa kwako kaburi lako limeijaza nchi
Duuuu!
 
Ukute sasa watu wanavyoitana, "mke wangu...mume wangu", Kumbe ni chenga tupu. Hapo kuna mmoja anapotezea tu, mda ukifika anachukua mwingine anaoa!!!
 
Back
Top Bottom