Nashukuru Mungu kwamba angalau Tanzania ya hoja kwa hoja inarejea taratibu.
Kumeibuka kundi la watu linaloshinikiza Mhe. Rais Mama Samia afikiri kama Hayati magufuli. Haieleweki vyema kwa nini wanafikiri hivyo ila kimsingi sio fair kabisa.
1. Mzee Mwinyi hakufikiri kama Nyerere, Mzee Mkapa Hakufikiri kama Mwinyi, Mzee wetu Kikwete hakutumia akili ya Mkapa, Hayati Magufuli hakutumia akili ya Mzee Kikwete, sasa kwa nini tufikiri Mhe. Rais Mama Samia anatakiwa kufikiri kama Magufuli? Sio fair kabisa yani.
2. Kila mtu huzaliwa na uwezo wake wa kipekee na 'purpose' maalum kwenye hii dunia. Kwa lugha nyingine, Mungu kamleta kila mtu kwenye dunia hii ili kutimiza jukumu fulani na amempa uwezo unaomuwezesha kutimiza jukumu husika. Ndio maana tunatofautiana busara, hekima, uvumilivu, uungwana roho nzuri na mbaya e.tc. Hivyo kutaka Mh. Rais Mama Samia afikiri kama Magufuli sio fair Kabisa!
3. Kila mtu huzaliwa 'original'. Hivyo ili mtu aache 'legacy' ni lazima abaki kuwa 'original' wakati wote. Kutaka Mhe.Rais Mama Samia afikiri kama Hayati Magufuli, ni kutaka kushinikiza asiwe 'original ' na hiyo sio fair kabisa.
4. Moja ya kitu kibaya sana duniani ni utumwa. Na utumwa mbaya zaidi ni wa kifikira, yaani kutumia misimamo ya mtu mwingine balada ya kutumia experience na utashi kufikia conclusion binafsi. Sasa kwa nini Mhe. Rais Mama Samia ashinikizwe asiwe anatengeneza conclusion kutokana na utashi na experience yake mwenyewe? Hiyo sio fair kabisa
Hitimisho;
Tumpeni nafasi Mhe. Rais Mama Samia afanye vitu kulingana na dhamira, experience na utashi wake. Afikie conclusion zake yeye kama yeye maadam havunji katiba, sheria au kudhulumu mtu. Huo ndio uungwana.
Mungu alimuweka Hayati Magufuli ili afanye aliyoyafanya na yatokee yaliyotokea kwa sababu maalum. Kadhalika, Mungu kamuweka Mama Samia kuwa Rais ili atimize 'role' fulani muhimu kulingana na mipango ya Mungu. Ni vizuri akapewa nafasi ili atimize 'role' hiyo, badala ya kumshinikizwa ageuke kuwa copy ya mtu mwingine. Huo ndio uungwana.
Katika kipindi cha uongozi wake, atahukumiwa kwa atakayoyafanya yeye kama yeye, ataacha legacy kwa yale atakayoyafanya yeye, na mbele ya Mwenyezi Mungu ataulizwa yeye kama yeye kuwa alichunga nini hapa duniani wakati wa uongozi wake.
Tuweni waungwana, tusimpotoshe Mama. Mama ni mtu mzima, mwerevu na muungwana. Aachwe awe yeye kama yeye maadamu havunji Katiba,sheria wala kudhulumu mtu.
Ramadhan Njema.