Sio dili, ni wajibu...

Sio dili, ni wajibu...

mickybaba

Member
Joined
Dec 30, 2014
Posts
50
Reaction score
34
Mzazi kumsomesha mtoto haipaswi kuwa uwekezaji unaosubiri faida siku moja. Watoto hawazaliwi kama mikataba ya kurejesha mkopo. Wanahitaji malezi bora, elimu na upendo—si kwa sababu watatulipa kesho, bali kwa sababu ni jukumu letu leo.

Mzazi anapaswa kutoa elimu bila masharti, na kulea bila matarajio ya kurudishiwa. Maisha hubadilika, si kila mtoto atakuwa na uwezo au nafasi ya "kulipa fadhila". Lakini kila mtoto aliyelelewa kwa moyo safi hujua thamani ya malezi, na atajitahidi kulipa kwa njia anayoweza—hata kama si kwa pesa.

Kama mzazi, acha moyo wako uwekeze katika utu, si matarajio. Fanya jukumu lako kwa upendo. Dunia ya kesho itakushukuru, hata kama si mtoto wako mwenyewe.
 
Attachments

  • 175196094141398769.jpg
    175196094141398769.jpg
    30.1 KB · Views: 18
  • 175196076479095713.jpg
    175196076479095713.jpg
    179.3 KB · Views: 17
Lakini kuwatunza wazazi pale wanapozeeka na kutojiwezani jukumu la watoto pia pale wanapokuwa japo si suala la lazima
 
Hiyo ni kwa wenzetu Ila kwa nchi zetu za kiafrika 😂

Nashukuru Mungu wazazi/walezi wangu hawana wanachonidai, kila siku hupenda kusema "sisi tumemaliza wajibu wetu tunachotaka kuona unaishi maisha yako na ndoto zako, sisi ukituombea Dua tu inatosha"
 
Elimu sio urithi.
Wazazi toeni na mali yoyote yaani kitu chochte kinachoshikika kulingana na UWEZO wako.
 
Yaani kuna wazazi wengine kama waganga hvi wanajua kuagiza tuuu...

Tuma hiki..
Tuma madaftari...

Sasa nashangaa sijui ujana wake yeye alikua anacheza ile nyimbo ya chee chee unapenda dezo dezo.. che che maisha yako dezo dezo...
 
Yaan ndo.mana ujana wangu wote huu nataka nipambana kwa hali na mali ili napokuja kutoa hao watoto niache kabisa habari za kuomba msaada kwao...
 
Lakini naelewa kwanini jamii kubwa ya kiafrika kusomesha au kulea mtoto ni deni ambalo mtoto lazima aje kulilipa katika siku za usoni.

Sababu kubwa jamii zetu nyingi tumekuwa kijumuia "extended family" unalelewa na mjomba shangazi n.k hivyo once unafanikiwa automatic unajikuta unalipa fadhila sio tu kwa wale waliokulea bali ni kwa wewe pia kubeba "mzigo" mwingine kwenye familia either kusomesha wadogo zako au ndugu wengine and the cycle keeps going.
 
Hiyo ni kwa wenzetu Ila kwa nchi zetu za kiafrika 😂

Nashukuru Mungu wazazi/walezi wangu hawana wanachonidai, kila siku hupenda kusema "sisi tumemaliza wajibu wetu tunachotaka kuona unaishi maisha yako na ndoto zako, sisi ukituombea Dua tu inatosha"
Una bahati sana, kibongobongo ukizaliwa tayali una deni la kurejesha.

Kukuzaa ni mkopo wa maisha inatakiwa umlipe mzazi.
 
Una bahati sana, kibongobongo ukizaliwa tayali una deni la kurejesha.

Kukuzaa ni mkopo wa maisha inatakiwa umlipe mzazi.
Jumlisha na deni la taifa 😂, BTW, I'm always grateful for my life.
 
Yaani kuna wazazi wengine kama waganga hvi wanajua kuagiza tuuu...

Tuma hiki..
Tuma madaftari...

Sasa nashangaa sijui ujana wake yeye alikua anacheza ile nyimbo ya chee chee unapenda dezo dezo.. che che maisha yako dezo dezo...
che che cheche kodi ya nyumba hulipi, maji yameshakatwa, oparesheni kata umeme inakuja...

che che cheche unapenda dezo dezo, pombe za bure hulipi, wewe bwana wee yatakushindaa..
 
che che cheche kodi ya nyumba ulipi, maji yameshakaywa, oparesheni kata umeme inakuja...

che che cheche unapenda dezo dezo, pombe za bure hulipi, wewe bwana wee yatakushindaa..
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Yatakushinda kweli aiseeeee

Et pombe za bure hulipuli.... We bwana weeeeee we bwana weeeeee we bwanaa weeee yatakushinda
 
Back
Top Bottom