Ilikuwa tarehe 25 mwezi wa 5 mwaka 2012 safari yangu ya kwanza kwenda South Africa, nikiambatana na dadaangu ni Mdogo kwangu tukielekea kwa madiba, tena ikiwa yeye dadaangu ndo mwenyweji wangu uko tuendako, japo yeye pia hajawahi kufika.
Lakini mchongo kaitwa na shemeji yangu ambae mimi, simjiu, lkn kwa maelezo ya dada yeye shemeji ananijua, na hata kwangu napoishi na Mdogo wangu alikuwa anakuja akiwa bongo na hata mke wangu anamjua, japo mimi na huyo mtu hatukuwahi kufahamiana.
Turudi nyuma kidogo, kwa kipindi hicho kabla ya safari, mimi nilikuwa nna ofisi ya ufundi wa simu mtaa wa Agrey Kariakoo na huyo dadaangu ndo nilimfanya mtu wa mapokezi, ofisini.
Siku moja ndio ananambia Kaka kuna shemeji yako anaishi South Africa ananiita niende, nikamuuliza unamjua vizuri, akaniambia sana mbona hata wifi anamjua (ambae ni mke wangu), kwamba akiwa bongo anakujaga home ki wizi.
Nikamwambia kwa kuwa yeye nimtu mzima Ana maamuzi yake, anavoona yeye kama inafaa aende tu maisha popote, basi jamaa akamtumia pesa ya passport na mambo mengine.
Wiki moja kabla ya safari dada akaniambia kaka sema kule nasikia kazi za ufundi simu zinalipa vizuri sana, nikamjibu nasikia pia, akaniambia ngoja niongee na jamaa kama vipi twende wrote.
Itaendelea.......