"Sintosahau Maishani"...!!

Mkuu Sizinga sometimes hizi mambo zinatokea bana..
Mie kinachoniuma ni pale unapofanya 'uungwana' kwa kufikiri demu atauona huo 'uungwana' wako ili akupe credit..
Kinyume chake unakuja kusikia kuwa kamegwa kwenye mazingira ambayo wewe uliyaona kuwa hayakuwa 'fair'..
Binafsi i got the same story like this and when i met the lady next day..she was laughing at me!..nilijiona mdhaifu sana aisee..
KUMBE NA WEWE dhaifu!!1 SnowBall
 
Last edited by a moderator:
NTOA MADA UNA MATATIZO NA HILI LINAWAKUMBA WENGI WA JINSIA YAKO,
1.HAKUWA DEMU WAKO
2.HUJAWAHI KUMTONGOZA UNAMEZA MATE TUUUU
3.NI RAFIKI TU KWANINI UUMIE VILE WEWE ANGEKUWA MKEO SAWA,DEMU WAKO SAWA!
4.KUMEGW MARA MOJA SIO SABABU UNGEMTONGOZA NA WEWE KWANI TATIZO LILIKUWA WAPI ALIENDELEA NA HUYO MKENYA ?KAMA HAWAKUENDELEA UNGEPIMA UCHUKUE MZIGO NA WEWE UMEGE 100%
HAINIINGII AKILINI KILICHOKUUMIZA MPAKA USISAHAU Sizinga INAMAANA MTU AKIMUOA DADA YAKO UTAUMIAEEEEEEEEE

Basi itakuwa naina matatizo kweli lakini kwanini anifanyie hivi infront of me...?? kwanini wasipange kivyao wakafanye huko wanakokujua?? Anyway imeshatokea.....akiolewa sista yangu haiwezi kuniuma dear!!
 
Usiumie sana, hapo ni mungu amekupigania mara tatu, kuna kitu alikuwa hataki ukutane nacho. Mara tatu hizo ni:
1. Ulipojifanya mustaarabu, ni mungu alikuongoza ili usimpate siku hiyo;
2. Mungu alimuongoza yule Boss wa Hostel awatimue pale kwa kisingizio cha Passport kwani mngelala pale tena lazima ungem-do;
3. Kitendo cha kupata hifadhi kwa jamaa zenu wa Kenya na demu kuchukuliwa na Mkenya, bado ni mungu alikuwa anakuweka mbali na huyo kicheche.
Usiumize sana moyo wako, kuna kitu God amekuepusha lakini unaweza usikigundue sasa hivi, ila baada ya muda fulani mbele ukapata picha halisi.
 
Nikiwa Chuoni mwaka wa pili, semester ya kwanza a.k.a semester ya 3, ilitokea classmate wangu wa kike alikuwa anafunga ndoa. Na mie kwakuwa nilikuwa foreigner nikawa wa kwanza kupata mwaliko kwenye ile ndoa. Nakumbuka tulikuwa kwenye free time tumerelax kichit-chat zaidi, kwa pembeni nimekaa na dada mmoja mrembo zaidi from A-Town, na alikuwa kivutio kwa kila anayemwangalia machoni, na alikuwa ni gumzo sana kwa wale wenye nchi yao (coz we were foreigners there)...

Nakumbuka hapo ndipo nilipoletewa mwaliko wa hiyo ndoa. Yule sista pale pembeni akawa anasikia ninavyopewa huo mwaliko na yule classmate!! Basi badae akaniambia nayeye angependa kufuataa na mimi kwenye ile ndoa. Na ile ndoa ilifanyikia mji mwingine umbali wa masaa 10 kwa treni ya umeme toka huo mji nilipo....

Kumbuka huyu mdada hakuwa na BF then, na hapo mwanaume nikajiona bahati iliyoje kwenda faragha na huyu dada huko kwenye ndoa, tukajipanga vilivyo na after 3 day tukaanza safari ya huko, bila washkaji kujua...

Nakumbuka ilikuwa majira ya saa 11 jioni tukiwa tunaingia mji mpya ambapo kwa siku 2 mbele ndipo kutakuwa na sherehe ya harusi...tukachukua tax tukaanza kutafuta hotel kwa ajili ya kujistiri(tulishapanda tukae hotelini kwa siku zote mpaka harusi ipite)...

Kwa haraka haraka tulienda hotel kama 3 hivi tukaambiwa zimejaa!! Hizi zilikuwa ni 3-star hotel. Tukajishusha tukaendelea kutafuta sehemu nyingine, lakini bila mafanikio, kwani baadhi ya hotel tulizopata wakihitaji passport na sie hatuzichukua kwahiyo ikawa ni inshu kulala kwenye hizo hotel, sanasana ni kutokana na matukio ya kigaidi na vitu kama vile...just rules!!

Ikawa imefika saa 3 usiku hatujapata sehemu ya kulala bado. Basi kwa bahati nzuri tukafika kwenye hostel flani kama zinavyojulikana wakatuambia rooms zipo wakatuuliza passport hakutkuwa nazo, sema mie nilikuwa na ID ya chuo ila nikiruhusiwa ila yule dada hakuwa na kitu chochote, hata copy ya ID hakuchukuwa ikawa ngumu kweli kupata room..ila yule jamaa akaturuhusu tulale pale coz ilkuwa tayari usiku!!

Taabu sasa ilianzia hapo!! Kumbuka huyu dada sikumtongoza lakini alionyesha feelings za kunipenda(na-declare interest hapa). Tukazama room tumepumzika story nyingi nk. Muda wa kuoga ulivyofika yule binti kaivalia khanga moko...ndembe-ndembe!! na mwanaume sikuona kingi kwa takribani mwaka nzima!! Kanipita kaenda kuoga, mi moyo unanienda mbio vibaya.

Baadae alivyotoka khanga imelowa vibaya, nikapiga moyo konde nikaenda kuoga na mie. Sasa ikawa naisoma akili yake, nikajipa moyo kwamba huyu dem SIMTONGOZI, kwani nikitongoza itakuwa nimeharibu mno, coz tutalala litanda kimoja then mi kwangu haitakuwa kazi...ni kuvuta ungo tu na kuweka pepeta!!

basi nilivyotoka kuoga tukaingia kitandani kulala....LOL, binti yule kweli kaumbika ma mie moyo wangu unaeenda kasi vibaya mno!!...nakumbuka usiku nzima ulipita sikumgusa yule dada na wala hata mie sikulala, nikajipa moyo kwamba usiku ujao wa kesho yake hapo lazima nimletee ununda tu huyu binti, I mean lazima kieleweke!!

Basi ile asubuhi tumeamka vizuri,tumejiandaa freshi kwenda kunywa chai,ghafla tunasikia mlango unagongwa, kufungua tunakutana na muhudumu anatuambia tunaitwa na bosi receiption, tukashuka ngazi tukaenda. Yule bosi akatumabia hatupati tena admission mpaka tupeleke copy za passport, kama hatuna tuondoke...Dah....tukawa hatuna jinsi, tukaenda kuchukua virago vyetu tukaondoka.

Sasa kwa jana tulitafuta sana room tukakosa..tukawa hatuna tena hamu ya kutafuta hotel, option iliyokuwepo ni kwenda kwa rafiki zetu wa kikenya walikuwa wanakaa nje kidogo ya mji. tukawasiliana nao kweli tukaenda.
Usiku ulipofika mie nikapangwa nilale kwa mshkaji flani hivi na yule demu alale kwingine. Hili ndilo kosa nililolfanya mpaka nimeandika hii story hapa.

Yule demu alilala na mshkaji flani mkenya ambaye wakati tupo mwaka wa kwanza alishawahi kumtongoza. Dah...hali ilikuwa mbaya sana usiku ule, sikulala tena ule usiku, nilikuwa frustrated sana!! Nakumbuka nilijipa .... kama 3 hivi that night...na nakumbuka kama ningekuwa na kisu ningewaua hawa wote kwa kitu walichonifanyia...(Mungu aliepusha hii).

Ile asubuhi nikaenda hadi room ya mshkaji(mkenya) nikawakuta amemuandalia chai,mayai mazito na mapokopoko mengine...iliniuma sana!! Kiufupi Jamaa alikuwa tayari ashamega mzigo( 100% sure). Na hata kwenye ile Ndoa sikwenda tena!!
Hali hii ilinipelekea semester ya 3 kusup sana masomo yangu(supplimentary). I was totally confused na nilifanya bifu kubwa sana na yule dada na karibu chuo kizima walikuja kujua hii kitu...dah hii siwezi kuisahau kabisa kwenye maisha yangu....

lakini Mungu mkubwa, hai ilirudi ikwa sawa, na nikasema siwezi tena kuweka bifu na mwanamke yeyote, its waste of time by the way...!!

Je wewe ni story gani ambayo huwezi kuisahau maisha yako....ningependa ziwe stori za namna hii, zisiwe za misiba na vifo.

My Regard!!

2i9m911.jpg

jidhjp.gif

umenisikitisha na kunifurahisha..pole sana kijana..
 
Agrrrrr sema hukujua yatakayotokea,ungejua mbona hata usingempeleka kwenye hiyo harusi,nisote naye kwenye mahoteli na kila option ananitegemea hata mwaliko nimealikwa mimi,kumbe unamwandalia mazingira mwingine amege.
 
chelewa chelewa mwana si wako,uswahilini mtu unapiga sound hapo hapo halafu mnapanga hapo hapo kucheza game,mpaka mwezi uishe umeferenga kijiji kizima halafu aje kuku wa kisasa unamwangalia tu,we vipi bhana.
 
Usiumie sana, hapo ni mungu amekupigania mara tatu, kuna kitu alikuwa hataki ukutane nacho. Mara tatu hizo ni:
1. Ulipojifanya mustaarabu, ni mungu alikuongoza ili usimpate siku hiyo;
2. Mungu alimuongoza yule Boss wa Hostel awatimue pale kwa kisingizio cha Passport kwani mngelala pale tena lazima ungem-do;
3. Kitendo cha kupata hifadhi kwa jamaa zenu wa Kenya na demu kuchukuliwa na Mkenya, bado ni mungu alikuwa anakuweka mbali na huyo kicheche.
Usiumize sana moyo wako, kuna kitu God amekuepusha lakini unaweza usikigundue sasa hivi, ila baada ya muda fulani mbele ukapata picha halisi.

Aiseee!! Umeweka vizuri hizo points zako!! Unajua nini baada ya kuendelea na maisha yule dada alikuwa hatulii kabisa mazingira ya Chuo kila siku ni safari na kurudi ni after some weeks/days, na ikasemekana alikuwa na washkaji wengine kwenye miji mingine huko...dah
I like your points broda!! Now I can say Thanks God...for avoiding that person!!
 
umenisikitisha na kunifurahisha..pole sana kijana..

Salito..kama umefurahi, Im happy too, coz I knw you learn somthing here!! Usisikitike sana kwani yameshapita, na maisha yanaendelea kama kawa, ila hawa wadada ni kuwa waangalifu tu always!!
 
Agrrrrr sema hukujua yatakayotokea,ungejua mbona hata usingempeleka kwenye hiyo harusi,nisote naye kwenye mahoteli na kila option ananitegemea hata mwaliko nimealikwa mimi,kumbe unamwandalia mazingira mwingine amege.

We yaani acha tu...ndio maana najiuliza kwanini afanye hivyo vitu mapachoni pangu ilhali mie ndio nilimdahamini kwenye ile safari, nikamchukulia powa, lakini badae akanifanyia usen..... yaani 99 hapa palikuwa pagumu sana kuwa stable....anyway.

chelewa chelewa mwana si wako,uswahilini mtu unapiga sound hapo hapo halafu mnapanga hapo hapo kucheza game,mpaka mwezi uishe umeferenga kijiji kizima halafu aje kuku wa kisasa unamwangalia tu,we vipi bhana.

Sasa hapa mbona unaniponda tena we mswahili....hahaaaaa...ndo hivyo bhana sikuwa uswahilini broda
 
Ohh AD...thankx mama!! nimeshapoa...lakini mzima wewe? muda mrefu sijakuona huku, usharudi homiz?? Mc ya!!

hahahahahahahahah nilidhani msichana wa Arusha unae muongelea ni mimi hahah lol..:)
Mi sijambo kabisa my dear , nimebanwa tu na "kama unavyojua" lolz ... dahhh kitambo
kweli hatujaongea bado uko kule mitaa ya juu????????? na unaendeleaje?
 
Ngoja nikuPm manake huku mmh....kuna wenyewe..si unajua ya Mungu mengi...ila nyie wasichana wa A-town mmhhhh....hivi kwanini mkiulizwa mnajibu mi ni Muarusha?? Sijawahi kusikia mnataja kabila lenu mkiulizwa...

Bt luckly enough most of them are beautiful.....hahaaa
 
We yaani acha tu...ndio maana najiuliza kwanini afanye hivyo vitu mapachoni pangu ilhali mie ndio nilimdahamini kwenye ile safari, nikamchukulia powa, lakini badae akanifanyia usen..... yaani 99 hapa palikuwa pagumu sana kuwa stable....anyway.

Sasa hapa mbona unaniponda tena we mswahili....hahaaaaa...ndo hivyo bhana sikuwa uswahilini broda
ila kuna situations ambazo hazina mjanja,sometimes unaweza kumheshim dem na kumwandalia mazingira mazuri ila wengine wanajimegea tu popote.
 
Ngoja nikuPm manake huku mmh....kuna wenyewe..si unajua ya Mungu mengi...ila nyie wasichana wa A-town mmhhhh....hivi kwanini mkiulizwa mnajibu mi ni Muarusha?? Sijawahi kusikia mnataja kabila lenu mkiulizwa...

Bt luckly enough most of them are beautiful.....hahaaa

labda tunasema "Muarusha" sababu ndo tumetoka huko..
ahhhhhhh mi napenda kabisa kusema kabila langu...

anyway rudi chumbani nimekujibu ...
 
labda tunasema "Muarusha" sababu ndo tumetoka huko..
ahhhhhhh mi napenda kabisa kusema kabila langu...

anyway rudi chumbani nimekujibu ...

Haya bhana...nisharudi nimekukuta umejaa tele....Im complishin smthng...just few min ahead
 
Aisee sisi wanawake sometimes tuna matatizo, hivi mtu anakubali kudo na yoyote tu ili mradi chance imepatikana??khaaaa!
 
Aisee sisi wanawake sometimes tuna matatizo, hivi mtu anakubali kudo na yoyote tu ili mradi chance imepatikana??khaaaa!

Lakini purple sio wadada wote wako hivyo...ni hulka na tabia za mtu...differs always, ila wasiojitambua huwa hivyo...vicheche
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom