Sintaksia finyizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sintaksia finyizi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ustadh Mtu, Dec 2, 2011.

 1. Ustadh Mtu

  Ustadh Mtu New Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwamba sintaksia finyizi imekubalika na wataalam wengi kama nadharia ya ya lugha yenye uwekevu zaidi na bado inaendeleza malengo ya sarufi zalishi. Malengo haya ni kuandaa sarufi bia ya lugha ya mwanadamu pamoja na kutafuta uhusiano na taaluma nyinginezo za lugha kama vile fasihi, isimujamii miongoni mwa mengine. Hata hivyo, matumizi ya nadharia hii iliyoanzishwa na Noam Chomsky inahitaji kufafanuliwa kwa udhahiri zaidi na wanaisimu wa Kiswahili.
   
 2. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Unaleta maada ya lugha mpya ilhali hii ya kiswahili hatujaijua, tufundishe kiswahili kwanza.
   
 3. Ustadh Mtu

  Ustadh Mtu New Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio tofauti na Kiswahili tulichokizoea ila ni hatua yenye kuzama katika uchanganuzi wa sentensi kama inavyoangaliwa kipindi cha sasa na wasomi wa lugha, yaani wanaisimu. Isimu ikiwa ni sayansi ya lugha.
   
 4. k

  kassimamari New Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kasumba kubwa tu iliyojikita juu ya dhana ya kukitumia kiswahili kwa mawanda katika fani ya elimu na masuala mtambuka ya nchi juu ya utawala.Kasumba hizo zinakwaza kwa kiasi kikubwa hali ya kiswahili kuzidi kushika kasi ya kukua na kuenea duniani.Kila nchi iliyorazini inatoa kipaumbele zaidi katika kuhakikisha inaifanya lugha yake kuwa na muwaa kitaifa na kimataifa.Wakati wa kubadilika ni huu kwa kuwa sintofahamu inayoikabili juu ya lugha ya kiswahili itumike katika elimu au la kama lugha ya kufundishia imekuwa ni kitendawili kikubwa sana kilichokosa jibu la uhakika.Wazalendo wa lugha hii ni lazima tuoneshe mfano kuwa inawezekana kabisa kuanzisha shule za mfano za kiswahili kuanzia ngazi ya msingi hadi kidato cha sita na wanafunzi wakasoma kwa kiswahili vizuri na kufaulu kwa kiwango kikubwa tu.
   
 5. MSARO

  MSARO Member

  #5
  Oct 9, 2015
  Joined: Nov 26, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Ustadhi Mtu samahani naomba unielezee kwa upana zaidi maana ya sintaksia finyizi pamoja na malengo yake vilevile kama kuna chanzo kizuri ambacho naweza kusoma nijulishe ili niweze kuandaa wasilisho; email lawigodwin@yahoo.com phone 0725537036 au 0786012901(Tanzania) asante
   
 6. K

  Kifyatu JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2015
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,831
  Trophy Points: 280
  Nadhani Ustadh Mtu hapa anaposema sintaksia finyizi anamaanisha linguistics - ndipo Noam Chomsky alipojikita.

  Wataalamu wa lugha wanafahamu kuwa linguistics ni sawa sawa na physics ya lugha. Inachambua misingi (building blocks) ya lugha (kiswahili, kuzungu, kimakonde, au lugha mpya inayoanza leo). Ni fani moja nzuri sana iliyotuletea grammar checkers, google translators, nk.

  Mkuu Ustadh Mtu kama uko kwenye fani hii basi jikite sana. Bado tunahitaji wataalamu kama nyie kwa sababu tafiti zimebaki nyingi sana na huwezi kufa njaa ukiwa na taaluma hii.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...