Shenkalwa
JF-Expert Member
- May 3, 2011
- 580
- 132
Salamu zangu natoa kwa wana Magwanda, ambao hutoa kauli kanjanja
Ni watu sio makini zaidi ya ukanda , ambao dini kwao iko kwenye kiganja,
Magwanda ni mafukara wa kwanza, kwa hoja zao zisizo makini
Magwanda si chama cha siasa, bali ni wanaharakati kanjanja
Nayasema haya kwa umakini na weledi, watanzania ni mashahidi
Magwanda hawajali amani ya nchi, bali matumbo yao na umaarufu
Ni watu wahuni na si makini, wenye kujitafutia wao umaarufu
Magwanda si chama cha siasa, bali ni wanaharakati kanjanja
Hili somo tunawapa kama funzo, ili wao nao wajifunze
Amani ya nchi hii tuitunze, utulivu nao tuutunze,
Acheni ubaguzi wa kidini , na muwe wanaharakati makini
Magwanda si chama cha siasa, bali ni wanaharakati kanjanja
Ukisoma haya ndiyo utaona hali halisi ya mtanzania na hasa kichwani kwake. Huyo anayetuandikia hivyo jana usiku hakula kwa maana kwamba hakuwa hata na hela ya kula kalala na njaa. Wazazi wake huko kijijini pia hawajala hata hela ya kununulia mafuta ya taa (ya kibatali) hawana. Amelala kwa kamshumaa ambako kameshaisha hata leo hana cha kuwasha maana nchi iko gizani. Hakuweza hata kuangalia ka-tamthilia kupitia luninga kwa jirani maana nchi iko gizani. Leo asubuhi amefika kijiweni kwake hawezi kufanya kazi bila umeme matokeo yake amekaa ameduwaa na hajui mchana huu atakula nini. Mkombozi wake mafuta ya taa angalao ya kuwashia jiko la mchina sasa hayatanunulika kwa sababu yameongezwa bei kama mafuta ya gari ili kuwakomoa mafisadi wachakachuaji wa dizeli na petrol. Hapo alipo anawaza bei ya maharage, sukari, dagaa, sembe, nakadhalika nakadhalika bila kusahabu kodi ya mwenye chumba, madeni mpaka utosini, ka ada ka kijana na kale kahela ka kamtihani, nakadhalika nakadhalika. Na kamshahara kenyewe anakachukua leo kaishaisha hata kabla ya kufika nyumbani. Yote yaho na mengine anaona badala ya kujitundika aandike hiyo ngonjera hapo juu aimbe na kucheza ili kujisahaulisha na mawazo. Watanzania tumefikishwa mahali patamu kweli kila mtu abebe sehemu yake.