Single mpya ya CHADEMA hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Single mpya ya CHADEMA hii hapa

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by GeniusBrain, Jun 29, 2011.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Salamu zangu natoa kwa wana Magwanda, ambao hutoa kauli kanjanja
  Ni watu sio makini zaidi ya ukanda , ambao dini kwao iko kwenye kiganja,
  Magwanda ni mafukara wa kwanza, kwa hoja zao zisizo makini
  Magwanda si chama cha siasa, bali ni wanaharakati kanjanja

  Nayasema haya kwa umakini na weledi, watanzania ni mashahidi
  Magwanda hawajali amani ya nchi, bali matumbo yao na umaarufu
  Ni watu wahuni na si makini, wenye kujitafutia wao umaarufu
  Magwanda si chama cha siasa, bali ni wanaharakati kanjanja

  Hili somo tunawapa kama funzo, ili wao nao wajifunze
  Amani ya nchi hii tuitunze, utulivu nao tuutunze,
  Acheni ubaguzi wa kidini , na muwe wanaharakati makini
  Magwanda si chama cha siasa, bali ni wanaharakati kanjanja
   
 2. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesharudi eenhe!!
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Pole sana GeniusBrain, naona akili yako haiko makini
  Nguo yako ya kijani, haina tena thamani,
  Gamba limewakaa kichwani, huku jokakuu likiwa safarini,
  CCM bado mko ndotoni, CHADEMA wako mbioni kukomboa nchi.
   
 4. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii single underground, hata redioni haitopigwa
   
 5. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mikukuta inajulikana humu.
   
 6. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mnyika, dr slaa, mbowe, kitila et al
   
 7. M

  Michelle Hilton Senior Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  asante ndgu cdm mpooooo
   
 8. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,979
  Likes Received: 20,366
  Trophy Points: 280
  Singo yako imekaa kikuda kama sharo anayepakatwa
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  single zenu mnazo kibao mnajishaua tu
  umeme hakuna
  maji hakuna
  vitu bei juu
  shule duni
  hospitali duni
  chama kimejaa ufisadi tupu
  viongozi wanachekacheka tu wakati wowote
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Aaah 0 Brain punguani wa uswahilini,mtoto wa muuza vitumbua kutwa kucha unashinda kwenye Gahawa,
  UBONGO WAKO UNAFIRIA KWA %0.5 yaani ni sawa na kichwa cha kuku muda wote ni kuwaza pumba tu,aliye kupa hiyo kazi nadhani nae atakuwa na %0.9 mnazidiana kidogo tu,WAPE SAALAAM KIJIWENI.
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Yaani Nape anazidi kuajiri misukule yake tu, kweli magamba mna hela za kuchezea.
   
 12. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kweli watu wa magamba ni waajabu sana. katulia na kupoteza muda wake kuandika huu upupu kisa Nape aone mchango amuingize katika paylist. Mmezoea kuishi kwa dhuluma nyie ndio maana mnamuogopa Dr Slaa kama ukoma, akitoa tamko tu bosi wenu JK anatekeleza haraka. Mnakosa usingizi kabisa, jamaa amewakaba kila upande... Bungeni hampumui, mitaani maandamano, usiku giza mnalala saa mbili, kudadeki mwaka wenu huu wana Magamba mtakiona cha moto.
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  U must b in toilet or all the way from there!
   
 14. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Utu si ubinadamu, mshairi ninasema,
  Utu ni jambo adimu, wengi wameshauhama,
  Viumbe ni binadamu, lakini utu lawama,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.

  Utu si ubinadamu,itazameni kalima,
  Utu ni kitu adhimu, Mola wengi kawanyima,
  Utu wataka Halimu, na kubwa ndani hekima,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.

  Utu ya juu nidhamu, utadhani ni karama,
  Utu ya haki hukumu,bila kugwaya uhasama,
  Utu adili nadhimu, uadiifu wa dawama,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.

  Utu ni kutakadamu, mwenendo na tabia njema,
  Utu ni uislamu, fundisho mpaka kiyama,
  Sio wote wanadamu, utu wapewa heshima,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.

  Wapo vinara hakimu, viongozi wa heshima,
  Kadhalika wanajimu, nyota waliozisoma,
  Ila utu madhulumu, hawana cha chini kima,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.

  Wapo mashehe na walimu, na mapadri waadhama,
  Jichoni ni binadamu, kubwa twawapa heshima,
  ila nakisi yadumu, utu kwao umehama,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.

  Twawaona binadamu, utu vipofu nasema,
  Utu sio la ghanimu, wala kwa cheo kuvuma,
  Maskini huwa rahimu, malaika kumpema,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.

  Mtoto huufahamu, mkubwa kutokuusoma,
  Mjinga huwa karimu, mwenye akili kuzama,
  Nisai huwa hirimu, rijali akachutama,
  Utu si ubinadamu, wanasiasa watupoteza.
   
 15. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ukitaka kujua thamani ya magwanda na kijani we vaa kijani na suruali nyeusi na mwingine avae magwanda wote mtembee mtaani uatona jinsi utakavyo zomewa na raia kukushangaa kweli kweli mpaka utatamani kuvua
   
 16. tozi

  tozi Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wewe hauna kazi za kufanya nenda kwenu ukalale toa mchango kuhusu maendeleo ya nchi si kuropoka na kuleta ubwanyenye hapa
   
 17. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hongera malenga wa wiki. au hii ni bongo fleva?
   
 18. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wapashe Genius-Brain, CHADEMA wanahaha sasa. Mbunge wao wenyewe wa Maswa Magharibi anawaendesha bungeni.
   
 19. T

  The GreatMwai Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaazi kweli kweli.
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Weeee, hebu pata kitu hiki.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...