Single mother's ujumbe wenu mzuri huu apa

Ocran

JF-Expert Member
Jun 29, 2017
1,045
1,352
Picha hii ilipigwa mwaka 2013 katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara, nchini Kenya na mpiga picha za wanyama (wildlife photographer) Alison Buttigieg, na ilishinda kuwa picha bora ya mwaka katika tuzo za habari huko Australia.

Swala huyu anayesulubiwa na chui hawa, ni Mama wa watoto wawili. Akiwa na wanae kwenye maskani yao, walivamiwa na chui waliokuwa na njaa. Watoto wake walikuwa wadogo na hawakua na nguvu za kuweza kukimbia na kujiokoa. Mama yao angaweza kuaamua kukimbia na kuwaacha wanae ambao wangeweza kuwa chakula cha chui.

Lakini hakuwaacha alikimbia nao. Baada ya umbali kidogo akaona chui wamemkaribia. Akaacha wanae waende na yeye akapunguza mwendo. Alitaka kuhakikisha wanae wanakuwa salama hata kama yeye atadhurika. Chui wakamfikia na kumparamia.

Katikati ya chui wawili bado aliweza kusimama wima na kuwatazama wanae ambao walikuwa wakizidi kuyoyoma porini. Alikuwa akiwatazama kwa mara ya mwisho maana alijua hatawaona tena!!! Ilikuwa ishara ya kuwaaga.

Kwa macho yenye ujasiri aliwaaga wanae. Aliwakodolea macho hadi wakapotelea kabisa porini kabla ya kukubali chui kumgeuza chakula. Alihakikisha kitu cha mwisho kuona kwenye macho yake ni taswira ya wanae. Ilikuwa ni ishara ya kuwaaga. Alijua hatawaona tena, lakini hakusikitika maana alijua kifo chake kilikua ukombozi kwa wanae.

Picha hii inatuonyesha taswira halisi ya Upendo wa Mama....picha hii ni maalum kwa wanawake wote mnaolea watoto peke yenu..msiogope..Mungu yuko nanyi..pambaneni..#singlemamaseries coming soon..
38ecb661e02dc2517fe91f76afb4da6d.jpeg
 
Kwahiyo sisi wanaume ndiyo chui?

Tunaongeza changamoto kwa single motherz badala ya kuwasaidia?

Huu ujumbe ulipaswa uwalenge jamii nzima na siyo kundi la watu wachache. Maana suala la kulinda watoto lipo kwetu sote.

Au wewe unaonaje?
 
Kwahiyo sisi wanaume ndiyo chui?

Tunaongeza changamoto kwa single motherz badala ya kuwasaidia?

Huu ujumbe ulipaswa uwalenge jamii nzima na siyo kundi la watu wachache. Maana suala la kulinda watoto lipo kwetu sote.

Au wewe unaonaje?
Kweli kabisa ila akina mama hujitoa sana kwa watoto wao, kuna wakati sisi wanaume huwa hatujali kabisa muhimu nasisi tuwe na karibu na kuwafariji na sio kuwaponda, naona vijana wengi humu wakiwakashif sana hawa single mother lakn hawajui chanzo chakua ivyo ni nn.
 
Wengi wako hivo kasababu ya mapenzi ya dhati waliyokuwa nayo kwa wapenzi wao na hivyo kuamua labda nikimzalia itakuwa zawadi nzuri na atanioa. Kinyume na matarajio mwanaume anakuwa hapendi hicho kitu na mwisho wa siku anabaki kuwa single. Lakini cha ajabu, Mungu anawatetea mno hawa watu, pamoja na changamoto ya kuwa alone, God is always with them. Akiomba chochote, Mungu anamjibu fasta hasa akifahamu kuitumia hiyo fursa na kuacha kulalamika.
 
single maza hawahawa ambao ukiwanyima hela ya matunzo ya mtoto wa mwanaume mwenzio wanakuchukia kama nyoka
 
Single mother nimama zetu natunawapenda Sanaa.....

Dedicated song kwamama zetu 'upendo wamama wahali yajuu' sikumbuki muimbaji ila nimdada
 
Back
Top Bottom