Single mother ukifanya hivi utaweza kuolewa

Single mother ukifanya hivi utaweza kuolewa

Baba yenu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2016
Posts
1,053
Reaction score
1,418
Malalamiko ya single mother kuwa majanga ukiwaoa yameongezeka sana but naomba niwape ukweli na kuwasaidia

Kwanza hata mseme kuwa hampashi vipolo na wazazi wenzenu au mseme hilo wanalifanya wajinga ni kujidanganya kwa sababu yawezekana kweli hampashi vipolo lakini bado mna mawasiliano na wazazi wenzenu mkitumia kigezo cha mtoto na hilo ni kosa kubwa sana! Hakuna binadam anayeweza vumilia kuona laaziz wake akiwa na mawasiliano na mtu mwingine tofauti kirahisi tu na aone sawa!! Tena mtu mwenyewe walishawahi kufanya sex!!!! Haipo hiyo!!

Lafiki yangu alishawahi vunjikiwa ndoa mbili kwa sababu alikuwa ana watoto nje na alikuwa anawahudumia tu ila zile simu na mawasiliano na wazazi wenzie zikawashinda wanawake aliowaoa na hiyo ni kitu cha kawaida

Solution:- lazima mmoja kati yenu akubali kumpoteza huyo mtoto mpaka ukubwani

Mfano! Mimi nina mtoto tayali wa nje ya ndoa nilimpata nikiwa kijana,nilichokifanya kuepuka haya majanga ya mzazi mwenzangu ni kukaa na familia yake nikawapa fact za mawasiliano yetu yanavyoweza kuathiri ndoa zetu za badae na nikawapa sharti kuwa ni lazima mtoto amilikiwe na mmoja kati yetu jumla mpk atakapokuwa mkubwa,,,kama wanabaki nae wao siruhusiwi kupiga simu wala kumuulizia mpk atakapokuwa mkubwa anitafute na siruhusiwi kuchangia hata 10 ya makuaji yake au aje kwangu na wao wasipige simu wala kuulizia chochote juu ya mtoto nitake full responsibility mpk atakapokuwa mkubwa akitaka kumjua mamake ndo nimpeleke.

Sharti langu likawa gumu ila hatimae likafikiwa mwafaka nikawalipa gharama za malezi tangu akiwa mdogo mpk umri ule ingawa nilikuwa nawatumia pesa tangu alipozaliwa baada ya hapo nikakabidhiwa mtoto jumla.
Miaka mitano imepita no calls, hakuna anayeuliza chochote na hairuhusiwi na hii inasaidia niliyenaye asiwe na presure yoyote juu ya mama yake mtoto kuwa labda tunapiga vipolo wala nini.

Hii njia anzeni kuitumia itawasaidia jaman ni either u loose or upate!! Ila inabidi uwe na roho ya kijasiri sana. Lakini mkiendelea kuruhusu mawasiliano na ma ex kisa eti mtoto mtaendelea kukimbiwa na wanaume na kuonekana hampaswi kuolewa milele
 
Mtoto anatumia ubin wako? Hii ni nzuri mkielewana lakini familia nyingine ukiwaeleza hayo watakwambia mwisho wa mwezi babu au mjomba wa mtoto atafuata matunzo ofisini.
 
Mtoto anatumia ubin wako? Hii ni nzuri mkielewana lakini familia nyingine ukiwaeleza hayo watakwambia mwisho wa mwezi babu au mjomba wa mtoto atafuata matunzo ofisini.
Mnataka mbaki na mtoto basi sitoi hata 10 kwa sababu mnaweza kumtunza! Hamtaki nipeni na siwaombi hata 10 lasivyo leta huyo mjomba nimuoneshe ntakachomfanya hatarudia kukanyaga ofisini
 
Huyo mama kweli umemfanya asijue juu ya mtoto wake, una roho mbaya sana ndugu. Mungu aepushe wanawake mwanaume kama wewe. Haujiamini ndio maana na nahisi unampenda kiaina huyo mama mtoto.
 
Inferiority complex
Nakupenda wewe sasa hivi Huyo mwingine hana nafasi

Jiamini babaa....!!
 
Huyo mama kweli umemfanya asijue juu ya mtoto wake, una roho mbaya sana ndugu. Mungu aepushe wanawake mwanaume kama wewe. Haujiamini ndio maana na nahisi unampenda kiaina huyo mama mtoto.
Hahahaha una haki ya kuniona nina roho mbaya ila nilichokifanya ndicho kinachonipa aman katika ndoa ya sasa na ningefanya unavyotaka wewe ningeshaachana na niliyenaye kwa sababu hizo hizo za kisingle mother mnazozipigia kelele
 
Inferiority complex
Nakupenda wewe sasa hivi Huyo mwingine hana nafasi

Jiamini babaa....!!
Ndo unavyojidanganya but atlast ndoa huvunjika!! Hesabu ndoa za single mother zinavyovunjika kila wakati unajua sababu? Ni kuruhusu mawasaliano kisa mtoto! Why wazaz hawaruhusu kuoa single mother? Ni kwa sababu kuna mawasiliano na mzazi mwenzie
 
Hii si njia sahihi huko ni kumuharibu mtoto kisaikolojia.

Kama yupo kwako baba mpe masharti mama wa mtoto ni marufuku kunipigia simu kama unataka kuja kumuona mtoto njoo nyumbani au mpe namba ya mkeo(wajenge urafiki) ila katu asiwe wa kuwasiliana na wewe.

Kama yupo kwa mama, vivyo hivyo haina haja ya kuwa na mawasiliano na mama wa mtoto, kama una shida ya mtoto nenda anapoishi kamuone na kumuachia pesa ya matumizi ambayo utamkabidhi mtoto mbele ya mama yake na sio kumkabidhi mama(hapa kama ulimkuta 'mume' mwenzio na akaona unamkabizi mama pesa lazima atajisikia vibaya).

Njia nzuri ni hiyo.
 
Sijidanganyi kwa hvyooo....!!!

Mawasiliano ya kawaida tu haswa ya kumhudumia mwanawe...mfano kwenye ada nk

Ila sio mawasiliano ya kipumbavu pumbavu kama salamu hivi ni ujinga na Huyo mke atakuwa hajui wajibu wake...

Hao wazazi kukataza mtoto asioe single mother ni wao tu na maamuzi yao!

Ila wapo wengi wameolewa na wanajiheshimu pia!
 
Hahhahaha kwa njia yako hii wenzenu still hawatawaamin ndg!! Binadam akikupenda huwa akiona kitu cha kutilia shaka lazima mgombane! Yawezekana ukaiona njia yangu si sahihi lakini ndiyo imenipa aman ya ndoa yangu na yawezekana huko pia ana aman na ndoa yake ila tungekuwa tunawasiliana na tena kwa umbali huu wa dar mpk geita yangeshatuharibikia
 
Sijidanganyi kwa hvyooo....!!!

Mawasiliano ya kawaida tu haswa ya kumhudumia mwanawe...mfano kwenye ada nk

Ila sio mawasiliano ya kipumbavu pumbavu kama salamu hivi ni ujinga na Huyo mke atakuwa hajui wajibu wake...

Hao wazazi kukataza mtoto asioe single mother ni wao tu na maamuzi yao!

Ila wapo wengi wameolewa na wanajiheshimu pia!
Dada huwez kuwa na aman mmeo anawasiliana na mwanamke mwingine eti kisa mtoto huwez hata waongee mambo ya muhim mbele yako utawaza tu usipokuwepo wanaongeaje? Ongea reality
 
Dada huwez kuwa na aman mmeo anawasiliana na mwanamke mwingine eti kisa mtoto huwez hata waongee mambo ya muhim mbele yako utawaza tu usipokuwepo wanaongeaje? Ongea reality
Mi nna tabia ya kumuamini sana mwenza wangu kwa kweli!!

Hapo anapiga simu anaulizia kuhusu mtoto wala sijali najua kua ni zilipendwa yulee!Shaka sipati atajua mwenyewe na balaa lake!

Na tena Mimi sometimes namuuliza'hivi mtoto kule umeulizia hali yake?'

Au sikukuu namuambia jitahidi umnunulie nguo mtoto kule sio vizuri!!

So sina wivu wa kijinga huo then mie nkisema its over 'I mean it'
 
Mnataka mbaki na mtoto basi sitoi hata 10 kwa sababu mnaweza kumtunza! Hamtaki nipeni na siwaombi hata 10 lasivyo leta huyo mjomba nimuoneshe ntakachomfanya hatarudia kukanyaga ofisini
Mimi naishi na mtoto wangu, siwasiliani na babaake lakini anamhudumia 100%. Tumekubaliana kuwa anything kuhusu mtoto atawasiliana na mamaangu kwani ndo mlezi mkuu wa mtoto. Matumizi anatuma kwake, akitaka picha za mwanae anaomba kwake, akitaka kumuona mwanae anaongea nae wanaarrange. Nikihitaji anything kutoka upande wake nawasiliana na dadaake ananisaidia. Nashukuru inawork kwangu. Anamuona mtoto mara moja au mara mbili kwa mwezi na mimi na yeye ni mwaka na miezi sasa hatujaonana wala kutumiana hata message.

Hiyo unayofanya wewe ni kumnyanyasa mtoto, wacha ubinafsi!
 
Hana lolote huyo mwanamke aliyemuacha bado anampenda
 
Hana lolote huyo mwanamke aliyemuacha bado anampenda
Kwakweli, maana si kwa vikwazo hivo. Eti mtoto usimuone hadi awe mkubwa, labda kama sio mie niliyembeba miezi 9. Utahudumia au utasign document inayosema humtaki mtoto umeniachia mazima!
 
Kwakweli, maana si kwa vikwazo hivo. Eti mtoto usimuone hadi awe mkubwa, labda kama sio mie niliyembeba miezi 9. Utahudumia au utasign document inayosema humtaki mtoto umeniachia mazima!
Umeona eeehh!!!

Huyo Dada yaonyesha nae pia hana mpango na Huyo mtoto au hana uwezo wa kuhudumia
 
Mawasiliano yanauma bhana
Njia nzuri mmoja apate mwengine akose
Mtoto akiwa mkubwa atakuwa huru kuenda pande zote zote kama middle vile
 
Umeona eeehh!!!

Huyo Dada yaonyesha nae pia hana mpango na Huyo mtoto au hana uwezo wa kuhudumia
Ningekuwa sina uwezo wa kuhudumia nisingemchukua na sasa nina five yrs niko nae dogo yuko shule nzuri na now ana 10 yrs! A kiwa mkubwa atamtafuta mamake
 
Back
Top Bottom