Una mpango wa kuoa/kuolewa?
Kama jibu ni HAPANA . . kwanini?
Kama ni NDIO. . . je ni VIGEZO gani ambavyo vikifikiwa na mkaka/mdada utashawishika/penda kuingia ndoani?
Na ni MASHARTI (usichukulie neno masharti kwa uzito wake, namaanisha vitu ambavyo ni muhimu kuzingatiwa) gani ambayo yakizingatiwa unaamini ndoa yako itadumu?
Me?
Sijaoa,but nategemea kabla ya 2015 niwe nimeoa.
1.Nataka (thought yupo tayari) awe mtu aliye na hofu ya Mungu,na aliye mchagua Yesu
kuwa Advocate wake.
2.Asiwe mtumiaji wa kilevi chochote kile
3.Awe mvumilivu wa kila hali.
4.Awe tayari kumpenda mtoto wangu na kukubali kuishi nae bila kumpa kero yoyote
(Otherwise hatuta elewana kabisa)
5.Akubalike na mama yangu kwanza.
(She always tell me,sitakuchagulia mke,ila wanawake "tuko" hivi na hivi na hivi,...so ni rahisi kwake kufanya assessment)
6.Awe mtu atakae unganisha familia yangu na ya ndugu zangu (kama tulivyo siku zote),asiwe mtu wa kuja kutu tenganisha.
7.
AWE NATURAL AISEE (msisitizo zaidi,nahisi kinyaa nikimuona mtu kajichubua na mi-cosmetics and the like).
8.Asiwe mchaga au mpare please.
9.Asiwe mtembea uchi,....(i.e mtu wa vimini n.k).
10.Asiwe goli kipa (mama wa nyumbani tu kusubiri kuletewa kila kitu)
11.Anizoee sana,.....maana niko very strict.
"conditions" ngumu sana,....ila sio naona niliye nae kazipita zote.
Niliweka bandiko humu majuzi tu kwamba kigezo cha mama kakipita,soon tuta halalisha ndoa.