Single fathers and mothers njooni tujenge familia

Hicho ndio nachomshukru Mungu kila siku, niko na kakijana ka miaka mitatu ila kichwani kako vzr. Class hadi mwl wake ameshawaza mwakani aanze class one ila mm nimekataa. I am happy with my family, if God wishes one day ntampata single dady mwenzangu wa kuendeleza maisha hahahah
For sure! tuombeane tu
 
Mi ni single mother nina watoto wawili wa kike,mmoja miaka 9 na mwingine 6,,Mimi mwenyewe nina miaka 34,nilipata talaka mwaka 2014 baada ya mi kwenda UDOM kujiendeleza kielimu mwanaume akatekwa na ndo ikawa chanzo cha talaka,,nina imani hakuwa wangu wa kwangu atakuja,,bado nina imani katika ndoa,,tuombeane na kufarijiana wapendwa
Mungu atakuongoza
 
Hahahahahahaha. Utafiti usio rasmi humu single mothers ni wengi mno. Ukiuliza haja zao (nye.ge) wanapunguzaje apart from kuchemsha maji watakutoa nduki na jibu wasikupe.
At times ujinga raha sana
Jaribu tu kuwa na staha mkuu. Wengi wetu hatukupenda kuwa single parents
 
Hahahahahahaha. Utafiti usio rasmi humu single mothers ni wengi mno. Ukiuliza haja zao (nye.ge) wanapunguzaje apart from kuchemsha maji watakutoa nduki na jibu wasikupe.
At times ujinga raha sana
Afadhali umejigundua kwamba wewe ni mjinga mkuu
 
Huku kuna vituko

Wengine wanamshukuru mungu kuzaa kwa zinaa na wanafurahia uzao wa zinaa,wengine kujifariji tuu kwa zinaa walizopitia

Hakuna mwema hata mm nina yangu ila hapa unajidhalilisha na unamtukana Mungu japo hatukujui,bora ujutie hapa ila sio kujifurahia na hapohapo unamshirikisha Mungu katika upuuzi uliofanya ukazaa tunda linalokutesa sasa
Kuwa single mother sio uzinzi dada, kuna single mother hapa tulikuwa kwny ndoa, tulijitunza mpaka ndoa ndo tukazaa na mambo hayakuwa mazuri tumeachana ama wengine wenzi wao wamefariki so before judging or point a finger just think twice. Sio kila mwenye mtoto alimpata kwa kudanga/uzinzi usio rasmi. Hebu acha upuuzi
 
Mleta mada anataka tushirikishane changamoto ila naona wengi mmeenda nje ya mada. Am single dad with two kids mkubwa ni wakike mdogo ni wakiume, changamoto kubwa naipata kwa huyu wa kike hapendi kula kabsa tangu akiwa mdogo now ana 5 yrs, kuna wakati ili ale inabdi nimuimbie wimbo anaoupenda ndio atakula na hapo mpatane idadi ya vjiko atakavyokula na inabdi nitumie ujanja wa kuchota kijiko kilichojaa vzuri ili angalau ashibe. Then ni mtoto wa baba kwelikweli nikiwa safari au nikichelewa kurudi toka kazini anaweza kugoma kabsa kula mpaka nirudi so nikiwa safari inabdi nipge sim kabla ya saa za kula niongee nae na kumuhaidi kumletea zawadi nzuriii kwa maelewano kuwa asipokula simletei zawadi.

Huyu mdogo issue ya kula hasumbui kabsa kila msosi anagonga ila shida yake ni ubabe 2 yrs now ila ni bondia wa hatari,hapendi mtu ashike kitu changu chochote,huyo hana muda na mimi ila nikikaa wiki moja bilakua home basi akiona mwanaume yoyote yeye anaita baba! !!

For sure am happy with my kids, wao kwangu ni kilakitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Good father indeed
 
Back
Top Bottom