Single fathers: Wanaume mje msome

pisi jacky

Member
Oct 21, 2020
23
75
Nimeona sehem nyingi watu wanaongelea ongezeko la single mothers wanasahau mtoto n wa baba na mama leo nawaletea uzi maalum kuhusu single fathers

Kuna single fathers wengi kuna aliefiwa na mkewe kuna aliekua na mwanamke wakaoana na baadae wakaachana kuna ambae ye ndo kichaa kampa binti wa watu mimba kwa makusudi au bahat mbaya kama mnavoita afu katelekeza mtoto no kumlea no kufahamika kwao no what yaan unaendelea na maisha ako fresh tu afu kipindi iki maisha yanakua mazuri sana unakua na hela dem mkali iphone haikosi mkononi inshort mama mtoto wako anakua ni nuksi kubwa sana kwako

Sasa ntamuongelea huyu wa tatu ambae hana habar na mtoto Wala mama mtoto hasa vijana my friend nakusalimia alafu agiza apple punch baridiiiii unywe wakati unasoma uzi huu

Dear kijana wa kiume Mungu bwana n baba wa wote hua hachagui afu hamna mtu anaemlilia asijibu nawaletea true story za three different single fathers I've meet in person but kwanza niwaambie

Hamna single father alietelekeza mtoto akaoa afu ndoa ake ikawa na amani tu kama za wengine my friend hayupo ndoa zote Zina shida ila ndoa za hawa zinakua na special flovour

Mmoja ninaemfaham alioa jini kama jini kama unayaskia basi uyu bwana alioa jini anamlilia mama mtoto wake amsamehe mpaka sio vzur ila ndo basi tena mwanamama aligoma kumsamehe Nani akaliwe alipoliwa jini

Wa pili ninaemfaham mim alioa mke doctor very smart amesoma urusi wamezaa two hensam boys my friend uyu dada n mlevi wa pombe Kali asikwambie mtu tumeenda kwake siku iyo amekaa na lijackdaniels jikon amelipga vya kutosha my friend amepika samaki na nazi na machicha ake ilibd bwana ake atutoe tukale hotelini mwanamke n anakunywa hakuna mfano

Bwana amehama nyumba kaenda kupanga kamwachia mkewe nyumba kuepeuka tu zile kero za pombe maana anaenda kazin amelewa analud amelewa

Hiyo n michache naendelea mwanamke unaeolewa na mwanaume ambae unajua kabisa alimwacha mwanamke kwa matusi mengi na dharau nyingi nini kinakupa confidence mtadumu kwa amani kama aliweza muacha yule sweetheart your next joto lake n balaa ukimuuzi kidogo anatafuta mwingine maana ndio Tabia ake utapauka shoga angu ila vumilia muombee labda atajiludi si mlisikia ile hadithi ya yule dada alieolewa na mwanaume aliezaa na mwanamke mwingine akamtelekeza

Baada ya harusi mwanaume akaanza wasiliana na mama mtoto mambo yakanoga bwana akalala uko uko analudi mke anamuuliza ulilala wapi anajibu kwa ujasili kwa mama mtoto nilienda Jana mtoto alikua anaumwa alilia sana adi usiku nikaona nibaki uko uko dada na hasira zetu za kisomi akaanza kumpga pga tena mbele ya shoga zaake waliokua wameenda kumtembelea

Asubui baada ya mke kupiga sim usiku mzima kua haelewi mumewe alipo so wakawai kumfariji asubui wakiwa wanajadili mume kaingia mzima kabsa bibie kumuliza ndo kajibiwa ivo mbele za mashost kujifanya anampa vimakofi mbele ya mashost bwana alipgwa adi mashoga walitafuta mlango walioingilia adi kuvunjwa mguu na mume akabeba nguo na kwenda kuamia kwa mama mtoto my friend single fathers wanakua kama wanalaana inawafwata mgongoni maana wanakua wamemfanya mdada wa watu Alie wazazi wake walie yan kuna mbaba aliwai kufa presha kisa mtoto wake kapata mimba na katelekezwa my friend Mungu sio bamdogo ako yatakukuta one day

Naendelea single fathers mnaotelekeza na kwenda kuoa mnaosema mnawafeel my friend my own cousin yalimkuta alifanya uo ufala alioa tena pisi Kali yenye hela na familia inaheshmika bwana kumbe binti n mshirikina hakuna mfano alikua anamuwekea dawa ili asimsikilize mwanamke yoyote isipokua yeye na ivi alijua alishazaa so akawa anakoleza dawa haswa si akakosea siku moja dawa zikamlud

Mume vibaya akaumwa adi kua zezeta my friend shangazi angu nae hakua nyuma alimbeba adi malawi ndio alikoenda ponea mpaka leo ndoa ilikufa yupo yupo anaogopa wanawake kama ukoma

Dear single fathers Mambo Ni mengi lakin ni nin nataka kuwaambia yanini kujibebea laana mwanamke ana mimba mimba ako na mtoto n wakwako lea nenda jitambulishe kama baba mtoto sisemi uoe no hamna anaekulazimisha lakin ufala sana kumuacha mtoto ako akalelewe na mwanaume mwingine kwa sababu hata ukioa uyo unaempenda wewe my friend sio kweli kwamba u won't cheat na mwingine hata kama sio yule uliezaa nae

Always be a responsible man suleiman alikua na wanawake buku na wote anawasifia kama nin we kamwanamke kamoja eti nilizaa nae bahat mbaya simpendi mbwa yule matusi kibao my friend ukishndwa kumuheshim mwanamke aliekufanya uitwe baba ukazan ukioa unaeita wewe mke ninaempenda kibao kitageuka ile heshima wewe unampa yeye atakachokuludishia adi huruma

Namalizia wanaume acheni ufala unakataaje mtoto wako mwenyewe kuna kuzeeka kuna ajali kuna kufilisika mwengine alipata ajali akaumia pumbu kaambiwa huwezi kuzAa tena alizaa na mwanamke alimkataa mtoto kuambiwa ivo alimtafuta mama mtoto analia machozi na makamasi kwa pamoja wanawake tuna huruma alimsamehe mwoneni baba ommy dimpoz mwoneni baba dai unaweza kua mjanja saiz lakin 20 years from now hujui utakua wapi ten times oa wake wawili ukiona huyu umuelewi kiivo

Wanawake mnaosoma hapa mwanaume kama anahudumia watoto wewe anakuhudumia vzuri hana matatizo ya nguvu za kiume mtoto wa watu akitaka kuongeza mke muache aongeze kama anajiweza(sana sana wenye hela maskini hii aikuhusu kabisa) sema ufala wa wanaume ukipata b mdogo unaanza kumdhalau mkubwa my friend daudi alikua na wanawake wakutosha na leo yupo mbinguni na tunamsoma kwenye biblia Mungu aliwaagiza wapendeni wake zenu na kuna mahali alisema ishin nao kwao akili Sasa wanaume wa siku izi sijui ndo akili zimekimbia trust me mkifika mbinguni mtaambiwa kuoa mke zaidi ya mmoja haikua shida ila akili zenu ndo zilikua na shida

Dear future husband ukinitreat vzur nkala vzur mim na watoto wangu mbele za Mungu ukitaka kuoa mke mwingine we oa tu ila upendo wako usipungue na akili ako iwe active na hela uwe nazo

KUMBUSHO: single mothers wengi wanamajibu mabaya kwanza umemzalilisha coz umemkataa kila mtu anamuona malaya so wanakuaga na hasira sana na majibu ya shombo na mengine mengi lakin hamna mkamilifu labda uoe mkoba mjifunze kuchukuliana
 

Bajeti ya kunguru

JF-Expert Member
Sep 21, 2014
1,246
2,000
Ukisha angukia pabaya umeangukia pabaya tu ni ngumu sana kupata afadhali uitakayo kwa mwanamke mwingine naye utamkuta anayakwake ndio pale unaposikia wanawake ni walewale au mwalimu wao ni mmoja.MAGUFULI4LIFE.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom