Singida: Mkurugenzi(DED) wa Halmashauri ya Itigi adaiwa kumuua mwananchi kwa risasi

Vetting ya hawa viongozi muhimu sana. Wengine hawajui wanachofanya
Sidhani kama neno au dhana ya 'vetting' imo katika msamiati wa mfumo wa utawala wa CCM. Hivi ndio vyeo (DED, DC, nk) ambavyo mkulu huvitumia kuwazawadia wapambe, wapiga debe, nyumba ndogo, michepuko, wapwa, binamus, nk. JK alituonea sana, Katiba Mpya (rasimu ya Warioba) ilikuwa imekusudia kuleta nidhamu ya utawala bora. Huu uchafu ulikuwa uondoke.
 
Huyu Mkurugenzi wa Itigi akapimwe akili kwanza, utampigaje mtu risasi akiwa kanisani kisa amechelewa kulipa ushuru wa halmashauri? Nasikia Marehemu alikuwa akilima shamba la Tanganyika Packers sasa alikuwa amechelewa kulipa ushuru wa shamba hilo,Th thunder that will strike this Director is still doing some warm up on Mount Kilimanjaro, Magu never allow Impunity of higher magnitude to prevail in this peaceful Country,, This killer should be held responsible, May God strengthen the bereaved family, The killer may never know peace in his life,
 

Hivi huyu alistahili kweli kuwa DED? Tuwe makini katika vet. Badilisheni mfumo wa uteuzi. Kurundika madaraka ya uteuzi kwa mtu mmoja hayatusaidii sasa.
 
Radio one DC kasema kesi ipo polisi na hawana uhakika aliyefyatua risasi, ila mhu tunakoenda kubaya. Heri yake Nnape naye angekuwa marehemu kama siyo kuokolewa na watu.
duh..yamekuwa hayo kuwa hawana uhakika?aisee hyo ndo ntolee
 
Unapokuta ofisa wa serikali mteule wa Raisi anakusanya ushuru (mapato ya serikali) kwa kupiga watu risasi na kuua mchana kweupe una jiuliza jee tuna tofauti gani sisi na magaidi kama Boko Haramu wanaovamia makazi ya watu na kufyatua risasi kuua ili wajipatie kipato?
Kitendo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi kwenda kukusanya ushuru (kazi ambayo sio yake kimsingi) akiwa na silaha binafsi kisha kumtwanga mkulima aliyekuwa kwenye nyumba ya Ibada kabisa kunafikirisha sana na kufikia hitimisho la kauli ya Zitto kuwa tupo ndani ya United Republic of Gangstars kuwa yuko sahihi
 
Kuna taarifa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri moja huko mkoani Singida amempiga mtu risasi kanisani. Kisa kikielezwa ni migogoro ya ardhi. Mwenye taarifa za kina atujuze!
Radio One imetangaza ila wanasema hawana uhakika nani alifyatua risasi??????? Hapo sasa.
 
Mabina akiwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza aliuawa kwa kupigwa mawe na wananchi wenye hasira kali pale kisesa
1549346244328.png
 
Aibu. Vyeo hivi vya kiutumishi vifuate miongozo tunapoteua.

Sitoshangaa ikiwa huyu hajawahi kuwa mtumishi wa umma before uteuzi wake.

Malezi yake sio ya ki- public servant.
Utumishi wa umma uvumilivu, busara na kufuata taratibu na kanuni. Kudai kodi church?. Naamin kuna ambacho hatujaelezwa kwenye tukio hili. Siamin kama limetokea kama linavyoelezwa.
 
Kuna Habari ina sambaa na inasema hivi ;nna Nukuu.

Habari za jioni baada ya kufuatilia Jambo hili kwa kina nnaomba kutoa Taarifa ifuatayo kwanza Mkurugenzi mwenzetu yupo salama na ana endelea na Kazi na hakuhusika na kumfyatulia Mtu Risasi.Chanzo cha Tatizo ni kwamba kuna Wananchi na wawekezaji walipewa Mashamba ambayo ni ya Serikali kulima.Baadhi ya Wananchi wakawa wame anza kuhujumu Mashamba ya baadhi ya Wawekezaji na Wananchi kwa kuchoma Moto Vipando na Majengo ya wanao endeleza Mashamba hivyo Mkurugenzi pamoja na Mgambo walikwenda kuwa kamata Wananchi wanao haribu Mali za wenzao.

Wakiwa kwenye Eneo la Tukio Mkurugenzi aliwaacha Mgambo na kwenda kuwachukua Askari Polisi ili kuwaongezea Nguvu Mgambo.Huku nyuma baadhi ya Wananchi wakaanza kuwashambulia Mgambo ndio ktk kujitetea Mgambo mmoja alifyatua Risasi na kumuua huyo Mtu alie fariki wakati Mkurugenzi anafika na Polisi tayari tukio lilikuwa limesha tokea.

Mwisho wa kunukuu..
Ciril, tangu mgambo uanza kwenye early 70s ulishaona wanabeba silaha au wenyewe ni magongo?
 
Back
Top Bottom