Estone
JF-Expert Member
- Feb 6, 2012
- 631
- 651
uchumi wa viwanda lazima uende nao sawa kivyovyote😂😂🤣
i
i
Ha ha!! Watu wana mbinu hela inatafutwa ile hatari.. subiri na mtoa mada nae atakuja kukamatwa na tunguli zake sipati picha itakuwaje magazetini vichwa vitakuwa "mlozi abambwa" " mganga maarufu akwama kazini" "ama kweli nyani wakitoweka miti yote huteleza"
"Za mwizi ni arobaini" halafu wanasindikiza na picha yake tunguli mpaka kwenye kope[emoji23][emoji23]
Langu nitaandika "mkuki kwa kungurue kwa binadamu mchungu"
We endelea kuleta ya wengine yakwako pia yatakujia kamera zote kwako!!
Humpata kukuDua la kuku.....
Jr[emoji769]
acha kujihisi ndugu..Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda alimtaja Hakimu huyo wa Mahakama ya mwanzo kuwa ni Benard Modest Kasanda na kwamba alitenda kosa hilo Desemba 16, mwaka huu kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Naona umesoma heading tu ukiwa na judgment zako tayari kichwani... Wala hukuchukua muda kusoma habari yote vizuri
Jr[emoji769]
Huyu hakimu akipatikana na hatia apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.😀😀😀😀😀😀
[/QUOTn
acha kujihisi ndugu..
Mimi sio mwendawazimu nisome heading tuu.
kwa maana hiyo una maana kwamba nilikuwa Nina judgement zangu kichwani. nikushambulie bila sababu??
sawa unavyoona ndivyo hivyo.!
asante.
🤪🤪🏃🏃Humpata @kenzy
Jr[emoji769]
Hii tabia imeshajengeka sana kwa watumishi hawa wa Mahakama na pia Polisi baadhi wameshaona kuchukua rushwa kama ni haki yao vile kuna mmoja yupo Mafinga Victor dawa yake inachemka atakutana na za moto na kibarua chake kiote mbawa!TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Singida inamshikilia Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mtinko wilayani Singida, Bernard Kasanda (38) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya 250,000/- taslim kutoka kwa mwananchi mmoja ili aweze kumpa upendeleo kwenye kesi iliyokuwa mbele yake.
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Singida, Adili Elinipenda alisema mjini Singida jana kuwa licha ya kukamatwa na rushwa hiyo, mtuhumiwa pia alikutwa na visu vitano vinavyodhaniwa kutumiwa na mtuhumiwa kujihami wakati akijipatia maslahi hayo haramu.
Elinipenda alisema kuwa mtuhumiwa Kasanda alikamatwa Jumatatu Desemba 16, mwaka huu ofisini kwake baada ya kukabidhiwa maslahi hayo ya kificho ambapo mara baada ya kupokea, alizifutika kwa ustadi mkubwa ndani ya kasha la dawa ya meno la Whitedent lililoisha dawa.
"Ingawa mtuhumiwa huyu siku zote alikuwa akiwapa funguo za choo anachotumia yeye tu kwenda kuhifadhi kiasi cha fedha anachokubaliana na washitakiwa kisha kwenda kuzichukua baadae, siku hiyo alitumia mbinu nyingine tofauti ambapo alitumia kasha la dawa ya meno" alibainisha Mkuu huyo wa Takukuru.
Alieleza kuwa mtuhumiwa alipopekuliwa zaidi alikutwa na kiasi kingine cha fedha 489,100/-, visu vitano ( kimoja kikiwa kakichomeka kwenye soksi), vingine vikiwa kwenye droo ya meza yake na kwenye mkoba wake.
Mkuu huyo wa Takukuru alisema pia kuwa baada ya tukio hilo, wananchi wengine wawili waliodai wana mashauri mbele ya hakimu huyo walijitokeza na kusema nao pia walikuwa wamempatia 50,000/-na 200,000/- kama walivyo.
Alisema kuwa Taasisi hiyo inaendelea na uchunguzi wa mashauri hayo yote na kwamba umma utajulishwa baada ya kukamilika huku akisisitiza kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa kinyume na Kufungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya 2007.
Wakati huo huo, Mkuu huyo wa Takukuru ametahadharisha viongozi wa Serikali na watumishi wa Umma kutojihusisha na rushwa huku akitoa angalizo kuwa Taasisi hiyo iko macho wakati wote na kwamba itaendelea kutoa elimu kwa wananchi wote katika juhudi zake za kutokomeza mchezo huo mchafu.
Huyo hakimu au ninja!?TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Singida inamshikilia Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mtinko wilayani Singida, Bernard Kasanda (38) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya 250,000/- taslim kutoka kwa mwananchi mmoja ili aweze kumpa upendeleo kwenye kesi iliyokuwa mbele yake.
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Singida, Adili Elinipenda alisema mjini Singida jana kuwa licha ya kukamatwa na rushwa hiyo, mtuhumiwa pia alikutwa na visu vitano vinavyodhaniwa kutumiwa na mtuhumiwa kujihami wakati akijipatia maslahi hayo haramu.
Elinipenda alisema kuwa mtuhumiwa Kasanda alikamatwa Jumatatu Desemba 16, mwaka huu ofisini kwake baada ya kukabidhiwa maslahi hayo ya kificho ambapo mara baada ya kupokea, alizifutika kwa ustadi mkubwa ndani ya kasha la dawa ya meno la Whitedent lililoisha dawa.
"Ingawa mtuhumiwa huyu siku zote alikuwa akiwapa funguo za choo anachotumia yeye tu kwenda kuhifadhi kiasi cha fedha anachokubaliana na washitakiwa kisha kwenda kuzichukua baadae, siku hiyo alitumia mbinu nyingine tofauti ambapo alitumia kasha la dawa ya meno" alibainisha Mkuu huyo wa Takukuru.
Alieleza kuwa mtuhumiwa alipopekuliwa zaidi alikutwa na kiasi kingine cha fedha 489,100/-, visu vitano ( kimoja kikiwa kakichomeka kwenye soksi), vingine vikiwa kwenye droo ya meza yake na kwenye mkoba wake.
Mkuu huyo wa Takukuru alisema pia kuwa baada ya tukio hilo, wananchi wengine wawili waliodai wana mashauri mbele ya hakimu huyo walijitokeza na kusema nao pia walikuwa wamempatia 50,000/-na 200,000/- kama walivyo.
Alisema kuwa Taasisi hiyo inaendelea na uchunguzi wa mashauri hayo yote na kwamba umma utajulishwa baada ya kukamilika huku akisisitiza kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa kinyume na Kufungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya 2007.
Wakati huo huo, Mkuu huyo wa Takukuru ametahadharisha viongozi wa Serikali na watumishi wa Umma kutojihusisha na rushwa huku akitoa angalizo kuwa Taasisi hiyo iko macho wakati wote na kwamba itaendelea kutoa elimu kwa wananchi wote katika juhudi zake za kutokomeza mchezo huo mchafu.
YaaHuyu nae eti ni great thinker..!? PatheticView attachment 1296177