Maafisa misitu 2 wahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano kila mmoja kwa Ruswa ya milioni 8

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,408
Reaction score
4,987
Mahakama ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imechukua hatua kali dhidi ya vitendo vya rushwa baada ya kuwahukumu maofisa wawili wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Thadeus Mtui na Florian Kilango, kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano kila mmoja. Hukumu hiyo ilitolewa baada ya mahakama kuridhika kuwa watumishi hao waliomba na kupokea rushwa ya jumla ya shilingi milioni nane kutoka kwa mfugaji Yuda Male.

Mahakamani ilielezwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Daniel Mono, kuwa washtakiwa hao walichukua fedha hizo kwa awamu mbili, ambapo Novemba 2025 walipokea shilingi milioni mbili na Januari 2026 wakachukua milioni sita nyingine. Fedha hizo zilitolewa na mfugaji Yuda Male ili aepuke kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya kukutwa akiingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Chimala.

Hata hivyo, baada ya kuona anaendelea kusumbuliwa licha ya kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha, mfugaji huyo aliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola. Hakimu Mkazi Mfawidhi Irvan Msacky, mbali na kutoa adhabu hiyo, pia aliamuru fedha zote zilizochukuliwa zirudishwe, akisisitiza kuwa mahakama haitavumilia vitendo vya rushwa vinavyohatarisha uhifadhi wa rasilimali za taifa.
 
Hukumu ndogo namna hii ni ya 'pisha kombe mwanaharamu apite'!

Hapo hakimu ashakula rushwa sana toka kwa hao jamaa.

Fine laki5 kwa watu wawili yaani millioni moja kwa kesi ya kosa la millioni 8!

Ukute hapo hukumu ilipangwa bar katika jopo la wahalifu na hakimu na fine ikaandaliwa mifukoni siku ya hukumu.

Hakuna aliyechungulia mlango wa gereza pale.

Usanii mtupu.
 
Hakimu = Mtumishi wa mahakama analipwa na serikali
Maafisa misitu= Watumishi wa serikali.
Kwa kawaida watumishi wa serikali wana tabia ya kuokoana kwenye misala😀😀😀
 
Kwa adhabu laini na nyepesi za aina hii, rushwa haiwezi kupungua nchini.
 
Hakimu = Mtumishi wa mahakama analipwa na serikali
Maafisa misitu= Watumishi wa serikali.
Kwa kawaida watumishi wa serikali wana tabia ya kuokoana kwenye misala😀😀😀
Hakimu angekua na lengo la kuwasaidia wangeshinda kesi.
Kwa hukumi hiyo kinachpfuata ni kufukuzwa kazi, kwa mantiki hiyo hakimi hajawaokoa labda wakate rufaa then washinde.
 
Mahakama ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imechukua hatua kali dhidi ya vitendo vya rushwa baada ya kuwahukumu maofisa wawili wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Thadeus Mtui na Florian Kilango, kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano kila mmoja. Hukumu hiyo ilitolewa baada ya mahakama kuridhika kuwa watumishi hao waliomba na kupokea rushwa ya jumla ya shilingi milioni nane kutoka kwa mfugaji Yuda Male.

Mahakamani ilielezwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Daniel Mono, kuwa washtakiwa hao walichukua fedha hizo kwa awamu mbili, ambapo Novemba 2025 walipokea shilingi milioni mbili na Januari 2026 wakachukua milioni sita nyingine. Fedha hizo zilitolewa na mfugaji Yuda Male ili aepuke kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya kukutwa akiingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Chimala.

Hata hivyo, baada ya kuona anaendelea kusumbuliwa licha ya kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha, mfugaji huyo aliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola. Hakimu Mkazi Mfawidhi Irvan Msacky, mbali na kutoa adhabu hiyo, pia aliamuru fedha zote zilizochukuliwa zirudishwe, akisisitiza kuwa mahakama haitavumilia vitendo vya rushwa vinavyohatarisha uhifadhi wa rasilimali za taifa.
Faida sh. 7,000,000/=, Mungu awabariki.
 
Fine laki 5, rushwa milioni 8!!!
Hiyo rushwa kwao haijatumika, yote imeenda kwa wa kesi yao.
Takukuru nao wamekula parefu hivyo wakifungwa hao kwa kifupi faini yao roughly ni milioni thelathini, hizo laki tano ni za kwenye makaratasi tu ziingie serikalini zikaliwe na wengine.
Hakimu naye anakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Mahakama ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imechukua hatua kali dhidi ya vitendo vya rushwa baada ya kuwahukumu maofisa wawili wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Thadeus Mtui na Florian Kilango, kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tano kila mmoja. Hukumu hiyo ilitolewa baada ya mahakama kuridhika kuwa watumishi hao waliomba na kupokea rushwa ya jumla ya shilingi milioni nane kutoka kwa mfugaji Yuda Male.
Rushwa Milioni nane , faini laki tano.

Hata mimi Naina Tu, risk ni ndogo mno na unapata faida juu
 
Back
Top Bottom