Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,565
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana leo, baada ya kushikiliwa Polisi tangu Jumatatu Machi 2, 2020
Lema alienda kuripoti Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Polisi (RCO) Arusha kama alivyotakiwa kufanya baada ya kupigiwa simu na Polisi ambao walienda kwake na kumkosa
Baada ya hapo alisafirishwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi Singida ambapo alihojiwa akituhumiwa kutoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kuchonganisha Jeshi hilo na Wananchi
Aidha, Katibu wa CHADEMA Wilaya Singida Mjini, alisema Lema alimwambia kuwa kosa analodaiwa kutenda ni kutaja orodha ya watu 14 waliouawa Manyoni kwa kuchinjwa na kuchomwa moto.
PIA SOMA:
Godbless Lema aitwa na Ofisi ya RCO Arusha, asafirishwa na Polisi usiku kwenda Singida