Singida: Diwani wa kata ya Iseke ajiuzuru

Singida: Diwani wa kata ya Iseke ajiuzuru

Si kuna wawakilishi kwenye kamati za bunge na mawaziri vivuli mbona hawahoji suala hili, la uwendweshaji wa baadhi ya mashirika ya umma ambayo yanaendeshwa na hela za kodi ya taifa.

Ni hapo kwenye kamati ndipo wanaweza kuulizana menejiment inamfanyia nani kazi na pengine aitwe huyo director kuhojiwa mbele ya kamati kwa nini matukio fulani ambayo wengine waliona yana umuhimu kutopewa kipaumbele au sio kamati zote zenye wawakilishi wa upinzani.

Kuna vitu vingine inakuwa ilimradi kulalama tu lakini njia sahihi azitumiwi mbona ZZK huwa anaomba mafaili yanayohusiana na shughuli zake kutoka serikalini, sasa ni lini umesikia mhusika wa upinzani akiliuliza hili swala kwenye kamati au kutoa changamoto za mabadiliko, maana ZZK akimaliza kusoma asivyopenda serikalini kwenye uwanja wake huwa anaandika kwenye blog yake na kutoa mapendekezo.

Hapa sio TBC tu hata magazeti yanaoendeshwa na kodi hayastaili kuwa bias kamwe, wengine watakuwa walalamikaji miaka yote wakati njia za mabadiliko wanazijua.
 
Mbona wakati madiwani wa CCM Sinyanga walipojiuzulu haikuwa habari kwao??? Mbona hawajasema Mbowe kaupaitia mgogoro wa Karatu suluhu???
 
Tulishatangaziwa TBC siyo chombo cha habari cha taifa,ni chombo cha habari cha CCM!
 
Wangembembeleza Silaa kwanza mengine yangefuata mmemshindwa Silaa hamtaiweza Chadema moja kwa moja mpaka lkulu mtafurahi. Diwani ccmiz
 
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Iseke wilaya ya Ikungi, mkoa wa Singida ndg AMOS REUBEN kwa tiketi ya CHADEMA amejiuzulu wadhifa wake. Amesema uongozi wa CDM unamzuia kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo. Ndg Amos ameamua kujiunga na CCM.
 
Tuko kwenya mapambano, ni vizuri wasiokuwa na msimamo waondoke mapema kabla ya ukombozi kamili (2015).
 
Kata ya Iseke iko Tarafa ya Ihanja na Wilaya ya Ikungi. Lakini sio jimbo la Tundu Lissu, ni jimbo la Mohamed Misanga (ccm).
 
Unamzungumzia NJAU kwenye Siasa za Jimbo la Singida Mashariki kweli! NJAU hana uwezo wa kisiasa kabisa. Uwezo wake ni kwenye ujumbe tu ambao hata hivo anashindwa. Imani yangu ni kwamba CCM itasimamisha Mgombea ubunge imara na makini na sio huyo NJAU.
 
Kwa kifupi ni kwamba NJAU hana hata uwezo wa kumudu jukwaa hata kidogo. Hana uwezo wa kwenda kasi ya kisiasa iliyopo sasa. Kuna wanasiasa makini na imara kuliko Njau. CCM itasimamisha mgombea makini atakayemtoa Tundu Lissu. Njau hana uwezo huo.
 
SERA ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), ya kukataza wananchi kuchangia maendeleo yao, imesababisha diwani wa chama hicho Kata ya Iseka, Amos Rubein Mughenyi, jimbo la Singida magharibi, kujiuzulu.

Akitangaza uamuzi huo, kwa waandishi wa habari, Amosi alisema amejiuzulu nafasi ya udiwani huo kuanzia Desemba 21, mwaka jana.

Alisema uamuzi wake, haujatokana na kushawishiwa wala kulazimishwa na mtu au chama chochote cha siasa, bali umetokana na CHADEMA kumzuia kushirikiana na viongozi wa Serikali ngazi ya wilaya na mkoa kusimamia shughuli za maendeleo.

Alisema amekuwa akishinikizwa asikubaliane na changizo (michango) ya aina yoyote ya maendeleo ya kata yake, kwa madai kuwa jukumu la kuwaletea maendeleo wakazi wa kata ya Iseka, ni la Serikali pekee.

“Hivi sasa, Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Iseke (WDC), imeazimia kufanya harambee kwa ajili ya kutafuta fedha za ujenzi wa madarasa na maabara katika shule yetu ya sekondari. Tunapendekeza Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli awe mgeni rasmi katika harambee hiyo, CHADEMA wamenigomea,” alisema Amosi.

Alisema viongozi wa CHADEMA wilaya, wamemtaka akae pembeni asijihusishe na harambee hiyo na kama atalazimika kushiriki atajiondoa ndani ya chama.

“Nimeamua kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu wadhifa huu, ili wananchi wangu wawe huru kujipangia shughuli zao za maendeleo, bila kuzuiwa na itikadi ya CHADEMA,” alisema Amosi.

Amewaomba viongozi wa Serikali na hasa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Manju Msambya, kuendelea kuwaunga mkono wananchi wa Iseke ili wafanikishe harambee hiyo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Illuminata Mwendwa, amekiri kupokea barua ya Amos kujiuzulu.

Tundu Lissu mara kwa mara, amekuwa akiwaeleza wananchi wake watakuwa likizo ya kutochangia maendeleo hadi ubunge wake utakapokoma.




Source: Gazeti la Majira; Jumatano, Januari 02, 2013
 
Na hizo mil. 20 alizopewa huyo diwani zilitoka wapi? Maendeleo ni lazima wananchi wachangie? Je hawalipi kodi?
 
Alitakiwa kujua tangu uhuru wa nchi hii Tanzania iliingia kwenye ukoloni mpya wa mtu mweusi aitwaye CCM na tangu wakati huo kodi zimekusanywa na watu wamefungwa kwa kukaidi kulipa michango, tena ya sh 200 ilihali wawekezaji/wakoloni wenza wa CCM kutoka ulaya wanavuna kila wanachokiona ardhini yaani Madini mpaka wanyama wanawapandisha ndege na mchanga kubebwa kwenye chopa huku mwananchi mnyonge akikamuliwa kodi kuanzia kiberiti mpaka chupi anyovaa na inaishia kumnufaisha waziri na familia yake kama sio kulipia kodi za nyumba za vimada na familia zao..Go on Lisu..Kupambana na ukoloni kwanza goma kulipa kodi atakuachia tu maana hana cha kuchukua
 
Lisu ni kikwazo cha maendeleo jimboni mwake, 2015 asijisumbue kuchukua fomu ya kugombea ubunge
 
Ndo maana watu wa Singida wapo hoi kimaisha na kielimu.Mimi ukinita mtu wa Singida naona kama una nitusi
 
safisana kamanda lissu mwaka huu jikite jimboni sana ndio walio na watakaokuweka 2015 sera za lissu nzuri hela wanapewa wanaweka uswiss wanataka tuchange za maendeleo za uswiss za nini
 
Lisu ni kikwazo cha maendeleo jimboni mwake, 2015 asijisumbue kuchukua fomu ya kugombea ubunge

Masalia hamchoki tu.... Mods hii habari iunganisheni na thread inayohusu huyu diwani kuacha udiwani...
 
Back
Top Bottom