Impact yake imedondokea kwenye issue ya IPTL vs TANESCO, na itatupiga vibaya kama nchi, tena sana. Sidhani kama Jamhuri ilifanya sahihi kuwaweka ndani Ruge na Seth (Pia Yusuph Manji). Kulikua na njia nyingi mbadala za kufikia settlement.
Ruge na Seth, Serekali ingekaa nao na kufanya arbitration to reach amicable agreement yasingetokea haya ya IPTL na mengine. Kwanza kwa muda waliowekwa ndani mpaka sasa "wameshaficha na kuchafua ushahidi wote duniani". Japo mawakili wa serekali wameweza kuzuia wasisafiri nje ya nchi hata kwa matibabu, wasionane hata na wake zao na madaktari wao, ila kwa mwenye akili atajua wameshachafua ushahidi zamani, sasa hivi wanamalizia kuziba mashimo tu, ITS TOO LATE.
1) Utakuta kila siku usiku wataalamu wa ushahidi na wafuasi wa hao jamaa wanaingizwa gerezani kimya kimya kuonana nao na kupanga mikakati ila raia na jamhuri haijui.
2) Kama Serekali ilivyokua na uthubutu wa kuwaweka ndani, nao wana uthubutu kwenye baadhi ya ma bank makubwa duniani na makampuni makubwa pia, hizo bank zinauwezo hata wa kufuta transaction za account zao/ financial statement zao n.k. (We should learn to think).
3) Kama watashinda case zao, wanauwezo wa kuishtaki serekali kwa MALICIOUS PROSECUTION (kushitakiwa kwa makusudi/kushitakiwa kwa nia ovu) na wanaweza kudai fidia ndefu sana. Fidia wanayoweza kuadai itajumlisha madhara waliopata kibiashara/afya/muda waliokaa ndani/kuchafuliwa jina/madhara kisaikolojia waliopata/gharama za kuendesha case kutumia mawakili wa ndani na nje ya nchi n.k
Wakati mwingine, kama mtu una uelewa mzuri/timamu swala la kuonesha umma au nchi kwamba una uthubuti kwa maadui zako wala sio muhimu, na halina faida/tija bali lina hasara. (Kwa wachache ambao hawana uelewa hua wanashangilia hili jambo kwa uchochezi wa dini, rangi, kabila, pia uwezo wa pesa/umaskini).
Nachofahamu ADUI yako hata kama ni dhaifu vipi, akikukamata pabaya we kua mdogo na mshike mkono mwende nyuma ya pazia mkayamalize. Ila ukimuonesha jeuri halafu akapata watu wa kumshika maskio vizuri, umeumia.
Pia ninacho kiona hizi case zote kubwa, either za matajiri au watu wenye majina yao (kama vile Tido Mhando) jamhuri ina kazi nzito ili ishinde, wengi wanapelekwa mahakamani kwa kurupuka tu.