Mkuu muungano wa Singapore na Malaysia uliposhidikana mwaka 1962 ndipo LKY akawa first prime minister ndipo 1965 ikawa independent democratic state. In short image ya nchi ni kiongozi, ndio maana baada ya trh 26/03/2015 umeona tofauti ya kabla ya hiyo tarehe? Imekua shida media zimekua huru, vijana kama Amos Yee anatukana ovyo ovyo kwa sababu PM wa sasa ni democratic. Dawa ni kupata kiongozi dictator tu akisema barabara inapita hapa, no discussion.
Kuhusu kutawaliwa na wahindi, asilimia 73 ni Chinese, 21 Malay na 3 ni wahindi na iliyobaki ni mix ya waasia wengine. Na historia ya hiyo nchi ni tofauti sana na sisi. Wao toka watawaliwe na wajapan 1945 mpak Brits wakaja bado palikua na mchanganyiko huo wa watu. Huwez fananisha sisi na SiNGAPORE kwa multiculturalism blaza
Mkuu,
Umesoma kitabu cha LKY?
Kama hujasoma, jaribu kukisoma. Anaongelea habari zote zake na serikali yake, demokrasia na maadui zake. (Kinaitwa "The Singapore Story: Memoirs of Lee Kuan Yew)
He was far from being "democratic" leader. Yeye alikuwa na vision ya jinsi anataka Singapore iwe, mtu yoyote aliyempinga anamweka ndani au anamfilisi kwa kumtoza fine katika korti zake na sheria hii ipo mpaka leo.
Anaheshimika kwa kuwa ameijenga Singapore kibabe na kuipa heshima siyo kwa "democratic credentials" zake. Kwa sababu hiyo, mabaya yake wamemsamehe.
Kuhusu Wahindi wa Singapore, nakupinga kuwa wako tofauti na wakwetu. Pia wapo 7% siyo 3% ya Singapore. Vizazi vyao vyote vimetoka nchi moja, mkoloni mmoja huyo huyo ndiye aliyewaleta Singapore na Afrika Mashariki.
Mjapani katawala miaka mitatu tu - 1942-1945.
Mkoloni aliokaa hapo sana ni Muiingereza kuanzia 1819 na Sir Raffles kujenga bandari yao. Wakajitawala chini ya bendera ya mkoloni (self government) mpaka 1963, muungano na Malaysia haujafanikiwa na wakaamua kujitoa na kuwa nchi huru ya Singapore 1965.
(Singapore pia ni "demokrasia" tofauti na nchi za magharibi. Bakora mahakamani bado unapigwa kwa kuharibu mali za watu au wizi. Mtoto wa Kimarekani alichapwa hata baada ya Raisi wao kumwombea msamaha miaka ya nyuma. Yule mtoto Amos kawekwa ndani siku 54 kabla kuachiwa huru kwa kumtukana LKY katika YouTube, kitu ambacho hakiwezi kutokea nchi zenye uhuru wa maoni).
Tofauti ya Wahindi wao na wa kwetu ipo katika sehemu waliyotoka tu. Kama Tanzania, wengi wanaoa Wahindi wenzao. Mix ipo baina ya Malay na Waarabu/ Wachina/ Wazungu.
Watamil walipelekwa/ wameenda Singapore, Wagujarati wakaja/ wakaletwa Afrika Mashariki. Mpaka leo, nimewakuta watamil na misuri yao wanaletwa kufagia nchi/ gardener kama wanavyofanya Dubai au Muscat. Vizazi vya nyuma yao ni wasomi na hawataki kufanya kazi hizi tena.
Tofauti nyingine ni elimu. Kwa kuwa elimu yao ni bora zaidi na serikali inalipa Wafanyakazi wao vizuri (wasikimbie private sector) ndiyo unakuta wengi wamesoma na kufanya kazi serikalini Kama Raisi, mawaziri na mabalozi. Balozi wao Indonesia leo kwa mfano ni mwenye asili ya Kihindi.
Swali umelikwepa. Kama akitokea Mtanzania mwenye asili ya Kihindi au Kiarabu, amesoma na kuwa na sifa zote, atakubalika na jamii yetu kuwa Raisi? Au tutakuwa bado Xenophobic? Nadhani jibu unalijuwa.
Hujajibu pia, kama Watanzania watakubali wageni wasomi waruhusiwe kufanya kazi na kupewa PR visa/ uraia kama wanavyofanya Kanada, Singapore na Australia kuziba pengo la "skilled labour shortages".
Usikimbilie short cut tu za kutaka Dikteta aje alete maendeleo haraka Tanzania. Jipange.