SINEMA YA I: moja kati ya vitu vya ajabu ambavyo wengi vilitushangaza wiki iliyopita ni kitenda cha raisi na makamu wake kutembelea mahali ''ajali'' ya kuanguka kwa ghorofa kwa nyakati tofauti! sio tu kwamba hiki kilikuwa ni ktuuko bali ilionekana wazi ni kutotumika hekima na tabia ya viongozi wetu kupenda 'misifa'! ntafafanua kidogo..
kitendo cha 'wakubwa' wa nchi kufika tu eneo la tukio kwa wengi tulishuhudiwa kuona kuvurugika kwa zoezi zima la uokoaji kwani attention ilihama kutoka katika uokoaji na badala yake kwenda kwa raisi na baadae makamu wake, huku kila mmoja (wakiongozwa na kamanda kova) akijitahidi kupambanua umahiri na 'ushujaa' wake katika uokoaji! uwepo wao pale haukusaidia badala yake uli slow down juhudi za uokoaji MAONI YANGU ni kwamba raisi angefuatilia kwa makini tukio hili akiwa ikulu (kupisha juhudi za uokoaji) na angeenda eneo la tukio siku moja au mbili baadae..
SINEMA YA II: kuna tetesi kwamba eti kuna tafrija imeandaliwa ikulu kuwapongeza waytu walioshiriki katika uokoaji..
hebu tuwe serios kidogo hivi ni kweli unaweza kutrace kwa usahihi watu wote wale walioshinda pale wakifukua kile kifusi, au hawa watakao alikwa ikulu ni wale wahindi waliotuletea ''vifaru'' vyao pale kutusaidia katika uokoaji... then what??? wapige picha na rais ili iwe rahisi kwao kupata tenda kwenye halmashauri?
while this might seem as a very noble gesture by our president, mimi nadhani rasilimali hizi za muda na fedha za hiyo tafrija kuwekeza katika taifa letu kuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga??? maana kwa hali tuliyo nayo sasa kama tukipata yale majanga ''makubwa makubwa'' kama yale ya wenzetu (vimbuka na matetemeko), ni kudra za mwenyezi mungu tu ndizo zitakazo tuokoa..
hebu tusubiri tuone hii tafrija, na kama itafanyika, hakyamungu ntaamini kwamba ama kweli sasa tumeamua kuwa wendawazimu..