Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Sinema tosha mauaji ya bilionea Msuya

Hili ni jambo kubwa sana ambalo waharifu wengi wanaingia mtegoni kirahisi sana. Simu! Wacha kutupa tu, hata watu wako wa karibu usijaribu kuwasiliana nao kwa namba mpya (hata kama umebadilisha both handset na line). Pona yako ni kuacha kabisa kutumia simu yoyote kufanya mawasiliano na yoyote. Nje ya hapo ukipata polisi wapelelezi smart lazima wakudakue tu.

Na waganga wa kienyeji wengi ni mashushu pia. Kuna mtu aliwahi kunambia hata wachungaji/mapadre ambao tunaweza kuwaamini tukaenda kuungama kwao (kwa namna yoyote ile) wengine ni mashushushu.

Kuepuka yote hayo ni kuwa raia mwema tu.
True. Mi nimemkumbuka Mnajimu Maarufu wa EA!
 
Kubwa unalopaswa kujua siku zote ni kuwa huwa hakuna siri ya watu wawili. Inaweza kudumu kwa muda mfupi au muda fulani lakini lazima itatoka. Sasa idadi yote hiyo ingewezekanaje kutunza siri hiyo. Hata mke mnayekula naye kiapo kanisani siku mkichokana atatoa yote ndio watu watajua kuwa una mikopo na watoto siyo wako ila ni wa rafiki yako kama tulivyoshuhudia juzi ya Muna na Peter kuhusu yule mtoto. Siri huwa ni mtu mmoja basi na wa pili atakuwa ni Mungu. Ndiyo maana huwa nashangaa wanaposema eti siri za serikali. Serikali ni kikundi cha utawala kilichopo kwa muda fulani hivyo hakiwezekani kukawa na siri hasa watunza siri ikiwa ni kwa watu wanaolipwa. Ndiyo maana naamini katika mtiririko huo huo waliomdhuru Lissu ni suala la muda tu tutawajua wote hata kama walirudi kwa msafara wa king'ora. Azori itajulikana tu. Kama makaburi ya halaiki ya miaka ya 40 iliyopita yanajulikana leo itakuwa hao waliompoteza Ben? It's just the matter of time. Time is a very good teacher - Time'll tell
Nadhani msemo wa hakuna siri ya watu wawili umeshapitwa na wakati. Kuna maelfu ya wahalifu waliwahi kufanya uhalifu wakiwa peke yao na siri ikavuja na wakakamatwa! Na kuna wengine wamefanya wakiwa hata watano na hawakukamatwa na wala siri kuvuja. Mimi nadhani hapo issue siyo mko wangapi ila issue ni mko vizuri namna gani katika kutekeleza mpango. Dunia ya sasa yenye teknolojia siyo kama ile ya zamani ya kutegemea mtu aonekane na binadamu mwingine.
 
Imekaa vizuri. Ukweli ni kwamba jeshi la polisi wakikutaka hata ujifiche wapi, watakukamata tu. Ukitaka usikamatwe usitumie cm kabisa.

Kuna kisa kimoja kuna jamaa alikuwa akitafutwa kwa ujambazi na mauaji alikuja kukamatwa kama kuku.
 
Nimewaza tu kuwa, kama hii ingekuwa ya watu wasokuwa na pesa ingefika hapo?
 
Hata mhalifu anatakiwa awe na shule kidogo;hawa walikua hawajui hata ABC ya mawasiliano
 
Kule JI Jamii Intelligence kuna memba anaitwa kwa ID ya D'evils ( km sijakosea ID) miaka ya nyuma humu JF, ( enzi hizo ) aliwahi kutoa Mada ,jinsi gani Mauaji ya kupanga yanatakiwa kufanywa ,hao jamaa ukisoma vzr wanamakosa mengi wamefanya, but all in all big up and big thumps up kwa police na idara zao
 
Back
Top Bottom