Sina uhakika wa kupeleka watoto shule

Sina uhakika wa kupeleka watoto shule

chikambabatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
1,382
Reaction score
1,349
Wadau naelezea masikitiko yangu tu, nikiwa mkulima wa korosho, na mzazi. Muda unasonga, shule karibu zinafunguliwa January 7, na mvua zinanyesha. Sijawaandaa watoto wala shamba.

Kwa ukweli niliwekeza sana kwenye kilimo, na malengo yangu ndani ya miaka 5 niwe na uwezo wa kuvuna si chini ya tani 10.
Alipotanga bei tu ndipo nilipeleka korosho ghala la chama, malipo kimya.

Wawasi wangu korosho huzaa vema zikilimiwa mapema, shule wengine wanasoma "private school" najiuliza kama nitalipwa na kutimiza majukumu Kwa wakati, Shamba ninalo kadri ekari 35, kama malipo baada ya kukagua, naomba waarakishe.
 
Mwambie mzee baba wa magogoni akulipe dusko lako lile ndo jiwe bwana tatizo mlibisha na kushangilia
Mkuu kushabikia swala lingine na kulipa jambo tofauti, nipo serious katika hili, mwanangu hadi anakataa kwenda kanisani kwa kukosa nguo za sikukuu, si jambo Dogo kwangu.
 
Wadau naelezea masikitiko yangu tu, nikiwa mkulima wa korosho, na mzazi. Muda unasonga, shule karibu zinafunguliwa January 7, na mvua zinanyesha. Sijawaandaa watoto wala shamba.

Kwa ukweli niliwekeza sana kwenye kilimo, na malengo yangu ndani ya miaka 5 niwe na uwezo wa kuvuna si chini ya tani 10.
Alipotanga bei tu ndipo nilipeleka korosho ghala la chama, malipo kimya.

Wawasi wangu korosho huzaa vema zikilimiwa mapema, shule wengine wanasoma "private school" najiuliza kama nitalipwa na kutimiza majukumu Kwa wakati, Shamba ninalo kadri ekari 35, kama malipo baada ya kukagua, naomba waarakishe.
Kwa hiyo ukilima mapema korosho utavuna mwaka huo huo ama? We mamluki wa korosho kweli.
 
Ndugu mimi ni mkulima kweli, korosho zinahitaji mengi sana, na shamba ukitibua mapema usaidia kipindi kirefu cha kifuku kupata maji vizuri, ardhi inanywea maji hasa majangwani vinginevyo maua upukutika kipindi cha uzaaji. Katika hili changia ukiwa ufahamu wako,
 
Mie nikajua unapopeleka unalipwa hapo hapo kumbe ni mali kauli!!
 
Mkuu kushabikia swala lingine na kulipa jambo tofauti, nipo serious katika hili, mwanangu hadi anakataa kwenda kanisani kwa kukosa nguo za sikukuu, si jambo Dogo kwangu.
Hats ukiwa na pesa usimnunulie nguo Sikh za sikukuuu,nunua Siku za kawaida.S unaona sasa dogo anakuvuluga akili
 
Mie nikajua unapopeleka unalipwa hapo hapo kumbe ni mali kauli!!
Ni mfumo wa stakabadhi ghalani, ukipeleka wapege mnada ndio waje walipe, ila kwa sasa hamna mnada kwakuwa serikali ilitangaza bei, mikononi inapokea she.3,300/= Kwa kilo moja.
 
Poleni jamani
 
Mkuu kushabikia swala lingine na kulipa jambo tofauti, nipo serious katika hili, mwanangu hadi anakataa kwenda kanisani kwa kukosa nguo za sikukuu, si jambo Dogo kwangu.
Dah kazi kweli usiwazoeshe watoto kuvaa nguo mpya siku za sikukuu wapaswa kujua hilo.
 
Poleni jamani
Haina haja hata ya kuwapa pole hapa jiwe anawafundisha adabu maana msimu uliopita walileta dharau baada ya kupokea malipo yao wakaanza kuwanywisha soda mbuzi wao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jiwe hapendagi ujinga ujinga.
 
Ndugu kama ni kosa, adhabu kutolipwa kwa wakati? Muwe na utu, wajua kuwa, maisha yanaharibika, matokeo ni mabaya sana, yaani nahisi nimekosea sana kushiriki kilimo.
 
Nisamehe mkuu najua nimekukwaza ila lengo langu halikua hilo nilikua najaribu tu kupaka grisi kwenye mioyo yetu ili mradi kupunguza stress tulizonazo maana hata mi mwenyewe ni muhanga na mbaya zaidi sina hata shamba lenye mikorosho miwili ya kusingizia, ki ukweli hali ni mbaya kwa wote ambao mpaka sasa hivi bado hatujalipwa stahiki zetu na wala sioni dalili yoyote mpaka sasa hivi ya kupata haki zetu, ndio maana wenzangu wote wakizunguzia ishu ya korosho hua lazima nitaje mbuzi walivyokunywa soda msimu uliopita ili kuchangamsha baraza na kupunguza dukuduku lililo moyoni mwangu.
 
Back
Top Bottom