Sina imani na Kikwete je wewe bado una imani naye? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sina imani na Kikwete je wewe bado una imani naye?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Mar 14, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kikwete amekuwa madarakani kwa miaka sita. Alipoingiaalipendwa na kila mtu hata maadui zake.Je bado Kikwete ni yule yule au kalewa madaraka na kuharibikiwa? Hii ni kurayangu ya maoni juu ya kukubalika au la kwa Kikwete. Kwa madudu yote kuanziashutuma za kuhusika na EPA, IPTL, Richmond, mkewe kutumia WAMA kujineemesha nauchakachuaji nini maoni yako kuhusiana na mheshimiwa sana huyu?
  Ongeza na jinsi alivyokwenda kutanua wakati watu wanakufakutokana na mgomo wa madaktari pia kupenda kutumia mafweza kwenda kutanua njeakiacha matatizo nyumbani yazaliane.
   
 2. k

  kaka miye Senior Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  sina imani naye hata kidogo
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jinyonge
   
 4. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mi nilipoteza imani naye Tangu alipomfunga Babu Seya.
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hata alipotangazwa kuwa mgombea hapo 2005 sikuwa na imani naye kabisa, hii inatokana na mimi kutokuwa na imani na TANU mpaka CCM.
   
 6. O

  Omr JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtalialia sana mwaka huu mwisho mtanyamaza. Kikwete ndio Rais wa hii nchi na atabaki kuwa rais mpaka hapo 2015 atakapo mkabizi kiti mwanaCCM mwenzake.
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hata kama wewe ukiwa huna imani nae as long as bunge lina imani nae basi kaa kimya.
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,103
  Likes Received: 6,565
  Trophy Points: 280
  na hasa alipowachana madaktari na wanaharakati laivu kwenye hotuba yake
  juzi, ndo nimeishiwa imani naye kabisa.
   
 9. D

  DOMA JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  100% sina imani naye
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  1/40,000,000 ya watanzania ni sawa na kumwaga maji kwa kijiko baharini. Tukiacha majungu na chuki binafsi za makundi mbalimbali kama wanasiasa, wanaharakati na wanaotumiwa kama wewe, JK atabaki kuwa juu.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Thehe thehe thehe, Rais yuko juu bwana majungu yenu tu. Hongera kwa kumkubali JK, 100%=100/100=1. JK juu juu juu zaidi
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kumbe wana-haraka-tu hawachanwi live? kuna siri gani hapo. Big up JK. Sasa nadhani wako katika kikao jamaa zao wa CDM kujadili ulivyowapasha na kupanga namna ya kutoka tena.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Panda juu nenda ukazibe!
   
 14. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni mtu wa majungu, visasi na aliyekosa umakini kwenye mambo yake yote anayoyafanya. Kwa ujumla hajui loloteeeeee!!!! yuko pale ikulu kama picha tu, uwezo wake wa kufikiri umefikia mwisho.

  - Umasikini wa tanzania hajui sababu
  - Umeme yeye siyo mungu hawezi kuleta mvua
  - Posho za wabunge alishindwa kutoa maamuzi akawaacha kwenye dilemma
  - Madaktari hakuna la maana aliloliongea, zaidi sana amekwenda kuweka chumvi kwenye kidonda, n.k.
   
 15. l

  lemikaoforo Member

  #15
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa mada yako nzuri sanaa,licha ya hao wanaomfagilia jk kama wako seriuos basi wanafikiria toka chini
  Tuache majungu na mambo ya makundi nk,ungepewa swali darasani uandike walau mambo mawili ambayo mh jk atakumbukwa pindi atapotoka madarakani ni yapi
   
 16. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Udom na uhuru wa vyombo vya habari mpaka mtu Kama wewe imefikia kumsema vibaya rais wako.
   
 17. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  1. sina imani na Kikwete serikali wala Ccm
   
 18. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  sijawahi kumuamini huty jamaa sishangai anayoyafanya ni maigizo matupu
   
 19. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mambo ambayo baba Mwanaasha atakumbukwa kwayo akitoka madarakani.
  1. Upendo: Mzee huyu ana upendo bwana usipime, akinamama kawakumbukaje! Wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa wilaya, na juzi juzi wakati akijaribu kupanda mlima Kilimanjaro alitamani yule dada Mbotswana awe katibu muhtasi wake.
  2. Upole: Utagamba nini kwa upole wa huyu mzee bojo. Kawasameme wezi wa EPA, kawasamehe wauza unga, kafumbia macho rushwa, hata Sioyi Summari licha ya kukata ngawira mchana kweupe na kuwekewa evidence mezani kammezea na kumpigiaa debe. Mundu nnunu fijo uju.
  3. Utumishi uliotukuka. Yaani katika mwaka; siku 40 likizo (Serengeti), Siku 15 ikulu kuonana na cerebrities, siku 14 ikulu, kupokea mabalozi, siku 30 kuhudhuria vikao vya chama, siku 40 kuhudhuria sherehe mbalimbali nchini, siku 20 kuongoza vikao vya baraza la mawaziri, siku 5 kupitia miswada ya sheria na kuisaini, siku 40 za ziara za ndani ya nchi na kufungua miradi ya maendeleo, siku 160 ziara za nje ya nchi kuhudhuria mikutano mbalimbali, kutafuta wafadhili na mialiko mbalimbali toka kwa nchi marafiki, siku 1 kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka mzima na kutengeneza mpanga kazi wa mwaka unaofuata.
  4. Kwenda na wakati: Rais ni mtaalam wa kupima upepo na kwenda na wakati. Mfano, Jairo scandal, Posho za wabunge, Mgomo wa madaktari n.k
  5. Msema kweli: Rais ni msema kweli sana, kwani ni kweli hajui kwanini watanzania ni masikini. Pia anashangaa kwamba ati Tanzania ni nchi ya kijamaa. Hii Katiba lazima imechakachuliwa sio bure. Pia anawashangaa watu wa Mwanza, ati wanakula mapanki wakati minofu ya samaki imejaa tele, huo ni uongo tu.
   
Loading...