Profesa Karim Hirji: Sina Imani na viongozi wetu (Kikwete akiwemo)!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
203,004
2,000
Mhadhiri: Sina imani na JK

Thursday, 09 December 2010
Na Salim Said

KATIKA hali iliyovuta hisia za wasomi na wanazuoni, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Profesa Karim Hirji amesema hana imani na viongozi wote wa serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Profesa Hirji alitoa kauli hiyo jana katika Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara zilizoandaliwa na Taasisi ya Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kufanyika chuoni hapo.

Profesa Hirji ambaye alikuwa Mwasisi na Mhariri wa kwanza wa Jarida la Cheche lililochapishwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Mstari wa Mbele katika Ukombozi wa Afrika (Usaaf) ya UDSM ambalo alilifungwa na serikali ya awamu ya kwanza, alisema hana imani na rais, mawaziri na wabunge kwa kuwa mioyo yao imejaa ubinafsi, ubepari, ubeberu na ukoloni mamboleo.

Prof Hirji alikuwa Mhariri Mkuu wa Jarida la Cheche ambalo wajumbe wa bodi yake ya uhariri walikuwa Zakia Meghji, Henry Mapolu, George Hadjivyanis na Balozi Christopher Liundi.

Bodi hiyo ya uhariri iliyosambaratika baada ya jarida hilo kufungwa, imetunga kitabu kinachoitwa Cheche kilichocapishwa mwaka huu (2010) ambacho jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wahadhiri wa UDSM (Udasa) Dk Adolph Kibogoya.

Kitabu hicho chenye sura 12 na zaidi ya kurasa 200 ambacho dhana yake kuu ni kuendeleza mawazo ya gazeti la Cheche ya kuendeleza mapambano ya kweli ya ukomboi wa Afrika kimeandikwa na watu mbalimbali akiwemo Profesa Hirji, Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Wengine ni Prof Hajivayanis, Mapolu, Liundi na Zakia Meghji aliyeandika Sura ya Sita ya kitabu hicho kuhusu historia ya Zanzibar na fikra za kimapinduzi ambazo baadhi ya Wazanzibari walijengeka kwazo.

Akizungumza katika hafla hiyo Profesa Hirji alisema: “Leo kiongozi wa nchi (Kikwete) anasema eti ili aweze kuwapatia wananchi vyandarua lazima twende kuomba msaada Marekani. Mimi naona hilo ni jambo la aibu kubwa".

Aliongeza: “Baada ya kuangalia mambo haya kwa muda mrefu, mimi binafsi nimepoteza imani na viongozi wetu wote nchini na katika bara la Afrika. Nimepoteza imani na marais, mawaziri, wabunge na viongozi wengine wote wa kisiasa, kiuchumi na kijamii".

Ingawa Profesa Hirji hakumtaja kiongozi yeyote, mifano yake imeonyesha kuwa amekuwa akiilenga serikali ya Rais Jakaya Kikwete iliyokuwa madarakani tangu mwaka 2005.

Profesa Hirji ambaye amewahi kufundisha UDSM katika miaka ya 1960, baadaye aliwageukia wasomi wenzake akisema nao wametawaliwa na ubinafsi, ubepari, ubeberu na ukoloni mambo leo.

Alisema katika jamii yenye matatizo mengi kama Tanzania, kazi kubwa ya wasomi ni kutumia taaluma na ujuzi wao kuonyesha njia zinaoweza kuleta ukombozi na maendeleo lakini hali hiyo ni tofauti kwa Tanzania ambako wasomi wanajali zaidi maslahi binafsi.

“Sisi wasomi wa Tanzania kwa sababu tumetawaliwa na fikra na vitendo vya ubinafsi, ubepari na ukoloni mambo leo, tumeamua kukaa kimya,” alisema Profesa Hirji na kuongeza:

“Tunakimbilia marupurupu ya wahisani, kamwe hatuna moyo wa kujitolea na kujenga nchi. Hata ukiitisha mkutano wa wasomi bila ya kutoa posho na marupurupu au chakula, hakuna atakayehudhuria”.

Huku akishangiliwa na kupigiwa makofi na mamia ya watu waliohudhuria sherehe hiyo, Profesa Hirji aliendelea kusema: “Hata kama tunahudhuria mikutano katika hoteli za kifahari, matokeo yake hayana maana yoyote katika maendeleo ya jamii.”

Alisema maprofesa na wahadhiri wa vyuo vikuu, wanavaa suti na tai lakini mawazo yao kwa kiasi kikubwa, yamepitwa na wakati.

“Ndio maana mimi binafsi pia nimepoteza imani na wasomi wetu waliopata shahada za juu, maprofesa, wahadhiri na viongozi wa vyuo vikuu waliopo hapa na wasiopo. Nawaheshimu lakini sina imani na kazi, tafiti na uongozi wao," alisema Profesa Hirji

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maprofesa na wahadhiri kutoka vyuo mbalimbali nchini, Profesa Hirji alisisitiza kuwa hawezi kuwategemea kabisa kuelekeza nchi katika njia ya kujitegemea, kujenga usawa, kulinda haki za watu wa kawaida na kuleta maendeleo halisi na ya haraka.”

“Mawazo yetu (wasomi) yametawaliwa zaidi na njia za kujilimbikizia mali. Tafiti zetu ni za kijuujuu. Tunafundisha mambo ya kuigaiga na hata kazi ndogo kama hizi wengi tunakwepa kuzifanya swasawa," Prof Hirji alisema na kuongeza:

“Sioni msomi anayeuliza maswali magumu, anayekosoa mfumo wa ubepari na ukoloni mamboleo, anayesema wazi kuwa ujamaa ndio njia pekee ya kuleta amani, haki na maisha ya Watanzania, kama wapo ni mmoja au wawili.”

Profesa huyo alisema mambo hayo yanahitaji kufikiriwa kwa undani, kufanyiwa utafiti na uchunguzi wa dhati wa kitaaluma na kwamba kama wasomi hawatakuwa mstari wa mbele katika jukumu hili, hakuna atakayelifanya.

Hata hivyo, Profesa Hirji alisema hajapoteza imani na kundi kubwa la vijana nchini akiamini kuwa wana mioyo na mwelekeo safi ambao haujachafuliwa na fikra na vitendo vichafu vya ubepari na ukoloni mamboleo.

“Ndio maana naona ni jukumu lao kuungana, kujielimisha kwa nguvu zao zote, kuanzisha vikundi vya kujisomea na kuanzisha magazeti yatakayochambua ukweli wa mambo, kuuliza maswali magumu na kufafanua mbinu za kujikomboa kwa wananchi,” alisema.

Awali profesa Hirji alitaja misingi ya Gazeti la Cheche kuwa ni pamoja na ukombozi halisi wa Afrika hauwezi kupatikana bila ya siasa ya vitendo ya ujamaa. “Tanu chini ya Nyerere ilikuwa na maneno matamu lakini ilikuwa na mapungufu mengi katika vitendo. Cheche ya leo pia inasema hayohayo.”

Msingi wa pili alisema ulikuwa ni ukombozi halisi wa Afrika utapatikana kwa jasho na juhudi Waafrika wenyewe na sio mabepari.

“Hatuwezi kutegemea mabepari na mabeberu katika hili. Siku hizi wanaitwa wawekezaji na wahisani, huo ni udanganyifu, hao wote wanataka kuendelea kuiba rasilimali zetu. Lazima tuungane na kuwaondoa mabeberu wanaoiba mali zetu,”alisema.

Alifafanua kuwa, msingi mwingine wa Cheche ya zamani ni kuheshimu ukweli na kusema ukweli bila kumwogopa au kumhofia kiongozi au mtu yeyote kwa maslahi ya maendeleo ya taifa.

“Msingi wa nne wa Cheche ya zamani ulikuwa ni kujitegemea na msingi wa tano ulikuwa ni umuhimu wa kujielimisha katika masuala na fikra za kisayansi na ukombozi,” alisema Hirji.

Kwa upande wake aliyekuwa Mhariri wa Jarida hilo Zakia Meghji alimpongeza Profesa Hirji kwa hotuba yake hiyo na kusema ameonyesha kutobadili msimamo aliokua nao tangu alipoanzisha jarida hilo.

“Hongera profesa Hirji Wewe ni yule yule wa miaka 1960,” alisema Meghji.

Mshiriki wa sherehe hiyo Dk Salim Msoma aliyepewa nafasi ya kufanya mapitio ya kitabu hicho alipinga baadhi ya mambo katika kitabu hicho akisema yanapotosha vijana.

Alisema katika sura ya kwanza ya kitabu hicho cha Cheche, mwandishi ambaye ni Prof Hirji amezungumzia dunia ya ujamaa huku akizigusa nchi za Urusi na China.

“Katika hili mimi napinga kabisa. Hakuna kitu dunia ya ujamaa hivi kuna mjadala mkali katika hili. Wasomi wameandika vitabu vingi kuhusu jambo hili kwa hiyo mambo kama haya yanaweza kupotosha na kudanganya vijana wetu,” alisema Dk Msoma.
 

MashaJF

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
246
195
Hongera kwa Prof kaongea neno. Ni wakati wa kuelezana ukweli ili tulete maendeleo ya nchi. Hiki kitabu kinapatikana wapi? Nahitaji nakala yake ndani ya wiki hii, jamani ukiona "bookshop" kinapopatikana tujilishane. Nitaanzia kukisaka "bookshop ya UDSM".

Kuhusu Ujamaa una uhuru wa kutoa maoni yako, japo si lazima tukubaliane na yote.
 

We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
195
Bila shaka mawazo ni mazuri, lakini baadhi ya members wa Cheche ninawasiwasi nao. Au ndio waliomchoma Prof. Hirji na kulifunga jarida?
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,952
2,000
Mijadala kama hii inasaidia sana kujenga kizazi chetu kinachokua ambacho hakina na hakijui history wala mifumo.....wao wametekwa na wimbi kubwa la utandwazi....inasaidia sana kufanya wengi wajue tulitoka wapi na kwa nini kosa lilikuwa wapi....hadi tupo hapa leo iwe rahisi sasa kuamua tufanye nini na nani wa kutufanyia!!
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
203,004
2,000
Mijadala kama hii inasaidia sana kujenga kizazi chetu kinachokua ambacho hakina na hakijui history wala mifumo.....wao wametekwa na wimbi kubwa la utandwazi....inasaidia sana kufanya wengi wajue tulitoka wapi na kwa nini kosa lilikuwa wapi....hadi tupo hapa leo iwe rahisi sasa kuamua tufanye nini na nani wa kutufanyia!!

Penye ukweli uongo hujitenga.....................
 

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,325
2,000
mh habari imeandikwa vizuli ila ikiwa presented na mlevi hata kusoma inakuwa ngumu,huwezi kuweka space watu wasome vizuri?
duuh
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,213
2,000
Zakhia Meghji...!!
Prof.Hirji ameongea maneno mazito sana, ambayo ndiyo ukweli halisi unaoing'ata Tanzania kwa sasa...Huyo niliyemtaja hapo juu ni katika mifano mizuri kabisa ya wasomi na wanataaluma ambao ni wabinafsi kupita kiasi, ambao hata hawakutakiwa kuwamo kwenye list ya kutoa mchango wao katika kitabu hicho, na amechangia nchi hii kuwa hapo ilipo sasa!!
 

kambipopote

Senior Member
Nov 15, 2010
122
195
Zakhia Meghji...!!
Prof.Hirji ameongea maneno mazito sana, ambayo ndiyo ukweli halisi unaoing'ata Tanzania kwa sasa...Huyo niliyemtaja hapo juu ni katika mifano mizuri kabisa ya wasomi na wanataaluma ambao ni wabinafsi kupita kiasi, ambao hata hawakutakiwa kuwamo kwenye list ya kutoa mchango wao katika kitabu hicho, na amechangia nchi hii kuwa hapo ilipo sasa!!
Huyo mama ni fisadi hana lolote nadhani walimshirikisha kwa sababu tu ni mmoja wa waasisi wa Cheche, nadhani hata yeye nafsi ilimsuta sana wakati wa maadhimisho ya uhuru mwaka huu. Unajua huwa inakera sana kuongea mambo ambayo unajua huyatendi na unajua kuwa hata jamii inatambua hivyo. Nahisi alifedheheka saana. Natamani ningekuwepo nimuangalie anavyo jiuma uma:angry:
 

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Profesa Hirji ambaye alikuwa Mwasisi na Mhariri wa kwanza wa Jarida la Cheche lililochapishwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Mstari wa Mbele katika Ukombozi wa Afrika (Usaaf) ya UDSM ambalo alilifungwa na serikali ya awamu ya kwanza, alisema hana imani na rais, mawaziri na wabunge kwa kuwa mioyo yao imejaa ubinafsi, ubepari, ubeberu na ukoloni mamboleo.

Professor Mbona umeniibia zaidi ya nusu ya maneno sahihi yanayoelezea sababu za mimi kuwachukia hawa jamaa!!!! Hakika kila nikiwakumbuka rohoni najisikia tu HARUFU YA DAMU.

Hawa jama na wala hua hawatambui UHURU WA WANATAALUMA kusoa kadri wanavyoweza alimradi wanaonyesha EVIDENCE kama ambavyo umeonyesha hapa. Kwa mwenye akili, atachukua sehemu hiyo alimokosolewa na wasomi na kuyafanyia kazi ili kuongeza ufanisi zaidi lakni kwa wengine utaona hata zile GHARAMA za kumpata PROFESA mmoja katika taifa wala haziwaingii kichwani. Badala ya kufanyia kazi wazo la msomi mara utasikia ni msomi husika mwenyewe ndio kafanyiwa kazi.

Professors Chachage, Othman, na wengine wengi, naweza nikatabiri kwa kipindiki hiki tunapodai katiba mpya nyinyi mgekua mnatema cheche za aina gani hapa. Hata hivyo juzi nilifarijika sana na wenzenu wengine machachari balaa nao hapa!!

 

kingmaker

Member
Oct 21, 2010
51
70
Ingawa ni article nzuri ila cha ajabu, Prof. Hirji mwenyewe ni marehemu na alifariki Arusha mwanzoni mwa mwaka sasa huyo aliyeongea haya maneno sijui ni Prof. Hirji gani? I cants stand uandishi wetu wa nyumbani..pengine aliyesema haya maneno ni Prof. Shivji! Shame on the journalist, inabidii uiombe familia nzima ya Prof. msamaha!
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,068
1,250
The target was Kikwete, Mukandara, Bana and their co-pilot members in corruption!
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,071
2,000
Watu wengi hapa nyumbani tumezoea kumsoma na kumsifia sana Professor Issa Shivji lakini huyu mwingine Karim ni msomi mahili na mchambuzi safi wa mambo ya kijamii lakini kwa hulka yake ni mtu mkimya sana na mara nyingi hajitokezi hadharani ; lakini pale anapojitokeza kutema cheche wakina Mahmood Mamdani, Yash Tandon na hata shemejie Issa Shivji hupenda kujumuika naye.

Ni msomi adimu ambaye ni mkweli kwa fani yake na pia kwa nchi yake na zaidi ya yote sio mnafiki; asingekuwa hivyo akili alizonazo hivi sasa angekwisha lowea marekani. Hongera sana Karim kwa uzalendo wako!!
 

mapambano

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
535
0
Hongera Prof Hirji, Prof Hajivayanis, Mapolu, Liundi na Zakia Meghji kwa mchango wenu katika taifa hili. Your struggles did not start today no did it end. I hope the younger generation will learn from these struggles and carry on this spirit.
 

mapambano

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
535
0
Ingawa ni article nzuri ila cha ajabu, Prof. Hirji mwenyewe ni marehemu na alifariki Arusha mwanzoni mwa mwaka sasa huyo aliyeongea haya maneno sijui ni Prof. Hirji gani? I cants stand uandishi wetu wa nyumbani..pengine aliyesema haya maneno ni Prof. Shivji! Shame on the journalist, inabidii uiombe familia nzima ya Prof. msamaha!

mwandishi anaongelea Prof Karim Hirji sio Prof Hirji (marehemu) unayemuongelea wewe. Ni majina yanafanana
 

mapambano

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
535
0
African Books Collective: Cheche. Reminiscences of a Radical Magazine

Cheche. Reminiscences of a Radical Magazine Edited by Karim Hirji

Cheche, a radical, socialist student magazine at the University of Dares Salaam, first came out in 1969. Featuring incisive analyses of key societal issues by prominent progressives, it gained national and international recognition in a short while. Because it was independent of authority, and spoke without fear or favor, it was banned after just a year of existence.

The former editors and associates of Cheche revive that salutory episode of student activism in this book with fast-flowing, humor spiced stories, and astute socio-economic analyses. Issues covered include social and technical aspects of low-budget magazine production, travails of student life and activism, contents and philosophy of higher education, socialism in Tanzania, African liberation, gender politics and global affairs. They also reflect on the relevance of past student activism to the modern era.

If your interests cover higher education in Africa, political and development studies, journalism, African affairs, socialism and capitalism, or if you just seek elucidation of student activism in a nation then at the center of the African struggle for liberation, this book presents the topic in a lively but unorthodox and ethically engaging manner.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,544
2,000
Kumbe si bure vijana wa zamani kama kina Prof. Hirji, Jenerali Ulimwengu au mwanamuziki Patrick Balisidya wa Afro 70 band wote walielewa kuwa Ukombozi wa Mwafrika utaletwa na sisi wenyewe Watanzania.

Inaonekana miaka hiyo ukiwa msomi unaandika ktk kijarida cha CHECHE, ukiwa mwandishi wa habari kama Jenerali Ulimwengu unamwaga ujumbe huu muhimu ktk makala zenye vina ktk magazeti au ukiwa mwanamuziki kama wana Afro 70 Band mnatunga wimbo wa kimapinduzi kuwazindua waafrika na watanzania kuwa kila kitu ki- mikononi mwetu tukitaka maendeleo na uhuru wa kiuchumi, kifikra n.k sikiliza ujumbe huu wa afro 70 wa dakika tatu tu:

Patrick Balisidya And Afro 70 Band-UKOMBOZI WA AFRIKA

Kwa kumalizia wawapi watu kama hawa( wa miaka ya 1960/70) zama hizi, kweli kama Prof. Hirji alivyosema naona sisi wana JF ndio tunaowapa angalau matumaini vijana wa zamani kuwa tunachambua kile kinachoendelea sana ktk jamii yetu na kujaribu kupata majibu ya kuharakisha maendeleo ya Mwafrika na Mtanzania.

Wana-JF tuendeleze hizi harakati za kujikomboa mpaka kieleweke.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom