Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,069
UONGOZI unapimwa kama redio. Ukikosea masafa (frequencies) utasikia mawimbi au redio itakoroma. Ukiyapatia masafa, sauti itasikika barabara. Hakutakuwa na mawimbi wala kukoroma.
Kama ambavyo redio hutoa sauti za mawimbi (waves) na kukoroma pale inapokosewa masafa au upatikanaji wake kuwa wa shida kutokana na Jiografia (umbali na mazingira ya eneo), ndivyo na uongozi huzalisha manung'uniko kwa wananchi makosa yanapofanyika.
Mtu wa Mungu, Khalifa Omar bin Khattab (Khattwab), nyakati za uongozi wake alionesha namna ambavyo kiongozi anapaswa kuhusika kiuongozi. Hii ni baada ya kifo cha Mtume Muhammad (S.A.W) na Khalifa wa kwanza, Abdullah ibn Abi Quhaafah, almaarufu Abu Bakr Siddiq.
Omar nyakati za usiku, alikuwa anazunguka kwenye nyumba za watu na kutega sikio madirishani na milangoni, kusikiliza kile ambacho wananchi walikuwa wanazungumza kuhusu utawala wake. Mtindo huo ulimsaidia Omar kutatua kero nyingi za watu wake ambao walimpenda sana.
Ndani ya Biblia, soma Joshua umuone alivyotukuka kiuongozi. Joshua alionesha kuwa kiongozi lazima awe mtumishi wa watu. Na mtumishi huzingatia matakwa ya watu wake, hujiepusha na yale yenye kuwatia hofu. Kiongozi huongoza kwa kuwaondoa hofu watu wake.
Soma Torati uone jinsi kiongozi wa watu Musa alivyopambana kuwaokoa wana wa Israel mikononi mwa Pharaoh. Unapata picha timilifu ya namna ambavyo kiongozi anapaswa kuhusika kwa watu wake.
Mafanikio ya Omar, Joshua na Musa katika uongozi wao, ndiyo kutimia kwa dhana ya legitimacy ambayo inafundishwa katika somo la Sayansi ya Siasa (Political Science), ikibeba tafsiri ya ridhaa ya watu kwa mamlaka inayowaongoza. Yaani imani chanya ya wananchi kwa viongozi.
Legitimacy ni baraka ya wananchi kwa mamlaka na ni matokeo ya viongozi kufanya au kuonesha dalili ya kutimiza matarajio ya wengi.
Legitimacy ni uongozi shirikishi, yaani mwananchi wa kawaida ajione ndani ya uongozi uliopo madarakani. Uamuzi wa uongozi uwe unaakisi moja kwa moja matakwa ya wananchi walio wengi.
Yapo mambo sita ambayo hufanikisha kuiweka hai legitimacy katika uongozi wowote uleule. Zingatia kuwa legitimacy siyo tu uongozi wa nchi, unahusika pia kwenye taasisi mbalimbali kwa wafanyakazi na menejimeti, vilevile katika familia.
MOSI; Kwamba kiongozi anawaongoza watu kuelekea kwenye kesho yao ambayo wanaiamini kwa pamoja kuwa ina thamani kwao.
PILI; Kwamba uongozi unawasisimua wananchi katika njia ambayo ni shirikishi kwa kila mmoja.
TATU; Kwamba uongozi unakuwa imara katika kutimiza malengo na unanyumbulika kwa umahiri mkubwa pale kunapotokea vikwazo au changamoto zenye kutengeneza nafasi (gape) kati ya uongozi na wananchi.
NNE; Kwamba kiongozi hamezwi na maslahi binafsi au kutingwa na upofu wa mamlaka. Kiongozi mwenye kiburi cha mamlaka hupoteza legitimacy mapema.
TANO; Kwamba kiongozi anatunza na kusimamia thamani na viwango alivyopewa na wananchi wake.
SITA; Kwamba kiongozi anaheshimu kuwa mamlaka aliyopewa na wananchi siyo haki yake ya kuzaliwa, bali ni zawadi tu, hivyo badala ya mamlaka kumjengea kiburi, yamfanye awe mnyenyekevu kwa wananchi.
Ongezea na pointi hii; Kiongozi mtunza legitimacy ni yule ambaye hugombana na wasaidizi wake kwa maslahi ya wananchi wa kawaida walio wengi.
Mwanafalsafa wa Kiingereza, John Locke aliyeishi kuanzia muongo wa nne wa Karne ya 17 mpaka mwanzoni mwa Karne ya 18, aliwahi kuandika katika andiko la Consent of the Governed (Ridhaa ya Anayeongozwa) kwamba mamlaka yoyote haina legitimacy mpaka ipate ridhaa ya wananchi kwa kila uamuzi.
Mwanafalsafa wa Kijerumani, Jurgen Habermas mwaka 1973 alianzisha dhana inayoitwa Legitimation Crisis (Mgogoro wa Ridhaa), kwamba ni kuondoka kwa imani ya wananchi kwa mamlaka.
Mtaalam wa falsafa za sayansi, jamii na siasa, Aristotle, aliyeishi Karne ya nne mpaka mwanzoni mwaka Karne ya Tatu Kabla ya Yesu Kristo (BC), katika kitabu chake alichokiita Politics, alisema kuwa serikali hupoteza uimara wake kama itatenda vitu ambavyo watu watatafsiri kuwa siyo haki.
Aristotle anachambua legitimacy kuwa hubebwa na misingi ya utawala wa sheria (rule of law), ridhaa ya hiari (voluntary consent) kati ya mamlaka na wananchi, vilevile kuzingatia maslahi ya umma (public interest).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, aliingia ofisini katika hali ya mshikemshike, vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vilipinga ushindi wake.
Hii ina maana kuwa Dk Magufuli hakuanza kazi akiwa na legitimacy ya asilimia 100. Mitaani ilinong?onwa kuwa ushindi wake ni matokeo ya wizi wa kura. Kwamba aliyepaswa kushika usukani ni Edward Ngoyai Lowassa.
Hoja ya Magufuli kushinda kwa wizi wa kura ilikuwa mbeleko tu ya kisiasa, kwamba tumeshindwa lakini lazima tuwe na kisingizio. Vipo viashria vingi kuthibitisha uhalali wa ushindi wa Magufuli. Kwa kuweka pembeni ubishani huo, tuushike ukweli kuwa ilimchukua wiki moja tangu kuapishwa kwake, kuanza kuwageuza wale waliokuwa wakiamini kwamba ushindi wake haukuwa halali, kisha kugeuka na kuanza kumshabikia.
Novemba 20, mwaka huu alipohutubia bunge, aliongeza wigo wa legitimacy. Shughuli iliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam, kuibua madudu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, vigogo mbalimbali waliofanikisha utoroshwaji wa makontena na ukwepaji kodi, vilifanya uongozi wa Magufuli kugeuka tumaini pekee la Watanzania.
Kutokana na kasi ambayo ilioneshwa, ghafla ikageuka fasheni kumshangilia Magufuli. Ipo orodha ndefu ya watu waliokuwa wanampinga Magufuli, baadaye waligeuka washangiliaji na watetezi wake. Hali ya hewa ilibadilika kiasi ambacho kuonekana unampinga Magufuli ilikuwa haramu, sawa na Muislam safi kumlisha nguruwe.
Unaanzaje kumpinga Magufuli mbele za watu? Aligeuka kuwa nyota wa nchi. Siyo vizuri kuzungumza kauli hii lakini ni ukweli kuwa uwajibikaji wa Magufuli ndani ya muda mfupi, ulisababisha viongozi waliopita waonekane hawakuwa na viwango. Habari Magufuli. Furaha Magufuli. Amani Magufuli. Matarajio Magufuli. Matumaini Magufuli!
Sidhani kama Magufuli amewahi kuvimba kichwa kutokana na kukubalika na wananchi. Hivyo, nahitaji kumfahamisha kuwa mitaani yeye ndiye mtu bora mno kwa nyakati za sasa. Wanampenda na wanamtarajia kwa mambo mengi.
Mtanzania wa kawaida anaishi kwa chuki. Hasira zao ni watu wachache ambao wamekuwa wakionekana kuwa wanufaika wakuu wa rasilimalia za nchi. Watanzania huibeba vita ya ufisadi kwa hasira na jicho baya dhidi ya wenye nacho.
Zile zama za mtumishi wa umma kufanikiwa kwa haraka na kuitwa mwenye akili zimekwisha. Mtanzania amebadilika, imani yake kwa sasa ni kuwa mtumishi wa umma kupata mafanikio ya haraka ni wizi, ni ufisadi.
Mabadiliko haya ya kihisia kwa Mtanzania, huwezi kuyasema bila kusifu uwazi uliotengenezwa na Serikali ya Rais wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete. Uwazi katika ukaguzi wa serikali na meno ya kibunge, vilisababisha matukio kadhaa ya ufisadi kuwekwa kweupe.
Kazi nzuri iliyofanywa na Rais Kikwete haikuweza kusaidia kumpa legitimacy, badala yake watu walijenga chuki kuwa lipo kundi kubwa la watu ambao wao kazi yao ni kufilisi nchi. Serikali ya Rais Kikwete iliwezesha mafisadi wengi kugundulika. Hata hivyo, kasi ndogo ya kuwashughulikia, ilifanya waonekane wanalindwa. Chuki ya wananchi iliongezeka zaidi. Walichukia kwamba vigogo hawaguswi.
Magufuli anakumbuka kuwa wakati anajinadi kuomba urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wapinzani wake hawakuwa na hoja nzito za kuwaaminisha wananchi kuwa yeye hafai, hivyo hoja kubwa ambayo ilibebwa ni kwamba CCM ni mfumo, na Magufuli angeendeleza yaleyale.
Kitendo cha Magufuli kuja tofauti na kuonesha dhamira ya dhati ya kuwashughulikia mafisadi, kililazimisha hata waliokuwa wanampinga wageuke washangiliaji wake. Unaachaje kumshangilia mtumbua majipu? Mtu anayewanyoosha wala nchi?
Hili lazima lifahamike kuwa Magufuli anashangiliwa kwa sababu Watanzania wengi ni maskini. Maisha yao ni magumu mno. Mahitaji yao ya kila siku yanawashinda. Lakini wanawajua wenzao ambao wanatumia fedha kwa kufuru kama wanamiliki mashamba ya miti ya fedha.
Hivyo, Mtanzania anapobaini kuna watu wanaiba mabilioni kwa siku, anapata hasira. Anaona kumbe ugumu wa maisha yake unasababishwa na hao. Anapotokea mtu anawashughulilkia wezi wenye kuchukiwa na wengi, lazima ageuke kipenzi cha wengi.
Ni sababu kubwa kwamba Magufuli aligeuka kipenzi cha mamilioni ya Watanzania wanaoishi kwa shida lakini hajawahi kuwa kipenzi cha vigogo serikalini wala wafanyabiashara wakubwa. Unapokubaliana na hoja hiyo, sasa tunaweza kukubaliana kuwa Magufuli amependwa na wengi kwa sababu ya kushughulikia kero kwa kundi kubwa la wengi. Kiongozi unapopendwa na wengi, maana yake unakuwa na legitimacy.
Nilitarajia kuona Magufuli akitunza legitimacy. Nilipenda kuona anaendelea kushikilia unyenyekevu wake kwa Watanzania. Nilitamani kuona hali hiyo imekuja kama bahati hivyo kushikilia pale palipompa thamani aliyonayo.
Kwa yote hayo, niliamini yeye ni binadamu na anaweza kuteleza wakati wowote. Ila ningependa ateleze kwa bahati mbaya, siyo kwa kuamua. Watu wanaokupenda sana ukiwaangusha, upendo hugeuka chuki. Magufuli ni msomi na hili analijua. Sijui kwa nini hajazingatia.
Mtanzania wa leo, anaweza kumtetea askari wa usalama barabarani anayepokea rushwa lakini siyo fisadi serikalini. Kibaka wa mtaani anaweza kupona lakini siyo vigogo wanaochezea rasilimali za nchi.
Ni sawa na kusema kuwa asilimia kubwa ya Watanzinia hawana radhi na Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo, kutokana na kumbukumbu ya ufisadi mkubwa uliofanyika Benki Kuu ya Tanzania kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.
Hakuna namna yoyote ile ambayo inaweza kufanyika kumuondoa Muhongo kwenye kashfa ya ufisadi wa shilingi bilioni 320 za Tegeta Escrow. Zaidi ya yote, Muhongo anastahili kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi kutokana na ufisadi mkubwa uliofanyika.
Kuweka kumbukumbu sawa; Novemba 2014, Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilifanya kazi kubwa ya uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Ripoti ya CAG ilionesha kuwa zaidi ya shilingi bilioni 320 za mgogoro katika Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), zilichotwa bila kufuata utaratibu.
Pan Africa Power Solutions Ltd (PAP) ambayo uhalali wake haupo, ikisajiliwa nchini kwa ?wiziwizi? tu, kisha kujitambulisha kama wamiliki wa hisa saba (asilimia 70) za IPTL, ilizonunua kutoka Kampuni ya Menchmar ya Malaysia, ikachotewa fedha na kukabidhiwa.
PAP ikatumia fedha hizohizo za mgogoro (shilingi bilioni 320) kununua hisa za kampuni mshirika wa IPTL, VIP Engineering & Marketing Ltd.
Niliwahia kutolea mfano wa mauziano ya hisa za IPTL, sawa na wamiliki wawili wa duka, mmoja kukubali kuuza umiliki wake kutokana na faida waliyopata, badala ya kugawana kwanza faida, kisha mauziano ya umiliki yafanyike kutokana na mtaji wao.
Upande wa pili hakuna mwenye uhakika kama kweli Menchmar imeuza hisa zake kwa PAP. Maelezo yaliyopo ni kuwa PAP ilinunua hisa za Menchmar kutoka Kampuni ya Piper Link.
Mwanasheria wa Tanesco aliyekwenda Malaysia kufanya uchunguzi wa kujiridhisha, alirudisha majibu kuwa PAP siyo kampuni inayotambulika na kwamba mmiliki wake, Harbinder Singh Sethi ndiye huyohuyo mmiliki wa Piper Link.
Skendo ya Tegeta Escrow inaonesha kuwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema ndiye hasa aliyeivalia kibwebwe kuhakikisha fedha zinatolewa Benki Kuu na kulipwa kwa PAP, kwamba Tanesco wala Serikali ya Tanzania hawakuwa na chao.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alionesha shaka ni kwa nini PAP wapewe fedha hizo, tena bila hata kukatwa kodi. Baada ya siku nne, akalainika na kugeuka mtetezi wa fedha hizo kulipwa. Maswi alilainishwa na nini?
Muhongo ndiye aliyesimama bungeni na kusema zile fedha za Tegeta Escrow hazikuhusu Tanesco na kwamba ni za wanahisa wa IPTL. Majibu yakawa kuwa Muhongo alisema uongo na alilidanganya bunge kwa sababu Tegeta Escrow ilifunguliwa ili kupisha maridhiano kuhusu mgogoro wa tozo kubwa la gharama za umeme kati ya Tanesco na IPTL. Hapa Muhongo anakutwa na kashfa ya kusema uongo. Kulidanganya bunge na kupotosha umma.
Kosa la pili, Muhongo ndiye alitamkwa kuwa dalali wa mauziano ya hisa kati ya PAP na VIP. Ilielezwa na CAG kisha kushereheshwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa aliwakutanisha Singh na James Rugemalira (mmiliki wa VIP), kwenye ofisa ya Waziri wa Nishati na Madini.
Kosa la tatu, udanganyifu ambao ulifanyika wa PAP kusajiliwa nchini ?kimagumashi?, ulisababishwa na uzembe wa Muhongo, kushindwa kutumia mamlaka yake ya Waziri wa Nishati na Madini, kuifanyia PAP uchunguzi wa kujiridhisha (due diligence).
Kumbuka pia kuwa Rugemalira baada ya kupokea malipo yake, aligawa fedha nyingi kwa viongozi mbalimbali serikalini. Profesa Anna Tibaijuka, anaendelea kutafunwa na matokeo ya kupokea fedha za Tegeta Escrow kama ilivyo kwa Andrew Chenge, William Ngeleja na wengineo.
Bado tunazo kumbukumbu kuwa CAG alieleza kuwa fedha za upande wa Rugemalira zilizogawanywa kupitia Benki ya Mkombozi, ni kiasi kidogo lakini ndipo majina ya walionufaika na mgawo yalipatikana. Ilielezwa na PAC kuwa fedha nyingi zaidi ziligawiwa kupitia Benki ya Stanbic, kwamba wanufaika wa mgawo huo walitorosha mabilioni na mamilioni kwa mifuko ya sandarusi, lumbesa, viroba, magunia na kadhalika.
CAG alitoa taarifa hiyo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ilieleza pia kuwa inafanyia kazi majina ya walionufaika na mgawo wa Tegeta Escrow kupitia Benki ya Stanbic ambao majina yao hayajawahi kuwekwa wazi.
Kimsingi Tegeta Escrow ni kashfa nzito, ni wizi mkubwa mno uliofanyika. CAG, Takukuru na bunge, walitoa maelezo yenye kuuaminisha umma kwamba wizi na uzembe mkubwa ulifanywa na Muhongo.
Watanzania wengi hawana imani na Muhongo, ndiyo maana waliridhika aondolewe kwenye wizara hiyo. Kitendo cha Magufuli kumrejesha tena, siyo tu kwamba kimewaudhi wananchi bali yeye mwenyewe anachezea legitimacy. Na Muhongo anaposemwa hafai, hakuna maana ya chuki za vitalu vya uvunaji wa gesi asilia. Kilichomgharimu ni makosa aliyoyafanya akiwa chini ya Rais Kikwete, kusababisha uchotwaji wa fedha za Tegeta Escrow.
Wakati tukijenga hoja hii, ifahamike kuwa ipo kumbukumbu ya kibunge (hansard) ya mahojiano kati ya CAG na Muhongo na ndani yake, Muhongo akikiri kwa sauti kuwaunganisha Singh na Rugemalira.
Pengine Magufuli ameona kwa sababu anakubalika sana, kwa hiyo anaweza kufanya anavyotaka. Hapo anakuwa anafanya makosa makubwa sana. Kosa moja linaweza kubadili legitimacy kuwa legitimation crisis (rejea tafsiri zake hapo juu).
Kosa alilolifanya Magufuli, nalifananisha na mgema kusifiwa kisha tembo kulitia maji. Mapenzi makubwa ambayo anayapata kwa Watanzania, analazimika kwenda nayo kwa unyenyekevu. Yakimjengea kiburi, gharama yake ni kubwa mno.
Nilipita mitaani nikazungumza na kusikiliza maoni ya watu kuhusu uteuzi wa Baraza la Mawaziri, wengi walioneshwa kushangazwa na wapo walisema ni yaleyale ya awamu iliyopita kama Muhongo amerudishwa.
Watanzania wengi walitegemea Mugufuli atachukua Maazimio 8 ya Bunge la 10 kuhusu kashfa ya Tegeta Escrow na kwenda mbele kutoka pale ambapo Rais Kikwete aliishia.
Waliobeba fedha Stanbic kwa magunia ni akina nani? Uchunguzi unapaswa kuendelea kufanyika na matokeo yaonekane. Muhongo alikuwa mtetezi namba moja wa wizi uliofanyika na zaidi alikutwa na hatia ya kufanikisha mchongo wote.
Magufuli asilione la Muhongo ni dogo, yupo kiongozi aliyepata kuitwa Masiha wa Afrika, Muammar Gaddafi. Pamoja na kufanya mambo mengi mazuri mno kwa wananchi wake wa Libya lakini alifanya kosa moja tu, kuwaruhusu watoto wake kuishi maisha ya kifahari kuliko hali halisi ya Walibya wengine.
Walibya walipoambiwa kuwa wanachopata wanapunjwa sana, kwani wanastahili zaidi, kisha wakaambiwa wanaibiwa kwa kutolea mfano ufahari wa watoto wa Gaddafi. Kwa hilo tu, Masiha wa Afrika alipoteza legitimacy. Alipinduliwa na kuuawa kinyama. Sizungumzii majuto ya Walibya hivi sasa baada ya kifo cha Gaddafi. Nazungumzia kosa moja lilivyougharimu utawala wa Gaddafi na maisha yake kwa jumla.
Nicolae Ceausescu wa Romania, hakuwa na lengo baya kwa nchi yake. Alitaka tu kulipa madeni ya nje. Uamuzi huo ulipochukiza wengi alipoteza legitimacy kisha akauawa mbele ya kadamnasi kwa kupigwa risasi yeye na mkewe.
Tanzania yetu ni salama, hayawezi kutokea ya Gaddafi na Ceausescu. Nakumbusha kuwa Gaddafi alipendwa mno. Ceausescu alikubalika sana. Magufuli ndiye roho ya Watanzania kwa sasa. Asichezee haya mapenzi yaliyopo, yakiondoka, yatamgharimu sana. Namkumbusha kuwa mnyenyekevu!
Najua hili analitambua kuwa Watanzania wengi walishiriki na kutekeleza agizo lake kwamba siku ya Uhuru wa Tanzania Bara Desemba 9, mwaka huu iadhimishwe kwa kufanya usafi. Wengi walijitokeza kwa sababu mtoa agizo ni kipenzi chao. Wanampenda Magufuli. Hawana kinyongo naye. Kama asingewafurahisha kwa safisha-safisha yake Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), asingepata matokeo yale. Japo usafi ni faida ya kila mtu lakini wangetega tu. Nazidi kumkumbusha!
Hapo sijawazungumzia Dk Harrison Mwakyembe, Nape Nnauye na January Makamba ambao wapo wachache wanaponda uteuzi wao, lakini hoja zao hazina mashiko. Nimegusa pale ambapo kumekuwa na 'kaharufu kabaya' ambako kanabadili hewa nzuri aliyoanza nayo Dk Magufuli.
Mungu Ibariki Tanzania.
By Luqman Maloto