Simulizi

Mokes Junior

Member
Aug 20, 2022
7
0
HEKALU LA WACHAWI sehemu ya 02.

Inaendelea...Kuanzia kipindi hicho nilibaki mkiwa mimi Pamoja na mdogo wangu mmoja wa pekee wa kiume aliyeitwa James. Baadae kidogo baada ya matanga ya baba yetu kuisha, mama mdogo aliyemfuatia mama yangu kwa kuzaliwa alitufuata mimi Pamoja na mdogo wangu James tukaishi na kusomea kwake lakini bibi alikataa kata! kata! sisi kuondoka na mamamdogo. Tuliendelea kuishi na bibi yetu bila kujua yatakayokuja kutokea kwani waswahili husema jambo usilolijua ni Kama usiku wa giza.

Leo naandika simulizi hii nikiwa mpweke mwenye baridi kali moyoni mwangu, tena mwenye masononeko mazito sana ndani ya nafsi yangu. Bibi yangu kaniumiza sana tena kaurarua moyo wangu na kuuchochoma bila huruma. Mimi ni binadam kwa mwonekano ila moyoni mwangu najiona shetani kutokana na haya niliyopitia hakika ni mazito Kila nikiyakumbuka huwa nalia kwa uchungu Sana.

Baada ya mama kufariki wakati anajifungulia nyumbani kijijini kwetu aliniacha nikiwa darasa la nne. Baada ya mama kufariki nilianza kuwa mtoto shuleni muda mwingine nilikosa hata wa kuninunulia sare ya shule kwani baba yangu alikuwa anamsikiliza sana mama yake ambaye ni bibi yangu sijui alikuwa amemfanyaje. Nilishindwa kuendelea na shule mwaka 2007 baada ya kufika darasa la sita. Baada ya vifo vya Wazazi wetu wote wawili tulibaki wakiwa sana mimi Pamoja na mdogo wangu James kwani tulibaki tukiishi na bibi yetu bila kufaham kama haya yaliyotukuta yalisababishwa na mtu wetu wa karibu tena tunayemheshimu Sana. Itaendelea sehemu ya 3.
 
Wakina George .r.r.martin walianza hivyo hivyo mpaka leo wanatikisa kupitia game of thrones na j.k Rowling na yeye herry potter wewe endelee hivyo bila kuacha utafika mbali

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom