Simulizi za ajabu na kustaajabisha Dunia

Simulizi za ajabu na kustaajabisha Dunia

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
3,450
Reaction score
6,211
Makubwa Ya Kombe La Dunia: Mlinzi Aliyewafungulia Wafungwa Gerezani Hispania!

Ndugu zangu,
FAINALI Za KOMBE LA DUNIA ina maana ya msimu wa kuamka kwa hisia za utaifa.
Na hakika kandanda ina miujiza yake na inaweza kuwafanya watu wapagawe, wawe kama wendawazimu.

Kule Hispania miaka ya sabini kuna kisa cha mlinzi wa gereza aliyewaachia huru wafungwa kwa furaha ya ushindi wa timu ya taifa ya nchi hiyo wa bao moja dhidi ya Ureno.

Ilikuwa ni katika moja ya mechi muhimu za kufuzu kucheza Kombe la Dunia . Kipenga cha kumaliza mpira kilipopigwa, mlinzi yule wa gereza aliruka kwa furaha na kushangalia kwa sauti;

"Viva la Espana! Viva la Espana!

Alifungua mlango wa chuma wa chumba cha wafungwa gerezani. Alishangaa kuwaona wafungwa wale wakizungumza na kupiga kelele zao za ndani ya gereza bila kufahamu kilichotokea juu ya ushindi wa Hispania dhidi ya Ureno.

Mlinzi yule wa gereza, huku akishangilia aliwaambia wafungwa wale;

" Hivi mnafahamu kuwa Hispania tumewafunga Ureno?

Mara, wafungwa wale walilipuka kwa furaha na kuanza kushangilia huku wakitoka mlangoni na kutimkia uraiani.

Hakuna mfungwa hata mmoja aliyerudi gerezani , walitoroka kwa furaha!

Mlinzi yule alifikishwa mahakamani kwa kosa la uzembe uliosababisha wafungwa watoroke.

Kesi ile ya mlinzi wa gereza ilivuta hisia za Wahispania wengi, na mahakama ilifurika watu kila siku iliposomwa kesi ile mahakamani.

Na ikafika siku ya hukumu. Akisoma hukumu yake, Jaji wa mahakama alilidhika kuwa mshatakiwa alifanya uzembe mkubwa kiasi cha wafungwa kutoroka.

Jaji aliendelea kuorodhesha makosa ya mlinzi wa gereza na madhara yake kama yataendelea kufanyika katika nchi.

Kila mmoja alisubiri kusikia ni miaka mingapi jela mlinzi yule wa gereza angehukumiwa.

Jaji wa Mahakama aliinamisha kichwa, kisha akamtazama mlinzi wa gereza kwa kupitia juu ya miwani yake; akatamka;

"Hata hivyo, kitendo cha mlinzi wa gereza kuwafungulia wafungwa na hatimaye wakatoroka gerezani kinadhihirisha mapenzi ya dhati ya mlinzi wa gereza kwa taifa lake la Hispania, kwamba aliona ni jambo la fahari kubwa habari za ushindi ule mkubwa wa Hispania ziwafikie hata wafungwa walio ndani ya gereza. Huo ni uthibitisho wa uzalendo na mapenzi kwa nchi yake. Mshtakiwa kuanzia sasa nakuachia huru!”
 
*HAKIKA HUU NDIYO MKOA WA NJOMBE WENYE MAUZA UZA YA KUTOSHA.*

Njombe ni mmoja wa mikoa 31 ya Tanzania, uliorasimishwa kuwa mkoa mwaka 2012 mara baada ya kutenganishwa na Iringa inayopatikana Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania. Hapo awali Njombe ilikuwa ni wilaya ndani ya mkoa wa Iringa ikiwa ina ukubwa wa eneo la mraba la Km 21,347. Sensa ya mwaka 2012 ilionesha kuwa Njombe ina wakazi wanaofikia kuwa 702,097. Mkoa wa Njombe ni maarufu kwa kilimo cha mahindi na viazi.
Makabila makubwa ya wenyeji mkoani Njombe ni Wabena, Wakinga na Wapangwa, na uwiano wao ni 37:11:3.

Kama ilivyo mikoa mingine, Njombe ina historia yake ya kipekee. Neno "Njombe" lenyewe limetokana na jina la mti unaoitwa "Mdzombe" ambao ulipatikana kwa wingi eneo la Mdandu yalikokuwa makao makuu ya Ngome ya Mjerumani wakati huo (Bomani). Mkoa wa Njombe Una vivutio vingi sana vya utalii, Nyumbanitu ni kimojawapo.

NYUMBANITU NI NINI?
Neno "Nyumbanitu" ni muunganiko wa maneno mawili; nyumba na nitu. Neno "Nitu" manaake ni Giza au Nyeusi. Hivyo Nyumbanitu maana yake ni nyumba yenye Giza au nyumba nyeusi.

Nyumbanitu si nyumba kama lilivyo neno lenyewe, bali ni msitu mdogo wenye ukubwa wa hekta mbili na nusu (2.5) tu. Msitu huu mdogo wenye mambo ya kustaajabisha upo katika Kijiji cha Mlevela, Kata ya Mdandu Wilaya ya Wanging’ombe, ni Km 15 kutoka Njombe mjini.

Kwa sasa msitu huo unatunzwa na wanandugu , Julius Vangameli Msigwa na Alex Vangameli Msigwa, ambao kabla ya kutembeza wageni msituni huwa lazima waulize nia ya ujio wa wageni husika. Kuna ambao huenda nyumbanitu kuomba mizimu iwape baraka Katika mambo yao. Kuna ambao huenda kuchuma dawa, wengine huenda kujifunza Mila na desturi za mahali hapo nk.

Kabla ya kuingia ndani ya msitu huo mdogo ni lazima wenyeji (Familia ya Msigwa) ambao ndio wenye msitu wao wafanye maombi mafupi Kwa mizimu ili wapate ruhusa ya kuingia. Si kila mahali unaweza kutumia kuingia ndani ya msitu huo, kuna njia maalumu ambayo Si rahisi kuijua, labda wenyeji tu.

Iwapo utathubutu kuingia ndani ya msitu huo bila kibali cha familia iliyopewa jukumu la kuulinda, itakuwia vigumu kutoka. Utatembea Sana ndani ya msitu bila kuiona njia ya kutokea. Na kuna uwezekano mkubwa wa kufia humo labda tu wenyeji wakunusuru Kwa kuiomba mizimu ikuachie.

Mita kadhaa baada ya kuingia ndani ya msitu huo utaona sehemu ya mapokezi ambayo huwa pana vyungu vyeusi vyenye umri mkubwa sana, vingine vikiwa vina maji ya mvua na vingine vikiwa na unga wa mtama. Utaona pia vigoda, mkuki, tunguli, vibuyu, mti uliovishwa kaniki, nyungo na sarafu za zamani sana. Hivi vyote hutumika wakati wa zoezi la tambiko. Vifaa hivyo vyote vinadhaniwa kuwa mahali hapo tangu karne ya 14 au 15.

Maajabu ya msitu huo ni uwepo wa kuku weusi wenye midomo myekundu ambao wahifadhi wanasema kuwa kuku hao hawazeeki, hawafugwi na wala hawaliwi. Kuku hao huonekana kwa wingi wakati wa mavuno na inapofika masika, hawaonekani tena. Kuku hao wakitoka nje ya msitu, hakuna mwanakijiji ambae husumbuka kuwabughudhi au kuwaiba kwa kuwa wana madhara iwapo utafanya hivyo. Wengi waliojaribu kwenda kinyume na mifugo hao; eidha kwa kuwaiba au kuwachinja, walipata matatizo.

Inasemekana pia kuna ng’ombe, mbuzi na kondoo weusi ambao huingia kwa msimu ndani ya msitu huo bila kujua ni wapi hasa wametokea. Wanyama hawa waliingizwa kwa mara ya kwanza miaka mingi sana huko nyuma. Waliletwa mahali hapo kama adhabu kwa wale ambao walikiuka utaratibu wa kimila, badala yake wakaambiwa wapeleke aina hiyo ya wanyama na ndege ili wasamehewe makosa yao. Mpaka Leo hii, ndege (kuku) na wanyama hao (ng'ombe, mbuzi na kondoo) hawazeeki, hawaliwi wala kuchungwa na yeyote. Hata kuonekana kwa viumbe hawa kumekuwa ni kwa msimu tu.

Kuna nyakati, kila ikifika asubuhi, kuna sauti ya kengere za ng'ombe kutoka ndani ya msitu huo kuashiria kuwa ng'ombe wanaamka na kuelekea malishoni, na ikifika jioni pia sauti ile hujirudia kuashiria kuwa ng'ombe wanarudi kutoka malishoni japo hawaonekani wakitoka.

Ndani ya msitu huu kuna rupia ambazo huwa zinawavutia wengi na hivyo kuingiwa na hamu ya kuziiba, lakini kimaajabu hujikuta wakishindwa kutoka ndani ya msitu hadi pale wenyeji wanapoamua kuwanusuru.

Kuna mapango makubwa ambayo watu zaidi ya mia wanaweza kuishi, huku simulizi zikieleza kwamba mapango hayo yalitumika kujificha wakati wa vita, ni pale ambapo Chifu Mkwawa alivamia maeneo hayo. Si tu mapango hayo yalitumika kujificha dhidi ya uvamizi wa Chifu Mkwawa, vilevile yalitumika kujificha wakati wa vita ya Majimaji iliyopiganwa na makabila mbalimbali dhidi ya Mjerumani mwaka 1904---1907. Mapango hayo yana giza totoro na vijito vya maji yanayotiririka.

Si ruhusa Kwa wanawake walio katika siku zao, yaani kwenye hedhi kuingia ndani ya msitu huo. Ni mwiko kabisa, na ikiwa mwanamke atajidanganya kufanya hivyo, basi miaka yake yote atabaki akitokwa na damu ya hedhi bila ukomo na hakuna dawa ya kumtibu. Wanawake wajawazito pia hawaruhusiwi kuingia. Marufuku hii imeandikwa kwenye ubao maalumu nje kabisa ya msitu huo mdogo. Ili kuhakikisha kuwa wageni (watalii) hawakiuki marufuku hiyo, mwenyeji huirudia marufuku hiyo kwa mdomo ili kutilia mkazo.

Sharti jingine kabla ya kuingia msituni humo ni kuvua viatu, kofia na vilemba. Baada ya kufuata taratibu zote, mwenyeji (Mzee Julius Vangameli Msigwa) huomba ruhusa ya kuingia msituni kwa kuongea maneno ya kibena;
“Hodi! Hodi Mutwa! Avagenzi ava vanuhile! Vihwandza...(hutaja lengo la ujio)! Hodi vamkongwa, Hodi vamwafute! Hodi Vakiswaga!....twisuka mwanuhile avagenzi ava,”

Baada ya maneno haya, mwenyeji huruhusu watu waingie wakiwa kwenye mstari mmoja mnyoofu. Mara nyingine wageni huambiwa waingie kinyumenyume kwanza na kisha wageuke kawaida, na hata muwapo ndani ya msitu huo hamruhusiwi kushika matawi ya miti inayoziba njia, badala yake mnatakiwa kuinama ili kuikwepa na si kuishika.

Kama ni msimu wa kiangazi, basi utawaona kuku weusi ndani ya msitu, wakiwa bize na kujitafutia chakula. Utaiona mimea ya kipekee ambayo imekuwepo hapo kwa zaidi ya karne mbili. Utashuhudia mapango yenye kutiririsha maji ndani yake huku yakiwa na giza totoro.

Wenyeji wa eneo hili na vijiji vya karibu wamekuwa wakitumia msitu wa nyumbanitu kufanya tambiko la kuomba mvua iwapo mvua haijanyesha kwa muda mrefu kipindi cha masika. Zoezi la tambiko huambatana na kuchinja ng'ombe kama kafara ya tambiko hilo. Mara baada ya tambiko wenyeji hujiandaa kuipokea mvua kubwa mno ndani ya muda mfupi. Kujilinda na mvua hiyo, watambikaji huenda na makoti makubwa au miamvuli, maana mvua haijawahi kutokunyesha baada ya tambiko.

Mwaka 1940 eneo hili la nyumbanitu lilikuwa likimilikiwa na Chief Mbeyela ambae alikuja kuliuza eneo hili kwa Wazungu waliotaka kulima chai. Ni wazungu waliokuwa wanamiliki kampuni iitwayo Tanganyika Wattle Company (TANWAT). Baada ya kununua eneo hili, Chief Mbeyela aliwapa sharti la kutunza eneo hili dogo la nyumbanitu ambalo lilikuwa ndani ya eneo kubwa zaidi lililonunuliwa na wazungu. Wazungu hawa walikubali lakini baadae wakakiuka sharti kwa kukata miti yote ya eneo hili la nyumbanitu ili wafanye shughuli zao za mazao. Asubuhi ya siku ya pili baada ya kukata miti yote ya eneo hili, walikuta pako vilevile kana kwamba zoezi la siku iliyopita ilikuwa ni ndoto tu. Miti yote ilirudi kama ilivyokuwa awali.

Wazungu walivyoona hivyo, wakachukua uamuzi wa kuchoma moto eneo hilo la nyumba nitu. Zoezi lilifanikiwa. Masika ilipofika, hakuna mvua iliyonyesha mpaka kiangazi kilipokaribia. Wazee wa kijiji wakaamua kuwafuata wazungu ili kuwaambia chanzo cha ukame wa mwaka huo. Suluhisho la ukame huo lilikuwa ni wazungu kukabidhi kaniki, kuku mweusi na ng'ombe mweusi ili wasamehewe kosa lao. Wazungu wakakabidhi vitu hivyo na tambiko likafanyika. Muda mfupi tu baada ya tambiko, mawingu yakasogea na mvua kubwa ikaanza kunyesha. Hapo ndipo eneo hilo likaendelea kuheshimiwa zaidi.

Miaka ya baadae Chifu wa wabena, Mkongwa aliwaita wanae watatu na kuwakabidhi majukumu kulingana na uwezo wa kila mmoja.
Chifu Mkongwa alisoma tabia za watoto wake kisha akawakabidhi majukumu.

Mtoto wa kwanza aliitwa Fute, alipewa jembe kama ishara ya kuwa mkulima hodari, akitakiwa kuhakikisha anasimamia shughuli za kilimo ili kuepuka janga la njaa.

Mtoto wa wapili aliyeitwa Mkongwa alikabidhiwa mkuki kama ishara ya kupewa ruhusa ya kupambana na maadui, huku akipewa kazi ya utawala.

Mtoto wa mwisho alikabidhiwa ungo kwa maana ya kuwa mganga wa jadi. Huyu ndiye aliyepewa jukumu la kufanya matambiko na kuongoza vikao vyote vya kimila.

Mtoto huyo ndiye aliyepewa kazi ya kuulinda na kuutunza msitu huo. Zana zote walizokabidhiwa watoto hao zimehifadhiwa ndani ya msitu huo hadi leo na ndizo zinazotumika kuoneshwa kwa wageni. Zoezi la kurithishana utunzaji wa msitu limeendelea mpaka Leo hii ambapo familia ya Julius Msigwa ina jukumu hilo.

Mwaka 1993, waumini fulani wa makanisa ya kikristo (walokole) walienda nyumbanitu ili wafanye maombi ya kuvunja nguvu zote za giza za eneo hilo bila kufuata taratibu za kimila kwa imani kuwa chanzo cha mikosi na matatizo ya watu wa eneo hilo ni uwepo wa nyumbanitu. Baada ya maombi ya siku nzima, waumini hao walishindwa kutoka ndani ya msitu huo. Badala yake wakaanza kupiga kelele kuomba msaada. Wakiwa ndani ya msitu walipotea njia ya kutokea nje. Wasamalia Sema wakaenda kutoa taarifa kwa wazee ili walokole hao wanusurike na madhira hayo.

Zoezi la maombi ya walokole lilisababisha kukosekana kwa mvua kipindi cha masika baada ya mizimu ya mahali hapo kuchukia.

Ili kurudisha mvua, waumini wote waliohusika na maombi hayo, waliitwa ili waombe msamaha kwa mizimu kwa kuleta kaniki, kuku mweusi, ng'ombe mweusi na sarafu ambazo waliiba mahali hapo. Waumini hao walitii agizo hilo la wazee na zoezi la kuomba msamaha kwa njia ya tambiko likafanyika. Haukupita muda mrefu mvua kubwa ikaanza kunyesha kama ishara ya kusamehewa makosa yao.

Mpaka muda huu naandika makala hii, nyumbanitu ipo na inatembelewa na wageni wengi kwa sababu mbalimbali. Karibu mkoa wa Njombe ujionee mwenyewe nyumbanitu na vitutio vingine kama Makaburi ya mashujaa wa Kibena, Mawe ya ajabu, Majengo ya kale ya wajerumani, Maporomoko ya maji ya Luhaji.

KARIBUNI SANA MKOANI NJOMBE.
 
MWANAHARAKATI DR MARTIN LUTHER KING -'I HAVE A DREAM'

Huenda maisha tunayaona jana na leo lakini si rahisi kuyaona kesho .....Marehemu Mbarak Mwinshehe aliimba ukiishi kwa kupiga mayoye utapoteza muda mwingi kukumbukwa kesho ni vyema ukayaishi maneno kwa vitendo vyako ili kesho ukumbukwe maana utakumbukwa si kwa magari, majumba wala hela ulizoacha bali ni jinsi gani Maisha yako yaliwagusa watu.

Jana ilikua ni miaka 50 tangu kuuliwa kwa kupigwa risasi kwa Mmarekani mweusi Martin Luther na kundi la wazungu waliochukia harakati zake za kupigania haki za weusi.

Aliuwawa tarehe 04/04/1968. Anakumbukwa kwa hotuba yake maarufu ya I have a dream yaani nina ndoto.

Martin ni miongoni mwa wanaharakati wengi walioishi kwa muda mchache sana Duniani ila wameacha kasumba/legacy kubwa sana Duniani. Pamoja na kuwa inasemakana aliuwawa kwa maagizo ya FBI chini ya Murugenzi katili John Edgar Hoover miaka 50 iliyopita lakini amebakia kuwa mtu mashuhuri na maarufu sana na unaweza ukasema amefariki jana tu.

Kuna mkanganyiko mkubwa juu ya akina Martin Luther kwa kuwa wote wawili wana majina yanayoelekeana sana mwanzo na mwisho. Hawa ni Martin Luther wa ujerumani aliyekuwa mwanaharakati wa kidini aliyekuwa mwanamatengenezo ambaye aliwezesha kuzaliwa kwa dhehebu la Lutherani duniani na wa pili ni Martin Luther king Jr wa marekani ambaye alikuwa ni kiongozi wa kidini na kiongozi wa harakati za kumkomboa mtu mweusi marekani.

Hivyo tofauti kubwa ya watu hawa ni mataifa mmoja ni wa marekani na mwingine ni wa ujerumani. Na mmoja ni mwenye asili ya afrika(Martin Luther king Jr) na mwingine ni mjerumani mweupe(Martin Luther).

Katika makala haya nitamuongelea Martin Luther king Jr wa marekani ambaye alikuwa ni kiongozi wa kidini na kiongozi wa harakati za kumkomboa mtu mweusi marekani kutokana na ubaguzi wa rangi.Makala hii inajikita katika kuangalia chimbuko la yeye kuwa kiongozi, sababu za uongozi kuwa imara, udhaifu katika uongozi wake na mafunzo kwa viongozi wengine.

Martin Luther King Jr ni moja ya wanaharakati wakubwa sana nchini Marekani hasa ktk kupigania haki za waamerika Weusi ktk karne ya 20.

Akimtambulisha kama gwiji wa maadili wa karne ya 20, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa alijitoa uhai wake akitetea usawa, haki na mabadiliko ya kijamii bila ghasia na alitwa tuzo maaru ya amani (Nobel) mnamo mwaka 1978

Bwana Guterres anasema miongo mitano hata baada ya kifo chake, bado Martin Luther King Jr. ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu wengi kote ulimwenguni, hususan wale wanaosaka haki za binadamu, wanaobaguliwa na kukandamizwa.

Alizaliwa Januari 15,1929 huko Atlanta ,Georgia nchini Marekani .Wazazi wake walimlea ktk maadili ya Dini ya kikristo na inasemekana walikuwa viongozi wa Dhehebu la Baptist.

Nje ya kuwa mwanaharakati wa masuala ya Haki na Usawa kwa wamarekani weusi Luther alikuwa ni Mhubiri wa Dhehebu la Baptist.

Kwa hiyo kuwa mwanaharakati wa haki za Binadamu na kuwa mhubiri ni jambo la kawaida na Mwenyezi Mungu hakatazi popote pale ktk maandiko yake matakatifu ,kwanza Mungu mwenyewe anapenda haki anachukia dhuluma,manyanyaso,Ubaguzi wa namna yeyote ile na yeye ndiye mwanzilishi na Msingi wa haki chamsingi harakati zako zisivuke mipaka ya neno lake na Taratibu za nchi yako husika.

Alijibebea umaarufu mkubwa sana kwenye Hotuba nzito sana inayojulikana kama "I HAVE A DREAM" Aliyoitoa Agosti 28,1963 mjini Newyork ktk Mnara wa Kumbukumbu wa Rais Abraham Lincoln .Katika hotuba hiyo alielezea matumaini Makubwa kwa watu weusi akisema ipo siku wamarekani weusi wataupata Uhuru na Usawa ktk Ardhi ya Amerika.

Katika hotuba hiyo watu takribani 200000 walihudhuria kumsikiliza mwanaharakati huyu wa kupinga ubaguzi ktk Amerika na Duniani kote. Aliuchukia ubaguzi wa Kirangi,Kidini,Kipato n.k .

Wakati wa karne ya 20 huko Marekani kuliibuka ubaguzi mkubwa wa Kirangi kwenye Taasisi za Kielimu ,kiafya na kidini ,vyombo vya usafiri ,Kwenye kumbi za Starehe ,Kwenye Ofisi za Umma ,Kwenye mashamba,Kwenye Viwanda, Kwenye maduka,Kwenye masoko,n.k waamerika weusi walinyanyapaliwa sana

Ilikuwa ukimuona mzungu na umekaa kwenye seat unampisha ikiwa gari limejaa,ukigoma unaadhibiwa vibaya sana,mwaafrika ulikuwa huruhusiwi kula hoteli moja na mzungu ,Mwafrika hakuruhusiwa kusoma Shule na Mzungu au mtoto wa kizungu ,Ilikuwa hairuhusiwi mzungu na mwafrika kuoana na lilikuwa ni kosa kubwa sana kufanya hivyo n.k .Hivyo kulikuwa na hotel,hospitali ,maeneo ya burudani ,makanisa n.k ya wazungu na waafrika .

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya akina Marcus Garvey ,William Dubois ,Malcolm X walisimama kidete kutoa hotuba za kulaani vikali vitendo vibaya vya kibaguzi vilivyokuwa vinafanywa na wazungu kwa kutumia majarida,vitabu ,kuandika mapendekezo ya sheria zinazolinda watu weusi dhidi ya wazungu katika Bunge la Marekani ,walitumia Redio na Televisheni kupinga ubaguzi wa Rangi,walitumia mbinu ya maandamano kuamusha hisia za Tabaka baguliwa (Waamerika weusi) n.k .Watu hawa walifanya kazi kubwa sana ya kupinga ubaguzi uliofanywa na wazungu.

William Dubous na wanaharakati wengine walianzisha mpango uliojulikana kama "BACK MOVEMENT " Ukimaanisha kuwa sasa waafrika warudi kwao wakaijenge Afrika yao ,wengi walirudi na wengine wengi pia walibaki wakiamini kuwa ipo siku wangepata Uhuru na Usawa katika Ardhi ya Amerika.William Dubous alionyesha mfano kwa kuhama Marekani na kuja kuishi Afrika ktk nchi ya Ghana mjini Accra.

Martin Luther King Jr ni moja ya watu walioamini kuwa ukombozi utapatikana huko huko Marekani na hakuamini katika kuikimbia Marekani .Funzo tunalopata haki haipiganiwi ukiwa ng'ambo Bali ukiwa ktk nchi yako.Waswahili wanasema fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

Luther aliendelea kuwapigania waafrika huko huko Marekani na kujitwalia Tuzo kadhaa za Amani (Nobel Prizes) baada ya kuutsmbua mchango wake ktk kuwapigania waamerika weusi .

Harakati za kupigania Uhuru na Usawa kwa wamarekani weusi zilikuwa ngumu sana kwani kulikuwa na kikundi cha Siri kilichojulikana kama Ku Klux Klan au Kuklux Clan kilichoundwa na wazungu ili kufifisha harakati za wamarekani weusi kudai Uhuru na usawa huko Marekani. Kikundi hiki kilikuwa hatari sana kwani kilikuwa kinawalenga viongozi wa harakati ili kiwaue .

Martin Luther king Jr aliuwa kwa kupigwa Risasi Hapo Aprili 4,1968. Kijana aliyetekeleza unyama huu alikuwa ni wa kizungu alijulikana kwa jina la James Earl Ray huko mjini Memphis, jimbo la Tennessee.

Martin Luther king Jr atakumbukwa kwa mbinu zake za kudai haki ,Uhuru na Usawa miongoni mwa wazungu na watu wa jamii ya kiafrika .Alidai haki ,Uhuru na usawa bila kuofia kulipa damu yake ktk harakati za ukombozi .

Martin Luther king Jr alituma ujumbe mzito Barani Afrika,Amerika ya kusini na Asia kuwa Uhuru ,Haki na Usawa unapaswa kuheshimiwa kwa Binadamu wote bila kujali wewe ni wa Rangi gani ,kipato gani,Dini gani ,n.k

Martin Luther king Jr atakumbukwa sana hasa ktk hotuba yake maarufu ya "I HAVE A DREAM" Akimaanisha "Nina ndoto" ambayo ilitoa unabii mkubwa sana wa Uhuru, haki na Usawa na hatimaye Dunia ilishuhudia Marekani ikiongozwa na mwamerika mweusi mh.Barack Obama wakati miaka ya nyuma ilikuwa ni marufuku kwa wamarekani weusi kushiriki ktk medani za kisiasa na hata kupiga kura hawakuruhusiwa .
Harakati za Martine Luther umeleta mafanikio makubwa ndani ya
Amerika ya Leo. Kuna tofauti sana na Amerika ya Jana hasa katika kuutazama usawa kati ya Marekani mweusi na mmarekani mweupe. Hivyo kupitia history hii niwaambie wanaharakati wetu kuwa kuna siku matunda ya kazi yao yataonekana

...............ITAENDELEA.................
 
HUYU NDO THOMAS SANKARA RAIS MASKINI KULIKO WOTE KUWAHI KUTOKEA BARANI AFRIKA, MWENYE UZALENDO WA KUSHANGAZA.

Mnamo august 1983, vijana wawili, makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas Sankara na Blasius Compaore, waliipindua serikali ya Rais wa wakati huo katika nchi iliyokuwa ikijulikana kama Upper volta, rais huyu aliitwa Baptiste Ouedraogo.

Vijana hawa wakiwa katika fikra za Karl Max, wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga Upper volta, walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, maanake nchi ya watu, country of honorable citizen.

Uchapakazi wa vijana hawa (Sankara na Compaore), Thomas sankara akiwa ndiye rais unaweza kufananishwa na ule wa Fider Castrol na Che Guavera, kabla haujachuja kule Cuba..

Haiyumkini Sankara alikuwa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo, wakati pacha wake (Compaore) wakiwa kama pete na kidole.

Urafiki wa makapteni hawa wa jeshi la Burkinabe, ulikuwa mkubwa kiasi ambacho, wakati wanausalama walipomwambia Sankara kuwa Compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua, yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, labda mtu mwingine.

Blaise Compaore alikutana na Thomas Sankara mwaka 1976 katika mafunzo ya kijeshi Morocco na hapo walianza urafiki wao uliokuwa wazi kwa karibu watu wote waliokuwa wakiwafahamu nchini Burkina Fasso na nchi jirani.

Thomas Sankara alikuwa akiwaeleza wanausalama wake kuwa, hata kama Compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia.

Ni wazi kuwa Kapteni Thomas Isidore Sankara alikuwa karibu sana na Blaise Compaore, kwa kiasi ambacho Blaise Compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya Sankara.

kama ilivyotabiriwa na watu wengi wa karibu wa Thomas Sankara, Blaise Compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha Sankara mnamo mwaka 1987, na yeye mwenyewe (Compaore), huku akishuhudia rafiki yake kipenzi Sankara akiuwa, Akawa ndiye mrithi wa kiti cha Urais wa iliyokuwa Upper Volta baadaye Burkina Fasso.

Thomas Isidore Noël Sankara ni nani??

Isidore Noël Thomas Sankara alizaliwa tarehe 12.12.1949 Mjini YOKO katika nchi iliyokuwa ikiitwa Upper Volta (Volta ya juu) na kuuawa tarehe 15.10.1987 na wanajeshi wenzake wakiongozwa na rafiki yake Rais Blaise Compaore katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou akiwa katika kikao cha utendaji wa kazi.

Thomas Sankara alipanda ngazi za kijeshi hadi cheo cha kaptenu pamoja na mwanajeshi Rafiki yake Blaise Compaore ANAYEJUA SIRI YA KIFO CHA CHA THOMAS SANKARA .

Kuna nyakati ambazo Blaise Compaore alipata kunena kwa kinywa chake katika shirika la kutetea haki za Binadamu duniani kwamba “kifo cha Thomasi Sankara kilikuwa ni ajali tu.

Mwaka 1981 Thomas Sankara alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais wa wakati huo wa Burkinabe ya zanani (Upper Volta) Jean Baptiste Major. Dr. na baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali ya Rais Major Jean Baptiste Dr kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi kwa watu wote wa Volta ya Juu na kupendelea Marxist Revolution theories.

Thomas Isidore Noël Sankara alikuwa Rais wa Upper Volta (Volta ya Juu) kuanzia mwezi Agosti 4 1983 hadi mwezi Octoba 15 1987 baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Major Dr Jean Baptiste yakiongozwa na Blaise Compaore na kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au BURKINA FASO baada ya kubadilishwa jina na Sankara.

Thomas Sankara aliyejulikana kama Che – Guevara wa Afrika alianzisha Program mbalimbali za kijamii na kiuchumi kuleta mabadiliko katika nchi za Afrika. Alibadilisha Upper Volta na kuwa Burkina Faso (land of Upright Men).

Alianzisha kampeni ya kuboresha Elimu na kutanua
Huduma za Afya kwa watu wa Burkina Faso maeneo ya vijijini hasa kwa watoto walio athirika na magonjwa ya Uti wa mgongo , Homa ya manjano, na surua.. na watoto karibu milioni 3 walipata tiba hizo..

Pia alianzisha kampeni ya upandaji wa miti kitaifa, na takribani miti Milioni kumi ilipandwa nchi nzima..

Pia alianzisha kampeni ya usafi nchini kote, kila mwananchi alipaswa kufanya usafi eneo alipo na Sankara mwenyewe alikuwa anashika fagio na kuingia barabarani kufanya usafi. Hiyo ni kampeni iliyoitwa mfagio wa mwananchi (le balai citoyen).

Aliongeza idadi ya wanawake katika serikali yake, ikiwa ni kampeni yake nchi nzima kupinga tohara kwa wanawake, pia alianzisha kampeni na baadae utaratibu wa kisheria wa kuwataka wasichana waliopata mimba wakiwa mashuleni kuendelea na masomo pia akaajiri wanawake jeshini, akawapa ajira katika sekta za umma ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na kuleta uwiano na usawa nchini Burkina Fasso.

Pia ndoa za wasichana wadogo na za kulazimishwa haswa za kimila katika maeneo mengi ya Burkina Fasso zikapigwa marufuku.

Thomas Sankara ambaye hakutaka makuu kabisa na wananchi wa Burkina Fasso. Akiwa kama Rais wa nchi, alivaa nguo zilizotengenezwa Burkina Faso badala ya suti kutoka Paris na London. mara nyingi alionekana akiwa kwenye gwanda la jeshi.

Pia Thomas Sankara alifuta matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi na watumishi wote wa umma, yeye kama Rais alikuwa akitumia baiskeli au miguu kwenda kwa wananchi vijijini kuhimiza na kusimamia shughuli za kimaendeleo.

Alijikita sana kwenye kusimamia na kukuza sekta ya afya katika Burkinabe, alihimiza watu kujihusisha na kilimo akiwapelekea zana za kilimo na pembejeo bure kwa watu wa vijijini na kugawa ardhi kwa wananchi ili wajihusishe na kilimo.

Kwa muda mfupi sana akiwa kama Rais wa Burikna Fasso, aliweza kuifanya nchi hiyo kuagiza chakula kutoka nchi za nje na kuifanya nchi hiyo kuanza kuuza vyakula vyake nje akaanza kuifanya Burkina Fasso kuwa imara kiuchumi.

Sankara aliwahimiza watawala wa Afrika waache kuwaibia wananchi, waache kutegemea sadaka kutoka nje.

Sankara akawaambia madeni ya Afrika hayana uhalali kwa vile yalitokana na mikataba mibovu.

Ndio maana hakuna maendeleo yaliyotokana na mikopo ya kigeni.

Sankara akataka Afrika iache kulipa madeni yasiyolipika.

Mwalimu Nyerere naye wakati huo alisema mtu hawezi kulipa madeni wakati watoto wanakufa njaa.

Thomas Sankara alisema ukitaka kujua maana ya ubeberu angalia sahani yako ya chakula, utaona kila aina ya chakula unachokula kinatoka nje. Ndipo akahimiza Afrika ijitegemee kwa chakula, akisema: "Anayekulisha anakutawala"

Thomas Isidoré Nöel Sankara ni wazi aliwakasirisha sana mabeberu wa kimagharibi, hasa ubeberu wa Kifaransa uliokuwa ukitawala kupitia vibaraka wake wa Afrika kama Rais Felix Houphouet- Boigny wa Ivory Coast.

Chini ya uongozi wake (Thomas Sankara), Burkina Faso ililima chakula chake badala ya kuagiza kutoka nje.

Kwa hatua hiyo, Thomas Sankara akawa amewaudhi wakubwa wa dunia (mabeberu) kwa kukataa kwake mipango ya kurekebisha uchumi ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) huku hoja kubwa ya sankara ikiwa ni kwamba, mipango hiyo ni ya kinyonyaji.

Thomas Sankara aligawa ardhi kwa wakulima wadogo baada ya kuchukua kutoka kwa wawekezaji wa nje ambao walikuwa wameipora baada ya kupewa na uongozi uliopita.

Katika huduma za jamii alileta mabadiliko makubwa katika huduma za elimu, afya, maji na kuboresha miundombinu ya barabara kuunganisha sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

Sankara katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinahudumia wanachi wa kawaida, Sankara alipambana na rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, huku akimtaka kila mwananchi kujituma kulijenga taifa.

Thomas Sankara alikuwa mtu anayechukia rushwa na ufisadi, uvivu, uzembe, dhuluma na unyonyaji wa wananchi na rasilimali zao. Alitaka kuona watu wake wakifaidika kwa rasilimali za nchi yake.

Huyu ndiye Thomas Sankara ambaye alipunguza mshahara wake hadi dola 450 kwa mwezi, ambaye alitembea kwa baskeli katika mitaa ya Ouagadougu bila ya kulindwa. Alipoulizwa kwanini hana walinzi alisema wananchi ndio walinzi wake, hivyo hahitaji kuambatana na wanajeshi wenye bunduki.

Washauri wake mara kwa mara walimshawishi aachane na matumizi ya baisikeli.

Akaamua kutumia gari lenye bei ya chini (Renault 5) badala ya msururu wa mashangingi kama tuonavyo leo katika Afrika...

Hata hivyo alibaki na baiskeli yake mpaka alipokutwa na mauti, na akaunti yake ya benki ilikutwa na akiba ya dola 400 ambayo ni sawa na Tsh 850, 550/= (laki nane elfu hamsini na tano namia tano hamsini), kwa sasa, badala ya mabilioni mengi kama wanayoficha huko Uswisi watawala wetu leo.

Kumbuka, Thomas Sankara amedumu kwenye uongozi kwa kipindi cha miaka 4 pekee kabla ya mapinduzi yaliyoongozwa na Rafiki yake kipenzi. Blaise Compaore ambaye aliondoka na uhai wake, lakini kwa kipindi hiko cha miaka 4 akihudumu kama Rais, alitengeneza mageuzi makubwa sana.

Ndoto kubwa ya kila siku ya Thomas Sankara, ilikuwa ni kuifanya Burkinafasso kuwa moja kati ya mataifa makubwa Afrika kiuchumi.

Thomas Sankara alikataa hata picha yake (yeye kama Rais) kutundikwa katika majengo, na taasisi za serikali alisema hataki kutukuzwa.

Sankara alikuwa akipokea mshahara wa dola 450 kwa mwezi, mshahara mdogo kuliko viongozi wote barani Afrika kwa wakati huo.

Huyu ndiye Thomas Isidore Noël Sankara anayejulikana kama Ernesto Che Guevara wa bara la Afrika (alikuwa akivaa mavazi kama Che Guevara, mwenendo, matendo na malengo yake yalifanana na Ernesto Che Guevara, pia walikuwa marafiki wakubwa), aliyeiongoza nchi kwa muda wa miaka minne kabla ya kuuliwa na maadui wa mapinduzi wakiongozwa na kapteni Blaise Compaoré Aliuliwa nyakati za usiku na mara moja akazikwa kwa haraka. Ernesto Che Guevara naye alikuwa mwanamapinduzi wa Marekani Kusini aliyeuliwa na majasusi wa Marekani (CIA) na kisha kuzikwa kisirisiri.

Thomas Sankara aliyekuwa muumini wa fikra za kupigania Umoja wa Afrika au Pan Africanist mara nyingi alionekana kutopendwa na mataifa ya magharibi kutokana na fikra zake za kupinga dhuluma za wakoloni kunyonya watu wanyonge.

Mwaka 1985, Thomas Sankara alikaririwa akisema kuhusu falsafa yake kisiasa iliyokuwa maarufu, ilikuwa ikisema;

‘you cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness’, yaani kwa tafsiri isiyo rasmi, hauwezi kuleta mageuzi ya msingi bila kuwa na kiasi fulani cha ukichaa ndiyo maana mabeberu walieneza propaganda kwamba Sankara ni kichaa anayeingoza Burkina Fasso.

Pamoja na yote na mengi mazuri, wapinzani ndani na nje ya nchi ya Burkinafasso, walisikika wakimlaumu Sankara kwa kupiga marufuku vyama huru vya wafanyakazi na vyama vya siasa.

Pia Sankara alianzisha Mahakama za wananchi ‘people’s revoluntionary tribunals’ ambazo zililenga kutoa hukumu kwa wapinga mapinduzi, wafanyakazi wazembe Jambo ambalo lilileta hamasa ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa nguvu wakiogopa hukumu.

Ila hatua hiyo ilipigwa vita saba na wapinzani wake.

Kumbukumbu kubwa ya wananchi wa Burkinabe (Burkina fasso), kuhusu Kapteni Thomas Sankara, ilikuwa ni wiki moja kabla ya kuuwawa kwake alitabiri, na alikaririwa akisema:

“Wanamapinduzi wanaweza kuuliwa, lakini fikra za kimapinduzi zitaendelea kuishi daima”

Hapo alikuwa akinukuu maneno ya Mwanamapinduzi maarufu Duniani, Ernesto Che Guevara ambaye aliwahi kusema..

“Revolutionaries and individuals can be murdered, but ideas never die.”

Thomas Sankara alifariki Oktoba 15 mwaka 1987 baada ya kupinduliwa na Blaise Compaore kuchukuwa utawala nchini Burkina Faso kwa muda wa miaka 27.

Inafahamika kwamba, kwa mara ya kwanza mwaka 1997, familia ya marehemu Thomas Isodoré Noël Sankara, ilifikisha ombi la kutaka mwili wa Sankara ufukuliwe ili ufanyiwe uchunguzi.

Taarifa zinafahamisha kuwa serikali ya Blaise Compaore ilitupilia mbali ombi kutoka familia ya Thomas Sankara la kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu kifo cha Sankara.

Kwa mujibu ya ripoti ya kifo cha Thomas Sankara, serikali ilifahamaisha kuwa Thomas Sankara alifariki kifo cha kawaida.

Familia ilitaka kufahamu kama ni kweli katika kaburi hilo ndipo mwili wa Thomas Sankara ulipohifadhiwa.
 
Chief nadhani mabandiko baadhi hayahusu hili jukwaa jaribu kwenda kule J Intelligence na uanzishe uzi huu kule ahsante
 
HUYU NDIYE ADOLF HITLER MFALME WA MADIKTETA WOTE DUNIANI.

Adolf Hitler Alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake.
Alizaliwa nchini Austria katika mji wa Braunau am Inn karibu kabisa na mpaka kati ya Ujerumani na Austria 20, April 1889 katika familia ya Alois Hitler na Clara Hitler.

Adolf Hitler alikuwa mtoto wa sita katika familia ya Alois Hitler na Clara Polz,
Japo kaka zake na dada zake wote walikufa wangali wachanga akiwa na umri wa miaka sita familia yake ilihamia Passau huko ujerumani na tena 1894 ikahamia leonding.

Hata hivyo mwaka 1895 Alois alistaafu kazi yake huko Hafeld ambako akawa mkulima na mfugaji wa nyuki. Shughuli za kilimo na ufugaji zilifeli vibaya sana na familia ya hitler ililazimika kuhamia Lambach, Hitler alianza kujifunza kuimba nyimbo za dini kanisani na alidhamiria kuwa muhubiri, mwaka 1898 familia yake ilihamia makazi ya kudumu Leonding.

Mnamo mwaka 1900 mdogo wake Hitler Edmund alikufa kwa ugonjwa wa surua kifo ambacho kilimuathiri sana jambo lililopelekea Hitler kubadilika kitabia kwa sehemu kubwa akawa mbishi, mtundu na akadiliki kupigana na baba yake na walimu wake tofauti na awali ambapo alikuwa ni mtoto mtiifu na mwelewa.

Baba yake alipata mafanikio makubwa katika shughuli za usimamizi wa mila na desturi [chifu] jambo amabalo alitaka mwanae Adolf Hitler afuate nyayo zake jambo ambalo lilipingwa vikali na mwanae ambaye alitaka apelekwe kwenye shule ya sanaa hii ilipelekea kutokea tofauti kubwa kati yao.

Mwaka 1900 Alois Hitler alimpelekea mwanae katika shule ya secondary iliyojulikana kwa jina la realschule, ambapo hitler alikubali kwa shingo upande na akafeli vibaya sana katika mitihani yake hii alifanya makusudi kwa kujua kuwa baba yake akiona maendeleo yake mabovu shuleni angebadili uamuzi wake na kumpeleka katika shule ambayo ni ndoto yake [sanaa] na hivyo kushindwa kuendelea na masomo kama vijana wengi wa Kijerumani.

Hitler alianza kushika asili na desturi za kijerumani ambazo kwa kipindi hicho ilikuwa ni ya kibaguzi, Hitler na marafiki zake walianza kutumia salamu ya kijerumani [heil] na kuimba nyimbo za kijerumani badala ya zile za Austria.

Baada ya kifo cha baba yake kilichotokea 3 january1903 maendeleo ya kitaaluma kwa Hitler yaliendelea kuzorota kwa kasi na baadaye mama yake alimuondoa kwenye shule hiyo Kutoka mwaka 1905 Hitler aliishi na mama yake yakiwa maisha mapya baada ya baba yake kufariki, mwanzo alifanya kazi ndogondogo na baadaye akawa anafanya kazi za upakaji rangi ikiwa ni pamoja na kuchora, kuuza rangi za maji nk.

Alidhamiria kuendeleza kipaji chake cha sanaa kwa kuomba kujiunga na chuo cha vienna, Academy Of fine Art lakini alikataliwa kwa mara ya kwanza 1907 na baadaye akakataliwa tena 1908.

Kiongozi wa chuo alitoa maoni kuwa Hitler alikuwa na uwezo mkubwa katika uchoraji lakini hakuwa na sifa za kitaaluma yenye ushahidi kwakuwa hakuwa na cheti cha kuhitimu elimu ya secondari.

Mnamo 21/12/1907 mama yake Clara Hitler akiwa na umri wa miaka 47 alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya titi, kifo cha mama yake kilisababisha mfumo wa maisha yake kuyumba na kulazimika kupoteza lengo la kusoma kichwani mwake na akaanza maisha mapya kwa kutafuta kazi za vibarua kwa ajili ya kujikimu, maisha hayo yalifanya kuwa mtoto wa mitaani asiye na pa kukaa.

Kwa muda ambao Hitler alikuwepo vienna kulikuwa na chuki za kidini pamoja na ubaguzi wa rangi, hofu ya kuchukuliwa kama mkimbizi kutoka mashariki ilitwala na kuenea kwa kasi.

Hitler alipendelea kusoma magazeti ya Deutsche volkblatt ambayo yalivumisha chuki kwa wakristo ambapo hitler alikuwa ni mmoja wao Mei,1913.

Hitler alikabidhiwa shamba lake ambalo lilikuwa ni urithi wa marehemu baba yake na alihamia Munich kukwepa kujiunga na jeshi la Australia hii ni kwasababu jeshi hilo lilikuwa na mchanganyiko wa jamii tofautitofauti jambo ambalo hakulipenda Hitler.

Katika vita ya kwanza ya Dunia, Hitler alikuwa akiishi Munich na alijitolea kulisaidia jeshi la Bavaria akiwa kama ni mwananchi wa Australia na aliwekwa kwenye kikundi cha Reserve Infantry Regiment namba 16 combania namba 1.

Na alikuwa kama mpeleka taarifa kikosi cha magharibi ya mbele Ufaransa na Ubelgiji na muda wote alikuwa nyuma ya mstari wa kikosi kilichokuwa mbele ya mapigano vikosi alivyotumikia wakati huo ni kikosi cha ypres, Sommers, arras na psschendaele na alijeruhiwa bega la kulia alipokuwa Sommers.

Alifanya kazi kwa juhudi kubwa na baadaye akatunukiwa nishani ya msalaba wa chuma na akapanda cheo kuwa Private, mwaka 1918 Kwa amri ya Lieutenant Hugo Gutmann, Hitler alitunukiwa nishani ya chuma daraja la kwanza na kupandishwa cheo kuwa coplo.

Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipawa chake cha kuhutubia watu, akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha Nazi alikopanda ngazi haraka.

Hitler alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini kiongozi wa kifashisti wa Italia aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake kuelekea Roma.

Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya Bavaria - kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin - lakini alikamatwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku.

Hitler akiwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Chamberlain aliyedai kwamba kuna aina mbalimbali za watu wenye tabia na thamani tofauti sana.

Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampala ("Mapambano Yangu") alikojaribu kueleza imani na siasa zake.

Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari. Katika itikadi hiyo mbari ya juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria na wale ambao ni duni zaidi ni watu weusi.

Vikundi vingine vimo katikati. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hiyo ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu upande mmoja, lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine.

Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria. Kujenga chama Baada ya kutoka gerezani alirudia siasa.

Alijitahidi kushika utawala wa chama cha NSDAP akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano.

Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS " ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi.

Chama chake hakikufaulu hadi 1929 , wakati uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani ulipoporomoka vibaya katika mdodoro mkuu Mamilioni waliachishwa kazi na kuona njaa .

Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali. Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu.

Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% za kura na kuwa chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge .

Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hitler katika serikali mwaka 1933.

Chansela na kiongozi wa Ujerumani Tarehe 30 Januari Hitler akawa Chansela wa Ujerumani. Mara moja alichukua nafasi kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani.

Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali wapinzani wengi walikamatwa na kupelekwa katika makambi ya KZ Hitler alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini akibahatika kwamba uchumi wa dunia ukapaa tena A.

Hitler alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyoweka mipaka kwa ukubwa wa jeshi lake kuwa watu 100,000 tu akajenga jeshi kubwa zaidi, akaanzisha utawala wa kidikteta wa "Dola la Tatu akipiga marufuku vyama vya upinzani.

Alitesa wapinzani wote na watu wa mbari alizochukia, hasa Wayahudi Siasa dhidi ya Wayahudi Chuki dhidi yaWajerumani waliokuwa Wayahudi aliionyesha kwa sheria mbalimbali zilizokuwa kali zaidi na zaidi. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo, takriban nusu milioni kati ya wakazi milioni 62.

Kila Mjerumani akitaka kuajiriwa na serikali au kupata nafasi ya masomo alitakiwa kuorodhesha wazazi na mababu hadi kizazi cha pili.

Kwanjia hiyo Hitler alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria "(ambao hawana Wayahudi katika familia), "Wayahudi" (watu wenye asili ya Kiyahudi, hata kama wameshakuwa Wakristo tangu vizazi kadhaa au hawakufuata dini "Wayahudi nusu" kama mzazimmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" kama mmoja kati ya mababu na mabibi wanne alikuwa Myahudi.

Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwakatika ajira ya serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali.

Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi" waliondolewa uraia kamili.

Tokeo moja la siasa hiyo lilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938 mwelekeo huo uliongezeka.

Hasa wanasayansi na wasanii wengi walihamia nchi huru. Siasa yake katika mwaka 1939 ilisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia Hitler alifuata mwanzoni siasa ya kukusanya Wajerumani wote wa Ulaya katika Dola la Ujerumani. Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Ucheki bila upingamizi wa kimataifa.

Lakini aliposhambulia Poland tarehe 1 Septemba tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza walisimama imara kwa mikataba ya kusaidiana na Poland. Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi.

Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake, hasa wakati wa vita dhidi ya Poland na Ufaransa.

Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekani yalikuwa mwanzo wa mwisho wake. Nguvu ya kiuchumi wa Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote.

Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wote wa Ulaya na inakadiriwa alifaulu kuwaua takriban milioni sita (2/3 ya Wayahudi wote wa Ulaya) pamoja na watu vya mbari mbalimbali kama Wasinti (kati ya 200,000 na 1,500,000).

Hasa alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa suala la Kiyahudi" lilichukuliwa mwisho wa mwaka 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi wachache.

Mnamo Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee Baadaye siasa ya kuwatenda Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani ilibadilishwa kulenga Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake.

Hadi mwisho wa vita Wayahudi walikusanywa kutoka kote Ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti Mwisho wa vita na kifo Maafisa wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler lakini hawakufanikiwa.Tarehe 20 Julai alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberglakini hakuuawa.

Mwishoni mwa vita Hitler alikaa Berlin hadi jeshi la Kirusi lilipokuwa limeshaingia mjini. Tarehe 30 Aprili alijiua kwa sumu pamoja na mpenzi wake Eva (alimwoa masaa tu kabla ya kujiua) na mbwa wake mpendwa "Blondi Maiti zilichomwa kwa petroli lakini zilitambuliwa na Warusi kutokana na meno yake'.
 
*ILI UWE NA UWEZEKANO WA KUWA AFISA USALAMA BASI JITAHIDI UWE NA SIFA HIZI.*



Lakini kuna swali nimekuwa nalipata sana mara nyingi PM na wengine wakinitumia jumbe za simu. Sijajua ni kwanini huwa naulizwa hili swali, lakini imekuwa common sasa kupata jumbe za.. "Nina passion ya kuwa afisa usalama, nisaidie broh.!"
Mara nyingi huwa sijibu hizi jumbe. Don't know why napata jumbe za namna hii...

Leo nimeona "nijaribu" kuadress hili suala japo kiduchu tu kwa kadiri ninavyofahamu.


Kwa muda sasa nimekuwa natamani kuandika kuhusu masuala ya dara ya Usalama wa Taifa lakini nimekuwa nasita kwa kuwa nchi zetu za ulimwengu wa tatu tunaishi kwa kuzingatia desturi ya kufanya ni mwiko kuongelea hayo masuala.


Ziko makala nyingi zilizochambua ni namna gani mtu anafikia hatua ya kuwa afisa usalama.
Lakini kitu nilichokiona kwenye makala hizi karibia zote zinaonyesha 'traditional ways' zinazotumiwa na Idara kupata maafisa wake.

Mfano, njia hii inayoongelewa sana ni kutoka kwenye depo za jeshi, polisi, vyuo vikuu na kadhalika. Kwamba 'mawakala' wanakuwepo huko ili kuangalia vijana wenye 'potential' ambao wanaweza kuwa watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.


Sasa njia hizi ni za bahati nasibu sana, na ni ngumu mno kwa mtu mwenye kutamani kuwa Afisa usalama kuweza kubahatika kuwarecruited.


Hii ndio sababu iliyonifanya niandike andiko hili fupi kuongelea machache yanayoweza kusaidia kukufanya uweze labda kuwashawishi "mawakala" wa usalama wa Taifa hapo ulipowapendekeze uwe recruited kwenye Idara.


Nimesema "hapo ulipo" kwa kuwa ndio, wako hapo ulipo… kila mahali ulipo! Kwenye sekta yako ya ajira, kanisani, misikitini, mitandaoni, vijiweni n.k. (sio kila kijiwe na kila kanisa au msikiti)



Ndio maana nasema, nitaeleza machache yanayoweza kusaidia labda watu wa Idara kuvutiwa nawe.


Kabla sijaongea vitu hivyo vichache unavyoweza kuvifanya kuwashawishi "Maafisa" wakufanye kuwa mmoja wao, ni vyema kujifahamu japo kwa uchache nadharia ya recruitment ya Idara za Usalama duniani kote na hasa hapa kwetu.


*Yaani kwanini Idara inafanya recruitment? Ni swali jepesi, lakini naomba nilizungumze..*


*1. Idara ni lazima iendelee kuwepo.*



Hii ndio nadharia ambayo imetumika kwa miaka mingi sana... Kwamba "tuna Taifa tunalohitaji kulilinda, tuna Taifa tunalotakiwa kuhakikisha liko Salama!", hivyo lazima Idara iendelee kuwepo muda wote.

Hii nadharia ndio inazaa ile "traditional procedure" ya recruitment… yaani kuchukua vijana kutoka vyuoni, jeshini, polisi n.k.

Yaani kwamba, kuna maafisa wanastaafu kila mwaka, kufariki, kuacha/kuachishwa na kadhalika. Hivyo wanahitajika kuwa replaced… lakini pia Idara inahitajika kukua kwa maana ya kuongeza idadi ya maafisa ili kuendana na ukuaji wa population ya nchi na kuongezeka kwa changamoto mpya… hivyo lazima kufanya recruitment ya maafisa wapya.…

Yaani lazima Idara iendelee kuwepo, haijalishi nchi iko kwenye tishio au iko tulivu.! Idara lazima iwepo na ifanye kazi muda wote.

*2. Uhitaji Maalumu.*

Nadharia ya pili inayotumika kuamua kufanya recruitment katika Idara ni pale panapoibuka hitaji maalumu la kiusalama.
Uzuri (au ubaya) ni kwamba katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kukua kwa teknolojia, kuongezeka kwa idadi ya watu, kuendelea kwa utandawazi, kukua kwa uchumi wa nchi, na mwenendo wa Dunia, masuala haya ya "uhitaji maalumu" yamekuwa ni endless. Yanaibuka kila leo.

Inafika kipindi kwamba watu/maafisa wanaokuwa recruited kwa kazi maalumu wanakuwa wengi kuzidi hata wale wanaokuwa recruited in a traditional procedures.



Mara nyingi watu wanaokuwa recruited kwa shughuli maalumu huwa wanatumika kwa sababu maalumu na kwa muda maalumu. Lakini wapo "assets" kadhaa ambao baadae wanabahatika kuwa "Maafisa" kamili.

Kwa kuzingatia kwamba nchi yetu haina mfumo au desturi ya kuweka wazi ajira za Idara Ya Usalama wa Taifa Kuombwa hivyo basi katika andiko hili nitatumia sana nadharia hii ya pili kujaribu kuonyesha ni mambo gani muhimu yanayoweza kukusaidia kuwashawishi Idara Ya Usalama kukufanya kuwa afisa wao.






Nitoe tena angalizo,


Nimeandika andiko hili kwa kuzingatia kanuni na desturi ya usiri unaopaswa kulindwa kuhusu Idara hii nyeti.
Hivyo basi si lengo la makala hii kuongelea siri au taarifa zilizo "classified"!

Makala hii inalenga kutia moyo, na labda kufumbua macho vijana wenye matamanio ya kuwa Maafisa wa Idara ya Usalama, namna wanavyoweza kujiunga na Idara kutimiza ndoto zao.
Pia nimeamua kuandika andiko hili ili kuwatia moyo vijana hawa wenye matamanio haya, kwa kuwa naamini kiwango cha juu kabisa cha uzalendo ni kufanya utumishi kwa nchi yako.



Pia nisisitize kwamba kabla ya kukuza mno matamanio yako ya kutaka kuwa Afisa Usalama ni vyema kujitathimini kama kweli unatosha? Na njia nzuri zaidi ya kujitathimini ni kujiuliza kwanini unataka kuwa Afisa usalama!
Je unapenda tu ile haiba yao, mavazi ya Kaunda suti na waya sikioni? Au ni kweli kwa dhati kabisa una nia ya kujitoa nafsi yako kutetea na kulinda nchi yako?

Ukishajijibu, unaweza kughairi au kukuza zaidi matamanio yako..


Pia niseme kuwa haya nitakayo yaeleza sio guarantee kwamba utaajiriwa na Idara ya Usalama… isipokuwa yanakuweka kwenye nafasi nzuri endapo kukiwa na uhitaji wa kufanya recruitment.


Nitaeleza machache hayo.





*1. JIFUNZE LUGHA NGUMU NA MAHUSUSI.*


Kadiri siku zinavyoenda ndivyo ambavyo umuhimu wa ujasusi wa kimataifa unavyoongezeka. Utandawazi, teknolojia na kukua kwa uchumi kunachochea muingiliano wa nchi yetu na mataifa mengine. Hii inaongeza ulazima wa Idara Ya Usalama wa Taifa kuwa makini zaidi ili kutambua maadui na kuwajua vyema hata wale ambao tunawahesabu kama nchi "marafiki".


Moja ya changamoto kubwa ninayoiona katika Idara yetu ya Usalama wa Taifa, ni kutokuwa na maafisa wa kutosha wenye ufasihi katika 'mission-critical languages'.

Mfano upande wa magharibi mwa nchi yetu na kaskazini magharibi, tunazungukwa na nchi zenye kutumia Kifaransa kama lugha kuu ya mawasiliano.

Ubaya ni kwamba Kifaransa si lugha ngumu kujifunza na kama ikitokea Idara wanataka kuweka 'spy ring' kwenye nchi hizo, maafisa wanaopelekwa huko wana uwezo wa kujifunza Kifaransa kwa muda mchache.

Lakini kama utakuwa na ujuzi wa Kifaransa inakupa points za ziada.

Kifaransa, Kiarabu na Kihispaniola nazichukulia kama lugha adhimu (zinakupa points), lakini sio muhimu zaidi ndani ya Idara.


Ukitaka kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi, jifunze lugha ngumu kama vile Kichina, Kikorea na Kihindi.

Nchi yetu imekuwa na muingiliano na mfungamono mkubwa na mataifa ya India, China na Korea.
Kuna umuhimu na uhitaji mkubwa kuwa na maafisa wenye ufasahi katika kuzungumza na kuzielewa lugha hizi (hasa Kichina na Kikorea).

Haina maana kuweka 'spy ring' nchini china au Korea wakati majasusi wenyewe hawana ufasihi katika lugha hizo. Hawawezi kufanya espionage kwa ufanisi.
Hivyo uhitaji wa maafisa wenye kuzielewa lugha hizi ni mkubwa mno.


Pia lugha nyingine ambayo iko juu kwenye orodha ya 'mission-critical languages' ndani ya Idara yetu ya Usalama wa Taifa nchinu, ni Indonesian.
Japokuwaa umuhimu wake hauwezi kufikia ule wa Kichina na Kikorea, lakini Indonesian ipo kwenye ngazi ya juu pia ya umuhimu.

Pia uzuri ni kwamba Indonesian ni lugha rahisi sana kujifunza. Ni moja ya lugha chache duniani ambayo muundo wake wa sentesi ni rahisi kiasi kwamba mfano binafsi nilishangaa nilipojifunza kukuta hii ni moja ya lugha ambayo haina uwingi (plurals), au tenses.

Ukiwa na ufasaha kwenye lugha hizi (au hata mojawapo) inakuweka katika nafasi nzuri zaidi.







*2. JIPE 'EXPOSURE'.*



Moja wapo ya sifa zinazochochea mtu kuwa recruited na Idara ya Usalama wa Taifa ni kiwango chake cha 'exposure' katika mataifa mengine.

Hii inasaidia mtu huyu pale anapotakiwa kupandikizwa nchi nyingine ili afanye shughuli za clandestine, inakuwa rahisi kwake kunyumbuka na jamii husika ya nchi hiyo.

Kama haujawahi kufika ulaya, basi jipe exposure hata katika nchi zinazotuzunguka.
Uelewa wako kuhusu jamii za nchi nyingine, lugha zao, na tamaduni zao zinakupa sifa za ziada ikitokea Idara inataka kufanya recruitment mahali ulipo kwa shughuli maalumu.


*3.UONGEZA UELEWA WAKO KUHUSU TEHAMA.*



Moja kati ya vitu critical zaidi ambavyo kila afisa usalama anapaswa kuwa na utaalamu navyo katika zama hizi ni utaalamu wa tehama. Japokuwa bado wapo maafisa wachache wakongwe ambao hawako vizuri na mambo ya tehama, lakini maafisa wapya wote wanaoajiriwa na Idara ya Usalama wa Taifa sasa hivi, wakiwa kwenye mafunzo katika kituo cha tiss lazima wapite kwenye kozi ya Tehama.


Hii inatokana na mwenendo wa ulimwengu ulivyo sasa. Dunia nzima iko kidigitali na kitehama.


Pengine ndio sababu ya Rais Kumteua Mkurugenzi wa Usalama msomi nguli wa masuala haya ya Sayansi ya Kompyuta.


Kama wewe ni expert katika mifumo ya Kompyuta inakuweka kwenye nafasi nzuri zaidi.
Lakini kama hujafikia hatua ya kuwa expert basi walau jifunze hata a, be, che kuhusu 'hacking' na masuala yanayorandana na hayo.


Hii itakuweka kwenye nafasi nzuri pia.




*4. HAKIKISHA UNA REKODI NZURI YA MASUALA YA KIFEDHA.*


Afisa yeyeto kabla ya kuajiriwa ni lazima ahakikiwe kuhusu masuala yake ya kifedha, kwa maana ya vyanzo vya mapato, matumizi na madeni.

Rekodi ya masuala ya kifedha inaeleza Mengi kuhusu haiba ya mtu.

Kumekuwa na visanga vingi vya maafisa usalama kuingia matatani kutoa siri baada ya kuhongwa fedha. Kwahiyo rekodi yako ya fedha inaeleza mengi kuhusu wewe.

Mfano mtuwenye mkopo Finca, hapo hapo analipa mkopo mwingine NMB, na hapo hapo ana mkopo kwenye vikundi… huyu hawezi kuwa afisa muadilifu. Ana kilala dalili kuwa ni mtu mwenye kupenda na wanaweza kutokea maadui waka-exploit desperation yake ya kutaka kuondokana na madeni na kumfanya kibaraka.


Kwa hiyo kama una fikiria siku moja kuwa afisa Usalama, hakikisha rekodi yako ya kifedha iko vyema.

(Pia na rekodi yako kuhusu uhalifu... Japo hii ina exception na complicated kidogo ndio maana sijaiweka kwenye orodha)





*5. KUWA BORA ZAIDI YA WENGINE MAHALI ULIPO.*


Kufanya kazi katika Idara ya Usalama wa Taifa ni fursa adhimu kwa walio wengi na nadra kuipata.
Pia shughuli hii inahitaji umakini wa hali ya juu mno.

Hii ndio sababu ya Idara kurecruit watu ambao ni bora zaidi katika sekta zao husika.

Kwenye kazi yoyote ambayo unaifanya sasa hakikisha kuwa siku zote unakuwa bora kuliko wengine. Kama wewe ni banker, mwalimu, polisi, hotelia, mjasiriamali n.k. kuwa bora zaidi ya wenzako mlipo kwenye sekta hiyo. Jitahidi kujenga competence ya hali ya juu katika hilo unalolifanya.

Idara ya Usalama wa Taifa ni mahali kwa watu "elites" (au inapswa kuwa hivyo).


Hii ni moja ya njia bora zaidi inayoweza kukufanya kwa haraka sana kuwa recruited na Idara ya Usalama wa Taifa.
Kwenye Idara kuna saikolojia kwamba, mtu yeyote aliye bora kwenye sekta fulani, anapaswa kuwa "asset" (au afisa kabisa) wa usalama wa Taifa.





*6. UZALENDO.*


Hii nimeiweka mwishoni kabisa lakini ilipaswa kuwa ya kwanza.


Unapokuwa afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, unaaminiwa na siri nzito zaidi kuhusu Taifa hili. Unaaminiwa kujua mambo ambayo mamilioni wengine hawayajui. Unaaminiwa kufahamu siri ambazo maadui zetu wa Taifa hawalali wakizisaka.

Hivyo basi afisa yeyote ni lazima awe na kiwango cha hali ya juu cha uzalendo kwa Tanzania.

Kwahiyo kama una ndoto ya siku moja kuja kuingia Idarani, hakikisha matendo yako, maneno yako, misimamo yako, na mawazo yako yana akisi na kuonyesha dalili ya uzalendo iliyo ndani mwako.


Hii ndio sifa kuu ya kuweza kupata fursa ya kujiunga kuwa afisa wa usalama wa Taifa. Uzalendo. Kuweka nchi yako kwanza kuliko kingine chochote kile.


Pia...

Najua kuna hoja huwa inaongelewa sana kwamba ili upate fursa kwenye Idara ni lazima uwe na msimamo wa kisiasa unaoendana na chama fulani... Hoja hii ina ukweli na uongo.
Ukweli ni kwamba, labda kuna watu waliwahi kupatiwa fursa hii kutokana na misimamo yao ya kisiasa. Labda kuna hayo makosa yalikuwa ynafanyika huko nyuma.
Uongo ni kwa sababu hii sio kanuni ya Idara kupata maafisa wake. Kanuni rasmi ya Idara ni uzalendo, na kwa mujibu wa maadili rasmi kabisa ya Idara, afisa ambaye amekula kiapo hapaswi kufungamana na mlengo wowote wa kisiasa.


So I know all this talk about chama fulani cha siasa... But its half truth!
Na nasikia kuna juhudi kubwa sana ndani ya idara kuhakikisha hiki kiapo kinazingatiwa ipasavyo (nchi kwanza). No petty politics.



Kwa leo niishie hapa na nimalizie kwa kurudia kusema kwamba, jitathimini kama kweli unatosha kuwa afisa wa Usalama wa Taifa.

Kazi ya Usalama wa Taifa si sawa na kazi nyingine za kuingia ofisini saa mbili asubuhi na kutoka saa nane au kumi jioni.
Ni kazi ya long hours… kuna siku ambazo hautalala hata siku mbili nzima uko macho na unatakiwa kuwa active na makini kwa muda wote huo na utimize majukumu yako kwa ukamilifu na ufanisi wa hali ya juu bila chembe ya errors.


Ni kazi yenye mengi nyuma ya pazia kuzidi suti za kaunda na nyaya masikioni unazoziona na kuvutiwa nazo kwa maafisa walio kwenye Protection Unit.
Ni kazi ambayo shughuli zake zinatekelezwa kila siku kwa kiwango kikubwa cha 'urgency'!
Ni kazi ambayo maisha yako yanakuwa hatarini kila siku unayoishi.


Ni kazi ambayo ukitaka kuimudu kwa usahihi unapaswa kuwa na uzalendo haswa moyoni.




Ukijitathimini na kujiona unatosha… basi muombe Mungu, siku moja labda itakuwa!.
 
*UJASUSI DHIDI YA UJASUSI.*



Takribani miaka 24 iliyopita, Januari mwaka 1994, aliyekuwa Rais wa Urusi, Boris Yeltsin, aliunda upya Shirika la Kijasusi nchini humo, maarufu kama KGB (Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti).

KGB (Kiingereza; Commitee for State Security )ni kati ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani yaliyopata kutambulika hivyo. Mwaka 1983 kwa mfano, Jarida la Time liliripoti kuwa shirika hilo ni bora zaidi katika kukusanya taarifa za kijasusi.

Wakati Yeltsin akiwa madarakani, KGB ilikuwa chini ya Wizara ya Usalama ya Urusi. Uamuzi huo wa kuvunja wizara na shirika hilo lenye rekodi ya ubora duniani linatusogeza katika swali la msingi; je, kwa nini Yeltsin alichukua uamuzi huo?

Kwa nini aliamua hivyo tena akipuuza rekodi kongwe na bora ya shirika hilo? Maelezo yaliyotolewa nyuma ya uamuzi huo ni kwamba; shirika hilo halikuweza kukabili changamoto za mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa kama alivyotaka Rais.

Kwa lugha nyingine, KGB ilikuwa kikwazo kwa Rais Yelstin kuongoza nchi kwa kasi aliyoitaka hususan mabadiliko ya msingi kiuchumi na kisiasa.

Ingawa katika kueleza sababu za uamuzi huo Yeltsin pia alikuwa na hasira binafsi, lakini angalau pia ndani ya uamuzi wake aligusa mambo ya msingi kwa maslahi ya nchi yake.

Ndiyo, Yeltsin alikuwa na hasira binafsi pia na hasa pale alipopata kueleza kuwa kati ya sababu za uamuzi wake huo dhidi ya KGB ni pamoja na shirika hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Usalama, kutompa taarifa kamili za uchaguzi.

Alidai KGB na Wizara ya Usalama kwa pamoja walishindwa kumpa taarifa kamili juu ya uwekezano wa chama cha Liberal Democratic (LDP), kupata ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Desemba 12, mwaka 1993.

Pengine kwanza tuelezane baadhi ya kazi za msingi za KGB ambazo ziko bayana katika machapisho mbalimbali ya masuala ya ulinzi na usalama na labda, kwa kuzingatia kazi hizo, Yeltsin aliona kuna tatizo na hivyo mabadiliko yalihitajika.

Mbali na jukumu la kupambana na mitandao mizito ya uhalifu, KGB ilikuwa na majukumu mengine ambayo ni kukabili mbinu za majasusi wa nchi nyingine ambao huingia Urusi kwa malengo maalumu.

Malengo hayo maalumu ni pamoja na kutaka kujua siri za nchi hiyo ambazo zinaweza kutumika na nchi nyingine hasimu kusababisha maafa au kuyumbisha Urusi (wakati huo Umoja wa Kisovieti).

Ili tuelewane vizuri zaidi kuhusu eneo hilo mahususi kimajukumu (nchi moja kufanya ujasusi dhidi ya nchi nyingine), nirejee mfano wa tukio la Aprili, mwaka 1999, wakati Marekani ilipofanyiwa ujasusi na China ambayo kupitia kwa jasusi wake waliiba teknolojia kutoka maabara ya Marekani.

Ilikuwa hivi; Aprili, 1999; Marekani (kupitia shirika lake la ujasusi CIA- Central Intelligence Agency) ilikuwa ikiendelea na uchunguzi dhidi ya wizi wa taarifa za siri kuhusu masuala ya nuklia, kwenda China.

Aliyekuwa Waziri wa Nishati wa Marekani, Bill Richardson, Aprili 28, mwaka huo alithibitisha kuwa, Wen Ho Lee, mwana-sayansi wa kichina (jasusi?) aliyekuwa akifanya kazi katika Maabara ya Taifa la Marekani ya Los Alamos, amefukuzwa kazi tangu mwezi Machi mwaka 2014.

Alifukuzwa kwa tuhuma za kuiba siri hizo na kuzituma kwao China. Katika wizi wake, Wen Ho Lee, alifanikiwa kusafirisha kiwango kikubwa cha takwimu (data) kutoka kompyuta za Marekani zenye kiwango cha juu cha ulinzi.

Tukio hili lilikuwa zito katika masuala ya usalama Marekani na Aprili 21, mwaka 1999, maofisa ujasusi wa Marekani walifanya tathmini na kutoa taarifa kwa Rais na Bunge (Congress).

Katika taarifa hiyo walikiri kwamba China imefanikiwa kunasadata kuhusu silaha za nyuklia na kwa hivyo, China ipo rasmi katika ujasusi dhidi ya Marekani.

Kama nilivyoeleza awali, huu ni mfano tu kwa hiki ninachoeleza kuhusu uamuzi wa Yeltsin kuvunja KGB na moja ya majukumu ya KGB kuwa ni kudhibiti majasusi wa nchi nyingine wanaoingia katika nchi yao.

Majukumu mengine ukiondoa hilo na mfano niliotumia, ni pamoja na kuhakikisha ulinzi wa nchi, kuendesha oparesheni maalumu za kijasusi, kudhibiti huduma za mawasiliano baina ya Rais na Serikali na masuala mengine nyeti.

Baada ya uamuzi huo wa Yeltsin kuvunja KGB, itakumbukwa kuwa msemaji wake (Rais) kwa wakati huo, Viacheslav Kostikov, alitoa ufafanuzi kuhusu hatima ya majasusi ambao kibarua kimefikia mwisho.

Kostikov alieleza tu kwamba wafanyakazi waliokuwa wa Wizara ya Usalama watahamishiwa katika idara nyingine za Serikali na baadhi ya majasusi watahamishiwa katika shirika jipya litakaloundwa kwa vigezo maalumu.
 
*KUTANA NA MAZINGAOMBWE YA KABILA LA WAGWENO.*



Wagweno ni kabila la watu wenye asili ya Kenya wanaoishi Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro, upande wa Kaskazini wa Milima ya Ugweno.

Lugha yao ni Kigweno. Kiasili Wagweno ni katika jamii zilizotoka Uhabeshi ya kale na ndiyo maana ukiangalia kwa makini utamaduni wao utaona kwamba hazifanani sana na Wabantu. Na hili unaweza kulithibitisha hata katika ngoma ya Kigweno ambayo wanaiita mrangi [mwanzi] hawatumii ngoma kama Wabantu.



Inasemekana asili yao wametoka maeneo ya Taita na Voi nchini Kenya. Kilichowakimbiza Kenya ya kale na kuhamia eneo linalojulikana kama milima ya Ugweno kwa sasa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Taita na Voi.

Lakini kuna nadharia moja inayosema kwamba kabla Wagweno hawajahamia rasmi katika milima hiyo ya Upare walituma wapelelezi kwanza, walifika eneo husika na kisha wakarudisha taarifa yao wakasema, "Mringa ua khona" (yaani mito ya huko inatoa sauti katika kutiririka kwake) na hapo jina Ugweno likazaliwa, yaani kughona ni muungurumo.

Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwamba Mgweno ni yeyote aliyekuja na kufanya makazi yake katika milima hiyo mizuri ya ugweno.


Kwa asili, Wagweno hapo kale walikuwa Wapagani wanaoabudu mungu jua *[Rubha],* *Pamwe* na mwandani wake *Mwiri [Mwezi],* mkewe jua, sanjari na watoto wao nyota.


Ibada hii ya kuelekea jua iliambatana na kuabudu mizimu na ndiyo maana kuhani wa Kigweno alipochinja mnyama na kumchuna ngozi yake aliweza kutazama maini kupiga ramli kwa kutumia viungo kwenye tumbo la mnyama.

Tena wanyama hao walichinjwa kwenye eneo maalumu liitwalo kwa Kigweno *Ngondinyi.* Mara nyingi eneo hili walihusika wanaume (bighairi) wanawake kwa sababu kwa mila ya Kigweno wanaume ndio *makuhani.* Mara nyingi katika eneo la kuzunguka Ngondinyi kulipandwa mimea maalum iitwayo *Mathale,* ambayo kwa mujibu wa mapokeo ya Wagweno ni mimea *mitakatifu.*




Mnyama anapochinjwa kuhani hukata vipande vidogovidogo na kuviweka eneo husika, kisha huchukua pombe ama mbege au dengelua kisha atatazama mbinguni huku ameshika mkononi pombe kama ishara ya tambiko na kusema *rubha kaghu ngoma mbai (yaani, naamini mungu yuko juu, lakini chini kuna mizimu).* Kisha humwaga pombe na kusema anachokusudia, kama anataka mvua inyeshe au anakusudia kuondosha *msinyanyo [mkosi].*


Kwa maana kwa mujibu wa mapokeo ya Wagweno mkosi kwao ulikuwa jambo kubwa sana na ndiyo maana hata mtoto aliyezaliwa na ulemavu wa aina yoyote alitolewa kafara kwenye jiwe la watoto, kwa Kigweno *ighwe ya bhana.*


Mhanga alikuwa anachukuliwa kwenye jiwe husika, mamaye humbembeleza, akiisha kulala hulazwa kwenye kilele cha jiwe na anapoamka ghafla huporomoka na kufa na watakuwa wameondoa mkosi katika jamii na kumfurahisha *mahoka.*

Kuna *kisa kimoja* cha kale juu ya bwana mkubwa mmoja aliyeitwa *Kindobhai* wakati anafukuzwa na maadui kunako eneo ambalo kwa sasa kuna hifadhi ya wanyama ya Tsavo karibia na ziwa Jipe. *Inasemekana alipiga fimbo yake kwenye maji na yeye, mifugo na wafuasi wake wakavuka salama!.*


Masimulizi juu ya Wagweno ni mengi sana, kiasi kwamba unaweza ukastaajabu. Mpaka leo kuna mawe ya ajabu ambayo yako mithili ya watu; inasemekana *maadui hapo kale walikuwa wanakuja kuiba mifugo* huko, lakini kulingana na ujuzi wa wazee *wakageuzwa mawe kwa njia ya miujiza.*
 
KISA CHA BWANA MWAMWINDI MKULIMA ALIYEHUKUMIWA KUNYONGWA KATIKA UTAWALA WA MWALIMU NYERERE.

Nimefika Nyumbani kwa Amani Mwamwindi. Ni majira ya saa kumi na nusu jioni. Ni nyumba ya kawaida sana katikati ya eneo wanaloishi watu wengi, karibu kabisa na soko. Ni kata ya Mlandege.

Nagonga mlango mkuu. Anayenifungulia ni Amani Mwamwindi.
" Karibu Bwana Mjengwa". Tunafahamiana, tumewahi kukutana kabla. Miguuni hana viatu, amevaa soksi nyeusi.

Ananikaribisha kiti sebuleni. Anaagiza nilitewe kinywani. Naye anakaa kitini. Mazungumzo ya ana kwa ana. Kichwani najiuliza; unaanzaje mahojiano na mtu aliyefiwa baba yake kwa kunyongwa miaka arobaini iliyopita?

"Bw. Mwamwindi, pole sana kwa tukio lile la mwaka 1971. Mimi nimelifuatilia kiasi. Kuna simulizi nyingi mitaani.

Vijana wengi wanaonyesha kuwa na kiu ya kutaka kujua ukweli hasa wa tukio lile. Kwa vile uko hai, nikaona nikutafute tusikie kutoka kwako."

Mwamwindi ananiangalia usoni.
" Alaa!" Anatamka. Kisha kinafuata kimya.

Nakumbuka, kuwa nimetoa maelezo ya utangulizi, sijauliza swali.
" Je, ni kweli kuwa Dr Kleruu alikwenda Isimani kwa marehemu mzee Mwamwindi kuhimiza suala la kilimo ndipo akakutana na kifo chake? " Namwuliza kwa staili ya kurusha mshale bila kulenga hasa ninachotaka kupiga. Namjengea mazingira ya kuogelea katika kile anachokijiua. Na swali hili kwake analiona zuri sana.

" Swali zuri, umeuliza kama Kleruu alikwenda kuhimiza kilimo. Hapo ndipo lilipoanzia tatizo."

Nakumbuka swali muhimu kabla hajaendelea.

" Mzee Mwamwindi, hivi ulikuwa na umri gani siku hiyo ya tukio?"
" Nilikuwa na miaka 21, na marehemu mzee alikuwa na miaka 42."

Nauliza tena.
" Tunasoma kuwa ilikuwa siku ya Krismasi. Je, ilikuwa ni Jumapili au siku gani? Na wewe ulikuwapo nyumbani kwa mzee?"
" Ni kweli ilikuwa siku ya Krismasi, Desemba 25, 1971. Ni siku ya Jumamosi" Anajibu Mwamwindi.

" Turudi kwenye tatizo lilipoanzia" Namwomba Mzee Amani Mwamwindi.

" Kulikuwa na tofauti ya kimtazamo. Na ugomvi ulianzia siku ya Alhamisi, Desemba 23 kwenye ukumbi wa welfare pale Mshindo. Kleruu aliwakusasanya wakulima wakubwa wa Isimani. Nataka ujue kuwa Isimani ilikuwa na wakulima wakubwa sana na mmoja wao ni marehemu baba yangu. Mle ukumbini kulitokea malumbano makali sana baina ya wazee wale na mkuu wa mkoa Kleruu.

Wazee hakukubaliana na Kleruu kuwaita pale kuzungumzia kilimo cha eka mbili au tatu wakati wao kila mmoja ukubwa wa shamba ulianzia eka mia mbili. Na tayari walikuwa na ushirika wao. Mimi nikiwa na miaka 21 nilikuwa karani wa chama cha ushirika.

Siku ile Mzee alitoka kwenye mkutano ule na kuja nyumbani kwangu hapa tulipo, Mlandege. Akanieleza juu ya mkutano ule na jinsi walivyokosana kimazungumzo na Kleruu. Akaniambia, kuwa mle mkutanoni alimwambia Kleruu ni vema akawasaidia wale ambao hawajaanza hata kutembea kuliko kuhangaika na watu wenye uwezo wa kutembea na kukimbia. Na baba yangu hakwenda shule.

Kwenye Umoja wao wa wakulima wa Isimani, baba na wenzake walijipanga vema. Walishaanza kuzungumzia haa uwezekano wa kumlipa mwanasheria, hata kama ni wa kutoka Uingereza, aje kuwatetea katika uovu ule wanaotaka kufanyiwa. Hawakukubaliana na utekelezaji wa sera za Ujamaa kwa staili ile aliyotaka Kleruu. Kuingia kwenye ushirika na wengine wakati wao walishaanza zamani. Fikiri, wao walifyeka mashamba yao tangu miaka ya hamsini. Hoja yao ni kuwa mapori yalikuwa hayajaisha kwa wengine kwenda kufyeka na kulima. " Anazungumza Mzee Mwamwindi. Anaonekana kuwa na mengi sana, na hamu ya kusimulia zaidi. Nabaini pia, kuwa kwake yeye mkuu yule wa mkoa ni Kleruu na hamtaji kama ' Dr Kleruu'. Namwacha aendelee.

" Sasa baada ya ile alhamisi, mzee akashinda Ijumaa. Jumamosi ikawa siku ya Krismasi. Kwa vile wafanyakazi wake wa shambani walikuwa mapumziko ya krismasi. Na yeye ni mwislamu, na alikuwa mchapa kazi kweli, basi, alikwenda shamba lake la jirani akiwa na mdogo wangu, sasa ni marehemu, anaitwa Mohamed. Wakawa wanalima kwa trekta.

Siku hiyo Kleruu, pamoja na kuwa ni Mkristo, aliamua kutokula Krismasi. Alivaa kofia yake ya pama. Inaaminika alibeba pistol yake pia. Kleruu akaendesha mwenyewe gari lake la mkuu wa mkoa aina ya Peugeot Injection, rangi ya bluu. Katika orodha yake, Kleruu alikuwa na watu watatu wa kuwashughulikia miongoni mwa wakulima wale wakubwa wa Isimani. Target nambari moja alikuwa Bw. Rashid Juma wa Nyangólo. Nambari mbili ni marehemu baba. Namba tatu simjui.

Kleruu alipofika Nyang'olo hakumkuta mkulima Rashid Juma. Siku hiyo ya Krismasi Rashidi Juma alipata habari, kuwa kuna ng'ombe wake walipotelea milimani. Alikwenda huko milimani kusaka ng'ombe wake. Hivyo, Kleruu akafunga safari kurudi kwa target namba mbili, baba yangu Mzee Mwamwindi. Ni njia hiyo hiyo, Nyang´'olo iko mbele ya ilipokuwa ngome ya mzee." Anasema Mwamwindi akionekana kuzama katika simulizi inayomgusa. Nami namsikiliza kwa makini.

"Basi, Kleruu akafika kwa Mzee. Baba akiwa shambani akaliona gari la Kleruu limesimama nje ya mji wake. Kisha akamwona Kleruu akitembea kumfuata shambani. Baba alihisi tu, kuwa Kleruu amekuja na shari.

Kleruu akamwuliza Mzee kwa ukali, " Mbona mnafanya kazi leo siku ya Krismasi?". Baba akamwomba Kleruu waende wakuzungumze nyumbani. Akamwambia mdogo wangu Mohammed aendelee kulima. Mzee akatangulia mbele, nyuma anamfuatia Kleruu. Kabla ya kufika kwenye nyumba yake wakayapita makaburi. Kleruu akamtamkia baba mzee Mwamwindi; " Hapa ndipo unapozika mirija yako?" Alitamka hivyo huku akimtomasa tomasa mzee na kifimbo alichoshika mkononi.

Jambo hilo lilizidi kumkasirisha marehemu mzee. Akafika nyumbani kwake. Mlangoni alisimama mke wake mdogo. Inaonekana mzee alishafanya uamuzi. Jana yake alikwenda kuwinda. Hakupata mnyama. Bunduki yake moja aia ya riffle kati ya bunduki zake mbili ilikuwa bado ina risasi. Akamwambia mke wake mdogo huku Kleruu akiwa anasikia;
" Kanichulie bunduki yangu"

" Je, aliposikia hayo Dr Kleruu alifanyaje?"

" Nadhani alipigwa na butwaa. Hakuamini kama baba angefikia hatua hiyo"

"Na ilikuwaje basi Mwamwindi alipoletewa bunduki?"

" Ilienda haraka, Mzee Mwamwindi akainua bunduki yake. Tayari ilikuwa loaded na risasa tangu jana yake alipotoka kuwinda. Kleruu aliinua mikono yote miwili kama mtu anayesalimu amri. Mwamwindi akampiga risasi ya kwapani. Kleruu akabaki hai. Akapiga risasi nyingine. Ikamwua pale pale." Anasimulia Mzee Amani Mwamwindi.

Kinafuatia kimya. Anainama, namwona usoni, kuwa huzuni imemjia. Bila shaka, ni kitendo kile cha baba yake kumpiga risasi na kumwua Dr Kleruu ndicho kilichoashiria mwanzo wa ukurasa mgumu katika familia ya Mwamwindi , Isimani na pengine Iringa kwa ujumla.

Nafikiria kumwuliza swali lifuatalo; Risasi ya pili ya Mzee Mwamwindi ilimpiga Dr Kleruu katika sehemu gani ya mwili? Nasitisha swali hilo. Litasubiri mara nyingine. Mzee Amani Mwamwindi anaendelea kunisimulia;

" Mdogo wangu Mohammed akiwa shambani alisikia mlio wa bunduki. Alidhani kuwa baba amepigwa risasi. Alikimbia kurudi nyumbani. Na pale ilipowekwa kumbukumbu ya Kleruu nyuma yake ndio ilipokuwa nyumba ya mzee. Hivyo, pale ulipowekwa mnara ni mbele ya nyumba. Kwa sasa nyumba hiyo haipo.

Alipofika nyumbani, Mohammed akamkuta baba amesimama, na Kleruu amelala chini, amekufa. Mzee alichukua kofia ya pama ya Kleruu, akaivaa. Akaingiza mkono mifukoni mwa Kleruu, akachukua funguo za gari la Kleruu. Mzee alimwambia mdogo wangu amsaidie kumwinua Dr Kleruu. Mzee alimshika miguuni na mdogo wangu Mohammed alimshika kwenye mikono. Wakamwingiza kwenye buti la gari.

Baba akaendesha mwenyewe gari lile la Mkuu wa Mkoa Kleruu, Peogeot Injection, rangi ya bluu likiwa linapepea bendera ya taifa. Aliendesha kuelekea mjini Iringa. Njiani kuna walioshangaa kumwona Mwamwindi akiendesha gari la Mkuu wa Mkoa huku akiwa kichwani amevalia pama la Kleruu.

Mzee alipoingia mjini Iringa breki ya kwanza ilikuwa hapa tulipo, nyumbani kwangu Mlandege. Kama nilivyosema, wakati huo nilikuwa kijana wa miaka 21. Nilishakuwa na mji wangu, nilijenga kibanda changu hapa tulipo. Nilifanya kazi kama karani wa Ushirika. Siku ile ya tukio nami nilikwenda kwenye shamba langu Ifunda.
Basi, Mzee alipofika hapa nyumbani akaambiwa kuwa nimekwenda shamba Ifunda. Alisikitika sana." Anasema Mzee Mwamwindi huku naye bado akionyesha huzuni machoni. Miaka 40 baada ya tukio.

Alipotoka hapa alipita nyumbani kwake pale Mshindo, na baadae akasimama kwa binamu yake. Ile nyumba ya njano nyuma ya benki ya CRDB, si unaijua?" Ananiuliza.

" Ndiyo" Namjibu.
" Pale alikuwa anakaa binamu yake na baba. Basi, alipofika pale akakutana n abinamu yake. Binamu yake yule alishangaa kumwona mzee akiwa na damu kwenye nguo zake. Akashangaa pia kumwona akiwa na gari la Kleruu lenye bendera ya taifa ikipepea. Akamwuliza nini kimetokea? Mzee hakuweza kuongea akaeleweka. Alitamka; " Nimeenda kwa Amani ( Mimi) nimeambiwa kaenda shambani kwake Ifunda". Alionekana kuchanganyikiwa.

Akaingia kwenye gari. Akaendesha moja kwa moja hadi Kituo cha polisi. Akamkuta polisi kijana. Akashuka, akamwambia; " Njoo chukua mzigo wako". Akaweka chini pia kofia ya pama ya Kleruu.

Polisi alipofungua buti ya gari akashangaa kuona mzigo wenyewe ni mwili wa Mkuu wa Mkoa, Dr Kleruu. Mzee akawa amejisalimisha.

Niliporudi nyumbani kutoka Ifunda nikazikuta habari hizo mbaya. Nikaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Mzee pale Mshindo. Nikawakuta akina mama wanalia. Ilikuwa ni kilio. Hiyo bado ilikuwa ni Jumamosi, siku ya Krismasi. Nikauliza; kuna aliyekwenda kumwona baba pale polisi? Jibu likawa hapana. Nikaenda moja kwa moja polisi ili nikamwone baba na nimsikie kauli yake.

Nilipofika polisi nikaanza kujieleza kwa askari polisi kuomba ruhusa ya kuongea na Mzee. Wakati nikifanya hivyo mzee nae alisikia sauti yangu. Akatamka; " Mwanangu huyo, mruhusu niongee nae". Nikaongea na Mzee."

Baadae alipelekwa mahakamani hatimae akahukumiwa kunyongwa, Mwalimu Nyerere akasaini kisha hukumu
 
Mwamundi
IMG-20180703-WA0023.jpg
 
*HUYU NDIYO ALLY SYKES MZEE WA FITINA.*


UHURU wa Tanganyika haukuwa kazi rahisi kupatikana kama ambavyo wengi wanadhania.

Ili kuwa ni shughuli pevu iliyohitaji kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha Waafrika kutoka Tanganyika ambalo lilikuwa koloni la Uingereza, wanajitawala.

Jitihada hizo zilifanywa na wapigania uhuru mbalimbali waliounganishwa kupitia chama cha Tanganyika National Unioni (TANU), kilichoundwa na na watu waliojawa na shauku la kujitoa kwenye makucha ya kikoloni.

Ally Kleist Sykes mzaliwa wa Mtaa wa Gerezani, Kariakoo Dar es Salaam, ni miongoni mwa waasisi waliopigania uhuru wa Tanganyika ambaye ana mengi ya kukumbukwa.

Mzee huyo aliyezaliwa Oktoba 10 mwaka 1926 kisha kufariki Dunia Mei 19 mwaka 2013 alikuwa mzalendo aliyeanza harakati za kisiasa kwenye miaka ya 1950.

Ally Sykes ndiye aliyemwandikia na kumkabidhi Hayati Mwalimu Julius Nyerere kadi ya TANU namba moja.

Pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa TANU, kati ya wazee watu saba waliokuwa katika kamati ya TAA iliyounda TANU.

Alikuwa miongoni mwa wafadhili wakuu wa TANU, huku akiwa tegemeo la chama hicho katika kutekeleza mikakati hatari dhidi ya utawala wa Uingereza.

Katika siasa za sasa Mzee Ally Sykes anaweza akaelezewa kama "Mzee wa fitna" kwani alikuwa majukumu ya kuwagombanisha wananchi dhidi ya serikali ya kikoloni.

Majukumu hayo aliyatelekeza kwa kuchapa karatasi ambayo Waingereza waliyaita ya kuchochea ghasia kwani majasusi wa serikali ya kikoloni walimfahamu kwa uhodari wa kutengeneza mambo.

Waingereza walipata wakati mgumu kumkabili kwani licha ya uhodari wa kisiasa aliokuwa nao, Ally Sykes pia alikuwa na medali ya mlenga shabaha mahiri, aliyopata kwenye Vita Kuu vya Pili ya Dunia.

Kwenye vita hiyo Ally Sykes alikuwa kwenye bataliani ya sita (Battalion 6 Burma Infantry) King's African Rifles (KAR)

Hakika Ally Sykes alikuwa mzalendo, mweledi wa mambo na miongoni mwa waasisi muhimu wa TANU ambaye sahihi yake ndio iko katika kadi ya TANU ya Mwalimu Nyerere.

Umaarufu wake ni kama aliurithi kutoka kwa Baba yake Mzee Kleist Sykes aliyekuwa watu mashuhuri Dar es Salaam katika miaka ya 1900 hadi alipofariki mwaka 1949.

Baba yake alikuwa maarufu kwa kuwa alilelewa na Affande Plantan aliyekuwa askari kiongozi katika jeshi la Wajerumani lilokuja Tanganyika na Herman Von Wissman.

Kleist alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Association mwaka 1929 chama kilichokuja baadae kujibadili na kuwa TANU ambacho Ally Sykes akiwa mmoja wa waasisi.

Pia baba yake aliasisi Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na kupitia jumuia hiyo akajenga shule ya kwanza ya Kiiislam Dar es Salaam, ambayo ilisomesha Qur’an pamoja na elimu ya kimagharibi.

Jumuiya hiyo ilichangia vijana wengi wa kiislamu kuingia kwenye siasa za TAA na TANU katika harakati za kudai uhuru.

AKUTANA NA NYERERE

Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndio watu wa mwanzo kumpokea Mwalimu Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952.

Nyerere alifika nyumbani kwa akina Sykes na ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa udugu mkubwa wa mapenzi ya dhati si baina yao tu bali hata kwa wake na mama zao.

Mama yake Nyerere, Bi. Mugaya mara kwa mara alipenda kumtembelea nyumbani Bi Mruguru biti Mussa ambaye ndiye mama wa Sykes.

Pia Mama Maria Nyerere alikuwa mwenye urafiki wa karibu na Bi. Zainab ambaye ni mke wa Ally Sykes aliyekuwa akiishi Mtaa wa Kipata.

Wakati huo harakati za kuanzisha TANU zilikuwa zimepamba moto huku fitna za Waingereza kuwatokomeza viongozi shupavu wa TAA kama Hamza Mwapachu, Dk. Vedast Kyaruzi, Dk. Wilbard Mwanjisi, zilikivunja nguvu chama hicho.

Ndio maana TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka 1954 Ally Sykes kadi yake ya TANU ikawa namba mbili, Nyerere namba moja, Abdulwahid Sykes kadi yake namba tatu, Dossa Aziz kadi namba nne na John Rupia kadi yake ilikuwa namba saba.

Kipindi hicho Ally Sykes alikuwa Katibu wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA) na vilevile alikuwa mwakilishi wa chama hicho katika Kamati ya Uajiri ya Serikali (Government Establishment Committee).

Thomas Marealle ndiye alikuwa rais wa TAGSA na Rashid Kawawa alikuwa mwanakamati.

Wanasiasa hao walijipa jina la ‘’Wednesday Tea Club’’ wakikutana kila siku ya Jumatano kunywa chai pamoja na kupanga mikakati ya kuwang’oa Waingereza katika ardhi ya Tanganyika.

Kupitia Ally, Abdulwahid na Dossa Aziz, Nyerere aliweza kujuana na wenyeji wa Dar es Salaam maarufu baadhi yao ni Sheikh Hassan bin Amir, Mshume Kiyate, Jumbe Tambaza, Sheikh Suleiman Takadir, Clement Mtamila, Titi Mohamed na Tatu biti Mzee.
 
*MJUE KIUNDANI VLADIMIR PUTIN RAIS WA URUSI, PAMOJA NA UTAJIRI WAKE.*




Vladimir Putin akiwa amebakiza siku chache kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu, ameanika kiasi cha fedha alizojipatia kipindi cha miaka mitano iliyopita ambacho si kikubwa kama ambavyo ilifikiriwa.
Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Urusi imeeleza kuwa, Rais Putin alijipatia mapato ya Rouble Milioni 38.5 za Urusi sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 1.9 kati ya mwaka 2011 na 2016.
Hiyo maana yake ni kwamba kiongozi huyo wa nchi ya Urusi ana mshahara wa Dola za Kimarekani 143,000 kwa mwaka.
Fedha hizo hazizidi hata theluthi moja ya ule anaopokea Waziri Mkuu wa Australia, Malcom Turnbull ambaye hulipwa Dola za Kimarekani 527,852.
Kwa mujibu wa Gazeti la Washington Post, Rais Putin pia ameorodhesha akaunti 13 za benki mbalimbali ambazo kwa pamoja zina akiba ya Dola za Kimarekani 307,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 650.



Rais Putin pia ameorodhesha kumiliki nyumba zake mjini St Petersburg, hisa katika benki moja pamoja na magari mawili ya kimichezo ya nyakati za uliokuwa Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR).



Ingawa mshahara wa Rais Putin unaweza kuwa mdogo ikilinganishwa na viongozi wengine duniani, ni mkubwa mno ikilinganishwa na wanaopata raia wa Urusi.
Raia wa Urusi kwa wastani hupata Dola za Kimarekani 8500 kwa mwaka nao hupata watu wachache.

Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti hivi karibuni kuwa Rais Putin alitakiwa kutoa takwimu za kipato chake na mali alizonazo kama sehemu ya mchakato wa usajili kwa wagombea urais kutokana na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 18 mwaka huu.



Taarifa hizo zimekuja huku wakosoaji wake wakidai kwamba Rais Putin ana utajiri wa kupindukia na wakimuweka daraja moja na hata zaidi ya matajiri mabilionea wa dunia.



PUTIN NI NANI?
Rais Putin alizaliwa Oktoba 7, 1952 na ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisiasa cha Muungano wa Urusi na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa nchi hiyo wa Belarus.
Ratiba ya kila siku ya Vladimir Putin ina mambo mengi zikiwemo saa kadhaa za kuogelea, kuchelewa kulala, kutokunywa pombe kabisa. Unapotaka kumfurahisha Rais wa Urusi, Vladimir Putin, mpatie vitu viwili, mbwa mtukutu kabisa na kifungua kinywa cha mayai ya ndege wa porini aina ya tombo. Jarida la Newsweek la Marekani limeripoti kuwa vitu hivyo vinapatikana kutoka “mashamba ya rafiki yake ambaye ni kiongozi wa dini nchini Urusi anayeitwa Kirill.
Hiyo ni kwa mujibu wa wasifu wa Putin ulioandikwa mwaka 2014 na mwandishi wa jarida la Newsweek, Ben Judah aliyetumia miaka mitatu kumfanyia utafiti Rais huyo wa Urusi kwa ajili ya kitabu chake kinachoitwa, “Fragile Empire: How Russia Fell in and Out of Love with Vladimir Putin.”

Rais huyu wa Urusi hivi karibuni amekuwa akitajwa nchini Marekani kwa mambo mbalimbali ikiwamo kufanya utafiti unaolenga kubaini kampeni za Rais wa Marekani Donald Trump, msimamo wake juu ya mgogoro nchini Syria na alichokiongea kuhusu Marekani kujitoa katika majadiliano ya hali ya hewa nchini Ufaransa.

LAKINI AKIWA NYUMBANI KWAKE MAMBO YAKOJE?
Alikaimu kiti cha urais mnamo Desemba 31, 1999 mara baada ya Rais Boris Yeltsin kujiuzulu ghafla, na kisha Putin akashinda uchaguzi wa rais mwaka 2000. Mwaka 2004, alichaguliwa upya na kushinda, hivyo kuendelea na kipindi chake cha pili hadi Mei 7, 2008 kabla ya kuachia utawala wa nchi kwa Damitry Medvedev aliyeshinda kiti cha urais.
Medvedev kwa kutambua umuhimu wa Putin, mara moja alimteua kuwa Waziri Mkuu katika kile kilichoelezwa kuongoza kwa pamoja bila kinyongo (tandemocracy).




Jina lake lina asili ya watu wa mashariki mwa Urusi likiwa na maana ya mila katika mji wa Leningrad alikozaliwa.



NI LUTENI KANALI
Kwa miaka 16 Putin alikuwa Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Urusi likifahamika kwa kifupi KGB, akipanda cheo hadi kufikia Luteni Kanali kabla ya kujiuzulu na kuingia kwenye siasa akijiunga na chama kilichoanzishwa huko Saint Petersburg, mwaka 1991.
Baada ya kuwa kwenye chama hicho kwa miaka mitano, mwaka 1996 alihamia jijini Moscow kuungana na utawala wa Rais Boris Yeltsin ambako alipaa kwa haraka hadi kuteuliwa kuwa kaimu rais Desemba 31, 1999 baada ya Yeltsin kujiuzulu ghafla.
Septemba 2011, Urusi ilifanya Marekebisho ya Katiba yake katika kipengele cha muda wa rais kukaa madarakani. Marekebisho ya kutoka miaka minne hadi sita na Putin akatangaza kuwania madaraka ya urais kwa mara ya tatu katika uchaguzi uliofanyika Machi 2012.



Nia hiyo ya Putin ilipingwa kwa maandamano katika miji mbalimbali nchini Urusi, lakini alipambana na kushinda. Mipango mingi ya Putin haipiti kwa wepesi kwani huwa inakutana na changamoto au vikwazo vingi kutoka kwa watu wa kawaida hadi hata waangalizi wa kimataifa kuona kuwa demokrasia imekiukwa, lakini mwisho wa siku, anashinda.



Tangu mwaka 2011, Putin amekuwa mbabe akitangaza Urusi yenye mabadiliko ya kweli katika kila sekta badala ya kuwa na serikali isiyo na mamlaka.
 
Back
Top Bottom