Simulizi yenye mazingatio. Kama una muda pitia

jagabule

Member
Joined
Feb 19, 2019
Posts
43
Reaction score
70
Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lkn ghafla nilimwona dada yangu nyuma yangu akinitazama. Na akaniambia nimpe elfu moja ili asimwambie mama, nikamwambia sina ila tafadhali usimwambie mama.

Siku iliyofuata mama alimwambia dada aoshe vyombo na kusafisha mazingira. Lakini dada akamwambia mama Joseph amesema atafanya, dada akaja na kuniambia nifanye zile kazi la sivyo atamwambia mama nilimuua bata mzinga. Pasipo kulaumu nikazifanya.

Siku iliyofuata mama akamwita tena dada na kumwambia akachote maji na kujaza pipa. Dada akamwambia tena mama nimesema nitafanya, akaja kwangu akaniuliza unakumbuka ulimuua bata mzinga? Sasa jaza maji kwenye pipa kama hutaki nimwambie mama.

Ikanipasa nikachote maji nijaze pipa. Siku hyo hyo jioni mama akamtuma sokoni kununua nafaka na azisage. Akamamwambia tena Joseph amesema ataenda, akaja kwangu akasema "kumbuka kwamba bata mzinga bado amekufa" nenda sokoni ukanunue mfuko wa nafaka kisha ukasage, kama hutaki basi nitamwambia mama.

Nilisimama nikaenda kwa mama huku nikitiririka machozi machoni na nilimkuta amekaa ndani, nikapiga magoti na kumwambia huku nikilia.

"Mama nisamehe tafadhali nisamehe mno. Mm ndio nilimuua bata mzinga kwa bahati mbaya, tafadhali mama nisamehe.

Mama akajibu- "Mwanangu siku ile ulipomuua bata mzinga nilikuwa dirishani na nilitazama kila kitu kilichotokea. Dada yako amekufanya mtumwa kwasababu hukutaka kuja kwangu kukiri na kuomba msamaha. Sasa umefanya hv uko huru na dada yako hawezi kukutumia tena.

FUNZO,
Kila mara tukiwa tunatenda dhambi Mungu anatuona, na dhambi hakika hutufanya kuwa watumwa siku zote. Hivyo tukienda mbele zake tukikiri na kuomba msamaha yeye ni mwingi wa rehema na atatusamehe.

Mungu atusamehe dhambi zetu na atuweke huru... Amin.
 
Asante sana kwa kutukumbusha ya kuwa tunatakiwa KUTUBU DHAMBI ZETU, PIA MSAMAHA! Mungu akubariki sana kwa Neno la Hekima. Uwe na siku njema.
 
Hii hadithi, naifananisha na ya yule kijana aliyeua Kuku wa bosi wake.

Mwandishi wake ni mzaliwa wa Kanda ya Ziwa
 
Dada ≈ shetani
Mama ≈ Mungu
Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lkn ghafla nilimwona dada yangu nyuma yangu akinitazama. Na akaniambia nimpe elfu moja ili asimwambie mama, nikamwambia sina ila tafadhali usimwambie mama.

Siku iliyofuata mama alimwambia dada aoshe vyombo na kusafisha mazingira. Lakini dada akamwambia mama Joseph amesema atafanya, dada akaja na kuniambia nifanye zile kazi la sivyo atamwambia mama nilimuua bata mzinga. Pasipo kulaumu nikazifanya.

Siku iliyofuata mama akamwita tena dada na kumwambia akachote maji na kujaza pipa. Dada akamwambia tena mama nimesema nitafanya, akaja kwangu akaniuliza unakumbuka ulimuua bata mzinga? Sasa jaza maji kwenye pipa kama hutaki nimwambie mama.

Ikanipasa nikachote maji nijaze pipa. Siku hyo hyo jioni mama akamtuma sokoni kununua nafaka na azisage. Akamamwambia tena Joseph amesema ataenda, akaja kwangu akasema "kumbuka kwamba bata mzinga bado amekufa" nenda sokoni ukanunue mfuko wa nafaka kisha ukasage, kama hutaki basi nitamwambia mama.

Nilisimama nikaenda kwa mama huku nikitiririka machozi machoni na nilimkuta amekaa ndani, nikapiga magoti na kumwambia huku nikilia.

"Mama nisamehe tafadhali nisamehe mno. Mm ndio nilimuua bata mzinga kwa bahati mbaya, tafadhali mama nisamehe.

Mama akajibu- "Mwanangu siku ile ulipomuua bata mzinga nilikuwa dirishani na nilitazama kila kitu kilichotokea. Dada yako amekufanya mtumwa kwasababu hukutaka kuja kwangu kukiri na kuomba msamaha. Sasa umefanya hv uko huru na dada yako hawezi kukutumia tena.

FUNZO,
Kila mara tukiwa tunatenda dhambi Mungu anatuona, na dhambi hakika hutufanya kuwa watumwa siku zote. Hivyo tukienda mbele zake tukikiri na kuomba msamaha yeye ni mwingi wa rehema na atatusamehe.

Mungu atusamehe dhambi zetu na atuweke huru... Amin.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom