Simulizi ya Mwinyi vita ya ‘Magabachori’

Tumbiliwaulaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2020
276
500

Simulizi ya Mwinyi vita ya ‘Magabachori’​

mwinyipic

Summary

  • Katika mfululizo wa simulizi za kitabu cha ‘Mzee Rukhsa; Safari ya Maisha yangu’ Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameendelea kuibua mambo yaliyomsumbua wakati wa utawala wake, likiwemo la mvutano wa wafanyabiashara nchini.
Dar es Salaam. Katika mfululizo wa simulizi za kitabu cha ‘Mzee Rukhsa; Safari ya Maisha yangu’ Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameendelea kuibua mambo yaliyomsumbua wakati wa utawala wake, likiwemo la mvutano wa wafanyabiashara nchini.

Mzee Mwinyi ambaye pia katika kitabu hicho ameeleza mageuzi ya kiuchumi aliyoyafanya katika utawala wake, ameibua namna wafanyabiashara wenye asilia na Kihindi walivyoathiriwa na sera za ujamaa ambazo kupitia Azimio la Arusha walinyang’anywa mali zao, zikiwemo nyumba, mashamba, viwanda na biashara.

“Inakadiriwa kuwa karibu Wahindi 50,000 walikimbia nchi baada ya mali zao kutaifishwa kwenye miaka ya 1970 na wakati wa vita ya uhujumu uchumi miaka ya mwanzo ya 1980, wengi wakienda Uingereza na Canada,” ameandika Mwinyi.

Ameongeza kuwa hali hiyo iliwafanya wazawa kuona kuwa wafanyabiashara hao hawakuwa wazalendo. Hata hivyo, ameandika kuwa baada ya kuingia madarakani alifanya mageuzi ya kiuchumi yaliyoweka wazi milango kwa wafanyabiashara waliokimbia kurejea nyumbani.

Ameendelea kueleza kuwa kupitia mwanya huo, wafanyabiashara, hasa wenye asili ya Kihindi walikuwa wakifanya biashara za magendo, meno ya tembo na dawa za kulevya.

“Zilikuwepo tuhuma kuwa wamejijengea kinga ya kutokamatwa kwa kuwahonga baadhi ya viongozi wa siasa na Serikali ikiwemo kwenye baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama,” ameandika.

Ameandika kuwa chuki baina ya wafanyabiashara wenye asili ya Afrika na Wahindi iliibuka huku baadhi ya wanasiasa wakiitumia kama mtaji wao wa kisiasa kwa kueleza jinsi Wahindi walivyopewa upendeleo. “Yalikuwepo maneno mengi, ilimradi kukawa kumeibuka chuki na kwa kweli uadui baina ya wafanyabiashara wa Kiafrika na wa Kihindi.

Mambo ya ajabu kabisa!” Akerwa na neno ‘Magabachori’ na ‘Walala hoi’ Amemtaja aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi akisema “Mchochezi mkuu alikuwa Christopher Mtikila ambaye aliwaita wafanyabiashara wa Kihindi ‘Magabachori’ na Watanzania wenye asili ya Kiafrika ‘Walalahoi.

“Jambo hili liliniudhi na kunisikitisha sana. Si jambo la ajabu hata kidogo kuwepo kwa ushindani mkali baina ya wafanyabiashara, la kutisha na kusikitisha ni pale ushindani na pengine wivu wa biashara unapogeuka kuwa uadui kwa msingi wa ubaguzi wa rangi, dini au ukabila,” ameandika.

Amesema suala hilo lilikuwa ni hatari kwa Taifa, kwani lingeachwa lingezaa chuki zaidi hata kwa wafanyabiashara kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, hasa Wapemba.

“Baada ya hapo tungeshuhudia malumbano pengine baina ya ‘wazawa’ wenyewe kwa wenyewe. Kwani inawezekana kabisa wafanyabiashara wa Kihaya wasiwapende wale wa Kichaga na wa Kichaga wakawachukia Wakinga.”

Akitoa mifano ya nchi zilizokuwa na ubaguzi wa kibiashara, zikiwemo Indonesia, Malaysia, Rwanda na Burundi, Mwinyi amesema alikemea vikali hali hiyo. “Kwa mfano, Reginald Mengi alipokea barua ya vitisho kwa uhai wake na usalama wa mali zake.

Serikali ikachukua hatua za kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani na yeye mwenyewe tukampa ulinzi kwa muda wa kutosha pamoja na mali zake.

“Hali kadhalika wafanyabiashara wa Kihindi nao walipokea barua za vitisho kwao, familia zao na mali zao,” ameandika.

Amebainisha kuwepo kwa kikundi kilichoitwa black mamba chenye lengo la kutaka kuwadhuru Wahindi. “Nao pia tulianzisha uchunguzi dhidi yao kutaka kujua kama kweli wapo na malengo yao ni yapi.

La muhimu ilikuwa ni kutoa ulinzi kwa wote ambao walikuwa na sababu za kutosha kuhofia athari kwa maisha yao na mali zao,” ameandika.

Licha ya kukiri kuwepo kwa vitisho hivyo, pia ameandika kuwa visingesababisha madhara ya aina yoyote, bali ulikuwa ni ushindani wa kibiashara uliotishia kwenda kusikofaa.

Ameandika kuwa ushindani huo ulisababishwa na mageuzi ya kiuchumi aliyoyafanya katika utawala wake yaliyosababisha wafanyabiashara kujitanua zaidi.

“Sikutazamia ambao huko nyuma walikuwa na ukiritimba wa biashara fulani watachukia au kujaribu kuzuia wengine wasifanye biashara kama yao.

“Tulitaka kujenga uchumi huria katika hali ya amani na utulivu, maelewano na kusaidiana; kila raia mwema awe huru kufanya biashara anayoitaka bila bughudha,” amesema.

Simulizi ya Mwinyi vita ya ‘Magabachori’
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,017
2,000
Hakukuwa na mageuzi yoyote ya kiuchumi zaidi ya RUKHSA kwenye kila kitu. Hayo ndiyo niliyoyasikia kwa wakubwa wakati huo. Rushwa nje nje ugongaji wa viwanja vya kujengea nyumba nje nje na mkewe mama siti alishiriki sana katika biashara hiyo haramu pia mama siti alikamatwa Dar Airport akitokea Zenj kuelekea Uarabuni na dhahabu kibao alizokuwa akienda kuuza kule. Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo John Mrema akafunika funika kisha likapotea kirahisi rahisi tu.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,696
2,000
Hakukuwa na mageuzi yoyote ya kiuchumi zaidi ya RUKHSA kwenye kila kitu. Hayo ndiyo niliyoyasikia kwa wakubwa wakati huo. Rushwa nje nje ugongaji wa viwanja vya kujengea nyumba nje nje na mkewe mama siti alishiriki sana katika biashara hiyo haramu pia mama siti alikamatwa Dar Airport akitokea Zenj na dhahabu kibao alizokuwa akienda kuuza kule. Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo John Mrema akafunika funika kisha likapotea kirahisi rahisi tu.
Sema wewe kiazi, mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi! Eti nini? Mageuzi ya kiuchumi? Wanatutania hawa! Kuachia nchi ijiendee yenyewe kama hakuna uongozi ndiyo wanaita mageuzi ya kiuchumi? Hatujasahau!
 
Turnkey

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
7,258
2,000
Bakhressa pale vingunguti kwenye vinu vyake ...Mrema na vijana wake walienda kuzunguk eneo lile ili wakaguwe baada ya kupata habari kuwa kuna pembe za ndovu..ikapigwa simu kutoka Ikulu waondoke Mara moja..alafu jitu la juzi linasifia matajiri uchwara hawa...
 
mtaa umetulea

JF-Expert Member
Nov 17, 2020
1,680
2,000
Bakhressa pale vingunguti kwenye vinu vyake ...Mrema na vijana wake walienda kuzunguk eneo lile ili wakaguwe baada ya kupata habari kuwa kuna pembe za ndovu..ikapigwa simu kutoka Ikulu waondoke Mara moja..alafu jitu la juzi linasifia matajiri uchwara hawa...
Si wanasema alikua anauza maji barabaran
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
29,920
2,000
Ally Hassan Mwinyi alikuwa anamuogopa Mchonga ila angeliweza kuibadilisha Katiba na kuiindoa Nchi kwenye Ujamaa uliofeli.

Demage iiloyofanywa na Ujamaa ni kubwa sana ndio imetufikisha hapa leo ccm haijui hata vipaumbele vya Nchi

Wananchi hawana huduma na Umeme Wanafunzi wanasomea kwenye Mapagara halafu Phd feki inakurupuka kwenda kununua Ndege Mpya kwa Keshi.
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
662
1,000

Simulizi ya Mwinyi vita ya ‘Magabachori’​

mwinyipic

Summary

  • Katika mfululizo wa simulizi za kitabu cha ‘Mzee Rukhsa; Safari ya Maisha yangu’ Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameendelea kuibua mambo yaliyomsumbua wakati wa utawala wake, likiwemo la mvutano wa wafanyabiashara nchini.
Dar es Salaam. Katika mfululizo wa simulizi za kitabu cha ‘Mzee Rukhsa; Safari ya Maisha yangu’ Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameendelea kuibua mambo yaliyomsumbua wakati wa utawala wake, likiwemo la mvutano wa wafanyabiashara nchini.

Mzee Mwinyi ambaye pia katika kitabu hicho ameeleza mageuzi ya kiuchumi aliyoyafanya katika utawala wake, ameibua namna wafanyabiashara wenye asilia na Kihindi walivyoathiriwa na sera za ujamaa ambazo kupitia Azimio la Arusha walinyang’anywa mali zao, zikiwemo nyumba, mashamba, viwanda na biashara.

“Inakadiriwa kuwa karibu Wahindi 50,000 walikimbia nchi baada ya mali zao kutaifishwa kwenye miaka ya 1970 na wakati wa vita ya uhujumu uchumi miaka ya mwanzo ya 1980, wengi wakienda Uingereza na Canada,” ameandika Mwinyi.

Ameongeza kuwa hali hiyo iliwafanya wazawa kuona kuwa wafanyabiashara hao hawakuwa wazalendo. Hata hivyo, ameandika kuwa baada ya kuingia madarakani alifanya mageuzi ya kiuchumi yaliyoweka wazi milango kwa wafanyabiashara waliokimbia kurejea nyumbani.

Ameendelea kueleza kuwa kupitia mwanya huo, wafanyabiashara, hasa wenye asili ya Kihindi walikuwa wakifanya biashara za magendo, meno ya tembo na dawa za kulevya.

“Zilikuwepo tuhuma kuwa wamejijengea kinga ya kutokamatwa kwa kuwahonga baadhi ya viongozi wa siasa na Serikali ikiwemo kwenye baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama,” ameandika.

Ameandika kuwa chuki baina ya wafanyabiashara wenye asili ya Afrika na Wahindi iliibuka huku baadhi ya wanasiasa wakiitumia kama mtaji wao wa kisiasa kwa kueleza jinsi Wahindi walivyopewa upendeleo. “Yalikuwepo maneno mengi, ilimradi kukawa kumeibuka chuki na kwa kweli uadui baina ya wafanyabiashara wa Kiafrika na wa Kihindi.

Mambo ya ajabu kabisa!” Akerwa na neno ‘Magabachori’ na ‘Walala hoi’ Amemtaja aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi akisema “Mchochezi mkuu alikuwa Christopher Mtikila ambaye aliwaita wafanyabiashara wa Kihindi ‘Magabachori’ na Watanzania wenye asili ya Kiafrika ‘Walalahoi.

“Jambo hili liliniudhi na kunisikitisha sana. Si jambo la ajabu hata kidogo kuwepo kwa ushindani mkali baina ya wafanyabiashara, la kutisha na kusikitisha ni pale ushindani na pengine wivu wa biashara unapogeuka kuwa uadui kwa msingi wa ubaguzi wa rangi, dini au ukabila,” ameandika.

Amesema suala hilo lilikuwa ni hatari kwa Taifa, kwani lingeachwa lingezaa chuki zaidi hata kwa wafanyabiashara kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, hasa Wapemba.

“Baada ya hapo tungeshuhudia malumbano pengine baina ya ‘wazawa’ wenyewe kwa wenyewe. Kwani inawezekana kabisa wafanyabiashara wa Kihaya wasiwapende wale wa Kichaga na wa Kichaga wakawachukia Wakinga.”

Akitoa mifano ya nchi zilizokuwa na ubaguzi wa kibiashara, zikiwemo Indonesia, Malaysia, Rwanda na Burundi, Mwinyi amesema alikemea vikali hali hiyo. “Kwa mfano, Reginald Mengi alipokea barua ya vitisho kwa uhai wake na usalama wa mali zake.

Serikali ikachukua hatua za kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani na yeye mwenyewe tukampa ulinzi kwa muda wa kutosha pamoja na mali zake.

“Hali kadhalika wafanyabiashara wa Kihindi nao walipokea barua za vitisho kwao, familia zao na mali zao,” ameandika.

Amebainisha kuwepo kwa kikundi kilichoitwa black mamba chenye lengo la kutaka kuwadhuru Wahindi. “Nao pia tulianzisha uchunguzi dhidi yao kutaka kujua kama kweli wapo na malengo yao ni yapi.

La muhimu ilikuwa ni kutoa ulinzi kwa wote ambao walikuwa na sababu za kutosha kuhofia athari kwa maisha yao na mali zao,” ameandika.

Licha ya kukiri kuwepo kwa vitisho hivyo, pia ameandika kuwa visingesababisha madhara ya aina yoyote, bali ulikuwa ni ushindani wa kibiashara uliotishia kwenda kusikofaa.

Ameandika kuwa ushindani huo ulisababishwa na mageuzi ya kiuchumi aliyoyafanya katika utawala wake yaliyosababisha wafanyabiashara kujitanua zaidi.

“Sikutazamia ambao huko nyuma walikuwa na ukiritimba wa biashara fulani watachukia au kujaribu kuzuia wengine wasifanye biashara kama yao.

“Tulitaka kujenga uchumi huria katika hali ya amani na utulivu, maelewano na kusaidiana; kila raia mwema awe huru kufanya biashara anayoitaka bila bughudha,” amesema.

Simulizi ya Mwinyi vita ya ‘Magabachori’
Sukuma gang wana mambo yao.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,660

Nani alikuwa mtazama uvaaji wake, kwanini hakumuweka vizuri tai yake hapa
1620920992678.png
 
JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,101
2,000
Hakukuwa na mageuzi yoyote ya kiuchumi zaidi ya RUKHSA kwenye kila kitu. Hayo ndiyo niliyoyasikia kwa wakubwa wakati huo. Rushwa nje nje ugongaji wa viwanja vya kujengea nyumba nje nje na mkewe mama siti alishiriki sana katika biashara hiyo haramu pia mama siti alikamatwa Dar Airport akitokea Zenj na dhahabu kibao alizokuwa akienda kuuza kule. Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo John Mrema akafunika funika kisha likapotea kirahisi rahisi tu.
Upumbavu tu.

Ukipewa ruksa ya kufanya biashara utakavyo unakuwa mwizi, ukipewa uhuru wa maoni unatukana tukana hovyo . Ndo baadhi ya raia wa TZ hao.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,353
2,000
Bakhressa pale vingunguti kwenye vinu vyake ...Mrema na vijana wake walienda kuzunguk eneo lile ili wakaguwe baada ya kupata habari kuwa kuna pembe za ndovu..ikapigwa simu kutoka Ikulu waondoke Mara moja..alafu jitu la juzi linasifia matajiri uchwara hawa...
Kuna mengi huku duniani!
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,660
2,000
“Mchochezi mkuu alikuwa Christopher Mtikila ambaye aliwaita wafanyabiashara wa Kihindi ‘Magabachori’ na Watanzania wenye asili ya Kiafrika ‘Walalahoi.

“Jambo hili liliniudhi na kunisikitisha sana. Si jambo la ajabu hata kidogo kuwepo kwa ushindani mkali baina ya wafanyabiashara, la kutisha na kusikitisha ni pale ushindani na pengine wivu wa biashara unapogeuka kuwa uadui kwa msingi wa ubaguzi wa rangi, dini au ukabila,” ameandika.
What would happen kama ingekuwa katika awamu ya juzijuzi
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,017
2,000
Wapumbavu kama wewe ni tatizo kubwa sana Tanzania. You’re all suffering from Acqured Stupidity eti alileta mageuzi ya kiuchumi!!!! Kwa kufanya lipi!? Na mageuzi hayo ya kiuchumi yaliinuaje uchumi wa nchi na wa Tanzania na kuboresha maisha yao? Pato la Taifa liliongezeka? Kwa kiasi gani? Pato la Mtanzania liliongezeka kwa kiasi gani? Hakuna hizo data za kusupport uongo wake wa kuleta mageuzi ya kiuchumi.
Upumbavu tu.

Ukipewa ruksa ya kufanya biashara utakavyo unakuwa mwizi, ukipewa uhuru wa maoni unatukana tukana hovyo . Ndo baadhi ya raia wa TZ hao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom