Simulizi ya maisha: KABURI LA MSOMI

Simulizi ya maisha: KABURI LA MSOMI

JJ FORMAR

Member
Joined
May 29, 2025
Posts
34
Reaction score
32
KABURI LA MSOMI.

Karibuni sana wapenzi wa simulizi, leo naitambulisha kwenu simulizi hii iitwayo KABURI LA MSOMI. Ndani ya simulizi hii utakutana na visa, mikasa na matukio ya maisha kwa ujumla, vimbwenga, mapenzi wivu, usaliti, chuki na mauaji. Mwandishi anakukaribisheni kutoa maoni ushauri na mapendekezo usomapo simulizi hii.

Jina la simulizi: KABURI LA MSOMI.
Na Mtunzi wako.

COOOOOOOOUUUUUUUUTTTT!!!
Ilikuwa ni sauti ya juu iliyosikika vema ndani ya chumba cha mahakama kuashilia kuwa shauri lililokuwa likiendeea mahakamani limefungwa kwa siku ile, hivyo wote waliokuwemo mle ndani walinyanyuka vitini na kusimama wima ikiwa ni ishara ya kutoa heshima kwa mamlaka ya Mahakama na mheshimiwa Hakimu alisimama na kutoka mle ndani akifuatiwa na wasaidizi wake.
Kilipita Kimya kidogo kabla ya sauti na minong'ono kuanza kusikika tena. Hazikuwa sauti za kueleweka kwani kila mmoja alikuwa akiongea la kwake, huyu akiongea kwa kukenua na kucheka, huyu akiongea kwa hasira na kuchukia, hawa walikumbatiana na kupongezana hawa walinuniana na kusonyana yaani kulikuwa na hisia mchanganyiko ndani ya ukumbi wa Mahakama ile. Hata hivyo kwakuwa tayari waheshimiwa walikwishaondoka, hata wale wasikilizaji wengine walianza kuondoka, mmoja mmoja kwa walionuna pasipo kuongeleshana, huku kwa wenye furaha wakishikana mikoni na kuongozana kwa madaha na mbwembwe mithili ya maharusi watokapo kanisani kufunga pingu za maisha.

Nje ya Mahakama wanaonekana mamia ya watu, waliojikusanya mafungu mafungu, hawa wameketi na wengine wamesimama ilimradi kila mmojawao alikuwa yupo uelekeo wa Mahakama ile. Katikati ya mamia wale wanaonekana wachache waliokuwa ndani ya sale safi huku wakiwa makini kufatila kila kilichokuwa kikifanywa na umati ule. Bila shaka, hawa walikuwa Askari Polisi waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kawaida kuhakikisha usalama wa raia wale. Haikueleweka ni nini hasa kimewakusanya raia wengi kiasi kile nje ya Mahakama ile maana haukuwa utaratibu wala mazoea ya raia wa mji ule kujazana nje ya mahakama eti kwa sababu wanafuatilia kesi.
Hali kama ile ingetokea katika baadhi ya kesi za watu maarufu, hasa wale wanasiasa vipenzi vya wananchi, ndipo ungeweza kushuhudia umati wa watu wengi namna ile, nje na ndani ya viwanja vya Mahakama, lakini leo hii hali ilikuwa tofauti kabisa maana ijapokuwa haikuwa kesi ya kisiasa, umati ulikuwa mkubwa nje ya Mahakama ile ndogo ya wilaya.

Ukubwa na ongezeko la mkusanyiko wa watu ndio uliwafanya askari polisi waliokuwa zamu siku ile kutoa taarifa kwa wakubwa wakiielezea hali hiyo iliyoonekana kutokuwa ya kawaida na kuomba ongezeko la askari wengine ili hata ikitokea sintofahamu yoyote iwe rahisi kuikabili. Haukupita mda mrefu, zilionekana gari mbili zenye nembo ya jeshi la polisi Ubavuni zikiingia kwa kasi sana ndani ya eneo la Mahakama. Kabla hazijasimama kisawasawa, baadhi ya askari waliruka kutoka ndani ya magari yale na kudunda chini kwa ukakamavu wa hali ya juu. Jambo hilo lililopelekea umati kupiga mayowe na kelele za kushangilia. "Jambo Afande" "Jambo" "Jambo Afande" Walipeana salamu na bila kupoteza wakati walipangiana majukumu ya kutekeleza mahali pale.
Kusemakweli hali ya hewa ilikuwa nzuri sana siku hiyo maana licha ya uwepo wa mawingu kiasi lakini bado mvua haikunyesha, hivyo umati ule uliendelea kusubiri pale nje kwa utulivu mkubwa sasa tofauti na mwanzoni ambapo walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa. Labda ungesema wamechoka, lakini hapana, maana bado walionekana kuwa na shauku ya kuona madai yao yakitekelezwa, ogezeko la maaskari polisi ndiyo kilikuwa chanzo cha utulivu ule, ni wakati ambapo Mahakama ilikuwa ikiendelea kulitafutia utatuzi lile lililokuwa limevuta hisia za watu wengi kiasi kile.

Hali ilibadirika baada ya wale waliokuwa ndani kujitokeza nje, hapo ilianza minong'ono ya sauti za chinichini kabla ya mwanaume mmoja kuanza kuimbisha wimbo kwa sauti ya juu,
Haki itendeeke, ee
Haki itendeeke, eee
Hatutokaa kimya!!!!
Mpaka mnyonge apewe haki yake!!!!!

Aliimba kwa nguvu na kwa sauti ya juu kabla ya wenzake kudakia ikawa sasa ni kuimba kwa kupokezana na umati wote ulikuwa ukitamka na kuimba maneno yale kwa sauti moja ungezani ni wanakwaya waliopitia mafunzo ya uimbaji. Hali ilibadirika zaidi pale alipojitokeza mwanaume mmoja toka ndani ya Mahakama, alikuwa mwanaume mfupi mfupi aliyevalia tracksuit ya bluu, miwani machoni, raba nyeupe miguuni nywele nyeusi zilizoonekana kutunzwa sana, na mkononi alishikilia kibegi kidogo cha mkononi huku akitafuna kitu mdomoni. Ukimwangalia kwa haraka ungemwona kuwa na uso uliosawajika, hakuwa na furaha japo alijitahidi kuficha hilo.

Watu Walichafukwa zaidi baada ya kumuona mwanaume huyu, nyimbo ziliimbwa zaidi na kwa sauti ya juu, wengine walitoa kauli chafu kumtukana mwanaume yule ambaye hakuonekana kujali sana kuhusu kilichokuwa kikiendea pale nje ya mahakama kwani kile kilichotokea ndani ya Mahakama kilikuwa kimechanganya na kumuumiza zaidi.

Alikuwa Akitatembea kwa hatua za taratibu mithili ya aliyeogopa kujikwaa, hakuwa sawa kabisa mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani mwake hasa kila alipokuwa akijaribu kutafakari yaliyokuwa yanampata sasa. Mwanzoni hakujisumbua na Kelele za watu wale mpaka pale alipopigwa kichwani na chupa ndogo iliyorushwa na kijana mmojawapo wa makutano waliuwepo mahali pale.
Hapo alishtuka akijishaangaa kwa kuwa mjinga kiasi cha kushindwa kuwa makini na hatua zake,hata hivyo aliamua kuwa mpole maana katikati ya umati ule asingeweza kufanya chochote, aliinama na kuiokota ile chupa akataizama kwa kitambo kidogo huku akiiminya kwa hasira kisha akaitia ndani ya kibegi alichokishikilia mkononi.
Wengi walibaki kumshangaa maana hata polisi waliokuwa wakijaribu kumrinda asifikiwe na baadhi ya raia wenye hasira kali walishindwa kuelewa nini hasa kilikuwa kikimpa jeuri namna ile kiasi cha kusimama akionekana kutokuwa na haraka ya kutoweka katikati ya raia walioonyesha chuki za waziwazi juu yake.
Ni kama alizubaa zaidi maana alisimama jambo ambalo lilikuwa ni hatari sana kwake, na kadili alivyozidi kupoteza mda mahali pale ndivyo umati ulivyokuwa ukimkaribia, kama siyo uimala wa askari basi huenda angeishia katika mikono ya raia wale ambao bila shaka wangemuumiza kwa kumjeruhi vibaya au hata kuumuua kabisa maana walimtamani kweli.
Mmoja wa wasaidizi wake alimfata na kumshika mkono alimshinikiza kwa kumvuta na kumlazimisha kuiingia ndani ya gari ambalo liliwashwa haraka na kutoweka kwa kasi mahali pale kiasi cha kuwatimulia vumbi raia wale ambao walikitafsiri kitendo kile kuwa kosa la makusudi alilolifanya mwanaume yule na baadhi yao walijiapiza kutomsamehe kamwe.

Matukio yote hayo yalikuwa yakifatiliwa kwa ukaribu zaidi na jopo la wanaume wanne waliokuwa wameketi kuzunguka meza moja yanye screen iliyokuwa ikionyesha yote yaliyokuwa yakiendelea nje ya Mahakama. "Kazi nzuri sana imefanyika, naamini huu ni mwendelezo mzuri, na kwa kasi hii naona tutafanikiwa hata kabla ya wakati kufika" Aliongea mmoja miongoni kwa watu wale aliyeonekana kuwa kiongozi wao na baada tu ya kauli ile wote walisimama na kutoweka mahali pale pasipo kufanyika maongezi zaidi.

Juu ya jengo moja refu kidogo lililokuwa mkabara na Mahakama ile wanaonekana vijana wawili waliokuwa wakikusanya na kupakia baadhi ya vifaa vyao ndani ya begi kubwa walilokuwa nalo "mpaka hapa kazi yako nimeikamilisha, nafikiri sasa ni mda wa malipo, nikatie asilimia zangu nitembee" Aliongea mmoja ambaye mda huo alikuwa kainama akikusanya baadhi ya vifaa vyake.
Hata hivyo hakupokea majibu toka upande wa pili, aliamua kunyanyuka na kumtazama mwenzake aliyekuwa kimya mda wote akionekana kutafakhari kitu. "sawa bwanamdogo, haina shaka malipo yako utapata kama tulivyokubaliana" Alijibu mwanaume yule kuutoa wasiwasi wa mwenzake. "sasa hela yangu naipataje bosi, maana mda tuliokubaliana ndiyo huu, baada tu ya kumaliza kazi, sasa naona unanitazama tu hufanyi utaratibu wowote mimi nikapata hela yangu" Aliongea tena yule kijana ambaye sasa ameshasimama, kashikilia begi lake mkononi.
"Punguza wasiwasi dogo, hela ipo, okota kwanza hiyo frashi hapo chini tushuke mtaani nikakutolee pesa yako benki". "Haina noma mkubwa, kikubwa mimi nipate changu maana kazi yenyewe ni ngumu sana, kurekodi hii video kwenye eneo kama hili bila kibari maalumu ni jambo hatari sana kaka, ukibainika adhabu yake siyo ya kitoto, na ukizingatia sina mtu serikalini wa kunitete,,,,,, "
Kauli yake ilikatishawa na shambulio la ghafla alilofanyiwa, alijikuta kabanwa shingo na mikono yenye nguvu na kwakua hakuwa amejiandaa kwa tukio hilo aliishia kufurukuta akipambana kujinasua toka kwenye kabari ile. Alifurukuta bila mafanikio kwani adui yake alikuwa mwenyenguvu zaidi, kadili mda ulivyozidi kwenda pumzi zilianza kumwishia, miguu ilikosa nguvu na alijikuta mwenyewe bila kupenda akianguka chini. Kitendo hicho hakikumfanya adui yake kumuachia hivyo alianguka naye akiwa bado kalishikilia kwa nguvu shingo lake.
Ni mpaka pale alipojilidhisha kuwa uhai umeshauacha mwili wa windo lake ndipo aliuachia mwili wa kijana yule, mwanaume muuaji alisimama huku akihema sana kutokana na pulukushani aliyoipata wakati wa kutekeleza mauaji yale, inaonekana hakuwa binadamu wa kawaida, kuua kwake lilikuwa suala dogo ambalo angalifanya mda wowote kwa ustadi wa hali ya juu sana. Aliiwasha simu yake na kuipiga mahali, "Bosi, namba mbili imekamilika sasa" Aliongea maneno hayo mala baada ya simu kupokelewa na mtu wa upande wa pili ambaye hakutoa jibu lolote zaidi ya kuikata simu ile. Baada ya simu kukatwa mwanaume muuaji alilichukua lile begi, aliangaza huku na kule akikikaagua chumba kile kwa awamu ya mwisho kabla ya kufungua mlango na kutokomea nje.

Nje ya Mahakama umati ulikuwa ukizidi kupungua, watu walikuwa wakitoka makundi makundi, baadhi yao waliendelea kuimba nyimbo za kuhanikiza kufanyika kwa yale wayatakayo huku wengine wakipiga kimya ungedhani sio wao waliokuwa wakizomea mda mchache uliopita.
Kulikuwa na misafara mikubwa miwili ya watu, wapo walioelekea upande wa kusini wengine wakishikana kuelekea kaskazini, hata hivyo bado askari polisi waliokuwepo mahali pale wakiendelea kuwadhibiti watu wale kuepusha mtafaruko zaidi. Mda huo simu ilipigwa ikaitikiwa, "Halloo bosi" "Vipi mbona mpaka sasa sijapata mrejesho wowote" Iliuliza sauti ya upande wa pili wa simu, naye mpokeaji akajibu "Bosi, namba moja tayali ilishakamilika dakika tano zilizopita, lakini nilish,,,,, "
Simu ile ilikatwa na aliyekuwa upande wa pili pasipo kumpatia nafasi muongeaji kumalizia kauli yake. "Huyu naye fala kweli, sasa mbona amekata, anashindwa kusubiri nikamwelezea kuwa nilichelewa kumtaarifu kwa sababu sikupata muda wa kufanya hivyo, sasa raia wengi kiasi kile anafikiri ingekuwaje, mda mwingi nilikuwa makini kuwawangalia zaidi ya kufanya jambo lingine. Hata hivyo atajijua mwenyewe kikubwa kazi nimeifanya kama ilivyotakiwa" Alibaki akijiongelesha mwenyewe, akionekana kutofurahishwa na kitendo cha kukatiwa simu na mtu aliyekuwa upande wa pili.

Ni ndani ya nyumba moja ndogo ambayo licha ya kunakshiwa kwa rangi nzuri ya bluu lakini bado inaonekana kuwa ya zamani sana kutokana na muundo wake, aina ya ujenzi na muonekano wake, ilikuwa ni nyumba iliyoezekwa kwa vigae vilivyokwishakuwa vikuukuu sana kiasi cha kuruhusu nyasi kuota juu yake. Kwenye moja ya vyumba vya nyumba hii anaonekana msichana mmoja, amejilaza kwenye sofa kubwa lilokuwa mle ndani, mkononi ameshika grasi ya wine nyekundu akiendelea kukigigida kinywaji hicho taratibu kabisa bila hofu yoyote, mala nyingi jicho lake akiligeuza kwa madaha na mbwembwe kuiangalia simu ndogo iliyokuwa mbele yake juu ya meza ndogo ya kioo.
Kwa kumwangalia tu alikuwa ni aina ya wanawake ambao shida haikuwa sehemu ya maisha yao, mwanamke mrefu kidogo, mweupe, aliyesuka nywele za bei mbaya akiwa ndani ya kijinguo cha kulalia kiliyoiacha wazi sehemu kubwa ya makalio yake.
Kutokana na aina ya uvaaji wake ni wazi kabisa siku hiyo hakuwa na mpango wa kutoka nje ya nyumba ile, pengine labda kulikuwa na kazi maalumu alikuwa akiifanya mahali pale maana hakufanania kuwa mwenyeji wa nyumba ile. Ghafla ile simu ndogo juu ya meza ilitoa mwanga mkali na kuanza kuunguruma kwa nguvu "nshwssss, mda wote ulikuwa wapi, mbona hukupiga!"
Alisonya msichana yule na kutoa maneno hayo huku akijinyanyua kivivu na kukaa. Aliichukua simu ile na kubonyeza kitufe cha kupokea, hakuongea mpaka pale iliposikika sauti ya upande wa pili " Sikiliza Emmy tupo hatua nzuri sasa, mpango namba moja na namba mbili tayali imekamilika, vijana wanajiandaa kukamilisha namba tatu na ndiyo itakuwa kazi ya mwisho kufanyikia mjini kwa siku ya leo, namba nne na namba tano ni juu yako, jitahidi mala kila kitu kitakapokuwa sawa ulikamilishe hili, kumbuka tunakutegemea sana katika hili" Baada ya maelezo hayo, mtu aliyekuwa upande wa pili alikata simu pasipo kungojea jibu lolote.
Baada ya simu ile kukatwa, yule msichana ambaye sasa tunamfahamu kwa jina la Emmy alitoa pumzi ndefu kisha alinyanyuka na kujishikilia kiuononi mithiri ya mchezaji wa mpira wa miguu aliyechoka. Aliinyanyua grasi ile ya wine na kukitazama kinywaji hicho kilichokuwa kikiumwagilia moyo wake kwa wakati huo, alikigigida kinywaji chote mdomoni kwa mkupuo kisha akaiweka grasi mezani na kutoweka mle chumbani.

Pembeni kidogo ya jengo la Mahakama kulikuwepo na kituo cha mafuta ambacho wenyeji wengi wa mji ule hupendelea kukiita "sheli" Ndani ya sheli ile shughuli zilikuwa zikiendelea kama kawaida, siku hiyo biashara ilikuwa nzuri sana kutokana na uwepo wa watu wengi maeneo yale, hivyo biashara hasa ya vinywaji na vitafunwa vilivyokuwa vikipatikana kwenye supermarket ndogo ya sheli hiyo viliuzika sana. Tokea upande wa kuingilia linaonekana gari dogo aina ya "Spacio" likiingia ndani ya sheli ile, na kwenda kupaki uelekeo wa supermarket ile, akashuka kijana mmoja aliyeonekana kuwa na umri kati ya miaka 24 au 25 hivi. Kijana huyu anaonekana kuwa mwenyeji wa maeneo yale, alimchangamkia na kuongea na binti muhudumu wa duka lile kisha akatoweka mahali pale.
Hakwenda mbali na sheli ile bali alizunguka na kuchoma ndani ya jengo moja la ghorofa lililokuwa kwa nyuma, alizipandisha ngazi harakaharaka kuelekea ghorofa ya juu. Alipofika juu ni kamavile alichanganywa na mandhari ya mle ndani "du! Licha ya uenyeji wangu maeneo haya lakini sijawahi kuufaidi utamu wa huu mjengo" Aliwaza wakati ambao alikuwa akijihangaisha kusoma namba zilizoandikwa kwenye milango iliyozunguka korido ile.
Japokuwa hakuwa mgeni wa jengo lile lakini yaelekea alichanganywa na mpangilio wa vyumba, bado hakuwa amekipata kile alichokuwa akikitafuta. Alichukua simu yake ya kupangusa aina ya Tecno Common 20, aliigusa mala mbili haraka haraka ikawaka, akaingiza nywila na kwenda moja kwa moja sehemu yenye kumbukumbu ya jumbe alizokuwa akituma na kutumiwa, hapo alitafuta kidogo mpaka pale alipolipata jina la Morisi wa pili, akaligusa na kuanza kuangalia jumbe walizokuwa wakitumiana yeye na mtu huyo.
Aliweka utuo kwenye ujumbe mmoja ambao sasa aliusoma na kuuelewa "KIWILA HOTEL, room no 23, upper floor, around 8:30am" Baada ya hapo aliirudisha simu yake mfukoni na kuelekea upande wa kulia kwake, alitembea kidogo kuuelekea mlango mmoja, alipoufikia aliunyanyua uso wake na sasa aliweza kuyaona vema maandishi yaliyoandikwa juu ya mlango huo "No 23" ilikuwa imeandikwa kwa namna ya kuchonga na rangi ya manjano ya kukoleza. Mpaka hapo alijua yupo mahali sahihi kabisa, hivyo pasipo kupoteza mda alianza kubisha hodi kwa kugonga mlango taratibu "ngo ngo ngo",,,,
 
Ndiyo narudi tena JF, nakutana na vitu vyangu kabisa. 🙏🙏🙏🙏🙏
 
ILIPOISHIA
Aliweka utuo kwenye ujumbe mmoja ambao sasa aliusoma na kuuelewa "KIWILA HOTEL, room no 23, upper floor, around 8:30am" Baada ya hapo aliirudisha simu yake mfukoni na kuelekea upande wa kulia kwake, alitembea kidogo kuuelekea mlango mmoja, alipoufikia aliunyanyua uso wake na sasa aliweza kuyaona vema maandishi yaliyoandikwa juu ya mlango huo "No 23" ilikuwa imeandikwa kwa namna ya kuchonga na rangi ya manjano ya kukoleza. Mpaka hapo alijua yupo mahali sahihi kabisa, hivyo pasipo kupoteza mda alianza kubisha hodi kwa kugonga mlango taratibu "ngo ngo ngo",,,,

ENDELEA.

"Ngo ngo ngo" "Ngo ngo ngo" Alifanya hivo kwa awamu tatu mfululizo pasipo kupata jibu lolote, kidogo hali hiyo ilimuogopesha; akaiangalia saa yake ya mkononi akajilidhisha kuwa ulikuwa mda sahihi aliopanga kukutana na rafiki yake mahali hapo, "au atakuwa ameshamaliza kazi na yupo mahali anapata msosi?" aliwaza na hapo wazo la kumpigia simu likamjia, aliitoa simu yake mfukoni lakini aliishia kuiangalia tu pasipo kufanya chochote. Kumbukumbu za mda mfupi uliopita kabla hajafika mahali hapo ndizo zilipelekea akalipuuzia wazo lile, alikuwa amejaribu kumpigia rafiki yake zaidi ya mala ishirini bila mafanikio. Mwanzoni simu ingeita na kukata pasipo kupokelewa lakini baadaye ikawa haipatikani kabisa, jambo hilo ndilo lilimfanya kufika mahali hapo kwa haraka kufuatia kile walichokubaliana asubuhi na huyo rafiki yake; waliwa wamekubaliana kukutana mda kama huo sehemu hii hii alipo sasa kama ilivyokuwa imeandikwa kwenye ujumbe ule aliotumiwa. "Isijekuwa yupo na demu humu ndani maana ndivyo vitu vyake" Alitabasamu kidogo baada ya kuwaza hivo; mawazo ambayo yeye mwenyewe aliyaona kuwa ya kipuuzi sana, hata hivyo alitamani kuhakikisha kwanza mawazo yake. Alisogea karibu na kitasa cha mlango wa chumba kile akalitega sikio lake kama dishi la kingamuzi kusikiliza kama kuna milio yoyote toka mle ndani. Hata hivyo hakuambulia chochote, alijaribu kwa mala nyingine awamu hii akiongeza umakini zaidi lakini bado hakuna alichokisikia toka mle ndani zaidi ya ukimya uliotawala. Hapo aliamua kuugonga tena mlango safari hii akigonga kwa nguvu kidogo ingawaje hakukuwa na majibu yoyote hivyo akaamua ajaribu kufungua aone kama umefungwa au vipi. Kama bahati mlango ulikuwa haujafungwa, alipougusa tu na kukizungusha kitasa mlango ulifunguka bila kipingamizi chochote.

Hali ile ilimshangaza kidogo, inaonekana hakuwaza wala hakutegemea kama mlango ule ungekuwa wazi "ndiyo maana" alijisemea hivo akiamini kwamba rafiki yake atakuwa alifanya makusudi kuuacha mlango wazi ili yeye akija asisumbuke kuja kumfungulia hivyo akaamua aingie ndani. Taratibu taratibu aliusukuma mlango kwa namna ambayo ingekuwa ngumu mtu aliyeko ndani kusikia, alipanga amfanyie surprise mkulupusho rafiki yake huyo wa tangu utotoni, pasipokufanya kelele yoyote mithili ya simba anayelivizia windo lake, aliurudishia mlango baada ya kuingia ndani; mbele yake ilikuwa ni sebure ndogo iliyopangwa na kupambwa vizuri kama zilivyo sebule nyingi za hoteli za hadhi ya kati, hakukuwa na mtu yeyote pale sebuleni, lakini mazingira yalionyesha uwepo wa mtu au watu mahali pale maana vitambaa havikuwa katika mpangilio mzuri, baadhi vilisambaratika na kujikunja ishara ya kwamba kuna mtu alikuwa amelala au kukaa mahali pale hapo kabla.
Kuna waya mdogo mweupe aliuona juu ya meza ndogo iliyokuwa pale sebuleni, hapo akapata uhakika kuwa yupo mahali sahihi, alitembea kuuelekea mlango wa chumba uliokuwa upande wake wa kulia, hata hivyo ni kama alighairi kwenda kule, akaamua kukaa kwenye moja ya masofa yaliyokuwa pale sebuleni. Alichukua rimoti na kuwasha luninga iliyobandikwa ukutani, alifungulia chaneli moja iliyokuwa ikipiga mziki wa kizazi
kipya, akaweka sauti ya juu kabisa ili mwenyeji wake aisikie na ajilete mwenyewe pale sebuleni, hata hivyo hakusikia harakati zozote za kuashilia ujio wa mtu. "Litakuwa limelala hili" alijisemea hivo kisha akaanza kuita "oy msela,, Morisii,,, oya Morisi,,, wajinaa,," Aliita lakini hakukuwa na itikio lolote, ndipo alipoamua aingie kule chumbani akamwamshe jamaa yake maana kuendelea kukaa pale ilikuwa kupoteza mda wake bule.

Aliufungua mlango wa chumbani ambao nao haukuwa umefungwa kama ulivyokuwa ule wa nje, hapo ndipo macho yake hayakuamini kile alichokiona na kukishuhudia mbele yake. Ingekuwa rahisi kwake kuwaza labda ni mchezo alikuwa akifanyiwa na rafiki yake maana walikuwa marafiki walioshibana sana today enzi, hivyo angewaza alikuwa akimuigizia kama walivyokuwa wakifanyiana siku za nyuma.
Fikra zake ziligoma kabisa kukubaliana na hilo, kwanza ile namna aliyomkuta rafiki yake amelala pale chini namna alivyokuwa amelikunja shingo lake na jinsi macho yalivyokodoa, hakufanania kuwa amejilaza tu kwa kuigiza, aliona lazima kutakuwepo na kitu cha ziada hapo. "Morisi, Morisi" aliita huku akiwahi pale chini alipokuwa amelala mwenzake yule. "Morisi, Morisi, Morisi" Mara hii aliita kwa nguvu akiwa kaukumbatia mwili baridi wa rafiki yake kipenzi, alikuwa ameshajua sasa kuwa uhai haumo tena ndani ya mwili huo na swahiba yake tayali amefariki. "Morisi, morisi, Moriiiiiisii" Morisiiiii" bado hakuamini, aliendea kuita jina la rafiki yake akilia kwa uchungu sana, hakuamini kama kweli rafiki yake ndiye yule asiyeweza hata kujitetea, kujisemea au hata kujitikisa kidogo tu. Ama kweli kifo si kifo tu kama baadhi wanavyoamini, msiba haujawahi kuzoeleka hata siku moja, kijana huyu leo alikuwa akilia kama "mwanamke" akiomboleza kifo cha rafiki yake wa utotoni, halikuwa jambo la kawaida kwa kijana huyo kulia tena kwa sauti, yakimtoka machozi namna ile; kwa waliokuwa wakimjua hapo awali ungewaeleza hiki kilichokuwa kikitokea sasa wasingekuamini mpaka kesho.
Zilipita kama dakika tano, akiwa bado kaukumbatia mwili wa rafiki yake pale chini, chozi la uchungu lilikuwa likimtoka, hakuelewa afanye nini zaidi kwa ajili ya rafiki yake aliishia kumtazama tu. Hapo wazo likamjia, halikuwa moja bali yalikuwa mengi; aliwaza ajaribu
kuita majirani waje wamsaidie au awataarifu wahudumu wa pale hotelini au aite gari la wagonjwa au atoe taarifa polisi, ama kweli alikuwa kachanganikiwa hasa maana kwa wakati ule lolote lililoelekea kuwa la maana aliliwaza na alitamani kulifanya. Ghafla alinyanyuka na kutimua mbio kuelekea nje ya chumba kile, alishuka ngazi za jengo lile kwa kasi ya ajabu pasipo kujali hatari ya kuanguka, akili yake yote ilimtuma kuwahi kituo cha polisi kutoa taarifa kuhusu kifo cha rafiki yake. Hata hivyo ni kama hakuwa amewaza vizuri maana rahisi zaidi ilikuwa ni kuwapigia simu polisi kupitia namba yao ya dharura ambayo aliifahamu. "Agghhhhhh" Alilalama kwa maumivu kijana yule baada ya kuupiga take ukuta wa jengo lile kwa hasira, alijihisi kuwa mjinga aliyetaka kufanya kitu cha kijinga, yaani kukimbia kwa miguuu mpaka kituo cha polisi akatoe taarifa ulikiwa ni ujinga haswa, na kwa nini polisi, watasaidia nini, hapo alichukuwa simu yake akapiga namba ya dharura ya moja ya hospitali maarufu ya pale mjini, simu ilipopokelewa akatoa maelezo ya muhimu yaliyohitajika kisha akaikata.
Hapo kidogo alipumua kuona kwamba labda wakiwahi wataweza kumsaaidia rafiki yake "nani anajua labda ikawa hajaf,,,,," alikatisha kuwaza na akaamua kurudi kule ndani, akiharakisha kama chizi kiasi kwamba hata wahudumu wa pale mapokezi walibaki kumshangaa kijana yule. Alipofika ndani moja kwa moja alikwenda kuunyayua mwili wa rafiki yake aliyejulikana kwa jina la Morisi na kuuweka juu ya kitanda, hapo ndipo alipata wasaa wa kuuangalia vizuri; huenda alibaini mengi lakini zaidi aligundua shingo ya rafiki yake ilikuwa imevunjwa. Kuna kitu aliwaza kukifanya hapo; akaufunika mwili ule kisha akanyanyuka na kwende kusimama karibu na dirisha la chumba hicho. Haikueleweka alikuwa anapanga nini lakini ni kama alikumbuka kitu, alichukua simu yake na kuwapigia polisi kutoa taarifa za tukio lile.

Umbali wa kama kilomita nne uelekeo kaskazini nje ya mji wanaonekana wanaume wapatao kama kumi hivi, miongoni mwao wawili waliokuwa wamesimama wengine wakiwa wamekaa chini huku kila mmoja akiwa kashikiria kibegi kidogo cha mkononi. Vilikua ni vibegi vyeusi na vilionekana kuwa na ujazo wa kutosha, "Sasa vijana kama
nilivyokwisha waambieni, sitaki kosa lifanyike, hakikisheni mizigo inawafikia wahusika, wale watakaoonekana kunusa chochote taarifa zao nizipate mapema ili ufanyike mpango wa kuwanyamazisha kabla hawajafanya chochote na baada ya hapa tutakutana tena wakati wa utekelezaji wa awamu ya pili. Sitomfuatilia yeyote kujua namna gani atadili na vijana wake lakini niwahakikishie tu kwamba kosa au uzembe wowote utakaofanyika nitaishughulikia roho ya muhusika mimi mwenyewe, nadhani hapo nimeeleweka". Aliongea mwanaume mmoja miongoni mwa wale wawili waliokuwa wamesimama, na kisha wakatoweka mahali pale wakiwaacha wenzao bado wamekaa pale chini.

"Vipi Osama, unaonaje? Mpango upo kwenye mstari!" "Ndiyo, tupo vizuri mpaka sasa, na tunakoelekea kutakuwa kuzuri zaidi maana, yule jini wa kike namuamini sana, hatotuangusha" "vipi namba mbili haikusumbua!" "alikuwa mdebwedo tu, ilikuwa kazi nyepesi ambayo hata tungemwachia Kipensi naamini angeimaliza vizuri" Wawili wale waliendelea kupiga soga muda ambao walikuwa wameshafika sehemu lilipo gari lao, walipanda na kuondoka kwa mwendo wa kawaida. "Vipi usafi kule machinjioni umeshafanyika?" Swali lile ni kama lilimshitua Osama aliyekuwa akiendesha gari mda huo. Aliamua kutafuta eneo zuri na kuipaki gari kisha akageuka kumwangalia yule mwenzake ambaye naye alikuwa kamkazia macho asielewe nini anataka kufanya. "Kwakua leo niliyechinja ni mimi, basi Kipensi ndiye alipaswa kusafisha machinjio kama ilivyo ada, lakini,,,," alisita kidogo kuongea hapo akafungua droo ndogo kwenye "dashboard" ya gari, huko zilionekana simu mbili, aliichukua moja na kuipiga mahali, "Kazi iliyofanyika leo usafi halikuwa jukumu langu, hata hivyo sina uhakika kama Kipensi ameshalishughulikia hilo, ninapatwa na wasiwasi sana; maana tokea asubuhi sikumuona kwamba alikuwa yupo kikazi, ni kama vile alikuwa na ratiba zake; ninahofia isijekuwa ameenda viwanja na kama itakuwa hivyo basi nitakuwa na uhakika zaidi ya asilimia miamoja kazi haijafanyika" Alitoa maelezo hayo mda ambao simu yake ilipokelewa na mtu wa upande wa pili "Niaje kaka mkubwa" Iliongea sauti ya upande wa
pili ikitoa salamu ambayo haikumfurahisha Osama "usafi umeshafanyika?" Aliuliza swali hilo kwa sauti kavu pasipo kujihangaisha kujibu salamu aliyopewa. Swali hilo huenda lilimshitua sana Kipensi maana ilimchukua muda mrefu kidogo kujibu, huku upande wa Osama aliona tayali wasiwasi wake umetimilika, alikunja sura na kumwangalia mwenzake. "aaa, a, leo machinjio ni wapi bosi" Ilikuwa sauti ya Kipensi ikijibu swali aliloulizwa kwa njia ya kuuliza swali lingine, majibu yale yalikuwa ni ya kipuuzi kutolewa na mtu kama yeye maana yaliashiria kazi haikuwa imefanyika na muhusika hakuwa na taarifa yoyote ya wapi akaifanye kazi husika. Hapo Osama alikasilika kiasi cha kutamani kuipasulia chini simu yake, hata hivyo alijituliza hasira zake kabla ya kuongea "KIWILA HOTEL, room no 23" kisha akakata simu. "Unajua huyu bwana mdogo anazingua, ni vile tu mzee unamkubali lakini mimi sioni kama anastahili hiyo nafasi, ona mpaka muda huu ni zaidi ya lisaa zima sasa machinjio hakujasafishwa maana yake ni nini, yeye mwenyewe anaonekana kashalewa kwanza na hakumbuki hata machinjio yalipo, sasa hii kazi unafikiri ataifanyaje huoni kama raia wakifika kabla yetu itakuwa noma" Aliongea Osama kwa hasira akilalamikia uzembe uliofanywa na Kipensi. "Upo sahihi kabisa, lakini ulipaswa ukumbuke kuwa mwenzio alishazoea kuchinja tu; sina kumbukumbu ya kumuona Kipensi akisafisha machinjio kwa wakati wowote hapo kabla, hata hivyo sasahivi siyo mda mzuri kuanza kulaumiana maana huenda mpaka sasa tumeshachelewa sana, washa gari twende mjini tukajue kinachoendelea". Hakukuwa na maongezi zaidi, Osama aliwasha gari na kuitoa kwa kasi sana kuwahi mjini.

Hakuwa mbali sana na eneo lile, baada ya kutoka kule ndani alikuja nje ambapo aliingia kwenye kijumba kidogo ambacho bila shaka ndicho kilikuwa choo cha nje kama vilivyo vyoo vingi vya uswahilini. Huenda hakikuwa choo tu kama ambavyo ungezania, maana alipoingia mle ndani alifanya kuinama kama anayejisaidia licha ya kutokuwepo kwa tundu lolote mahali pale, alibakia kachuchumaa kama nusu dakika hivi akipima utulivu wa eneo lile kisha kuna sehemu aliigusa upande wake wa mkono wa kushoto mala eneo lile alilosimama likaanza kutitia kwenda chini. Kilikuwa kitendo cha sekunde kama tatu
hivi alijikuta yupo chini kabisa eneo ambapo lilikuwa la wazi, hakikuwa chumba kipana sana bali kilikuwa kidogo tu, kulikuwa na meza kubwa iliyozungukwa na viti, juu ya meza ile ilikuwepo kompyuta ndogo, kuta za chumba kile ziling'arishwa kwa rangi nyeupe, kulikuwapo saa kubwa iliyobandikwa ukutani na kalenda ndogo iliyoning'izwa chini kidoga ya saa ile.
Emiliana au Emmy kama wengi walivyozoea kumuita alikuwa ameweka umakini mkubwa kuiangalia ile kalenda, aliisogelea na kuichomoa pale ilipokuwa imeninginizwa, akatoka nayo na kwenda kukaa kwenye moja ya viti vilivyokuwemo mle ndani. Aliiangalia vizuri kalenda ile hapo likachanua tabasamu mwanana usoni mwake, alichukua kalamu akaizungushia tarehe 12 ya mwezi wa 2 mwaka 2024 kisha akajisemea moyoni "Mpaka hapa kazi itakuwa imekamilika, kitakachofata ni kula bata". Aliisogeza ile kompyuta uelekeo wake kisha akaiwasha na kuanza kubonyezabonyeza huku na kule mpaka pale alipokipata kile alichukua akikutafuta, ilikuwa ni video na hapo aliweka utuo kidogo wakati akiingalia video ile. Alitumia kama dakika tano hivi kuiangalia ile video, aliirukisha na kusimamisha baadhi ya maeneo aliyoyaona yeye kuwa ya muhimu. Baada ya kumaliza kuiangalia video ile alichukuwa frashi ndogo toka ndani ya mtoto wa meza na kuichomeka kwenye ile kompyuta, kilichofata ilikuwa ni sauti za batani za kompyuta ile iliyokuwa ikibonywezwa haraka haraka mithili ya kisimu cha kiswaswadu. Yaonekana kuna kitu alikuwa akikitengeneza juu ya video ile maana baada ya kumaliza kazi ile aliichomoa frashi yake akanyanyuka na kuelekea upande wa kulia wa chumba kile ambapo aliirudisha ile kalenda mahali pake kisha kuna sehemu alibonyeza ukuta ule ukafunguka.
Haukuwa ni ukuta kama tulivyozania bali ulikuwa ni mlango ambao kwa mtu yeyote asiye mwenyeji wa chumba kile asingeweza kuufahamu, Emmy alipitia pale mlangoni kuingia chumba cha upande wa pili. Chumba kile kilikuwa kikubwa na kipana zaidi ya kile cha mwanzo; kilionekana kama mojawapo ya vyumba vya studio ya kisasa zaidi; kulikuwapo na mitambo kadhaa, mashine za kutolea kopi, kamera za kurekodi video,
sehemu maalumu ya kurekodia sauti na vifaa vingine vingi vya kisasa. Kulikuwa na kiti kimoja nyuma ya kompyuta kubwa na hapo ndipo Emmy alienda kukaa.

Ni zaidi ya robo saa sasa Emmy akiwa bado mle ndani; mlango ulifunguka akatoka mkononi akiwa kashikilia karatasi moja ndefu yenye maandishi na picha mithili ya gazeti. Moja kwa moja alirudi tena ndani ya chumba kile alipokuwa amelala awali, awamu hii alionekana kuchoka hivyo alienda kufungua jokofu na kuchukua chupa kubwa wine, akajimiminia kwenye grasi na kuanza kuinywa taratibu kwa maringo na mbwebwe za kike. Alijilaza kwenye sofa mala hii akikitoa kinguo chake cha kulalia na kujiacha mtupu kabisa, labda ni kwa sababu ya joto la huko alikotokea maana alijitanua kidogo kuuruhusu mwili wake kupata hewa. Aliitazama ile simu ndogo pale mezani kisha akaichukua na kubonyeza namba fulani kisha akaipiga mahali.

Alikurupuka baada ya simu iliyokuwa mfukoni kwake kuanza kuita, "atakuwa nani huyu anataka kunichanganya tena kichwa changu" aliongea kwa kulalama akiwa anaitazama simu ile pasipo kuipokea, aliiacha mpaka ilipokatika, "wapuuzi tu hawa, baada ya mambo kuharibika ndipo wananitafuta" Alikuwa akiwaza hivo; mala simu ile ikaanza kuita tena, awamu hii hakujihangaisha nayo kabisa, hakuwa tayali kupokea au kumsikiliza yeyote kwa wakati ule. Alijilaza kwenye siti ya gari lake akafumba macho kuuruhusu utulivu wa akili, mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani mwake; alikuwa akiwaza namna ambavyo biashara zake zimeingia mkosi ghafla, namna kile alichokitafuta kwa jasho na damu kilikuwa kikipotezwa kirahisi na wenye mamlaka. Siyo kwamba adui zake hakuwafahamu, alikuwa akiwafahamu tena vizuri sana, shida ilikuwa ni kwa namna gani angeweza kuwakabili haliyakuwa wao ndiyo wenye mamlaka na wangeweza kufanya chochote wakati wowote watakao. Mwanzoni alijiamini sana kwamba angeweza kulimaliza suala lile yeye mwenyewe, alikuwa na jeuri; jeuri ya fedha kama ujuavyo; ni nani angeweza kumsumbua tajiri huyo!. Lakini sasa mambo yalikuwa tofauti, yeye mwenyewe alikiri kwamba awamu hii maji yamemzidi kimo; shauri lake lipo mahakamani kwenye mikona ya sheria, ambapo yeye aliona ni rahisi sana kwa wenye
mamlaka kufanya chochote watakacho sehemu hiyo kuliko wenye pesa tu maana mamlaka inayo pesa pia kama aliyokuwa nayo yeye. Kila hasebu aliyoipaga haikumletea jibu sahihi la tatizo lake, kila hatua aliyofika ni kama upande wa pili wameshapita hapo saa nyingi sana, kwa sasa alikuwa kakamatika; hana pa kutokea; amefika hatua ambayo anakiri kushindwa kulitatua tatizo linalomkabiri.
Hakuwa na namna nyingine tena, ni kama akili yake imefika mwisho; yeye kwa macho yake haoni chochote mbele hivyo itamlazimu kuwa na mtu wa kumuongoza sasa; mtu atakayemshika mkono na kumuelekeza njia sahihi ya kwenda. Suala hili lilikuwa gumu sana kwake, yaani kumuachia mtu mwingine kushughulikia jambo linalomuhusu yeye moja kwa moja! Ilikuwa vigumu sana kufanya hivo katika nyakati ambazo angekuwa mzima, yaani suala lolote linalomhusu yeye au familia yake angepambana alimalize mwenyewe. Hapo kabla yalishamkuta; alishawahi kuionja radha chungu ya usaliti aliofanyiwa na watu aliowaamini akawaweka kusimamia vitu vyake mwisho wakamfanyia ubaya, tokea hapo alijifunza kujitegemea; kujipambania hasa kwenye mambo yanayomhusu moja kwa moja, na kwa kuwa alikuwa msomi mwenye taaluma ya sheria mala zote angesimama mwenyewe kujitetea mahakamani bila kutegemea usaidizi wa msomi mwingine. Wakati huu hakuwa na namna nyingine tena, kama mwanajeshi aliyezidiwa mbinu za kivita hakuwa na budi kunyanyua mikono juu. Aliichukua simu yake na kupiga mahali, "naam kiongozi" Iliitika sauti ya upande wa pili "vipi wakili msomi, uko wapi kwa sasa?" aliuliza swali ambalo lilijibiwa na mtu wa upande wa pili; alikata simu akaliwasha gari lake na kutoweka mahali hapo.

Gari lilikuwa likikimbia kwa mwendo wa kasi sana maana tayali alishachelewa sana kufika machinjioni, mpaka mda huo ilikuwa imepita zaidi ya nusu saa tokea alipopigiwa simu na mkubwa wake kazini. "Kimbia wewe mpuuzi, tupo nje ya muda mpaka sasa," Alifoka Kipensi baada ya kijana wake kupunguza mwendo wa gari wakati akiikunja kona kuingia barabara iendayo KIWILA HOTEL
ITAENDELEA.
 
ILIPOISHIA.
Gari lilikuwa likikimbia kwa mwendo wa kasi sana maana tayali alishachelewa sana kufika machinjioni, mpaka mda huo ilikuwa imepita zaidi ya nusu saa tokea alipopigiwa simu na mkubwa wake kazini. "Kimbia wewe mpuuzi, tupo nje ya muda mpaka sasa," Alifoka Kipensi baada ya kijana wake kupunguza mwendo wa gari wakati akiikunja kona kuingia barabara iendayo KIWILA HOTEL.

ENDELEA.

Ilikuwa hivi,,,,, tokea asubuhi ya siku ile Kipensi hakuwa na ratiba yoyote ya maana ambayo ingemfanya kuwaza hivyo aliamua kutembelea kumbi moja ya starehe; huko hakwenda peke yake bali aliambatana na vijana wake wa kazi, kwa pamoja waliamua siku hiyo wakayafaidi mema na matamu ya dunia maana siku kama hizo huwa hazijirudii. "SHINING HELL" Lilikuwa jina maarufu miongoni mwa wale wapenda kula bata ndani ya mji ule. Lilikuwa eneo lililojitenga nje kidogo ya mji; huko ungepata kila aina ya starehe pendwa ya vijana hasa wale wanaojiita watoto wa mtaa, watumia kijiti. Hapa ndipo Kipensi na wenzake walifika, kila mmoja alikuwa akitanua kwa namna apendayo yeye. Pombe na mademu ndivyo vilikuwa vilevi pendwa vya Kipensi; siku ile alikuwa ndani ya chumba kilichojitenga akila bata na madadapoa wawili na huko kilichokuwa kikifanyika kilimfanya kujisahau kabisa kuwa yupo katika dunia ya kawaida. Alikuwa akikatikia nyuma ya kiuno cha mmoja wa wale dadapoa mda simu yake inaanza kuita, haraka sana malaya mmoja alijitoa pale kitandani na kwenda kuichukua simu na kumpatia, alitazama jina la mpigaji na hapo alishtuka kidogo, "niaje kaka mkubwa" aliongea kwa sauti yenye kitetemeshi kidogo tofauti na vile alivyokuwa akiongea na warembo wale. Hapo ndipo alipopewa maelekezo yale na Osama ambaye ndiye aliyekuwa kampigia.
Hakukaa kuendelea tena na michezo ile aliyokuwa akifanya na wale warembo; alinyanyuka haraka na kwenda kuvaa nguo bila hata kujisafisha, "Jamani Beiby ndiyo unaniacha hivi jamani" ilikuwa sauti ya kulalamika ya mmoja wa changudoa wale ambaye mpaka dakika ya mwisho ndiye alikuwa akimkatikia mwanaume yule. Kipensi hakujihangaisha kujibu sauti ile ambayo sasa aliiona kuwa ya ajabu, alipomaliza kuvaa alichomoa noti kadhaaa na kuzitupia pale kitandani kisha akaondoka kwa kasi bila hata kuaga. Haraka haraka aliwakusanya vijana wake wakapanda gari na kuondoka mahali pale. "We mpuuzi mbona hukunikumbusha kama leo nina kazi ya kusafisha machinjio?" Alikuwa kalivuta sikio la kijana wake mmoja aliyekaa Upande wake wa kulia aliyekuwa kalewa vibaya. Kuanzia leo nakunyang'anya cheo cha uratibu wa mipango, Kiba wewe ndiye utakichukua hicho cheo harafu wewe fala baada ya hapa uje nikupe adhabu yako." Alikuwa akibwabwaja maneno yale kwa sauti ya ulevi iliyowafanya vijana wengine kucheka namna bosi wao alikuwa akivigawa vyeo. Kipensi na vijana wake watano walikuwa wakielekea upande wa katikati ya mji kuwahi kufanya kazi waliyoagizwa. Gari ile ilikimbizwa kwa kasi sana mpaka mda wanafika kwenye kona na ndipo wakashika balabala iendayo KIWILA HOTEL. Iliwachukua kama dakika tatu wakawa wamefika pale hotelini. Nje ya hoteli kulikuwepo na magari mawili ya polisi, mpaka hapo Kipensi alijua kuwa walishachelewa, wamewahiwa na raia aliyepiga simu kuita polisi. Aliwazuia vijana wake wasishuke ndani ya gari lile maana alielewa uwepo wao ungezua taharuki eneo kama lile yalikofanyika mauaji na ukizingatia vijana wenyewe walijulikana kama wahuni wa mtaani.
Zaidi ya dakika tano zilipita, bado wote wakiwa wamekaa ndani ya gari pasipo kushuka mtu yeyote, walihitaji kwanza kujua nini kilikuwa kikiendelea mahali pale. Hata hivyo ni kama kuna baadhi ya polisi walikuwa tayali wameanza kulitilia shaka gari la kina kipensi, "gari limeingia kwa kasi eneo yalikofanyikia mauaji, ni zaidi ya dakika tano sasa haonekani yeyote kushuka toka ndani ya gari like" Askari mmoja alikuwa akija uelekeo lilipo gari like, bila shaka alihitaji kuuthibitisha wasiwasi wake. Ndani ya gari, Kipensi na vijana wake walikuwa wakimwangalia kwa umakini sana askari yule, tayali walishaelewa nini kinafuata maana kukutwa na askari mahali pale haikuwa salama sana kwao, wangejiteteaje wao ni akina nani au walikuwa wamefata nini mahali pale mda kama huu na kwanini hawashuki ndani ya gari.
Askari yule alizidi kulikaribia gari lile, "Oya kamanda tunafanyaje hapa maana huyu mpuuzi anazidi kutukaribia" Aliongea Kiba ambaye sasa ndiye alikuwa msemaji wa vijana wale, "tulia dogo huyu nitajua namna gani nitamalizana naye" Alijibu Kipensi wakati ambao alikwishaishikiria vizuri bastora yake mkono wa kulia uelekeo wa Askari yule. "Halafu namjua kabisa huyu jamaa huwaga ana sifa sana, ndio alitukamata mala ya mwisho kipindi tunambaka yule bibi kizee, Oya mkubwa tutoweke mahali hapa maana akitukuta hatuchomoki, huyu jamaa ni hatari sana anatujua vizuri" Kiba alikuwa akiongea kwa kumshawishi mkubwa wake watoweke mahali hapo maana Askari aliyekuwa akija upande walipo ni hatari sana kwao, anamjua vizuri maana yeye na wenzake walishawahi kudhibitiwa na Askari yule. "Tulia wewe muoga wa maisha, huyu akifika nampasua kichwa mala moja, tunashuka chapo tunaingia ndani tuna chukua mwili tunatembea" Alijibu Kipensi akitoa maelekezo hayo ambayo vijana wake walielewa ndiyo maelekezo na mpango wa mkubwa wao hivyo ikawalazimu kila mmoja kujiandaa, "lakini mkubwa huoni kama itakuwa balaa mda huu, ni mchana pia eneo hili lina watu wengi, alikatishwa kauli hiyo na kofi kali la mgongo alilopigwa na Kipensi, " Tulia wewe muoga wa maisha, kukupa cheo kidogo tu tayali unataka kunipangia cha kufanya eti, mpango ndiyo uko hivo kama nilivyowambia, huyu akifika namla kichwa kwanza alipie dhambi ya kuwaonea vijana wangu baada ya hapo tunaingia ndani, chumba na 23, tunabeba mwili na kutoweka, safisheni kila takataka" Aliongea mda ambao sasa vijana wake walishajiandaa, kila mmoja kashikilia bunduki ndogo aina ya SMG na mda ambao tayali Askari yule alishalifikia lile gari na kuzungukia upande wa dereva na kuanza kugonga mlango, "Ana bahati hajagonga huku" Aliongea Kipensi muda ambao alikuwa akimpa ishara dereva wake asifungue. Upande wa nje yule Askari alikuwa akigonga mlango wa gari ile bila majibu, alijitahidi kuangaza ndani ya gari pasipo kuona chochote maana vioo vya gari lile havikuruhusu mtu wa nje kuwaona waliopo ndani, aliliangalia gari lile kwa umakini mkubwa sana sasa, tayali kengere ya hatari ilishagonga ndani ya kichwa chake, hakuwa mgeni na mbinu kama ile itumiwayo zaidi na magaidi wanapotaka kutekeleza mauaji, alikuwa kajiandaa vema kukabiliana na lolote ambalo lingetokea.

Wakati uleule liliingia gari jingine dogo jeusi, liliingia na kusogea karibu na pale lilipokuwa lile la kwanza, alishuka mwanaume mmoja na kwenda moja kwa moja upande wa hoteli ile pasipokujali kizuizi cha usalama kilichowekwa na polisi kuashiria kufungwa kwa hoteli ile kwa muda ambapo watu wangeruhusiwa kuingia au kutoka kwa utaratibu maalumu.
Suala lile lilimfanya askari yule kumkimbilia yule mtu aliyekimbilia kule ndani maana aliingia kinyume na utaratibu na yeye ndiye alikuwa kaachwa pale kama mlinzi, kuondoka kwa Askari yule ilikuwa nafasi zaidi iliyokuwa ikisubiliwa na Osama, alishuka haraka na kwenda pale lilipo gari la Kipensi "Tokeni haraka mahali hapa, kazi imeshakuwa ngumu nitajua mwenyewe namna ya kulimaliza hili" Alitoa maelekezo ambayo haya kutekeleza haraka kama alivyotarajia, badala yake mlango wa upande wa abiria ulifunguliwa akatoka Kipensi ambaye alionekana kutofurahishwa na kilichotokea "kwahiyo mmemfukuza ndege wetu na bado mnataka tuondoke" Aliongea kwa sauti ya hasira na kutojali kwamba aliyekuwa akiongea nae ni mkubwa wake kazini, hata hivyo Osama hakukurupuka kumjibu, alimsogelea na kumnong'oneza kitu, kisha akamuacha na kurudi ndani ya gari alilokuja nalo. Hapo ni kama Kipensi hakuelewa afanye nini, alisimama pale kama sekunde kadhaa hivi kabla ya kuingia tena ndani ya gari ambalo liliwashwa na kutolewa kwa kasi mahali pale. Ni mda huo ndipo yule Askari alikuwa akirudi, alifanikiwa kumuona Kipensi akiwa kasimama nje ya gari lile alilolitilia shaka mwanzoni mpaka anaingia na kuliondoa kwa kasi mahali pale alikuwa akishuhudia yote "huyu jamaa ni nani" Alijiuliza swali hilo wakati ambapo alisharudi eneo alipokuwa mwanzoni kabla ya ujio wa gari lile.
Akili yake bado haikuwa imetulia, kuna namna alihisi vitu haviko sawa, kuanzia ujio wa gari ya kwanza, kitendo cha kumgongea dereva asifungue mlango wa gari, ujio wa gari la pili na kitendo cha mtu aliyetoka ndani ya gari lile kupita kizuizi cha usalama makusudi na kupetelea ndani ya hoteli. Kilichomchanganya zaidi ni jamaa aliyekuwa ndani ya gari kuliondoa gari kwa kasi baada ya kumuona yeye, "hapana" Aligoma kuamini kwamba kilichotokea ilikuwa ni bahati mbaya tu, alitamani kwenda kuikagua ile gari iliyoachwa pale lakini alijionya kukiuka maagizo ya mkubwa wake, "lakini hawa watu wanaonekana kuwa kitu kimoja" Aliwaza hivo wakati akilitazama gari lile kwa umakini. Toka ndani ya gari ile, Osama alikuwa makini sana na nyendo zaidi Askari yule tokea mwanzo, alikiangalia kioo cha simu yake akajiridhisha kuwa kazi aliyokuwa kaifanya ilikiwa nzuri, kuna ujumbe uliingia, pale pale pasipo kupoteza hata sekunde moja alilitia moto gari lake na kutoweka kwa kasi eneo lile. Askari alipatwa na mshituko wa aina yake "inamaana hakuwa peke yake" jambo hilo siyo kwamba lilimshangaza tu bali kwa namna fulani lilimpa hakikisho la hisia zake kwamba watu wale walikuwa kitu kimoja. Alitamani kulifuatilia gari lile lakini aliona usingekuwa uamzi mzuri angemkwaza mkubwa wake tena.

Baada ya kutoka ndani ya eneo lile, Osama alikunja upande wa kushoto kuifata balabala inayokatisha mbele ya mahaka, sasa alikuwa akitembea kwa mwendo wa taratibu kwenye balabala ile ambayo hujulikana kama balabala ya serikali ambako magari hayakuwa yakiruhusiwa kutembea mwendo kasi. Alilingalia kwa kina jengo la mahakama ile, lilikuwa jengo la ghorofa mbili kwenda juu, jeupe lililozungushiwa uzio mfupi wa matofari ya kuchonga. Mbele ya jengo lile kulikuwa na bendera mbili zilizokuwa zikipeperushwa taratibu na upepo juu ya milingoti imala, bendera ya kwanza aliitambua kama bendera ya nchi yake, ile ya pili hakuitambua sana ila alishawahi kusikia mahali wakisema kuwa ndiyo bendera maalumu ya mahakama za nchi yao. Aliongeza mwendo wa gari lake baada ya kuiacha barabara ile na kuchepukia upande wa kushoto alipoifuata barabara iliyokuwa ikikatisha umbali wa kama mita mia tano nyuma ya KIWILA HOTEL. Alipunguza mwendo wa gari lake baada ya kumkaribia mwanaume mmoja aliyesimama pembezoni ya balabala, mwanaume yule alilidandia gari lile pasipo kusimamishwa hapo Osama akalitia kasi zaidi na kutoweka maeneo yale.
Hali ilikuwa tulivu, hakuna aliyekuwa kazungumza chochote tokea walipoliacha eneo la hotelini kule, mwanzoni aliwaza kuendesha kukimbilia nje ya mji lakini sasa alihitaji kumsikia mkubwa wake anasemaje maana kujiamulia mwenyewe ingemletea matatizo kwa mkubwa wake ambaye alikuwa mtata sana asiyependa ujinga; "Vipi kaka mkubwa, tunaelekea wapi sasa, maana mda wote upo bize tu na simu hutoi maelekezo yoyote" "Endesha gari acha kuulizauliza maswali ya kijinga" Ndilo jibu alipewa na mkubwa wake, hapo sasa aliamua kuendesha kuelekea kule yeye alikokutaka. Kipensi alikuwa yuko bize na simu yake akifuatilia kile alichoambiwa na Osama wakati ule pale nje ya hoteli. Kipensi alipokuwa akimtolea kauli mkubwa wake kuonesha kutofurahishwa na kile alichokuwa kakifanya, kitendo kile alikiona kama kuingiliwa kwenye majukumu yake tena mbele ya vijana wake, hata hivyo Osama aliyekuwa mtulivu alimfata na kumnong'oneza "mwili umeshatolewa hapa, ondokeni maana hata hawa polisi ni watu wetu, taarifa zaidi utaipata mtandaoni". Maelezo yale yalitosha kumfanya aondoke mahali pale maana hata angeamua kubaki asingeweza kabisa kufanya kazi moja chini ya Osama. Aliingia ndani ya gari na kumuamuru dereva wake kulitoa gari haraka maeneo yale, akiwa ndani ya gari ndipo aliichukua simu yake ili aangalie kile alichoambiwa.
Moja kwa moja aliingia kwenye ukurasa ambao huaminika kwa kuotoa taarifa za kweli na huko ndiko aliweza kuyapata mengi ambayo yalimshangaza hata yeye mwenyewe akajikuta akishawishika kufahamu zaidi nini kilikuwa kikiendelea maana uhalisia aliokuwa akiujua ni tofauti na kilichokuea kimesambaa mtandaoni. Hali hiyo ndiyo ilimfanya kuwa bize kiasi cha kushindwa kutoa maelekezo kwa dereva wake ambaye sasa alikuwa akilipeleka gari kule alikokutaka yeye. Kipensi alishtuka baada ya kuhisi gari imesimamishwa maana hakuwa akizisikia tena zile purukushani za matairi kuichambua lami, baada ya kutazama ndipo aligundua kuwa dereva wake alikuwa kawarudisha tena kule "SHINING HELL". Aliwatazama vijana wake ambao walikuwa wamechangamka sasa maana walijua wao kuwepo eneo lile ilikuwa ni mwendo wa kula bata. "Wewe mpuuzi nani kakwambia uje huku" alifoka Kipensi akimtazama dereva wake ambaye kwa mda huo alikuwa akijiandaa kutoka nje ya gari, "lakini mkubwa wewe ndiye uliyeniambia nije huku" Alijitetea uongo hata hivyo Kipensi hakuwa na kumbukumbu zaidi kama aliweza kutoa maagizo hayo au la.

"MTATUZI LAW FIRM" maneno haya yalikuwa yameandikwa kwa kurembwa kwenye bango moja kubwa mbele ya jengo lililoonekana kuwa na ofisi nyingi. Hakuwa mgeni wa eneo hili; mala nyingi angepita mahali hapa akiwa katika mizunguko yake au zile mala chache alipokuwa akifika mahali hapa kumsalimia rafiki yake. Ilikuwa ni ofisi ya wanasheria na mawakili wa kujitegemea iliyokuwa ikiongozwa na rafiki yake aliyesoma naye chuo. Alienda kuiegesha gari yake eneo maalumu la maegesho nje ya ofisi ile kisha akaingia ndani ambako alipokelewa na binti aliyekuwa kwenye chumba cha mapokezi ambaye baada ya kumuona mwanaume yule alimuongoza moja kwa moja mpaka ndani ya chumba kimoja chumba kilichoonekana kuwa sehemu ya wageni kukaa. "Karibu sana MTATUZI LAW FIRM, hapa utapata msaada na ushauri mbalimbali kuhusu mambo mbalimbali ya kisheria, karibu kiti uketi, sijui utapendelea kinywaji gani nikupatie". Aliongea binti yule kauli ambayo ilimchefua mwanaume yule, "hivi wewe binti unanijua mimi ni nani kweli, mpumbavu kabisa wewe, yaani badala unipeleke nakotakiwa kwenda unanileta hapa", japo yule binti alionekana kujiamini sana lakini kauli na namna alivyojibiwa ilimfanya kuchukia, alimtazama juu chini mgeni wake pasipo kumuelewa, "kwahiyo wewe umekuja hapa utukane watu au vipi, mbona sikuelewi, tuliza kisilani ueleze shida yako nikusaidie" Majibu haya alimanusura yamdondoshe chini kwa presha, alifoka sana kwa hasira akitamani kumtia mabanzi binti yule aleyemuona kutokuwa na heshima na watu wazima. "Jamani nini tena kinaendelea hapa ndani mbona kelele nyingi" Ailisikika sauti ya mwanaume aliyekuwa akiingia pale chumbani "si huyu mteja, amefika namuelekeza utaratibu anaanza kunitukana" yule binti aliongea kujitetea mbele ya bosi wake ambaye sasa alimwangalia vizuri yule mteja na kufahamu. "Mr Isaya!" Aliongea kwa mshangao asiamini kama huyo mgeni ndiye alikuwa akigombezwa na binti mfanyakazi wa mapokezi. "Samahani sana Mr Isaya kwa usumbufu uliojitokeza na ninaomba radhi kwa ujinga alioufanya binti huyu" Aliongea meanaume huyu aliyeonekana kumfahamu zaidi mgeni yule aliyemtambulisha kwa jina la Mr Isaya, "wakili Gero nimemkuta" aliuliza swali lililojibiwa haraka "ndiyo yupo, naomba tuongozane nikufikishe ofisini kwake au nimuite aje hapa hapa" "twende huko aliko" Aliongea hapo yule kijana akaongoza njia waondoke. Mr Isaya aliipiga hatua mbili kisha akageuka kumwangalia yule binti, "Ningekijua chuo ulikojifunzia huo ujinga ningekinunua na kukigeuza kiwe zizi nifugiepo ng'ombe wangu huenda kita kuwa na faida kwa taifa tofauti na hivi kinavyodharisha wapumbavu namna hii eti waje wahudumie wananchi" aliongea maneno hayo kisha akaondoka. Kilichomuumiza binti yule siyo ile kauli bali ile namna anavyotukanwa na kuonekana mjinga wakati anayatekeleza majukumu yake vizuri tu, hajakosea chochote kiasi cha kuombewa msamaha. "Atakuwa nani yule ambaye wakili anamnyenyekea" alijiuliza pasipo majibu akaamua arudi kule chumba cha mapokezi akaendelee na majukumu yake, alishaelezwa tokea mwanzo kwa hiyo changamoto kama hiyo aliichukulia kawaida. "Karibu sana Mr Isaya rafiki yangu na pole sana kwa changamoto zinazojitokeza sasa" Yalikuwa maneno ya wakili Gero akimkaribisha mgeni wake, "Nimesikitika sana kwamba licha ya kutoa taarifa hukuwaeleza vijana wako kuhusu ujio wangu" kauli ile ilimchanganya kidogo wakili Gero ambaye mpaka hapo hakuelewa chochote kilichotokea kule mapokezi, kijana wake alimsogelea na kumnong'oneza akimueleza kilichotokea na hapo ndipo alikasilishwa sana na tokio lile. "Kutoa taarifa hakukuwa na umuhimu lakini nakushangaa sana, vipi umekuwa mzembe sasa kiasi cha kuajiri watu wasio na uwezo, au ulihadaika na uzuri wake"
Maneno haya machungu yaliingia moja kwa moja moyoni kwa Gero, hakuelewa ajitetee nini mbele ya rafiki yake maana alichoambwa kilikuwa karibu kweli. "Samahani sana rafiki yangu, naamini kilichotokea utakielewa kama sehemu ya changamoto ya kibinadamu" aliamua ajishushe ili mambo yawe machache. "Nafikiri sasa lile suala langu limefikia pabaya, nimefikiria niliache rasmi chini ya ofisi yako" Wakili Gero aliielewa vizuri kauli ile ilimaanisha nini, alinyanyuka na kwenda kufungua kabati na kutoka na faili moja kubwa akampatia Mr Isaya ambaye anaonekana kulishangaa faili lile hivyo analifungua haraka kutaka kujua nini kimeandikwa, alisoma kwa ufupi kile kilichukuwamo ndani kisha akamtazama rafiki yake kama mtu aliyehitaji maelezo zaidi. "Nimekuwa nikiifatilia kesi hii kwa ukaribu sana, japo sikuwa nahudhuria mahakamani lakini nimefatilia kila hatua kama unavyoweza kuona sasa, na kwa kuwa umeruhusu nafikiri tutakuwa na mwanzo mzuri wa kuanzia kazi yetu". Wawili Hao waliongea mambo mengi kuhusiana na jambo lile, walikua ni marafiki wa mda mrefu tokea maisha ya chuoni mpaka sasa walipokuwa wanauanza uzee, waliongea na kuweka mipango kuhusu kesi ile iliyokuwa ikiwakabili. Mr Isaya aliiweka kesi yake chini ya mikono salama ya rafiki yake kupitia MTATUZI LAW FIRM maana huyo ndiye angemuamini baada ya yeye kushindwa kulikabili suala hilo. Kila kitu kilikuwa kikienda vizuri, walikuwa kiongea wakifurahi kwa kukumbushana baadhi ya matukio ya nyuma, wakili Gero aliona hilo angalau ilikuwa sawa kumuchangamsha rafiki yake wa mda mrefu.
Furaha waliyokuwanayo ilitoweka ghafla mithili radi baada ya kijana mmoja kuingia kwa kasi sana pale ndani bila hata kubisha hodi, "Senior, kuna taarifa mbaya sana zimesambaa mtandaoni kumhusu tajiri Isaya inasemekan,,,"
ITAENDELEA.
 
TULIPOISHIA

alikatiza sentensi yake ghafla, baada ya kubaini uwepo wa mtu mwingine pale ndani zaidi ya wakili Gero ambaye yeye humuita senior kumaanisha mkubwa wake wa kazi. ",,Shi,,shik,kamoo bosi, sa,a,samahani bosi sikujua kama upo hapa, nimeona kuna taarifa zinasambaa kwa kasi mtandaoni, sijui kama utakuwa umeziona bosi" Aliongea kijana yule kwa sauti ya hofu mala hii baada ya kugundua mtu yule wa pili ndiye tajiri aliyekuwa akimzungumzia. Taarifa ile ilimshitua sana Gero, haraka haraka aliiwasha simu yake ili ajionee mwenyewe nini kilichokuwa kikiendelea mitandaoni, hata hivyo hali ilionekana kuwa tofauti kwa upande wa tajiri Isaya ambaye hakuonekana kushtushwa sana na taarifa iliyotolewa na kijana yule, ni kama tayali alikwishaelewa nini hasa kinaendelea ijapokuwa taarifa yenyewe bado haikuwa imetolewa. Alikuwa kainamisha kichwa chake juu ya meza, akakaa kwa mtindo huo kwa muda kidogo akionekana kuwa na tafakuri nzito moyoni mwake. "Mambo mengi lazima yatakupata tena ni kawaida sana kutokea hasa pale unapokuwa umeingia kwenye anga la washenzi, haya niambie kijana, ni taarifa gani hiyo" Hapo yule kijana akaeleza kwa ufupi kilichokuwa kikiendelea, "Yaani huwezi kuamini bosi, sijui watu hawakujui vizuri, eti mtu mzuri kabisa wewe wanakusingizia kitu kikubwa hivi, eti umekamata na kuwaua baadhi ya raia waliokuwa msitari wa mbele kushinikiza uhukumiwe pale mahakamani" "Sheeeeeet" Alimaka kwa sauti ya juu na hasira sana Mr Isaya akibamiza viganja juu ya meza, "kwanini mauaji ee, kwanini mauaji tena? Inamaana umekosekana mbadala kiasi cha kutoa roho zisizo na hatia?" Alilalamika kwa hasira sana mwanaume yule,akasimama na kuanza kuzungukazunguka ndani ya ofisi ile. Alikuwa mithili ya mtu aliyehitaji kujibiwa maswali yake, apewe maelezo ya kutosha ambayo labda yangeipoza nafsi yake, hata hivyo hali haikuwa hivyo maana hakukuwa na yeyote wa kumpa majibu hayo. Hakuelewa kitu gani afanye juu ya yaliyokuwa yakiendelea mtandaoni kwa mda ule.

Joto lilimpanda sana Gero baada ya kuiona video ile ambayo ilikuwa ya moja kwa moja na yakueleweka haswa kuhusu unyama aliokuwa kaufanya rafiki yake. Aliindoa tai yake shingoni maana aliiona ni kama inamniga tu, mda huo alihitaji kupata upepo kwanza maana kazi aliyokuwa akienda kuikabiri sasa ilizidi kuwa ngumu. Mpinzani alionekana kuzichanga karata zake kwa umalidadi wa hali ya juu kiasi cha kutompatia nafasi yoyote ya kupumua, kwa huruma alikuwa akimwangalia rafiki yake aliyekuwa akizungukazunguka mle ofisini kama chizi aliyechanganyikiwa, "Sijui kama nitaweza kukusaidia kupona katika hili" aliwaza wakili huyu maana kutokana na mrorongo wa kesi ya rafiki yake tokea mwanzo jumlisha jambo lililokuwa likiendelea sasa tayali ameshauona ugumu wa kesi ya rafiki yake ambaye mda huo alikuwa akizunguka zunguka pale ofisini. Aliamua kumuacha pasipo kumuongelesha chochote maana aliielewa vizuri hali aliyokuwa akiipitia. "Najihisi kushindwa kabisa kwa sasa, nahitaji kupumzika" Aliongea Mr Isaya wakati ambapo alikuwa kalejea kuketi mahali pale pa mwanzo, "pole sana rafiki yangu maana suala hili linaendelea kuchukua mwelekeo mpya kadili siku zinavyoenda, ninahisi kutakuwepo mtu nyuma ya yote haya maana hii siyo kawaida, inawezekanaje suala hili kutokea? Na vipi kuhusu hizi taarifa zinazosambaa zina uhalisia wowote jamaa yangu?" Gero aliuliza akihitaji kusikia zaidi maoni ya rafiki yake kuhusu uvumi uliosambazwa mtandaoni. Kauli ile haikupokelewa vizuri na Isaya maana aliona ni kama rafiki yake hakuwa akimwamini tena, la sivyo asingekuwa mwepesi kuamini taarifa zile zilizokuwa ni za mtandaoni tu, hata hivyo alijionya kuwa mpole maana alimhitaji zaidi wakili Gero kwa wakati ule. "Kwa sasa nahitaji kupumzika, suala hili lishughulikieni kadili mtakavyoweza, nawategemea sana katika hili, kuhusu yanayoendelea mtandaoni sihusiki nayo kabisa kwahiyo sina chochote cha kukueleza kuhusu hayo". "Labda kama una chochote cha kuongea sasa maana uvumi huu ijapokuwa ni wa mtandaoni tu; lakini ni mbaya sana kwako, huoni itakuwa shida zaidi kama hatutafanya lolote kwa sasa?" alihoji Gero akionekana bado kuhitaji kusikia chochote toka kwa rafiki yake. "nahitaji kupumzika sasa tayali usiku unaingia" Aliongea kisha akaaga na kutoka mle ndani, Gero naye alitoka kumsindikiza rafiki yake mpaka nje ya jengo lile, "sikuoni kama upo kwenye hali nzuri kuendesha gari kwa sasa, kuna kijana hapa atakuendesha akufikishe nyumbani" Gero alitoa pendekezo hilo ambalo lilikubaliwa, hivyo akamuita kijana wake mmoja na kumpa maelekezo na wawili wale waliingia ndani ya gari na kutoweka taratibu eneo lile. Alisimama mahali pale mpaka gari la rafiki yake lilipotokomea uelekeo wa katikati ya mji, "Aisee! kazi imeshakuwa ngumu sasa, sijui hatima yake itakuwaje" Alijisemea kisha taratibu akaanza kurudi ndani ya ofisi yake kwa hatua za kivivu mithili ya kinyonga, kichwani akiwaza mingi mipango ya namna gani ataikabiri kesi ile. "Shida jamaa yangu ni mbishi na mbinafsi sana, yaani baada ya mambo kumharibikia ndipo ananishirikisha kwenye hili, anategemea nini sasa" alijisemea kimoyomoyo, mda ambao alikuwa ashafika pale mapokezi.
Alitabasamu baada ya kumuona binti wa mapokezi akiwa bize na kompyuta ndogo iliyokuwa juu ya meza ya pale mapokezi, baada ya kugeuka pande zote na kijiridhisha kwamba hakukuwa na mtu mwingine eneo lile alijiweka sawa kiume na kumsogelea yule binti. "Vipi ulikuwa wapi mda ninatoka; mbona sikukuona?" Alihoji, "Niliwapisha kwanza mpite na mteja wenu mpendwa maana ningejitokeza msingeacha kunitolea kauli za kejeli na dharau". Alijibu binti yule kwa sauti ya kudeka akionesha wazi chuki dhidi ya Mr Isaya aliyezozana naye mda mfupi uliopita. Hapo tayali Gero alishaelewa nini kilikuwa kikimsumbua binti yule, alimsogelea na kumwambia "Hapana mrembo, usijizeeshe sura yako nyororo kwa kuwaza hivo wala kuiumiza midomo yako mizuri kwa kusema hivo, yule ni mteja wetu kama wateja wengine kwahiyo hana umaalumu wa kukufanya unune hivi na kukukosesha raha kioo cha ofisi yangu" Aliongea Gero mala hii akiwa kamsogelea sana binti yule ambaye alikuwa akijaribu kuuepuka mkono wa mwanaume yule uliokuwa ukimtomasa tomasa begani. "Sasa kama ni hivyo mbona alivyofika wote mlikuwa mkimtetea na kuniona mimi ndiye mbaya, sijapenda wala" alizidi kuongea binti yule kwa namna ya kudeka na sauti iliyomsisimua zaidi mwanaume aliyekuwa naye, "Hapana, siyo kwamba wote walikuwa upande wake ni basi tu kwa sababu tu anavijisenti-senti ndiyo maana anapokuja hapa wengi huigiza kumuheshimu ili wazichote noti zake si unajua tena kula na kipofo! au wewe hupendi pesa mrembo!"
Maneno yale ni kama yaliigonga akili ya binti yule ambaye alionekana kuwa mdhaifu wa pesa kama walivyo mabinti wengi wa sasa. "Niachie bana ujue ninaona aibu mwenzio" Aliongea binti yule akijaribu kujitoa kwenye mikono yenye nguvu ya mwanaume yule ambaye alizidi kumsogelea kiasi cha kumkumbatia. Ghafla ikasikika sauti ya mlango ukifunguka, akaingia mwanamke mmoja mahali pale jambo lililomfanya wakili Gero kumuachia haraka sana binti yule, hapo akaanza kuzuga kutoa maagizo kwa binti kisha akaondoka mahali pale akapishana na mwanamke yule ambaye hata hivyo alikuwa bize na simu yake akionekana kutojali ama hakuwa ameona kilichokuwa kikiendelea. "Vipi Aisha upo sawa!" Alihoji mwanamke yule akimtazama binti yule ambaye sasa tunamfahamu kwa jina la Aisha, ambaye alijibu kwa kuinua kichwa chake juu chini kwa aibu kuashiria kwamba kila kitu kilikuwa sawa. "Sawa, mimi ninaondoka ila jitahidi kuwa makini sana kwa wakati mwingine maana hawa ndio matajiri wenyewe, ndivyo walivyo, unatakuwa kuwazoea haraka sana". Aliongea mwanamke yule kisha akaaga na kuondoka akimuacha Aisha akiwa kaganda mahali pale asielewe nini alipaswa afanye kwa wakati ule. Kauli ya mwanamke aliyekuwa akimheshimu na kumchukulia kama mlezi wake mahali pale ndiyo iliyomchanganya zaidi, hakuelewa ni vipi mwanamke yule anasapoti jambo ambalo yeye mwenyewe licha ya kuwa ndiye aliyelifanya lakini aliielewa wazi kuwa halikiwa jambo Zuri. Hata hivyo kwa kuwa tayali mda wa kazi ulishaisha, Aisha alipanga vitu vyake harakaharaka ili aondoke, alipanga kuwahi nyumbani siku ile.
Ile hali ya upweke uliotawala ndani ya nyumba ile ndiyo iliyomfanya kuchukia sana kuwepo mahali pale, kwa mtazamo wake ni kama ameshinda kakaa tu bila kufanya kazi yoyote ajabu alijihisi uchovu usiopimika hapo akaamua kwenda kasimama nje ya nyumba akijaribu kujiliwaza kwa mandhari ya eneo hilo ambalo halikumvutia kabisa. Alitamani siku ziende haraka jukumu alilokuwa nalo likamilike aweze kuyarudia maisha yake aliyoyazoea, kuendelea kuwepo mahali pale ilikuwa ni zaidi ya adhabu kwake. "Yaani ninashinda ndani kama mgonjwa aliyepooza mwili mzima" Alijisemea kauli ambayo labda kwa upande wake ilikuwa sahihi lakini kwa yeyote aliyemjua angekwambia kuwa hicho kilikuwa ni tofauti kabisa na uhalisia wake, maana kazi aliyoifanya kwa mikono yake mwenyewe siku ile ndiyo ilikuwa imeichangamsha mitandao ya kijamii kwa siku ile. Ilikuwa ni zaidi ya gumzo kwa jioni ile hivyo kama mtu angemsikiliza asingekubaliana na madai yake kuwa hakuwa amefanya kazi yoyote kwa siku ile.
Hata hivyo yeye hakuhesabu alichokifanya kama jukumu gumu la kumchosha, alikuwa ni mzoefu wa kazi zile ndiyo maana hata alivyoingia kule chumba cha siri chini ya ardhi hakuwa na papala kwa kile alichokuwa akikifanya, alitulia mbele ya komputa na kuanza kuiangalia video ndefu aliyokuwa ametumiwa. Ilikuwa video ndefu sana ikionesha matukio mbalimbali yaliyotokea siku ile ndani ya ukumbi wa mahakama na nje ya mahakama ilikokuwa ikisikilizwa kesi ya tajiri Isaya, video ile iliambatanishwa na picha kadhaa zikionesha miili ya watu waliouliwa kikatili katika maeneo mbalimbali. "I see! You are so handsome" aliongea kimombo baada ya kuiona picha ya maiti wakati akijaribu kuzikagua picha zile, ulikuwa mwili wa kijana wa kiume ukiwa umelazwa juu ya kitanda ndani ya chumba kilichoonekana kuwa cha hoteli kutokana na mpangilio wa mandhari yake. Hakukaa kuendelea kupoteza mda hivyo akaamua moja kwa moja kuianza kazi yake, hapo akaanza kuikatakata video ile akichukua vipande vya muhimu tu alivyoviona kumfaa, akavihamishia kwenye frash yake kisha akaingia chumba cha ndani ambako kulikuwa na mitambo zaidi kwa ajili ya kazi yake.
Huko alifanya 'editing' zaidi ya video ile na kuzitengeneza kwenye muundo mzuri utakaoeleweka kwa haraka na yeyote atakayetazama video ile na picha zile. Hakuishia hapo bali aliandaa taarifa fupi ya maandishi kuelezea muhtasari wa maudhui yaliyowasilishwa ndani ya video ile. Baada ya kukamilisha kazi yake aliwasha runinga kubwa iliyokuwa ndani ya chumba kile na kuicheza video ile, ilikuwa ni video ya dakika sita ikionesha mtiririko wa matukio mbalimbali yaliyotokea siku ile kule mahakamani, ikiambatana na picha mbalimbali za matukio yenye dhumuni la kumchafua tajiri Isaya. "Kazi nzuri sana Emiliana," Alijipongeza baada ya kuhakikisha kila kitu kimeenda sawa, akachukua frash akaitia mfukoni, kisha akachukua gazeti moja kubwa lilokuwa mle ndani na kuanza kujipepea mithili ya malikia wa tawala za ughaibuni kisha akatoka ndani ya nyumba ile ya siri.
Aliporudi nyumba ya juu moja kwa moja alichukua simu na kuipiga mahali hata hivyo haikupokelewa, alifanya hivyo kwa mara tatu mfurulizo bila majibu yoyote, hapo akaamua kuachana nayo aendelee na ratiba zake. Baadaye kidogo simu ile ilianza kuita ndipo akaipokea, "Kazi nimeshaikamilisha hivyo ninataka nikazurule mjini, nimeboeka sana kukaa hapa mda wote peke yangu" Aliongea maelezo ya moja kwa moja ambayo hayakujibiwa na mtu wa upande wa pili. Baada ya simu ile kukatwa, Emmy aliingia bafuni kujiandaa maana alijua mda mfupi ujao angepata ugeni, alipanga amtumie mgeni huyo kufika atakako.
Baada ya dakika chache kupita inaonekana pikipiki ikizikatisha kwa kasi kona za balabala ya mtaa ule, moja kwa moja ikaja mpaka mbele ya geti moja ambalo lilijifungua lenyewe bila jitihada yoyote ya mtu kutumika, pikipiki ile iliingia moja kwa moja na kwenda kupaki karibu na nyumba iliyokuwa ndani ya uzio ule.

Alishuka dereva na kwenda kuugonga mlango wa nyumba ile. "Fanya haraka Emiliana tayali mgeni ameshafika" aliongea Emmy baada ya kusikia sauti ya kugongwa kwa mlango wa nje, hata hivyo asingeweza kwenda kwa wakati huo maana ndiyo kwanza alikuwa akimalizia kuoga akiwa mtupu bila chochote mwilini. "Nisubiriiii nakujaaaaa" ndiyo sauti aliyoisikia dereva bodaboda akiwa nje, aliiangalia saa yake mkononi kisha akaanza tena kugonga mlango akionekana kutotaka kabisa kupoteza mda wake mahali pale. "Ngo ngo ngo" "Ngo ngo ngo" aliendelea kugonga mpaka pale aliposikia sauti ya hatua za mtu aliyekuwa ndani. Hapo ni kama aliridhika akarudi ilipo pikipiki yake akijiandaa ili aliyepo ndani akija achukue kilichomleta aondoke. Ulipita mda kidogo ndipo mlango alifunguliwa na Emmy ambaye sasa tayali alishajiaandaa kwa namna ya kupendeza sana.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA,
"Nisubiriiii nakujaaaaa" ndiyo sauti aliyoisikia dereva bodaboda aliyekuwa nje, aliiangalia saa yake mkononi kisha akaanza tena kugonga mlango akionekana kutotaka kabisa kupoteza mda wake mahali pale. "Ngo ngo ngo" "Ngo ngo ngo" aliendelea kugonga mpaka pale aliposikia sauti ya hatua za mtu aliyekuwa ndani. Hapo ni kama aliridhika akarudi ilipo pikipiki yake akijiandaa ili aliyepo ndani akija achukue kilichomleta aondoke. Ulipita mda kidogo ndipo mlango alifunguliwa na Emmy ambaye sasa tayali alishajiaandaa kwa namna ya kupendeza sana.
ENDELEA
Emmy alikuwa ni msichana mwenye umbo matata sana lililojigawa mafungu mawili kuunda umbo maarufu lililopewa hadhi ya namba nane na wataalamu wa mambo. Alikuwa kavalia gauni refu la njano lililomfanya kuonekama kama mmoja wa mabinti za mfalme mwenye mali nyingi sana. Nywele fupi nyeusi zilizonyolewa kwa mfumo maarufu ujulikanao kama nusu denge. Uso wake ulichanua tabasamu la haja lililotosha kuziamlisha hisia za mwanaume lijali, alikuwa msichana mwenye sura nzuri iliyokolezwa kwa mafuta mazuri yaliyoifanya ngozi yake kuonekana kama ya mtoto mchanga. Huenda ni kwa sababu hakupata mda wa kutosha kujipodoa sana ndiyo maana hakuwa amejipamba sana kama wafanyavyo mabinti wengi wa rika lake, lakini bado alionekana kupendeza mno. Mkono wake wa kushoto ulishikilia pochi ya kike yenye weupe wa kung'ara na ule wa kulia ulishikilia mfuko mkubwa wa nailoni. Alifunga mlango na kumfata dereva bodaboda yule ambaye akili yake kwa wakati huo ni kama ilihama kabisa baada ya kumuona msichana mwenye uzuri usiopimika mbele yake, "Ama kweli wakubwa wanafaidi sana, yaani mtoto kasimama de_de_de,,,," alikurupuka toka kwenye mawazo hayo baada ya kuguswa na msichana aliyekuwa mbele yake wakati akimpatia mfuko ule, "mambo vipi mrembo" alimsalimu kwa sauti ya kiume akijaribu kutoonesha udhaifu mbele ya binti yule, hata hivyo Emmy hakuijibu salamu ile zaidi ya kumkabidhi mfuko ule na hapo akataka kupanda pakipiki ile lakini dereva bodaboda akaonesha upinzani. "Nimeelekezwa kuja hapa kufata mzigo tu wala siyo kupakiza mtu yeyote" aliongea kwa sauti iliyoonesha wazi kutokuwa na tone la masihara, huenda alichukizwa na kitendo cha binti yule kutojibu salamu yake kwa makusudi. "Wewe vipi usitake kunichanganya mda huu, ujue nimeshajiandaa kutoka, sasa kama hutaki kunipakiza basi ondoka na sitokupatia mzigo ulioagizwa" Alijibu Emmy kwa sauti ya juu, hapo bodaboda yule akapunguza jazba maana bila kufanya hivyo kazi yake ingekuwa ngumu, "fureshi tu, si unalingia matako ndiyo yanakupa jeuri, omba usijekujaa kwenye mifumo ya Israel hapa, nitakutafuna mpaka uombe po" aliwaza dereva bodaboda yule, mda huo tayali Emmy alishapanda juu ya pikipiki na hapo akaiondoa kwa kasi kitendo kilichomfanya abiria wake kumkumbatia kwa nguvu ili asianguke, "mambo si ndiyo haya sasa" aliwaza dereva yule mda huo akaongeza kasi na kutokomea mtaani.

Ilikuwa safari ya kama dakika kumi hivi tayali wakawa wameifikia balabala kuu iendayo mjini, "niache hapo ofisi za zimamoto" yalikuwa maelekezo yaliyotolewa na Emmy na hapo bodaboda yule alichepuka kidogo kuiacha balabala kuu na kuifata ile ya kulia iliyokuwa ikifika mpaka mbele ya bango moja kubwa lenye maandishi ya ZIMAMOTO yaliyochorwa kwa rangi ya manjano ya kukolezwa. Hapo Emmy alishuka na kutoa pesa kwenye pochi lake alipie nauri lakini dereva yule aliikataa pesa ile, "baki nayo hiyo mrembo, hesabu kama ni hisani umefanyiwa na bodaboda wako" Aliongea akiwa kamkazia macho Emmy ambaye hata hivyo hakujali hilo, aliirudisha hela yake na kuanza kuondoka kuelekea ndani ya ofisi zile, "vipi baadaye hautohitaji usafiri wa kukurudisha kule nyumbani kwako?" Ilikuwa ni sauti ya bodaboda akimuuliza mteja wake, "nitahitaji" Akajibu Emmy pasipo hata kugeuka jambo lililomfanya yule bodaboda kumsogelea "kwahiyo tunafanyaje maana mimi ninavyoondoka saa hii kurudi ni baadae kidogo, nipatie namba yako mimi nitakutumia meseji utaiona namba yangu ili ukiwa tayali unipigie nije nikuchukue mrembo" aliongea kwa tabasamu sana maana aliona huo kuwa mpango mzuri. Hapo Emmy aligeuka na kumtazama kwa jicho legevu la kike lililozivuruga vibaya hisia za badaboda yule "Sihitaji huduma yako ya bure maana hainiridhishi, bodaboda wako wengi sana tena wataalam haswa wanaonifanyiaga huduma nzuri tena kwa malipo" Aliongea kwa sauti kavu kabisa kisha akageuka na kuondoka, lakini akasimama baada ya ujio wa mwanaume mmoja toka ndani ya ofisi ile, mwanaume yule alimpiga jicho bodaboda yule ambaye aliiwasha pikipiki na kuondoka kwa kasi. "Siyo mbaya ni mwanzo mzuri, nitakupata tu" alijisemea wakati akiingia balabala kuu na kupotelea uelekeo wa mjini.

Emmy alisimama baada ya kumuona mwanaume yule maana alimjua na ndiye alikuwa amemfata mahali pale, mwanaume yule alifika na kumkabidhi Emmy funguo za gari kisha akarudi kule ofisini. Ni kama alishaanza kuizoea hali ile ya wenzake kutopenda kumuongelesha sana hivyo hakushangazwa na kitendo kile cha yule mwanaume kufika na kumkabidhi funguo bila hata salaamu wala kumuongelesha chochote, alizunguka kwenda nyuma ya jengo lile ambako kulikuwa na magari kadhaa. Alifurahi sana baada ya kuliona gari alilokuwa ameandaliwa na mwanaume yule, alifika na kulizunguka kwa furaha akilikagua "gari zuri sana hili, mji utanikoma leo" aliwaza mda akifungua mlango na kuingia ndani ambako nako alipakagua vile vile akionekana kulifurahia sana gari lile, kisha akaliwasha lakini kabla hajaondoka kuna pikipiki iliingia kwa kasi sana maeneo yale na kwenda kupaki nyuma ya gari lake alishuka mama mmoja na kuingia ndani ya ofisi kupitia mlango wa nyuma. Tukio lile lilimfanya kukumbuka namna alivyomzingua yule dereva bodaboda aliyeonesha waziwazi kumtamani, "kazi nzuri sana Emiliana, unajua kunikomeshea mafala" aliongea kisha akawasha mziki kwa sauti ya juu na kulitoa gari taratibu akayaacha maeneo yale.

Yapata saa moja za jioni sasa, tayali giza limeanza kuuvamia uso wa dunia na kufanya kile wengi hukiita usiku kutokea. Dangi alikuwa akikatisha mitaani kwa mwendo wa harakaharaka sana akionekana kuwahi mahali, hii ni baada ya kukamilisha ratiba ya majukumu yake kwa siku ile kama Askari mwaminifu wa jeshi la polisi. Hivyo baada ya kufika nyumbani aliamua kubadirisha sare zake za kazi, akavaa nguo zake ambazo yeye mwenyewe huziita nguo za kazi maana sale za jeshi kwake hazikuwa nguo tu bali ndiyo ilikuwa kazi yenyewe. Ilikuwa suruali nyeusi aina ya Jeans nzito na juu alivalia tisheti nyepesi ya kijivu yenye mikono mirefu na kumalizia kwa koti jeusi kujihami dhidi ya baridi kali la jioni ile, kichwani alivalia kofia ya pama yenye bendera ndogo ya taifa lake upande wa mbele ambako alipakunja kuifunika bendera ile isionekane vema. Alikuwa akitembea mwendo wa haraka haraka akikatisha chocho za mitaa ile mpaka pale alipohakikisha kuwa amefika eneo husika.

Umbali wa mita miamoja toka ilipo KIWILA HOTEL ndipo Dangi alipokuwa kasimama chini ya kivuli cha moja ya miti iliyopandwa pembezoni mwa balabala. Macho yake yalikuwa makini akiitazama hoteli ile kwa kina sana, kichwani akitafakari tukio lile lililotokea mahali pale mchana wa siku ile, alishindwa kabisa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea ndani ya hoteli ile. Kila akikumbuka tukio la mchana namna walivyofika ndani ya hoteli ile kufuatia taarifa iliyotolewa na raia mwema kwamba kuna mwili ulikutwa ndani ya moja ya vyumba vya hoteli ile, kweli waliuona mwili ule na baada ya itifakhi kuzingatiwa waliwaruhusu wahudumu wa afya kuupeleka hospitali ili ukahifadhiwe. Lakini taarifa ya jioni ile ndiyo iliziamsha sana hisia zake kama polisi mwenye mafunzo tayali kengere ya hatari iligonga kichwani mwake maana baada ya kuitazama vizuri video iliyosambaa mtandaoni ikionesha wale waliosadikika kuuliwa na vijana wa tajiri Isaya, alibaini kwamba hata picha ya mwili ule alioushuhudia hotelini ilijumuishwa tena ikiwa eneo lililoonekana kuwa kama msituni au kichakani. Suala lile ndilo lilimchanganya sana, yaani iweje mwili alioushuhudia hotelini na ukachukuliwa na gari la wagonjwa toka pale hotelini picha yake ionekane ndani ya video ile tena ukiwa eneo tofauti na hotelini? vipi umefika huko kabla au baada ya kufikishwa pale hotelini?. Inamaana mauaji yalifanyikia wapi sasa hotelini au wapi! Harafu ikawaje kuna watu watu watakuwa waliuleta pale hotelini? maswali hayo yalimchanganya sana hasa pale alipojaribu kulinganisha na tukio la ujio wa magari mawili nje ya hoteli. Kwamba kwa nini kuna magari yalifika na kutoweka mchana ule akayatilia mashaka, kwanini waliokuwa ndani ya gari la kwanza hawakushuka mpaka lilipofika gari la pili, na kwanini yule mtu aliyetoka ndani ya gari la pili alikimbilia ndani ya hoteli pasipokujali uwepo wa kizuizi cha polisi, na vipi alifanikiwa kupotelea ndani ya hoteli pasipo kuonekana na Askari yeyote hali ya kuwa kule ndani walikuwemo Askari wa kutosha?. Tayali alishaamini kwamba gari la kwanza lina uhusiano na gari la pili, sasa aliwaza kwanini mtu yule aliyekuwa ndani ya gari la kwanza alitoka ndani ya gari baada ya yeye kuingia ndani na kwanini aliliondoa gari kwa haraka baada ya kumuona yeye akirudi. Maswali hayo na mengine mengi ndiyo yalimfanya usiku ule kuwepo mahali pale. Yeye ni mbwa aliyefunzwa hasa namna ya kuwinda, ameshanusa harufu hivyo aliamini kuna uwepo wa windo ndani ya chaka lile wewe unafikiri angewezaje kuondoka kabla ya kulikagua chaka lile athibitishe hisia zake?. KIWILA HOTEL ndiyo lilikuwa chaka lenyewe alihitaji kulikagua na kulipekua haswa kujua mbivu na mbichi zilizopatikana ndani ya hoteli ile, aliamini lazima atapata mwanga wa kilichokuwa kikiendelea kupitia hoteli ile.

Tokea pale aliposimama aliweza kuiona vema hoteli pamoja na kituo cha mafuta kilichopo mbele ya hoteli ile, alikuwa makini kuangalia na kuyakagua mazingira ya eneo lile akiamini labda ataweza kubaini kitu cha tofauti kinachohusiana na tukio la mauaji. Alisimama pale zaidi ya robo saa lakini bado hakubaini utofauti wowote, hakuna cha maana alichokiambulia zaidi ya kuona magari yaliyopishana balabalani yakikatisha na kuingia ndani ya kituo cha mafuta, hakuona chochote cha kutilia shaka. Mpaka hapo alithibitisha mazingira ya nje yapo sawa, akaamua aingie ndani ya hoteli akiwa na uhakika wa kupata mwangaza wa tukio la mchana na mengi zaidi kumhusu kijana aliyeuawa mahali pale, alipanga kwenda kufuatilia taarifa za kijana yule na lini alichukua chumba pale hotelini. Hakuwa na shaka kuhusu uwepo wa taarifa hizo kutokana na utaratibu wa kawaida wa mji ule ambapo kila hoteli ilitakiwa kuwa na taarifa za wateja wake kabla ya kuwapatia huduma. Aliyaacha maficho yale akaivuka balabala na kuingia ndani ya eneo la kituo cha mafuta ambapo angezunguka kwa nyuma atokezee mbele ya hoteli.
Ulikuwa wakati akilimaliza kukatisha eneo lile ndipo aliposikia maongezi yaliyomvutia na kuziamsha sana hisia zake akatamani kuendelea kusikiliza zaidi lakini hilo lilikuwa gumu kwani eneo lile lilikuwa la wazi hivyo ilikuwa ngumu kwake kufuatilia maongezi yale bila wahusika kumuona na kushtukia lengo lake. Alisimama na kuzuga kupokea simu japo hakuwa akiongea chochote, ilikuwa mbinu ya kubaki eneo lile bila kushtukiwa lengo lake na hapo sasa akawa akiyasikiliza vizuri mazungumzo ya wanawake wawili waliokaa nje ya duka. Binti muuza duka na mwenzake, walikuwa wakiongea mengi kuhusu kile kinachoendelea mitandaoni kwa usiku ule, kilichomvutia zaidi ni pale mmoja wao alipogusia habari ya gari iliyoegeshwa pembeni ya duka lile.
"Kwahiyo shoga yangu una mpango gani na hili gari lake maana yeye ndiyo kashaondoka hivo"
"Nawaza nikatoe taarifa polisi waje walichukue"
"Harafu wakilichukua ndiyo iweje! acha ujinga wewe, huoni hii ni bahati Mungu kaamua kukupatia utajiri kwa njia hii, au unafikiri ni kawaida tu mtu aje akuachie gari harafu akauawe? Jiongeze wewe, Mungu kaamua kukupatia kwa namna hiyo au unataka Mungu akupatie kwa namna gani shoga yangu, hapa cha kufanya hili gari tunaliuza tupate hela tuishi vizuri"
"Hapana Jenita, siwezi kufanya hivyo, siwezi kuuza gari lisilo la kwangu ni bora niliache tu"
Denge alikuwa akiyafatilia kwa umakini mkubwa mazungumzo hayo aliyoyaona kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na tukio lililotokea hotelini.
"Lakini umehakikisha kuwa amefariki kweli?"
"Ndiyo, niliwasikia wale Askari walisema kijana aliyeuawa jina lake ni Morice"
"Kwani kuna mtu mwingine anajua kuwa mala ya mwisho alikuja kuegesha gari hapa"
"Mimi sijui hayo, maana,,,"
"Basi kazi ni nyepesi, wewe kaa kwa kutulia, usimwambie yeyote kuhusu hili, mimi nitamtafuta mteja wa kununua gari hili atupatie pesa"
"Utajua mwenyewe mimi simo"
"Kwahiyo unamaanisha nikipata mteja, utaniachia hela yote mimi mwenyewe!"
"Mimi utanipatia kidogo tu"
"Hahahahaaaaa! acha kujifanya mlokole Salma wakati hata msikitini huendagi, wewe kaa kimya usiseme chochote kuhusu hili, mimi nitatafuta mteja ainunue hii gari tupate hela" Aliongea Jenita kwa sauti ya chini maana alishaanza kuwa na hisia mbaya juu ya mwanaume aliyekuwa amesimama karibu yao kwa mda mrefu sasa.
"Sasa unaenda wapi tena"
"Naondoka"
"Usitake kuniambia ndiyo unaenda kumtafuta huyo mteja mda huuhuu."
"Punguza sauti wewe watu wasikusikie, mteja tutamtafuta kesho, sahivi inabidi tutafute mtu anayejua kuendesha gari atusaidie kulitoa hapa, umeelewa?" Aliongea Jenita wakati akinyanyuka na kuondoka.
Mazungumzo hayo yalikuwa na maana kubwa sana kwake, aliiona nafasi kubwa ya kupata ukweli kuhusu mauaji ya hotelini kupitia wanawake wale walioonekana kumjua vizuri kijana aliyeuawa hotelini.
ITAENDELEA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom