Simulizi ya kusisimua Part 1-(Revolution woman)

Simulizi ya kusisimua Part 1-(Revolution woman)

Okay...ntajifunza kuweka hyo link...right now sifaham jinsi ya kuweka unless unielekeze
Mkuu au Uwe Unaweka namba ya mwendelezo kama hio comment yako ni namba #20 ili watu waifate kwa urahisi pia
 
Sehemu ya Pili (Revolution girl)

Jackson alipata mshituko mkubwa baada ya kupata taarifa ile kwnye simu,nguvu za miguu zilimuisha na kujikuta anakaa chini pale pale mlangoni na kutoa kilio ndipo yule mke wake ambaye anaitwa Ravit kumsogelea na kuanza kumbembeleza

Vyombo vya habar vilitanda habari juu vifo vya hao matajiri wakubwa duniani na hata Nchini kwao shughuli zote zilisimama na bendera kushushwa nusu mlingoti kuashiria pigo kubwa kwa nchi hio.

Jackson na mkewe Ravit kufunga safari kuelekea Nchini kwao kutokea ufaransa na kupokelewa na wasaidizi airport na kupelekwa hadi nyumban ili kuandaa mazishi

Raisi wa nchi hiyo akatangaza siku mbili za maombolezo na viongozi wengi wa nchi walikwenda kumpa pole Jackson na kumtia moyo japo Raisi wa nchi hiyo alipata faraja ya kuwa uchumi wa nchi yao utabaki salama kwani alikuwa anajua uwezo wa jackson kwenye uchumi na hivyo uwekezaji mkubwa wazazi wake nchini humo utaendelezwa vizuri kwani kuporomoka kwa uwekezaji wa Mr & Mrs Rupert nchini humo kutapelekea majanga ya nchi kwani asilimia kubwa ya uchumi mwa nchi hyo iko mikononi mwa familia ya Jackson

Yule house girl ambaye aligewa mimba na jackson anajulikana kwa jina la Mary alikwenda nyumban kwa jackson siku ya mazishi na tumbo lake likiwa kubwa ili apate nafasi ya kumpa pole Jackson lakini alikutana na umati mkubwa wa watu ambao waliokuja kwenye mazishi ambayo yalikuwa yanafanyika nyumban kwa akina jackson na hivyo kulikuwa hakuna namna ya kuonana na Jackson.

Baada ya mwez kupita maisha yakaanza kurudi kama kawaida japo jackson alikuwa yupo kwenye mawazo ya kuwakumbuka wazazi wake na hivyo kupelekea kumuachia kazi nyingi mke wake Ravit za kiutawala Kwenye mali za ndani ya Nchi hiyo tu na zile mali za nje ya nchi yaan uwekezaji wa Mr & Mrs Rupert kwenye nchi zingine alibaki jackson kuendesha kwa kutumia mtandao akiwa nyumban

Ravit alianza kutokea kwenye vyombo vya habar kma Mrs Rupert na ndipo Mary(housegirl) akajua kuwa Jackson ameoa uku akiwa ameshajifungua mtoto aliyempa jina la Michael

Raisi wa nchi hiyo akawa anakutana na Ravit(mke wa jackson) kujadili uchumi wa nchi hiyo na kugewa heshima kubwa kama ya Mrs Rupert na Raisi akimuuliza Jackson alipo, Ravit anajibu kuwa Jackson bado ajawa sawa kurudi kazini amemuachie yeye ashikirie kwa muda

Ravit alianza kuhisi fahari kwa heshima anayogewa na viongoz wa nchi hiyo na kila hotel au sehemu akiingia ana thaminiwa

Baada ya miaka mitano kupita Ravit hakuweza kushika mimba..alitumia madawa mengi lakini ikashindikana na akaanza mawazo ya kufikiri kuwa Jackson atakuja kuoa mwanamke mwengne na yeye kuachwa kutokana na hilo tatizo na hiyo ikapelekea Ravit kutafuta sumu itakayoweza kumuathiri mfumo wa damu pole pole.

Ravit akitoka kazini jioni wakat wa chakula cha mezani anawahi kabla ya Jackson na kuweka hizo sumu.

Baada ya wiki mbili zile sumu zikaanza kufika sehemu ya ubongo wa jackson na akaanza kupoteza kumbukumbu pole pole ila hakujua Tatizo ni nini

Jackson uwa anabaki nyumbani na kufuatilia biashara za familia Mr & Mrs Rupert za nje ya Nchi ambazo Ravit hakuwa anazifahamu kwani biashara za ndani ya nchi hiyo zilikuwa ni nyingi mno na kutokuwa na mawazo ya hizo nyingine za nje.

Password ya Laptop ya Jackson ambayo utumia kufuatilia Biashara za Nje ya Nchi ndio namba ya akaunti ya fedha zote za uwekezaji wa nje uwekwa ambayo bank hiyo ipo uswizi ila akaunti ya fedha ambazo uingia kwa uwekezaji wa ndani ambao mkewe Ravit anaendesha ilikuwa ndani ya nchi hiyo na password pamoja na akaunti namba mkewe Ravit alikuwa navyo.

Kutokana na tatizo la kusahau sahau la Jackson ikabidi siku aende mtaani kwa wanaochora tatoo na ulikuwa umbali mrefu sana wa gari lake la kifahar na ilikuwa sehemu za ndani ndani ambako dereva wake alimpeleka baada ya kumwambia anacho kihitaji kuwa ni tattoo

Alipofika maeneo yale Jackson alishangaa kuona watu wanaishi maisha magumu ambayo hajawai kuyaishi..watu wanaangaika kwenye dampo ambalo mary(house girl) alitokea uko japo hakujua hilo Jackson

Jackson alienda sehemu hiyo kwani hakutaka kwende sehemu za mjini kuchora tattoo hiyo kwan hakutaka kupata karaa ya watu wanaomfaham.

Jackson alimuacha dereva wake kwenye Gari baada ya kuonyeshwa kibanda cha uyo mchoraji alipoingia kwenye hicho kibanda na kumueleza mchoraji anachokihitaji ni kuwa achore namba ambazo aliziandika kwenye kikaratasi juu mkono wake wa kushoto kma tattoo.

Bila ya kuhoji yule mchoraji alizichora zile namba kwa mstari wa kwanza ni 1352789104 na mstari wa pili ni 1713 kwani ilikuwa ni akaunti namba na paasword ya akaunti ya uswizi ili awe anaikumbuka kirahisi wakati akiingia kwenye laptop yake.

Baada ya kumaliza aliuliza malipo ambayo yalikuwa ni Dola 5 lakini akatoa Dola 100 na kumwambia achukue yote ndipo yule mchoraji akashangaa kwani kazi ilikuwa rahisi na alikuwa hamfaham jackson kwani watu wa sehemu hiyo wanaishi kimaskini sana wanabaki kumsikia Jackson na hyo familia ila kwa sura hamjui basi Jackson akaondoka maeneo ayo na dereva wake kurudi nyumban.

Jackson alipofika nyumban akakuta mkewe karud anamsubiri sebulen ndipo mkewe akamuuliza alipotekea kabla hajajibu Jackson akaanguka uku damu ikitoka puani kwani zile sumu zilikiwa zishaanza kuzidi mwili ndipo mkewe akapiga simu ya ambulance ije kwani hakutaka Jackson afie nyumban na kuleta wasi wasi kwa watu na alitaka yote yatokee hospitali.....itaendelea
 
Kiongozi kma una husika na lile group la hadith the bold naomba niunganishe pls nilijitoa kwa bahati mabaya
 
asante sana kwa simulizi ..
ila ole wako isiendelee ...nita wahonga pesa mods wakupige ban ya maisha""
 
Mkuu simulizi ya kwanza uliitoa 2017 mwezi w 10. Mwendelezo umeutoa march 2018!! Itakayofuatia itakua miezi sita ijayo. Kwa hio tungojee hadi mwezi wa tisa???!
Lakini hongera na pongezi mno kwa hadithi nzuri japo hatujui mwisho wake. Kila jema liwe kwako.
 
Mkuu simulizi ya kwanza uliitoa 2017 mwezi w 10. Mwendelezo umeutoa march 2018!! Itakayofuatia itakua miezi sita ijayo. Kwa hio tungojee hadi mwezi wa tisa???!
Lakini hongera na pongezi mno kwa hadithi nzuri japo hatujui mwisho wake. Kila jema liwe kwako.
haha...kesho naleta muendelezo
 
Ni kitabu nasoma...nikirefu kichizi zen nakuja kutafsiri kwa kiswahili
 
Back
Top Bottom