Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 489.
Baada ya kufunguliwa mlango na mhudumu mwenye asili ya kiarabu alievalia suti , Edna alishangazwa kukuta sio mtu anaekutana nae bali ni jopo la watu kama ishirini waliojipanga kwenye meza na ajabu ni kwamba mara baada tu ya kuingia wote walisimama kiheshima , kati ya sura alizozifahamu ni moja tu ambaye ni Nadia Alfonso mwanasheria wake.
Edna na Suzzane walihisi wamekosea chumba walichopaswa kuingia na Edna alitoa ishara ya kuomba msamaha kwa kuingilia kikao.
“Karibu sana Madam Persephone” Waliongea wote kwa pamoja kwa lugha ya kingereza na kisha waliinamisha vichwa kuonyesha ishara ya heshima jambo ambalo lilimpagawisha Edna na moyo wake kupiga kwa nguvu , alijihisi ni kama anaota na akishituka ingekuwa ndoto.
Kwa mara ya kwanza alihisi jina la Madam Persephone ambalo alilikuwa akiitwa mara kwa mara bila ya kujua sababu yake alihisi sio la kwake , ule ujasiri aliokuwa nao kwa muda huo ulimpotea na aliishia kuduwaa.
Suzzane pia alikuwa kwenye mshangao asijue nini kinatokea mbele ya macho yake , walikuja hapo kwa minajili ya kukutana na Tajiri Khalifa kutoka Dubai , mtu ambaye alichangia kiasi kikubwa cha pesa katika taasisi ya Edna Foundation na uwepo wao hapo ni kutii wito wa kuonana na tajiri huyo , lakini mambo yanaonyesha kuwa tofauti.
Licha ya kwamba alihisi yupo ndotoni lakini ulikuwa uhalisia na jinsi watu waliokuwa mbele yake walivyokuwa wakimwangalia alijua kabisa walimlenga yeye na ndio ambaye alikuwa akisubiriwa, lakini bado alijiuliza kwanini yeye na ni maigizo gani yanafanyika.
Kwanza chumba kilionekana kilikuwa cha mikutano ndani ya hoteli hii ya Peacock, pili mpangilio wa hapo ndani ulikuwa ni wa kikao muhimu kutokana na watu waliokuwepo , ilikuwa ni meza ndefu ambayo inajumla ya watu kumi kila upande kukamilisha watu ishirini na ni kiti kimoja tu ambacho kilikuwa wazi , kiti cha katikati ambacho huruhusu mkaliaji kuona nyuso za kila mtu aliekuwa mbele yake , ni rahisi kusema ndio kiti cha mwenyekiti kama ni kikao ambacho kinatarajiwa kufanyika.
Watu waliofahamika ambao wapo ni Shekhe Assad , Tajiri Khalifa , Mellisa Luiz , Pastor Cohen , Nadia Alfonso , Zoe Kovacic , Phill Knight na wengine wengi ambao ilionyesha ni wanachama wa Ant- illuminat.
Mwanadada mmoja aliekuwa wa kifilipino , alievalia suti alimsogelea Edna na kuinamisha kichwa mbele yake kwa namna ya heshima na kisha akavuta kiti kilichokuwa wazi na kumuonyesha ishara ya kukaa.
Edna bado aikuwa kwenye mshangao na alishindwa kujua achukue maamuzi , ya kuondoka au abaki na hata aliponyeshwa kiti cha kukaa bado hakupiga hatua kukisogelea maana alijua kukaa kwenye kile kiti ni kama yeye ndio anakwenda kuongoza kile ambacho kingekwenda kuendelea hapo ndani , kitu ambacho hata hakijui ni nini.
“Madam!!!” Suzzane alimshitua Edna ambaye bado alishindwa kufanya chochote licha ya kuonyeshwa kiti cha kukaa.
Edna aliinua uso wake na kuanza kuangalia kila mmoja ambaye yupo ndani ya hiko chumba, kuna wengine alikuwa akiwafahamu na kuna wengine hakuwahi kuwaona popote.
Lakini ghafla tu Edna alitoa tabasamu hafifu kama vile anavyofanyaga akiwa kwenye kampuni yake akiwa na kikao na wafanyakazi wake na alisogelea kile kiti na kuketi na kuwaangalia watu wote waliokuwa hapo ndani kama vile alikuwa akiwajua.
Ni kintendo ambacho hakikumshangaza Suzzane tu lakini kila mmoja kilimuacha na maswali lakini sio hivyo tu pia kiliwafanya kuwa na tumaini.
**********
Roma baada ya kuambiwa na Afande Kweka kwenda kuonana na Zenzhei , hakutaka kuchelewa sana , alikuwa na shauku ya kujua kwanini Zenzhei anataka kurudi Hongmeng baada ya kuishi Tanzania kwa muda mrefu.
Alitaka pia kujua ni jambo gani ambalo Zenzhei alitaka kumwambia , alikuwa na shauku kubwa kutokana na kwamba alikuwa na mpango wa kuivamia Hongmeng siku moja hususani muda huo ambayo alijua kabisa yeye ni adui na jamii hiyo , hivyo alitaka kukusanya kila taarifa iliokuwa ikihusiana na jamii hizo ili kumsaidia huko mbeleni.
Roma alimuaga sekretari wake kwamba anatoka na anagerudi siku iliokuwa inafuata , Tanya alishangaa kutokana na kwamba kuna baadhi ya maamjuzi yalikuwa yakimpasa kuyashughulikia siku hio hio lakini alikosa ujasiri wa kumzuia Master wake.
Ni zaidi ya miezi sasa tokea Tanya achukue majukumu ya Amina kama Secretari na alionekana ashanza kuipenda kazi yake na kuizoea na alikuwa ni msaada mkubwa kwa Roma kwani mambo mengi aliyafanyia kazi.
Muonekano wake ulikuwa umebadilika kwa asilimia mia moja na ilikuwa ngumu kujua ndio anaehusika kuongoza kundi la Yamata kutoka Japani ambalo linamilikiwa na Roma.
Roma alitumia muda machache sana kufika nyumbani kwa babu yake na baada ya kusalimiana na Afande Mstaafu Camilius Kweka ilisalimiana na Zenzhei pia wote walikuwa wamekaa nje kwenye bwawa la kuogelea na ilionekana walikuwa wakiongea.
“Nitawaacha muongee”.
“Camilius haina haja ya kuondoka , ninachoongea na Mr Roma sio kipya kwako”
“Hapana umesubiria muda mrefu na huu ni muda wako, Wewe mtukutu ukimaliza unione kwanza kabla ya kuondoka”Aliongea Afande Kweka na kisha aliondoka eneo hilo.
“Mr Roma samahani kama nimekuchukulia muda wako , muda huu ulipaswa kua kazini”
“Usijali kuhusu hilo , nilipaswa kuja hata jioni lakini kwasababu sikuwa na kitu cha kufanya kazini nimeona nije mapema”Aliongea Romana kumfanya Zenzhei kutingisha kichwa kumuelewa.
Na muda huo mfanyakazi aliwaletea Juisi ya matunda na kuweka mbele yao na kisha akaondoka.
“Mr Roma muda wangu wa kukaa kwenye ulimwengu wa kawaida umeisha”
“Nilipoambiwa unaondoka nimeshangaa , kwani ulikuwa na ukomo wa kuishi Duiani?”
“Nadhani ushawahi kisikia sheria za miliki za kijini juu ya binadamu au viumbe wanaojifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi?”
“Najua watu wa jamii kutoka miliki za kijini na binadamu ambao wamefikia katika levo ya Nafsi hawapaswi kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida”
“Upo sahihi Mr Roma na mimi muda wangu wa kuishi hapa duniani ushafikia ukomo?”
“Lakini uliishi kwa miaka mingi hapa Tanzania na naamini bado ulikuwa kwenye levo ya Nafsi , kwanini unaondoka sasa?”
“Ni stori ndefu Mr Roma ambayo nataka unipe muda wako nikuelezee ili upate kujua nia ya mimi kutaka haya maongezi na wewe”
“Nipo tayari kukusikiliza”Alijibu Roma kwa msisimko na Zenzhei alianza kumuhadhithia Roma kila kitu kuanzia namna ambavyo Zenzhei na familia yake walivyokimbia katika miliki za kijini na kuja katika ulimwengu wa kawaida , alielezea namna ambavyo baba yake mzazi na mama yake mzazi walivyopambana na wajumbe kutoka Hongmeng mpaka kuwaua , aliendelea kuelezea namna ambavyo baba yake alipambana na mtu asieonekana ambaye ndio aliyakatisha maisha ya wazazi wake mbele yake , namna ambavyo alipona , namna ambavyo alijiunga na kundi la kininja la Yamaguchi kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa The Doni.(Rejea episode ya 317).
Roma alishangazwa na stori nzima ya Zenzhei na sasa alielewa uwepo wa Zenzhei kwenye maisha ya Afande Kweka ni kutokana na misheni aliopewa na kundi la Yamaguchi kukaa nae karibu.
Roma alikuwa akielewa kuhusu Yamaguchi lakini kwenye maisha yake hakuwahi kulipa umuhimu kundi hilo na yote hayo ni kwasababu aliyachukulia kama makundi mengine tu ya kininja ambayo yalikuwa yakiua kwa ajili ya pesa ,lakini hakufahamu kuna zaidi ya hayo.
“Kwahio kundi la Yamaguchi hawakuweza kukufahamu kama unatokea Hongmeng?”
“Hawakuweza kunifahamu mpaka baadae sana nilipowakatalia misheni ya kumuua Cammilius”
“Ushawahi pewa mishenni ya kumuua Afande Kweka?”
“Ndio lakini sikutekeleza agizo, Camillius nilifahamiana nae kwa muda mrefu tokea mke wake akiwa hai na amenisaidia kwenye mambo mengi ambayo yalinigusa moja kwa moja na kwangu nilimchukulia kama ndugu,nilipomuelezea ukweli juu ya kwanini nipo kwenye maisha yake hakukasirika na aliniacha nifanye chaguzi mimi mwenyewe kumchagua yeye au kundi na mamuzi nilioyafanya ni kumchangua yeye na ndio nilipokuja kuwa mlinzi wake mpaka leo hii”
“Nikupe pole kwa yaliokukuta , lakini bado sijapata jibu la moja kwa moja umeishi miaka mingi ndani ya Tanzania na Hongmeng hawajakusumbua , kwanini sasa hivi?”Aliuliza Roma , alishangaa kwani ni kweli Zenzhei alikuwa kwenye levo ya Nafsi na kwa sheria za Hongmeng hakutakiwa kuishi kwenye ulimwengu wa kawaida , lakini ajabu ameshaishi miaka mingi sana bila ya kurudishwa.
“Wazee wa Hongmeng hawakufahamu uwepo wangu duniani , walifahamu nimekwisha kufariki miaka mingi iliopita”.
“Lakini mara ya mwisho ulisema ulikuwa na mawasiliano na Hongmeng”
“Ambao wanafahamu uwepo wangu hawakuuweka wazi kwa Wazee wa Hongmeng , ndio maana nikasema Wazee hawakufahamu uwepo wangu duniani”
“Kama ni hivyo naweza kutafsiri ulikuwa na mawasiliano na wajumbe wa Hongmeng pekee na walificha uwepo wako lakini ukawa unaendelea na mawasiliano nao kama ni hivyo naamini kuna sababu wakaamua kuficha uwepo wako”Aliongea Roma.
“Upo sahihi kuna sababu kubwa ya kuficha siri ya uwepo wangu duniani na ni kutokana na ahadi ya faida”
“Ahadi ya faida?”
“Ndio Mr Roma unaweza kusema niliwaahidi kitu chenye faida ili waendelee kunifichia siri ya uwepo wangu hapa Tanzania”
“Kama ni hivyo kwanini sasa hivi wanataka urudi?”
“Kwasababu ahadi sijaitimiza na siwezi kutimiza kutokana na nia yangu ya kulipiza kisasi kwa kile kilichowatokea wazazi wangu, kutokana na kutotimiza ahadi walinitishia mara nyingi kwenda kutoa taarifa kwa Wazee , lakini nilijitahidi kuwa mjanja kwa kuwasubirisha kwa maneno nikisubiria ujio wako”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa ujio wake tena.
“Unamaanisha nini kusubiria ujio wangu?”Aliongea Roma na Zenzhei alitabasamu.
“Kwasababu kuna mtu nilikutana nae miaka iliopita na akaniomba msaada na kisha akaniambia ikiwa ni muda sahihi rudia haya maneno ‘ Damu na Giza ni laana’”Aliongea Zenzei nakumfanya Roma kutoa macho.
“Ulishawahi kukutana na mtangulizi wangu?”Aliuliza Roma akiwa haamini Zenzhei anafahamu hayo maneno kwasababu yalikuwa ni maneno ambayo ni fumbo.
Mara ya mwisho Roma kuongea na Hades wa zamani alimwambia maneno hayo ya fumbo na kumpa maelekezo mtu yoyote ambaye angeyatamka mbele yake anapaswa kumsaidia.
“Mr Roma kukujibu swali , nitasema ndio nilikutana nae mara moja tu na aliniomba msaada wa kumtambua mwalimu”Aliongea na kumfanya Roma kuzidi kujawa na shauku na mshangao kwa wakati mmoja na Zenzhei alijua Roma hakumuelewa hivyo akamwelezea kwa kirefu.
Kwa maelezo ya Zenzhei ni kwamba Hades wa zamani alimuomba msaada wa kumtajia mwalimu ambaye anaweza kufundisha binadamu mbinu za uvunaji wa nishati ya mbingu na ardhi kwa njia ndefu yaani ile ya Maandiko ya urejesho isio na kikomo ambayo ndio hio aliojifunza Roma na mtu ambaye alimtajia ni Tang Chi yaani master wake Roma.
Kwa lugha nyepesi Zenzhei alimpendekeza Tang Chi kwa Hades wa zamanni na Tang Chi akaja kuwa Master wa Roma.
Roma alishangazwa na ufunuo huo wa mambo lakini bado ilimchanganya kwani kwa namna ambavyo alikutana na Tang Chi ilikuwa ni kabla alipokutana na Hades wa zamani , kuna kitu kilimwambia huenda Master Tang Chi aliagizwa na Hades wa zamani kumfundisha yeye mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
Roma alijikuta akikumbuka namna ambavyo alikutana na Master Tang Chi ilikuwa ngumu sana kuamini alikuwa ameagizwa na mtu.
“Mr Roma najua mtangulizi wako hajakuambia mambo mengi na mimi pia sio jukumu langu kukuambia yale ambayo hajakuambia kwani hata hivyo siyajui , nilimpendekeza Tang Chi kwasababu ndio binadamu pekee ambaye nilimfahamu kwa mara ya kwanza kujifunza tamaduni za jamii zisizoonekana na tokea nilipomsaidia hatukuwahi kuonana tena , lakini aliniambia msaada niliompatia ukizaa matunda basi nitayashuhudia kwa macho yangu na ndio ninapaswa kutamka maneno ya Damu na Giza ni laana”Aliongea Zenzhei na kumfanya Roma kukuna kichwa , ni kweli hakuwa akijua mambo mengi kuhusu Hades wa zamani na ilikuwa sawa kutokumuelewa, kwanza mtu mwenyewe aliishi miaka mingi hivyo huenda alikuwa na mipango mingi, Roma alifikiria na alijikuta akivuta pumzi.
“Kama ni hivyo nadhani unapaswa kuniambia shida yako na mimi nitakusaidia”Aliongea Roma na kumfanya Zenzhei kuvuta pumzi.
“Ninarudi Hongmeng kwasababu nahitajika kurudi , lakini naenda kukusubiria, mpaka sasa Mr Roma umekuwa adui namba moja wa Hongmeng na muda na saa yoyote watatoka huko walipo na kuja kukushambulia kabla ya muda huo kufika unapaswa kuwa wa kwanza kuchukua hatua”
“Unamaanisha niende Hongmeng na kupigana nao?”
“Ndio njia pekeee ya wewe kuwa salama na watu wako unaowapenda , mbinu uliojifunza ni hatari zaidi na hakuna mtu wa hongmeng yoyote ambaye amefanikisha kufikia leo ya Kuzaliwa upya”
“Lakini kama nitakuja kupambana Hongmeng watanizidi kwa uwezo wangu niliokuwa nao huu na isitoshe taarifa zinaonyesha ni wengi ambao wameshavuka levo ya Dhiki”
“Kuhusu uwezo wako sina wasiwasi umeweza kufikia levo ya kuipita Dhiki ndani ya umri mdogo sana hivyo natarajia utaenda juu zaidi ndani ya muda mfupi sana , nimekuambia nimevunja ahadi ndio maana Wazee wakagundua uwepo wangu duniani basi kile nilichoahidi nitakupatia wewe”Aliongea.
“Unamaanisha?”
“Mr Roma haikuwa bahati mbaya familia yangu kushambuliwa ni kwasababu ukoo wetu ulimiliki kitu cha thamani sana ambacho Baba na Mama hawakuwa tayari kukiweka wazi”Aliongea na kisha akampatia Roma karatasi.
“Hio karatasi imejaa taarifa ambayo ndio inanifanya nirudi Hongmeng, ndio urithi wa pekee kutoka kwa familia yangu nilioutunza kwa muda mrefu, nakupatia wewe kwasababu ni mtu sahihi wa kuwa nao”Aliongea na kumfanya Roma aifungue ile karatasi na alijikuta akishangaa baada ya kuona ni kanuni ya utengenezaji wa vidonge vya kusaidia mafunzo ya kuvuna nishati ya mbingu na Ardhi.
“Hii ni kanuni ya kutengenezea vidonge vya Poya?”
“Inaonekana ushalifahamu tayari jina lake , jibu ni ndio kama utaweza kufanikisha kutengeneza hivyo vidonge itakuwa rahisi kwako kupanda levo ya juu zaidi na hakuna kiumbe chochote kutoka Hongmeng kitakuwa tishio kwako”Aliongea na kumfanya Roma macho yake kuchanua kwa furaha na kupitia kwa haraka ile katatasi.
“Kwanini hukutengeneza hivi Vidonge wewe na kukuwezesha kupanda levo za juu zaidi na kulipiza kisasi?”
“Mr Roma nimekupatia kanuni tu , uwezekano wa kukamilisha utengenezwaji wa hivyo vidonge haitokuja kuwa rahisi na haikuwa rahisi wangu pia kutengeneza nikiwa hapa duniani na sitoweza kutengeneza nikiwa Hongmeng wewe pekee ndio naamini unaweza kukamilisha”Katika siku ambayo Roma alipata kitu cha thamani basi ni siku hio, hakuamini Zenzhei alikuwa na material muhimu na hamwambii mpaka wakati anaondoka , huenda angemsaidia hata kutafsiri kanuni hio.











SEHEMU YA 490.
Abu Dhabi- UAE.
Ni baada ya mwezi mmoja tokea waanze uchunguzi wa kile ambacho alifanya Chriss , kitendo cha kutaka kumuua Edna, waliamini kabisa majaribio ya kuuwawa kwa Edna ni nje ya malengo ya jumuia yao hio ya siri na ndio maana walitaka kuufahamu ukweli , kwanini Chriss kafanya maamuzi alioyafanya.
Uchunguzi ulikamilika mara baada ya Nadia Alfonso kumuhoji Roma na kupata majibu ya kile kilichotokea na pia kumuhoji Suzzane kwa kile ambacho kilitokea na baada ya kupata maelezo yao na kuona yanafanana waliendelea na uchunguzi wa kutaka kujua zaidi kuhusu Chriss aliishi wapi mara baada ya kuokolewa na Hades wa zamani gerezani katika mikono ya CIA.
Naam sasa ilikuwa ni siku ya ijumaa mara baada ya swala ya mchana muda wa saa tisa katika moja ya makazi ya Tajiri Khalifa ndani ya Abu Dhabi kulikuwa na kikao cha siri sana ambacho kilikuwa kikiendelea.
Ni kikao ambacho hakikuhusisha watu wengi sana ,waliohudhuria ndio mhimili wa umoja huo wa siri ufahamikao kwa jina la Ant Illuminat.
“Mmefikia katika hitimisho?”Aliuliza mwanaume mmoja alievalia kilemba kichwani na kanzu.
“Ndio Shekhe”Alijibu kijana alievalia suti huku akiwa ameshikilia kishikwambi mkonnoni na jibu lake liliwafanya watu sita walioketi kwenye meza ya pembe nne wamwangalie kwa shauku ya kutaka kumsikiliza.
“Unaweza kuendelea”Aliongea mwanaume mwingine alievalia suti na miwani , alikuwa ni mzee ambaye umri wake ulionyesha kuwa mkubwa kutokana na nywele zake kuwa nyeupe.
“Nadia Alfonso alifanikisha kufanya mahojiano na Roma Ramoni juu ya kile kilichotokea na ameweza kutupatia majibu yaliorahisisha uchunguzi”Aliongea na kisha akafanya ‘casting’ ya kishikwambi chake na Screen ya TV ya nch 85 ya kampuni ya Sumsung na palepale ilionekana picha ya ua.
“Mnachokiona kwenye Screen ni ua adimu linalofahamika kwa jina la Blue Ghost Orchid, kwa maelezo ya Mr Roma Ramoni kutoka Tanzania anasema kabla ya Chirss hajamshambulia CEO Edna na Miss Suzzane alitokea mwanamke na akawaokoa na baada ya Chriss kufariki mwanamke huyo aliacha zawasi ya hilo ua , Maelezo haya yanafanana na ya Bi Suzzane ambaye pia tulichukua maelezo yake”Aliongea na kisha akapozi kidogo na kuangalia kishikwambi chake na kwenda ukurasa wa pili.
“Blue Ghost Orchid ni utambuisho wa taasisi ya siri yenye makao makuu nchini Singapore lakini pia ni utambulisho rasmi wa mwanachama baada ya kupokea ua hilo kama zawadi kutoka kwa The Doni”aliongea na kuwafanya wale wazee kuangaliana.
“Kwa maelezo yako tunapaswa kuamini The Doni ndio aliemuokoa CEO Edna si ndio?”Aliuliza na kumfanya kijana yule kutingisha kichwa na kisha akaendelea.
“ Kwa maelezo ya Bi Suzzane na Mr Roma mwanamke aliemuua Chriss ni Clellia Allisanto ambaye ni katibu mkuu wa umoja wa mataifa”Aliongea na kuwafanya wote kuangaliana.
“Mr Alban unatuambia kwamba aliemuokoa Edna ni Katibu mkuu wa umoja wa mataifa?”Aliuliza mzee mwingine wa kiafrika alievalia suti.
“Tumeshindwa kufikia kwenye hitimisho kutokana na kwamba hakuna namna yoyote ya kuthibitisha kama Clellia Allisanto ni The Doni”Aliongea na kuwafanya waanze kuongeleshana wao kwa wao kwa dakika kadhaa na kisha wakamgeukia.
“Vipi kuhusu Chriss, aliishi wapi mara baada ya kutolewa gerezani na kwanini alitaka kumuua Bi Edna kuna dhamira yoyote mmepata kuifahamu?”.
“Kamati yetu ya uchunguzi iliweza kupokea nyaraka iliotumwa kwetu kwa njia ya barua pepe na mtu ambaye hakujitambulisha jina na imetoa majibu ambayo tumeshindwa kuyahakiki na nitayaweka wazi”Aliongea na kisha alienda kwenye Gmail na kufungua nyaraka iliotumwa na palepale ilionekana kwenye Skrini na kuwafanya wale wazee wenye miwani kuziweka vizuri ili kusoma na wale ambao macho yao yalikuwa imara walikodoa macho.
“Nyaraka hii inaonyesha Chriss aliishi ndani ya Vatican mara baada ya kutolewa gerezani nchini Marekani na alikuwa ni mkutubi wa maktaba Chemba namba 4”Alielezea ile nyaraka na kuwafanya wale wazee kuendelea kushangaa.
“Kuna taarifa yoyote inaonyesha alikuwa na dhamira ya kutaka kumuua Bi Edna?”Aliuliza na Alban alitingisha kichwa kuashiria jibu ni ndio na kisha akapangusha kishikwambi chake na akatoa nyaraka nyingine iliotumwa kwao kama barua mfumo wa portable file(PDF).
“Hii ni barua ambayo tunaamini imeandikwa na Chriss mwenyewe kabla ya kutekeleza misheni ya kutaka kumuua Bi Edna nchini Tanzania na inaonyesha sababu kwanini alifanya maamuzi tofauti na misheni aliopatiwa.”Aliongea na palepale alianza kuisoma.
Kwa maelezo ya barua inaonyesha ni kweli Chriss alikuwa akiishi ndani ya Vatican kwa kipindi chote tokea atoroshwe kwenye gereza chini ya serikali ya kimarekani , anasema kwamba aliishi kwa Dilema ni upande upi anapaswa kuegamia kutokana na mfanano wa malengo ya dunia ijayo kati ya taasisi mbili tofauti yaani hio ya Ant-Illuminat na nyingine ambayo hakuitaja.
Anaendelea kusema maamuzi alioyafanya ni chaguzi alioifanya yeye mwenyewe na barua hio kama wataisoma basi atakuwa tayari amekwisha kufariki na misheni yake imefeli.
Mwisho kabisa anawafunulia kwamba misheni aliopewa kwa ajili ya Ant -illuminat ni kuwajuza kwamba kiongozi wanaemgojea sio yule ambaye wanamfikiria bali ni yule ambaye anapewa ulinzi na yule wanaemfikiria na ushahidi wa maneno yake upo kwenye mchoro wa unabii.
Mwisho kabisa wa barua anasema kama watakuwa wamefanikisha kupata barua yake basi misheni aliopewa na aliemuokoa imekamilika na atapumzika kwa amani akimlenga Hades wa zamani aliempatia misheni.
“Mchoro wa unabii!!??”Walijikuta wakiongea wote kwa wakati mmoja kwani hawajaelewa.
“Barua hii ni ya kweli inetokea kwake kutokana na sahihi na nadhani kabla ya kufikiria mchoto wa unabii tunapaswa kujua kauli yake: ‘yule tunaemfikiria sio mwenyewe bali yule anaelindwa na tunaemfikiria’ tuanzeni na kufumbua kauli yake”Aliongea mwanaume alievalia suti na Collar ya kiuchungaji.
“Albani kuna taarifa nyingine ambayo bado haujatupatia?”
“Hakuna Shekhe”
“Kwasasa uchunguzi wenu uhamie upande wa Clellia Allisanto ili kufahamu kama ndio The Doni, kuhusu kuthibitisha uwepo wa Chriss ndani ya Vatican tutatumia koneksheni tulizokuwa nazo”Aliongea Shekh na Albani alitingisha kichwa kukubali.
“Unaweza kwenda kwasasa , tunapaswa akujadili”Aliongea na kisha Albani aliondoka , haikueleweka alikuwa akitokea kitengo gani ndani ya taasisi hio ya Ant-illuminat lakini ni dhahiri ni sehemu ya kamati ya uchunguzi ilioutwa kutafiti kifo cha Chriss.
“Pastor Cohen nini maoni yako?”Aliuliza Shekhe na kumfanya mzee alievalia suti na kuwa na kipara cha nywele nyeupe kuvuta pumzi na kuzishusha.
“Mpaka kufikia leo hii ni mengi ambayo yamefanyika na tumejipanua sana ndani ya mabara karibia yote na tuna washirika wengi wa kutuunga mkono kupambana na uovu , lakini licha ya mapambano yetu hatukuwa na kiongozi na wote tunajua tarehe 24 ya mwezi wa nne kwa mujibu wa Kalenda ndio siku ya kumtambua kiongozi wetu , nadhani alichoongea Chriss tunapaswa kukifiria mara mbili ili kupata majawabu lakini pia kuihakikisha kauli yake”Aliongea Paster Cohen kwa lugha ya kingereza.
“Naungana na Pastor Cohen ,nadhani ni wakati sahihi kwanza kuchambua kile alichoandika kwenye barua yake ili tufanye reasoning”Aliongea mwingine.
“Tunaefikiria siku zote kama kiongozi wetu ajae ni mrithi wa Hades ambaye ni Mr Roma Ramoni lakini kama sio yeye kwa kauli ya Chriss je anaemlinda ni nani?”
“Nadhani kujibu swali hilo kwa wepesi ni sisi kujiuliza ni nani wa muhimu kwenye maisha ya Hades mpya?”
“Mke wake ndio muhimu zaidi”
“Upo sahihi Shekhe Assad, nadhani hili pia linatoa majawabu ya kauli ya Chriss kuwa katika Dilema”Aliongea mwingine .
“Kwa haraka haraka inaonyesha Chriss hakuwa akifanya kazi tu kama mkutubi ndani ya Vatican , huenda kuna watu aliokutana nao na kujenga nao mahusiano ambayo yamempelekea kwenye dilema na huenda dilema aliokuwa nayo ni katika kuchagua upande aidha wa kwetu au wa kwao na ni sahihi pia kuamini huenda ndio wamemuonyesha kitu alichokiita mchoro wa unabii”
“Unafikiri huo mchoro wa unabii unahusiana na Edna?”
“Kama Bi Edna anapaswa kuwa kiongozi wa umoja wetu ambaye amechaguliwa na Hades wa zamani nadhani kuna uwezekano mchoro huo wa unabii unamzungumzia na ndio maana Chriss akachagua kutaka kumuua kwa kuagizwa na upande mwingine”
“Lakini kama mchoto unamzungumzia Edna kuwa kiongozi wetu kwanini na The Doni akamuokoa?”.
“Hili ni fumbo gumu , lakini naamini majibu yake tunayo wenyewe”
“Unamaanisha nini Paster Cohen?”
“Wote tunajua namna ambavyo Hades wa zamani alivyomuhusisha Seventeen kwenye mpango LADO, mnafikiri ilikuwa bahati mbaya , Seventeen na Edna ni mapacha tena wa kufanana kabisa na mpaka sasa hatujui Seventeen yuko wapi na tukumbuke yeye ni mwanachama wa ant-illuminat na ndio ambaye alimwingiza Zoe Kovac kwenye uanachama na haikuwa hivyo tu, Seventeen alikuwa na madaraka ya kuchagua mwanachama mpya wa ‘first echelon’ cheo ambacho ni kikubwa katika jumuia yetu na ni madaraka makubwa”
“Lakini wote tunaamini kiongozi wetu amekabidhiwa muhuli na Hades wa zamani , si ndio ulivyosema Shekh Assad namna ya kumtambua?”
“Uko sahihi kwa maelezo ya Hades wa zamani tutamtambua kiongozi kwa kutuonyesha pete ya muhuri(signet ring)?”
“Basi nadhaini hilo ni jibu la hiki tunachojadiliana hapa, kama maneno ya Chriss yapo sahihi na Hades mpya sio mwenye umiliki wa pete yenye muhuri basi mke wake Edna atakuwa nao”
“Upo sahihi ndugu Khalifa , lakini kalenda yetu inatupa muda mchache sana wa kutambua nani mmiliki wa pete hio ya muhuri wa uongozi , kalenda yetu inaonyesha tarehe 24 mwezi wa nne ndio siku ambayo tunapaswa kumtambua kiongozi”Aliongea na kuwafanya watu wote kuingia kwenye mawazo na waliona ana point.
“Nadhani kuna namna moja tu ya kuthibitisha maneno ya Chriss ni ya kweli au ya uongo?”Aliongea Shekhe Assad.
“Unataka kusema nini?”
“Tarehe ishirini na nne ndio siku katika kalenda yetu ya kumtambua kiongozi wetu na Chriss katuachia tayari fumbo na wote tunafahamu mtu muhimu katika maisha ya Hades mpya ni Edna mke wake , nadhani hili ni jibu tosha kwetu, Kama Edna kweli ni kiongozi wetu basi lazima atakuwa na pete ya muhuri wa uongozi na siku hio anapaswa kutuonyesha”Aliongea na kufanya chumba kukaa kimya.
“Wajumbe mnasemaje juu ya wazo la Shekhe Assad?”
“Kama kweli fumbo la Chriss linamuonyesha Edna ndio kiongozi wetu basi lazima atakuwa na muhuri wa uongozi”Alirudia mwingine kauli ileile ya Shekhe Assad.
“Na kama hatokuwa na pete ya muhuri basi tutatambua moja kwa moja yeye sio mlengwa na sio kiongozi wetu na fumbo la Chriss sio sahihi”Aliongea na wote walikubaliana na wazo lake.
“Kama ni hivyo tunafanikishaje kumfanya atuonyeshe pete hio?”Aliuliza Tajiri Khalifa.
“Tunatakiwa kumfanya atuonyeshe na ili hilo lifanikiwe lazima tuwe na mpango, Miss Edna anaweza kuwa na muhuri lakini hana ufahamu wowote kuhusu jumuiya yetu”
“Naunga mkono hoja na matukio mengi yanaonyesha ndio kiongozi wetu na wote hatujui hapa huenda Hades mpya amemkabidhi Edna pete hio kwa maelekezo ya Hades wa zamani”
“Ni kweli kabisa hakuna ambaye anajua nini Hades wa Zamani na Hades mpya waliongea wakati wakukabidhiana urithi , huenda alimwagiza Edna apatiwe muhuli na yeye ndio anaepaswa kumlinda”
“Mimi nina mawazo tofauti , kwa maelezo ya Hades wa Zamani hajamwambia Hades mpya kitu chochote kuhusu Ant illuminat na ameseme yeye mwenyewe angefahamu kitu kimoja kimoja kadri ya muda unavyosonga,tutaomba CEO Edna atuonyeshe muhuri wa uongozi kama kweli anao lakini tusiende na wazo la kuamini kwamba Hades mpya kampatia pete hio ya muhuri wa uongozi, nadhani mpaka sasa tunaelewa kwamba Hades hajamwambia mkewe chochote kuhusu Seventeen kuwa ni pacha wake , unafikiri ingekuwa rahisi kwake kumpatia Muhuri”Aliongea Shekhe na maneno yake yalionekana kuwa na mantiki.
Makubaliano ni tarehe ishirini na nne mwezi wa nne kuonana na Edna ili aonyeshe pete ya muhuri wa uongozi wa jumuia hio ya ant-illuminat.
Naam Edna kukutana na jopo la watu hao kwa kisingizio cha kuonana na Tajiri Khalifa ilikuwa ni mbinu tu, lakini vipi kuhusu hio pete.





SEHEMU YA 491.
ROME – ITALY- Miezi miwili iliopita.
Ni miezi miwili iliopita mashariki mwa jiji la Rome katika moja ya jengo la makumbusho ya kitaifa usiku wa saa mbili na nusu kwenda tatu kulikuwa na kikao cha watu wazito.
Ni watu wazito haswa kutokana na itifaki za ki usalama ambazo zilikuwa zimekwisha kuchukuliwa , jengo hilo lilikuwa kikitumika kama la makumbusho na mara nyingi muda wote linakuwa wazi mpaka saa nne za usiku kuruhusu watu , lakini siku hio jengo hilo lenye muundo wa kikale lilifungwa kwanzia muda wa saa kumi za jioni.
Ilikuwa ni sehemu sahihi sana kwa kufanyia mikutano ya siri kutokana na muundo wa jengo lenyewe lakini kitu kingine barabara ya kuingia ndani ya hili jengo haikuwa na pilikapilika nyingi kama barabara za katikati ya jiji.
Sasa usiku ndani ya vyumba vya Ardhi ndani ya jengo hili kulikuwa na kikao ambacho hakikujumuisha watu wengi sana , jumla ya watu waliokuwa wakifanya kikao walikuwa ni wanne tu, watatu wote walikuwa wamevalia suruali nyeusi na mashati ya rangi ya bluu iliokolea na kuvaa na Collar ambazo kwa harakaraka ziliwatambulisha kama wachungaji.
Mtu mmoja pekee ndio ambaye alivalia suti pamoja na tai , mwanga wa hapo ndani haukuwa mkali sana kutokana na taa zake za rangi ya njano zilizokuwa zikiendana na muundoo wa chumba.
“Barrack nadhani unaelewa sipendezwi na vikao vya dharula”Aliongea mzungu mmoja ambaye umri wake kwa haraka haraka ni kama miaka sabini hivi.
“Andre siwezi kusahau jambo muhimu kama hilo , lakini leo tulipaswa kuonana kwa dharula na nimefarijika mmeweza kutii wito kwa haraka”Aliongea yule mwanaume ambaye amevalia suti na tai akiwaangalia wale wenzake ambao walionyesha kuwa ni wachungaji au mapadri..
“Nini kimetokea?”
“Ni kuhusu Chriss mkutubi wetu ambae alienda Tanzania kwa maagizo yetu”Aliongea na kuwafanya wale wachungaji kuangaliana lakini mwanaume alieitwa kwa jina la Andre alionyesha utofauti.
“Nini kimetokea kuhusu Chriss , makubaliano yetu ajiingize ndani ya jumuia ya Ant Illuminat ili kupata kujua kila kitu kinachoendelea”
“Pastor Michal hiko ndio ambacho kimenifanya kuitisha hiki kikao cha dharula , taarifa zilizonifikia mpaka sasa Chriss amefaiki”Aiongea mwanaume aliefahamika kwa jina la Barrack na kimya kilitawala.
“Nini kimetokea? Je amegundulika ni shushu wetu?”
“Hilo haliwezekani ndio maana nahitaji kusikia kutoka kwenu wote,sisi wanne ndio tunajua kuhusu Chriss na Pastor Andre ulihusika kumbadilisha Chriss na kuwa double agent kazi ambayo ilichukuwa muda mrefu na hata aliporudi kuwa chini yangu ulinihakikishia ni Asset ya faida kwetu na ndio maana nilimsamehe na kumpa nafasi nyingine”
“Mr Barrack tunataka kusikia nini kimepelekea kifo cha Chriss?”Aliongea mchungaji michael.
“Taarifa nilizopata inaonyesha alienda kinyume na misheni aliopewa na Hades wa zamanni ndani ya Ant illuminat na akamshambulia Edna Adebayo mke wa Hades”Aliongea na kufanya wote kumaka lakini Andre muonekano wake haukutafsirika na Barrack aligundua hilo.
“Andre mbona unaonekana kutoshangaa?”
“Chriss alipaswa kunitafuta mara baada ya misheni”Aliongea Andr.
“Unamaanisha nini Andre”
“Ni mimi niliewasiliana nae dakika za mwisho kabisa na kumwambia misheni imebadilika”
“Kwanini?”
“Wameniambia kama hatuwezi kubadili unabii tunaweza kubadili matokeo”Aliongea na kuwafanya wenzake wote kushindwa kumuelewa.
“Nilipokea ujumbe kutoka kwa baraza la 33rd degree ya kumbadilishia Chriss misheni yake na wakati nawasiliana nae aliniambia ashafika eneo la tukio na muda si mrefu angekutana na Edna Adebayo”
“Mbona mimi ndio niliwasiliana nae na kumbadilishia misheni siku moja kabla nini kinaendelea?”Aliwaza ndugu Barrack.
“Andre ni watu gani hao?”
“Prior of sion, wanajua kila kitu ambacho tunakifanya na mipango yetu na hata kifo cha Chriss waliniambia wao wenyewe muhusika mkuu ni Minerva”
“Athena ndio aliemuua Chriss?”Aliuliza Barrack huku akionyesha wasiwasi.
“Hivyo ndio walivyoniambia”
“Papa Andre , ulishawahi kunihadithia umekutana na Athena ana kwa ana nadhani huu ndio muda wa kutuambia anafanana vipi? Je ni kweli Clelia Allisanto ndio yeye?”Aliuliza kwa kutanguliza jina la Pope Mwanzoni.
“Clellia Alisanto katibu wa umoja wa mataifa sio Minerva bali Athena anatumia Clone nina uhakika na hilo”
“I knew it”Aliongea akimaanisha kwamba alijua tu.
Naam mwanaume anaefahamika kwa jina la Barrack ni raisi mstaafu waMarekani na Andre ni Pope , wawili ni Michale ambaye cheo chake haikuwa wazi na pia John cheo chake haikuwa waz.

*********
MASAA KADHAA NYUMA
Ni muda wa saa sita usiku mara baada ya Roma kuondoka nyumbanni na kwenda kuzamia nyumbani kwa Nasra kwa kupitia balkoni, muda huo huo katika chumba chake alionekana mtu mwingine akiibukia na kuanza kuangalia mazingira ya hapo ndani na mara baada ya kuridhika aliingia kwenye chumba anacholala Roma na kuwasha taa na baada ya kuona kitanda hakina mtu alitabasamu kwa kebehi.
“Kulikuwa na haja gani ya kufanya sherehe kubwa na kutuharibia maua kama unakuja kulala mwenyewe”Aliongea kwa lugha ya chini huku akigeuka nyuma.
Alikuwa ni Hermes au Prince Raphaeli ambaye mwezi mmoja nyuma alimuokoa Denisi kwa kumdhibiti Roma kupitia ndoto.
Baada ya kukagua chumba cha Roma kwa dakika kadhaa alitoka kwenye chumba hiko na kuingia kwenye korido na ndani ya dakika chache tu aliibukia kwenye chumba cha Edna.
Baada ya kuingia ndani ya chumba hicho hakuacha kuangalia mandhari ya chumba kizima na kisha akahamia kwenye kitanda na kumwangalia Edna na Lanlan ambao wamelala fofo,
“Hades unaishi na mtoto wako lakini mpaka muda huu umeshindwa kumfahamu, aliesema huna akili kweli kapatia”Alijiwazia huku akimwangalia Lanlan aliemuwekea Edna mguu kwenye shingo.
“Athena sijui ananitakia nini , Hades akiniona namwangalia mke wake namna hii lazima ataniua, inabidi nifanye haraka kilichonileta na kuondoka”Alijiwazia mwenyewe na kisha akanyanyuma mkono wake na kumnyooshea Edna kama vile anamwombea na muda uleule Edna alianza kutingisha kichwa kama vile mtu ambaye yupo ndotoni na Hermes alidumu vilevile kwa dakika kama tano na kisha akaonyesha kuridhika na akageuza macho kwa Lanlan na kumnyooshea mkono kama alivyofanya kwa Edna na Lanlan alianza kutafuna tafuna kwa kasi kama vile kuna kitu analishwa na Hermes alitabasamu na kisha akaondoa mkonno wake.
“Persephone , kwanzia kesho utafanya mambo yako yote bila kujielewa chini ya udhibiti wangu ukiwa ndotoni”Aliongea huku akimwangalia Edna kwa dakika na kisha akafungua mlango wa kutokezea kwenye balkoni na palepale alipotea kufumba na kufumbua.
*********
“Madam Persephone tusamehe kwa kukufanyia hii surprise , yote yamefanyika kwa kuzingatia itifaki za kiusalama wa kuficha kile ambacho kinakwenda kuzungumziwa hapa ndani, nadhani upo kwenye mshituko lakini kabla ya kuendelea na hatua ya pili tutaomba utoe wasiwasi kabisa na kama kila kitu kikienda sawa huenda sisi wote tukawa chini yako”Aliongea Shekh Assad na Edna alishindwa kujibu chochote na alishangaa pia uwepo wa Nadia Alfonso.
“Kwa majina yangu naitwa Ally Assad na ndio msemaji mkuu wa hili jopo lote la watu waliopo mbele yako na Kabla ya kujitambulisha kwako mmoja mmoja na kukuelezea dhumuni la uwepo wetu hapa ndani tunataka ututhibitishie kwa kutuonyesha pete ya muhuri unaokutambulisha kama kiongozi wetu”Aliongea.
“Shekhe Ally Assad unaweza kuketi”Aliongea Edna bila wasiwasi na Shekh Assad alikaa chini na watu wote walimwangalia Edna kwa shauku ya kile ambacho anakwenda kufanya.
Edna hakuonekana kuongea chochote zaidi ya kuchukua mkoba wake na kutoa kijiboksi kidogo cha rangi nyeusi , ni viboksi flani kama vile vya kuwekea pete au mkufu.
Kitendo kile cha kushikiria kile kiboksi kabla hata ya kukifungua kiliwafanya watu wote hapo ndani kuwa na mchecheto wa aina yake.
“Kwasababu wote mmekuja kukutana na mimi leo hii , basi sina budi kuwadhirihirishia kwenu muhuri ambao unanitambulisha kama kiongozi wenu”Aiongea Edna akiwa kama sio yeye vile na kisha akafungua kile kiboksi na ndani yake ilionekana pete ambayo kwa kuiangalia tu haikuwa ya kawaida, ilikuwa na mchoro juu yake ulionakshiwa kwa madini ya shaba , mchoro ulikuwa kama vile ni tunda ambalo limekatwa kwa mshazari katikati sasa ule muonnekano wake wa ndani ndio ulifanana na hio pete.
Edna aliitoa na kuishikilia mkononi na kisha kwa mbwembwe zote aliingiza kidoleni katika mkono wake wa kulia na akaunyoosha juu ule mkono kuelekezea ule upande wa pete kuonekana kwa watu waliokaribu.
“Shekh Ally Assad hii ni Signet ring inatumika kama muhuri na ni kwa muda mrefu haijatumika , unaweza kuiangalia kwa ukaribu kuona kama mchoro wake unafanana na muhuri unaonitambulisha kama kiongozi wenu”Aliongea Edna na Shekhe Ally Assad aliangalia kwa umakini ile pete na alijikuta akipatwa na mshangao usiokuwa wa kawaida na palepale aliwageukia wenzake wote na kuwapa ishara ya kuashiria ndio muhuri wenyewe na wote kwa pamoja walisimamaa na kuinamisha vichwa chini kwa mara nyingine.
“Karibu sana Malkia wetu Persephone”Waliongea kwa mara nyingine baada ya kusimama na Edna alinyoosha mkono juu kuwazuia na akawaambia waketi chini na walitiii.
Suzzane na Nadia walikuwa na mshangao kwani hawakutegemea kutokutana na upinzani kutoka kwa Edna , lakini alionyesha kana kwamba watu waliopo mbele yake anawafahamu mbaya zaidi aliongea kimadaraka.
“Leo nimejitambulisha kwenu kikalenda , lakini muda wangu wa kuwaongoza bado , mpaka muda utakapokuwa sahihi nitawatafuta, kwasasa Shekh Assad ataendelea kuongoza jumuia yetu kwa niaba yangu na malengo yote yanapaswa kutimia kabla ya siku ya kurudi kwangu”Aliongea na kuwafanya kuonyesha sura za kutoelewa maana ya maneno.
*********
Blandna alijikuta akishangaa mara baada ya kuambiwa na raisi Senga kuhusu Roma kile alichomfanyia Desmond mtoto wa raisi Jeremy, hakujua jambo hilo kama limetokea kwani Roma na Edna hawakumwambia.
Usiku wa juzi walivyorudi alijua kabisa kuna jambo ambalo limetokea lakini hakuhoji sana kwani Roma alimwambia hakukuwa na tatizo na ni sherehe tu ambayo haikuwa nzuri.
Na yeye alipotezea baada ya kuwaona Edna na Roma asubuhi walikuwa wamepatana na ile hali ya kununiana ilikuwa imeisha na ndio maana hakuhoji sana.
“Kwahio hiki ndio ambacho ulitaka kuongea na mimi?”Aliuliza Blandina
“Kuna lingine ambalo ulitarajia kusikia kutoka kwangu , nimekuita hapa kukuambia kile alichokifanya mtoto wako ili umuonye kwani akiendelea kuchafua amani ya nchi yangu nitamchukulia hatua”Aliongea na kumfanya Blandina kumwangalia Senga kwa huzuni.
“Kwanini unamwita mtoto wangu peke yangu Senga , Wewe sio mtoto wako? Au ni kwasababu amebadilisha jina na kuitwa Roma ndio kinachokupa shida ya kumtambua, Senga najua huwezi kunisamehe lakini Roma bado ataendelea kuwa mtoto wako”
“Kimya!!!, wewe na Roma kwangu mlishakufa na ndege na sitaki kuhusika na maisha yenu , ninachotaka kutoka kwako ni kumuonya Roma aache kuharibu diplomasia ya nchi”
“Senga tangu lini ukawa mnafiki wa hisia zako mwenyewe?”
“Unamaanisha nini?”Aliongea Raisi Senga huku awamu hii akionyesha kakarisika maradufu.
“Maneno yako yapo tofauti na hisia zako Senga, unafikiria sijui kinachoendelea kwenye moyo wako , ulifikiri nitashindwa kujua kile unachojisikia , sijakusahau Senga”
“Kimyya , Blandina naomba usinikasirishe zaidi kukaa na mimi chumba kimoja usijipe ujasiri wa kuongea unavyojisikia , wakati ule ulishapita na sasa nimekuwa raisi kwa juhudu zangu wakati wewe ukijificha”
“Kinachokusumbua Senga ni kwasababu Roma ana nguvu zaidi kuliko wewe , uwezo wake na nguvu zake zinakufanya ujihisi huwezi kuwa baba mbele yake, Senga acha kuishi kwa mateso unapaswa kuachilia baadhi ya mambo megine yasahaulike kwenye moyo wako”
“Kuna vitu naweza kusahau , lakini siwezi kumsahau mwanamke alienisaliti”Aliongea na kumfanhya Blandina kuanza kutokwa na machozi.
Muda huo maongezi yao walikuwa wakiyafanyia ndani ya chumba cha hoteli hivyo ilikuwa ngumu kwa mtu wa nje kujua kile ambacho kinaongelewa na ilikuwa mara ya kwanza kwa Senga na Blandina kukutana wakiwa peke yao tokea arudi Tanzania na huenda ni mwanzo mzuri wa mapatano.
“Najua Senga huwezi kusahau na huwezi kunisamehe lakini upendo wangu kwako hakuwahi kupotea kwa miaka yote ambayo hukuweza kufahamu nipo hai”
“Blandina acha kuwa mnafiki mbele yangu utanikasirisha , nimekuja hapa kukuonya kuhusu Roma kuingilia amani ya taifa”
“Una uhakika ndio kitu pekee ambacho ulitaka kuniambia mpaka kutaka kuongea na mimi kwa kujificha ficha?”Aliuliza na kumfanya Senga amwangalie Blandina huku akikosa neno la kuongea.
Alichoongea Blandina ni ukweli mtupu, kama kweli alitaka kumuonya tu kuhusu Roma haikuwa na haja ya kumuita hotelini kwenye chumba cha Presidontial Suite tena kwa siri.
Blandina alimwangalia kwa muda namna ambavyo amekosa neno la kuongea na kisha akaangalia mkoba wake na akauchukua.
“Kwa mra ya kwanza nimefurahi kukuona kwa ukaribu Senga, nitamwonya Roma kutokuingilia uongozi wako”Aliongea na kisha alisogelea mlango akitaka kutoka.
“Subiri..!!!”Aliongea na kumfanya Blandina kusimama na kugeuka na Senga aliingiza mkono kwenye mfuko wa koti na ilionekana kuna kitu anatoa.




SEHEMU YA 492
Roma hakujua kinachoendelea kabisa na baada ya kutoka kwa Afande Kweka hakupitia nyumbani kabisa , akili yake ilimwambia aende kuonana na Rufi kwanza kuongea nae kuhusu kanuni aliopewa na Zenzhei ya kutengeneza vidonge vya nguvu za kijini , alikuwa na muwashawasha wa kufahamu kama Rufi angeweza kuelewa kanuni zote.
Dakika chache mbele mara baada ya kuendesha gari aliweza kufunga breki chini ya jengo la apartment anapoishi Rufi na alitoka kwenye gari na kuzisogelea lift.
Baadaya kuingia kwenye lift na kubonyeza kitufe cha floor husika simu yake ilitoa mtetemo wa ujumbe wa meseji ulioingia ,alifungua na kuona ni ujumbe ulitoka kwa Xiao Xiao na aliupotezea palepal.
Ilikuwa ni siku zaidi ya mbili msichana huyo wa kichina hakukata tamaa kutuma jumbe za kumsalimia Roma na nyingine za kuchombeza lakini Roma hakujibu hata moja , hakutaka matatizo na mke wake lakini pia alijua akiwa na ukaribu na msichana huyo itakuwa rahisi kwa Rufi uwepo wake hapa Tanzania kufahamika kwa wepesi , hivyo alijiambia anapaswa kumuepuka kwa nguvu zote.
Baada ya kutoka kwenye lift alibonyeza kengere na mlango kwa ndani ulifunguliwa na Rufi ambaye amevalia tisheti ya jezi ya Man U huku mkononi akiwa ameshikilia juisi ya matunda.Alitabasamu na kumpa ishara ya kuingia na Roma alifanya hivyo.
“Inaonekana unapenda sana mambo ya kompyuta , kwa mwonekano wako ulipaswa kujifunza vitu vilaini vilaini visivyotumia akili nyingi”Aliongea Roma mara baada ya kuona tarakishi ikionyesha namba namba ambazo hata hakuelewa.
“Kompyuta naipenda kwasababu nahisi kama dunia yote naiona , nimejifunza mambo mengi sana na kwasasa najaribu kutafuta Proffesional Hacjer anielekeze baadhi ya mambo madogo madogo”
“Kwahio unataka kuwa mdukuzi , haupendezi kabisa kwa fani hio?””
“Kipi kinanipendeza? Au kutapeli watu ndio kazi nzuri inayonifaaa?”Aliongea na Roma hakumjibu na aliishia kumwangalia tu kuona kama ana shida yoyote kwani tokea amuache mara ya mwisho hakuwasiliana nae kabisa na kumpa habari za Xiao Xiao msichana wa kichina aliemkimbia.
“Unaendelejeaje, ulitoka kweli humu na kwenda kutembea?”
“Naogopa hata kwenda Supermarket na hofia naweza kukutana nae tena” Aliongea huku akijibwaga kwenye sofa kivivu na kumfanya Roma amuonee huruma.
“Unapaswa kutoka bila ya kuhofia chochote hakuna mtu yoyote wa kuja Tanzania na kukufosi urudi ilihali mimi nipo”.
“Ah .. najua unaweza kunilinda lakini hawatoacha kuja mara kwa mara lazima watalazimisha nirudi sitaki kukuongezea zaidi matatizo”
“Nishakuambia usiwe na wasiwasi juu ya hilo nimefuatilia taarifa za msichana uliekuwa unamkimbia yupo Tanzania kikazi”
“Kweli?”
“Unafikiri nakudanganya? , umeacha lini kutokuniamini?”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kutabasamu na kushindwa kuongea chochote na Roma aliona apotezee mada hio na kwenda moja kwa moja kwa kile kilichomleta.
“Nimekuja kukuuliza namna ya kutengeneza vidonge”
“Unataka kutengeneza vidonge!?”
“Kwanini unaonyesha kushangaa ,ushasema mwenyewe vidonge ni muhimu katika kusaidia kupanda levo naweza nisihitaji mimi lakini warembo wangu nataka niwapatie ili viwasaidie”
“Ndio vidonge ni muhimu sana kwa wanaoanza mafunzo , lakini kuna mahitaji yake na kanuni za kutengeneza”
“Ndio maana nimekuja kwako nataka kujua hayo mahitaji”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kufikiria kidogo.
“Kama kweli una nia ya kutengeneza vidonge. kuna changamoto tatu ambazo unapaswa kuzivuka , Changamoto ya kwanza lazima upate mimea ambayo hutumika kutengenezea, hii sio rahisi kwasababu mimea hio ni adimu sana kupatikana na hata ile ambayo inatengeneza vidonge vya thamani kubwa imepotea kabisa, katika miliki za kijini kwenyewe huwezi kuipata hio mimea na ndio maana licha ya uwepo wa wenye ujuzi mkubwa wa kutengeneza wameishia kutengeneza vidonge vya kawaida tu”
“Lakini umesema kuna wanaokuja huku duniani kutafuta hio mimea ?”
“Ndio kuna wanaosafiri mpaka duniani kwa ajili ya kutafuta mimea ya kutengenezea vidonge lakini mara nyingi huishia maeneo ya karibu na bara la Asia , kwani wengi wao wanasema wanaogopa kuvunja sheria za the gods treaty”
“Kama ni hivyo basi uwezekano wa kupata hio mimea upo ,ninachotakiwa kufanya ni kutuma watu wangu wajaribu kufatilia, je ni wapi ambapo unaamini mimea hio inawezekana kupatikana?”
“Sina uhakika ila marra nyingi ni sehemu ambazo ustaarabu wa kale ulianzia kama vile Misri na maeneo mengine kama hayo”Aliongea na kumfanya Roma kutingisha kichwa kumuelewa.
“Vipi kuhusu changamoto inayofuatia?”
“That is even harder , You would need a high Quality Cauldron”Aliongea akimaanisha kwamba changamoto ya pili ni ngumu zaidi kwasababu atahitajika kuwa na Cauldron.
“Cauldron?”Roma aliuliza.
“Ndio Cauldron ni Dhana ambayo ipo mfano wa chungu kikubwa ambacho kimetengenezwa kwa madini maalumu ambayo yalipatikana enzi za kale,ni madini ambayo yana uwezo wa kuhimili kiwango kikubwa cha joto , kwa uelewa wangu katika miliki za kijini vipo vitano tu hivyo vyungu , Kekexil wanavyo vitatu ,ukoo wa wakwe zangu wanacho kimoja na Hongmeng wenyewe wanacho kimoja , kama kuna jamii nyingine ambazo wana aina hio ya chungu kinaweza kuwa nje ya matumizi hivyo haitokuwa rahisi”
“Changamoto ya tatu ni kuweza kudhibiti moto wa njano na mweupe ambao ndio hutumika kutengenezea hivyo vidonge kwa joto kubwa sana zaidi ya joto la kuyeyushia chuma na kubalansi na Chungu hiko”Chungu kinachozungumziwa hapo ni cha kijini ambacho ni kama Cauldron
“Changamoto ya tatu ya kudhibiti moto wa rangi ya njano na mweupe sio tatizo”
“Unamaanisha unao uwezo huo?”aliuliza huku akionyesha mshangao na Roma alitingisha kichwa.
“Kwanini hujazungumzia kuhusu andiko la kanuni za kutengenezea hizo dwa?”Aliuliza Roma akimaanisha andiko la kanuni alilopatiwa na Zenzhei.
“Kila koo ina kanuni zake , lakini ilisemekana mwanzoni Hongmeng walikuwa na andiko la kanuni ambayo hutengeneza vidonge vyenye uwezo mkubwa sana ,lakini bahati mbaya andiko hilo lilipotea, ndio ninachojua japo sina uhakika,lakini hilo lisikupe shida haina haja ya kuwa na hizo kanuni kikubwa ni namna ya kudhibiti joto la moto wa kichawi mweupe na wa njano ukishafanikisha kupata hiko Chungu”Aliongea
“Nitakuwa naendelea kuvuna nishati huku nikisubiria watu wangu waweze kutafuta hayo maeneo uliozungumzia , unaonaje kama wakifanikisha unisindikize”
“Mimi? , unamaanisha twende pamoja?”
“Ndio ,najua itakuwa usumbufu lakini siwezi kujua mimea inayohitajika nikienda mwenyewe”
“Lakini inawezekana ikawa ni mbali na Tanzani misituni huko”
“Usiwe na wasiwasi nishaishi sana msituni hivyo nina uzoefu wa kutosha”Aliongea Roma.
“Mimi sina tatizo lakini vipi mkeo anaweza akakasirika?”Aliongea kwa sauti ndogo huku akiona aibu.
Na kabla Roma hajajibu simu yake ilianza kuita na aliitoa na kuangalia mtu anaempigia na alishangaa ni Bi Wema , alipokea harakaharaka na kuweka sikioni.
“Mr Roma nadhani Miss Edna kapatwa na tatizo”
“Unamaanisha nini kapatwa na tatizo Bi Wema , nini kimetokea?”
“Amerudi kutoka kazini saa kumi kamili za jioni na akasema ana usingizi , amelala mpaka muda huu na nimejaribu kumuamsha haamki , Lanlan na yeye amejaribu kumuamsha kwa nguvu lakini hajashituka”Aliongea Bi Wema huku sauti yake ikionyesha wasiwasi na kumfanya Roma kuguna.
“Ana pumua?”
“Ndio kifua kinapanda na kushuka ndio hivyo haamki , nadhani ni vyema ukarudi umuangalie nina wasiwasi kwani sio kawaida mtu kulala na kushindwa kuamka”Aliongea Bi Wema na kumfanya Roma apumue kidogo kwa ahueni.
“Nakuja sasa hivi Bi Wema”Aliongea Roma na kisha akata simu.
“Nadhani mke wangu kapatwa na tatizo , ngoja niwahi”Aliongea Roma na Rufi alitingisha kichwa .
******
Afande CammiliusKweka alionekana kuathirika sana na taarifa ya Zenzhei kutaka kurudi Hongmeng , alijitahidi kuonyesha kuwa sawa lakini ukweli alikuwa akiumia kiume lakini hakuwa na uwezo wowote wa kumzuia kutoondoka kwani asingeweza kumlinda zidi ya Hongmeng.
“Zenzhei niseme asante sana’Aliongea Afande Kweka kwa sauti hafifu na muda huo ni kama masaa mawili mara baada ya Roma kuondoka.
“Camillius kwanini unanishukuru?”
“Asante sana kwa kwa kujjifanya kuwa mzee mbele ya macho ya watu ili mradi unilinde bila watu kukushitukia , asante kwa kufanya kazi za hapa kama vile ni mfanyakazi wa ndani , asante sana kwa kumfanya mke wangu kipindi kile kufa kifo cha amani”Aliongea Afande Kweka huku macho yakiwa makundu na hata Zenzhei mwenyewe alishindwa kujizuia na kudondosha chozi.
“Hupaswi kusema hivyo Cammilius ulikuwa ni wajibu wangu”
“Hapana, nimekukatili sana kwa kipindi chote ulichokuwa na mimi lakini bado nikakosa aibu na kuwa mbinafsi na kukufanya uendelee kuwa karibu yangu”
“Camillius usiongee hivyo nilikuwa na furaha kuishi na wewe”
“Zenzhei matumaini yangu ni kwamba hutonichukia , najua kwanini ulikaa na mimi kwa miaka mingi sana lakini nilishindwa kufanya chochote juu ya hisia zako kutokana na kukosa ujasiri , nilishindwa kuzipokea na mpaka sasa nashindwa kuzipokea licha ya uzee huu”Aliongea afande Kweka na kumfanya Zenzhei kufumba macho yake huku machozi yakimtoka.
Ni kweli alikuwa akimpenda Afande Camillius Kweka tokea mara ya kwanza walipokutana , lakini licha ya kuonyesha hisia zake kwa mzee huyo hakuchukua hatua yoyote na yeye kukosa ujasiri wa kuchukua hatua zaidi.
“Camilius kabla sijaondoka nitarudi kwenye mwonekano wangu wa mwanzo wakati tunakutana nadhani itakufanya usijione mwenye hatia” Aliongea Zenzhei na palepale mwili wake ulibadilika taratibu ,ilikuwa ikishangaza mno kwani ndani ya nusu dakika alibadilila na kuwa msichana kama wa miaka ishirini na nne mwanamwali , ilikuwa ni sahihi kusema alikuwa akifanana kabisa na Xiao Xiao japo yeye kidogo alikuwa na umbo la kuvutia na huenda angekutana na Roma angefanya jambo la kueleweka.
Ilionekana ili kuishi na Afande Kweka ilibidi ajizeeshe ili kuficha ujini wake , kwani kama asingefanya hivyo angebakia kuwa msichana mdogo ilihali Afande Kweka alikuwa anazeeka.
“Nakumbuka mara ya kwanza tulipokutana Sudani ulikuwa na miaka hamsini Camilius”Aliongea Zenzhei na sio sura tu iliobadilika hata sauti yake pia ilikuwa imebadilika.
“Haha.. bado urembo wako uko vilevile hakujabadilika chochote”Aliongea huku akitoa kicheko chenye machungu na kumfanya Zenzhei kutabasamu akikosa neno.
“Nadhani hii ni kwaheri ya moja kwa moja, naamini siku ukirudi nitakuwa tayari nimeshakufa”aliendelea kuongea na kumfanya Zenzhei kuingiwa na huzuni.
“Kwaheri ya kuonana Camilius” Aliongea Zenzhei.
“Kwaheri ya kuonana Zenzhei hakikisha unakuwa na maisha ya furaha na kutafuta mtu anaekupenda”
“Asante sana Camilius”Aliongea na kisha wakaangaliana usoni kwa madaki kakadhaa na Zenzhei alikosa ujasiri wa kuendelea kusimama mbele ya Camilius na palepale alipotea kwenye macho yake.Na hio ndio safari ya Zenzhei kurudi ujinini ikaanza rasmi.
 
SEHEMU YA 493.
Roma kwanza baada ya kufika nyumbani alijaribu kumuasha Edna kwa njia ya kawaida kwa kumshitua , lakini ilionekana kweli Edna hakuwa akiamka na jambo hilo hata yeye kwake lilimshangaza.
Alianza kuukagua mwili wake kwa kuupiga X-Ray na nguvu zake za kijini na alionyesha kuwa sawa kiafya na hakuwa na shida yoyote lakini jambo moja kubwa tu la kushangaza ni mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda kasi mno.
Roma aliamua kumuingizia nguvu ya kimaandiko ya urejesho kiasi kidogo akidhamiria kumuondolea uchomvu na baada ya kumaliza tu Edna alishituka kutoka usingizini na kufumbua macho yake taratibu..
Baada ya kushituka alionekana kushangaa Roma akiwa mbele yake na alianza kuangaza mazingira ya chumba, Roma alimwangalia kwanza pasipo ya kumuongelesha neno.
Edna mara baada ya kuangalia saa ya mshale iliokuwa kwenye meza alijikuta akishangaa na palepale alitoka kitandani na kusogelea dirisha na kisha akasukuma pazia na kuangalia nje.
“Roma nini kinaendelea mbona ni saa moja na nusu usiku sio asubuhi?”Aliuliza Edna huku akionyesha hali ya kuchanganyikiwa na kumfanya Roma hata yeye mwenyewe amshangae na kujiuliza mke wake kapatwa na nini au kuna kitu kilimpata.
“Mbona hunijibu sasa hivi ni saa ngapi?”Aliuliza kwa mara nyingine na Roma alimsogelea na kisha akamshika mkono na kumkalisha kwenye sofa alijua moja kwa moja huenda amemka na mawenge.
“Nini kimekuchosha kazini mpaka ukapatwa na usingizi mzito mpaka unatia watu wasiwasi?”Aliuliza Roma lakini Edna alishindwa kujibu na haikueleweka alikuwa akifikiria nini kwenye kichwa chake na hata Roma alishindwa kumuelewa.
Edna katika uhalisia tukio la mwisho ambalo alikumbuka ni usiku wa jana yake muda ambao alikuwa akimwangalia Lanlan uso wake wakati wote wakiwa kitandani na hata muda ambao alipotelea usingizini hakukumbuka na matukio yaliotokea siku nzima mara baada ya kuamka asubuhi kwake ilikuwa ni kama ndoto na ndio kwanza ameshituka kutoka usingizini akitarajia muda huo iwe ni asubuhi.
Roma kuna kitu alihisi sio cha kawaida na palepale alimsogelea Edna na kumshika mabega.
“Edna niangalie usoni”Aliongea Roma na Edna alimwangalia Roma kwa namna ya kuchanganyikiwa na upande wa Roma alichokuwa akidhamiria ni kutaka kuangalia kiini cha macho ya Edna , kuna jambo alihisi ndio maana alitaka kufanya hivyo.
“Edna niambie umeota nini?”Aliongea Roma mara baada ya kuona kitu ambacho alikuwa akikitafuta kwenye macho yake.
“Edna unakumbuka ulichokiota?”Aliuliza Roma kwa mara nyingine mara baada ya kuona Edna hatoi majibu na Edna alitingisha kichwa kama anakumbuka alichokiota na Roma alijikuta akipata ahueni na kukaa kwenye sofa pembeni yake.
“Anza kukumbuka taratibu taratibu na unifahamishe ulichoota katika mtiririko wa matukio?”Aliongea.
********
Ndoto yake ilianzia asubuhi ,alianza na taratibu zake za kawaida za kila siku kama ilivyozoeleka na hata muda ambao alikutana na wanafamilia na kuwasalimia hakuna ambaye alijua mwenzao anaota.
Edna siku hio ndio aliemsindikiza Lanlan mpaka barabarani na kuchukuliwa na bus lao la shule na baada ya hapo alirudi ndani na akajiandaa na akaelekea kazini kama kawaida na baada ya kuingia ndani ya jengo la makao makuu ya kampuni alisalimiana na wafanyakazi baadhi aliokutana nao njiani , akiwemo Dorisi , Nasra na Benadetha.
Na kila kitu kilikuwa sawa kabisa , bado hakuna aliejua kabisa Edna akili yake muda huo ilikuwa chini ya utawala wa mtu mwingine na alichokuwa akikiona kwake ni kama ndoto.
Baada ya kuingia kwenye ofisi yake Recho msaidizi wake aliingia na kisha akamsomea ratiba zake za siku hio kwanzia asubuhi mpaka muda wa kutoka kazini na baada ya kuridhika akampa maagizo ya kazi ambazo anapawa kufanya kwa siku hio na kisha akatoka.
Baada ya kufanya kazi kama nusu saa tu mlango uligongwa na akaruhusu mgongaji kuingia na alikuwa ni Recho ambaye mkononi alionekana kushikilia Parcel iliofungwa kwa karatasi za Khaki.
“Boss kuna mzigo wako umefikia kutoka mapokezi”Aliongea Recho kwa heshima na Edna alimpa ishara amfikishie mezani kwake.
Baada ya kupokea kwanza alianza kusoma anuani ya mzigo huo na hakika yeye ndio aliekuwa mlengwa kwani jina lake liliandikwa kwa usahihi na mahali ambapo mzigo ulipaswa kufika, lakini kati ya mizigo mingi ambayo anapokea huu ndio mzigo ambao haukuwa na jina la mtu alietuma.
“Unaweza kwenda” Aliongea na kumfanya Recho kuinamisha kichwa na kisha akatoka ndani ya ofisi hio na Edna alichana ile bahasha ili kuangalia nini kipo ndani yake na hapo ndipo alipokutana na kiboksi cha rangi nyeusi , vilikuwa ni viboksi ambavyo alikuwa akivifahamu vinahifadhia vito vya thamanni kwa mfano pete , mikufu na Saa.
Alishangaa kupokea mzigo wa aina hio ambao ulitoka kwa mtu ambaye hajaweka jina lake wazi , lakini kwakuwa alikuwa na shauku ya kutaka kujua nini kipo ndani yake , hakutaka kupoteza muda bali alifungua ndani na kuangalia na hapo ndipo alipojikuta akitoa macho mara baada ya kuona pete.
“Hii petee…!!”Alijikuta akikosa neno la kuongea na kuitoa taratibu na kuishika na mkono wake wa kulia na kuanza kuiangalia kwa namna ya kuichunguza.
Ni pete ambayo ilikuwa mpya kwenye macho yake lakini kwa wakati mmoja haikumshangaza, kwake ilikuwa ni kama pete ambayo ashawahi kuimiliki katika nyakati ambazo ni kama amezisahau kwenye maisha yake na baada ya kuiona ni kama kumbukumbu zilikuwa zikija na kupotea.
Aliiangalia kwa muda kama wa nusu saa kwa kuichunguza mpaka muda ambao Recho aliingia tena kwenye ofisi yake na kumjulisha dakika kumi tano zijazo atakuwa na kikao na idara ya uhasibu na mipango na taarifa hio ilimfanya airudishe ile pete kwenye kijiboksi chake na kisha kaweka kiboksi kile ndani ya mkoba wake na akageukia tarakishi yake na kuanza kusoma baadhi ya taarifa ambazo alipaswa kuzi ‘adress’ siku hio kwenye kikao cha asubuhi.
Kwa kawaida Edna hufanya vikao viwili mpaka vitatu kwa siku hivyo mpaka inafika muda wa mchana alikuwa alishakamilisha taratibu zote za kawaida na kutoa maagizo na ratiba iliokuwa imebaki ni moja tu ya saa tisa kamili,ambayo alipaswa kwenda kuonana na Tajiri Khalifa akiwa yeye na Suzzane.
*******
Edna alikuwa akimuelezea Roma kuhusu ndoto yake , lakini kwa wakati mmoja alihisi kile alichokielezea ni kama kumbukumbu , ilikuwa ni kama mgonjwa ambaye amepoteza kumbukumbu na sasa ndio zinaanza kurejea ndio kilichokuwa kikiendelea katika kichwa chake kadri alivyokuwa akisimulia.
Upande wa Roma kuna jambo ambalo sio la kawaida amegundua kupitia macho ya Edna na hata kumwambia amuelezee upya kile alichokiota alikuwa na maana yake.
Mpaka Edna anakuja kumaliza aliweza sasa kuona hakuwa ndotoni na kila kitu alikifanya katika uhalisia , hata ile hali ya kuchanganyikiwa ilianza kupotea ,alianza kushangaa nini kimetokea kwani dakika zilizopita nyuma alijihisi kama alikuwa ndotoni na baada ya kurudia kumuelezea Roma kile alichokiota kila kitu kiligeuka kuwa uhalisia kwa kumbukumbu zake kukaa sawa.
“Ikiwa mtu umeshikiliwa ufahamu na uhalisia kugeuka ndoto, ili kutoka kwenye mtego unachotakiwa kufanya ni kukumbuka mwanzo na mwisho”Aliongea Roma na kumfanya Edna kutokumuelewa..

“Unamaanisha nini kushikiliwa ufahamu?”
“Sasa hivi unajionaje , unahisi ulichonielezea ni ndoto?”Aliuliza Roma akipotezea swali lake.
“Sijui hata nini kinanitokea?”Aliongea huku akionekana kuchanganyikiwa kuna baadhi ya vitu hakuweza kuelewa , hata kama kile alichohadithia hakikuwa ndoto kwanini alifanya baadhi ya vitu bila ya uelewa wake.
Roma alijua Edna atakuwa mwenye kuchanganyikiwa na hakutaka kumuona akizidi kuumiza kichwa. alichokifanya ni kumshika mkono na kumpitishia nguvu ya kijini ambayo ilimfanya Edna kuegamia kwenye sofa na kupotelea usingizini kwa mara nyingine.
Baada ya kulala alimbeba na kumlaza kitandani na kisha akasogelea mkoba wake alioenda nao kazini.
Katika maelezo ya Edna alisikia neno pete na ndio ambacho alitaka kutafuta na aliweza kuona boksi la rangi nyeusi ndani ya mkoba wake na akahisi huenda ndio ambao alikuwa amezungumzia.
Mpaka hapo Roma alishajua mke wake siku hio kuna mtu alimchezea kwa kushikilia ufahamu wake na alijiambia hatua yakwanza kuthibitisha kile kilichotokea ni kuanza na ushahidi wa pete ambayo alizungumzia.
Katika maisha Roma alishapitia vitu vingi vya ajabu ambavyo vingi kwa binadamu wa kawaida vilikuwa ni vya kustaajabisha , hivyo hata swala la Edna halikumshangaza bali lilimuacha na maswali mengi.
Roma mara baada ya kufungua kijiboksi alichokuta katika mkoba wa Edna aliona sio kile ambacho anatafuta , kiboksi alichotoa kilikuwa kina saa ya pocket watch ambayo alimpatia Edna na ilionekana Edna alitengnenezea boksi lake ili kuitunza.
Roma aliangalia uwepo wa kitu kingine ambacho kingeendana na maelezo ya Edna lakini hakuona kitu na alijiuliza pete aliokuwa akizungumzia iko wapi.
Mpaka hapo aliona njia pekee ya kupata kufahamu ukweli ni kwa kumtumia Nadia Alfonso na Suzzane kwani katika maelezo ya Edna mtu ambaye alimtambua ni Nadia Alfonso na Suzzane
Roma alitoa simu yake na kisha akapiga na ndani ya muda mchache tu iliweza kuita na kisha ikapokelewa na Roma alimuuliza Nadia yupo wapi muda huo na alijibiwa yupo Mbezi Beach nyumbani kwake.
Roma alifikiria kwa dakika na kuona haina haja ya kuonana na Nadia usiku huo aliona aonane nae kesho, alihofia jambo baya kumpata tena Edna na ndio maana alitaka kuchukua tahadhari kwa kubakia nyumbani.
Baada ya Nadia kumkubalia waweze kuonana kesho alikata simu mara moja na kisha akatoka ndani ya chumba hicho na kushuka chini sebuleni , alipaswa pia kumtoa Bi Wema hofu ya kile kilichotokea.
Alijua Edna alipatwa na shida lakini hakuwa na mpango wa kuwaelezea kila kitu kilichotokea kwa kuhofia kuwachanganya na wangeshindwa pia kumuelewa.
“Roma ameamka?”
“Ndio Bi Wema usiwe na wasiwasi , inaonekana alikuwa na uchomvu sana”Aliongea Roma na sababu yake haikumwingia akilini Bi Wema lakini alishindwa kuhoji , kwenye maisha yake hajawahi kumuona Edna akalala muda mrefu tena fofo na kushindwa hata kushituka.
“Lanlan unachora nini?”Aliuliza Roma mara baada kumuona Lanlan akiwa bize kuchota na kalamu zake za rangi, namna ambavyo alikuwa bize ilimfurahisha Roma.
“Lanlan anachora wanafamilia”Aliongea na kumfanya Roma amsogelee na kutaka kuangalia hao wanafamilia lakini Lanlan alificha akimzuia Roma asione.
“Hutaki baba wa familia kuona eh , unachora wanafamilia gani hao”
“Mama ndio wa kwanza kuona , Lanlan amemchora mama kwanza”Aliongea na kumfanya Roma atabasamu kwa uchungu maana katika maisha ya Lanlan mama yake ndio kitu cha kwanza na wengine wote walikuwa wa ziada.
Asichokijua Roma Lanlan maisha yake yote alilelewa na mama ndio maana kwake ndio kipaumbele na baba na wengine ni wa ziada tu.
Lakini hata hivyo Roma alifurahia uwepo wake hapo nyumbani na hata kushikwa na tamaa zaidi ya kupata watoto na wazo hilo lilimfanya akumbuke hajawasiliana na Sauroni juu ya kuwapa maelekezo baadhi ya vijana wake kutafuta maeneo ya kale ambayo wameishi watu na kwa muda huo yametelekezwa.
Kwa maelezo ya Rufi hizo ndio sifa ambazo aliamini mimea ambayo ingeweza kutengeneza vidonge vya kijini ingepatikana.
Baada ya kuongea kwa madakika kadhaa na Sauroni kwa lugha ya kilatini ulikuwa ni muda ambao na chakula kishaiva na Lanlan ndio aliekuwa wa kwanza kukusanya kila alichokuwa akikifanya na kukimbilia mezani na kukalia kiti chake cha siku zote , alikuwa na kiti chake ambacho hakutaka kikaliwe na mtu na kama atakuta mtu amekaa anasimama pembeni halafu anajinunisha, tabia yake iliwafanya wanafamilia kuwa na tahadhari na kiti chake.
Wakati Roma anapanga kupandisha juu kumuamsha Edna alishangaa kumuona akishuka yeye mwenyewe na ilionyesha amaamka muda, Roma alimwangalia kwa macho ya kumkagua na Edna alimwangalia Roma kwa dakika na kisha bila ya kuongea neno alitembea mpaka jikoni.
Roma alijiambia ili kuhakikisha usalama wa mke wake lazima achimbe ajue ukweli nini kilichomtokea siku hio nzima kuna hisia zilimwambia huenda ni Hermes aliefanya kitendo hiko , lakini alikosa sababu za msingi za kumshuku.
Roma alikuwa akielewa jicho ni dirisha la nafsi na alielewa iwapo binadamu atavamiwa na nguvu ya ziada na nguvu hio ikataka kuukimbia mwili basi sehemu pekee ambayo huacha alama ni kwenye macho na ndio maana aliyachunguza macho ya Edna na kuweza kugundua mara moja akili yake ilikuwa imetawaliwa kichawi na kitendo cha kulala muda mrefu bila kushituka ilimpa uthibitisho wa kipi kilimtokea na ndio maana alitaka Edna kusimulia kila kitu ambacho alihisi alikuwa akiota , ilikuwa mbinu ya kumuweka Edna sawa kiakili ili asisahau kilichotokea.
“Bi Wema simuoni Mama”
“Karudi mchana na kuaga anaenda nyumbani kumuangalia baba mzazi , kasema atarudi kesho”
“Ah.!”Aliongea na kisha akamgeukia Roma.
“Roma unaonaje tukimtembelea Babu Atanasi , najua tokea mara ya mwisho kumuona hujawahi kwenda tena”Alipendekeza Edna.
“Hata mimi naunga mkono hoja ni wazo zuri na Lanlan pia ataweza kumuona babu yake”Aliongea Bi Wema na Roma aliona Edna alipendekeza jambo zuri na alijishangaa siku zote hakuwahi kuwa na mawazo ya kwenda kumsalimia.
………….
Siku iliofuata Roma alimpigia simu Nadia Alfonso ili kujua wanaonana saa ngapi kwani jioni ya siku hio alipaswa kwenda kumsalimia Mzee Atanasi.
Edna yeye siku hio ya jumamosi hakutoka kwenda kazini na Roma aliona amefanya maamuzi mazuri.
Ukweli sio kwamba Edna hakutaka kwenda kazini lakini ni alikuwa amechanganyikiwa na kila kitu kilichotokea jana yake na aliamini hata kama angeenda kazini angekuwa kwenye mawazo.
********
Upande mwingine katika hoteli ya Maple iliopo Kunduchi a alionekana Prince Rapahaeli akiwa amekaa kwa kujiachia kwenye sofa huku akiwa ameshikilia Kishikwambi cha kampuni ya Appple,alionekana kuna mtu aliekuwa akiongea nae kwa njia ya Vidio call huku akicheka.
Sura iliokuwa ikionekana kwenye skrini ni ya mwanaume alievalia kikofia cha rangi nyeupe na Apron pia ya rangi nyeupe na shati la rangi nyeusi ndani yake.
“Unaniuliza maswala ya vyakula kama vile unapendelea , nipe mrejesho wa kilichokupeleka Tanzania”
“Kwanini siku hizi una shauku ya kila ninachokifanya”
“Sina shauku ya kufahamu unachokifanya ila nataka kujua kwani ni maswala yanayonihusu”
“Kama yanakuhusu unapaswa kuhusika kuliko kuwa mnafiki”
“Hahaha….Uniambie usiniambie najua mwisho wa siku lazima utahitaji msaada wangu na sio kwangu tu wote tuliobakia”
“Unamaanisha nini kuhusu kuomba msaada?”
“Najua mipango ya Athena ya kufufua roho ya Gaia ili kuweza kuamsha roho za ndugu zetu zilizomezwa na binadamu lakini unafikiri kwa teknolojia iliopo kwa sasa atafanikisha, lazima atahitaji msaada wetu”Aliongea kwa kijerumani na kumfanya Prince Raphaeli kukaa vizuri kwenye sofa.
“Lakini hatufahamu wapi Zeusi alificha jiwe lenye Roho yake mpaka sasa na imetuchukua miaka mingi kutafuta sana kati ya binadamu”
“Nikajua unaamini unabii Hermes”.
“Unabii ule niliacha kuamini muda mrefu lakini Athena bado anaamini Hades ndio njia ya kufanikisha kuupata moyo wake”
“Haha.. wewe ni mnafiki sana Hermes kama upoTanzania kwa maagizo ya dada yako basi ni dhahiri bado unaamini unabii”..
“Haijalishi najali kuhusu unabii au lah , kwangu mimi matokeo ni muhimu”
“Nieleze kwanza matokeo uliyoyafanikisha kwa Persephone , ninashauku ya kufahamu”
“Kuna kitu hakipo sawa kwa Persephone, ni binadamu wa kwanza nilietumia nguvu nyingi sana kuidhibiti akili yake”.
“Niambie zaidi , ni kipi kimetokea?”
“Poseidon kwanini unashauku sana na Persephone”
“Nielezee bwana unaelewa kwanini nina shauku ya kujua”Aliongea na kumfanya Hermes kufikiria kidogo kama mtu anaetafuta maneno ya kuongea na kumfanya Poseidon kumwangalia kwa shauku.
“Unajua mbinu pekee ya kutawala ufahamu wa mtu ni kupitia mawazo yake mwenyewe?”
“Hilo naelewa”
“Kazi niliopaswa kufanya ilikuwa ni kuhakikisha anatambulika kama kiongozi wa ant-illuminat kama mbadala wa Seventeen na kazi yangu kubwa ilikuwa ni kutumia akili yake kumthibitisha lakini jambo la kushangaza nilifanikisha kuyatawala mawazo yake kwa muda mrefu lakini nilifeli kutawala namna anavyopaswa kuongea na wanachama mara baada ya kuonyesha Pete ya Muhuri wa uongozi”
“What …!!”Alishangaa.
“Ilikuwa ni kama kuna nafsi nyingine iliojificha ndani yake, wakati nikiwa nimeshikilia nafsi yake nikashindwa kuzuia nyingine kuchukua nafasi yake”
“Kwahio unamaanisha kuna nafsi inautawala mwili wake bila yeye kufahamu”
“Ndio na kitendo cha kutumia nguvu nyingi kutawala mwili wake naamini ndio chanzo kilichoamsha nafsi yake nyinginew, lakini bahari nzuri tulichotaka kilifanikiwa na sasa ataweza kurithi nafasi ya pacha wake”Aliongea na kumfanya Poseidon kufikiria kidogo.
“?Kwanini usingejaribu kusoma mawazo yake huenda ungejua nafsi yake nyingine iliolala”
“Nilijaribu kwa kumfanya alale usingizi mzito ili kutafuta kumbukumbu zinazohusiana na nafsi hio lakini sikuambulia chochote , yuko imara kuliko isivyokuwa kwa binadamu wa kawaida”
“Na Athana anasema nini juu ya hilo ?”
“Unafikiri angejibu nini?”
“Haha,,, naona lazima amesema kila kitu kipo chini ya udhibiti wake”
“Hakika ndio jibu ambalo amenipatia” Aliongea na wakaanza kucheka tena.









SEHEMU YA 494.
Saa tano kamili Roma aliweza kufika nyumbani kwa Nadia,ilikuwa mara yake kufika hapo na kulikuwa na umbali mfupi sana kutoka nyumba ya Amina ilipo, hivyo ilikuwa ni kamaa majirani tu.
Nadia ilionekana alikuwa na furaha sana na ujio wa Roma, mwanadada huyu mrembo mwenye rangi ya kibantu mapenzi yake kwa Roma huwa hayapimiki na siku zote alijiambia kadri atakavyokuwa chini ya kundi la Ant-Illuminat ndio Roma atazidi kumuhitaji na itatokea tu siku akaja kuwa sehemu ya wapenzi wake.
“Hili jumba ni zuri hongera sana”
“Mafanikio yangu kama mwanasheria yamefikia hapa kwasababu yako”Aliongea huku akiwa anatabasamu na Roma alitoa tabasamu hafifu na kuketi.
“Vipi mgeni nikuletee maji , juisi au bia”
“Niko vizuri unaonaje ukaketi ili tuongee”Aliongea Roma na kumfanya Nadia kumwangalia kwa muda na kisha akatoa tabasamu hafifu na kwenda kukaa mbele ya Roma na kukunja nne na kufanya kigauni chake kuyaacha mapaja yake wazi na Roma hakutaka kuyakodolea macho maana alikuwa akijua nini kingetokea kama angejihusisha na Nadia.
“Nataka kujua kwanini jana mlimwita mke wangu kwenye kikao chenu bila kumjuza mapema”Aliongea Roma huku akiweka usiriasi.
“Hata mimi nilishangaa kumuona mkeo Edna kujitambulisha kama kiongozi wetu”
“Unamaanisha nini?”
“Nimepewa ruhusa ya kujibu maswali yako yote utakayo uliza , nikianza na swali lako ujio wa Edna kwenye kikao chetu haukuwa wa bahati mbaya na hilo nilijua mara baada ya kikao kuisha …..”Alianza kuongea kwa kumuelezea juu ya hitimisho lililofanyika juu ya uchunguzi wa sababu ya Chriss kutaka kumuua Edna.
Na kwa maelezo yake anamwambia Roma Chriss aliacha ujumbe ambao unamuonyesha Edna ndio kiongozi wa jamii yao ya siri na uwepo wa mchoro wa unabii ambao bado hawajapata kuuona.
Maelezo yalimshangaza Roma kwasababu moja Chriss alifikishwa Vatican na Hades wa zamani na kwa haraka haraka aliamini kuna misheni ambayo alipewa kufanya ndani ya nchi hio ndogo ya kikanisa.
Kwa maelezo ya Nadia Roma aliona anapapaswa kuanza kuchukulia siriasi ya kile kinachoendelea kama anataka kumlinda mke wake.
Ukweli Roma hakutaka kujihusisha na maswala ya ulimwengu tena kwasababu alitaka amani, katika maisha yake aliamini kadri atakavyoingilia mambo yaliokaa kisasa ataishia kutengeneza maadui wengi kwani asingevumilia propaganda na uongo.
Roma imani yake kubwa ilikuwa ni kuilinda familia yake isipatwe na shida yoyote na sio kujiingiza kwenye mambo ya kibinadamu ambayo yalikaa kisiasa zaidi.
“Roma kuna mambo mengine unaweza kusema hayakuhusu , lakini kadri yanavyojikusanya na kuwa makubwa yatakuletea athari”
“Nadia unahisi kuna mambo gani ambayo unaona yananihusu na nayapotezea?”
“Kwa mfano Edna alitaka kushambuliwa na Chriss ni juhudi ganii ambazo umefanya kujua ukweli wa kile kilichotokea au ni dhamira gani ambayo imempelekea kuamua kufanya vile? Ungeujua ukweli itakuwa rahisi zaidi kumlinda”
“Kuna mambo mengine sio ya kutumia nguvu kuyafuatilia nikitaka kufuatlia kila kinachoendelea dunia hii unafikiri nitaweza kuishi kwa amani”
“Lakini kuna vitu vingine sio vya kupotezea kabisa”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa na kujiambia Nadia anamjua nini yeye , mpaka muda huo alikuwa akijitahidi sana kuiheshimu mipaka yake kisheria na ndio maana hakupenda kuungana na upande wowote.
“Kwahio mnamdhania mke wangu ni kiongozi wenu?”
“Jana ilikuwa ni hatua ya kwanza ya kumtambua kiongozi na nilichoweza kusikia kuna zaidi ya hatua tano na kama Edna ni kiongozi wetu kweli atatimiza hatua zote tano, Roma umoja wetu ni mkubwa sana na watu ambao Edna amekutana nao jana ni wawakilishi tu”
“Sitaki kuwaingilia sana na kile mnachokifanya na ndio maana sijataka hata kuyafahamu malengo yenu , Edna ni mke wangu mimi na sio kiongozi na kama mnatarajia kuona akifanikisha hatua zote tao mtapoteza muda”Aliongea Roma.
Kuna kitu hata hivyo kilikuwa kimfikirisha na aliamini Nadia asingekuwa na majibu anaoyataka.
Mchoro wa unabii alihitaji kuuona lakini kitu kingine alihitaji kujua nani ambaye jana alimteka kiakili mke wake na kumfanya akajitambulisha mbele ya watu ambao hata hawafahamu.
"Kwasasa siwezi kusema neno lolote kwani uchunguzi wangu haujakamilika ila nawatahadhalisha muwe makini na mnachokifanya , inaonekana kuna watu wanaona kila kitu"Aliongea Roma na kuzidi kumchanganya Nadia.
“Unamaanisha nini kusema kuna watu wanaona kila tunachofanya?”Aliuliza lakini Roma alitingisha mabega kama hajui na kumfanya Nadia kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha
"Nadia kwa leo nishasikia nilichotaka kusikia na kabla sijaondoka nataka nikuombe uniambie kitakachojili mkipata huo mchoro wa unabii"
"Unataka niwe shushu wako??
"Mbona unafikiria mbali ninachotaka ni taarifa moja tu ambayo ni hio ya mchoro , ili niweze kujua kama unamuhusu mke wangu".
"Nipo tayari kuwa spy kwa ajili yako" Aliongea huku akitabasamu kimadaha , alijiambia ndio, hivyo ndio alikuwa akitaka , aliamini lazima Roma kuna siku atataka kujua kile kinachoendelea katika jumuia yao ya siri na mtu wa karibu ambaye anaweza kumuomba taarifa ni yeye, umoja wa kundi hilo hata hivyo malengo yake yalikuwa ni kunsaidia yeye mwenyewe huko mbeleni kushindana na uovu , alijiambia kama kwa kutumia sheria imeshindikana kumuweka Roma karibu basi atatumia njia nyingine.
"Nadia unajua maana ya kuwa Spy ??"
"Spy ni neno lenye maana kubwa katika ujasusi na kazi ambayo unataka nikusaidie kufanya haiko mbali na U spy"Aliongea na kumfanya Roma ashindwe kujua hata namna ya kumjibu alitaka kujua kuhusu mchoro huo wa unabii unahusiana vipi na Edna.
Roma alianza kujifikiria na kuona kama mchoro huo kweli upo, na Chriss aliweza kuuona moja kwa moja alijiambia kuna jamii nyingine ya siri ambayo imeuona pia na huenda ndio maana wakataka kumuua Edna.
Siku ile wakati anapata taarifa juu ya kile kilichomkuta Chriss kwa Athena kumlinda mke wake alijua huenda ni swala ambalo linahusiana na mpango LADO na ndio maana alikuwa makini katika kulishughulikia swala hilo , hata hivyo mpango LADO ulikuwa ukimuhusu yeye na Seventeen.
Roma alijiambia kuna kitu alikuwa akipotezea kukifanyia kazi na huo ndio muda muafaka.
“Nadia sitaki uwe shushu kwa ajili yangu , mpaka sasa nakuona upo kwenye hatari na kadri unavyojihusha na jamii hio unakuwa adui mlengwa na jamii nyingine ambayo mnaenda nazo kinyume na mimi sitoweza kukupaatia ulinzi kwani sitaki kuongeza maadui”Aliongea Roma na kumfanya Nadia ile sura yake iliopambwa na tabasamu kupotea.
“Nitakuambia nikipata taarifa yoyote inayohhusiana na mkeo usijali sana kuhusu usalama wangu kwani hata hivyo sio kama wewe ni boyfriend wangu?”Aliongea na kumfanya Roma atingishe kichwa kukubaliana nae tokea afahamiane na Nadia miaka mingi iliopita hakuwahi kumuomba msaada na huenda hio ndio siku ya kwanza kwake na aliona huenda ndio maana Nadia alitaka kumsaidia kazi yake ingali ya uhatari wenyewe lakini alishangazwa na maneno yake yaliokaa kimitego.
“Utafanya nini kuhusu mchoro maana sio rahisi kuupata”
“Chriss amewaambia ili kujua uhalali wa kiongozi wenu ni kutumia mchoro huo wa unabii si ndio?”Aliuliza Roma.
“Ndio barua yake ilivyoweka wazi”
“Mnafahamu Chriss ni jamii gani ya siri aliokuwa akijihusisha nayo?”Aliuliza Roma.
“Hilo hatufahamu na tunalifanyia kazi”.Aliongea na kumfanya Roma afikiria kitu na kisha akasimama.
“Unaondoka?”
“Ndio kilichonileta nishakipata”
“Ah.. nikajua unakaa kaa”Aliongea kwa sauti ya chini na kumfanya Roma amwangalie Nadia kwa kumchunguza na kisha akaona ni muda muafaka wa kuaga na kisha akaondoka akisindikizwa na Nadia mpaka nje.
Mara baada ya kutoa gari Nadia alitoa tabasamu hafifu na kisha akarudi ndani na kuchukua simu yake na akaingiza namba kwa kuziandika na kisha akapiga.
“Umefanikiwa kuongea nae”
“Ndio nimemaliza maongezi na nimemwambia kila kitu kilichotokea inaonekana ni kweli kama mlivyodhania”
“Amesemaje kuhusu mchoro wa unabii?”
“Hajaongea chochote kuhusu mchoro ila ameonyesha kuvutiwa na taarifa hio”
“Kama ameonyesha kuvutiwa hiko ndio tulichokuwa tukitaka ,kwasasa utabakia Tanzania hakikisha unajenga ukaribu na Edna”
“Sawa Madam”Aliitikia na kisha simu ilikatwa.
Roma baada ya kutoka nyumbani kwa Nadia akili yake ilimwambia aende kwanza Kigamboni kuonana na Diego kabisa ana kwa ana , alihitaji kujua uchunguzi kuhusu Chriss ulifikia wapi.
Roma mambo mengine hakuwa na haja ya kuyatolea maagizo na wanajeshi wake wenyewe walipaswa kujiongeza hivyo hata swala la Chriss sio kama halikuwa likifanyiwa uchunguzi ila ni kwamba uchunguzi ulikuwa ukiendelea na ulichukua muda mrefu kutokana na Chriss kutojulikana mahali alipoishi kwamuda mrefu hivyo taarifa zake kuwa ngumu kupatikans
Roma hakutana kuamini moja kwa moja kama Raisi mstaafu waMarekani ndio alitaka kumuua Edna kwa kumtumia Chriss alitaka kwanza ushahidi wa kueleweka ndio aweze kuchukua hatua, hata hivyo Raisi Barrack Mabo katika ile sauti ambayo ilirekodiwa hakuwa akiongea kuhusu Edna kuuwawa tu lakini pia alionyesha alihusika katika mpango LADO na ndio maana Roma alijiambia anapaswa kuwa makini.
Baada ya dakika kama arobaini na tano aliweza kufika Kigamboni Mbutu na kuingiza gari ndani ya geti na alipokelewa na Diego.
“Mfalme Pluto sikutegemea ungetutembelea leo”Aliongea na kumfanya Roma kuona kweli alikuwa na siku nyingi hajafika hapo.Alianza kukagua mazingira na kuona hakuna kilichobadilika.
“Hii sehemu imetulia sana Diego”
“Ndio mfalme Pluto kila mmoja ametawanyika kwenda kutimiza wajibu wake na kwasasa yupo Bram na mimi hapa ndani”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa wanajeshi wa The Eagles waliongezeka na kuwa wengi ,inakuwaje wote wakawa wametawanyika kwenda kwenye majukumu.
“Kuna kazi ya ziada ambayo Sauron amewapatia kuifanyia kazi?”
“Ndio mfalme Pluto nilipaswa kutoa ripoti baada ya kukamilika”
“Inahusiana na nini?”
“Zeros organisation!!!”Aliongea Diego na kumfanya Roma asimame mbele ya mlango na kumwangalia Diego.
“Ndio mfalme Pluto mwezi uliopita tulipata ‘intel’ ya kufuatilia taarifa zinazomuhusu Joseph Bikindi”Aliongea Diego na kumfanya Roma kuvutiwa na maongezi na aliingia ndani kwanza ili aweze kupata kumsikiliza vizuri.
“Joseph Bikindi ni nani na anahusiana vipi na Zeros organisation?”Aliuliza Roma maana alishindwa kukumbuka jina lake na muda uleule na Bram alievalia Headphone alitokeza na kumsalimia Roma.
Na kisha wote waliingia kwenye chumba cha kuendeshea mitambo yao ya kuchakata taarifa.
“Mfalme Pluto hii ni picha ya Joseph Bikindi”Aliongea Diego na Roma aliweza kuona picha ya mwanaume mweusi alievalia Jacketi la baridi na boshori ni picha ambayo ilikuwa ikimuonyesha akiwa kwenye mandhari yake ya miti iliofunikwa na barafu na aliweza kugundua eneo hilo kwa harak.
Roma baada ya kuangalia picha hio kwa umakini aliona kama sura inakuja na kupotea ni kama alishawahi kukutana na mtu huyo lakini alimsahau .
“Mfalme hii ni picha nyingine iliopigwa hivi karibuni’Aliongea Diego na kisha Bram akaonyesha picha nyingine ambayo ya wakati huu ilikuwa na sura za watu wawili ambao alikuwa akiwatambua.
Ilikuwa ni picha ya Kizwe na Lekcha wakiwa na mwonekano ambao aliweza kuutambua , haraka haraka kumbukumbu zake zilimrudisha siku ambayo alikutana na Lekcha Club B akiwa na kizwe , siku kadhaa mara baada ya kumfanya Kizwe abakwe na mafukara.
“Mfalme Pluto umegundua nini kwenye hii picha?”Aliuliza Deigo na Bram alirudisha picha ya mwanaume wa kwanza ambayo alimuonyesha na palepale sasa aliweza kuelewa Joseph Bikindi aliekuwa kwenye picha yenye mandhari ya eneo lenye barafu alikuwa ni mwanaume aliemuona ameambatana na Kizwe.
Kwa maelezo ya Diego ni kwamba walipokea taarifa ya kufatilia taarifa za Joseph Bikindi na hata picha ambayo alimuonyesha Roma ilitumwa kwao na mtu ambaye hakufahamika.
Na baada ya kufanya uchunguzi ndipo walipoweza kugundua Joseph Bikindi alikuwa nchini Tanzania muda mrefu akijifanyisha ni fukara ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuokota makopo huku akifahamika kwajina maarufu la Lekcha.
Kilichomshangaza Roma zaidi ni pale alipoambiwa Lekcha aliishi kwenye chumba chake yeye ambacho alitumia kabla ya kukutana na Edna , haraka haraka kwa maelezo hayo alihisi haikuwa bahati mbaya.
“Imekuwaje mkamuunganisha Jospeh Bikindi na Zeros organisation?”Aliuliza Roma.
“Mfalme kupitia hii picha ndio tuligundua Joseph sio mtu wa kawaida”Aliongea Diego na kumfanya Roma aiangalie , ni picha ambayo ilikuwa ikimuonyesha mwanaume wa kizungu aliekuwa kwenye gari katika msururu foleni ya magari akiwa ameshusha kioo akimwangalia omba omba mmoja akiwa amenyoosha mkono kama vile anasaidiwa kitu na yule mzungu.
“Huyo anaetoa msaada mfalme Pluto anafahamika kwa jina la Efani Trudman ni ajent wa siri wa kundi la Dhoruba nyekundu lakini pia ni mwanasayansi kitengo cha utafiti katika kampuni ya J&J kampuni ambayo Joseph Bikindi katika CV yake inaonyesha alifanya kazi hapo kabla ya kufukuzwa”Aliongea na kisha akatoa taarifa zote ambazo zilikuwa zikihusu taaluma ya Joseph Bikindi na Roma alishangaa zaidi baada ya kuona Lekcha alikuwa msomi wa kiwango cha juu.
“Kwanini alifukuzwa kazi?”
“Mfalme Pluto kama nilivyosema bado tunaendelea kufanya uchunguzi lakini wiki iliopita tuliweza kupata ufunuo ambao umetuaminisha moja kwa moja huenda ndio sababu ambayo imemfukuzisha kazi”Aliongea na kisha akapozi na kumpa ishara Bram na palepale alifukunyua picha na kuzionyesha kwenye skrini.
“Inaonyesha Joseph alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na huyu mrembo , anafahamika kwa jina la Clelia Allisanto ambaye ni katibu wa umoja wa mataifa wa sasa”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na taarifa hio.
Kwa haraka haraka Roma alijua kila kitu kuhusu Lekcha yalikuwa na maigizo na hata kuwa na Kizwe huenda ilikuwa ni mipango lakini kuwa na mahusiano na Clelia ilimshangaza mno na isitoshe mrembo huyo alikuwa akimshuku kuwa ni Athena ila tu hakuthibitisha.
Alishindwa kupata majibu zaidi ya maswali yake kwani Diego hajakamilisha uchunguzi.
“Ukiachana na huyu Bikindi kuwa na ukaribu na Efani kuna sababu nyingine ambayo inamuunganisha na Zeros?”
“Ndio mfalme Pluto baba yake Joseph alikuwa ni mwanasayansi chini ya kampuni ya kisayansi ya utafiti ya Innova kutoka Italia kabla ya kuacha kazi na kujiunga na taasisi ya utafiti ya siri iliokuwa chini ya Zeros organisation ambayo ilikuwa na Research Base katika visiwa vya madagascar mwaka 2004”
“Unaweza kunionyesha picha ya Bikindi?”Aliongea Roma mara baada ya kusikia neno Madagascer na Diego muda uleule alitoa picha na kisha akamuonyesha Roma na kumfanya ashangae na simu yake ilianza kuita na kuitoa mfukoni na kugundua anaempigia ni mama yake , alipokea palepale na kuweka sikioni.
“Roma babu yako kafariki”Ilikuwa sauti upande wa pili ya mama yake ambayo ilisikika kinyonge.
 
SEHEMU YA 495.
Roma alishangazwa na kupatwa na huzuni ya taarifa hio ya kifo kwani siku hio hio ndio walipanga kwenda yeye Edna na Lanlan kumtembelea, kwao ilikuwa ni kama wamechelewa kwenda , lakini hata hivyo hakujilaumu sana kwa kutowahi kwenda kumuona.
Mzee Atanasi ni moja wapo ya wazee waliokula chumvi nyingi na alikuwa akikaribia kutimiza miaka mia moja na moja na kwa uzito wake ndani ya serikali ya Tanzania ni sahihi kuitwa babu wa taifa.
Ndio mwanajeshi pekee aliebaki ambaye alipigania uhuru wa Tanzania pamoja na Raisi Nyerere.
Roma hakuwa na haraka ya kwenda moja kwa moja msibani , alitaka kwanza kumaliza kilichomfikisha hapo na kisha ndio arudi nyumbani na kuelekea huko , ile safari yao ya kwenda kwa ajili ya kusalimia iligeuka na kuwa safari ya kwenda msibani.
Roma baada ya kukata simu kwa kumpa mama yake pole aliwageukia Diego na kuwapa taarifa hio ya msiba na Diego na Bram walimpatia pole.
Roma aligeukia kwa mara ya pili picha iliokuwa ikionekana kwenye skrini , picha ya mwanaume aliefahamika kwa jina la Bikindi , alikuwa ni baba mzazi wa Lekcha na Roma alimkumbuka kwasababu ni moja ya wanasayansi wa Zeros organisaiton aliowaua.
“Mfalme Pluto unamfahamu huyu mwanaume?”Aliuliza Diego na Roma alitingisha kichwa kuashiria anamjua.
“Mmefanikisha kuchunguza taarifa za Joseph Bikindi za hivi karibuni”
“Ndio mfalme Pluto kwa taarifa tulizoweza kupata kutoka Rwanda mpaka miezi michache iliopita alikuwa mkufunzi wa chuo kikuu cha taifa lakini kwa wiki kadhaa sasa ameripotiwa kutoonekana chuoni bila ya taarifa”.
“Endeleeni kumchunguza kwa ukaribu zaidi na sura yake iunganishe na mfumo wetu wa ‘facial recognition’ ili kama itatokea akiwepo Tanzania tuweze kutambua mara moja”Aliongea Roma huku akipata hisia huenda Lekcha alikuwa Tanzania kwa kutafuta namna ya kulipiza kisasi na kwa muda huo ambao Kizwe alionekana kutokuwa wa kawaida aliamini huenda wapo wote na wanajiandaa na mipango ya kulipiza kisasi , hakusahau na Denisi alikuwa hivyo hivyo tu ndio maana alihitaji kuchukua tahadhari mapema.
Jambo lingine ambalo lilimfanya kuwa na wasiwasi ni juu ya Athena ,tokea apewe cheo cha Hades hakuwahi kujionyesha kwake na alikuwa akijua ana mzunguka lakini hakuwa akijua sababu ni ipi ,lakini alijiambia maadamu yupo hai basi kuna siku tu wataonana na atathibitisha maswali yake yote.
“Vipi kuhusu uchunguzi wa Chriss mlikamilisha?”
“Mfalme Pluto taarifa za Chriss imekuwa ngumu sana kuzipata na mpaka sasa hatujapiga hatua lakini kuna jambo moja tu ambalo tulifanikiwa kupata”
“Mmepata nini?”Aliuliza Roma kwa shauku na Diego alitoka ndani ya chumba hiko na ndani ya muda mfupi aliweza kurudi na mfuko wa plastic ambao ndani yake ulionekana kuwa na mkufu uliofungwa na kishaufu cha madini ya almasi.
“Huu ni…”
“Ni mkufu ambao unaonyesha Chriss alikuwa mwanachama wa Freemason”Aliongea Diego na kumfanya Roma kuchukua na kuangalia vizuri na kweli aliweza kugundua maana ya mchoro uliokuwa kwenye kishaufu(Pendant).
Ijapokuwa sasa ameweza kuanza kupata ukweli wa Chriss alikuwa akitokea jamii ya siri ya freemason lakini ilikuwa ngumu kwake kuweza kuamini kama watu wa jamii hio ya siri ndio walitaka kumuua mke wake na moja kwa moja alijua huenda majibu yapo kwenye mchoro.
Roma ilibidi kwanza amuelezee Diego na Bram kile ambacho alikuwa akitambua kuhusu Chriss.
“Mfalme Pluto hata sisi tunashindwa kuelewa kama Chriss alikuwa mwachama wa Ant- illuminat”
“Kwanini mnaamini hawezi kuwa mwanachama unajua taarifa zote za umoja huo?”
“Ndio mfalme Pluto najua taarifa zote zinazohusiana na umoja wa ant- illuminat na baadhi ya mipango yao ya mbeleni japo mpaka sasa hakuna uthibitisho kwani ni taarifa ambazo ni kama uzushi”
“Ni taarifa gani ambazo unafahamu?”
“Mfalme Pluto ushawahi kusikia kuhusu mpango TASAC?”
“Mpango TASAC!, si huu ulioanzishwa na serikali ya Urusi kuyafanya mataifa ya Afrika kutounga mkono wala kukataa vamizi anazozifanya Raisi wa Urusi nchini Ukraine?”
“Ndio mfalme Pluto lakini ni ngumu kusema mpango TASAC umeanzishwa na Urusi”
“Kwanini?”
“Taarifa za siri za daraja la tatu zinaonyesha mpango TASAC waanzilishi ni Ant- illuminat”Aliongea na kumfanya Roma kuguna ilikuwa habari mpya kwake na huenda angekuwa anafatilia sana maswala ya siasa angekuwa ashaijua , huenda ilikuwa sahihi kwa Christen kumwambia hayuko ‘flexible’ kama mtangulizi wake”
“Uzushi mwingine unaoenezwa kuhusu Ant-illuminat ni juu ya mataifa ya kiarabu kuwekeza zaidi katika mataifa yalioendelea ya kimagharibi katika nyanja ambazo zinagusa moja kwa moja hisia za watu mfano kwenye vilabu vya mpira na kadhalika”Aliongea Bram.
“Na pia ndio kinara wa mapambano ya sarafu ya Dola ya kimarekani kutaka kuiangusha”Aliongezea Diego.
“Inaongekana mnapenda sana uzushi”
“Your Majesty if no Somke no Fire “Aliongea Diego akiingiza msemo ambayo unaoendana na ule wa kiswahili usemao yasemwayo yapo na kama hayapo yaja au penye moshi hapakosi moto.
Roma hakutaka kukaa sana hapo kwani kuna msiba ambao ulikuwa ukimuhusu na mpango wake ni kuunganisha kwanza msibani kujua kile kinachoendelea na kujua taratibu zinazofuatia, hivyo alitoa msisitizo wa usalama zaidi wa watu wake wa karibu kuzingatiwa hususani muda huo ambao alijua na Lekcha ni adui yake mpya alieingia kwenye orodha.
Akiwa garini alijaribu kuwasiliana na mke wake kumuulizia kama kapata taarifa na ilionyesha Edna alikuwa na taarifa na alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kufika msibani pamoja na Bi Wema na Roma alimwambia angemkuta huko huko kwani anatangulia.
Baada ya kufika Masaki nyumbani kwa Tajiri Azizi aliweza kuona watu wengi waliokuwa wakiingia ndani ya nyumba hio na kutoka na pia kulikuwepo na baadhi ya waandishi wa habari.
Kwa haraka haraka Roma alishajua msiba huo ni wa kitaifa hivyo wageni wengi lazima wangefika kutoa salamu zao za pole.
Roma hakuingiza gari ndani ilibidi apaki pembeni kwa kuhofia ndani kusingekuwepo na nafasi na baada ya kuegesha aliingia moja kwa moja ndani na alikuta tayari maturubai yashasimamishwa pamoja na viti ambavyo vilikuwa vikipangwa.
Mtu wa kwanza kuonana nae alikuwa ni Kassimu mtoto mkubwa wa tajiri Azizi ambaye alikuwa akipokea wageni na alimkaribisha Roma na kumpeleka kuonana na mama yake pamoja na wanafamilia wengine.
Dakika chache mbele na Edna aliweza kufika na kutoa pole , msiba haukuwa na vilio sana zaidi ya sura za majonzi tu huenda ni kwasababu mzee huyo kaishi miaka mingi na muda wake umewadia hivyo alipaswa kutangulia mbele za haki .
Ratiba ya msiba ilikuwa ni siku inayofauta mwili kuagwa katika viwanja vya Karimjee na kisha safari ya kuelekea Kilosa kijijini ingeanza ili kumpumzisha Babu Atanasi.
Katika watu ambao walikuja kutoa salamu za pole ni Samweli Nguruma kiongozi wa kundi la ZoaZoa na ilikuwa ni kama amekuja kumtafuta Roma kuongea nae.
Roma alishawahi kuwasiliana na bwana huyo kwa kupitia simu ila hakuwahi kukutana nae ana kwa ana na siku hio ndio waliweza kufahamina kwa mara ya kwanza.
Samweli Nguruma baba yake na Benadetha alikuwa ni kama bosi mtu mwenye kitambi na kipara cha nywele na ilikuwa ngumu kuamini ndio ambaye alikuwa akijihusisha na biashara za magendo lakini hata hivyo Roma hakutaka kumtoa dosari ukizingatia hata Rose hakuwa na mwonekano wa kuongoza kundi la Tembo.
“Mr Roma unamwonaje mtoto wangu Benadetha?”Aliuliza Samweli Nguruma na kumfanya Roma kushangazwa na swali hilo.
Ilikuwa ni saa za mwisho mwisho za kuaga mwili ili safari ya kuelekea Morogoro ianze ndio maana Roma alishangaa.
“Kwanini unauliza hivyo mzee?”.
“Nataka kujua maoni yako, umefanya nae kazi kwa muda mrefu kidogo hivyo sio dhambi kutoa maoni yako unavyomuona na tabia yake kwa ujumla”Roma ijapokuwa muda huo aliona hakupaswa kujibu swali hilo kutokana na muda kutokuwa mzuri lakini aliona ni kheri kujibu kile anachokiona kwa Benadetha.
“Namuona kama msichana mzuri mwenye sheria zake na inaonyesha ashatambua mapema kama mwanamke anataka nini katika maisha yake”Alijibu Roma na kumfanya Samweli nguruma kutabasamu.
“Upo sahihi Benadetha ni binti mwenye msimamo na mara nyingi uwezo wake mkubwa wa kujielewa unanifanya hata mimi baba yake kumhofia”
“Hongera kwa malezi, kwa ninavyomuona atakuja kuwa na maisha yenye furaha sana mbeleni”
“Furaha ya mwanamke inakamilika pale akiridhika na kila kitu kunachomzunguka, asipo ridhika ataishia kutangatanga kukidhi haja ya moyo wake”Aliongea
“Ndio maana nikasema Benadetha atakuja kuwa na furaha kwasababu kama mwanamke ukishafahamu kwenye maisha unataka nini mapema ni rahisi pia kuridhika”
“Upo sahihi Mr Roma lakini ushawahi kujiuliza kwanini kipindi Benadetha alipopelekwa kituoni na mkeo nilitaka wewe ufanye kazi ya kumtoa?”
“Kwanini?””
“Nilijua tayari mkeo ashafahamu hisia za Benadetha kwako”Aliongea na kumfanya Roma ashangae.
“Mzee labda utakuwa haujamfahamu Benadetha vizuri , mimi na yeye hatuna ukaribu huo na hata kama Benadetha anipende mimi kama mwanaume siwezi kumpokea kwani tayari nina mke”Aliongea Roma bila ya wasiwasi.
“Haha.. Mr Roma nimekutana na vijana wengi ila ujasiri wako na kujiamini ni wa viwango”
“Na wewe pia ujasiri wako ni wa viwango kumnadi mtoto wako wa kike kwangu ilihali tayari nina mke sio jambo la kawaida kabisa kwa tamaduni za kiafrika”
“Upo sahihi imenichukua ujasiri kuongea na wewe kuhusu maswala ya binti yangu na nimetidhika pia kama huna nia ya kumfanya kuwa sehem ya wanawake wako”Aliongea na kumfanya Roma kumchanganya na kuona huenda habari za yeye kuwa na wanawake wengi zilikuwa zikifahamika kwa watu wengi.
*********
Tokea kumalizika kwa maziko ya Babu Atanasi siku zilienda haraka haraka mno na katika watu ambao walikuwa wako bize basi ni Roma ,kuna muda alijiambia uwepo wa Lanlan kidogo ulikuwa umesaidia sana kupunguza migogoro yake na Edna.
Kwani kitendo cha Lanlan kung’ang’ania kulala na mama yake ilimpa nafasi Roma ya kila usiku kutembelea wanawake wake kwa zamu na hilo pia lilisaidia sana kuyafatilia maendeleo yao.
Vidonge ambavyo aliweza kuvipata baada ya kuwaua watu wa hongmeng vilisaidia sana katika kumfanikisha Rose kupanda levo na Roma aliona kabisa muda si mrefu Rose angefanikisha kupata ufunuo wa nguvu ya mbingu na Ardhi jinsi ya kutumia elementi zote za dunia.
Katika mafunzo ya kijini kila mmoja alitofautiana na mwenzake katika kupata ufunuo wa namna ya kutengeneza maajabu kwa kutumia elementi za dunnia na hicho ndio ambacho kilimfanya Roma kupatwa na hamu kubwa ya kuwaona wakifikia levo ya kupata ufunuo.
Mage na yeye hakuwa mbali sana na ilionyesha juhudi zake zilionyesha manufaa kwani alianza kuelewa levo ya nusu mzunguko kikamilifu na Roma aliona kabisa muda si mrefu angeweza kuingia levo ya mzunguko na alijiambia kama atafanikisha mpango wake wa kutengeneza vidonge vyenye nguvu basi huenda ndani ya mwaka mmoja kila mmoja anaweza kuingia kwenye levo ya Nafsi na matumaini ya kuweza kupata mtoto yangekuwa juu.
Upande wa Amina msukumo wa ndani zaidi kujifunza mafunzo hayo ni kwa ajili ya kutunza urembo wake na kufanya tahajudi muda mrefu haikuwa kazi kubwa kwake, ,ijapokuwa maendeleo yake yalikuywa ya taratibu lakini alileta matumaini na hata hivyo Roma alifurahi kuona Amina alikuwa mzoefu wa mazoezi ya Yoga na hilo ndio lilirahisisha.
Neema Luwazo ndio ambaye alikuwa akijifunza kwa fujo sana na tamaa kubwa ya kufikia levo za juu na Roma aliona huenda ni kwasababau alikuwa akiukaribia utu uzima ndio maana alitaka kupanda levo kwa haraka ili asiendelee kuzeeka na kubakia na mwonekano wa ujana.
Lakini licha ya fujo alizokuwa nazo za kutaka kujifunza maendeleo yake yalikuwa ni ya taratibu mno kulinganisha na wengine wote kutokana na utu uzima wake kwani ilikuwa rahisi kwa vijana kujifunza na kupanda levo kwa haraka tofauti na watu wazima na Roma ilibidi achukue jukumu la kumtuliza.
“Roma nimeachia majukumu kabisa ya kampuni kwa Alhaji kwa ajili ya kujifunza”Aliongea Neema usiku Roma alipomtembelea.
“Umefanya vizuri lakini unatakiwa kwelewa mbinu hizi huwa zinaendana na utulivu wako wa akili ukiwa na tamaa ya kupanda levo kwa haraka utakosa utambuzi wa kunyaka kila viashiria vinavyokujia wakati wa kufanya Tahajudi na ndio maana nakushauri usichukulie sana hili swala siriasi lifanye kama ni moja wapo ya starehe, kama unavyokaa kwenye Jakuzi ukiwa umeshikilia glasi ya mvinyo ukiyafurahia mafanikio yako”Aliongea Roma nakumfanya Neema kutabasamu.
Na alfajiri Roma alijaribu kufanya nae mafunzo na sasa angalau aliona akili yake ilikuwa imetulia , ilionekana maneno yake ya jana usiku yalikuwa yamefanya kazi.
Upande wa Edna na Nasra maendeleo yao yalikuwa ya kinyonga lakini yalioleta mabadiliko kwenye miili yao.
Zamani Edna alikuwa akimhofia Lanlan kumrukia kutokana na uzito wake lakini kwa kipindi chote alichokuwa akichukua mazoezi alikuwa ameimarika na kumudu hata uzito wa Lanlan vizur.
*******
Ni baada ya wiki moja kupita hatimae Omari na Queen waliweza kufunga ndoa yao rasmi kwa tamaduni za dini ya kiislamu ambazo zilimtaka Queen kubadili dini jambo ambalo Mzee Alex hakupinga, hata hivyo ni Omari pekee ambaye alionyesha kumpenda mtoto wake kwa mapenzi ya dhati licha ya kwamba alikuwa mjamzito hivyo hata swala la Queen kubadili dini kuwekwa mezanni kwake hakuwa na kipingamizi.
Saa tano na nusu za usiku ndio muda ambao Roma na Edna walirudi kutoka kwenye sherehe ya harusi hio ya Omari na Queen na wakati Roma anaingiza gari ndani ya geti alishangazwa kuona nyumba bado inatoa mwanga wa taa kutokea sebuleni kwani kwa muda huo aliamini wanafamilia wote wangekuwa washalala.
Roma usiku huo akiwa njiani alikuwa akipanga kwenda kuburudika na mke wake Edna usiku kucha kwa kuamini muda huo Lanlan angekuwa tayari amekwisha kulala na Qiang Xi.
Lakini sasa ile wanaingia sebuleni lile tumaini lake lote lilipotea baada ya kumkuta Qiang Xi na Lanlan wakiwa wamekaa sebuleni na hata Edna mwenyewe alishangaa kuwakuta hapo kwani muda ulikuuwa umeenda.
“Qiang mbona mpaka muda huu Lanlan hajalala na asubuhi anatakiwa kuwahi kuamka”
“Madam nimejaribu kumfanya alale lakini hana usingizi na anasema anakusubiria”Aliongea Qiang Xi huku akionyesha hali ya uchomvu ilionekana alikuwa akijitahidi kuwa macho kwasababu ya Lanlan na alikuwa amechoka.
“Lanlan kwanini unashindwa kulala?”
“Mama sipati usingizi , Lanlan anataka kulala karibu na mama”Aliongea na kumfanya Roma akunje sura alijiambie kama watoto wake watakuja kuwa kama Lanlan basi maisha yake yangekuwa magumu sana.
Edna alimuonea huruma kuona alikosa usingizi na swala hilo lilikuwa likimsumbua kichwa namna ya kulitatua kuishia kujiuliza kama siku nyingine asingekuwepo na Lanlan angelala vipi.
Upande wa Roma alishajua kwanini Lanlan alikuwa akikosa usingizi , sababu ilikuwa ni kutokana na damu yake kuchemka kila wakati na kumfanya kukosa utulivu wa akili ndio maana alikuwa akikosa usingizi na njia pekee ambayo aliona huenda ingemsaidia Lanlan ni kumfundisha ya mbinu ya kimaandiko ya urejesho ili aweze kudhibiti uwezo wake lakini alimuona Lanlan ni mdogo na hata kama angejaribu kumfundisha kutamka maneno ya maandiko na kuyageuza kuwa nguvu ingekuwa ngumu kwake.
Hivyo suluhisho la muda mfupi ambalo aliona lingefaaa kwa muda huo ni Lanlan kuendelea kulala na Edna mpaka atakapogundua namna ya kumsaidia kupata usingizi bila ya uwepo wa Edna.
Roma mara baada ya kurudi kwenye chumba chake akijiandaa kwenda bafuni kujimwagia maji alale simu yake ilitoa mlio wa ishara ya mwaliko wa mtu kumpigia kwa njia ya Vidio Call.
Baada ya kuangalia inatoka kwa nani aligundua ni Sauron na alijikuta akiwa na shauku ya kumsikia maana ni kama mwezi unakaribia kuisha tokea ampatie Sauroni kazi ya kusambaza vijana kutafuta maeneo walioishi binadamu enzi za kale , maeneo ambayo yalifanikisha ukuaji wa mila na tamaduni za kijamii za mwanzo kabisa(Ancient Civilization) lakini baada ya muda maeneo hayo yakatelekezwa , aliamini upatikanaji wa maeneo hayo ingekuwa rahisi kwake kuweza kupata mimea anayojitaji itakayosaidia katika utengenezaji wa vidonge vya kijini.




SEHEMU YA 496.
Licha ya mwonekano wa kutisha kutokana na mtindo wake wa nywele nyingi alizokuwa nazo kwa upande wa Roma alikuwa ashamzoea na kumuona mtu wa kawaida lakini kwa mwingine huenda mwonekano wa Sauroni ungemkosesha amani hususani wakati anapokuwa siriasi.
Ilionekana muda huo Sauroni upande wa kwao kulikuwa ni mchana maana alionekana ndani ya ofisi huku kwenye meza yake kukiwa na mafaili mengi, huku yeye mwenyewe akiwa amevalia miwani ya kusomea.
Roma mara baada ya kupokea simu na kubadilishana salamu na Sautoni ilibidi amwambie aende moja kwa moja kwani alitaka kulala.
“Mfalme Pluto nishakutumia mafaili yanayohusiana na taarifa ulizo omba kupitia barua pepe yako , tumefanikisha kupata maeneo nane yanayofanana na sifa ulizotupatia”Aliongea Sauroni
“Asante sana Sautoni kwa juhudi zako zilizopelekea kufanikisha , vipi kuna changamoto yoyote uliweza kupata?”
“Sijapata changamoto kubwa mfalme Pluto lakini nina shauku ya kufahamu kwanini unahitaji taarifa za hayo maeneo kwani kwa uelewa wangu hayo maeneo sasa hivi hayakaliwi na binadamu na huenda hata uwepo wa hio mimea ni kwasababu hio na binadamu wa kawaida ambaye angesafiri kwenda kwenye hayo maeneo asingeweza kutoka hai”Aliongea na kumfanya Roma kucheka kidogo
“Maeneo ambayo watu waliishi na sasa hawaishi ndio ambayo ninayatafuta kwani naamini inaweza kufanikisha kupata kile ninachohitaji , najua una shauku lakini nitakuelezea siku nyingine kwasasa taarifa hii ulionitumia nitaipitia na kuanza na mikakati ya kuelekea huko”Aliongea Roma na Sauroni aikubali na kisha akakata mawasiliano
Roma alighairi kwanza kwenda kuoga na kuanza kupitia taarifa ambazo ametumiwa na Sauroni na ilionekana ziliandikwa vizuri ili kueleweka kwa urahisi, ni ‘Document’ ambayo ilikuwa na peji nane ambazo zilikuwa zikielezea maeneo husika ambayo yalikuwa yakikidhi vigezo.
Na mpaka anakuja kumaliza alikwisha kupata sehemu ambayo aliona inafaa kuanzia kutafuta mimea hio lakini kwakuwa hakuwa mzoefu sana alitaka kwanza kusikia maoni kutoka kwa Rufi na kwasababu muda huo ulikuwa ni usiku sana aliona angewasiliana nae asubuhi.
Siku iliofauta jambo la kwanza ilikuwa ni kuwasiliana na Rufi na akamtumia na faili la taarifa alizotumiwa na Sauroni na wote walijikuta wakiachana na baadhi ya maeneo yalio orodheshwa kwa sababu za aina moja, waliachana na eneo la Eveglades ambalo lipo kusini mwa Marekani , Msitu wa Panama , msitu wa Amazoni na maeneo mengine na wakaja kuchagua eneo lililofahamika kwa jina la Arnhem Land ambalo lipo kaskazini mwa bara na nchi ya Australia.
Arnhem Land ni eneo ambalo walichagua kutokana na historia yake kwani sio tu kwamba miaka ya hivi karibuni halikukalika lakini miaka mingi iliopita lilikaliwa na watu wa asili zaidi wa nchi ya Australia na ilikuwa ni eneo ambalo ni kama tamaduni nyingi zilizaliwa na hivyo ndio vigezo ambavyo Rufi alipendekeza.
Eneo ambalo lilikaliwa na watu wa asili na kuzaa tamaduni na mila ndio ambalo lingekuwa na mkusanyiko wa nguvu nyingi za kiroho ambazo zingefanikisha upatikanani wa malighafi za Alchemy.
Roma alikuwa akielewa Australia ilikuwa kusini mwa ncha ya dunia na kwa mwezi huo wa nne kwenda wa tano ni kipindi cha Vuli na kama angevuta muda vuta muda basi mwezi wa sita ingekuwa ni hatari zaidi kwenda kwani ingekuwa ni kipindi cha baridi kali na kwasababu hakuwa akienda mwenyewe alitakiwa pia kuzingatia hali ya kiafnya ya Rufi na ndio maana aijiambia ni kheti kuharakisha kufanya safari na kwenda kutafuta hio mimea na kuanza harakati zingine.
Rufi alikuwa ashakubali kuongozana nae kwani hakuwa na shughuli ya maana ya kufanya Tanzania na maisha yake yalikuwa ya upweke sana na aliona ingekuwa kama utalii kwake kusafiri mpaka Australia.
Tatizo ambalo Roma aliona ni changamoto ambayo alipaswa kuitatua ni kwa mke wake , alijua akimuaga kwamba anaelekea Australia na Rufi angemuwekea ngumu lakini hata hivyo aliona lazima akubaliane na matakwa yake kwani anachokifanya sio kwa faida yake mwenyewe bali ni kwa faida ya wote.
Usiku baada ya Roma kupata chakula aliona ndio wakati muafaka wa kumweleza Edna mpango wake wa kusafiri na Rufi na Roma alimsubiria kwanza Edna amalize kumwandaa Lanlan kwa ajili ya kulala na ndio aongee nae.
Roma mara baada ya kukaa chini na kumuelezea anachopanga mwanzoni hakushangazwa na taarifa hio lakini Roma alipokuja kusema anataka kwenda na Rufi alihisi hatari.
Tokea aanze kuwa na ukaribu zaidi na mume wake alikuwa mwangalifu mno hakutaka Roma aongeze mwanamke kabisa na ndio maana hakutaka mazoea kati ya Rufi na Roma kuongezeka kwani mwisho wake usingekuwa wa kheti kwake.
“Najua unaweza kuona sio sawa mimi kwenda na Rufi lakini hili ni swala ambalo napaswa kulifanya na hata hivyo Arnhem sio sehemu ambayo ipo kiburudani ni kama gereza na kila kitu ni msitu hivyo kwenda na Rufi kule ni kama nampeleka kuzimu, hivyo mke wangu usiwe na wasiwasi na toa ruhusa yako niweze kuondoka nae”Aliongea Roma kwa unyenyekevu baada ya kuona mabadiliko yake.
Edna alifikiria na alionekana kama mtu ambaye amechanganyikiwa, moyo wake siku hizo za karibuni ulikuwa tofauti na zamani, alikuwa tayari kuona Roma akiendelea na wanawake wale wale aliokuwa nao na asione wivu lakini kumuona mwaamke mwingine mpya kwake ilimuuma na kumuogopesha kwa wakati mmoja na hata yeye mwenyewe alijishangaa na hata Roma alivyoweka wazo hilo akili yake ilimwambia na yeye aungane nae ili aweze kumlinda vizuri , lakini alifikiria uwepo wa Lanlan aliona asingeweza kuongozana na Roma na kumuacha peke yake.
Wazo moja tu ambalo lilimjia katika akili yake na kuona ndio njia mbadala ni kumteua mtu mwingine wa kuongozana nae kwenda huko na ingekuwa rahisi kuzuia mahusiano kuibuka zaidi na zaidi
“Nimekubali unaweza kwenda nae lakini lazima uende na mtu mwingine pia”Aliongea Edna na kumfanya Roma kushangaa.
“Mtu mwingine kwenda nae sio tatizo kwangu , nani unaona anafaaa kunisindikiza?”
“Mage”Aliomngea akiwa ni mwenye sura iliojaa usirias na kumfanya Roma moyo wake kupiga kite , alikuwa na mahusiano na Mage lakini alikuwa akiyafanya siri Edna asifahamu.
“Unashangaa nini Mage ndio mtu pekee ambaye unaweza kwenda nae ningewaruhusu mwingine lakini kwa walivyokuwa wadhaifu kwako wasingeweza kukuzuia kufanya jambo la kishenzi?”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa.
Roma alikuwa na mahusiano na Mage lakini hakuwahi luyaweka wazi na ndio maana alikuwa kwenye mshangao bara baada ya Edna kutaja mtu wa kuongozana nae kwenda Australia kuwa Mage, hali hio ilimfanya kuvhanganyikiwa yeye mwenyewe kwa kuona Edna alikuwa akifahamu siri yake halafu alikaa kimya.
"Mbona uko hivyo au Mage hafai ?"
"Sio kwamba hafai lakini kuna ulazima wa kutangulizana na mwanamke?"
"Ndio nataka utangulizane na mwanamke tena mwanamke huyo akiwa Mage ndio mtu pekee ambaye anaweza kukuzuia usifanye ujinga na Rufi na ndio sharti langu"Aliongea
"Edna ulifahamu lini?"
"Kuhusu nini?"
"Mimi na Mage tuna mahusiano" Aliongea Roma kwa ujasiri lakini kwa hofu ndani yake na swali lake lilimfanya Edna kucheka kidogo kwa uchungu.
"Hilo swali muulize Mage mwenyewe atakuwa na majibu" Aliomgea Edna na kisha hakutaka mazungumzo zaidi na kuondoka kwenye chumba hiko cha kujisomea na kumuacha Roma bado akiwa kwenye sintofahamu.
Ni kweli alikuwa na mahusiano na Mage lakini siku zote alikosa ujasiri wa kumuweka wazi Edna , lakini alishangaa Edna kutambua juu ya hilo bado lakimi aka kaa kimya bila ya kuzungumza.
Roma alijiuliza Edna alifahamu lini maana kama ingekuwa ni siku hio basi huenda angemnunia siku nzima lakini ajabu walikuwa sawa na hata siki yao iliisha bila shida.
Ila kitendo sasa cha Edna kuondoka wakiwa hawajamaliza mazungumzo alijua lazima angekuwa na hasira na yeye kutokumuambia ukweli lakini hata hivyi asingejuwa namna ya kujitetea kama hajui ni lini ameweza kujua ukweli.
Roma hapohapo aliona majibu ayapate kuroka kwa Mage mwenyewe , muda ulikuwa umeenda lakini alijua lazima Mage atakuwa macho na kweli baada ya simu yake kuita muda mfupi ilipokelewa haraka.
"Babe Mage mbona kama ulikuwa ukisubiria simu yangu"
"Mh ..! Roma vipi kuhusu Edna"
"Edna ana nini?"
"Mama leo kaharibu kila kitu"
"Kaharibu nini??"
"Sijui kaongea nini na Mkeo ila kamwambia kuhusu sisi baada ya Magdalena kakataa mchumba anaetaka kumuoa...."
Kwa maelezo ya Mage ni kwamba mtoto wa waziri wa sayansi na teknolojia afahamikae kwa jina la Jumbe alifika nyumbani kwa Mage na kuweka nia yake wazi ya kutaka kumuoa Magdalena jambo ambalo lilipokelewa kwa mikono miwili na Mama T.
Mwanamama huyu alikuwa ashachoshwa kuona watoto wake wa kike wakikosa ndoa ilihali wakina mama ambao ni marafiki zake watoto wao walikuwa wakiolewa na kuoa kwa sherehe kubwa na yeye kuishia kutoa michango pekee.
Na kilichompa shida zaidi ni kila mara alipofikiria Mage hawezi kuolewa tena kwa kuamua kuwa mchepuko wa Roma jambo ambalo hata mume wake alilibariki hivyo tumaini lake kubwa ilikuwa ni kwa Magdalena.
Alielewa watu wakiona Mage hajaolewa wangemnyooshea vidole na kumsema lakini kwasababu ilikuwa ni kwa ajili ya furaha yake hakutaka kumzuia lakini jambo hilo hilo hakutaka kuona likitokea kwa Magdakena pia na ndio maana Jumbe alupoweka nia yake wazi ya kutaka kumuoa mtoto wake alipokea taarifa hio kwa mikono miwili.
Lakini sasa kilichomshangaza ni baada ya Magdakena kukataa akisema hawezi kuolewa na Jumbe kauli ambayo ilimfanya kuhisi uchizi.
"Magdalena kama humtaki Jumbe inamaana tayari una mchumba kama ni hivyo mlete tumuone na nikiridhika nae nitakuruhusu uolewe nae" Aliongea Mama na kumfanya Mage aliekuwa amekaa upamde wa kushoto kushindwa kuongea chochote na kumuonea huruma dada yake kwani alikuwa akijua kike kilichokuwa kikiendelea kwenye moyo wake.
"Mama sina mchumba ila sipo tayari kuolewa na Jumbe" Alijibu Magdalena na kumfanya Mama T kushindwa hata kuelewa watoto wake wamekumbwa na nini , kwenye maisha ykje alijitahidi kuwalea kimaadili na kutegemea waje kuolewa na kuwa na furaha kakini imegeuka kuwa tofauti .
"Mume wangu mbona huongei chochote jamani hawa watoto wanataka kunitia uchizi?"
Afande Tobwe alikosa cha kusema kabisa kwani alikuwa ashajua muda mrefu sababu ya Magdalena kukataa ndoa na Jumbe , alikumbuka vizuri siku ya Roma alipokuwa akipambana na Yan Buwen namna ambavyo Magdalena alitaka kumuokoa Roma kwa kujitoa Muhanga yeye mwenyewe uhai wake.
Kwanzia kipindi hiko alikuwa akishindwa kujua tatizo la Magdakena linaisha vipi , kwenye maisha yake licha ya kuwa mwanajeshi likija swala ka familia yake alikuwa akizingatia zaidi watoro wake waje kuishi na furaha na ndio maana hata Mage alipo onyesha kuwa na mapenzi na Roma hakusita kumruhusu licha ya kujua Roma ana mke tayari na mwanae angekwenda kuwa mchepuko tu, lakini swala la Magdalena ilikuwa ngumu kumruhusu kuwa na mahusiano na Roma na wakati huo na pacha wake akiwa na mahusiano na Roma.
Jambo hilo kama angeruhusu jamii isingemuelewa na sio hivyo ru hata dini yake ilimzuia kuruhusu kitu kama hiko.
"Magdalena kama huna mahusiano, Jumbe anakufaa usikatae , najua kwa zama za sasa wazazi hawapaswi kuwachaguliwa watoto wao wachumba lakii siku zote mzazi anamuombea mtoro wake kuwa na furaha hivyo kuelewa ni kipi bora kwako , Jumbe anakupenda hivyo hata kama humpendi utajifunza"Aliongea Afande Tobwe kwa usiriasi na kisha akaamka na kuondokaneneo hilo la sebuleni.
Huku nyuma akiacha sura ya Magdalena kuwa katika hali isioelezeka , alitarajia baba yake kumuunga mkono lakini akaishia kumkandamiza kwa.kusimama upande wa mama yake.
Wakati wa mchana Edna alipofika dukani kwa ajili ya kutafuatilia mwenendo wa mauzo ya mavazi alioingiza sokoni kupitia kampuni yake kwa kutumia malighafi mpya ndio alipokutana na Mama T.
Walikuwa hawajaonana muda mrefu tokea Edna asafiri kwa ajili ya harusi yake hivyo waliongea sana huku Mama T akitaka kuona Edna alipendezaje na katika mwendelezo wa stori ndipo Mama T alipojikuta akiropoka kuhusu mtoto wake Mage kuwa na mahusiano na Roma.
Mwanzoni Edna alihisi kuna kitu kinaendelea kati ya Mage na mume wake lakini alikosa ushahidi wa wazi wa kuthibitisha kile anachowazia.
******
Upande mwingine nchini Rwanda mheshimiwa Jeremy alikuwa akizunguka zunguka kwenye ofisi yake huku na huko akionyesha kama mtu mwenye hasira nyingi na hio yote ni mara baada ya kupata taarifa ambazo zilithibitisha Kizwe ndio ambaye alimtorosha Desmond hospitalini wiki kadhaa zilizopita.
Raisi Jeremy mara baada ya kumtoa Desmond Tanzania moja kwa moja alimsafirisha mpaka India kwa ajili ya matibabu , hakuwa akiamini maneno ya daktari wa Tanzania kwamba mtoto wake hawezi kupona kiungo chake cha uzazi na ndio maana alikuwa radhi kufanya lolote kwa ajili ya mtoto wake huyo na isitoshe ndio ambaye alikuwa ni mrithi wake akitaratjia siku za usoni kumwachia nchi aiendeshe , lakini akajiuliza kama Demsond hatokuwa na uanaume wake je angeweza kuendesha nchi kisawasawa na jibu lilikuwa hapana.
Upande wa Desmond mara baada ya kushituka katika kupoteza fahamu na kujua hakuwa na uwezo tena wa kumfanya chochote mwanamke wakiwa kitandani alilia sana na kuomboleza na maumivu yake yalikuwa ni zaidi ya siku aliopokea taarifa za kifo cha mama yake.
Mpaka muda huo alijiona hakuwa ni wa thamani tena kama mwanaume na ndio maana alijawa na huzuni isiokuwa ya kifani huku lawama zote akimwangushia baba yake mzazi ,kwani aliamini kama sio matendo yake basi huenda asingepatwa na kadhia hio.
Ilikuwa ni adhabu kubwa mno ambayo Roma alikuwa amemfanyia , ilikuwa ni zaidi ya kifo kwake na hakujiona wa thamani kabisa.
Hata pale raisi Jeremy alipomtembelea katika wodi aliolazwa hakutaka kumuona kabisa na alitangaza waziwazi kwamba anamchukia na hali ilio iliamsha sana huzuni kwa Raisi Jeremy ,hakujua ni kwa namna gani angemsaidia mtoto wake kupona kwani alishakuwa tayari Eunuch ,kwa mtazamo wake hata kama angetaka kulipiza kisasi kwa Roma asingeweza na pia ingekuwa laana kwake kushindana na mkwe wake.
Kuna muda aliona huenda matendo yake ndio yaliokuwa yakimfikisha katika hali kama hio, alikuwa na mafanikio katika uongozi wake lakini likija swala la familia alikuwa amefeli pakubwa na alijiona kama mtu ambaye hakuwa na bahati.
Madaktari wa kihindi walijitahidi kufanya juhudi za kila namna ili kumponyesha Desmond tatizo lake lakini majibu hayakuwa na tofauti sana na yale ambayo yalitolewa Tanzania.
Kwa ufupi ni kwamba mtoto wake hakuwa mwanaume mwenye makali tena , taarifa ambayo ilikuwa mbaya sana na kuishia kumlaani Roma kwa kumfanyia hivyo mtoto wake.
Wakati akiendelea kutafakari namna gani ya kumsaidia Desmond akiwa nchini India kwa siri, ndipo alipopokea taarifa za Desmond kutoweka hospitalini kwa hali isiokuwa ya kueleweka jambo ambalo lilimshangaza mno na sio kwake tu hata vitengo vya ulinzi vya hospitali vilishangazwa na jambo hilo kwani hakukuwa na Kamera yoyote ilionasa tukio la Desmond kutoroshwa na kitu kingine zaidi ni kwamba CCTV Kamera zote zilikuwa zikifanya kazi.
Kwa maelezo hayo mafupi alioyapata Raisi Jeremy alijua moja kwa moja Kizwe atakuwa anahusika katika hilo.
Tokea siku ambayo aliweza kupata taarifa za Kizwe kuwa hai kutoka kwa Linda ilimshangaza sana Raisi Jeremy kwani ilikuwa ni taarifa ambayo kwake ni kama anaambiwa mfu kafufuka , alishuhudia yeye mwenyewe kifo cha mke wake na kumuona akizikwa inakuwaje akawa hai.
Linda hata yeye mwenyewe alishindwa kuamini kama Kizwe alikuwa hai , aliweza kupata kuigundua sura ya Kizwe siku kadhaa wakiwa wanafanya uchunguzi ndani ya chuo cha taifa cha Rwanda mara baada ya Lekcha kupotea na walipoangalia kamera za Chuo ndio walipoweza kuona sura ya mwanamke anaefanana na Kizwe kabisa akiwa katika ujana.
Tena inasemekana wakati Kizwe anaondoka na Lekcha katika chuo hicho Kizwe aliangalia Kamera ya ulinzi na kisha akatabasamu kifedhuli na kutamka maneno kwa namna ya kuonyesha ishara za midomo yake, alifanya hivyo kama mtu ambaye aliamini kabisa Footage za sura yake zingemfikia Jeremy.
Katika rekodi hio ya camera Kizwe alikuwa akionyesha ishara kama ya kumtahadharisha Jeremy kwa kumwambia kwamba anarudi kulipiza kisasi.
Baada ya taarifa ya mwanamke anaefanana na Kizwe kumfikia raisi Jeremy kwanza kabisa hakuamini na aliweza kupitia hatua zote tano za mshituko ili kujibu hali ya taarifa hio na baada ya masaa mengi ya kufikiria ndio uamuzi wa kufukuliwa kaburi(exhumation) la Kizwe kwa siri sana ufanyike nyakati za usiku kazi ambayo iliongozwa na Linda.
Na ilichukua siku tatu kwa mchakato wote kumalizika na mara baada ya raisi Jeremy kuwekewa majibu mezani alijikuta akipagawa , mwili ambao ulifukiwa haukuwa wa mke wake Kizwe kwani vinasaba vilithibtisha hilo.
Sio kwake tu ambaye alishangazwa na hilo lakini hata Linda pia alishangaa na kutaka kuthibitisha hilo na hapo ndipo walipoanza kuwasiliana na wanasayansi na vitengo vya serikali nyingine ili kuweza kuthibitisha uwezekano wa mtu aliefariki kufufuka na katika majibu mengi ambayo walipokea moja wapo ni kesi ya siri sana iliomtokea raisi mstaafu wa China lakini kesi hio hio ikajirudia nchini Tanzania baada ya mwili mtoto wa tajiri wa makampuni ya Maya kuonekana akiwa hai mara baada ya kifo chake kuthibitishwa.
Taarifa zilikusanywa kwa kutumia idara za kitelijensia na zilipomfikia Raisi Jeremy ndipo alipotambua sasa jina la mwanasayansi Yan Buwen ambaye alikuwa amepewa hifadhi ya kufanya majaribio yake nchini Tanzania.
Intellijensia ya Rwanda iliweka kila kitu wazi na kweli Yan Buwen wakati wa maombolezo ya kifo cha Firsr lady alionekana kuingia nchini Rwanda , muunganiko huo wa matukio ndio ulikamilisha uchunguzi wa kuamini Kizwe alikuwa hai bado na aliehusika kumrudisha hai ni Yan Buwen.
Na Raisi Jeremy alijiona mjinga kwa kuona alizidiwa akili na mke wake na hata kitendo cha Lekcha kumbakisha hai ulikuwa pia ni mpango uliosukwa , hatari aliweza kuiona mbele yake na kuanza kumuogopa Mwanamke aliekuwa ni mke wake na hata ulinzi wake aliongeza maradufu huku akihakikisha Desmond mtoto wake hafahamu ukweli wowote kuhusu hilo.
Asichokijua raisi Jeremy ni kwamba Desmond ndio moja wapo ya watu walioshuhudia mama yake mzazi akifufuliwa na Yan Buwen na hata nyakati za maombolezo ya taifa alikuwa akijifanyisha tu kuwa na huzuni.
Baada ya kifo cha raisi Kigombola pamoja na Yan Buwen Raisi Jeremy alipata unafuu na safari yake ya kuhudhuria maziko ya raisi Kigombola ilikuwa na sababu ya ziada ambayo ni kuona uwezekano wowote ambao ungemkutanisha na mke wake.
Siku ambayo Fredi aliandaa Party ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na Edna na Roma kualikwa ndio siku ambayo pia hata yeye mwenyewe aliweza kupokea ujumbe kutoka kwa Kizwe akimwambia afike Maple speed Resort kama anataka kuonana nae.
Lakini Kizwe hakuwa na mpango wa kuonana na Jeremy bali aliandaa mpango wa kumfanya Jeremy kushuhudia Kaka akimbaka mdogo wake kwa macho yake lakini kwa bahati mbaya mpango wake huo ukaja kufeli mara baada ya bangili aliovalishwa Edna kuingilia kati na matokeo yake ni Desmond kuharibiwa uanaume wake.
Sasa zikawa zimepita siku kadhaa tokea Desmond apotee nchini India huku akiamini moja kwa moja muhusika ni Kizwe ambaye amebadilika na kuwa wa tofauti sana , sio tu kwamba alikuwa amefufuka lakini pia akarudi ujana.
Asubuhi hio aliokuwa akizunguka katika ofisi yake ni mara baada ya Kizwe kumthibitishia Jeremy kwamba yupo na Desmond na ajiandae kuachia uongozi wa nchi , kauli ya Kizwe kwake ilikuwa kama ya vitisho na ndio maana alikuwa na hasira na kuzunguka huku na huko huku akikosa namna ya kumshughulikia mwanamke huyo ambaye muda huo hakumuona kama mke wake tena bali alimuona kama shetani.
Mbaya zaidi aliogopa kwa kuamini na Desmond atakuwa amejazwa ujinga na mama yake kwa wakati huo .
Ilikuwa kama laana kwake kwa baba wa familia kushindana na familia yake na jambo hilo lilimkosesha amani kabisa.
ITAENDELEA.
 
Duuu yule nurse wa rufi kule wingereza anaitwa grace nasikia yupo level ya kushinda shida!😂😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom