83.
Treni hio ilisimama na mlango ukafunguka, Alex alimbeba Rose na kushuka. Mbele yake kulikuwa na mlango, alitebea mpaka katika malango huo na kuufungua. Alishangaa kuona nyumba ile ilivyokuwa imefanana na ile waliokuwepo manzo kila. Kutokana na ufanano huo hakupata shiada kujua maabara iko wapi. Alielekea katika Maabara na kumlaza Rose kisha akachukua vifaa na kuanza kumchunuza, baada kumpatai huduma ya kwanza alimuacha apumzike yeye akatoka na kuelekea katika chumba kimoja ambacho aliamini ndio kama chumba alichokiacha kule alipotoka. Aliingia na kuelekea chooni na kujimwagia maji, alipomaliza alielekea jikoni na kujiandalia chakula. Alipomaliza alipata maakuli kisha akaelekea maabara kumuangalia Rose ambae alikuwa amelala hajitambui. Alikaa pembeni ya kitanda hicho na kujipumzisha. kutokana na uchovu na kuchoka sana usingizi ulimchukua gubigubi. Alikuja kushtuka baada kuhis kama akiguswa na mtu, alipofumbua macho alikutana natabasamu zuri usoni mwa rose. Lakini alishangaa kumuona akiwa ameshabadilisha nguo, hata hivyo alipojaribu kumuongelesha hakumjibu kitu badala yake alikuwa akitabasamu tu ila ghafla alianza kutoka damu nyingi mdomoni. Alex alikurupuka kutoka usingizini huku akihema kama mtu aliekuwa akifukuzwa. Alimuangalia Rose ambae alikuwa bado amelala hajitambui, alianza kuziangalia mashine ambazo zilikuwa zikifuatilia maendeleo yake lakini aligundua mapigo ya moyo yalikuwa yanasomwa katika kiwango cha chini kabisa. Hofu ilianza kumtanda, alitoka maabara na kuelekea gereji. Alitoa gari na kuipeleka mbele ya nyumba, alirudi ndani na kumbeba na kumpeleka kwenye gari kisha safari ya hospitali ikaanza. Aliendesha mwendo wa kiasi mpaka akiafika, alishuka na ufungua mlango wa nyuma. alimbeba na kukimbia nae ndani ya hosipitali. Wahudumu walipomuona walichukua kitanda cha matairi na kumfata. Alex alimlaza kwenye kitanda na hapo alikimbizwa katika chumba cha matibabu ya dharura, na baada kufanyiwa uchunguzi wa awali ikagundulika kuwa yupo katika hali mbaya. Hivyo dakatari mkuu anaemsimamia alitoa amri ahamishiwe chumba cha wagonjwa mahututi na ikafanywa hivo. "kijana nakuomba utulie utuache tufanye kazi yetu" Daktari huyo aliongea na kuzama katika chumba hicho cha wagonjwa mahututi.
Agent Darling alipiga simu kituo cha polisi cha karibu na nyumba aliokuwa anakaa Alex, dakika tano baadae kilifika kikosi cha askari kikiambatana na gari la zima moto pamoja na gari ya kubebea wagonjwa. Alitoa maelezo yote hayo lakini hakuomtaja Alex. Baada ya hapo aliacha polisi wafanye kazi yao, yeye akarudi kwenye gari yake na kuondoka. Kwa sabau ulikuwa ni usiku alirudi nyumbani kwake na kupumzika lakini mawazo yake yote yalikuwa ni kutaka kuua wale waliomvamia Alex walikuwa wanahusika nae vipi. usiingizi ulimchukua bila hata kutegemea, alikuja kushtuka asubuhi baada ya saa yake kupiga kelele. Alipoangalia aligundua kuwa siku hiyo amechelewa kuamka, alikurupuka kiatanani na kuingia chooni. Alioga haraka na kutoka, alivaa nguo za kazi na kutoka bila hata kunywa chai. Aliingia kwenye gari na kuondoka, siku hiyo kamera za barabarani zilipiga picha za kutosha za gari hio kutokana na mwendo kasi. Alifika ofisini na kukuta wenzake wote wakimshangaa, "hebu acheni kunitolea mimacho" aliongea na kuingia katika ofisi yake.
*************************************
Daktari alotoka katika chumba hicho huku akionekana ni mwenye huruma "nambie mpenzi wangu anaendeleaje" alijikuta akimuita hivo wakati anauliza. "kijana nakuomba utulie kwanza kisha ndio nikueleze" Daktari aliongea huku akimuweka kitako Alex ambae aliokana kama kuchanganyikiwa. "pole kwanza kwa kilichowakuta, na kwa upande wa mgonjwa sisi tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini uwezo wake wa kuishi ni mdogo sana". "unasemaje" Alex alipanik kusikia hivo, "tulia sasa, kwa nje anaonekana hakuumia sana lakini ameumia sana ndani, tumetoa vipande sita vidogo vidogo vya vyuma. Vilikuwa vimeganda katia moyo wake na kupelekea moyo kuoteza nguvu ya kusukuma damu hivo kupeleka sehemu nyingi katika mwili wake kukosa damu ya kutosha. Hiyo imepelekea kupata tatizo la ubongo na pia kibaya zaidi utapoteza watu wawili, tumemkuta na uja uzito siku chache. Mpaka sasa kiumbe kilichokuwepo tumboni mwake kimeshakufa. Na tunahitaji kauli yako ili tuziondoe mashine zinazomuweka hai, hakuna uwezekano wa kupona kutokana na kua karibu nusu na robo ya seli zake za ubongo zimeshakufa. Usifanye maamuzi ya haraka, fikiria kwa umakini mkubwa hili swala kwa sabau ni swala la kifo na uhai" Daktari alimaliza kuongea na kumpa pole Alex kisha akainuka na kuondoka. Machozi yalianza kumtoka japo alijitahidi kuyazuia, "kwa nini mimi kila siku" alijisemea moyoni. .
Aliinuka na kuelekea katika chumba alichwekwa Rose na kuomba kumuona, manesi walimruhusu na kuingia. Alikwenda pembeni na kumuangalia mwanamke huyo ambae alionekana kupauka, alikaa pembeni na kuanza kuongea "hivi hata wewe unaondoka unaniacha peke yangu, kwanini lakini wote mumeamua kuondoka mapema kiasi hichi. Basi ungesubiri japo nikupe zawadi yako" Alex alizidi kulalamika, wakati anendelea kuongea alihisi kama mkono ukimgusa. Aliinua macho na kumuangalia Rose ambae alionekana kutabasamu. Akampa ishara amuondole kifaa kilichokuwa mdomo ili aongee na Alex alifanya hivo "mbona bado sijafa, unaweza kunipa hata saa hivi hiyo zawadi yangu" Rose aliongea japo kwa shida kidogo, Alex alitabasamu huku akitokwa na machozi kisha akamuonyesha ishara kuwa amsubiri anakuja. Alimrudishia kile kifaa cha kupumulia na kutoka kisha yeye akatoka na kuomba kuonana na daktari. Alielekezwa ofisi kwa daktari na kuongea nae,baada dakika tano alitoka na kutoka kabisa hospitali hapo. Nusu saa baadae alirudi na boxi kubwa na kuwakabidhi manesi, na kwa sababu walikuwa washaambiwa na mkuu wao jambo litakalo kwenda kufanyika. waliingia katika chumba alichokuwa amelazwa Rose na kufanya kama walivyoelekezwa. Alex aliekezwa katika chumba kingine na kubadilisha nguo. Alivaa suti moja safi sana na kutoka "maandalizi yamekamilika" Daktari aliongea, na kuongoza njia mpaka katika chumba alichokuwa Rose. Waliingia ndani na kumkuta padri akiwa tayari ameshafika. "karibu kijana" aliongea mzee huyo, "asante" Alex alijibu kukaa pembeni ya Rose. "unajua kama unachotaka kukifaya ni kitu kikubwa sana" aliongea tena mzee huyo. "naelewa" Alex alijibu, taratibu zilifanyika na muda wa ndoa ukafika. "bwana Alex Jr Jason umekubali kumchukua bi Rose kuwa mke wako halali wa ndoa kuanzia leo hadi mwisho wa uhai wako", "nimekubali" Alex alijibu bila kusita. "bi Rose umekubali kumchukuwa bwana Alex kuwa mume wako halali wa ndoa kuanzia leo hadi mwisho wa maisha yako", "nimekubali" Rose alijibu. Basi Padri aliwatangaza wawili hao kuwa mume na mke rasmi kuanzia muda huo. Wote waliokuwa wakishuhudia tikio hilo walikuwa wakitokwa na machozi kwa sababu walielewa kuwa mwanamke huyo asingeweza kutoboa hata masaa matatu yajayo. "Rose hii ndio zawadi yako" Alex alijibu na kumkumbatia" walipigwa pica kadhaa kama kumbukumbu za tukio hilo.
Baada hapo Alex aliwaomba wote watoke ili abaki na mke wake, na wote wakatoka. Baada nusu saa Alex alitoka huku analia na kumwambia daktari kuwa tayari. Gakatari alielewa nini amemaanisha na kumsogolea Alex ambae alikuwa anashindwa kuyazuia machozi "pole kwa kumpoteza mtu unaempeda" aliongea huku akimpiga piga begani. Maiti ya Rose ilitolewa na kuplekwa kwa ajili ya maandalizi ya safari ya mwisho. Baada hapo taratibu za mazishi zilifanyika na waliohudhuria wengi walikuwa ni miongoni mwa wale wauguzi wa hospitali, baada ya kuzika watu wote walioondoka kasoro Alex alibakia pale pale na mvua ilianza kunyesha lakini wala hakujali hilo. "nisalimie Allen huko unakokwenda na usijali ombi nitalishughulikia kama ulivosema na nakuhakikishia hatobaki mtu hata kama itabidi nipambane na duni nzima nitafanya hivo" Aliongea kisha akondoka eneo hilo la makaburi na kurudi nyumbani kwake, nyumba hiyo aliiona kubwa sana.
*************************************
"Alex niahidi kuwa kifo changu hakitokwenda bila kulipwa", "nakuahid na wala usijali wote waliohusika na kifo chako na cha Allen watalipa kwa maisha yao, hatobakia hata mmoja". "nafurahi kusikia hivo" Rose aliongea huku akianza kukosa pumzi, "vipi unaumia" Alex aliuliza huku akimsogeza karibu, "hapana siumii kabisa, nitaumiaje wakati naondoka katika mikono ya mwanaume nnaempemda" Rose alijibu huku akimuangalia Alex usoni. Kadri muda ulivyokwenda ndivo hali yake ilivyozidi kuwa mbaya. "Alex muda wangu umefika" Rose aliongea huku akimgusa Alex usoni kwa mikono yake ambayo ilikuwa ishapoa tayari na haikupita hat sekunde tano ilianguka na hapo alitoa pumzi ya mwisho na kuaga dunia. Alex alilia kwa nguvu mpaka waliokuwepo nje ya chumba hicho walisikia na wao wakakijukuta wakitokwa na machozi lakini wangefanyaje na kazi ya Mungu haina makosa.
"umetumwa na nani" Agent Darling alikomaa na swali hilo, "unadhani nitakwambia" alijibu kijana mmoja miongoni mwa vijana wa Shadow alikamtwa wakati wakijaribu kutoroka. "narudia kwa mara ya mwisho, ni nani aliekutuma" alifoka sasa, "kama nilivokwambia mwanzo, huwezi kuoata chochite kutoka kwangu ni bora uniue tu" aliibu kijana huyo. Ilibidi kwanza Agent Darling atoke katika chumba hicho maalum cha mahojiano. "huyu jamaa amepewa mafunzo ya kuhimili maumivu ya aina yoyote ile" aliongea Agent Darling huku akiwa amekunja sura. "kuna taarifa zozote kuhusu Alex" alimuuliza Joe ambae alikuwa akindela kutafuta kitu atika computer yake. "hapana mkuu sijapata chochote mpaka sasa" Alijibu Joe, "dah ni wiki nzima sasa huyu kiumbe hajapnekana atakuwa amejificha wapi" alijisemea Agent Darling. .