62.
Siku ya pili mapema asubuhi Alex aliamka na kama kawaida yake kufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka mwili sawa. Aliingia chooni na kujifanyia usafi, baada kumaliza kila kitu ndani ndipo akaamua kutoka nje. Alikuta chakula mezani, "habari zaasubuhi" Christine alimuuliza. "nzuri tu" Alex alijibu na kukaa kwenye kochi. "kariu mezani tupate kifunguwa kinywa halafu tuingie kazini kuna mambo mengi sana unatakiwa uyajue" alisemea Christine huku akisimama na kuelekea mezani Alex nae hakuwa nyuma hasa ukizingatia jana yote baada kula asubuhi hakula tena mpaka wakati huo. Wakati wanakula "hivi umenijuaje" Alex alivunja ukimya, "nilijua tu utaniuliza swali hilo" Christine alijibu kisha akaendelea.
"Mimi nakujua kuliko unavojifahamu wewe mwenyewe, ila kiufupi nilikuwa nikifanya kazi kama secretary katika kitengo cha upelelezi nchini Marekani lakini kutokana na mambo ambayo bosi wangu alikuwa akinifanyia ilibidi niache kazi kwa kufeki kifo, mpaka muda huu tunaoongea wanaamini nimekufa. Na nilijipa ahadi moyoni kama lazima nitalipa kisasi" Aliongea Christine huku macho yake yakionesha ishara ya kujaa maji. "dah pole sana lakini kwanini ukanisaidia" Alex aliuliza, "ni kutokana na kuwa na ugumu kulipa kisasi mimi kama mimi ndio maana nikaamua kukusaidia kwa sababu mimi na wewe tunashare adui mmoja" Alijibu. Maongezi yalienedelea mpaka walipomaliza kula. .
Christine aliinuka na kumwambia Alex amfuate, moja kwa moja walielekea katika chumba maalum ambacho kilikuwa kimepambwa na computer nyingi sana. "karibu humu ndio ofisini kwangu" aliongea Christine na kukaa kwenye kiti, "unafanya kazi peke yako humu" aliuliza kwa mshangao Alex. "ndio, ila nina wasaidizi wangu ambao ndio wale waliokuletea bahasha na yule alikuja kukupokea uwanja wa ndege. "si mchezo" Alex alijikuta akisema tu maneno hayo, "ok hatuna muda wakupoteza muda si mrefu Allen James atajua uko wapi, inabidi tufanya haraka na tuondoke eneo hili" Christine aliongea.
"hivi imekuaje huyu Allen akawa hatari kiasi hichi" Aliuliza Alex, "huyo mzee ni miongoni mwa watu wa mwanzo kujaribiwa na kemikali ya CODE X, mwanzo kemikali hiyo ilikuwa kali sana na wenzake wote walikufa wakati wa mchakato. hata hivyo mkewe ndie mtu ambae aliivumbua kemikali hiyo, na baada kugundua madhara yake ikiwa itaangukia mikononi mwa wa baya. Aliiharibu na kupoteza ushahidi wote, na pia aliitengeza keikali nyingine kwa ajili ya kuizimuwa lakini matokeo yake ndio akatengeza kiumbe kama huyo" Christine alimueleza, Alex alikuwa hoi baada kusikia hivo "sasa huyu jamaa nitapamabana nae vipi unadhani". "hatuna haja ya kupamabana nae, tunachotakiwa kufanya ni kumkwepa tu mpaka tuhakikishe tunamaliza kazi yetu.
.
Allen James anatoka nje ya uwanja wa ndege mjini Moscow, "Alex utakuwa umejificha wapi" Aliongea na kutafuta mgahawa wa karibu na kuingia. Alitoa laptop yake na kuanza kuhack computer za uwanja ndege kwa ajili ya kuangalia kama atapata chochote cha kuanzia. Lakini bahati mbaya sana hakukuta hata video moja iliomuonyesha Alex, tayari Christine alishafuta picha na video zote zilizomuonyehsa Alex. "vizuri sana lakini hapa umegonga mwamba ulioizamisha titanic" Allen alijisemea moyoni na kuatabasamu, kisha akaanza kuhack katika mafaili yaliofutwa. "bingo" Alijisemea baada kuzipata video zilizofutwa na zilimuonyesha Alex akitoka uwanjani. Video zilionyesha kila kitu mpaka alivopokewa na Nicolay, alifanikiwa kupata namba za gari ya Nicolay. "wacha mchezo uendelee" aliongea na kufunga laptop yake kisha akaondoka kwenye mgahawa huo. Alikodi taxi na kuelekea mpaka anapokaa Nicolay, aligonga mlango "nani wewe na unataka nini" alitoka mwanamke mmoja wa makamo hivi. "naomba kuonana na Nicolay" aliongea kwa upole, "Nicolay ndio nani" aliongea na kutaka kufunga mlango. Allen aliweka mguu na kutoa bastola yake na kumuwekea katika paji la uso, yule mwanamke alianza kutetemeka huku kijashi chembamba kikimtoka. "hakuna haja ya kuekeana bastola" ilisikika sauti ikitokea nyuma, "karibu" Nicolay aliongea kwa tabasamu. Allen aliingia na kumshukuru. Nicolay aliumuonyesha ishara yule mwanamke na kuondoka, "mimi nataka kujua tu kuhusu sehemu alipo Alex" Aliongea Allen. "na nisipokwambia je utanifanya nini" Nicolay aliongea kwa kujiamini, "utaniambia tu hata kama itabidi nijue kwa kutoa tone moja moja la damu katika mwili wako basi nitafanya hivo" Alijibu Allen akionekana kuwa hana masihara hata kidogo na jambo aliloongea.