18
Niliendelea kumshushia kipondo, kwa mbali nikamsikia mtu akiniambia "acha" kwa ukali, nikshangaa kuona mwili wangu unatii amri hiyo. Kisha akanambia "Njoo" basi nami nikafanya hivo na nilipofika alipo akaniambia "kaa" nami nikakaa, yote hayo niliyafanya bili akili yangu kufanya maamuzi yoyote yale. Nilihisi kweli sasa nimekuwa mbwa maana siwezi kukataa amri yoyote ntakayopewa, nilitamani kulia lakini mbele za watu ingekuwa aibu. Hali hiyo ya kuendeshwa kama mbwa iliendelea kwa muda mrefu takriban miaka mitatu, kuna wakati nilitumiwa sms usiku nikiwa faragha na mke wangu. Nilijikuta naacha kila kitu na kuelekea kazini. Hali hiyo iliitia dosari familia yangu na furaha ilitoweka, siku moja mke wangu akaniambia kuwa anahitaji kwenda kuwaona wazazi wake Miami. Na kwa hali ilivokuwa ikiendelea ndani ya nyumba yangu nilihisi nisipomruhusu basi ndoa yangu ingevunjika, nilikubali na siku ya pili mapema akaondoka pamoja na mwanangu.
Ukweli niliwalaumu sana kitengo changu kwa kuniharibia maisha yangu, maana nilikuwa sina maamuzi tena juu ya maisha yangu. Siku zilipita, na wiki zikakata na hatimae mwezi bila kuiona familia yangu, niliomba ruhusa na kuelekea miami kwaajili ya kuungana na familia yangu. Nilikubaliwa nasiku ya pili mapema nilifunga safari ya kuelekea huko, nilifurahisi sana kuonana na mke wangu, wakwe zangu pamoja na mtotot wangu ambae alishkilia kusema "baba umeniletea pipi". Nilimkabidhi mfuko mzima wa pipi kutokana na uchovu wa safari nilitaka kupumzika, mke wangu akanipeleka kwenye nyumba nyingine. Aliniandalia maji na kuniogesha kisha akaniandalia chakula na pia alinilisha, kwa kweli nilishangaa sana alifanya yote hayo utadhani mtu aliekuwa anakaribia kuiga dunia. Kisha alinisindikiza kitandani na yeye akiwa pembeni yangu na bila kuchelewa tukajikuta tupo katika huba za dunia. Baada jambo hilo nilipata usingizi mzito sana uliojaa ndoto nzuri, nilikuja kushtuka asubuhi baada kusikia kelele za watu na kwa mbali kupitia dirisha langu nikawa naona moshi mzito sana. Nilivaa nguo haraka na kutoka nje ili kama kunahitajika msaada nitoe. .
Sikuamini kama ilokuwa inangua ni nyumba ya wazazi wa mke wangu, nilijikutanikienda mbio na kuingia ndani bila kujali kama ningeungua au laa. Nilichokutana nacho ndani ndo kilonifanya nikaishiwa nguvu, miili minne ilikuwa chini, na kwa haraka niliitambua yote kuwa ni ya wakwe zangu,mke wangu pamoja na mtoto wangu. Nilipoangalia vizuri niligundua kuwa bado mke wangu alikuwa hai, nilimfata nimbebe lakin akanishika mkono na kutaka kunambia kitu "CODE....." hakuwahi kumalizia alikata roho. Machozi ya lianza kunitoka na kujikuta napoteza fahamu."
Nilizinduka kutoka katika usingizi huo huku jasho likinitoka kama maji, "karibu tena duniani MR Allen James" niliiskia ile computer ikiongea, "ile ni ndoto au" niliuliza kwa mshangao. "hapana yale ni maisha yako kabla ya kuitwa Allen James, zote ni kumbukumbu za maisha yako ya nyuma". Nilishindwa kujizuia na kuanza kulia kama mtoto mdogo, lakini swali lilikuwa ni nani alieiteketeza familia yangu yote.