Xav Emmanuel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2018
- 214
- 315
- Thread starter
- #21
Simulizi; “MATUNI” (09)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================
“Damu!!!” Neno hilo likagonga moja kwa moja mdomoni mwa Tumaini. Aliona Damu pale kwenye mfereji badala ya maji. Akapiga ukungwi wa nguvu Tumaini. Hakuwai kuona jambo kama hilo katu. Alipiga kelele nyingi mno.
----------
Tumaini aliamka toka katika hiyo ndoto, mwili mzima ulijawa na jasho. Alikua anatililikwa na jasho tu Tumaini. Haraka akakaa kitako. Hakuna alichokikumbuka katika ndoto hiyo. Maajabu. Tumaini hakukumbuka kitu chochote kile…..
ENDELEA SEHEMU YA 9…
“TUMAA..!, Tumaaa..!” Bosco alisikika akimwita Tumaini nje ya nyumba yao. Hakuitika Tumaini zaidi ya kuvuta kanga yake ileile aliyeizoea na kuburuta ndala zake kuelekea nje alikoitwa. Alisimama mlangoni akijifuta tepe la usingizi na ganya lake.
“Bosco!” aliita Tumaini huku bado akionekana hayupo sawa.
“Kanisani mpendwa!” alisema Bosco huku macho yake yakiishia mapajani mwa Tumaini aliyeshikilia nguo yake kwa kuikunjia kifuani na mkono mwingine ukiendelea kuikunja nguo yake.
“Mh!, kumefanyaje?” aliuliza Tumaini kana kwamba aelewi kazi ya kanisa.
“Kwani leo juma ngapi?” naye Bosco akamtupia swali Tumaini. Tumaini hakuonesha wasiwasi wowote ule, alitoka nje mzima sasa. Akaikusanya kanga yake na kuivutia miguuni, akakalisha makalio yake mlangoni hapo.
“Unataka nikasalishe?, au unataka nikatoe mhadharaa.. aagh!, kwanza umetubu wewe?” lilikuwa swali kwa Bosco. Tumaini aliuliza hivyo mara baada ya kuona Bosco yupo makini kuangalia sehemu zilizobaki wazi katika mwili wake.
“Tumaini… uliniahidi tutaanza kwenda wote lakini?!” alilalama Bosco na kuonyeshwa kuchukizwa na kitendo hicho.
“Wiki lijalo!” alitoa ahadi mpya Tumaini. Alimpenda sana Bosco kwa kuendelea kumjali kila siku. Hakuacha kutabasamu Tumaini.
“Naa.. na.. na ile siku ya kulala na mimi ndio kesho?” aliuliza Tumaini kabla Bosco ajanyanyua mguu wake. Hakujibu chochote Bosco, alimwangalia tu Tumaini kuanzia kichwani hadi kwenye mapaja yake, akaishia hapo. Akaikata tamaa yake na kuondoka. Ulikuwa mguu wa kanisa.
“Boscooh!, ah!. Nakupenda sana hujui tu!.” Alijiongelea mwenyewe Tumaini kwa kujiliwaza.
Si alikuwa pekee pale, akaiachia nguo yake ambayo tayari alijishikiza katika kifua chake. Mikono yake ikawa bize sasa kukata kucha zake. Alikua anawaza penzi la kijana huyo, ambaye licha ya kutojua mambo yanayoendelea kijijini hapo alikuwa bize kuhudhulia kanisa.
********
“Mume wangu!” aliita Mama Bosco akimwangalia mume wake ambaye alikuwa makini kusikiliza redio.
“Mama Bosco!” mumewe akajibu, akasubiri neno kutoka kwa mke wake.
“Unahakika Bosco yupo kanisani kweli?” aliuliza Mama Bosco.
“Sasa nawee!, la!, mimi ndiye kanisa? Au mchungaji wa zamu!, najuaje!” alijibu kwa ukali Baba Bosco.
Swali kutoka kwa mkewe halikuwa na maana kwa wakati ule kwa maana wote walimshuhudia Bosco akiongoza njia ya kwenda ya kwenda Kanisani. Sasa jambo la Mama Bosco lilimpa shida Mumewe kulitatua.
“Baasi Baba eh!, Pilipili ndimu!, kachumbali haina radha!, hadi vya ugomvi!” Mama Bosco akampa dongo mumewe ambaye tayari aliongeza sauti ya redio.
Nyumba hii ilikuwa haina ushirikiano wa kifamilia. Baba na Mama mara kadhaa wameingia katika mchuano wa kutafuta kichwa cha familia, kila pande ikiongoza mashambulizi. Bado mshindi hakupatikana.
“Na siku nikimkuta yupo na Tumaini, namkata miguu yake!” aliongeza neno Mama Bosco. Alionesha kumchukia sana Tumaini. Alikua anaongea mwenyewe kwa sasa. Mumewe alikuwa mbali na redio yake.
“Bosco, Bosco, Bosco!, Soma wewe mtoto, unataka nikushirikishe kwenye mambo haya mapema hivi?, hapana bado mdogo wewe!, bado mdogo kabisa huwezi kuyabeba, ila ukilazimisha tu, utanijua mimi ni nani!. Utanijua Bosco!.” Mama Bosco alikua anajiongelea pekeyake tu, macho yake yakamrukia mumewe kama aliyasikia maneno yake, Hora!, alikuwa bize mumewe. Bize na yeye. Mtangazaji wa redio alimkosha sana na kumsahaulisha vituko vya mkewe.
“Huyu mzee naye anahitaji tiba!, ngoja!!, mana nishamchoka mimi, tende tendee, kila siku tende tendee wakati amelima mahindi!. Nitawachanganya hawa, we Subiri!” bado mama Bosco alikuwa pekeyake. Alikua anazungumza na moyo wake. Alitamani kuonesha hadharani uwezo wake kwa familia yake, lakini onyo la moyo wake likamkanya na kumwambia anyamaze.
Hata aliporudi Bosco bado mambo yalikuwa ni yaleyale, Mama alianza mauzauza mapema mno.
“Unahakika ulikua kanisani?” ndio swali amabalo Bosco alikutana nalo kutoka kwa Mama yake.
“Kwanini?!” aliuliza kwa mshangao.
“Hata kama ulienda!, basi umechelewa?” Mama alikomalia hapo sasa.
“Sikuelewi Mama yangu, nini unazungumza?
“Ah, bado mtoto sana wewe!, mkubwa wako akikukanya basi kuwa mwelewa!” Bado alishindwa kueleweka kwa ufasaha Mama Bosco.
“Shida ni kujua mimi niemeenda kanisani au shida ni kujua kama nilichelewa?”
“Vyote ni shida tu!, Tumaini? Hujakutana nae leo?” alipunguza sauti Mama Bosco. Kwa maana ugomvi huu wa kumuhusisha Tumaini Mume wake aliukataa katakata. Hakujua nini kinaendelea. Baba alikua anaona kila analofanya mwanae yupo sawa, ila mama alikuwa na vipingamizi. Tumaini!!. Hataki hata kulisikia jina hili Mama Bosco.
“Hhahaha!, ndio shida yako hiyo!, unahitaji tu nimtaje Tumaini asubuhi yote hii?, si ulikataza mama. Niende kwa nini sasa!. Nikukosee heshima mama yangu?!” alijitetea Bosco.
“Hhahahaha, kweli kijana bado hujakua kabisa!?, nikikuonya jambo fikiria mara mbili, alafu….!, katu usilifanye!, sitaki nikupoteze mwanangu. Sihitaji ukutane na Tumaini tena. Nimesema siitaji! Sawa baba?” aliongea Mama Bosco.
“Lakini Mama kwa nini Tumaini?”
“Kwa sababu sijakuhusisha bado. Hadi ukomae mwanangu!, usilolijua ni sawa na usiku wa giza!” aliishia hapo Mama huyo na kumwacha mwanae na swali kedekede!.
“Huyu Mama nahisi ni mchawi!, la!, hapana, siwezi mkosea heshima hivi!, ah! Sasa kwanini Tumaini?, Tuma hataki kumwongelea Mama, mama anamwongelea Tuma kila siku, tena kwa Shari tu!, au?, nikamu—ulize Tuma au!. Ah lakini wanawake bhana, usikute walinyimana chumvi tu au moto. Wakalianzisha.. hahahahahahaha!” Bosco alijiongelea pekeyake alikuwa anawaza tu nini kinaendelea…
Maisha ndani ya familia hiyo yalikuwa ya kufa kupona, nyumba mbovu, maisha magumu ila hawakuacha kabisa kutafarakana. Mama na siri nzito kwa mtoto. Baba na Mama wanaongea wakati wa kula tu, nje na hapo zikipita dakika mbili waongee salama basi ni sherehe siku hiyo. Baba mkali, Mama mkali, hakuna aliyejishusha. Siku hii ikaisha kwa mtindo huo.
********
SIKU hii ya jumatatu ilikuwa maajabu sana kwa Tumaini kulala usingizi usio na mauzauza, alijilalia na kuamka bila shaka. Leo kwa hakika alijiandaa kwenda kuionesha shule.
Alitaka afungue upya ukurasa wa masomo yake ya sokendari. Alikuwa bado kidato cha pili. Leo Tumaini aliamka mapema kujiandaa.. alitaka kumfurahisha kipenzi chake. Mtu ampemndae kwa dhati baada ya bibi yake!, basi!!, ni hao tu wawili. Hakuna jirani wala rafiki mwingine.
Punde tu Tumaini alianza kutafuta nguo zake za shule zilizofungiwa siku zaidi ya saba. Alishaacha kabisa kwenda shule. Akavuta sanduku toka chini ya kitanda cha bibi yake na kulifungua. Ulitoka moshi mweupe na kupotelea angani.
“Mh!, kuna usalama kweli hapa?” aliuliza Tumaini huku akichukua shati la shule na kujipima kama litakuwa linamruka. Alicheka Tumaini baada ya kulivaa.
“Nimekua!” alijisemea huku uso wake ukinakshika kwa tabasamu.
Alikua mzuri Tumaini. Hakuna kipingamizi!. Aliendelea kujichunguza chuchu zake ambazo kwa sasa dhairi shairi zilikuwa kubwa mno. Alichongeka kiasi kwamba kutaka kutoboa shati lake nyepesi la shule, hakuwa na nguo ya ndani maharufu kama sidilia. Hakuona tabu. Akakongeka shati lake hivyohivyo.
“Mwenye tamaa na akufe?” alijiongelea Tumaini akichomekea na sketi yake damu ya mzee. Alijigeuza geuza mwenyewe kwa maana hakuwa hata na kioo. Macho yake yalikuwa shaidi tosha.
Umbo la sasa la tumaini ndio lilifaa kuvaa aina hizi za nguo. Bibi yake alimshonea nguo kubwa mno kiasi kwamba azivae wee hadi mwisho wake wa kuhitimu kidato cha nne. Kwa sasa shati lilianza kumbana na kuwa fupi kiasi kutokana na mpanuko wa kifua chake. Sketi nayo ilianza kumtupa mkono, kwani ilianza kuwa fupi kutona na ukubwa wa hipsi yake!, si alikuwa mfupi Tumaini. Vitu vilimwacha tayari akiwa kidato cha pili tu!. Akatinga hivyohivyo. Safari shuleni!.
“Siamini!, wewe huyo Tuma?” aliuliza Bosco alipomkuta Tumaini mlangoni kumsubiri.
“Samahani Baba, naitwa Tumaini ilo Siamini sijui la nani.. au basi, twende kipenzi” tayari alishamshika mkono Bosco.
“Tuma, hakuna kushikana mikono huku tuendako!, nguo zenyewe zimekuchoraaa da sijuii!!!.., na… na…” alijikuna kichwa Bosco.
“Mkoba!, mkoba wako upo wapi?, ona sasa hujabeba!.”
“Booscooh!, usijali siku ya leo ntaandika kwenye daftari lako. Hapana shida!” alizua jipya Tumaini. Yaani maandalizi yote yale na shule hakubeba daftari!, Mhh labda anaenda kufanya mazoezi ya viungo shule, ngoja tuone…..
---------
ITAENDELEA…