Simulizi ya kichawi: "MATUNI" (Nafsi 1 Sehemu 3 Tofauti)

Xav Emmanuel

JF-Expert Member
Jul 12, 2018
214
315
MATUNI
“NAFSI MOJA SEHEMU TATU TOFAUTI”
By Author Xav


Simulizi; “MATUNI” (01)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================
-UTANGULIZI-
NI Tumaini, binti ambaye anarithishwa uchawi akina na lika la miaka kumi na sita tu. Licha ya kuhusishwa na mambo ya kishirikina na Bibi yake Bi Sembe toka kuzaliwa kwake.
TUNI ni uchawi ambao unaabudiwa na watu waliopo duniani… wananguvu ya kutenga na kutengua kauli yoyote ya binadamu. Kuishi kwao kunategemea na chakula ambacho ni mwili wa Binadamu…
Swali ni Je; Kwanini MATUNI??

NA HII NI SEHEMU YA KWANZA!..
“Mjukuu wangu Tumaini bin Makungu, Leo ni siku pekee kabisa ambayo maelfu ya dakika yalisubiri kwa hamu kubwa. Tumaini nataka nikufanye moja kati ya nguzo kuu ya ‘TUNI’, najua hunielewi maana yake, ila usiache kunisikiliza.

Nilikua nimeishi maisha ya utwa wa kufa na kupona na wewe Tumaini.., sikuwa na nidhamu hii ya dunia ambayo wengi hujisifia kuwa wao ni wa muhimu sana kuliko sisi.
Mjukuu wangu, ‘Tuni’ ni moja ya dunia ambayo wachache wanaishi kwa ajili ya wengi. Dunia ambayo maamuzi kuchukuliwa mkononi ni moja kati ya sheria, kuua na kumbadilisha mtu ni jambo ambalo lipo na limewekwa katika sheria ya Tuni, mjukuu wangu, tuni ina katiba ambayo huongoza watu wa huko wasivuke mipaka ya dhehebu lao. Nashukuru Mungu tuni imenisaidia kusuluhisha matatizo yangu mbalimbali na kunifanya niishi kwa faraja hadi leo.

Natamani nikwambie mengi sana lakini leo nitajibu tu maswali macheche ambayo ulikuwa ukiniuliza kila siku, maswali yako yalinifanya nikasilike kwa mda, nicheke kwa mda, na kuna kipindi vyote vinatokea kwa pamoja, yaani sikitiko na furaha vinakuja kwa pamoja.

Mjukuu wangu, naomba nikupe kwanza ghadhabu ya muda mfupi kwa kukuambia ukweli kuusu uzao wako, yaani baba na mama yako mzazi. Najua hujawahi kuwaona.. Nataka nikuambie mjuu wangu.

Mwanangu, hapa nilicheka sana ulipokuwa unaniuliza mara kwa mara, “Yupi Baba…? Wapi Mama….?”, hasa pale ambapo kuna mda ulisahau kabisa na kuniita mimi mama yako.

“Hahahahahaha”, nacheka ya mwisho kwani ukweli wa maisha ya wazazi wako yako katika kifua chako Tumaini. Labda tu niseme kuwa, hukufanikiwa kukutana na wazazi wako toka umeeanza kujielewa sababu kubwa ni TUNI. Si kila fumbo nikufumbulie, mengine kazana mwanangu... Moyo wako utakufafanulia jinsi ambavyo maisha yanaenda. polepole tu utaju.

Tuma Mwanangu!!, Tuni ilinifanya nianze kumpoteza Baba yako pindi tu mama yako alipopokea mimba yako, nakumbuka katika Tuni ilikuwa ni zamu yangu kutoa mtu kwa ajili ya watu wengine, yaani niue mtu ambaye yu na muunganiko na familia yangu.

Basi nikaamuliwa nimtoe mama yako!, Lakini kwa kuwa na mimi nina nguvu nikageuza mambo na kushawishi kutolewa kwa baba yako. yaani baadaya kumtoa mama yako, nikaamua kumtoa baba yako mzazi, mda ukafika baba yako akapotea duniani, tukazika, tukasahau.

Hmmm!!!, Tumaini Usitikise kichwa mwanangu, utaelewa tu. Hiyo ndio Tuni. Basi tukaishi weee!, hadi mwaka ukafika ambapo nawe mjukuu wangu kipenzi Tumaini ulikuwa umeshazaliwa. Ikawa tena zamu yangu ya kutoa mtu katika familia, kila nikiangalia hivi sioni watu wengine wa kuwatoa zaidi ya Mama yako na wewe mjukuu wangu Tumaini ambaye bado moyo wangu ulikuwako upande wako. nilikuwa na nafasi mbili tu sasa. ufe wewe au mama yako.. Tumaini.!!.

Kwa safari hii, mbio zangu za kukutetea zikagonga mwamba. “Bi Ndaku” ambaye ni mkuu wa matuni hadi sasa alitoa oda ya kutolewa wewe. Nikagoma katakata lakini sikuweza kutengua.
Basi ukaletwa mbele ya Tuni, sadaka ikaanza lakini mtoa tuni akasema haikua sawa kutolewa mtoto ambaye bado hajajielewa vizuri na inaashiria kuwa mtoto huyo ananguvu kubwa ya kuiongoza Tuni, kwa maana ukitunzwa vizuri waweza kuwa kiongozi wa Tuni, yaani wewe Tumaini.

Basi ukaondolewa pale na zoezi la sadaka likaamia kwa mama yako. Lakini pia mama yako naye hakutolewa sadaka badala yake akatolewa mtu mwingine ambaye alifanya kosa lisilovumilika. Mama yako akauzwa koo nyingine.

Tulikuwa na tamaduni ya kubadilishana watumwa ambao wamenusulika kifo. mama yako akapelekwa koo nyingine ambayo kwa sasa ni mahasimu mno na koo yetu ya Tuni. Lakini duniani tulishamzika mama yako, hayupo!. Duniani Tumemzika na Tuni hayupo.. yu koo nyingine.

Ukawa mwisho wa wewe kuwaona wazazi wako, ulikuwa bado kachanga sana. Hakuna unachokielewa.

Toka hapo umeishi maisha ya kutomjua mama yako wala baba yako, wewe na bibi, bibi na wewe. Umekula vyakula vingi usivyovifahamu, vingi sana matuni….” BIBI Tumaini akaacha kuongea na akainamisha kichwa chini kwa aibu, akafungua sehemu ya kanga katika mwili wake na kufuta machozi, baadae akainuka na kuendelea na maongezi. aliendelea kuongea na mjukuu wake.

“TUMAINI umekula vingi bila kufahamu, siwezi taja vyote ila vingi ni mchanganyiko wa Damu za watu, nyama za watu, makohozi na hata vinyesi vya binadamu na hiyo ndio dawa ya Tuni mwanangu, uoni ulivyo imara sasa. Kila mtu anakushangaa, hehehehehe malezi ya bibi hayo...” BIBI Tumaini aliachia cheko fupi kabla ya kuendelea. Bibi Tumaini alibobea katika mambo ya furaha na huzuni kwa pamoja. alivichanganya vyote viwili bila wasiwasi. Alicheka tu.

“Sitaki mengi niongee mwanangu, ninachotaka ni kuwa nimekupa tu mwanga wa sehemu ya kuanzia, nakuacha mwanangu, yote utayajua kwa uwezo wako, wewe ni mtu mkubwa sana, hata mimi ni mdogo kwako ndio maana naamua kupotea ili nikupishe katika majukumu yako ya kuendeleza Tuni. Mimi ninapotea Tuma..

Labda niishie hapo kwa kukupa maneno machache kabla ya kukukaribisha kwenye TUNI. Mwanangu, Tuni ni Uchawi, tena uchawi ambao umeshindikana, haupo katika dunia hii ya karaha na shida nyingi.

Ukiwa huko ni raha tu mwanangu, hakuna kero wala nini, utacheza, utakula, utafanya kila kitu bure, sadaka ni kitu cha kawaida tu. Hakuna haja ya shule ukiwa TUNI, hakuna haja ya KANISA ukiwa Tuni, hakuna haja ya kubishana na mtu anaekukwaza; wote unawapoteza tu.

Sasa mwanangu naona koo langu lauma sasa kutokana na umri wa maneno mengi yaliyonitoka kwa pupa bila komo. Naomba niishie hapo kwa kukuambia jambo la mwisho na la uhakika zaidi. Mwanangu kuanzia leo mwanangu, jina lako ambalo litakujulisha uko uendako ni MATUNI, futa kabisa neno Tumaini ukiwa huko.....!. ukiwa Tuni wewe ni Matuni!.

ITAENDELEA..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi; “MATUNI” (02)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================

Naomba niishie hapo kwa kukuambia jambo la mwisho na la uhakika zaidi. kuanzia leo mwanangu, jina lako ambalo litakujulisha uko uendako ni MATUNI, futa kabisa neno Tumaini ukiwa huko.

ENDELEA SEHEMU YA PILI!...
… Hivyo nakubadili sasa kutoka TUMAINI hadi MATUNI. Jina lenye nguvu ya kusimamisha kila kitu duniani na kukuachia wewe njia ya kupita...” BIBI Tumaini aliongea kwa pupa kisha akashusha pumzi na kupunguza sauti.

“Mwanangu, siri zote zipo ‘KISHUMU’, Hii iko nje ya TUNI, itafute KISHUMU mwanangu, kwani ukweli ulioko uko ni kuwa baba na mama yao wako hai. Wanapata shida sana huko!.
Unanguvu mwanangu fanya liwezekanalo ufike mji huo, lakini wana Tuni wasijue, wakijua tu umekwisha, tumekwisha Tumaini… Doh!.”. BIBI Tumaini alikomea katika nukta hio, na kukwama kutoa neno lingine. Aliishia kutaja majina ya miji miwili inayokinzana, mji wa Tuni na mji wa Kishumu.

Bibi Tumaini alikuwa na mjukuu wake katika nyumba yao, alikuwa katika wasaa wa mwisho mwisho kumuaga mjuu wake kwa kumfahamisha mambo kadhaa ambayo hakuwai kuyafahamu kuhusu maisha yake.

Na rasmi alimkalibisha Tumaini katika jamvi la Tuni. Sehemu pekee ambayo Uchawi unaabudiwa kiliko chochote.

Naaam baada ya maneno machache ya Bibi Tumaini, sasa alianza kuonesha matendo tu, hakuongea neno lolote lile. Aliianza kwa kutetemesha maziwa yake yaliyo anzia kifuani na kushuka hadi kukalibia eneo la tumbo.

Hakika uzee wa bibi huyu ulionekana bila shaka ndani ya kaniki ile iliyoangaza, hakukuwa na nguo nyingine yoyote iliyositiri mwili wake zaidi ya mwanga hafifu wa kibatari, na mwanga utokao na matundu ya bati lake chakavu.. Bi Tumaini alikuwa uchi kwa ndani hakuvaa kitu kingine chochote kile.. ilikuwa kaniki tu inayoangaza..

Tumaini alionekana katika kona ya nyumba hiyo akiwa amevalia kanga moja tu nyepesi ambayo fito mbili za kanga hiyo zilizunguka katika mabega yake na kufungwa kwa nyuma, alikuwa kama mtu aliyezibwa mdomo kwa mda mrefu, hakupaswa kutoa neno lolote lile hadi kuruhusiwa. Ndani humo kulikuwa na mwanga hafifu wa mshumaa na mwanga mwingine mchache wa Mbalamwezi ambao ulifanikiwa kupenya katika matundu ya nyasi ya nyumba hiyo. Ulikuwa ni usiku.

Ngurumo za hapa na pale kutoka kwa Bibi Tumaini zilisikika. Alikuwa kama mwanamke ambaye yu katika muda wake wa kujifungua. Alilia kwa uchungu pamoja na mihemo ya ajabu kufuata. Kuna muda sauti ilitoka kama mbuzi na kuna muda mwingine sauti hiyo kubadilika kama kondoo jike aliyemaliza mafunguzi. Alitisha kwa kweli Bi Tumaini.

Lakini tumaini bado alijibanza katika kona hiyo huku akistaajabu kwa mihemuko ya Bibi yake bila kujua nini Bibi yake huyo anafanya. Tumaini alikuwa mpole sana, alitulia tuli kama mtu ambaye hana shida ya namna yoyote ile, Bado hakupata nafasi ya kusema. Mwili wake ulikuwa mzito mno kama mtu aliyebebeshwa dunia kutwa nzima bila kupumzika.

Bibi Tumaini baada ya ku-unguruma kwa muda mwishowe akaacha na kufanya zoezi ambalo lilikuwa jipya tena kichwani mwa Tumaini. Alifungua nguo nyeusi iliyokuwa karibu yake kwa muda mrefu, nguo hiyo ilikuwa na ungo wenye vitu vingi sana, si vubuyu tu na hirizi, pia mikonge kadhaa na matufe ya ajabu ajabu yalikuwepo. Aliifungua nguo hiyo.

Bibi Tumaini alichukua moja ya kibuyu kikubwa na kukimiminia kinywani kwake sekunde kadhaa, akanyanyuka na kusukutua kitu alichoingiza mdomoni. Baadae akayaachia “Puuu” hadi kichwani mwa Tumaini.

Akarudia tena zoezi hilo kwa ustadi uleule. Safari hii maji akayatemea pembeni mwa bega la kushoto la Tumaini, akafanya tena kwa mara ta tatu na kutemea upande wa kulia wa Tumaini. Tumaini alikuwa anatetemeka tu kwa ubaridi wa maji aliyokuwa ananyunyiziwa kutoka kwa bibi yake.

Bibi Tumaini akachukua kibuyu kingine kikubwa kinachofanana maumbile na kile kingine; akachanganyia vitu kadhaa vyenye asili ya unga unga na majani mabichi. Akakoroga kwa kutumia kidole chake cha shahada. Na hatimaye kunyunyiza mchanganyiko huo kichwani mwa Tumaini. Bado Tumaini alikuwa kama zuzu ambaye hakuna kitu alichokuwa anakielewa. Aliendelea kutetemeka tu.

“Hahahhahaha, hahahahaha….. haha.” Kilikuwa ni kicheko cha mwisho mwisho cha Bibi Tumaini. Alicheka kwa dharau huku akianza kurudi nyumanyuma pasipo angalia anakoenda. Alifanya hivyo taratibu bila kutoa neno lolote lile.

Taratibu alianza kupotea katika kona ya nyumba hiyo ambapo giza lilikuwa limeshamili sehemu hiyo. Wakati anaendelea kufifia kwa kutoonekana, macho yake bado yalikuwa usawa ambao Tumaini yupo. Huku ishara tu ya mkono wa kwaheri akiutoa kumpungia Tumaini. Bi Tumaini alikuwa anapotea.

Mwishowe Bibi Tumaini akapotea kabisa, bila kelele. Tumaini bado alikuwa kaweuka palepale alipoachwa na Bibi yake. Kichwa kilikuwa kizito sana kama mtu ambaye amebebeshwa mambo mengi sana. kichwa chake kilikuwa kinatembea angani kama upepo. Alikaa kwa muda sehemu hiyo pasi na kuongea wala kujinyosha kiungo chochote kile mara baada ya bibi yake kupotea. Alikuwa ameganda tu Tumaini kwenye ile kona. Na punde usingizi mzito ukumpitia. Akalala Tumaini.

ITAENDELEA….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi; “MATUNI” (03)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================

Mwishowe Bibi Tumaini akapotea kabisa, bila kelele. Tumaini bado alikuwa kaweuka palepale alipoachwa na Bibi yake. Kichwa kilikuwa kizito sana kama mtu ambaye amebebeshwa mambo mengi sana. kichwa chake kilikuwa kinatembea angani kama upepo.

Alikaa kwa muda sehemu hiyo pasi na kuongea wala kujinyosha kiungo chochote kile mara baada ya bibi yake kupotea. Alikuwa ameganda tu Tumaini kwenye ile kona. Na punde usingizi mzito ukumpitia. Akalala Tumaini.

ENDELEA SEHEMU YA TATU!...
TUMAINI alionekana katika giza zito lililochukua karibia chumba kizima. Sehemu ndogo tu kulikuwa na mwanga wa kijani ambao uliangaza kwa uchache sana. ilikuwa sio sehemu ambayo amewahi kufika.

Tumaini alishituka mno baada ya kutoka katika usingizi mzito na kujikuta katika hali ile. Alijikwakwamua kunyanyuka na kufanikiwa kukaa kitako huku akiruhusu macho yake kuperuzi kila pande ya chumba hicho. Alikutana na chumba ambacho kimepambwa na majani mengi yaliyosimama imara kama ukuta.

“Hallo” Matuni aliita kwa mashaka sana na kusubiri kuitikiwa kwa wito wake, lakini hakuna binadamu aliyethubutu kuitikia wito zaidi ya kusikia mwamgi wake tu ukijirudia.

Bado kichwa hakikuwa sawa, aliendelea kukizungusha kuangaza huku na huko na ghafla akukutana na wamama wawili waliosisima kama askari wakilinda geti la kutokea wafungwa. Mmoja akiwa upande wa kushoto na mwingine kulia.

Wote walivaa vitambaa vyeusi vilivyo gawanyika kuifunga miili yao kuanzia sehemu zao za siri na katika chuchu zao. Walikuwa kama wanawake wa utamaduni vile. Kichwani kwao kulikuwa na majani ambayo yalisimamishwa kama kiremba kwa mfumo wa taji. Kuonekana kwao kulisaidiwa na mwanga hafifu wa maajabu usio onekana wapi unatokea.

Hakukuwa na tatizo katika kuonekana kwao, lakini tatizo ni kutokea kwao; kwani kwa mara ya kwanza Tumaini anazinduka katika chumba hicho hakukuwa na mtu mwingine zaidi yake. Wamefikaje pale wakati hakukuwa na watu kabla?, swali hilo likabaki kichwani mwa Tumaini.

“Haloo nyie!” Tumaini aliita tena kwa ujasiri pasipo kuwa na hofu wala shaka. Bado zimwi la mwangwi liliibuka tena na kurudia sauti yake. Tumaini akawa anajivuta aweze kusimama pale alipo na kuwafuata wanawake hao, lakini alishindwa. Mwili ulikuwa mzito. Alishindwa kunyanyuka Tumaini.

“Nyie wadada!!” Alibahatisha tena. Safari hii aliita kwa sauti yake kali ambayo anatumia wakati wa kugombana tu na bibi yake.

Sauti hiyo ilizaa matunda, kwani baada ya mwangwi kuisha na wale wadada wakapotea mahali pale. Walipotea machoni mwa Tumaini. Ilikuwa ni ghafla tu hawakuonekana tena. Haikuwa ndoto kusema kwamba Tumaini atapikicha macho yake kuwaona tena la asha!. walipotea mazima.

Lilikuwa ni tukio ambalo lilitokea mbele yake. Alianza kugumia kwa kuomba msaada na kuleta kelele chumba kizima. Lakini hakuna aliyemsaidia. Zikaja nguvu za ghafla na akajikuta amesimama. Akasimama Tumaini!.

Hatua ya kutafuta sehemu ya kutokea ikafuata. Alikuwa analia kwa nguvu kwa kulalamika kama kuna msaada wa karibu. Aliangaza huku na huko lakini hakuona kitu zaidi ya ule mwanga. Akavaa roho ngumu kama ya Bibi yake na kusogelea sehemu hiyo yenye mwanga.

Naam! aliufikia, aliufikia mwanga huo wa maajabu. Kufanikiwa kuufikia mwanga huo akakutana na korido nyingi sana ambazo zimegawanyika kuelekea sehemu tofauti, korido zote hizo zilimulikwa na ule ule mwanga, ulikuwa mwanga wa kijani. Tumaini akasonga mbele kutafuta msaada. Akajichagulia korido yake moja na kusogea nayo.

Njiani hakukutana na mtu yeyote yule, na wala kitu chochote kile, lakini alifanikiwa kuona mikwaruzo ya kitu kama kucha au kifaa chenye ncha kali ambacho kilichubua katika pande za korido hiyo. Ilikuwa kama kuna watoto walijaribu kuchora baadhi ya herufi ambazo ziliwashinda kwa kukosa umahili wa kujua na kusoma na kuandika. Aliifuata mikwaruzo hiyo katika korido hadi kumfikia ukingoni. akafika mwisho Tumaini.

Tumaini akatikisa Kichwa kuashilia ni sehemu sahihi ambayo anatakiwa kwenda. Alikuwa anatafuta sehemu ya kutokea. Hakujua wapi yupo; na yupo kufanya nini. Akasimama kuangaza aende upande upi.

Akashangzwa kwa kuto kuona sehemu sahihi ya kutokea. Mbele yake ulikuwa ni mwisho wa korido hiyo na kulikuwa na uwanja mkubwa. Uwanja ambao hauna mwanzo wala mwisho unao onekana. Mwisho wa korido hiyo kulikuwa na kiza tu. Na chini yake kuna uwanja.

Tumaini akaangaza nyuma alipotoka na kurudisha tena macho mbele. Akaganda kwa kutafakari, amefikaje eneo hilo. Hakuwa na kumbukumbu kama kuna sehemu kama hiyo katika kumbukumbu zake ameshawai kufika. Akaangalia tena nyuma kuhakikisha anachokifikiri lakini safari hii kulisikika kishindo. Kishindo kilichotikisa korido hiyo kwa nguvu na kutuliza wenge la Tumaini.

Hajakaa sawa mwanga ambao ulikuwa unaangaza korido hiyo ukazima, ulikuwa ni ule mwanga wa kijani. Hofu ya Tumaini ikapanda mara dufu. Akajikuta anarukia katika uwanja uliopo mbele yake bila kupenda. Alipoangaza tena kuangalia ile korido hakuiona, korido ilikuwa haipo. imetoweka. Kilichopo mbele yake na nyuma yake ni uwanja tu. ulikuwa uwanja mkubwa mno usio na mwisho. Akaweuka Tumaini.

“Akha!.., Bibiii!!!” Aliita, lakini kimya.

Hakuna mtu; hakuna mwanga; hakuna kitu. Ni uwanja tu. Alianza kukimbia Tumaini huku akiita jina la bibi yake, alikimbia bila kufika mwisho. Alikimbia hadi kuchoka, lakini hakuna alichokutana nacho. Akatulia kwanza kwa muhemo wa kupumzika. Akayashika magoti yake kumsaidia kuhema kwa urahisi. Alihema Tumaini

"Whaaat!!, Kha!, Kha! Kha!...” Tumaini alishangaa mno mara naada ya kujiona yupo uchi. Hakuvaa kitu cha aina yoyote ile. Akainuka na kujitazama vizuri!, lakini hali ilibaki kuwa vilevile hakuna kilichobadilika. Tumaini alicheka!, tena alicheka haswa!, hakuacha kujichungulia na kucheka. Muujiza huo kwake alihisi ni ndoto tu iliyomshikilia bila kutoka.

Safari yake ikaishia hapo, hakuona la zaidi mahali pale. Aliona maruwe ruwe yanazidi. Hakujua toka mwanzo kama hana nguo hata moja. Hakulijua hilo Tumaini, alikuwa uchi kuanzia nywele hadi kucha za miguu. hakuna kilichomsitili. Kwa kuwa alikuwa pekeyake mahara pale hakuacha kucheka. Alihisi yupo kwenye njozi. njozi ya kweli ya kujitambua. Tumaini alicheka.

“Yaani mweee! Hahahahaha, Uchi!, sa nguo yangu kabeba nani?” Tumaini alicheka kwa sauti hadi akajishitukia kwa kuziba mdomo na mikono yake miwili. Bado macho yake yalimwambia ni usiku mno, hakuna mwanga. Hicho kilimsaidia kujiamini kwa kutembea bila nguo.

Tumaini bado alikuwa katika bumbuwazi la kuto kujua kwanini yupo pale na yupo akiwa uchi kabisa bila kuvaa kitu cha aina yoyote ile, hata miguuni Tumaini alikuwa hana viatu au kitu kilichomsitili. Akajishangaa mno kwa kuwa hakuhisi hali hiyo mwanzoni. Bado akawa katika tafakari.

Mungu sio Rashidi!, mbele ya Tumaini aliona mwanga mweupe ukiambaa ambaa, mwanga huo ulikuwa unaonekana hafifu sana lakini ulimpa Tumaini matumaini mengine ya kujua anapotakiwa kuelekea, hakujali na kuto kuwa na nguo akasonga mbele kutafuta msaada.

Alitembea sana bila kukutana na mwanga huo ukiwa halisi, kila akitembea bado alikuwa akikimbizana na mwanga huo, yeye akisogea na mwanga nao unasogea. Matusi yakamporomoka Tumaini. alitukana jinamizi hilo linalompoteza. Alianza kuikataa hali hile.

“Binti!, pita huku!” ilikuwa sauti iliyotoka kwenye giza, mara baada ya Tumaini kusimama. Sauti hiyo ikamwacha Tumaini akiangaza angaza mawimbi ya sauti hiyo imetokea wapi, hakuna mtu. Alisikia sauti tu, tena sauti ya kikongwe ambaye bila shaka amefikia tamati ya kupata mauti.

Jambo hilo lilimpa ujasiri Tumaini wa kutumbua macho yake kuangaza ni nani anamwonesha njia!, na njia inayooneshwa ipo wapi?. Hakuona Chochote tumaini. Alibaki kukodoa tu macho yake. Hakuambulia kitu.

“Wapuuzi nyie!, sa si mjitokeze?” aliongea kwa ujasiri lakini hakujibiwa na mtu.

Cha kushangaza mbele yake aliona ule mwanga aliokuwa anaufukizia upo karibu yake. Alihamaki mno. Ulikua sio mwanga utokanao na nishati, hapana!. Bali ni mwanga tu wa watu waliovalia mashuka meupe. Walikuwa wengi sana kiasi kwamba hakujuwa ni wapi wameanzia na wapi wameishia. Wote walikuwa wanachezesha vichwa vyao na kuongea lugha isiyoeleweka….

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi; “MATUNI” (04)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================

“Wapuuzi nyie!, sa si mjitokeze?” aliongea kwa ujasiri lakini hakujibiwa na mtu. Cha kushangaza mbele yake aliona ule mwanga aliokuwa anaufukuzia upo karibu yake. Alihamaki mno. Ulikua sio mwanga utokanao na nishati, hapana!. Bali ni mwanga tu wa watu waliovalia mashuka meupe. Walikuwa wengi sana kiasi kwamba hakujuwa ni wapi wameanzia na wapi wameishia. Wote walikuwa wanachezesha vichwa vyao na kuongea lugha isiyoeleweka….

ENDELEA SEHEMU YA SEHEMU YA NNE…
Tumaini bado alikuwa katika bumbuwazi, hapakuwa na umbali mkubwa toka sehemu ambayo umati huo umeanzia. Ilikuwa ni idadi kama ya hatua saba au nane tu. Akazipiga Tumaini. Tena alizipiga bila wasiwasi wowote ule. Bado alikuwa na shauku ya kutaka kujua ni wakina nani hao waliovalia nguo nyeupe, na mahali gani wapo.

“Ehy! Kaka, samahani eh!...” alimgusa mmoja wa watu aliyekuwako mbele yake, alikuwa amejifunika shuka kuanzia kichwani hadi miguuni.

Baada ya kumgusa na kumuongelesha mtu yule aliacha kutikisa kichwa kama walivyofanya wenzake. Mtu yule aliacha. Alikuwa kimya. Alitulia tuli kama maji mtungini. Aliwaacha tu wenzake waendelee kutingisha vichwa vyao kutoka kulia kwenda kushoto na kushoto kurudi kulia, huku wakiendelea kutokwa na maneno ya ajabu ambayo hayakuwa ya lugha aliyoifahamu Tumaini..

Kutulia kwa mtu yule aliyemgusa bila kusema lolote kulimpa shaka Tumaini. Akakumbuka kuwa bado yupo uchi wa mnyama. Hakuvaa chochote. Akatumia fursa hiyo kujisetiri kwa kuficha na mikono maungo yake ya siri kabla kaka yule aliyemshitua kugeuka.

Baada ya kuona kaka yule hakuna anachofanya zaidi ya kutulia tu, Tumaini alitumia tena fursa ya kumzunguka ili wakutane nyuso zao. Tumaini alijua watu hao wapo katika ibada na si rahisi kugeuka kama alivyodhani, akaamua kumjongea kwa mbele akiwa bado ameshikilia nyeti zake kwa mkono wa kushoto na chuchu zake kwa mkono wa kulia.

“Eti samahani…” alimshutua tena mtu yule ambaye bado alikuwa kimya tu. Kipindi hicho mtu yule tayari alikuwa ameshaacha kutikisika, aliendelea kutulia tu kaka yule.

Kwa kuwa tumaini alikuwa mfupi wa kina na mtu aliyemshitua alikuwa mrefu kumzidi, kiasi cha kutoweza kumwona vizuri usoni, Tumaini aliamua sasa kuachana na yule wa kwanza na kumshitua mwingine wa mbele yake ili pate msaada wa haraka. Akafanya hivyo.

Lakini bado shida ikabaki kuwa palepale wala haikubadilisha majira. Alitulia tu na yule mwingine aliyemstua. Kwa vile yule alikuwa mfupi, Tumaini akapata nafasi ya kumsogelea upande wa uso kumtazama kama anaweza kupata msaada.

Naye alikuwa kama wa mwanzoni kabisa, alijifunika shuka ilo jeupe karibia mwili mzima hadi kichwani. Naye baada ya kuguswa alitulia tu. Aliacha kuzungusha mwili wake na kichwa chake na kutulia tuli kama wa mwanzo na kuwaacha wenzake kuendeleza zoezi hilo. Walikuwa wengi sana watu wale.

“Bibiiiii…..!!” Lilikuwa yowe la tumaini mara baada ya kugundua kuwa mtu huyo aliye mbele yake hana mwonekano alio utarajia.

Tumaini alikutana na mtu ambaye hana sura. Upande ambao macho, pua na mdomo palikuwa hakuna chochote. Ni giza tu!, kulikuwa na giza usoni kwa yule mtu. Ni nguo tu ile nyeupe ndiyo ilimuonesha kama kiumbe cha kawaida lakini la asha!, Hakuwa mtu kabisa. Alikuwa ni kiumbe cha ajabu ambacho hakina sura.

Kitendo hicho kilimfanya Tumaini kusahau kama yupo uchi, aliitoa mikono yake katika kuficha nyeti zake na kuitumia mikono hiyo kupangua watu wale waliovaa mashuka meupe. Kila anayemgusa kwa kumpangua ili ampite alikuwa anaganda, yaani anaacha kutikisa kichwa na mwili kama alivyokuwa anafanya na kutulia tu kama sanamu. Wote walikuwa wana hali moja. wakaacha na hata ile hali ya kuongea lugha za ajabu. hali hii ilimwogopesha sana Tumaini.

Tumaini alikuwa mbio sana huku akiendeleza yowe la neno ‘bibi’ mdomoni mwake. Sikumbuki kama tumaini alifika mbele kwa kuwa watu wale walikuwa wengi sana hawana mwisho. Tumaini alinyong’onyea kwa kukosa nguvu na kujikuta anaanguka katikati ya watu wale wa ajabu.

Tumaini alijuwa ndio mwisho wake mahali pale, alikuwa amechoka sana na kuendelea kupumua kama mbwa baada ya kupata kitoweo kilichomtoa jasho. Alikuwa anatoa chozi Tumaini.

Aliendelea kuhema na kulilia uwepo wa Bibi yake ambaye alikuwa anamtegemea kwa muda mrefu. Kilio chake kizito kilifanya umati ule wote kuacha lile zoezi la kutikisha kichwa na miili yao, na sasa wote kutulia. Wote walitulia wima bila chembe ya sauti wala mtikisiko. Kuacha kwao kitendo hicho kikafanya sauti ya Tumaini kusikika kila kona ya mahali pale.

Hapakuchukua muda umati ule ulianza kujitawanya kuanzia sehemu ambayo Tumaini aliangukia. Walisogea kwa kuacha duara kubwa mno huku wakiwa kama wamemzunguka Tumaini. Kusogea kwao kulimfanya Tumaini kunyamaza. Aliacha kulia Tumaini. Akawaona tu watu wale wamesogea na kusimamia mbali na yeye. Sasa alipokuwepo Tumaini kulikuwa na duara ambalo katikati alikuwa yeye tu.

Sijui alipata wapi nguvu Tumaini, alinyanyuka mahali pale na kusimamia wima, Tumaini alisimama tu bila kuambiwa na mtu. Alionekana anashinikizwa kufanya kitendo kama kile. Alikuwa anafanya bila kupenda Tumaini.

Alinyanyuka na kusimama wima Tumaini, kilio chake kilikata ghafla. Baada ya hapo, akafumba macho yake na kisha kukunja ngumi mikono yake yote miwili ikiwa imeining’inia chini karibu na kiuno chake, alikuwa anafanyishwa hivyo Tumaini. ilionekana dhairi shairi kuwa matendo hayo Tumaini alikuwa naafanya kinyume na lidhaa yake. alifanya tu. Bado alikuwa uchi Tumaini.

Baada ya mda mchache mwanga mweupe ukaongezeka mahali pale. Kusini mwa duara lile kukatengenezeka njia, njia ambayo iling’aa haswa kwa mwanamke ambaye anapita. Alipita mwanamke ambaye bila shaka ndiye mkuu wa umati ule.

Alipita hadi kumfikia Tumaini. Alianza kwa kumzunguka tu. Alimzunguka Tumaini kwa takribani dakika tano. Tumaini alikuwa amefumba tu macho, mwili ukiwa wima kuelekea kusini mwa duara lile. Alikuwa hajielewi, kwa maana hata hakushitushwa na ujio wa mwanamke yule anayeendelea kumzunguka.

“MATUNI!, tumekusubiri kwa muda sasa kiongozi wetu. Karibu sana mpenzi!” maneno hayo yalimtoka mwanamama yule wa lika kumwendea Tumaini ambaye baada ya kusikia maneno hayo akazinduka. Akafumbua macho Tumaini.

Mbele yake alisimama mwanamama mwenye mapembe mawili makubwa kichwani, alikuwa na masikio makubwa mno mwanamke huyo. Alikuwa anatisha. Yote yalionekana katika mwanga ule mweupe kupita maelezo.

“MATUNI!!; TUNI yako ipo salama kabisa!. Tunategemea utakuwa kiongozi bora hapo baadae!” yule mama mwenye mapembe aliendelea kuongea pekeyake akiwa bado anaangaliana na Tumaini. Tumaini ambaye alikuwa anatambulika kwa jina la Matuni na yule mwanamama.

Tumaini hakuongea chochote kile bado alikuwa amefumbua macho yake na bado mikono yake alikuwa amekunja ngumi zilizobana vizuri kiuno chake. Tumaini alionekana tu akitikisa Kichwa kuashilia hayupo tayari na maneno ya yule mama. Alitikisa Kichwa kutoka kulia kwenda kushoto polepole kukataa. Alikuwa anakataa Tumaini.

“Ah! Mama, usitake kumaanisha haupo tayari!, Bora ukubali mwenyewe kuliko Tuni ikulazimishe. Tunajua unanguvu sana Matuni. Lakini fanya kukubali mama. Usitake kushindana na Tuni, eh! Mama.,” yule mama alionekana kumbembeleza Tumaini. Lakini bado tumaini aliendelea kutikisha Kichwa chake bila kuacha. Alikataa Tumaini.

Kitendo hicho kikafanya mama yule kukosa amani, akaangalia kushoto na na kulia na kurudisha macho kwa Tumaini. Ishara hiyo ikafanya ule umati uanze tena kutikisa vichwa yao kutoka kushoto kwenda kulia. Wote walifanya kwa umoja na kwa sasa walikuwa wanaunguruma kama wanyama tofauti tofauti wa mwituni.

Tumaini akafumba macho yake na kuvimba kidogo, alitanua kifua chake na kuanza kukoroma kama simba. Kitendo hicho kikafanya umati ule utulie na kuacha vile vitendo walivyokuwa wanafanya. Ilikuwa ghafla tu wakatulia. Tumaini akaendelea kukoroma na sauti yake ambayo ilikuwa kali na nzito kiasi cha kuumiza masikio ya yule mama mwenye mapembe.

Mama yule akatumia nguvu zake kumtoa Tumaini mahali pale, alijua Tumaini akipandisha hasira zake mahali pale, basi ataumiza wengi sana. Kimazingara akamzimisha Tumaini na kumrudisha alipotoka. Yule mama alikuwa alikuwa zaidi ya Mchawi. Tumaini hakufua dafu kwa wakati ule. Akapotea Tumaini kutokana na nguvu za yule Mama….

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi; “MATUNI” (05)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================

Tumaini akafumba macho yake na kuvimba kidogo, alitanua kifua chake na kuanza kukoroma kama simba. Kitendo hicho kikafanya umati ule utulie na kuacha vile vitendo walivyokuwa wanafanya. Ilikuwa ghafla tu wakatulia. Tumaini akaendelea kukoroma na sauti yake ambayo ilikuwa kali na nzito kiasi cha kuumiza masikio ya yule mama mwenye mapembe.

Mama yule akatumia nguvu zake kumtoa Tumaini mahali pale, alijua Tumaini akipandisha hasira zake mahali pale, basi ataumiza wengi sana. Kimazingara akamzimisha Tumaini na kumrudisha alipotoka. Yule mama alikuwa alikuwa zaidi ya Mchawi. Tumaini hakufua dafu kwa wakati ule. Akapotea Tumaini kutokana na nguvu za yule Mama….

ENDELEA SEHEMU YA 5…
**********
NDANI ya nyumba ya Bibi Tumaini, alikuwa Tumaini kitandani. Tumaini ambaye alionekana yupo katika usingizi mzito mno, alikuwa anaota Tumaini; alikuwa katika mahangaiko makubwa mno. Alikuwa anacheza cheza tu katika kitanda cha kamba kiasi cha kukitikisa kitanda hicho.


Sauti za mihemo na kelele za kitanda hicho zilifanya chumba kizima kizizime kwa fujo. Tumaini alikuwa anaangaika kitandani hapo, alikuwa kama mtu ambaye anapigisha degedege. Mikono, Miguu na kifua chake vilikuwa vinatetemeka mno. Alikuwa kama anajilazimisha kuamka Tumaini.

Baada ya muda mfupi akaamka Tumaini, alitoka katika zimwi lile la usingizi mzito. Usingizi aliopigana nao mda mrefu. Kuamka kwake kulifanya akae kitako kitandani hapo huku akisubiri kasi ya mapigo ya moyo wake ipungue. Tumaini alikuwa anavuja jasho haswa.

“Ndoto gani hizi jamani!” akalalama tumaini huku akijikagua mwili wake. Alikumbuka kuwa kwenye ndoto alikuwa uchi.

“Oooph!, ni ndoto” Tumaini alijipa moyo baada ya kujiona mwili wake umefunikwa kwa kanga. Kabla hajatoka kitandani hapo akavuta taswira ambayo ilimtokea tena kabla ya ndoto. Alikumbuka kuwa kuna muda aliagwa na Bibi yake, na kupotea katika mazingira ya ajabu.

Tumaini hakataka kuhakikisha kwa kwenda kumchungulia Bibi yake anapolala. Akashuka katika kitanda hicho cha kamba na kunyanyuka. Akapikicha macho yake na kujifunga vizuri kanga yake. Lakini kabla hajasogeza mguu akagundua kuwa yupo ndani ya chumba cha bibi yake. Tumaini alilala katika chumba cha bibi yake. Alishangaa.

“Nimefikaje chumbani kwa Bibi mimi wakati nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa katika hii kona?” Tumaini alijisemea mara baada ya kutoka hadi sehemu ambayo fikra zake zilimtua ndio sehemu ya mwisho yeye kuwepo. Alipotaka kuruhusu mawazo ya kumuwaza Bibi yake kichwa kilimuuma Tumaini. Mbio zikampeleka hadi chumbani mwake. Moja kwa moja akaingia hadi ndani.

“Khoho…, konhoo khho khho khhhonho..” Tumaini alikohoa mara bada ya kuona moshi unamwandama. Chumba kizima kilikuwa na moshi.

Wakati anaendelea kuhangaika kuweka sawa pumzi na macho yake. Alikuja kuhamaki tena chumba chake kilikuwa na maji. Maji yaliyotanda chumba kizima kama bwawa. Tumaini aliwehuka. Alikuwa chizi. Alihisi ndoto ile ya usiku bado inaendelea.

“Nini hiki!” Tumaini hakuacha kushangaa, akapiga hatua na kanga yake, na kutoka hadi nje. Bora hata ya ndani kulikuwa na maajabu yaliyovumilika. Lakini siyo aliyoyakuta nje. Kulikuwa na jambo linguine nzito sana.

Tumaini alikuta watu wengi nje. Alikuta watu wengi sana wakilia. walikuwa wanalia msiba. Akashangaa akiwa na kanga yake mlangoni. Aliwatazama watu wale waliokuwa bize kulia na kuendelea kufanya shughuli zilizofanana na za mazishi.

“Bibi Sembe, Bibi Tumaini, Bibi wa mtaa, kiongozi wetu!. Mbona mapema hivi Bibi?, umeondoka mapema ili umtese mjukuu wako?. Jamani!! Amebaki na nani Tumaini…” kilikuwa ni kilo cha jirani mmoja ambaye alithibitisha kifo cha Bibi yake Tumaini.

Tumaini alishindwa kufanya jambo lolote lile. Akabaki mlangoni tu kuwashaangaa wanakijiji wale walishikwa na uchungu wa msiba ambao hata yeye mhusika hakuujua. Alibaki kuwahurumia tu.
------
Bi Tumaini amabaye alikuwa maharufu sana kwa jina la Bibi Sembe, jina ambalo alilipata kutokana na historia ya yake mtaani hapo. Bi sembe alikuwa anatabia ya kwenda kuomba unga kwa majilani zake katika kila nyumba, leo akienda kwa Bibi Semeni, kesho kwa Bi Ndaku, siku ifuatavyo kwa Mama Juma alikadhalika kwa Binti charuka.

Alikuwa ombaomba Bi Tumaini. Na ni unga tu utokanao na Mahindi maharufu kwa Sembe ndio alikuwa akipita kuomba Bibi huyo. Jina hilo alilitumia hadi katika shughuli zake za ushirikina. Historia hiyo ya kupita kuomba unga wa sembe alikuwa nayo toka uchangani hadi kuzeeka kwake Bibi Tumaini. Sasa ulikuwa mwisho wake, watu walikuwa wanamlilia.
------

KUTOKANA na aibu ya kutovaa nguo zenye maadili Tumaini akarudi ndani, lengo ni kutafuta nguo nzuri ambayo itampongeza kwa mazuri. Kama kawaida ya mabinti wenye rika kama la Tumaini, rika ambalo ndio kwanza wanaanza kushudia upembukaji wa binadamu unavyotokea.

Rika ambalo ukikosea hatua moja wapo unaangukia katika zambi ya kukubali kila mwanaume. Rika chafu na lisilo na uvumilivu wa kufika uzee. Rika maharufu kwa jina la barehe. Tumaini alirudi ndani kuvaa vizuri. Alirudi ndani na kukosa nguo ya kuvaa.. akaamua kutoka tena na kanga yake.

Kurudi kwake ndani kulikuwa kosa Tumaini, kwani hakuna alichokikuta nje baada ya kutoka tena. Hakuwaona tena wale watu ambao walikuwa wanalia msiba wa bibi yake. Tumaini akarudi tena ndani ili atoke tena nje kushuhudia kama aliyoyaona mwanzo yatatokea tena au la!. Lakini hora!, aliweweseka Tumaini. Hakuwai kuyaona maajabu hayo toka azaliwe.

“Huu mtaa umejaa watu wachawi sana!, yaani!!” Tumaini alisha lishwa sumu na bibi yake tokea yu mtoto. Alikuwa ngangali mno kiimani. Aliaminishwa katika uchawi. Akafanya zoezi la kurudi katika kile chumba chake ambacho mwanzo kulikuwa na moshi na maji mengi.

Nako alikuta hali ni salama tu, hakuna moshi wala yale maji. Chumba kilikuwa kisafi sana, kila kitu kilikaa kwenye mstari. Tumaini akacheka kufa. Alicheka sana aisee. Haikujua mustakari wa maisha yake yanayoendelea. Haikujua kama tayari amekabidhiwa Tuni na bibi yake. Haikujua kama yeye ndiye kiongozi mkubwa wa wachawi anayefuata. Haikujua hilo Tumaini, alichojua yeye ni kucheka tu, alicheka kwa maluweluwe yanayoendelea kumkuta. Alicheka Tumaini….

ITENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi; “MATUNI” (06)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================

NA huko alikuta hali ni salama tu, hakuna moshi wala yale maji. Chumba kilikuwa kisafi sana, kila kitu kilikaa kwenye mstari. Tumaini akacheka kufa. Alicheka sana aisee. Haikujua mustakabariri wa maisha yake yanayoendelea.

Haikujua kama tayari amekabidhiwa Tuni na bibi yake. Haikujua kama yeye ndiye kiongozi mkubwa wa wachawi anayefuata. Haikujua hilo Tumaini, alichojua yeye ni kucheka tu, alicheka kwa maluweluwe yanayoendelea kumkuta. Alicheka Tumaini….

ENDELEA NA SEHEMU YA 6!...
“Bibi ametoweka!, Sawa!, Ndani kwangu mara yanajaa maji, Sawa. Niliwaacha watu hapa wanalia msiba, eti sekunde hii wote hawapo!, Hehee!!, kazi ipo. Kazi ipo nasema!”. Alibaki kuegema katika mlango mbovu wa nyumba hiyo. Lakini ghafla masikio yake yakacheza!.

“Ngoma!” neno hilo likajaa kinywani mwake, akataka alitapike. Alisikia kuna mlio wa ngoma maeneo ya jirani.

“Wapi huko” akajijibu mwenyewe!. Tumaini alikuwa kama mtu ambaye amechanganywa hivi. Matukio kadhaa yalikuwa yanapita bila mpangilio. Mengine ya kustahajabisha lakini anayachukulia poa tu. Huyo ndio Bibi Sembe!. Alimfundisha kutoogofya chochote kile.

“Uwiiii jamani Semeni!!” likamtoka yowe lililoambatana na jina la mtu. Mbio zikamtoka bila kuangalia nguo aliyovaa, alichochora hadi kumfikia sehemu ambayo ngoma hiyo unadundikwa. Akaweka kituo.

Naaam!, Tumaini alikuta umati mkubwa sana, wote walizunguka kitu katikati. Walikuwa wanaangalia kitu. Akawasogeza hadi kufanikiwa kuvuka mbele kabisa. Tumaini akashuhudia alichokiamini. Alichokihisi mwanzo kikatokea kweli.

“Nilijua tu!” alisema kimoyomoyo mara baada ya kuona mgomvi wake Semeni anaozwa bila kutarajia na aliyekuwa Bibi yake.

Ukizungumza suara la ugomvi kuto isha, basi zungumza kuhusu Tumaini na Semeni. Hawajawai kupendana hata kidogo. Damu zao ziligeuka kila moja pande yake huku ya Tumaini magharibi na Semeni Mashariki. Walichukiana toka watoto bila sababu. Yaani chuki tu!. Bila shaka Bi Sembe alifanya yake pia.

“Msyuuuuuh!” akasonya Tumaini na kurudi alikotoka. Moyoni alijutia kwa nini alikimbilia tukio kama hilo na kuacha kufanya mambo mengine. Akajipenyeza na kutoka sehemu ile. Akaishika njia tena taratibu kurudi kwake.

“Ivi Bi Sembe, ulinizaa ili niweje mimi?” Tumaini alijikuta anajiuliza maswali kana kwamba yupo na bibi yake njiani.

Alikuwa anamlaumu bibi yake sababu za kumzaa maana haoni cha maana alichowai kufanya toka ajitambue. Mdogo mdogo aliivuta nguo yake isiporomoke kwani hakuifunga, aliishikilia tu. Tumaini alikuwa na mambo jamani. Inaonekana dawa za Bibi yake bado hazijamtoka kichwani. Ndizo zinampa mawenge..

“Tuma…!, Tuma eh!” Sauti ya kiume ikasikika!. Ikafanya Tumaini asimame na kutabasamu. Alitabasamu tu Tumaini bila kuangalia aliyekuwa anamuita. Alishajua tayari, unacheza na uchawi bhana!. Alijua Tumaini nani anamuita.

“Tumaa! Ndio nini hiki sasa!” alihoji yule aliyekuwa anamuita.

“Boscoo!, kwani imefanyaje!” Tumaini aliivuta kanga yake na kuivaa vizuri sasa. Aliisonga songa tu kuanzia kiunoni hadi kifua kwake.

“Mhhh!, toka lini umeanza kutoka nje hivi Tuma!.” Aliuza Bosco baada ya kushangazwa na mvao wa ajabu wa Tumiaini.

“Ah! Boscoo!, usiongelee ilo bhana, vipi kwema!” alipotezea Tumaini. Alionekana yupo na mambo mengi sana Tumaini kinyume na alivyo kila siku. Sijui alilishwa nini Tumaini.

“Kwema wapi!!, pole!”

“Umeanza!!, hahahahahaha..!” alicheka Tumaini na kumshangaza Bosco. Alicheka kupewa pole.

“Mhh!!, wewe vipi leo Tuma!” aliboreka Bosco na kuanza kukasilika. Aliona Tumaini yupo kwenye matani.

“Hahahaha, nakucheka wewe!, pole ya nini sasa?” alieleza sasa Tumaini sababu ya kucheka.

“Pole kwa msiba wa bibi!” Bosco akamalizia pole yake.

“Bibi??!” aliuliza Tumaini. Alionesha taarifa hizo ni ngeni masikioni mwake. Alikaa kimya kwa dakika bila kutikisika. Kichwa kikionesha kutafuta kitu kando ya miti iliyopo mbele yake. Hakujibu kitu Tumaini. Akaanguka chini ‘Puuh!’.

“Alaaah!, Tumaa!.., we Tuma!!.” Bosco alimkimbilia Tumaini alipoanguka pale chini. Alihisi kuanguka kwa Tumaini, basi ni kutokana na mshituko wa taarifa ambayo Bosco alimpa. Alijua fika Tumaini alimpenda sana Bibi yake kuliko mtu mwingine yoyote Yule.

“Mh!, Jamani mpenzi!” alilalama kwa masikitiko Bosco huku akikusanya kanga ya Tumaini iliyojimwaga pembeni na mwili. Hakuvaa kitu ndani Tumaini. Alimwachia Bosco msala wa aibu kushindwa kutazama anachokiona.

--------------
Tumaini ni msichana pekee ambaye amelelewa na Bibi yake tu. Kutokana na Fununu za hapa na pale inasemekana kuwa wazazi wa Tumaini wote wawili walishafariki muda sana. Tena Tumaini mwenyewe hakushuudia vifo vya wazazi wake. Hii ndio sababu ya yeye kuchanganya majina ya Mama na Baba, majina yote hayo alimwita Bibi yake ambaye ndio humwona kila kukuchapo.

Tumaini katu hakuwai kumwona Bibi yake Bi Sembe kujishughulisha na kilimo, lakini walikula, hakuwa mfanyakazi wa kanisa, lakini walisali. Hakuwa na akili za darasani lakini aliongoza. Aliongoza wanakijiji wenzake. Wote walisalimu amri kutoka kwa Bibi Tumaini. Yote aliyaongoza katika kuamini uchawi. Bi Sembe alikuwa mchawi wa aina yake. Na sasa ameshamkabidhi Tumaini kushika nyazifa zake. Tumaini Yule tunayemjua sisi kama Tumaini au Tuma, siye yeye tena. Kwa sasa ni Matuni. Ita kwa jina kubwa. MATUNI!.
---------------

Akamkokota Tumaini na nguo yake moja hadi nyumbani kwake. Nyumbani kwa Bibi Sembe. Nyumba ambayo hata Tumaini tu bado haijamkalia sawa. Nyumba hiyo ndio kwanza ilimkalibisha Tumaini katika Uchawi.

Bosco akammwaga Tumaini karibu na mlango na nyumba yao. Akiwa na mawazo mengi kipi cha kufanya kumzindua Tumaini, Tumaini aliamka mwenyewe. Aliamka Tumaini. Tena aliamka na Tabasamu.

“Tuma!” aliita Bosco. Lakini Tuma hakujibu chochote.

“Dah!, Pole sana, nilikuja kukuona mpenzi wangu.

“Hhahahaha!, usijaliii..!” alicheka tena Tumaini. Bosco naye akatabasamu tu, mana hana la kufanya. Atahuzunika wakati mwenye msiba mwenyewe hana habari na huzuni?.

“Boscoo!” aliita Tumaini akimwangalia Bosco kwa huba la Mahaba.

“Naona leo umeweka rekodi eh!, hahahaha!” aliendelea Tumaini.

“Ah!, ya nini tena?”

“Kuja hapa!!, katu hujawai gusa nyumba hii, hahaha!” aliendelea Tumaini huku akimsogelea Bosco na kanga yake ambayo ananing’inia nayo tu, haikufungwa vizuri.

“Sa Bibi Mkwe naye si unajua tena. Mkali kama nini kwa Binti yake!”

“Weeh!, kwani ashawai kukuambia au kukugombeza kitu kuhusu mimi?”

“Hajawai, niseme ukweli tu hajawai. Ila nilikuwa namwogopa balaa!”

“Ahya!, kazi kwako sasa B wangu!. Nafasi hiyo”

“Nafasii…” aliwaza Bosco na kutulia. Hakuendelea.

“Leo tulale Pamoja!” aliongea Tumaini akiinua kidevu cha Bosco.

“No!, anhaa!, hapana Tumaini. Siwezi kabisa mimi. Labda siku nyingine. Nakuhaidi!.” Alinyanyuka Bosco. Hakutaka kabisa wazo la Tumaini. Kwani alimshangaa mno Tumaini. Kulala wote? Kuanzia lini.

“Ooh!, Sawa.. najua Sababu!.” Aliongea Tumaini.

“Tuma, unamjua Mama yangu lakini. Kwanza sijaaga kama nimetoka. Pili hapendi kabisa kusikia mimi nimekuja huku. Nakuhaidi, siku nyingine tutakuwa wote.”

“Nawe na Mama yako!, aya nambie lini waja?”

“Daah!, yani upo kweli na hilo suala?, mi naogopa Tuma.”

“Anha!, Hutaki!”.

“No, Basi tufanye Jumatatu!, nikitoka Shule nakupitia jamani.” Alinyanyuka Bosco.

“Ok, fanya juma-tatu njo asubuhi. Nataka twende wote shule”.

“Hhahahahahaha hahaha!” alicheka sana Bosco.

“Wewe!, huyuhuyu Tuma. Uende Shule. Aaagh!, hahaha we si ulishaacha shule wewe?”.

“Nimekuambia jumatatu njo mapema nipitie.” Alilazimisha Tumaini. Tumaini alikuwa na Takribani wiki nzima hakukanyaga shule. Jambo ambalo lilifanya wengi kujua ameacha kusoma. Na leo alihaidi kurudi tena shule.

Tayari walikubaliana. Bosco akakwepa kishawishi kutoka kwa Tumaini na kuomba ruhusa ya kuwai kwao. Alimkwepa Tumaini ambaye ni mfupi kwa kimo, rangi kama kale kajua ka jioni kanakowai kutokea na kuwai kutoweka. Ni mweupe wa asili Tumaini.

Bosco alinyanyuka na mawazo kedekede, kauli za Tumaini zilimchanganya Bosco, katu hakuwai kusikia kutoka kwa Tumaini suala la kulala nae pamoja, pia alishangaa Tumaini hana mawazo kabisa kuhusu bibi yake. Hii ilimshangaza mno Bosco. Akashika chochoro na kwenda kwao…

Tumaini naye alijikokota hadi ndani, alikuwa na hali tofauti mno. Hakuona njaa, ila alijiwa na hali mahututi sana. Mwili wake ulikuwa na washawasha wa mapenzi. Alipata hamu ya ghafla. Mwili ulimpelekesha hadi kitandani. Akajitupa kwa uchovu. Kanga aliyovaa ilishavulika mapema toka yupo mlangoni. Alikuwa uchi wa mnyama Tumaini.

Raha ya ajabu ikamjia Tumaini, alikuwa hajielewi kabisa yani, alikuwa anafanya matendo nje na upeo wake. Tayari alishagawanya mikono yake katika majukumu tofauti mkono wa kulia ukiwa kinywani, uliendelea kuchezea lipsi na meno mdomoni mwake.

Mkono wa kushoto, moja kwamoja alikuwa unapapasa sehemu ya maziwa yake yaliyoanza kuchomoza kwa ustadi, aliona haitoshi tayari alishafika katika sehemu yake ya haja. Akipapasa na kuacha, akaendelea hivyo hadi alipohisi kidole chake kimoja kipo ndani ya uke wake……

ITAENDELEA…….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi; “MATUNI” (07)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================

Raha ya ajabu ikamjia Tumaini, alikuwa hajielewi kabisa yani, alikuwa anafanya matendo nje na upeo wake. Tayari alishagawanya mikono yake katika majukumu tofauti mkono wa kulia ukiwa kinywani, uliendelea kuchezea lipsi na meno mdomoni mwake.

Mkono wa kushoto moja kwa moja alikuwa unapapasa sehemu ya maziwa yake yaliyoanza kuchomoza kwa ustadi, aliona haitoshi tayari alishafika katika sehemu yake ya haja. Akipapasa na kuacha, akaendelea hivyo hadi alipohisi kidole chake kimoja kipo ndani ya uke wake……

HII NI SEHEMU YA 7.
Tumaini bado alitamani raha ile anayoendelea kuhisi isiache na badala yake iendelee hadi majira yasiyo julikana..

Mchezo ukamnogea Tumaini hakuwai kufanya hivyo katu katika maisha yake. Sasa akapata ujasiri wa kuingiza na kutoa kidole chake ukeni. Akawa mzoefu sasa. Akaongeza na kingine na kuwa viwili. Hakuhisi chochote zaidi ya majimaji yaliyompa raha ya aina yake.

Toka alale kitandani Tumaini hakujaribu kufungua macho yake kuona uozo aliokuwa anaufanya. Alifanya hadi kuchoka. Mwishowe akakosa nguvu na kujikuta yupo katika usingizi mzito. Alilala tena Tumaini.
………………..

“Mwanekelengee Ehyi, Mwanekelengee!, Mwanakelengee Eoiia Mwanakelenge!” zilikuwa ni sauti za watu wakiimba kuzunguka mti mmoja mkubwa mno. Chini ya mti huo alikuwepo Tumaini aliyelala fofofo. Waliendelea kumzunguka huku wakiimba nyimbo za lugha isiyoeleweka.

Kulikuwa na baridi iliyopuliza mwanana kabisa kusindikiza usingizi wa Tumaini. Msafara wa waimbaji hao alikuwapo na yule na Mama mwenye mapembe. Alishika mti wake kama kawaida. Wote wakiwa wamevalia kaniki zao kuanzia mabegani hadi katika kingo za miguu yao.

“Mwanekelengee eiio Mwanekelengee!” waliendelea kuimba hadi pale waliposimamishwa kwa ishara ya mkono, yule Mama mwenye mapembe aliwaonyeshea mkono kuwasimamisha. Wote wakatulia kimya.

Akatoa ishara ya kuomba kitu, akapewa. Yalikuwa maji katika moja ya chombo mfano wa fuu la nazi. Akapuliza maji hayo kama mara tatu hivi kisha kuyazungusha na mikono yake kama duara. Yaani aliyapeleka kuanzia Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini. Kisha akafanya hivyo kwa kuanzia na Kusini kurudi hadi Mashariki. Haikutosha kabisa. Tayari Mama huyo alipitisha kifuu hicho katika sehemu mbalimbali za mwili.

Alianza shingoni. Akazungusha shingo nzima, akaja kiunoni, akazungusha kiuno kizima, mwishowe akaingiza katikati ya miguu yake miwili na kupokelea fuu ule upande wa nyuma ya makalio yake. Wapambe wake bado walikuwa kimya. Waliacha hadi kuzunguka kutazama mkuu wao anafanya nini. walisubiri agizo tu.

Mama yule mwenye mapembe alimimina maji yake mkono wa kushoto na kumwagia alipolala Tumaini. Alifanya hivyo mara kadhaa hadi alipoona inatosha. Alipomaliza akampa mpambe wake mmoja fuu hilo lenye maji.

“Mwanekelengee iiio Mwanekelengee!” alianzisha tena nyimbo ambayo mwanzo aliisitisha, wote waliopo pale wakaitikia na kuendelea kuimba nyimbo hiyo. Bado Tumaini alikuwa amalela tu.

Zoezi la kuimba likasitishwa tena aliponyoosha mkono kuwa ishara kuwa waache kuimba. Wote wakasimama wima. Waling’aa sana kwa unga wao walioupaka usoni na kaniki zao. Walikuwa kama watoto waliotoka kuogeshwa na kunyimwa chakula.

“MATUNII!!!”, aliita yule Mama mara moja kisha kusikilizia kama mwitiko wake umefika sehemu sahihi. Kimya.

“Matuni…!” akaita tena, lakini hora!. Kimya.

“Mwanekelengee uuuo, Mwanekelenge!,… Matuni!!” aliimba mwenyewe na kuita tena.

Naaam!, sasa Tumaini alishituka toka katika usingizi wake na kujikuta yupo katika alaiki ya watu. Akainuka na kukaa kitako, mwili ulikuwa sio wake, kwa maana ulilegea na kukosa nguvu. Hakuonesha kutaka kuongea badala yake kuzubaa tu.

“Ha ha ha ha hahah” akacheka yule Mama na kufanya wengine wote pale nao wacheke. Hawakujua nini kimemchekesha mkubwa wao lakini nao walicheka.

“Karibu tena katika Tuni Matuni.” Aliongea kana kwamba alikuwa anamkalibisha Tumaini katika koo yao. Mama huyo alikuwa na uso wa furaha licha ya kutisha na mapembe yake. Leo alimuweza mapema Tumaini. Alimdhibiti vilivyo Tumaini.

“Matuni!, wewe ni Taifa letu sasa. Hakika umepokea kwa azma kubwa sana Tuni yetu. Bado unamafunzo machache tu uwe mtu kamili. Mkuu wa Tuni hadi kustaafu kwako. Hilo ndio ilikuwa ndoto ya bibi yako. Karibu sana Matuni!.” Aliishia hapo Mama yule na kuomba tena Kifuu kile chenye Maji. Akamimina katika kiganja chake na kumwagia tena Tumaini.

Tumaini hakuongea wala kuonesha ushilikiano wowote ule, alikuwa anayumba yumba tu kutaka kudondoka na asidondoke. Hakuna alilokuwa anaelewa sehemu ile.

Mama yule akaanzisha tena nyimbo yake na kuanza tena kuzunguka, wote walifanya hivyo. Taratibu wakazunguka mti huo ambao Tumaini aliku chini yake. Ulipofika mzunguko wa tatu, Tumaini akasimama. Akasimama Tumaini bila kutegemea, tayari alipiga hatua walipo wenzake. Mdogo mdogo akajiunga nao, polepole akaanza kuzunguka kama walivyofanya wenzake.

Wote walikuwa nyuma ya mama yule mwenye mapembe na Tumaini akiwa wa mwisho. Tumaini peke yake ndio alikuwa hatoi sauti katika kuimba, ila alicheza na kuzunguka mti huo. Ulipofika mzunguko wa tano, wote wakatoweka. Pakabaki giza tu sehemu hile. Hapakuwa na mtu.
----------

NDOTO hiyo ilimtoa Tumaini kitandani. Ulikuwa ni usiku wa manene sasa, kelele za chura ndizo pekee zilibaki kulinda nyumba. Miti na nyasi ndefu zipigazo kelele kwa upepo hazikufanya hivyo siku hii. Tumaini alishituka akiwa kitandani huku giza likimmulika. Alikuwa uchi wa mmyama , akapapasa kutafuta kanga yake. Akafanikiwa. Akataka kunyanyuka kutoka kitandani lakini akahisi maumivu sehemu zake za siri.

“Oh!, Bibi wewe, mbona wanitesa sana… Sijazoea mimi ebu njoo basi!” alilalama Tumaini akiwa peke yake. Kwa sasa hadi kelele zile za chura zikaacha kabisa. Kijiji kizima cha Malindi kilikuwa kimya mno.

Tumaini akapapasa kutafuta kiberiti awashe koroboi yake. ‘Mzoefu wa shamba hujua hekari’ alikipata kibiriti kwa kuwa alishazoea nyumba nzima kipi kinakaa wapi na kwa muda gani. Akawasha koroboi yake na kujongea nayo kitandani.

Akatoa kanga yake na kuirusha chini. Sasa alikuwa mwenyewe na kibatari mkononi. Hakutaka kuhema wala kupumua ilimradi tu kibatari kisizime. Alikuwa makini na mwangalifu. Taratibu akazogeza mwanga wa kibatari katika sehemu yake ya siri. Alikutana na michirizi ya Damu ambayo alishakauka kitambo. Alikuwa na alama za damu Tumaini.

Macho yake yakakodoa moja kwa moja hadi katika nyeti yake. Akakutana na tobo kubwa kuliko alilokuwa nalo mwanzo. Nyama zilizokaza kila siku ziliachia taratibu na kusinyaa pembeni. Inaonekana ni athari ambazo amezipata baada ya kujichezea usiku kabla ya kulala.

“Ayaaah!” alishangaa Tumaini. Bado alikuwa hana elimu ya biolojia. Shule ndio hiyoo kidato cha pili tu alitangaza kuichoka. Aliacha kwenda kwa muda shuleni

Ndio shule hiihii ambayo alimuahidi Bosco kuwa ataanza kwenda tena. Labda aende sasa kuuliza kwa elimu hii anaishuhudia sehemu zake za siri. Hakukumbuka kabisa ndoto aliyoita punde. Yeye alidili na maumbile yake tu. Kwa hakika Bibi Sembe hajafa. Kazaliwa upyaaaa!, Tumaini hana tofauti kabisa na Bibi yake, walifanana vichwa hadi maisha yao.

Alipoona maswali anayojiuliza yanakosa majibu juu la jambo lile, akaamua kuzima kibatari na kujitupa tena kitandani. Hakujali kulala uchi tena. Upopo uliokaribisha mvua ukampuliza tena Tumaini na kumrusha mbali mno kwenye ndoto. Aliingia tena Tumaini katika ndoto usiku ule ule. Hii ni ndoto ya Mama, Baba na mdogo wake. Wote Marehemu……

ITAENDELEA…….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi; “MATUNI” (08)
Mtunzi; Author Xav
#StarXavEntertainment
====================

Alipoona maswali anayojiuliza yanakosa majibu juu la jambo lile akaamua kuzima kibatari na kujitupa tena kitandani. Hakujali kulala uchi tena. Upepo uliokaribisha mvua ukampuliza tena Tumaini na kumrusha mbali mno kwenye ndoto. Hii ni ndoto ya Mama, Baba na mdogo wake. Wote Marehemu……

ENDELEA SEHEMU YA 8!.
-------

KULIKUWA na upepo mkali sana siku hii, upepo ambao ulipeperusha vizuri miguu ya Tumaini bila ubishi. Jua lilikuwa kali kama kawaida. Hakukuwa na mtu mwingine sehemu ile zaidi ya Tumaini mwenyewe.

Tumaini alikuwa katika jangwa akiwa hajui wapi anaelekea na wapi anatokea. Tayari alishaonesha kuchoka na safari yake ya bila kujitambua. Bado upepo uliendelea kumsindikiza kumwonesha ukatili wa sehemu ya jangwa. Hakuna maji: hakuna chakula. Ni joto, vumbi na kiu tu ndivyo viliendelea kumuua Tumaini.

Aliendelea kuburuta miguu yake isio na hata theruthi ya mfuniko. Hakuvaa kitu miguuni Tumaini. Alikuwa badua. Hana la ndala wala chombo cha kukinga vumbi lile lenye mashaka ndani yake. Bado aliendelea kukwea vizingiti vya mchanga vilivyopo sehemu hiyo.

Safari bado iliendelea, Tumaini alionekana na mawazo mengi sana, miguu yake ilichota mchanga uliokanyagwa na kurusha kwa mbele, Tumaini alikauka kuanzia Machozi, Mate hadi Maneno. Mdomo wake ulikauka kwa njaa hadi kuanza kupasuka. Mwendo wake ulikuwa wa Matumaini kama jina lake. Akajikokota kusonga mbele.

Umbali wa kama hatua hamsini na saba hivi aliona kitu, Mti!, Hapana, Gogo? Hapana, ni kipi amekiona Tumaini. Alibidi asogee kupata msaada wa kitu hicho , japo kimletee kivuli kwa jua lile. Jua liliwaka na kuchoma kwa pamoja. Japo alichoka lakini akakaza mguu kufikia pale alipokusudia.

Alishamaliza hatua hamsini tayari, zikabaki saba na nusu kufikia sehemu hile, macho yake yakawa yanakosa ushirikiano na miguu, alijikuta anaanguka chini Tumaini kama mzigo ‘puuh’. Mwili wake ulikosa nguvu tayari, aliamua kuburuzika na tumbo kufikia mahali pale. Akaweza.

Hatimaye akafikia ndoto yake, alifika pale alipokusudia, pumzi yake ilitoka kwa shida sana. Mapigo ya moyo yalikuwa hatihani kusimama. Yalishindwa kuhimili mikiki ya mateso. Moyo ulimwamini Tumaini, Tumaini ambaye Alisha kata tamaa. Alifika na kuegema pale palipo na kitu kama gogo hivi. Hakujishulisha na chochote kile zaidi ya kujivuta na kukaa kitako japo kichwa tu kifaidi kimvuli kile kichache. Alihema kwa mafanikio sasa Tumaini. Macho hayakuwa na nguvu kabisa.

“Kolookoonko!” kuna kitu kilitikisika pale alipo. Aliinua uso wake kuangalia. Kilikua kibao.

“Kibao?” alijiuliza, hakuangalia vizuri alipoegema. Alijua ni gogo tu limechomekwa enzi za biashara ya watumwa. Sasa macho yake yalikutana na kibao. Kilijaa vumbi hata kisisomeke kilichoandikwa.

Akajitahidi kuinua mkono wake wa kulia japo kuweka sawa kibao hicho. Kililegea na kuwa juu chini, chini juu. Akazungusha kibao kile huku shingo nayo ikisaidia kichwa kuyainua macho kusoma kilicho andikwa.

“KISH..” hakuwa na nguvu ya kutoa sauti Tumaini, akasindikiza mkono wake kufuta vizuri kibao hicho. Akili yake ilijawa na shauku ya kujua wapi alipo.

“KISHUMU!” Naam! sasa kibao kilisomeka chote, kiliandikwa KISHUMU kwa herufi kubwa huku mbele ya maneno hayo kulikuwa na mshale ulioonesha upande wa kusini.

“KISHUMU!” Neno hilo likajirudia katika kichwa cha Tumaini, kama kuna siku au mtu alishawai kumtakia jina hilo.

Akawa mgumu kuwaza Tumaini. Akapotezea baada ya kuona jambo hilo linamuumiza kichwa. Akakiacha kibao hicho kilichosimikwa na mti mgumu. Kilionekana kuwekwa miaka kenda iliyopita.

Tumaini akarudia mkao wake ule ule wa kuhufadhi kichwa kwenye kivuli ambacho kinapatikana kutokana na kibao hicho. Kichwani alikua na mambo mengi sana, yote yalikuja nusu na kupotea mazima. Kila kitu alikua anakumbuka nusunusu tu. Njaa ikamfanya afumbe macho kabisa, alifumba macho japo kurudisha wema kwa Mungu wake. Alifumba macho Tumaini.

Kufumba macho kwa Tumaini kulileta Tumaini jingine jipya. Tumaini alihisi msikiko wa kitu kama maji hivi kupita katika mfereji. Ndio!, Ndio maji. Kulikua na mteremko wa maji kando tu alipoketi Tumaini. Akafumbua macho gafla.

“Maji!” alilitoa neno hilo bila kipingamizi, uchovu wote ukaisha. Ukanyanyuka ghafla bila kushurutishwa na mtu. Macho yake yote aliyatoa yote sehemu hiyo. Kichwa kikamsaidia kutafuta yalipo maji hayo.

Yes!, aliyaona Tumaini. Aliyaona maji. Kwanini asitimue mbio?. Haikujulikana amepata wapi nguvu hizo. Sekunde tu tayari macho yake yalitazamana na mfereji huo wa maji. Hakuwa na uhakika wa usalama na maji hayo. Akayafakamia. Akanywa na mengine kujirushia mwili mzima.

Mengine akawa anayachezea kwa kuyarusha kichwani kwake na kutelemkia mgongoni, kwa raha hiyo alijikuta anafanya kosa!, kosa la kufumba macho kuruhusu mhemuko wa kupata nguvu tena. Alihema kwa nguvu na kushusha pumzi hizo.

Kitu cha ajabu ni kuwa alipofumba macho alikutana na picha picha za watu wa ajabu, akanogewa kutaka kujua ni wakina nani wanaokuja katika fikra yake, akazamia katika fikra hiyo kwa makusudi ya kutaka kujua. Naam akapata alichokitaka. Nadhani hiki ndicho alichokuwa anatafuta. Si alitaka cha uvunguni, aliinama Tumaini.

Mbele ya macho yake kulikuwa na giza la ghafla, alisikia sauti za watu zikipiga kelele kupindukia, akili yake ikacheza na kujua sauti hizo ni: moja ya Mwanamke wa rika, pili ni Mwanaume wa rika na tatu ni Mtoto. Tena mototo mdogo kabisa. Wote walikuwa wanaonekana kwa hafifu sana na kupiga kelele za kuomba msaada.

“Msaaaada!, jamani Msaaaada, Msaaa… ah!” wote walikuwa wanalia msaada kwa pamoja, Tumaini katu hakutoka katika fikra hizo, bado alikua anajiuliza ni kina nani na atapataje nafasi ya kuweza kuwasaidia.

Ule mwanga mweusi ulipotea gafla na kufika mwanga mwekundu pyuu!, ilikuwa rangi ya damu!, sasa aliona fika sura za watu hawa. Walilowa damu kupita maelezo. Wote walikuwa uchi wa mnyama. Walikuwa wamejikumbata kwa pamoja kuomba msaada.

Tumaini aliona sura kwa ufasaha lakini alikuwa hana kumbukizi yoyote ile kichwani, ilimpa shida sana hali hile, watu wale walikuwa wanatisha sana sehemu walipo, Tumaini alianza kupiga hatua kwa kutaka kuwasaidia. Alikuja kusimama mara baada ya kuona watu hao watatu wamegeuka sura zao na kuwa watu wa ajabu.

Walikuwa watu wenye matundu usoni na sehumu zao za masikio, midomo na pua zilikua zinavuja damu tu, hadi yule mtoto kabisa naye alikuwa hivyo hivyo. Tumaini alianza kuogopa. Alianza kurudi nyuma nyuma mara baada ya watatu hao kuanza kusogea huku wakinyoosha mikono yao kupokea msaada ambao Tumaini alitaka kuwapo mwanzo. Walikuwa wanatisha mno na kumsogelea Tumaini huku wakiendelea kuomba msaada.

Tumaini aliishiwa nguvu, akabaki kuganda alipo, alishindwa piga hatua, hakuwa na sehemu ya kwenda, mikono ya watu hao ilimsogelea Tumaini. Wote watatu walimfikia na kutaka kumshika kwa pamoja. Alipiga kelele Tumaini. Kelele hizo zilimtoa katika fikra ile ya ajabu. Alikuja kuzinduka yupo palepale kwenye mfereji hule wa maji.

Ajabu!, mikono ya Tumaini yote ilikuwa na damu, tena damu nzito mno. Akahamaki mwilini mwake ambao nao wote ulikuwa unavuja damu tu. Macho yake yakatua hadi pale ambapo yalikuwa yanatililika maji.

“Damu!!!” Neno hilo likagonga moja kwa moja mdomoni mwa Tumaini. Aliona Damu pale kwenye mfereji badala ya maji. Akapika kungu la nguvu Tumaini. Hakuwai kuona jambo kama hilo katu. Alipiga kelele nyingi mno.
----------

TUMAINI aliamka toka katika hiyo ndoto, mwili mzima ulijawa na jasho. Alikua anatililikwa na jasho tu Tumaini. Haraka akakaa kitako. Hakuna alichokikumbuka katika ndoto hiyo. Maajabu!!. Tumaini hakukumbuka kitu chochote kile…..

ITENDELEA…
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom