Simulizi ya beyond pain

BEYOND PAIN
SEHEMU YA 29
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Saa tatu za asubuhi tayari tulikwisha funga mizigo yetu kwa ajili ya safari.Nilimuomba rafiki yangu Beka atupeleke uwanja wa ndege wa Kilimajnaro halafu abaki na gari langu.Saa tatu na nusu safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza.Nilikuwa na furaha isiyo kifani kwani nilitegemea kwamba sasa karaha zote za Emmy nitaziacha nyuma na mimi kuishi maisha ya furaha na amani nikiwa na malaika wangu Clara.Tuliwasili uwanja wa ndege tukaagana na Beka na sisi kuingia sehemu ya kusubiria ndege .
Hatimaye muda wetu ukafika na tukaombwa tuelekee ndegeni.Taratibu tukiwa tumeshikana mikono tukaungana na abiria wengine kuelekea mahala ilipokuwa ndege tutakayosafiri nayo.Kabla hajaikanyaga ngazi ya ndege Clara akasimama.
“ Wayne naishiwa nguvu ..siwezi tena kunyanyua mguu wa…….” Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ya Clara.Akaanguka na kabla hajafika chini nikawahi kumdaka.

ENDELEA………………………….

Emmy alikuwa amesimama mbele ya kioo kikubwa akiwa amefura na hasira na sura yake ameikunja..Kwa muda wa saa moja sasa alikuwa amesimama akitazama kioo kile kikubwa mfano wa luninga ,kilichokuwa kikimuonyesha kila kilichokuwa kinaendelea kati ya Wayne na Clara.Hakuwa ameongea chochote toka alipoanza kutazama luninga ile ikiwaonyesha Wayne na Clara walivyokuwa wanajiandaa kwa safari. Wayne na Clara wakiwa uwanjani walionekana ni wenye furaha kubwa .Walikuwa wamekaa wakisubiri zamu yao ya kupanda ndegeni ifike na baadae wakashikana mikono na kuanza kuelekea ndegeni.Clara akauma meno kwa hasira
“ Damn you Wayne..huwezi kunikimbia..Nitakutafuta usiku na mchana.Na huyo mwanamitindo wako ambaye amekupagawisha na kukufanya unitaliki atakiona cha moto..” akawaza Emmy .Muda wote huu mganga alikuwa amesimama pembeni yake akiwa na usinga wake mkononi akiupunga huku na huko huku akiongea maneno yake ya kiganga.
“ Emmy Wayne na Clara wanaondoka na bado haujafanya maamuzi yoyote.hii ni nafasi yako usiiache ikapita..Ukiacha wakiingia ndegeni na wakaiacha ardhi ya Arusha ,kurudi tena itakuwa vigumu mno.Kama bado unataka kuendelea na ile dhamira yako basi huu ndio wakati wake.Yeyote utakayemfunga siku ya leo hatapona hadi siku utakapokufa wewe.” Akasema mganga huku akimuonyeshea Emmy meza iliyokuwa na wanasesere wawili .Emmy hakusema kitu akageuka na kuiendea meza ile kisha akachagua mwanaserere mwenye umbo la mwanamke.Mganga akampa sindano.Emmy akasimama tena mbele ya kile kioo akawashuhudia Wayne na Clara wakikaribia kufika katika ngazi za kupandia ndege.Kwa hasira akauinua mkono wake wa kulia uliokuwa umeshika sindano ndefu na kuichoma upande wa kulia wa yule ukatoka moshi mweupe na sekunde ile ile Clara ambaye alikuwa anajiandaa kuikanyaga ngazi ya kupandia ndegeni akaanguka na hakuweza kuongea wala kuinuka tena.Emmy akatabasamu
" Leo nimekupata " akasema Emmy huku akitabasamu.
“ Kazi imekwisha” akasema mganga.
“ Kwa sasa huyu mwanamke kazi yake imekwisha.Nakuhakikishia Wayne lazima arudi kwako ndani ya muda mfupi. Atakufuata yeye mwenyewe.” Akajigamba mzee Mtuguru.
“ Nashukuru sana Mganga. Nakuahidi zawadi nzuri mno kama Wayne atafanikiwa kuja kwangu.” Akasema Emmy huku akitabasamu
“ Usiseme kama atarudi kwako.nakuhakikishia lazima arudi kwako na safari hii hataweza kuondoka tena.” Mganga akazidi kumpa moyo Emmy.

*************************

Clara..!! Clara !! ..” Niliita kwa nguvu baada ya kumdaka Clara alipotaka kuanguka lakini hakuweza kusema chochote..Nilichanganyikiwa ghafla.Mtu ambaye sekunde chache zilizopita tumekuwa tukiongea vizuri na kucheka lakini ghafla hawezi kuongea tena.Haya yalikuwa ni mambo ya ajabu sana kunitokea.Sikujua Clara amepatwa na ugonjwa gani uliomtokea ghafla namna ile.
Watu waliokuwa karibu wakanisaidia kumbeba Clara na kumuweka pembeni.Bado kichwa changu kilikuwa kizito kuamini kilichotokea.Nilihisi ni kama mchezo wa kuigiza lakini kadiri dakika zilivyokuwa zikisonga ndivyo nilivyojikuta nikilazimika kuamini kwamba Clara alikuwa amepatwa na ugonjwa wa ghafla ambao sikufahamu ni ugonjwa gani.Pamoja na ujasiri wangu wote niliokuwa nao nilijikuta nikitetemeka kila nilipomuona Clara na hali aliyokuwa nayo.Macho yalikuwa yamefumba,hakuweza hata kufumbua jicho.Mwili wake haukuweza hata kutikisika.Machozi ya uchungu yakanitiririka.Wanaume wawili wa makamo ambao nao walikuwa ni wasafiri wakanivuta pembeni baada ya kuiona hali nilioyokuwa nayo.
“ Jipe moyo ndugu yangu..Mungu atakusaidia..” akasema mmoja wao aliyekuwa amevaa suti nyeusi..
“ Tatizo hasa la mwenzio ni nini? Akauliza mwingine aliyekuwa amekaa kushoto kwangu..Nikajikaza na kusema
“ Sifahamu tatizo ni nini ..imetokea ghafla tu akapatwa na ugonjwa ule..” nikajibu kwa ufupi.Tayari uongozi wa pale uwanjani ukataarifiwa kuhusiana na kilichokuwa kimetokea na kwa haraka likatolewa gari kwa ajili ya kumkimbiza Clara katika hospitali ya Rufaa ya KCMC.Kwa kasi ya aina yake wahudumu wa pale uwanjani wakampakia Clara katika gari na mimi nikaingia ndani ya gari lile kisha tukaondoka uwanjani pale kwa kasi kubwa.
Kila nilipokuwa namuangalia Clara nilishindwa kujizuia kutokwa na machozi.Sipati neno ambalo linaweza kuelezea uchungu niliokuwa nao kwa wakati ule.Rangi ya ngozi ya Clara ikaanza kubadilika na kuwa na weusi weusi..nikazidi kuogopa.Nawashukuru watu niliokuwa nao mle garini walijitahidi kwa kila namna walivyoweza kunipa moyo ingawa hata nao nyuso zao zilionyesha mstuko na uoga wa dhahiri.
“ Ouh Clara..nini kimekupata malaika wangu?.. Nilisema kwa uchungu nilipomtazama Clara akiwa amelala mle ndani ya gari hajitambui.Niliogopa sana kwa hali aliyokuwa nayo. Gari ilikuwa inakwenda kwa mwendo mkali sana lakini niliona kama inachelewa kufika hospitali ili Clara aanze kupatiwa matibabu.
Hatimaye tukawasili katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi na kwa haraka wauguzi wakampokea mgonjwa na kuanza kumshughulikia mara moja. Sampuli za damu na vipimo vingine vikachukuliwa na kupelekwa maabara kwa uchunguzi.
Nilitoa malezo mafupi kwa madaktari kuhusiana na jinsi ugonjwa ule wa Clara ulivyoanza halafu wakaniomba nikasubiri nje ili waendelee na uchunguzi wao.Niliwaomba madaktari wale wafanye kila linalowezekana ili kuokoa maisha ya Clara kwani hali aliyokuwa nayo ilikuwa inaogopesha mno.Miguu haikuwa na nguvu nikatafuta sehemu nikakaa.Bado kichwa changu kilikuwa na mawazo mengi sana juu ya kilichotokea.Ilikuwa ni kama ndoto ya mchana na ilikuwa vigumu sana kuamini kilichotokea.Nilivuta picha ya kuanzia asubuhi tulipokuwa tunajiandaa kwa safari hii ambayo Clara hakutaka kuniambia tunaelekea wapi ingawa tiketi zetu zilionyesha kwamba tulikuwa tunaelekea Dar es salaam.Nikakumbuka tulivyoliacha jiji la Arusha nikiwa na matumaini kwamba nimeyaacha nyuma matatizo yote yaliyotokea kati yangu na Emmy.Sikutarajia kurejea tena Arusha.Niliamini kwamba ninakwenda kuanza maisha mapya nikiwa na malaika wangu Clara.Nilikumbuka tulivyoagana na rafiki yangu Beka pale uwanja wa ndege naye akarejea Arusha na gari langu.Nilimuahidi kuwa nikifika huko tunakokwenda ningemtaarifu kwa simu.Nikakumbuka pia tulivyokuwa tukipiga hatua kuelekea katika ndege na mara kumbu kumbu ambayo mpaka leo nikiikumbuka huwa inaniliza ikanijia kichwani. Ilikuwa ni kama ninatazama filamu.Clara alikuwa tayari ameinua mguu wake ili akanyage ngazi za ndege lakini hakuweza kufanya hivyo kwani alianguka ghafla na hakuweza kuongea tena.machopzi yakaanza kunitiririka tena.Nikafuta machozi nikachukua simu yangu na kumtaarifu rafiki yangu Beka kilichokuwa kimetokea.Hakuamini hata kidogo na alidhani ninamtania.Nilipomuhakikishia kwamba haukuwa utani aliamini na kunitaarifu kwamba tayari anaanza safari ya kuja Moshi kuungana nami katika wakati ule mgumu.Baada ya kuongea na Beka nikampigia simu baba mkwe na kumtaarifu kilichotokea halikadhalika naye akanitaarifu kwamba yuko njiani anakuna Moshi.Nikamtaarifu pia na Chris ambaye tayari tumekwisha maliza tofauti zetu . Kila mmoja niliyemtaarifu alistuka mno .hakuna aliyeamini moja kwa moja.
Nikiwa bado nimekaa pale nje nikiwasiliana na watu mbali mbali kuhusiana na kilichotokea,nikaitwa katika chumba cha daktari.Haraka haraka nikaingia na kuketi kitini.daktari akanitazama kisha akasema
“ Wayne tumemfanyia uchunguzi mgonjwa wako na tumegundua kwamba mgonjwa wako amepatwa na ugonjwa wa kupooza…”
“ What ? ..Unasema ??......Nikauliza kwa mshangao nikiwa nimesimama na macho kunitoka.Nilianza kusikia joto la ghafla.Hii ilikuwa ni taarifa ya kustusha sana.
“ Dakatari tafadhali naomba unielezee vizuri kwa ufasaha ili nikuelewe.Umesema Clara anaumwa nini? Nikauliza tena nikiwa bado nimesimama.
Kabla hajaendelea kunipa taarifa kuhusiana na ugonjwa wa Clara akaniomba niketi chini..
“ wayne mgonjwa wako amepatwa na ugonjwa wa kupooza upande mmoja wa kulia.”
“ Ouh my God !! ..” Nikasema kwa sauti kubwa mikono yangu ikiwa kichwani.Daktari akanitazama na kusema
“ Tulidhani labda tatizo hili limetokana na shinikizo la damu lakini kwa Clara kila kitu kiko katika hali ya kawaida.Vipimo vyote vinaonyesha hakuna tatizo.Bado tunataka kundelea kufanya uchunguzi zaidi ili tuweze kufahamu nini chanzo cha ugonjwa huu.Hata sisi imetushangaza kidogo” akasema Daktari kisha akanyamaza akanitazama na kuendelea.
“ Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata watu wengi kwa siku za karibuni .Lakini kwa upande wa Clara hali ni tofauti kidogo hivyo itatulazimu tufanye uchunguzi wa kina tujue nini chanzo cha tatizo hili Kwa sasa kuna kipimo kimoja ambacho tunahitaji kukifanya lakini kwa bahati mbaya mashine yetu imeharibika kwa hiyo itakulazimu uende jijini arusha kwa ajili ya kipimo cha CT Scan.” Akasema daktari..
“ Daktari naomba uniambie tafadhali..Clara atapona ? Ataweza kutembea tena kama zamani? Nikauliza maswali mfululizo.Daktari akanitazama na kusema
‘ Wayne usiwe na hofu ,mgonjwa atapona ingawa siwezi kukwambia lini anaweza akapata nafuu.Tiba kubwa ya ugonjwa huu ni mazoezi .Baada ya kujiridhisha na vipimo vyote kwamba hakuna tatizo lingine basi tutaanza kumfanyisha mazoezi mara moja ” Akasema daktari..
Pamoja na maneno yale ya kutia moyo ya daktari,niliinama na kuzama katika mawazo mengi sana.Nilijaribu kutafakari lakini nikakosa majibu . Nilihisi kama dunia inaniadhibu..
Niliongozana na daktari kwenda kumuona Clara aliyekuwa amelazwa katika chumba maalum cha peke yake.
Nilidondosha machozi nilipomshuhudia mwanamke ambaye masaa machache yaliyopita alikuwa na uzuri usioelezka lakini kwa sasa hata sura yake ilikuwa imebadilika.Alikuwa amelala kitandani hajitambui,rangi ya ngozi yake ilianza kuwa na weusi na mdomo wake ulikuwa umepinda tofauti na ulivyokuwa awali.
Beka na Chris wakawasili kila mmoja na gari lake na kila mmoja alistuka mno kwa hali aliyokuwa nayo Clara.
“ Wayne nina ushauri mmoja..” akasema Chris .
“ Kwa nini tusimuhamishe Clara na kumpeleka jijini Arusha.Kwa sasa kumefunguliwa hospitali moja kubwa ya kimataifa inayotibu magonjwa kama huu uliompata Clara.Kuna mabingwa wa kutibu ugonjwa huu toka nchini Marekani” akashauri Chris.Kwa pamoja tukashauriana na kuafikiana kwamba tumuhamishe Clara na kumpeleka katika hospitali hiyo mpya aliyoshauri Chris.

***************************

" Mganga nakuahidi kurudi tena nikiwa na zawadi nzuri sana ambayo hutaamini." akasema Emmy akiwa na tabasamu pana sana.
" Emmy nimekuhakikishia kwamba huyu mwaanume lazima atarudi kwako na hataondoka tena.Safari hii atakupenda kupita maelezo.Atafanya kila utakalomuamuru alifanye." akasema mganga
" Sipati neno la kukushukuru mganga..lakini utaona mwenyewe zawadi nitakayokuletea " akasema Emmy.Mganga akatoka kidogo na baada ya muda akarejea akiwa na kibuyu chenye dawa.
" Emmy ninakupa dawa hii.Hii ni dawa yenye nguvu sana na unatakiwa uipake mwilini pale tu unapokwenda kuonana na Wayne.Kwa sasa unatakiwa umtafute kwa udi na uvumba hadi umuone lakini usijaribu kumpigia simu.Unatakiwa umstukize .Wakati unakwenda kuonana naye unatakiwa ujipake dawa hii pekee na usichanganye na mafuta ya aina yoyote ile.Hilo ndilo sharti pekee la dawa hii.Ninakuhakikishia kwamba Wayne akikuona tu atastuka mno na dakika hiyo hiyo atakuomba msamaha na mtarudiana tena..." akasema mzee mtuguru na kisha wakaagana na Emmy akaanza safari ya kurejea Arusha.
" Wayne huwezi kunikimbia hata kidogo..wewe ni wangu pekee na siku zote utakuwa wangu..Hahahahaaa namuonea huruma huyo mwanamitindo wako..kwisha kazi yake.Sasa tuone hayo maringo na mikogo yake kama vitakuwepo tena.Nilimuonya asicheze na mali za watu lakini hakusikia.Hahahaaa..ukiona vimeng'aa ujue vimeng;arishwa." akawaza Emmy akiwa katika gari akirejea jijini Arusha.Alikuwa na furaha isiyo kifani nantabasamu halikukauka usoni mwake.
" Japokuwa bado nina majonzi ya kufiwa na mwanangu Baraka lakini ninafuraha kwa upande mwingine kwa sababu ninakwenda tena kurudiana na Wayne.Mimi ni mwanamke wa shoka nimempigania Wayne na mpaka sasa nimefanikiwa kumrejesha tena mikononi mwangu.Safari hii habanduki na hata hao wanga waliokuwa wananiroga ili nigombane na Wayne kwa sasa hawaniwezi tena.Kwa tiba niliyopewa mimi ni kisiki cha mpingo.Hakuna atakayeniweza kwa sasa.Nimejaa kinga kila mahala." akaendelea kuwaza Emmy.
" Kuna kitu nimekumbuka.Sheila alinidokeza kwamba James anaweza akarejea muda wowote katika wiki ijayo.Sijui itakuwaje akisikia kwamba mwanae Baraka amefariki dunia.Ah ! hilo halinihusu kwa sasa akili yangu yote ni kwa Wayne.Baada ya kumrejesha Wayne kwangu ndiyo nitaanza kushughulika na James.Nitamuweka sawa na atanielewa japokuwa itamuumiza sana kwa sababu hakuwahi kumuona mwanae kwani alipoondoka kwenda masomoni Urusi aliniacha nikiwa na mimba changa kabisa na toka wakati ule hajawahi kurejea tena.Ataumia lakini hakuna namna ya kufanya kumrejesha Baraka.Inauma sana lakini nimefanya haya yote kwa ajili ya kulipigania penzi langu.Safari hii ninataka nipate mtoto na Wayne.Nilifanya makosa makubwa sana kuzaa nje ya ndoa.Laiti kama ningezaa na Wayne haya yote yasingenikuta.Sijielewi ni kwa nini sikuwa naridhika na mume wangu hadi nikawa natoka na kwenda kubadilisha wanaume kama nguo .Wayne alinipa kila nilichokihitaji lakini bado nilitoka nje ya ndoa.Lazima nilikuwa nimerogwa.Safari hii watanikoma.." akawaza Emmy

*********************

Emmy alikuwa akiendesha gari lake kwa kasi kubwa kuwahi jijini Arusha.Uso wake haukukaukiwa na tabasamu .
" Ngoja nimpigie simu Sheila simu nimtaarifu juu ya mambo yanavyokwenda japokuwa alikimbia na kuniacha peke yangu." akawaza Emmy kisha akapunguza mwendo wa gari akachukua simu na kuzitafuta namba za simu za Sheila rafiki yake mkubwa akampigia.
" Halo Emmy, niambie shoga yangu" akasema Sheila baada ya kupokea simu ya Emmy
" Sheila mambo yanakwenda vizuri sana" akajibu Emmy huku akitabasamu
" Kivipi Emmy? akauliza Sheila ambaye sauti yake ilionekana dhahiri hakuwa akiyafurahia maongezi yale na Emmy
" Sheila yule mwanamitindo wa Wayne kwisha habari yake."
" Kwisha habari yake ! Mbona sikuelewi Emmy una maanisha nini ? akauliza Sheila
" Tayari nimekwisha mdondosha.Hatainuka tena" akajibu Emmy huku akicheka kicheko cha chini chini.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa
" Hallo Sheila upo ." akaita Emmy baada ya kimya kile cha ghafla.
" Nipo Emmy..Nimestuka sana kwa jambo uliloniambia.Ina maana amekufa yule mwanamitindo? akauliza Sheila
" Hapana sijamuua japokuwa nilikuwa na nafasi hiyo. Nilichokifanya ni kwamba nimempa ulemavu wa kudumu na hatainuka tena katika maisha yake.Hivi ninavyokwambia amepelekwa hospitali na hataweza kuinuka wala kutembea tena.Amepooza mwili.Hili ni fundisho kwake kuvamia mabwana wa watu" akasema Emmy.Sheila akavuta pumzi ndefu
" Sheila niko njiani ninarudi.Tutaongea mengi nikisha fika.Bado kuna kazi ninataka unisaidie "
" Nikusaidie tena?.Kuna kazi unataka nikusaidie? .Sheila akauliza kwa mshangao.
" Ndiyo ..mbona umestuka?
" Lazima nistuke Emmy .Wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na lazima nikueleze ukweli.Kwa sasa unatakiwa utulie Emmy.Vitendo unavyoendelea kuvifanya si vya kiungwana na havitakupeleka popote. Nakwambia hivyo kama rafiki yako na mtu ninayekupenda . Nimekwisha ona mwisho wa watu waliojihusisha na masuala hayo ya ushirikina .Siku zote mwisho wao huwa si mzuri hata kidogo.Angalia shoga yangu ni hivi majuzi tu umempoteza mwanao Baraka.Hata wiki moja haijapita Clara naye anapatwa na matatizo. Mpaka lini Emmy utaendelea kuwatesa watu? Hadi lini utaendelea kumtesa Wayne? Clara unayemtesa kitandani amekukosea kitu gani? Watu wengi wanazidi kuteseka kwa sababu yako Emmy. Tafadhali hebu achana na hayo mambo ya kishirikina.Muache Wayne aendelee na maisha yake.Ulishindwa kumtunza na kwa sasa muache afurahie maisha mengine aliyoyanza.Mtegemee Mungu na kama ikimpendeza kumrudisha Wayne kwako atafanya hivyo lakini si kwa kuwategemea waganga wa kienyeji..Emm................" Kabla Sheila hajaendelea Emmy ambaye uso wake ulikwisha jikunja kwa hasira kutokana na maneno ya shoga yake akainglia kati.
" Sheila unaongea maneno gani hayo? Mbona sikuelewi ? Wewe ndiye wa kuniambia maneno kama hayo leo ..?akafoka Emmy.
" Emmy ngoja nimalizie kile ninachotaka kukwambia...." akasema Sheila.Emmy akapunguza mwendo wa gari na kuliegesha kandoni mwa bara bara.
" Emmy napenda ufahamu kwamba mimi sikukifurahia kabisa kitebdo cha kunishirikisha katika masuala yako ya kishirikina.Wazazi wangu hawakunikuza katika misingi ya kuamini mambo kama hayo.Kitendo cha kunipeleka kwa yule mganga na kusababisha akanifanyia kitendo kama alichonifanyia bado kinaniuma mno.Sijui hata nifanye nini ili niweze kuifuta taswira ya kitendo kile katika akili yangu.Nimeumia sana Emmy na kwa maana hiyo naomba ufahamu kwamba urafiki wetu kwa sasa utakuwa na mipaka.Kama unataka urafiki wetu uendelee nakushauri achana kabisa na hayo mambo ya kishirikina ambayo hayana faida yoyote kwako.Ndoa yako umeivuruga wewe mwenyewe na kwa sasa umeanza kuhangaika kumtafuta mchawi wakati mchawi ni wewe mwenyewe.Nakushaur........................."
" Bastard.....!!!" Emmy akakata simu kwa hasira na kuitupa kitini.
" Stupid girl !!..akasema kwa hasira.
" Sheila leo anathubutu kunitamkia maneno kama haya ? Bado siamini kama hata Sheila naye amenigeuka.Mimi nimekuwa mtu wake wa karibu na nimemsaidia katika mambo yake mengi ikiwa ni pamoja na kumkopesha hata mtaji wa kufungua saluni ile anayoringia kwa sasa halafu leo hii ananitamkia maneno kama haya .!!..Hapana siwezi kukubali kudharauliwa na paka kama Sheila. Anaishi mjini kwa sababu yangu mimi na hakupaswa hata kidogo kunidharau.Kwa kuwa naye ameamua kunidharau basi nitamjumuisha katika orodha ya maadui zangu.Nitamuonyesha kazi.Nitamfundisha adabu.Nadhani bado hajanifahamu vizuri" akawaza Emmy akiwa amefura kwa hasira.
" Ninaapa Sheila lazima alikimbie jiji.Nitayafanya maisha yake magumu sana na lazima aje anipigie magoti..." akasema kwa sauti ya hasira kisha akawasha gari lake na kuendelea na safari ....

*************************

Wazo alilolitoa Chris la kumuhamishia Clara katika hospitali kubwa ya St Patrick inayomilikiwa na wamisionari lilikubaliwa hata na madaktari wa pale hospitali ya rufaa ya KCMC. Bila kupoteza muda taratibu zikaanza kufanyika na baada ya dakika chache kila kitu kikawa tayari Clara akapakiwa katika gari la wagonjwa na safari ya kuelekea Arusha ikaanza.Clara alikuwa amelala kitandani macho ameyafumba.Nilishindwa kujizuia kudondosha machozi niliposhuhudia akipakiwa garini.Chris aljitahidi kunisihi niwe mvumilivu katika wakati ule mgumu.Hata kama ungekuwa ni wewe mpenzi msomaji sina hakika kama ungeweza kuvumilia kumuona mtu unayempenda ambaye muda mfupi uliopita ulikuwa ukiongea naye na kucheka lakini ghafla anabadilika na haongei tena.
" Chris sijui nimemkosea nini Mungu .Ninaona ni kama ninaadhibiwa kila kukicha.Wakati nikiamini kwamba kwa sasa matatizo yote ninayaacha nyuma lakini linaibuka tena tatizo lingine. Sikutegemea kama lngetokea jambo kama hili kwa wakati kama huu.Clara alikuwa mzima wa afya na hakuwa na dalili zozote za ugonjwa .Sielewi ni kwa nini mambo haya yote yananitokea mimi tu..." nikamwambia Chris nikiwa katika gari lake tukielekea jijini Arusha tukimpeleka Clara katika hospitali ya St Patrick.
" Wayne naomba usife moyo ndugu yangu.Mungu wetu ni mwema sana na siku zote amekuwa akitusamehe makosa yetu hata tunapomkosea namna gani.Hii ni mitihani tu ya maisha ambayo hatuna budi kukabiliana nayo na inaweza ikampata mtu yeyote yule.Kitu cha msingi ni kukabiliana na ugonjwa huu wa Clara hadi apone.Nina uhakika katika hospitali ile ya St Patrick watamsaidia Clara na atapona kwa sababu kuna mama wa rafiki yangu naye alipatwa na matatizo kama haya ya Clara na akapelekwa pale lakini alipona na hadi sasa hivi huwezi kuamini kama alikuwa amepooza na hakuweza kuongea kwa muda wa miezi zaidi ya sita.Nina uhakika mkubwa sana hata Clara atapona na ataendelea na maisha yake kama kawaida." akasema Chris.
" Ninafikiria labda nimuhamishie nje ya nchi.." nikasema.
" Hapana Wayne.Bado ni mapema sana kufanya maamuzi hayo ya kumpeleka Clara nje ya nchi.Ugonjwa huu unaweza ukatibika hata hapa nchini.Kama litakuwa ni suala la kumpeleka nje ya nchi basi madaktari watatushauri hivyo lakini sina hakika kama kuna ulazima wa kumpeleka nje ya nchi" akasema Chris.
Sura ya Clara haikuweza kuondoka kichwani kwangu.Bado niliendelea kumuona akiwa katika tabasamu na kicheko chake kidogo
" masikini Clara..!!.." nikasema na kutoa kitambaa nikayafuta machozi ambayo nilishindwa kuyazuia kunitoka
" Its ok Wayne..usihuzunike sana .Clara atapona tu.Tunachopaswa kwa sasa ni kumuomba Mungu ampe uponaji wa haraka" akanipa moyo Chris.
" Chris hakuna ajuaye uchungu ninaousikia moyoni mwangu kwa sasa.Ninahisi ni kama moyo wangu unakatwa vipande vipande na kisu kikali sana.Ninasikia machungu ambayo hayaelezeki kwa maneno.Clara alikuwa ni maisha yangu.Clara alikuwa ni kila kitu kwangu. Clara amenifanya niyafurahie maisha japo kwa muda huu mfupi niliokaa naye. Clara ni mwanamke wa tofauti sana.Ana moyo wa ajabu na wa kipekee kabisa.Ana upendo wa dhati na wa kweli.Upendo wake unatoka ndani kabisa ya moyo wake.Kwangu mimi Clara namchukulia ni kama malaika anayeishi..Sikutegema hata siku moja kama angeweza kupatwa na maradhi kama haya.She doesnt deserve this Ouh Clara.why you..!!!..."
Chris akanitazama kisha akaendelea kuendesha gari.
" pamoja na yote yaliyotokea bado upendo wangu kwa Clara hauwezi kupungua.Hata kama itamchukua maisha yake yote akiwa kitandani..nitampenda Clara hadi siku ninaingia kaburini." nikasema nikiwa nimeinama chini.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Chris akasema
" Wayne kuna kitu nakifikiria"...Nikainua kichwa na kumtazama
" Kitu gani Chris? nikauliza
" I'm sorry to say this but I have bad feelings" akasema Chris
" What feelings? nikauliza.Chris akakaa kimya kidogo halafu akasema
" Inawezakana Emmy akawa anahusika na ugonjwa huu wa Clara" akasema Chris.Maneno yale ya Chris yakaifanya akili yangu ianze kufunguka .Muda huu wote sikuwa nimemuwaza tena Emmy.Akili yangu haikuweza kumkumbuka tena.
" Kwa nini umewaza hivyo Chris.? nikauliza
" Nimewaza hivyo kwa sababu ninamfahamu Emmy ana roho ngumu sana.Kama ameweza kumuua mwanae wa kumzaa mwenyewe hatashindwa kufanya kitu kama hiki kwa Clara.Hayo ni mawazo yangu tu Wayne na sina uhakika kama yanaweza kuwa ya kweli ama la" akasema Chris.Nilikuwa ni kama mtu niliyepigwa na bumbuwazi.Nilizama ghafla katika mawazo mengi.
" Wayne unawaza nini? akauliza Chris
" Chris umenikumbusha jambo ambalo sikuwa nimelitilia maanani kabisa.Maelezo yako yamenifanya nipate picha fulani .Usiku ule alipofariki Baraka dakika chache tu kabla ya kupokea simu ya baba mkwe akinitaarifu kwamba Baraka amefariki dunia ,Clara alikurupuka ndotoni .Alikuwa anaweweseka na jasho jingi kumtoka.Nilimuuliza amepatwa na nini akaniambia kwamba ameota ndoto ya ajabu sana na ya kutisha.Nilimuuliza ni ndoto ya namna gani aliyoota lakini hakuwa tayari kuniambia.Aliniomba tupige magoti tusali na tumtegemee Mungu.Sikuelewa alimaanisha nini kwa maneno yale.Baada ya muda mfupi baba mkwe akanipigia simu na kunitaarifu kwamba Baraka amefariki dunia.Ni usiku ule ambao Emmy alikuwa amekwenda kwa mganga Tanga.Jana asubuhi Emmy hakuonekana tena msibani.Hakuna aliyefahamu alikuwa amekwenda wapi.Nimeanza kupata picha kwamba Emmy anahusika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huu wa Clara.Aliapa kwamba atayafanya maisha yangu magumu na hii ndiyo kazi anayoifanya.Kwa nini amtese Clara kiasi hiki? Amemkosea nini? Kama alikuwa na kisasi na mimi alitakiwa kunitesa mimi na si Clara asiye na kosa lolote lile.Niliyemuacha ni mimi na hakupaswa kabisa kumgusa Clara. Kama ni kweli ni yeye ndiye aliyemfanya Clara hivi I swear this time ameingia katika moto.Mungu atanisamehe kwa nitakachomfanyia hayawani huyu" nikasema huku nikiuma meno kwa hasira.Chris akanitazama na kusema
" Wayne,ninamfahamu Emmy ni mwanamke mwenye roho ngumu sana na siku zote huwa hakubali kushindwa kwa maana hiyo anaweza akafanya jambo lolote lile ili kukipata kile anachokitaka. Kama lengo lake lilikuwa ni kupamaba na wewe basi nina uhakika mkubwa kwamba anaweza akawa amemfanyia Clara vile ili kulipa kisasi kwako..." akasema Chris.
" I swear this time I'm going to kill her " nikasema kwa hasira
" Wayne usiseme hivyo na wala usiweke ahadi yoyote ya kulipiza kisasi.Bado hatuna uhakika kwamba ni yeye ndiye aliyefanya hivi.Hizi ni hisia zetu tu.Kama ni yeye ndiye aliyefanya kitendo hiki basi fahamu kwamba hizi ni kazi za shetani.Shetani si lolote mbele za Mungu.Tunachotakiwa kufanya sisi ni kumtegemea Mungu na atamponya Clara.Mungu ni muweza na hashindwi na lolote. Siku zote tunaambiwa tumtegemeze yeye pekee.Tumuombee Clara apone na tumuombee pia Emmy." akasema Chris.Nilishangaa kidogo baada ya kumsikia Chris akiongea maneno yale.Toka nimemfahamu Chris sikuwahi kumsikia akiongea maneno kama haya .
" Chris ! umeongea maneno ambayo yamenistua sana.Sikuwahi kukusikia hata mara moja ukiongea maneno kama haya uliyoyaongea leo." Chris akatabasamu kidogo kisha akasema
" Wayne sikuwa nimekuambia lakini mimi kwa sasa nimeamua kujiweka karibu zaidi na Mungu na kuachana na haya mambo ya kidunia.Nimamua kupokea wokovu.Baada ya kitendo kile kilichotokea baina yetu niliamua kupokea wokovu na kwa sasa mimi ni mtu mpya kabisa na ndiyo maana nina uhakika mkubwa kwamba Clara atapona kwa nguvu za Mungu" akasema Chris.Ni kweli Chris alikuwa amebadilika sana kuanzia tabia na maisha yake kwa ujumla.Bado niliendelea kumshangaa.
" Usisahangae Wayne.Nimeamua kuyabadili maisha yangu.Kwa sasa moyo wangu una furaha na amani.Ninayafurahia maisha yangu ya sasa.Nitamuomba baba askofu ambaye atakuwa anamfanyia maombi Clara kila siku .Kwa maombi yetu na jitihada za madaktari wetu Clara atakuwa mzima tena." akasema Chris.Maneno yale yakaanza kuniingia.Kwa wakati huu nilikuwa tayari kwa lolote lile ambalo lingeweza kumsaidia Clara aweze kupona.
Mara simu yangu ikaita alikuwa ni baba mkwe.Alitaka kufahamu hali ya mgonjwa ilivyokuwa inandelea.Yeye alikuwa katika maandalizi ya kuja Moshi nikamtaarifu kwamba tunamuhamishia Clara katika hospitali ya St Patrick jijini Arusha kwa hiyo hana haja ya kusafiri kuja Moshi.Baba mkwe akaniambia kwamba anatangulia hapo hospitali na tutamkuta pale.Nilifarijika sana kwa namna watu walivyoonyesha kuguswa na ugonjwa ule wa ghafla wa Clara.Tulikuwa nyuma ya gari la wagonjwa lililokuwa likienda kwa kasi kubwa huku likipiga king'ora kuashiria kwamba lilikuwa na mgonjwa ndani yake.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
BEYOND PAIN

SEHEMU YA 30

MTUNZI : PATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Usisahangae Wayne.Nimeamua kuyabadili maisha yangu.Kwa sasa moyo wangu una furaha na amani.Ninayafurahia maisha yangu ya sasa.Nitamuomba baba askofu ambaye atakuwa anamfanyia maombi Clara kila siku .Kwa maombi yetu na jitihada za madaktari wetu Clara atakuwa mzima tena." akasema Chris.Maneno yale yakaanza kuniingia.Kwa wakati huu nilikuwa tayari kwa lolote lile ambalo lingeweza kumsaidia Clara aweze kupona.
Mara simu yangu ikaita alikuwa ni baba mkwe.Alitaka kufahamu hali ya mgonjwa ilivyokuwa inandelea.Yeye alikuwa katika maandalizi ya kuja Moshi nikamtaarifu kwamba tunamuhamishia Clara katika hospitali ya St Patrick jijini Arusha kwa hiyo hana haja ya kusafiri kuja Moshi.Baba mkwe akaniambia kwamba anatangulia hapo hospitali na tutamkuta pale.Nilifarijika sana kwa namna watu walivyoonyesha kuguswa na ugonjwa ule wa ghafla wa Clara.Tulikuwa nyuma ya gari la wagonjwa lililokuwa likienda kwa kasi kubwa huku likipiga king'ora kuashiria kwamba lilikuwa na mgonjwa ndani yake.

ENDELEA………………………..

Emmy aliwasili jijini Arusha .Alikuwa na hasira zisizo kifani kutokana na maneno aliyokuwa ameambiwa na rafiki yake kipenzi sheila.Moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa wazazi wake.
" Ngoja kwanza nielekee nyumbani nikawasalimu kwa sababu nafahamu , lazima watakuwa walijiuliza maswali mengi sana kwa namna nilivyopotea ghafla.Niliondoka bila kumuaga mtu yeyote yule.Sitaki mambo yangu yajulikane kwa mtu yeyote .Nikishaweka mambo sawa pale nyumbani nielekee nyumbani kwangu nikapumzishe kichwa changu nitafakari namna nitakavyoanza mapambano upya.Kwa sasa ameongezeka adui mpya katika orodha ya maadui zangu.Sheila atanitambua.Sijafurahishwa hata kidogo na kashfa alizonipa. Bado hajaufahamu upande wangu wa pili ukoje.Amefanya kosa moja kubwa sana katika maisha yake.Hakupaswa kunitamkia maneno ya kashfa namna ile.Ameniudhi sana na kwa hili sintamsamehe hata kidogo.Nitamuhamisha katika jiji hili." Akawaza Clara.
Alifika nyumbani kwao na kuingia ndani.Mama yake pamoja na baadhi ya ndugu jamaa na majirani ambao bado waliendelea kuomboleza msiba ule wa Baraka walikuwa wamekaa sebuleni kwa majonzi.Mara Emmy akaingia ndani na kuwafanya wote wastuke wakabaki wamemtumbulia macho kama wameona mzuka.Emmy akawasalimu kisha akapita akaenda katika chumba kingine.Wote wakabaki midomo wazi kwa tabia ile ya Emmy.Mtu ambaye amefiwa na mwanae lakini haonyeshi hali yoyote ya majonzi wala kujali .Mama yake Emmy akamfuata Emmy chumbani na kumkuta amekaa peke yake katika mkeka.Akasimama akamuangalia bila kusema chochote
" Mama mbona unaniangalia namna hiyo? akauliza Emmy.Mama yake akamsogelea na kuketi pembeni yake.
" Emmy mwanangu umepatwa na matatizo gani?
" kwa nini mama? akauliza emmy
" Kwani hujui matatizo uliyonayo mwanangu? akauliza kwa upole mama yake.
" mama mimi mbona niko sawa na wala sina tatizo lolote lile."
" Emmy mimi ni mama yako na ninakupenda sana .Sikutegemea kabisa kama ungekuja kuwa namna hii."
" Kwani nikoje mama? akauliza Emmy huku ameinama chini
" Emmy umekuwa ni mtu wa ajabu sana.Kila mtu anashindwa kukuelewa.Mwanao Baraka amefariki dunia na wewe hukujulikana uko wapi. Umeendekeza starehe na ukamsahau kabisa mwanao.Mpaka leo hii hujui na wala hujauliza nini kilimuua mwanao. Kwako wewe umechukulia hili ni jambo rahisi sana lakini kwa kweli Emmy sisi wazazi wako tumeumia mno.Umetuumiza mno Emmy.Kingine ambacho umetufanya tuumie zaidi na tushindwe kukuelewa ni kitendo cha kuondoka msibani bila kuaga siku moja tu baada ya mazishi ya mwanao.Emmy wewe ni binadamu wa namna gani? Kila mtu anakusema wewe.Hapa mtaani tumepata aibu ambayo haielezeki." akasema mama yake Emmy .Emmy hakujibu kitu alikuwa ameinama chini .
" Baba yuko wapi ? akauliza Emmy.Mama yake akamtazama na kusema
" Ina maana hujasikia kilichompata mwenzako?
" Mwenzangu nani?
" Clara.Yule mwanamke ambaye yuko na Wayne kwa sasa"...akasema mama yake Emmy na kumfanya Emmy acheke kicheko kikubwa
" Mama unanishangaza sana.Clara atakuwaje mwenzangu wakati yeye ndiye aliyemchukua mume wangu? Kwani amefanya nini huyo Clara? akauliza Emmy kana kwamba hajui kilichomtokea Clara
" Amepatwa na ugonjwa wa ghafla na amepelekwa hospitali.Inasemekana amepooza mwili ."
" Amepelekwa hospitali gani?
" Nasikia amepelekwa St Patrick Hospital."
Huku akitabasamu Emmy akasema
" Mama mimi siwezi kusema kwamba nimeumia au ninasikia uchungu wowote kwa sababu ni huyu huyu Clara ndiye aliyefanya mimi na Wayne tukatengana. Kwangu mimi nimefurahi sana kwani hii ndiyo dawa yake na akome kurukia mabwana wa watu.." akasema Emmy huku akicheka.Mama yake akamuangalia kwa macho makali
" Emmy huna haya hata kidogo ..wewe ndiye unaweza ukasimama na kuthubutu kutamka hayo maneno uliyoyatamka? Huna aibu hata kidogo.Umemfanyia Wayne mambo mabaya na ya aibu ambayo hayaelezeki .Baada ya mambo yote haya uliyomfanyia mwenzio unaweza kweli leo hii ukathubutu kusimama na kumlaumu Clara..Hayawani mkubwa wewe" akasema mama yake Emmy ambaye alianza kupandwa na hasira.
" Mama kosa langu nini hadi uniite hayawani? akauliza Emmy
" Ndiyo wewe ni sawa na hayawani.Umekuwa na roho ya kishetani hasa siku hizi.Hata mwanao amefar............." akasema mama yake kwa ukali lakini kabla hajaendelea zaidi Emmy akasimama.
" Stop it mother...Tafadhali naomba mniache mimi na maisha yangu. Msinifuate fuate .Tayari umekwisha niita mimi hayawani na ninaomba uniache na maisha yangu kama hayawani.Narudia tena mama nawaombeni mniache mimi na maisha yangu na sitaki mtu yeyote yule ayafuatilie maisha yangu.Hakuna hata mtu mmoja aliye upande wangu kwa hiyo niacheni niishi mwenyewe.Niacheni nilie mwenyewe..." akasema Emmy kwa ukali huku akiinuka na kuondoka kwa kasi mle chumbani akapanda gari lake na kuondoka zake .Mama yake akabaki chumbani akilia.
" Kuanzia sasa sitaki kabisa mtu yeyote ayafuatilie maisha yangu.Si wazazi wangu au mtu yeyote yule mwenye ruhusa na maisha yangu .Nitayaendesha maisha yangu kwa namna ninavyotaka mimi na si kwa namna wanavyotaka watu..." akasema Emmy akiwa amefura kwa hasira
" Kumbe Clara amepelekwa St Patrick hospital..hahahaaa..nitakwenda kumtembelea jioni ya leo.Kwanza ninaanza na Sheila halafu nitakwenda kumtembelea Clara jioni ..Mimi ndiyo Emmy bwana.hahahaaa.." Emmy akaongea mwenyewe huku akicheka wakati akikata kona ya kuingia nyumbani kwake.
Baada tu ya kuingia ndani mwake Emmy akajitupa sofani.
" Uuphh ! siku ilikuwa ndefu sana." akasema Emmy kisha akainuka akaelekea katika friji akachukua vipande vya barafu na chupa ya mvinyo akajimiminia katika glasi.
" Home sweet home “ akasema Emmy akiwa amekaa sofani
“This is my life now..Haya ndiyo maisha yangu mapya.Nyumba imepoa utadhani hakuna binadamu anayeishi humu.Lakini haya ni mambo ya mud amfupi tu kwa sababu muda si mrefu nina hakika Wayne atarejea na nyumba itakuwa na furaha tena. Nataka niwakate vilimi limi wale wote waliokuwa wakinicheka kwamba nimeachika. Najua wako wengi ambao walikuwa wakinicheka baada ya Wayne kuniacha.Baada ya Wayne kurudi kwangu watanikoma. Kwa kweli nilimfanyia Wayne vituko vingi sana na sikufahamu thamani yake kwa wakati ule lakini kwa sasa ndiyo ninaiona thamani yake.Japokuwa nina kila kitu .Ameniachia nyumba,gari na biashara zote lakini vyote hivi haviwezi kunipa furaha ya maisha yangu. Kwa mara ya kwanza ninaliona pengo la Wayne katika maisha yangu. Ninaapa nitatembea hadi mwisho wa dunia hadi nihakikishe Wayne anarudi katika nyumba hii.Lazima niishi naye tena.Sintaweza kumpata mwanaume mwenye moyo wa upendo na uvumilivu kama yeye." akawaza Emmy huku akipiga mafunda ya mvinyo mfululizo .
" Sina muda wa kupumzika ngoja kwanza nimuendee Sheila .Amenidharau kiasi ambacho siwezi kuvumilia.Mimi huwa sipendi kudharauriwa na hilo analifahamu fika.Alikosea sana kunitolea maneno yale ya kashfa." akawaza Emmy kisha akaingia bafuni kuoga.
" Baba na mama watakuwa wamechukia sana lakini watanisamehe kwa sasa.Niko katika kipindi kigumu mno cha kumpigania Wayne.Siwezi kukubali kupokonywa Wayne toka katika mikono yangu.Lazima nipambane kumrudisha kwangu.Ninafahamu katika mapambano haya mambo mengi yatatokea na moja wapo ni hili la kumpoteza mwanangu Baraka .Inaniuma kumtoa mwanangu sadaka kwa mizimu lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya .Yote haya nimeyafanya kwa ajili ya kumrudisha Wayne kwangu." akawaza Emmy akiwa bafuni amejilaza katika jakuzi.Mara akakumbuka kitu akastuka.
" Nimemuwaza Baraka nimekumbuka kuhusu baba yake.Sheila aliniambia kwamba James anaweza akarejea siku yoyote katika wiki ijayo.Sijui nitamueleza nini ili aweze kunielewa lakini hilo haliniumizi kichwa.Kitu pekee ambacho kinaniumiza kichwa kwa sasa ni kumrejesha Wayne kwangu.Hili la James ni suala dogo tu.Nitamuelewesha kwamba mwanae alifariki ghafla na atanielewa.Isitoshe hajawahi kumuona Baraka hata mara moja kwa hiyo haliwezi kuwa suala litakalomuumiza sana." akawaza Emmy kisha akatoka mle bafuni akavaa na kuondoka.
Breki ya kwanza iilkuwa katika saluni ya Sheila.Ni moja kati ya saluni kubwa na ya kisasa jijini Arusha na ambayo kila dakika huwa inajaa akina mama wanaokuja kujiremba.Emmy akashuka garini na moja kwa moja akaelekea ndani ya saluni ile.Hakuitika salamu ya mtu yeyote na moja kwa moja akamfuata Sheila aliyekuwa anamsuka nywele mteja.
" Nimekuja sasa.Naomba unieleze mbele ya macho yangu yale maneno yako uliyoniambia katika simu" akafoka Emmy bila hata salamu.Watu wote mle ndani ya Saluni wakapatwa na mshangao. Emmy na Sheila wamekuwa marafiki wakubwa kwa miaka mingi na hakuna mtu aliyetegemea kama siku moja wangefikia hatua hii.Sheila akamuacha yule mteja aliyekuwa anamsuka na kumgeukia Emmy.
" Emmy tafadhali kama unataka kuongea na mimi si wakati huu.NItafute kwa muda wako tuongee na si sasa hivi." akasema Sheila ambaye naye sura yake ilionyesha kuwa na hasira kwa ujio ule wa Emmy
" Sina muda wa kukutafuta.Nimegundua kwamba wewe ndiye mchawi wangu.Sikujua Sheila kwamba wewe ni mwanamke mbaya sana na kumbe kuachana kwangu na Wayne umefurahia sana.Hasidi mkubwa wewe" akafoka Emmy
" Mchawi ni wewe mwenyewe wala usinitake maneno.Umeshindwa kumtunza bwana kwa uzembe wako mwenyewe hadi akakuacha.Waache wenye kujua kulea wamchukue wamtunze.Nakwambai utatafuta mchawi hadi mwisho wa dunia lakini mchawi ni wewe mwenyewe.Acha kuumiza watoto wa watu ambaohawana makosa " akasema Sheila.Emmy akapandwa na hasira akataka kumvaa Sheila lakini watu waliokuwemo mle ndani wakawahi kumzuia.
" Sheila naomba unisikilize vizuri.Kuanzia sasa mimi na wewe urafiki wetu umekwisha .Nimekuweka katika kundi la maadui zangu.Nitapambana na wewe na nitakuonyesha kwamba mimi ndiye Sheila .Nakwambia ndani ya siku saba utakuwa umelihama hili jiji.Pili nataka mpaka kesho jioni uwe umenirudishia milioni saba zangu ama sivyo nitakuja kuchukua kila kitu humu saluni kwa sababu hii ndiyo inakupa kiburi na dharau .Narudia tena kesho unirejeshee pesa zangu.Ukisihindwa kuzirejesha mpaka kesho jioni utanitambua mimi ni nani" akafoka Emmy kisha akachukua mkoba wake akauvaa begani na kuanza kutoka kwa hasira.Shughuli ndani ya saluni hii zilikuwa zimesimama kwa muda watu wote wakiushuhudia ugomvi kati ya marafiki wawili wakubwa.Hakuna aliyeamini kama urafiki wa Emmy na Sheila ungefikia hatua hii.Walikuwa ni zaidi ya marafiki lakini kitendo hiki cha kurushiana maneno kilizua maswali mengi sana miongoni mwa watu walioufahamu vizuri urafiki wao.Sheila alikuwa kimya na hakutaka kuzungumza lolote licha ya baadhi ya shoga zake kutaka kufahamu sababu iliyopelekea yeye na Emmy kutoleana maneno makali namna ile hadi kutaka kupigana. Sheila hakutaka kuongea lolote kuhusiana na kilichotokea,akapanda gari lake na kuelekea nyumbani kwake.
"Ukweli niliompa Emmy umemuuma sana na sasa anataka mapambano na mimi.Mimi haniwezi bado ni msichana mdogo sana yule `kupambana na mimi.Anatakiwa ajipange vizuri kupambana na mimi. Anajivunia pesa alizonazo na uchawi anaotaka kujifunza.Mimi hanitishi kwa lolote lile na kama akihitaji kupambana na mimi nitapambana naye na atajuta kupambana na mimi.Mimi si kama hao akina Wayne ambao walikuwa wakimchekea kila alipokuwa akiwafanyia dharau." akawaza Sheila akiwa garini kuelekea nyumbani kwake.
" Najua lengo lake kwa sasa ni kutaka kuniaibisha kwa kunidai pesa alizonikopesha. N i pesa nyingi ambazo siwezi kumlipa kwa sasa.Amesema hadi kesho jioni niwe nimemlipa pesa zake na nisipofanya hivyo anaweza akaniaibisha kweli hayawani yule.Lazima nizitafute pesa hizo kwa kila jinsi leo hii ili niweze kumrejeshea Emmy kuinusuru saluni yangu .Saluni ile ndiyo pekee ninayoitegemea hapa mjini na lenbo lake ni kuifunga ili nikose kitu chochote cha kutegemea.Siwezi kukubali hilo litkee.Nitazitafuta pesa zake nimrejeshee.Lakini nani anayeweza kunipatia pesa hizo zote kwa muda huu mfupi? Sheila akazidi kuumiza kichwa.
" Mwanaharamu huyu amenipa wakati mgumu sana wa kuzitafuta pesa hizo.Lakini hakuna shaka nitazipata tu halafu nione atanitafutia wapi tena. Sikutegemea kama Emmy angefikia hatua hii aliyofika sasa hivi.Amemuua mwanae kwa ajili ya mwanaume ambaye hamtaki tena.Na siku ikitokea jamii ikajua kwamba amemuua mwanae kwa sababu ya kumrejesha Wayne kwake sijui watamfanya nini.James baba yake Baraka anarejea wiki ijayo sijui atafanya nini wapo ataufahamu ukweli kwamba Emmy alimtoa mwanae kafara kwa mizimu kwa ajili ya kurudiana na Wayne.Ninazifahamu siri nyingi za Emmy na ninaweza kuzitumia kumbomoa kabisa lakini sitaki kufanya hivyo .Kitu cha msingi ni kuachana naye kabisa na kumfuta katika orodha ya marafiki zangu.Kuna wazo nimelipata pengine linaweza kunisaidia kulitatua tatizo hili." akawaza Sheila.
" Chris anaweza akanisaidia kupata hizo pesa.Ninamfahamu Chris ni mtu pekee ambaye ananiamini na anaweza akanipatia kiasi hicho cha pesa kwa makubaliano ya kumrejeshea kidogo kidogo. Chris ni mtu mwelewa sana na isitoshe anamfahamu vizuri Emmy hivyo anaweza akanisaidia .Hata kama hatakuwa na fedha hizo anaweza akanidhamii mahala nikazipata.Ngoja nikifika nyumbani nimpigie simu" akawaza Sheila..


***********************


Clara alipokelewa katika hospitali ya St Patrick na kwa haraka akaanza kushughulikiwa.Huduma zilizokuwa zikitolewa na madaktari na wauguzi wa hospitali hii zilitia moyo sana.Kwa muda swa masaa mawili sasa tulikuwa tumekaa katika sehemu za kupumzikia tukisubiri taarifa ya madaktari waliokuwa wakimshughulikia Clara.Hospitali pale nilikuwa na rafiki zangu Beka na Chris pamoja na baba mkwe.Hawa ndio waliokuwa watu wangu wa karibu sana katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa wa Clara.Nilikuwa nimeinama nikiwa na mawazo mengi sana.Sikuwa naongea chochote kile.Nilikuwa katika maumivu makali sana ya moyo.Nilikuwa nikitafakari kwa kina juu ya kilichotiokea lakini sikuweza kupata jibu la haraka haraka nini hatima ya maisha yangu na mambo yanayozidi kunikuta.Tukiwa tumeketi pale sofani katika sehemu hii ya kupumzikia Chris akapigiwa simu akainuka pale sofani na kuijtenga mbali nasi.Wakati akiongea na simu baba mkwe akanigeukia na kusema
" Wayne nakuomba usihuzunike sana kijana wangu.Hii ni mitihani ya maisha ambayo inamkuta kila mtu kwa hiyo nakuomba uwe mvumilivu na tuzidi kumuombea Clara.Mungu atamsaidia atapona.Mungu ni muweza wa yote na hashindwi na kitu chochote.Tumtegemee yeye pekee." akasema baba mkwe.
" Ahsante baba.Ninaamini Clara atapona lakini ninaumia sana kumuona akiwa katika hali ile. Kuna wakati ninawaza sijui ni kwa nini nilikutana naye.Endapo nisingekutana naye haya yote yasingemfika.Ninaona ni kama vile mimi ndiye nliyesababisha haya yote kumtokea" nikasema
" Usiseme hivyo Clara.Jambo kama hili lingeweza kumtokea mtu yeyote yule na wala usijilaumu kabisa kwa jambo kama hili kumfika Clara.Kitu cha msingi tumkazanie matibabu atapona na kurejea katika hali yake ya kawaida." akasema baba mkwe.
Chris akarejea na kujiunga nasi pale sofani.Usoni pake hakuonekana kawaida.Sikumjali nikaendelea na tafakari zangu.Saa kumi na moja za jioni tukaitwa katika ofisi ya daktari Daktari yule mzungu ambaye alikuwa akifahamu Kiswahili kidogo alitutaarifu kwamba wamemchunguza Clara na wamegundua kuna ufa katika fuvu la kichwa na tayari matibabu yake yamekwisha anza mara moja.Alitusihi tuwe wavumilivu kwa wakati huu ambao Clara ameanza kupatiwa matibabu.Alitueleza mambo mengi kuhusiana na ugonjwa ule na kutupa moyo kwamba Clara atapona na wala hakuna haja ya kuwa na wasi wasi.
Baada ya maelezo yale ya daktari alitusihi tukapumzike kwani pale hospitali mgonjwa wetu atapata kila aina ya huduma inayotakiwa. Kabla hatujaondoka nilimuomba daktari anipeleke nikamuone Clara.Daktari akaniongoza hadi katika chumba alichokuwa amelazwa Clara .Nilimuinamia pale kitandania alipokuwa amelala amefumba macho. Sura yake nzuri ilikuwa imebadilika sana.Nilidondosha machozi kwa uchungu niliousikia.
" I'm sorry Clara kwa mambo haya kukupata.Nitaendelea kukupenda hadi mwisho wa uhai wangu" nikasema kimoyomoyo halafu nikatoka mle chumbani.
" Wayne jipe moyo ndugu yangu.Clara atapona tu.." akasema Beka baada ya kuniona jinsi nilivyobadilika baada ya kutoka katika chumba cha Clara.
" Wayne nina wazo moja." akasema Chris.
" Sikushauri urejee tena hotelini ulikokuwa unaishi.Nina nyumba kubwa na ninakuomba ukaishi pale kwangu kwa muda wote utakaohitaji.Wewe ni zaidi ya ndugu yangu nakuomba tukaishi wote nyumbani kwangu tafadhali." akasema Chris.Ulikuwa ni ushauri mzuri kwa sababu mpaka wakati huo nilikuwa sijapata nyumba ya kuishi.Nilikuwa nikiishi hotelini na Clara baada ya kumuachia Emmy nyumba yangu.Sikuwa na ubishi wowote kwa sababu tayari mimi na Chris tulikwisha zimaliza tofauti zetu.
Tuliwasili katika nyumba ya Chris maeneo ya Njiro.Chris alikuwa akishi na mdogo wake mmoja pamoja na mfanyakazi wa ndani.Nilikaribishwa ndani na kuonyeshwa chumba changu cha kulala.Nilimshukuru sana Chris kwa ukarimu wake huu mkubwa.Amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu kwa sasa.Baada ya kuoga niliitwa sebuleni kwa ajili ya chakula.Japokuwa sikuwa nikijisikia kula chochote niliamua kujilazimisha kula ili niweze kupata nguvu.Baada ya kula tulikaa sebuleni tukiangalia muziki wa Injili katika runinga kubwa iliyokuwamo mle sebuleni.Tukiwa bado sebuleni tukitazama muziki huku Chris akijaribu kunipa maneno ya faraja akinukuu vifungu vya biblia , mara akaingia mtumishi wa ndani.
" Kaka kuna mgeni wako" akasema yule mtumishi .
" Mkaribishe ndani" akasema Chris.
Nilishikwa na mshangao mkubwa baada ya kumuona Sheila akiingia pale mlangoni.Nilimtolea macho makali nikimtazama kama ni yeye kweli au nimemfananisha.Alikuwa ni mwenyewe .Sheila naye alistuka mno aliponiona nikiwa pale nyumbani kwa Chris.Nadhani hakutegemea kunikuta pale kwa Chris mida kama ile.Tulibaki tunatazamana .Nilikabwa na fundo kubwa moyoni kwani huyu ndiye alikuwa mshirika mkubwa sana wa Emmy.


***********************



Saa kumi na mbili za jioni Emmy akasimamisha gari katika maegesho ya hospitali ya St Patrick.Akashuka na kuelekea moja kwa moja eneo la mapokezi.
“ habari yako dada” akasema Emmy akimsalimu muuguzi aliyekuwapo mapokezi.
“ Nzuri dada karibu sana ” akajibu yule muuguzi
“ Samahani dada naomba kuuliza.” Akasema Emmy
“ Bila samahani dada unaweza ukauliza” akajibu yule muuguzi
“ Nina ndugu yangu mmoja ameletwa hapa mchana wa leo akitokea hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi.Nimeambiwa amelazwa hapa.” Akasema Emmy
“ Anaitwa nani mgonjwa wako?
“ Anaitwa Clara.”
Muuguzi yule akatazama katika kompyuta yake na kulikuta jina la Clara.
“ Clara ambaye amepatwa na matatizo ya kupooza mwili? Akauliza yule muuguzi.
“ Ndiye huyo huyo.” Akajibu Emmy
“ Amelazwa katika Private ward namba 4.” Akajibu yule muuguzi.
“ Ninaweza kuruhusiwa kumuangalia .?
“ Samahani dada yangu kwa muda huu huwa haturuhusu watu kuingia wodini kuwatazama wagonjwa.Mwisho wetu hapa huwa ni saa kumi na mbili za jioni” akasema yule muuguzi
“ Ninaomba unisaidie dada yangu ili niweze walau kumuona ndugu yangu .Nimekuja na ndege toka Dr es salaam baada ya kupata taarifa zake.tafadhali naomba unisaidie nimuone tu japo hata kwa dakika moja.Nakuomba sana dada yangu.” Akaomba Emmy.Muuguzi yule akaingiwa na roho ya imani akaamua kumsaidia Emmy kwenda kumuona Clara.Muuguzi yule akamuomba muuguzi mwenzake amshikie kwa muda pale katika dawati lake wakati anampeleka Emmy kumuona Clara.
“Mgonjwa wako ni huyu” akasema yule muuguzi walipofika chumbani kwa Clara.
Moyo wa emmy ukapatwa na furaha ya ajabu baada ya kumuona Clara akiwa amelala pale kitandani hajitambui.
“ Haya ndiyo malipo yako Clara kwa kupenda kuvamia waume za watu.Kama huu ndio mchezo wako basi safari hii uliingia sehemu mbaya sana.Na hili ni onyo kwa wengine wote ambao watajaribu kutaka kuwa na wayne.Wote nitawafanya hivi hivi.Wayne ni wangu na atabaki kuwa wangu milele.Nakusikitikia sana Clara kwa sababu utalala hapo kitandani kwa maisha yako yote yaliyobaki na utashangaa pale utakaposhudia Wayne akirudiana na mimi tena.Ona ulivyobadilika ghafla.Uzuri wako wote umepotea.Umekuwa ni kama kituko mbele za watu.Na huu ni mwanzo utateseka kwa maisha yako yote mshenzi wewe.Tena una bahati sana nilikuonea huruma ,nikaamua kukuacha hai.Wayne aliachana na mimi kwa sababu yako wewe.Wewe ndiye mchawi wa ndoa yangu lakini kwa sasa ujanja wako wote umekwisha .” akawaza Emmy wakati akimuangalia Clara aliyekuwa amelala pale kitandani.
“ dada nadhani kwa leo inatosha.twende tuondoke kwani daktari akikukuta huku juu saa hizi nitakuwa katika matatizo makubwa” akasema yule muuguzi.
“ nashukuru sana dada yangu kwa msaada wako” akasema Emmy kisha akaifungua pochi yake na kuchomoa bunda la noti nyekundu akampatia yule muuguzi kiasi cha shilingi elfu hamsini.
“ Chukua hizi ni ahsante yangu kwa msaada wako” akasema Emmy na kumpatia yule dada pesa zile ambaye alibaki akishangaa asiamini macho yake..
“ Ahsante sana ” akasema yule muuguzi huku akiufunga mlango wa chumba kile cha Clara.
“ Hujaniambia jina lako unaitwa nani ? akauliza Emmy wakati wakishuka ngazi
“ Ninaitwa Agnes “ akajibu yule muuguzi
“ Nafurahi kukufahamu Agnes.mimi ninaitwa Emmy” akajibu Emmy
“ hata mimi nafurahi kukufahamu Emmy “ akajibu Agnes.
“ Agnes kama hutajali unaweza ukanipatia namba yako ya simu? Ninaweza kuwa nakupigia ili kujua maendeleo ya mgonjwa wangu. kwa sababu mimi ni mtu wa kusafiri safiri sana .”
Bila kusita Agnes akampa Emmy namba yake ya simu halafu naye akachukua ya Emmy.
“ nashukuru sana kwa msaada wako Agnes.Tutazidi kuonana.Nitakuwa nikija mara nyingi tu kumjulia hali ndugu yangu” akasema Emmy
“ Karibu sana dada Emmy.Mara nyingi huwa ninakuwepo zamu ya usiku.” Akajibu Agnes.
Emmy akaingia katika gari lake na kuondoka.
“ Clara kwisha habari yake kwa sasa uwanja ni mpana kwangu kumrudisha Wayne.Namshukuru sana mzee Mtuguru kwa msaada wake huu.Nitamtafutia zawadi kubwa sana yule mzee .Hizi tiba za asili zinasaidia mno lakini watu wanazidharau.Ingawa wakati mwingine zinaweza kukugharimu uhai wa mtu kama ilivyonigharimu mimi lakini zinasaidia sana.Kwa sasa ninahesabu masaa tu kabla ya Wayne hajarejea tena nyumbani kwangu.Ninachotakiwa ni kuanza kufanya maandalizi kuanzia pale nyumbani. Itanibidi nipake nyumba rangi ,ikiwa ni pamoja na kubadilisha fenicha na kila kitu ndani ili Wayne atakaporejea tena nyumbani akute mabadiliko makubwa sana . “ akawaza Emmy huku akitabasamu usoni .


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………
 
BEYOND PAIN
SEHEMU YA 31
MTUNZI :pATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Bila kusita Agnes akampa Emmy namba yake ya simu halafu naye akachukua ya Emmy.
“ nashukuru sana kwa msaada wako Agnes.Tutazidi kuonana.Nitakuwa nikija mara nyingi tu kumjulia hali ndugu yangu” akasema Emmy
“ Karibu sana dada Emmy.Mara nyingi huwa ninakuwepo zamu ya usiku.” Akajibu Agnes.
Emmy akaingia katika gari lake na kuondoka.
“ Clara kwisha habari yake kwa sasa uwanja ni mpana kwangu kumrudisha Wayne.Namshukuru sana mzee Mtuguru kwa msaada wake huu.Nitamtafutia zawadi kubwa sana yule mzee .Hizi tiba za asili zinasaidia mno lakini watu wanazidharau.Ingawa wakati mwingine zinaweza kukugharimu uhai wa mtu kama ilivyonigharimu mimi lakini zinasaidia sana.Kwa sasa ninahesabu masaa tu kabla ya Wayne hajarejea tena nyumbani kwangu.Ninachotakiwa ni kuanza kufanya maandalizi kuanzia pale nyumbani. Itanibidi nipake nyumba rangi ,ikiwa ni pamoja na kubadilisha fenicha na kila kitu ndani ili Wayne atakaporejea tena nyumbani akute mabadiliko makubwa sana . “ akawaza Emmy huku akitabasamu usoni

ENDELEA……………………………..

Nilipandwa na hasira kwa kumuona Sheila pale nyumbani kwa Chris.Nilisimama huku uso wangu ukiwa umejikunja kwa hasira.Midomo ilikuwa inanitetemeka.Huyu ndiye alikuwa rafiki mkubwa wa Emmy na ndiye alikwenda naye kwa mganga Mombo na kumuua Baraka.Chris aliniangalia mimi halafu akamuangalia na Sheila ambaye bado alikuwa amesimama akitetemeka alikosa neno la kusema.Midomo yake ilikuwa inamtetemeka.
“Sheila unatafuta nini huku? Emmy amekutuma uje unipeleleze? Amekutuma uje unimalize na mimi? Haya yote miliyoyafanya hayawatoshi hadi mnifuate huku? Nimewakosea nini hadi mnifanyie ukatili wa kiasi hiki? Clara amewakosea nini mpaka mumtese kiasi kile? Nikasema kwa ukali huku nikimuangalia Sheila kwa macho makali,akaogopa sana.Akiwa bado amesimama pale mlangoni ghafla kwa kasi ya ajabu nikamfuata na kumshika mkono nikamvuta kumtoa nje
“ Toka ndani ya nyumba hii muuaji mkubwa wewe.Kamwambie huyo aliyekutuma kwamba siku zake zinahesabika na malipo ni hapa hapa duniani” nikasema kwa ukali.Chris akaniwahi na kunizuia
“ Wayne ! tafadhali punguza hasira.” Akasema Chris
“ siwezi kupunguza hasira Chris..Huyu ndiye mshirika mkubwa wa Emmy na ametumwa aje animalize.Tafadhali Chris niache nimshughulikie.Wamemuua Baraka ,na sasa wanamtesa Clara ambaye hana kosa lolote na kama haitoshi bado wananifuata hadi huku..” nikasema kwa ukali
“Wayne nakuomba ndugu yangu punguza hasira na tumsikilize Sheila amekuja kutafuta nini.” Akasema Chris huku akimshika mkono Sheila na kumuingiza ndani.Alikuwa analia.Nilitamani kumshushia kipigo kitakatifu mwanamke Yule lakini nikaheshimu ushauri wa Chris kwamba tumsikilize Sheila amekuja kutafuta nini usiku ule.
“ Sheila karibu sana.Habari za huko utokako? Akasema Chris .Sheila akafuta machozi na kusema kwa sauti ndogo
“ Kwema”
“ Nashukuru kusikia hivyo.Karibu sana” akasema Chris
“ ahsante Chris”
“Sema kilichokuleta na uondoke hapa haraka sana.Una bahati hapa ni nyumbani kwa Chris .Ingekuwa ni nyumbani kwangu nakuapia ningekukata shingo.Nakuchukia sana Sheila wewe na shoga yako Emmy” nikasema na kumfanya Sheila aendelee kuangusha machozi.
“ Hutaki kueleza alichokutuma muuaji mwenzako? Nikasema kwa ukali huku nikisimama kumuendea pale sofani
“Sijaja hapa kwa sababu ya Emmy na wala hajanituma chochote” akajibu Sheila baada ya kuona ninamuendea.
“Nini kimekuleta hapa basi kama Emmy hajakutuma? Nikauliza
“ Nimekuja kwa ajili ya maongezi na Chris na sikutegemea kama nitakukuta huku” akasema Sheila.Nikarudi mahala pangu na kukaa
“Nakusikiliza Sheila.ulikuwa na shida gani nami? akauliza Chris
“ Samahani Chris tunaweza tukaongea nje?
“ Hapana tuongelee hapa hapa mbele ya Wayne.Una tatizo gani?
Huku akisita Sheila akasema
“Nimekuja ninahitaji msaada wako Chris”
“ Msaada gani Sheila?
“Ninahitaji unikopeshe fedha”
“ Shilingi ngapi unahitaji?
“ Nahitaji shilingi millioni saba”
“ Millioni saba? Mimi na Chris tukastuka kwa pamoja
“ Ndiyo ninahitaji unikopeshe kiasi hicho cha fedha au hata kama huna basi nitafutie hata kwa marafiki zako na nitakurejeshea ndani ya kipindi kifupi”
“ Dah ! hizo ni fedha nyingi sana Sheila..una zihitaji lini na kwa tatizo gani?
“ Ni kweli ni fedha nyingi lakini ninakuahidi nitazirejesha ndani ya kipindi kifupi.Ninazihitaji kabla ya kesho jioni”
“ Kabla ya kesho jioni? Hilo haliwezekani Sheila.fedha hizi ni nyingi na hakuna uwezekano wa kuzipata ndani ya kipindi kifupi namna hiyo.Inahitaji muda kuzitafuta” Akasema Chris.Sheila akaonyesha uso wa kukata tamaa kwa jibu lile
“naomba unisaidie Chris.Nina shida kubwa na ya haraka” akasema
“ Una tatizo gani Sheila? Nikauliza.
“ kweli Sheila hebu tueleze una tatizo gani ili tufahamu pengine kunaweza kuwa na namna bora zaidi ya kukusaidia kulitatua tatizo lako” akasema Chris.Sheila akajikaza na kusema
“Nimekorofishana na Emmy na amenitaka nimlipe pesa zake alizonikopesha kwa ajili ya kufungua ile saluni.Ameahidi kunidhalilisha kama mpaka kesho jioni sintakuwa nimempatia pesa zake zote” akasema Sheila.Nilishindwa kujizuia nikacheka
“ Sheila huo uongo wako kamdanganye mtu mwingine na si mimi .Chris tafadhali usimsikilize huyu mwanamke.Kuna jambo lililomleta hapa na si hilo.Huyu hawezi hata siku moja kukorofishana na Emmy.Huyu ndiye mshauri wake mkuu na mambo yote haya ambayo Emmy amekuwa akiyafanya huyu ndiye mshauri wake” nikasema
“ Ni kweli Wayne nimekosana na Emmy naomba mniamini.”
“ Nini kimesababisha mkakorofishana? Akauliza Chris
“Kwanza kabisa naomba nikiri kwamba ni kweli kama anavyosema wayne kwamba mimi na Emmy tulikua marafiki wakubwa na kila mara Emmy alikuwa anakuja kuniomba ushauri lakini jambo moja ambalo nyote hamlifahamu ni kwamba sikuwa namkubalia Emmy katika masuala yote aliyokuja kuniambia lakini alikuwa mbishi na nyote mnamfahamu Emmy akiamua jambo hataki mtu mwingine amshauri visivyo”
“ Usitudanganye Sheila.Wewe si uliambatana na Emmy kwenda kwa mganga Mombo na mkamuua Baraka? Nikauliza.Sheila akakaa kimya
“ Mbona hujibu? Kama si kweli weka wazi” nikasema
“Ni kweli Emmy aliniomba niambatane naye kwa mganga kule Mombo” akasema Sheila
“ Nini lilikuwa dhumuni la kwenda kule na kitu gani kilifanyika? Nikauliza
“Emmy alidai kwamba kuna mtu aliyekuwa anamroga na ndiyo maana ukaamua kuachana naye kwa hiyo alitaka kwenda kumfahamu mtu huyo.Tulifika pale na dawa ikafanyika usiku…” Sheila akasita
“ Nini kikaendelea? Nikauliza
“ Ndiyo kama hayo yaliyotokea.Tulipofika hapa tukaambiwa kwamba Baraka amefariki ghafla” akasema
“Unataka kututhibitishia kwamba hamkujua toka mkiwa kwa mganga kwamba Baraka amefariki dunia?
“Mimi nilikuja kufahamu baada ya kufika huku Arusha lakini Emmy alionekana kufahamu kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa akifanyiwa dawa usiku ule na hata wakati wa msiba aliniambia kwamba hakujua kama Baraka alikuwa anatolewa kafara kwa mizimu kama malipo ya kukurudisha mikononi mwake.” Akasema Sheila na kwa hasira nikainuka.Chris akaniwahi na kuniomba niketi
“Jana alinitaka nimsindikize tena kwa mganga lakini nikakataa akaenda mwenyewe.Wakati akirudi akanipigia simu na kunitaarifu kwamba tayari amekwisha mmaliza Clara.Nilimweleza ukweli kwamba anachokifanya si kitu kizuri na kwamba aache kuwaumiza watu wasio na makosa.Kauli ile hakuipenda ndiyo maana akaamua kuja na kutaka kunidhalilisha.Kwa hivi saa urafiki wetu umekufa.wayne ninaomba msamaha sana kwa kushirikiana na Emmy.Najua tumekukosea sana na sijui nitafanya jambo gani ili uweze kunisamehe.” Akasema Sheila huku akitoa machozi.Nikamuangalia kwa macho makali na kusema
“ Kitu kimoja tu ambacho unaweza ukafanya kitakachonifanya nikusamehe.Nataka Clara arudishwe katika hali yake ya kawaida.Hapaswi kuteseka bila kosa.Ukiweza kulifanya hilo nitakusamehe Sheila na nitajua kwamba ni kweli unajutia ulichokifanya” nikasema na Chris akageuka na kunitazama..Sheila akainama chini
“ Unaweza ukafanya hivyo? Nikamuuliza
“ Wayne aliyefanya mambo haya ni mganga wa kienyeji na mimi sina nguvu zozote za kuweza kutengua uchawi huu alioufanya.Ninachoweza kufanya mimi ni kwenda kumuomba Yule mganga aweze kumponya Clara na amrudishe katika hali yake ya kawaida” akasema Sheila
“Unapakumbuka mahala anakoishi huyo mganga? Nikauliza
“Ndiyo napakumbuka”
“ Kesho asubuhi mimi na wewe tunaongozana hadi kwa mganga Mombo.Nataka nikaongee naye mimi mwenyewe na kama akishindwa kufanya ninavyotaka basi ama zake ama zangu” nikasema kwa hasira
“ Wayne..!! akasema Chris
“Chris niache niende kwa huyo mganga siku ya kesho.Nataka akatengue kila kitu alichomfanyia Clara.Siko tayari kumuona akiendelea kuteseka namna ile bila kosa” nikasema huku machozi yakinilenga kila pale sura ya Clara iliponijia kichwani
“Wayne sikushauri uende huko kwa mganga.Hizi ni nguvu za giza na siku zote nguvu za mwovu si lolote mbele ya nguvu za Mungu.Tumtumaini Mungu pekee na atamponya Clara.Atazivunja vunja nguvu zote za giza na Clara atakuwa mzima tena.Nimekwisha ongea na baba askofu na ameniambia kwamba kuanzia kesho atakuwa akienda kumfanyia maombi Clara mchana na jioni.Tafadhali naomba tumuachie Mungu tatizo hili” akashauri Chris
“ Chris najua kwa sasa wewe umeokoka na unamuamini Mungu na hata mimi ninamuamini Mungu lakini kwa hali aliyonayo Clara inanilazimu kumfuata huyo mganga na kumtaka atengue uchawi wote aliomroga Clara.Clara hawezi kuendelea kuteseka wakati mtu aliyemroga yupo na anajulikana.Kesho asubuhi ninamfuata huko huko Mombo” nikasema halafu kikapita kimya kifupi
“ Chris kwa hiyo utanisaidia kuhusu ule msaada niliokuomba? Akauliza Sheila
“Nashinda kukupa jibu Sheila kwa sababu mambo yangu kifedha hayaniendei vizuri sasa hivi.Nadhani ungenipa muda wa kama siku mbili hivi ili nikutafuitie hizo pesa” akasema Chris
“ Nitakukopesha mimi hizo fedha lakini mpaka baada ya kurejea toka kwa huyo mganga huko Mombo.” Nikasema

* * * *

Saa kumi na mbili za asubuhi tayari nilikwisha mpitia Sheila na tulikuwa njiani kuelekea kwa mganga baada ya kupita kwanza hospitali kwenda kujua hali ya Clara.Bado hali yake ilikuwa vile vile na hakukuwa na unafuu wowote.Nilimuelekeza Chris kwamba afanye mawasiliano na ofisi kuu ya Clara iliyopo afrika kusini na kuwataarifu kuhusiana na ugonjwa huu wa Clara.
Safari yetu ilikuwa ya kimya kimya .Nilikuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na mustakabali mzima wa kinachoendelea.Niliwaza ni chuki gani aliyonayo Emmy kwangu kiasi cha kunifanyia mambo ya namna hii.Nilimpatia kila kitu alichokihitaji na sikumbuki kama kuna kitu ambacho aliwahi kutaka akakikosa.Kama hakuna kitu chochote kibaya nilichomfanyia kwa nini basi anifanyie haya anayoyafanya? Ni mambo ambayo inahitaji moyo wa kipekee kuyavumilia na ninamshukuru Mungu nimeyavumilia yote lakini kwa hili la kumuumiza Clara namna ile sintakubaliana nalo hata kidogo,ni jambo ambalo limeniumiza mno” nikawaza huku tukiendelea na safari.Mawazo yale yakanipelekea nikumbuke kwamba pembeni yangu alikuwa amekaa mshirika mkubwa wa Emmy katika mambo haya yote.Nikageuza shingo na kumtazama Sheila akagundua kwamba sikumtazama kwa jicho zuri akainamisha kichwa.
Tulfika Mombo na Sheila akaniongoza hadi tulipofika nyumbani kwa mganga.
“ Ni hapa” akaema Sheila
“ Una hakika?
“ Ndiyo ni hapa” aaksema Sheila halafu tukashuka
“ Hodi wenyewe “ nikabisha hodi lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeniitikia.hakukuwa na dalili zozote za mtu pale nyumbani.Milango yote ilikuwa imefungwa
“ Sheila mbona hakuna mtu yeyote hapa nyumbani? Nikauliza
“ Hata mimi nashangaa sana lakini hapa ndipo nyumbani kwa mganga ambaye amekuwa akimfanyia Emmy mambo yote.”
“ Amekwenda wapi? Nikauliza
Siwezi kujua Wayne.Pengine anaweza kuwa amekwenda shambani au katika shughuli zake
“ Tutamsubiri hadi atakaporejea.Hatutaondoka leo hii kabla huyo mganga hajarejea na leo hii lazima atamrudisha Clara katika hali yake ya kawaida ama sivyo ama zake ama zangu” nikasema na kukaa juu ya jiwe.Nilikuwa na hasira sana.
Sikutaka kuondoka pale nyumbani kwa mganga hadi atakaporejea.Niliamini hatakuwa ameenda mbali sana .Wakati tukiendelea kumsubiri nilizunguka nyuma ya nyuma ile ili niiyasome mazingira lakini sikuona kitu cha maana zaidi ya vyungu vingi na vibuyu na ngozi za wanyama.Nilirudi na kukaa juu ya jiwe pembeni ya Sheila.Nikainamisha kichwa.
Tukiwa tumekaa tunaendelea kumsubiri mganga arejee simu yangu ikaita.Alikuwa ni Chris.
“ Hallow Chris” nikasema baada ya kupokea simu
“ Habari za huko Wayne? Umeshafika?
“ Tayari nimeshafika Chris lakini huyu mganga hayupo na siwezi kuondoka hapa bila kuonana naye.Ninamsubiri hadi atakaporejea. Maendeleo vipi?
“Niko hospitali na hakuna mabadiliko yoyote lakini kuna kitu ninataka kukufahamisha”
“ Kitu gani Chris?
“ tayari nimewasiliana na ofisi ya Clara kule afrika ya kusini na kuwafahamisha kuhusu ugonjwa wake.Wamenitaarifu kwamba tayari wamewasiliana na wazazi wa Clara walioko jijini Dar es salaam . Muda mfupi uliopita nimepokea simu toka kwa baba yake Clara akinitaarifu kwamba watawasili hapa Arusha na ndege leo saa tisa alasiri.”
“ baba yake Clara anakuja? Nikastuka kidogo
“ Ndiyo Wayne.Itakuwa vizuri kama ungekuwepo wakati watakapofika.”
“ sasa tutafanya nini Chris? Mimi bado naendelea kumsubiri huyu mganga” nikasema
“ Wayne ninachokushauri ni kuachana na huyo mganga na uanze safari ya kurudi ili uje uonane na wazazi wa Clara na kwa pamoja tuone namna tutakavyomsaidia mgonjwa“ akasema Chris.Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa nikitafakari kisha nikasema
“Nimekuelewa Chris.Ninaanza safari ya kurudi.”
“ Ok Wayne.Utanikuta hapa hospitali”
Baada ya kumaliza kuongea na Chris nikamgeukia Sheila aliyekuwa amejiinamia juu ya jiwe.
“ Sheila twende turudi Arusha.”
“ Kuna nini tena? Si ulisema tukae tumsubiri mganga?
“ Hapana hatuwezi kuendelea kukaa hapa.Tunatakiwa kurejea Arusha mara moja.Baba yake Clara anakuja Arusha kwa hiyo natakiwa niwepo” nikasema huku nikielekea garini.Clara naye akainuka na kuja garini tukaanza safari ya kurudi.
Kichwa changu kilikuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na nitakachowaeleza wazazi wa Clara kwani hadi matatizo yale yanamkuta mimi ndiye nilikuwa naye.
Tukiwa tumefika moshi mjini simu ya Sheila ikaita,akapokea na kuzungumza na mtu yule aliyempigia na baada ya kumaliza kuongea akanigeukia.
“ James amekuja”
“ james ?!! nikashangaa
“ Ndiyo James.Humfahamu?
“ hapana simfahamu kabisa.Ni nani huyo James?
Sheila akakaa kimya kidogo akafikiri na kusema
“Wayne naomba nikueleze ukweli
“ Ukweli gani tena Sheila?
“Huyu mtu anayeitwa James ndiye baba mzazi wa Baraka”
Nilistushwa na taarifa ile ikanilazimu kupunguza mwendo wa gari na kuliegesha pembeni .
“ baba mzazi wa Baraka? Nikauliza
“ Ndiyo Wayne.James ndiye baba mzazi wa Baraka?
Nikamtazama Sheila kwa muda halafu akasema
“ James na Emmy walianza urafiki wao zamani sana na katika mipango yao walipanga kwamba siku moja wafunge ndoa.Emmy aliolewa na wewe bila James kujua kwa sababu ni mtu wa kusafiri safiri kwenda nje ya nchi.Hata wakati akiwa tayari ameolewa na wewe bado aliendelea kutembea na James bila ya yeye kufahau kwamba alikuwa tayari ameolewa.Ilitokea James akasema kwamba anakwenda kusoma nje ya nchi na alipoondoka alimuacha Emmy akiwa na mimba changa kabisa ambayo alikudanganya kwamba ni ya kwako.”
Jasho lilianza kunitoka kwa taarifa ile.Kumbu kumbu za nyuma zikaanza kunirudia .
“James alinipigia simu wiki mbili zilizopita na kunitaarifu kwamba anarejea nchini na hii simu aliyonipigia alikuwa ananitaarifu kwamba tayari amekwisha rejea na kwamba anahitaji kuonana nami usiku wa leo.Amefikia hotelini na hataki mtu mwingine yeyote afahamu kama amewasili” akasema Sheila.
“ Huyo James anafahamu kwamba mwanae Baraka amefariki dunia?
“ Hana taarifa hizo na hajui kama alimuacha Emmy akiwa na mimba changa”
“ Too bad” nikasema halafu nikawasha gari na kuendelea na safari
“ Emmy ni shetani.Kwa nini nilimpenda mwanamke kama yule asiyekuwa na hata chembe ya ubinadamu? Kwa mambo aliyonitendea malipo yake yatakuwa hapa hapa duniani.” Nikawaza na sikutaka kichwa changu kijishughulishe sana na Emmy kwa wakati ule akili yangu yote niliielekeza kwa Clara.Sheila alikuwa kimya akitafakari na kuna wakati nilimuona kama anatabasamu
“ Unawaza nini Sheila? Nikauliza
“ Wayne Its pay back time..Emmy alidhani anauwezo wa kupambana nami basi leo ndio mwisho wake.Ninakwenda kumbomoa kwa James.Nitamueleza madhambi yake yote .Safari hii amelamba galasa.Nitamueleza james kila kitu ninachokifahamu kuhusu yeye.” Akasema Sheila
“ Fanya ufanyavyo Sheila lakini mimi sitaki kabisa kumsikia Emmy masikioni wangu..Mambo aliyonitenda ni makubwa na yanasikitisha.Sitaki tena kusikia chochote .Imetosha “ nikasema
Tuliendelea na safari yetu hadi tulipofika Arusha mjini,nikampeleka Sheila nyumbani kwake halafu nikaelekea hospitali.Mida hiyo ilipata saa moja za jioni na tayari giza lilikwisha ingia.Nilihisi uchovu mkubwa kwa safari ile ndefu isiyokuwa na manufaa yoyote.Pamoja na uchovu ule lakini ilikuwa ni lazima kufika hospitali kumuona Clara na kuonana na wazazi wake.
Nilimpigia simu Chris na kumfahamisha kwamba tayari nimekwisha rejea na kumuuliza kama alikuwapo hospitali,akasema kwamba alikuwa na wazazi wa Clara akiwasaidia kutafuta chumba hotelini kwa ajili kulala usiku huo .Baada ya kuongea naye nikaelekea moja kwa moja hospitali .Nilifika hospitali na kuonana na madaktari waliokuwa wanamshughulikia Clara.Bado hali yake haikuwa ya kuridhisha japokuwa madkatari walinipa moyo na kuniambia kwamba anaendelea vizuri .Sikutaka kumuona akiwa katika hali ile ya kutoweza kufanya chochote.hakuweza kula , kuongea wala kunyanyuka .Niliumia sana kwa hali ile.Nilikaa pembeni ya kitanda chake nikimuangalai huku machozi yakinitoka
“ Kwa nini uteseke namna hii Clara? Umekosa nini kiasi cha kumfanya Emmy akutese kiasi hiki? Nikasema kwa sauti ndogo huku machozi yakinitoka.

**********************

Meza ilikuwa imechafuliwa na chupa za pombe na nyama za kuku.Wanawake watatu walikuwa wameizunguka meza ile wakifurahi kwa kunywa pombe na kucheza muziki.
“ Kunyweni shoga zangu.Kunyweni watu wangu .Achaneni na yule shetani Sheila.Anadhani anaweza akapambana na mimi ? Nawaambia nitamuonyesha mimi ni nani.Nitamuonyesha kati yangu naye nani aliwahi kufika mjini.Sheila huyu ambaye ni mimi ndiye niliyemfanya akaonekana mtu kati ya watu lakini anakuja na kutaka kunipanda kichwani.Sintakubali hata kidogo.Na kwa nyie wote yeyote ambaye anaona kwamba hawezi kuendana na mimi ni bora akaondoka zake mapema na asisubiri hadi tukorofishane.Mimi nikikorofishana na mtu huwa nina kisasi kibaya sana.Mtaona kwa Sheila nataka nimuhamishe mji huu.tena ngoja nimkumbushe kuhusu pesa zangu.” Emmy akawaambia shoga zake wawili aliokuwa nao pale sebuleni wakinywa pombe.Akachukua simu ake na kumpigia Sheila
“ Hallo we mwanamke umeshazipata pesa zangu? Akauliza Emmy kwa dharau kubwa
“ Mbona unanisumbua kwa vihela vidogo kama hivi Emmy? Tayari ninayo pesa yako pita saluni kwangu kesho asubuhi uchukue vijisenti vyako” Sheila akajibu kwa dharau na kumfanya Emmy ahamaki.
“ Bahati yako umezipata lakini bado nitaendelea kupambana nawe na ninakuhakikishia vita hii haitakwisha mpaka hapo utakapokuwa umeuhama huu mji” akasema Emmy kwa hasira na mara akasikia kuna simu nyingine inaingia.Akatazama ilitoka kwa nani ,simu ile ilitoka kwa Agnes yule muuguzi ambaye jana yake alimpatia kitita cha fedha kwa ajili ya kumruhusu aingie amuone Clara katika chumba alicholazwa.
“ Agnes anataka nini? Ile kazi niliyomuachia tayari ameshaifanya? Akawaza Emmy halafu akaikata simu aliyokuwa amempigia Sheila akampigia Agnes
“Hallo Agnes habari yako?
“ habari nzuri dada Emmy”
“ Kuna habari gani hapo hospitali ? akauliza Emmy
“ dada Emmy yule mtu ambaye ulisema nikufahamishe pindi akifika hapa tayari amefika na ameingia chumbani kwa Clara”
“ Ouh good job Agnes.Nitakutafutia zawadi nzuri sana kwa kazi hii nzuri.Ninakuja hapo muda si mrefu” akasema Emmy na kukata simu.Uso wake ulichanua kwa tabasamu
“ ladies endeleeni kula na kunywa.Kuna mahala ninataka kwenda mara moja.Nitarejea muda si mrefu” Emmy akawaambia wale mashoga zake aliokuwa nao pale sebuleni kisha akaelekea chumbani kwake.Akaoga haraka haraka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kutoka.Baada ya kuhakikisha kwamba amependeza vilivyo akajipaka dawa ambayo alipewa na mganga kwamba ajipake mwilini siku atakayokwenda kuonana na wayne.Ilikuwa ni dawa yenye harufu kali hivyo ikamlazimu ajipulizie na uturi mkali kupoteza harufu kali ya ile dawa.Dawa nyingine iliyokuwa katika pembe la ng’ombe akaiweka katika mkoba halafu akatoka na kuingia garini akaondoka zake.
“ kama isingekuwa ni kwa ajili ya kumtaka wayne ,nisingethubutu kujipaka dawa hii yenye harufu kali na mbaya namna hii,lakini hata hivyo kwa ajili ya Wayne niko tayari kufanya kila linalowezekana .Nataka nimpate tena Wayne.Nitafanya kila ninaloweza na sintalala hadi nihakikishe Wayne amerudi kwangu tena.” Akawaza Emmy

**********************

Bado nilikuwa nimekaa pembeni ya kitanda cha Clara nikimtazama na machozi yakinitoka.Nilikumbuka toka siku ya kwanza niliyokutana naye ,tukaanzisha urafiki na hatimaye tukawa wapenzi.Niliumia sana kwani tayari nilikuwa na ndoto nyingi na mrembo huyu aliyeingia moyoni mwangu kuliko mwanamke yeyote niliyewahi kukutana naye chini ya jua.Nilijiona ni kama mtu mwenye mkosi kutokana na namna maisha yangu yalivyokuwa yakikabiliwa na matatizo.Chuki yangu dhidi ya Emmy ikaongezeka.
“ Bahati yake na yule mchawi kama ningemkuta leo sijui nini kingetokea.Ilikuwa ama zangu ama zake.” Nikawaza halafu nikamuinamia Clara na kumbusu
“ Nakupenda sana Clara na nitafanya kila linalowezekana hadi upone na urejee hali yako ya kawaida” nikamwambia Clara huku machozi yakinitoka
“ wewe ni mwanamke wa pekee kabisa kuwahi kutokea katika maisha yangu.Wewe ndiye maisha yangu na kila kitu changu.Ninakuahidi sintakuacha na nitafanya kila linalowezekana ili upone” nikasema na mara simu yangu ikaita.Alikuwa ni Chris.
“ hallow Chris “ nikasema
“ Wayne uko hapo hospitali?
“Ndiyo Chris niko hospitali” nikajibu
“ Ninakuja na wazazi wa Clara.Naomba tukutane hapo chini kwa ajili ya maongezi.Wanahitaji kuongea nawe”
“ sawa Chris mtanikuta pale chini nikiwasubiri” nikasema na kukata simu.Nikamuangalia tena Clara nikambusu na kutoka mle chumbani nikaanza kushuka ngazi kuelekea chini.baada ya kumaliza kushuka ngazi ghafla nikakutana na kitu kilichonistua mno na ambacho sikukitegemea kukuiona mahala pale.Nilikuwa natazamana na Emmy.Nilistuka sana nikadhani labda nilikuwa ndotoni lakini hapana ni kweli nilikuwa natazamana na Emmy ambaye ndiye mwanamke aliyefanya maisha yangu yakawa namna hii.Wote tulikuwa tumesimama tukitazamana.Kwa haraka haraka picha ya maisha yangu yote ya mateso na vitimbi toka kwa Emmy ikanijia.Nikajikuta nikipatwa na hasira za ajabu sana.
“ Wayne..” akasema Emmy huku akitabasamu kwa uoga .Nadhani hata yeye aligundua kwamba nilikuwa nimekasirika kupita kiasi
“Emmy unatafuta nini huku? Nikasema kwa ukali
“ wayne samahani sana....nimesikia kuhusu Clara na nikataka kuja kukupa pole kwa klichotokea..”
Kabla hajamaliza sentensi yake nikamrukia na kuanza kumshushia kipigo kikali.Nilimpiga kila mahala.Emmy akapiga kelele kubwa na watu wakaja pale kujua nini kinaendelea.Sikutaka mtu yeyote aniamue .Nilitaka niendelee kumshushia kipigo kikali mwanamke yule baradhuli.
“Nilikutafuta siku nyingi sana na leo nimekupata.Leo nitakufanya kitu kibaya sana Emmy.Nimekuachia kila kitu lakini bado unanifuata” nikasema huku nkiendelea kumshushia kipigo.Mara nikashikwa na mikono yenye nguvu .
“ Stop that Wayne.Huoni kama unaweza ukaua? Alikuwa ni Chris.
“ Chris niache nimmalizie huyu shetani.Amemfuata Clara mpaka hapa ,anataka ammalizie?? Nikasema kwa uchungu huku bado nikiwa nimeshikiliwa.Mwili ulikuwa unanichemka kwa hasira nilizokuwa nazo.Emmy alikuwa amelala chini akilia huku akivuja damu.Shati lake jeupe alilolivaa lililoa damu .wakati nampa kipigo mkoba wake ulifunguka na pembe iliyokuwa ndani ya mkoba ule ikaanguka.Watu wote wakaogopa kumsogelea na kumpa msaada.Lilikuwa ni tukio la kushangaza mno.Watu waliokuja kushuhudia ugomi ule walikuwa wakisemezana wao kwa wao kuhusiana na kile kilichokuwa kimetokea na hasa kuhusiana na ile pembe iliyokuwa imeanguka chini
Chris akanishika na kuniondoa mahala pale akanipeleka sehemu tulivu nikakaa halafu akamrudia Emmy aliyekuwa bado amekaa chini akilia.Emmy alikataa kata kuongea na mtu yeyote na wala hakutaka kwenda kutibiwa au kwenda kutoa taarifa polisi kama alivyokuwa ameshauriwa na baadhi ya akina mama waliokuwepo pale badala yake akainuka na huku akivuja damu akaelekea liliko gari lake akaingia na kuondoka.Pembe lake aliliacha pale pale chini lilipoanguka.Chris akafanya maombi mafupi halafu akalishika pembe lile na kwenda kulitupa mbali.


**********************

Meru view Garden ni moja ya hoteli bora kabisa na ghali jijini Arusha.Hii ni hoteli ambayo inafahamika kwa kufikia watu wenye uwezo mkubwa kifedha.Ni hoteli ambayo iko nje kidogo ya jiji na iliyo na utulivu wa kipekee.Saa mbili na nusu ilimkuta Sheila katika geti la hoteli hii tulivu akajitambulisha mapokezi kwamba alikuwa mgeni wa James .Wahudumnu wakawasiliana na James ambaye aliwaambia wampeleke Sheila katika chumba chake.Alikuwa amependeza sana usiku ule.Walifika hadi katika chumba kimoja kilichokuwa na walinzi wawili mlangoni waliokuwa wamevaa suti nyeusi ambao waliufungua mlango na kumruhusu Sheila aingie ndani
“ Hallo Sheila” akasema James aliyekuwa amejilaza sofani akitazama Luninga latika chumba hiki kikubwa.Sheila alisimama akimkodolea macho James.
“ James ni wewe !! akashangaa Sheila
“ Ni mimi Sheila kwani umenisahau?
“ hapana james siwezi kukusahau hata kidogo.Ninashangaa kwa namna ulivyobadilika.Ama kweli duniani hakuna mtu mwembamba” akasema Sheila huku akitabasamu
James akainuka akakumbatiana na Sheila halafu akamuelekeza aketi sofani.
“ karibu sana Sheila.Nimefurahi kukuona” akasema James
“ nashukuru sana James.Hata mimi nimefurahi sana kukuona .Ni muda mrefu sana umepita hatujaonana .James umebadilika mno.Nini siri ya mafaniko yako.? Au ni hali ya hewa ya huko imekukubali? Akauliza Sheila.James akatabasamu na kusema
“ Sheila kwanza kabisa kuna kitu ambacho unatakiwa ukifahamu.Unaponiita jina langu anza na neno Nabii.Nabii James ndilo jina langu kwa sasa”
“ nabii ?!! Sheila akashangaa
“ ndiyo Sheila.Kwa sasa mimi ni mtumishi wa Mungu ninaitwa Nabii James.Nimeamua kumtumikia Mungu” akasema James huku akiinua glasi yake ya kinywaji na kunywa
“ maisha yana maajabu sana..James umekuwa nabii?
“ ndiyo Sheila.Si jambo la ajabu kuwa nabii.Mungu amenichagua toka kundi lake la kondoo na kunipaka mafuta ili nimtumikie.Kwa hivi sasa makazi yangu ni nchini Canada na Norway.Hapa nyumbani nimekuja mara moja kuna jamo lililonileta kwa dharura” akasema James
“ karibu sana nyumbani nabii James.” Akasema Sheila na kumfanya james atabasamu
“ maisha yanaendaje Sheila,naona unazidi kupendeza .Wakati wengine wanabadilika na kuwa wazee kadiri miaka inavyosonga lakini kwako wewe ni tofauti unazidi kuwa binti mdogo nini siri ya urembo? Akauliza James na kumfanya Sheila acheke kicheko kikubwa
“ Ninajitahdi kujitunza ndiyo maana niko hivi” akajibu Sheila.
“ Maisha yanaendaje hapa Tanzania? Akauliza james
“ Tunamshukuru Mungu tuko wazima na maisha yanaenda vizuri” akasema Sheila
James akainuka pale sofani
“ Sheila naomba tukapate chakula .Nilijua unakuja kwa hiyo sikuwa nimepata chakula nikikusubiri” akasema James halafu wakaingia katika chumba cha pembeni kilichokuwa na meza yenye viti vinne iliyokuwa na aina nyingi za chakula mezani wakakaa na kula kisha wakarejea mahala walipokuwa wamekaa mwanzoni
“ Sheila ninashukuru sana umefika kama nilivyokuomba.Nimekuita hapa kuna jambo ambalo nataka uniambie bila kunificha” akasema James
‘ nabii James usihofu kitu.Uliza jambo lolote lile na siwezi kukuficha wewe ni mtumishi wa bwana” akasema Sheila
“ Sheila kama nilivyokwambia awali kwamba nimetua hapa Arusha kwa dharura lakini sikuwa na mpango wa kuja hivi karibuni na ndiyo maana nimekuja kimya kimya na kufkia hapa hotelini ,sitaki mtu yeyote afahamu juu ya ujio wangu.Kuna jambo lililonileta hapa.Ni kuhusu Emmy.Kwanza sijakuuliza chochote kuhusu maendeleo yake.anaendeleaje?akauliza James
“ Emmy anaendelea vizuri sana” akajibu Sheila huku macho yake yakionyesha wasi wasi kidogo
“ nafurahi kusikia hivyo.Sijataka afahamu kama nimekuja hapa nilitaka nisionane naye kwanza hadi nizungumze nawe kwanza kwa sababu najua wewe ni mtu wake wa karibu sana”
“Mimi na Emmy ni marafiki wakubwa.” Akajibu Sheila
‘ Nafurahi kusikia hivyo na kwa kulifahamu hilo ndiyo maana nimetaka kuonana nawe kwanza kabla hata sijaonana na Emmy.” Akasema James halafu akanyamaza akameza mate na kusema
“ Sheila kwa sasa mimi ni mtu mkubwa sana si hapa afrika bali duniani kwa ujumla .Hapa nyumbani sifahamiki sana lakini katika nchi nyingine za Ulaya na amerika ninafahamika na kuheshimika mno kutokana na kazi zangu za kinabii.Sitaki kuelezea kwa undani sana kuhusiana na mambo haya ya kinabii lakini naomba ufahamu kwamba nimechaguliwa na kupakwa mafuta na bwana ili nimtumikie.Kwa hapa ny7mbani iko siku itafahamika kwa sababu imeandikwa kwamba nabii hakubaliki kwao lakini siku itakuja watanikubali ” akasema James halafu akamtazama Sheila na kuendelea
“Kwa muda mrefu nilikuwa namuomba bwana anisaidie niweze kupata msaidizi yaani mke na siku moja nikiwa katika maombi mazito nikaona maono .Katika maono hayo bwana alinionyesha kwamba mwanamke ambaye atakuwa mke wangu anatoka Tanzania lakini sikuonyeshwa ni yupi na anatokea sehemu gani ya Tanzania.Baada ya kukaa na kutafakari kwa muda nikagundua kwamba mwanamke pekee ambaye nilionyeshwa katika maono yale ni Emmy.Mimi na Emmy tumekuwa wapenzi wa muda mrefu sana nadhani unafahamu urafiki wetu ulikotoka.Japokuwa tulikuwa tunakorofishana mara kwa mara lakini tulisuluhisha matatizo yetu na kusonga mbele.Ninampenda Emmy toka moyoni na ndiye mwanamke ambaye nina imani bwana ameniangazia ili awe mke wangu wa ndoa.Kabla sijaonana naye nimeona nikuite kwanza wewe ambaye ndiye rafiki yake wa karibu ili uweze kunipa maelezo kuhusiana na Emmy kwa sababu ni kipindi kirefu sijaonana naye.Nataka kufahamu anaishi wapi hivi sasa,maisha yake yakoje,yuko katika mahusiano ama la.nataka kufahamu kila kitu kuhusiana na Emmy.Nina imani kwamba hutanificha kitu chochote.” Akasema James halafu akainuka na kuingia chumbani halafu akarejea na bahasha iliyofungwa vyema akampatia Sheila.
“ kamata hii.Its ten thousand dollars to buy the information from you..so tell me the truth about her” akasema James.Sheila bado aliendelea kutetemeka mikono akiwa ameishika bahasha ile.Hakuamini macho yake.Ni katika kipindi kama hiki alikuwa akumiza kichwa angetoa wapi fedha za kumlipa Wayne ,fedha alizokopa ili aweze kumlipa Emmy ambaye alipanga kumdhalilisha na bila kutegemea amepata fedha ambazo alikuwa anazihitaji na zaidi.Alimtazama James kwa jicho la mshangao.
“ Ouh my gosh ! siamini.yaani james amefikia hatua hii? Anaweza akanipatia fedha hizi zote kwa ajili ya kupata taarifa ya Emmy tu ? Inaonekana mambo yake ni mazuri sana..” akawaza Sheila
“ Niambie Sheila .Nina hamu sana ya kutaka kufahamu.Hiki ndicho kitu pekee kilichonifanya nikuite hapa usiku huu” akasema James
“ Eemmy its pay back time” akawaza Sheila halafu akakohoa kidogo na kusema
“ Nabii James kwanza napenda nikushukuru sana kwa mzigo huu mkubwa.Wanasema kwamba Nabii hakubaliki kwao lakini wewe nimekukubali kwa sababu umekuja wakati nikiwa na shida ya fedha na umenipatia kiasi nilichokuwa nakihitaji hata na zaidi.Nimekukubali James wewe ni nabii wa kweli.” Akasema Sheila
“ usihofu Sheila.Pesa si tatizo kwangu hivi sasa.Muda wowoe ukihitaji fedha niko tayari kukupatia hata mara hamsini ya hizo.Haya naomba sasa uniambie ukweli” akasema James
“ Nabii James naomba nikiri kwamba maono yako yanawezekana yalimaanisha mwanamke mwingine na si Emmy”
“ kwa nini unasema hivyo Sheila? Akauliza James huku akijiweka vizuri sofani
“ Nabii James naomba nikiri kwako kwamba Emmy hayuko vile ambayo unamfahamu wewe.Emmy ni mtu mwenye sura zaidi ya moja.”
“ Sikuelewi Sheila unamaanisha nini.Hebu niweke wazi” akasema James na kujifuta jasho lililoanza kumtoka
“nabii james,kwanza kabisa naomba ufahamu kwamba katika siku zote za urafiki wenu hakukuwa na hata chembe ya ukweli ndani ya mahusiano yenu.It was all lies.Hakukuwa na mapenzi yoyote .”
“ Kwa nini unasema hivyo Sheila? I loved Emmy so much.I loved her with all my heart and she loved me too”
“ Ndiyo nabii james najua ulimpenda sana Emmy na hadi sasa bado unampenda sana lakini fahamu kwamba hakukupenda hata kidogo.Alikuwa anakutumia tu.Hana hata chembe ya upendo kwako” akasema Sheila
“ Ouh my gosh haya ambo ni mapya.Hebu nieleze ni kwa nini unasema hivyo Sheila? Akasema James
“James wakati ule mkiwa katika mahusiano,Emmy tayari alikuwa katika mahusiano na wanaume watatu tofauti na wewe ulikuwa wanne.Hakuna aliyemfahamu mwenzake na wote aliweza kuwatumia vile atakavyo.”
“Sheila una hakika na hicho unachoniambia? Akauliza James
“ Ndiyo James nina uhakika kwa sababu mimi ndiye rafiki yake mkubwa na kila kitu chake lazima anishirikishe”
“ Ok go ahead” akasema james
“Kitu ambacho hukuwa unakifahamu ni kwamba Emmy aliwahi kuolewa wakati ukiwa nje ya nchi na uliporudi kwa likizo hukujua chochote.”
“ real ???,…… akauliza James huku uso wake ukianza kubadilika
“ Ndiyo James.Emmy aliolewa na kijana mmoja anaitwa Wayne.”
James akavuta pumzi ndefu,alionekana kuchanganyikiwa
“Kuna mambo mengi sana ambayo nikikuelezea hapa tunaweza kukesha usiku kucha lakini kikubwa ambacho ninataka kukueleza ni kwamba,ulipoondoka kwenda Urusi kimasomo,ulimuacha Emmy akiwa na ujauzito mchanga.”
“ real ???? akasema James kwa mstuko
“ Ndiyo james. Emmy alibaki na ujauzito wako.Mume wake hakujua kama ujauzito ule ni wa kwako na Emmy akamdanganya kwamba mimba ile ilikuwa yake Wayne”
“ what happened then? Akauliza James
“Emmy alijifungua mtoto wa kiume”
“ Ouh thanx God..” akasema James huku akiinua mikono juu na kumshukuru Mungu
“ Sina cha kukupa Ee Mungu wangu.” Akasema James halafu akaanza kuongea maneno Fulani ambayo Sheila hakuyaelewa ilikuwa ni lugha gani.Aliongea akiwa amefumba macho.
“Sheila hizi ni habari nzuri sana ambazo nimezipata leo hii.Umeniletea habari njema ambazo zimenifurahisha mno. Ndiyo maana kila siku nilikuwa nikiota nyumbani kumbe kuna taarifa nzuri namna hii.Ahsante sana Sheila” akasema James halafu akainuka na kutoka pale sebuleni akaingia chumbani na baada ya muda mfupi akarejea akiwa na bahasha mkononi akampatia Sheila
“ kamata hii Sheila.Its ten thousand dollars again.Umenipa habari ambazo zimenifurahisha mno.Sijawahi kufurahi kama nilivyofurahi leo_Ouh Mungu ahsante sana ” akasema James na kurejea katika sofa.Sheila aliona kama yuko ndotoni. Ndani ya muda mfupi tayari ametengeneza zaidi ya shilingi millioni thelathini.
“ So how’s my baby boy.Is he handsome? Akauliza James kwa furaha.Sheila akasita kidogo kujibu.
“ I have to tell the truth” akawaza na kukohoa kidogo kisha akasema
“ yes he was very handsome”
“ He was ?? akauliza James kwa mshangao
“ yes he was….”akajibu.Sura ya James ikajenga wasi wasi
“James naomba niwe muwazi kwako kwa kila jambo.Miezi kadhaa iliyopita Wayne mume wa Emmy aligundua kwamba Baraka hakuwa damu yake.Jambo hili lilizua mtafaruku mkubwa sana uliopelekea ndoa yao kuvunjika na kila mmoja akaendelea na maisha yake peke yake. Baada ya kuachana na Wayne,Emmy alianzisha madai kwamba alikuwa amerogwa na ndiyo maana migogoro kati yake na Wayne haikuisha.Mwishowe aliamua kwenda kwa mganga wa kienyeji ili aweze kumfahamu mbaya wake na pia kumfanya Wayne arudi tena kwake.Mganga alimfanyia dawa na siku iliyofuata alirejea mjini lakini alikutana na taarifa mbaya.Mwanae Baraka alikuwa amefariki dunia ghafla usiku wakati akiwa kwa mganga.Naomba niwe muwazi kwako Nabii James,Emmy alimtoa kafara mwanae kwa mizimu” akasema Sheila.
Taratibu james akasimama na mara akajikuta ameishiwa nguvu na kukaa chini katika zuria.
“ Sheila that’s not true..Thats a lie..mwanangu haweze kufa..Mwanangu bado mzima” akasema James.Alikuwa anaweweseka huku akiongea maneno ambayo Sheila hakuyafahamu.Macho yake yalikuwa yamelowa machozi.
“Mwanangu Baraka..ouh Emmy how could you do that? Akalia James.Alilala pale katika zuria kwa zaidi ya saa moja.Alipoinua kichwa macho yake yalikuwa yamevimba na mekundu kwa kulia
“Sheila ahsante sana kwa taarifa hizi na kuwa mkweli kwangu.Naomba kwa sasa uondoke nataka nibaki mwenyewe.I need to be alone.I want to cry alone.Kesho nakuomba uje saa nne za asubuhi unipeleke mahala alikozikwa mwanangu Baraka nikalione kaburi lake” akasema James huku machozi yakiendelea kumtoka
Sheila akatoka mle chumbani kwa James na mmoja wa walinzi akamrudisha hadi nyumbani kwake kwa kutumia gari la hoteli.Aliumia moyoni baada ya kuikumbuka historia ile hasa walipokwenda na Emmy kwa mganga na akawafanyia jambo baya lakini kwa upande mwingine alifurahi kwa sababu aliweza kumuharibia kabisa Emmy kwa James.
“ James ameumia mno na niliyaona macho yake,sijui atafanya nini akionana na Emmy.Alilia sana hadi nikamuonea huruma.Sikuwa na namna nyingine na kufanya zaidi ya kumueleza ukweli James. Hii ni vita kati ya ngu na Emmy na katika vita ya kubidi utumie kila aina ya silaha uliyonayo kumbomoa adui yako.Nimetumia vyema silaha zangu.Yeye alianza na mimi nimemaliza.Alimwaga ugali na mimi nimemwaga mboga” akasema Sheila akiwa amezimwaga fedha zile alizopewa na James kitandani.Akazishika noti zile nyingi asiamini macho yake.
“ Twent thousand dollars !! akashangaa..
“ James amefikia hatua hii ambayo anaweza akampatia mtu fedha zote hizi bila ya kumfanyia kazi yoyote.Mhh lazima atakuwa na fedha nyingi sana.Lazima atakuwa ni bilionea.” Akawaza Sheila
Hata baada ya Sheila kuondoka bado James aliendelea kukaa katika zuria akilia.Habari za kwamba Emy alimuua mwanae kwa kumtoa kafara ilimsikitisha sana.
“ Nilifurahi mno baada ya kusikia kwamba Emmy alibahatika kuzaa na mimi mtoto lakini furaha yangu yote imeyeyuka baada ya kusikia kwamba mwanangu alikufa kwa kutolewa kafara kwa mizimu.Emmy kwanini ulifanya hivyo? Kwa nini ulimuua mwanangu? Yaani umediriki kumuua mwanangu kwa ajili ya mwanaume? Uongo wote ulionidanganya haukutosha ukaamua hadi kumuua mwanangu ?.Ninaona kama dunia yote imenigeuka na kuniadhibu.Emmy I’ll never forgive you for this.Emmy sintakusamehe hata kidogo.I swear in heaven and earth I’ll never forgive you.” Akasema James kwa hasira huku mwili wake mkubwa ukitetemeka

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
BEYOND PAIN

SEHEMU YA 32

MTUNZI :pATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Twent thousand dollars !! akashangaa..
“ James amefikia hatua hii ambayo anaweza akampatia mtu fedha zote hizi bila ya kumfanyia kazi yoyote.Mhh lazima atakuwa na fedha nyingi sana.Lazima atakuwa ni bilionea.” Akawaza Sheila
Hata baada ya Sheila kuondoka bado James aliendelea kukaa katika zuria akilia.Habari za kwamba Emy alimuua mwanae kwa kumtoa kafara ilimsikitisha sana.
“ Nilifurahi mno baada ya kusikia kwamba Emmy alibahatika kuzaa na mimi mtoto lakini furaha yangu yote imeyeyuka baada ya kusikia kwamba mwanangu alikufa kwa kutolewa kafara kwa mizimu.Emmy kwanini ulifanya hivyo? Kwa nini ulimuua mwanangu? Yaani umediriki kumuua mwanangu kwa ajili ya mwanaume? Uongo wote ulionidanganya haukutosha ukaamua hadi kumuua mwanangu ?.Ninaona kama dunia yote imenigeuka na kuniadhibu.Emmy I’ll never forgive you for this.Emmy sintakusamehe hata kidogo.I swear in heaven and earth I’ll never forgive you.” Akasema James kwa hasira huku mwili wake mkubwa ukitetemeka

ENDELEA……………………



Nilikaa ile sehemu ambayo Chris aliniweka ili nitulie na baada ya hasira nilizokuwa nazo kutulia akanichukua na kunipeleka kwa wazazi wa Clara.Nilisalimiana nao nikavuta kiti na kuketi.Chris akaanzisha mazungumzo
“Wayne kama nilivyokutaarifu awali , hawa ndio wazazi wa Clara” akasema Chris
“ Wazee wangu huyu ndiye Wayne ambaye alikuwa na Clara hadi dakika ambayo alipatwa na matatizo haya” baada ya Chris kufanya utambulisho ule nikasimama na kuwapa tena mikono wazazi wale
“ Ninafurahi kuwafahamu wazee wangu.karibuni sana Arusha na poleni kwa matatizo” nikasema
“ Hata sisi tunafurahi kukuona pia.Pole sana na matatizo Wayne” akasema baba yake Clara
“ Ahsante baba.Tumekwisha poa” nikasema
“ Wayne kama ulivyoelezwa na mwenzako kwamba sisi ndio wazazi wa Clara na tumetaarifiwa leo asubuhi na mtu mmoja aliyeko katika ofisi yake kule afrika kusini kwamba amepatwa na ugonjwa huu wa ghafla.Kama wazazi tulistuka sana na kujiuliza kwa nini hatukutaarifiwa mapema na watu amabo walikuwa karibu naye muda wote hadi tutaarifiwe na watu walioko nje ya nchi?.Tumejiuliza maswali mengi bila majibu na ndiyo maana tumeona hatuwezi kulala leo hii hadi tuonane nawe na utueleze kwa kina kwa nini mlifanya hivi.Je mlisubiri hadi mwanangu aage dunia ndipo mtutaarifu? Akasema mzee Yule ambaye alionekana kukabwa na donge kubwa kooni.Nilijua pale lazima kulikuwa na shughuli nzito ikanilazimu nitumie kauli ya kiungwana zaidi.
Kwanza nilikiri kosa .Ni kweli nilikosea kutokuwataarifu wazazi wa Clara mapema kuhusiana na tatizo lililompata mtoto wao.Niliwaeleza kwamba sababu kuu iliyofanya nishindwe kuwataarifu mapema ni kutokanana kuchanganyikiwa kwa ugonjwa ule wa ghafla ambao sikuutegemea.Niliwapa sababu ambazo walikubaliana nazo na wakanipa ushauri kwamba siku zote linapotokea tatizo la namna hiyo kwa mtu yeyote kuna ulazima wa kuwasiliana na ndugu wa karibu wa mgonjwa na kuwafahamisha mapema.Mzee Yule alitaka kujua mahusiano yaliyopo kati yangu na Clara.Nilimueleza kwa kifupi kwamba mimi na Clara tulikuwa tumekutana jijini Arusha tukajikuta tukipendanana na tukaanzisha mahusiano ya kimapenzi.Sikutaka kumficha kitu
“ Nilishangaa kwa nini Clara aliamua kuahirisha ghafla safari yake ya kurejea afrika kusini .Kumbe tayari alikuwa katika mahusiano.” Akasema baba yake Clara.Kikapita kimya cha muda mama yake akauliza
“Yule mwanamke uliyekuwa unagombana naye ni nani? Nilistuka sana kwa swali lile.Nilisikia aibu kubwa kwa wazazi ale kukishuhudia kitendo kile cha aibu kilichotokea usiku ule
“Ni aliyewahi kuwa mke wangu? Nikasema
“ Ulikuwa umeoa? Wote wakastuka
“ Ndiyo niliwahi kuwa na mke lakini tuliachana “
“ Alikuja kutafuta nini hapa hospitali mida ile na kupelekea mpigane? Akauliza baba mkwe nikajikuta nikikosa jibu la kumpa.Niliogopa kumweleza ukweli wa jambo alilolifanya Emmy
“Wakati mkigombana kuna pembe iliangika toka katika moba wa Yule mwanamke.Ilikuwa ya nini pembe ile? Akauliza mama Clara
“ Pembe ?? nikashangaa.Sikuwa nimeiona pembe wakati nikimshushia kipigo Emmy
“ Ndiyo kulikuwa na pembe na kila mtu aliiona.” Akasema mama Clara.Nikamgeukia Chris
“ Ni kweli Wayne.Katika mkoba wa Emmy kulikuwa na pembe ya mnyama lakini tayari nimekwisha iharibu na haina nguvu tena”
“Ouh my gosh ! nikashika kichwa changu kwa mshangao
“ Wayne inaonyesha wazi kuna mambo yanayoendelea hapa chini kwa chini.Sifahamu lengo lenu kwa mwanangu ni nini hasa.Inaonekana ugonjwa huu wa mwanangu si ugonjwa wa kawaida .Kuna namna imefanyika hapa.Mambo niliyoyashuhudia yamenipa uoga sana “ akasema baba Clara.Nilikuwa nimeinama nikitafakari na sikujua nimjibu nini.baada ya muda baba Clara akasma
“ Wayne na Chris sipendi kuchukua muda wenu mwingi kwani mnatakiwa muende kupumzika.Kwanza kabisa ninawashukuru sana kwa namna mlivyomshughulikia Clara toka alipopatwa na matatizo haya.Mmefanya kazi kubwa sana na hata madaktari wa hapa wamewasifu kwa kufanya kila jitihada ili kumtibu Clara.Nimeambiwa na madaktari kwamba kulikuwa na mpango hata wa kumpekeka nje ya nchi kwa matibabu lakini wakasema kwamba ugonjwa huu unatibika hapa hapa nchini.Ninawashukuru sana kwa kila jitihada mliyoifanya.Pamoja na hayo kuna maamuzi ambayo sisi kama wazazi tumeyachukua.kwanza kabisa kesho asubuhi tunaondoka na Clara.Tunakwenda naye jijini Dar es salaam na kuanza taratibu za kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu ya uhakika .Sisi ni watu wenye uwezo na tunataka mwanetu atibiwe katika hospitali bora zaidi nje ya nchi.Kwa hiyo kesho tutaondoka na Clara.Tayari tumekwisha andaa kila kitu kuhusiana na safari ya kesho.Jambo la pili ambalo najua ni gumu lakini ni lazima tulifanye Wayne tunakuomba uachane kabisa na Clara. Tumegundua kwamba wewe ndiye chanzo cha mtoto wetu kupatwa na matatizo haya yaliyompata.Hatujui mmekutana wapi na ni kwa kiasi gani mnapendana lakini ninachotaka kukuhakikishia ni kwamba sisi kama wazazi hautkukubali uwe na uhusiano wa kimapenzi na mwanetu,kaa mbali kabisa na mwanangu na si kwa wakati huu tu ambao anaumwa bali katika maisha yake yote.Sitaku tena kusikia masuala ya mahusiano kati yako na Clara.Kama unataka kuwa na mahusiano na mwnangu usubiri hadi nitakapokuwa nimefariki lakini kama bado niko hai sintaruhusu kamwe uwe na mahusiano na mwanangu.Naomba usinielewe vibaya Wayne ,wewe ni kijana mzuri mwenye moyo wa upendo ,jasiri ,makini na mwenye nidhamu lakini hufai kuwa na mwanangu.Najua ni jambo ambalo hukulitegemea na ambalo linauma sana lakini kuna nyakati katika maisha ni lazima tufanye maamuzi magumu na sisi kama wazazi tumefanya maamuzi hayo kwa faida yako wewe na mwanetu.” Akasema baba yake Clara.Nilihisi kama mwili wangu unaingiwa na ubaridi na kufa ganzi .Maneno yale aliyoyasema yule mzee yalikuwa mazito sana na ambayo katu sikuyategemea kuyasikia na hasa katika wakati ule ambao nilihitaji sana faraja..
“Mzee naomba usitamke hivyo hasa kwa wakati huu ambao Clara yuko katika matatizo.Ninampenda Clara kwa moyo wangu wote na yeye analifahamu hilo.Clara ni kila kitu kwangu.tafadhali mzee naomba usinifanyie hivi.” Nikasema huku machozi yakinilenga.Niliumia sana.Mama yake Clara alionekana kunionea huruma sana lakini hakuwa na maamuzi
“ Wayne tayari tumekwisha fanya maamuzi na hatuwezi kuyabadili tena.Kesho saa nne asubuhi tutamuondoa Clara na kumsafirisha.Tutakupa nafasi ya kuonana na Clara kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoka kwani baada ya hapo hutamuona tena katika maisha yako.Kama utakuwa tayari kuja kuagana na Clara basi ufike hospitali kabla ya saa nne za asubuhi” akasema baba Clara halafu akainuka.Mke wake alitaka kusema jambo lakini akamzuia.Wakaaga na kukodi taksi wakaondoka.
Nilibaki nimeinama kwa zaidi ya robo saa nikiwaza.Kwa mara nyingine tena nilihisi kuadhibiwa na dunia.Nilisikia maumivu makali sana ndani ya moyo wangu maumivu ambayo hayaelezeki.Ilikuwa ni zaidi ya maumivu.
“ wayne its time to go home” akasema Chris kwa sauti ndogo.Nikainua uso wangu ulikuwa umejaa machozi
“ Chris nimekosa nini kiasi cha kuadhibiwa na dunia kiasi hiki? Kwa nini kila mara iwe mimi tu? Nikasema kwa uchungu
“ Usijali Wayne.Kila jambo hutokea kwa sababu maalum.Jitahidi kuvumilia na kumtegemea bwana Mungu naye atakushindia.Be strong Wayne” akasema Chris
“I’m hurt Chris.kwa nini Yule mzee anifanyie hivi? Why??????????????? Nikasema kwa hasira
“ Calm down Wayne.Huna sababu ya kuumia sana .Kama Clara ndiye mwanamke uliyeandikiwa uwe naye basi siku moja utakuwa naye. Niamini nikwambiayo .Mapenzi yana nguvu kuliko kitu chochote kile.Mapenzi yanau wezo wa kuusambaratisha hata mlima.If you real love Clara one day you’ll be with her.believe me brother” akasema Chris.Maneno yale yalinipa moyo sana.Nikainuka pale kitini tukaelekea garini na kuondoka kurejea nyumbani kwa Chris
“ Mambo yote haya yanatokea its because of Emmy..” nikasema tukiwa njiani kurejea nyumbani
“ Kusema kweli Wayne Yule mwanamke ninashindwa kumuelewa hata mimi ni kitu gani hasa anachokitafuta kwako.Nilistuka sana baada ya kuiona pembe ile ikitoka katika mkoba wake.Kwa nini alikuja nayo pale hospitali? Akasema Chris
“ Emmy amefikia hatua mbaya sana kwa sasa.Sintasahau mateso na maumivu yote aliyonisababishia na ninakwambia Chris siku moja lazima Emmy atalipia uovu wake.Amesababisha mateso kwa watu wengi sana.Ameniumiza kwa mengi lakini kwa hiili la Clara alivuka mipaka na ndiyo maana nilipomuona nilipandwa na hasira nikampa kipigo kikali mno.Kama usingetokea kuja kuniamua nahisi ningeweza hata kuua kwa hasira nilizokuwa nazo.”
“ Pole sana Wayne. Vipi kuhusu kule Mombo mlikoenda na Sheila?
“ Hatukufanikiwa kumpata yule mchawi mkubwa.Na kama tungemkuta basi ingekuwa ama zake ama zangu.Ana bahati sana “ nikasema halafu nikakumbuka jambo Fulani
“ Hey Chris…unamfahamu mtu anayeitwa james?
“ James ? Chris naye akashangaa
“ Ndiyo James”
“ Kuna akina James wengi sana hapa mjini.Unamzungumzia James yupi?
“Nikiwa garini wakati tukirejea toka Mombo , Sheila alipigiwa simu na mtu mmoja anaitwa a James na kumuomba woanane usiku wa leo.kwa mujibu wa Sheila james ndiye baba mzazi wa Baraka.Alikuwa nje ya nchi kimasomo na wakati anaondoka alimuacha Emmy akiwa na mimba yake.”
Chris akavuta pumzi ndefu kwa taarifa ile
“Wayne nakuomba ndugu yangu ,mambo yote yanayohusiana na Emmy achana nayo kwa sasa.Muweke Emmy pembeni kabisa katika maisha yako na tukabiliane na mambo ambayo yako mbele yetu kwa sasa.”
“ Hilo unalosema ni jambo la kweli Chris.Baada ya mambo haya yote kutokea nadhani ni wakati sasa wa kufanya maamuzi sahihi” nikasema na kukaa kimya.bado maneno ya baba Clara yaliendelea kunitesa kila nikiyakumbuka .Niliumia mno na maneno yale ambayo yaliashiria mwisho wangu na mwanamke niliyempenda kuliko wote.

***************

Hatimaye kulipambazuka tena .Hii ni siku ambayo nitakwena kumuaga Clara na sintamuona tena kwani baba yake aliuvunja rasmi uhusiano wetu na aliweka wazi kwamba kama ninataka kuwa na mahusiano na mwanae Clara basi nisubiri hadi hapo atakapofariki.Niliamka kama mgonjwa kwani sikuweza kupata usingizi usiku.Nilikuwa na mawazo mengi sana.Niliwaza kuhusiana na mustakabali mzima wa maisha yangu,nilikotoka ,niliko na ninakokwenda.Nilijiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa na laana.
Saa tatu za asubuhi tuliondoka kuelekea hospitali.Tayari wazazi wa Clara walikwisha fika pale hospitalini na taratibu za kumsafirisha Clara zilikuwa zinaendelea.Tulisalimiana na mama Clara alionekana kunionea huruma sana
“ Usijali mwanangu.Kama wewe na Clara mnapendana basi atakapopona mtakuwa pamoja tena.Usiache kumuombea ili aweze kupona” akasema mama yake Clara baada ya mumewe kuondoka na daktari.
“ Nashukuru sana mama.Naomba nikiri kwako kwamba Clara ndiye mwanamke ninayempenda sana hapa duniani na kuumwa kwake ni pigo kubwa kwangu na katika maisha yangu.Lakini hata hivyo sina budi kuyaheshimu maamuzi ya baba na nitakaa mbali na Clara ingawa bado nitaendelea kumuombea ili aweze kupona.Pamoja na hayo mama ninaomba msaada mdogo sana toka kwako”
“ Msaada gani wayne?
Nikatoa kadi yangu ya mawasiliano na kumpatia
“ Hizo ni namba zangu za simu ninaomba walau mara moja moja uwe unanipigia na kunifahamisha kuhusu maendeleo ya Clara.Utakuwa umenifanyia jambo kubwa sana mama kama ukinifanyia hivyo”
“ Usijali Wayne.Nitakuwa nawasiliana nawe na kukufahamisha kila kitu” akasema mama Clara huku akiiweka kadi ile katika pochi yake.
Kabla Clara hajaondolewa wodini na kupelekwa uwanja wa ndege nilipewa nafasi ya peke yangu ya kuoana naye kwa mara ya mwisho.Clara alikuwa ananitazama lakini hakuweza kusema chochote. Macho yangu yalikuwa yanatoa machozi.Niliiona michirizi ya machozi machoni pake pia.Nikainama na kumkumbatia.Nililia sana kwani ilikuwa ni mara yangu ya mwisho kuonana naye
“ Clara toka ulipokuja katika maisha yangu umeweza kuyafanya yawe ni ya furaha kubwa.Ninaweza kusema kwamba nimeishi maisha yangu yote katika kipindi hiki kifupi nilichokutana nawe.Sijawahi kupata furaha na sintapata furaha tena katika maisha yangu kama niliyoipata nikiwa nawe.Siwezi kuzisahau zile nyakati nzuri za furaha tulizokuwa pamoja.Zitabaki ni kumbu kumbu pekee kwangu.Ninakupenda Clara zaidi ya ninavyoweza kueleza.Japo baba yako hataki tena mimi nawe tuendelee na uhusiano wetu lakini sintaacha kukupenda Clara.Nitakupenda katika siku zote za maisha yangu na sintakuwa na mwanamke mwingine katika maisha yangu zaidi yako.Ninakuombea upone haraka Clara” nikasema halafu nikambusu. Sina hakika kama kilio kile alikisikia lakini macho yake yalikuwa yamejaa machozi.Nikatoa kitambaa na kumfuta Mlango ukafunguliwa wakaingia madaktari na kuniomba niwapishe.Nikatoka mle chumbani huku nikifuta machozi.Kilikuwa ni kipindi kigumu mno kwangu.Sikuwahi kuumia kama nilivyoumia sasa.Chris alikuwa karibu yangu na akanipa moyo.Baada ya muda mfupi Clara akatolewa akisukumwa katika kitanda na kupakiwa katika gari la wagonjwa.Iliniuma sana.Mtu ambaye siku chache zilizopita alikuwa akitembea kwa mwendo wa madaha lakini leo hii hawezi kufanya lolote,na yote haya ni kwa sababu ya Emmy.Nilimlaani emmy kwa kila laana niliyoifahamu katika hii dunia.
Clara alipakiwa katika gari la wagonjwa na safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ikaanza.Mimi na Chris tulipanda katika gari la Chris ,na rafiki yangu mwingine mkubwa Beka alikuwa pamoja nasi.Sikuongea chochote njiani nilikuwa na mawazo mengi sana naman maisha yangu yalivyokuwa ya matatizo.Nilimuwaza Emmy na mambo yote aliyonitendea,sikuona adhabu gani nimpatie kwa maumivu aliyonisababishia.Nikaamua kumuachia Mungu mambo yote yeye ndiye atakayenilipia.
Tulifika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro,.Pale nikapewa tena nafasi nyingine ya mwisho ya kuonana na Clara.Niliinama na kumbusu mdomoni.
“ Nakupenda Clara na siku zote nitaendelea kukupenda.When u get better I’ll be here waiting for you” nikamwambia Clara.
“ Wayne nakushukuru sana kwa msaada wako mkubwa kwa mwanangu na nitazidi kukuombea afya njema kila siku.Mungu akujalie afya na mwanamke mwingne utakayempenda kama ulivyompenda Clara.” Akasema baba yake Clara halafu tukashikana mikono tukaagana.Sikuweza kumtamkia chochote kwa sababu nilihisi fundo kubwa kunikaba kooni.
“ Wayne usikate tamaa kijana wangu.Siku zote mtegemee Mungu naye atakusaida katika kila jambo.Endelea kumuombea mwenzako na Mungu akipenda siku moja mtaonana tena.Nitakuwa nakupigia simu mara kwa mara kila ninapopata nafasi na kukupa taarifa za maendeleo ya Clara.Ubaki salama Wayne” akasema mama yake Clara ambaye macho yake yalionyesha kulengwa na machozi.
“Wayne,.let’s go back home” akasema Chris .Sikutaka kuendelea kukaa pale uwanjani tukaingia garini na kurejea nyumbani kwa Chris.Nilikuwa kama mtu niliyechanganyikiwa akili.Sikujua nifanye nini kwa wakati huo.
“Chris kwa nini maisha yangu yamekuwa namna hii? Kwa nini yamekosa furaha ? Nimekosea nini Mungu kiasi cha kuniadhibu kiasi hiki? Nikamuuliza Chris tukiwa tumekaa sebuleni nyumbani kwake baada ya kutoka uwanja wa ndege kumsindikiza Clara
“ wayne sisi sote katika hii dunia ni wakosefu na sote tunamkosea Mungu kila siku lakini pamoja na makosa yote tunayomkosea bado Mungu amezidi kutupenda na muda wote yuko tayari kutupokea pale tunapotambua makosa yetu na kutubu..Mungu hutupokea akatukumbatia na kututakasa kutufanya wapya na kutuweka katika kundi la kondoo zake safi .Bwana Mungu hajatuacha katika vilio vyetu ,katika mahangaiko yetu lakini anataka tumlilie ,tumkimbile yeye pekee katika mahangaiko yetu.Wayne ni wakati muafaka sasa wa kufanya maamuzi katika maisha yako na kuitafuta amani ya moyo”
“ Chris sina hakika kama nitaipata hiyo unayoiita amani ya moyo.Nimeumizwa sana na moyo wangu umejaa hasira na visasi kwa Emmy.Moyo wangu utakuaje na amani wakati kila ninapotafuta furaha ya maisha yangu anatokea mtu mmoja na kuiharibu?.Siwezi kuwa na amani Chris…” nikasema
“ Wayne amani ya moyo inapatikana pale tu unapomrudia muumba wako.Mkubali Yesu sasa kama bwana na mwokozi wa maisha yako ,mtegemeze yeye katika kila jambo na nina hakika maisha yako yatakuwa na furaha.Achana na anasa na starehe za dunia hii bali yatafute maisha ya mbinguni.Nakuhakikishia ndugu yangu utakapompokea Yesu na kumfanya kuwa ni bwana na mwokozi wa maisha yako utakuwa na amani.Hautasumbuliwa kamwe na historia ya maisha ya nyuma.Mungu atakubariki ,atakupa amani,atakupa mke mwema,atakupa familia,atakupa kila unachokihitaji.Tazama mimi ,nina amani ya moyo.Nimejifunza kusamehe,nimejifunza kumtolea Mungu mateso na maumivu yangu yote.Nina hakika hata wewe ukiwa ndani ya kristu utajifunza kusamehe,utawasamehe wale wote waliokutenda vibaya” akasema Chris.Nikamuangalia na kusema
“ chris ungekuwa mahala pangu,ungeweza kumsamehe Emmy kwa mambo aliyonitendea?
“ katika Zaburi 86:5 maandiko yanasema "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao".Siku zote Mungu yuko tayari kumsamehe mtu yeyote anayetubu dhambi zake .Kama Mungu yuko tayari kumsamehe mtu yeyote anatufundisha kwamba hata sisi tuwe tayari kusamehe wenzetu hata katika zile dhambi kubwa walizotutenda.Kama Emmy angetambua kosa lake na kuomba msamaha ningemsamehe.” Akasema Chris
“ wayne nakushauri kama ndugu yangu,msamehe Emmy na uyaanze maisha yako mapya.yaliyopita yatabaki historia na utayafurahia mabadiliko.Utajifunza biblia,utamfahamu Mungu na utampenda.Ni wakati wa kufanya mabadiliko sasa”
“Chris maneno yako yana ukweli ndani yake.Ni kweli ninahitaji amani ya moyo,ninahitaji kuyaanza upya maisha yangu.Ninahitaji kuisahau historia yangu ya huko nyuma.Niko tayari kwa hilo na niko tayari hata kuokoka na kuishi maisha mapya lakini kabla ya kufanya hivyo kuna jambo ambalo ninataka kulifanya”
“ jambo gani Wayne?
“ Ninataka kwenda mapumzikoni mbali na hapa.Nataka nikatulize akili yangu kwanza kabla ya kufanya maamuzi yoyote kuhusiana na maisha yangu yajayo.Nimefikiria kwenda Zanzibar.Nimewahi kwenda Zanzibar na Clara ni sehemu nzuri na nina hakika itanisaidia sana kuifanya akili yangu irudi katika hali ya kawaida.”
“Hilo ni wazo zuri Wayne.Ni na hakika endapo utachukua mapumziko hayo yatakusaida sana katika kuifanya akili yako itulie na kuweza kufanya maamuzi yenye kufaa.Nakubaliana nawe moja kwa moja kuhusu suala hilo”
“ Ahsante sana Chris kwa kulitambua suala hili.Nitakaporejea tutaongea kwa undani zaidi kuhusu masuala uliyoniambia lakini kwa sasa sina jibu la moja kwa moja kuhusiana na masuala hayo.Kufanya maamuzi makubwa kama hayo kunahitaji utulivu mkubwa wa akili.”
“ Hayo unayoyasema Wayne ni ya kweli kabisa lakini nitazidi kukuombea ili maisha yako yabadilike na bwana atakwenda kufungua milango ya moyo wako na utakuwa mpya tena”
Chris aliendelea kunipa moyo na maneno ya faraja japokuwa bado kichwa changu kilikuwa kizito kwa mawazo

***********************

Saa nne na nusu za asubuhi Sheila na James wakawasili makaburini kama James alivyokuwa ameomba.Alitaka kuliona kaburi la mtoto wake Baraka.Wote walikuwa katika mavazi meusi.Sheila aliwaongozaJames na walinzi wake wawili hadi katika kaburi la Baraka.
“ Hapa ndipo alipozikwa Baraka” akasema Sheila
James akalitazama kaburi lile .Machozi mengi yakamtoka.Akavua miwani na kujifuta machozi.
“ Baraka mwanangu ninasikitika sikupata hata nafasi ya kukuona na kukaa nawe japo kidogo.Umeondoka katika wakati ambao ninakuhitaji sana.Nitakuenzi katika siku zote za maisha yangu.” Akasema James kwa sauti ndogo halafu akachukua shada la maua toka kwa mmoja wa walinzi wake akaliweka juu ya kaburi la mwanae.Akalibariki kaburi lile wakaondoka.
“ Sheila ninakushukuru sana kwa taarifa zote.Ninakushukuru kwa kunieleza ukweli kuhusu mwanamke ambaye nilidhani nimeelekezwa kwake kumbe nilikuwa nimepotea.Emmy ni mwanamke mbaya sana.Jana usiku nilifanya maombi na nikaonyeshwa ubaya wake.Emmy ni mwanamke katili sana.Katika maombi niliuona ukatili aliomfanyia mwanangu Baraka.Ninaomba usimweleze Emmy kitu chochote kuhusiana na wewe kuonana nami.Nitamuita na kuongea naye baadae.Ninataka nimsalimie tu na siku ya kesho nitaondoka.Sina hamu ya kuendelea kukaa tena hapa Tamnzania kwa sababu kitu kilichonileta tayari nimekwisha kikosa.” Akasema James wakiwa garini .Halafu akaingiza mkono mfukoni na kutoa kitita cha noti
“ Sheila hii ni ahsante yangu kwa yote uliyoniambia.Nisingeweza kufahamu chochote bila ya wewe.Nadhani pesa hizi kidogo zitakusaidia kutatua matatizo yako yote madogo madogo.Ninachoweza kuusia Sheila jitahidi usiwe kama Emmy.Jitahidi uishi maisha ya amani na upendo daima” akasema James halafu akamwambia dereva wake asimamishe gari.
“ Sheila nadhani itakuwa vyema kama ukishuka hapa na ukachukua taksi .Mimi ninaeleka moja kwa moja hotelini kwani sitaki mtu yeyote afahamu kuhusu uwepo wangu hapa Arusha.” Akasema James kisha akaagana na Sheila akashuka akakodi taksi na kurejea kwake

************************

Emmy akiwa nyumbani kwake akiuguza majeraha aliyoyapata kutokana na kipigo alichopewa na Wayne jana usiku mara simu yake ikaita.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika simu yake.
“ Hallo “ akaita Emmy baada ya kupokea simu
“ Hallow naongea na nani? Ikasema sauti ya upande wa pili
“mimi naitwa Emmy.wewe nani mwenzangu?
“ Mimi naitwa James,..habari yako emmy” Emmy akastuka
“ james ?!!
“ Ndiyo James.Umenisahau Emmy?
“ Sijakusahau James.Habari yako?
“ habari yangu nzuri sana James.habari za siku nyingi? Mbona unatumia namba za Tanzania? Uko wapi? Akauliza Emmy kwa wasi wasi
“ Niko Tanzania”
“ Tanzania? Umekuja lini? Mbona unakuja kimya kimya? Akauliza Emmy
“ hapa ni nyumbani Emmy kwa hiyo sina haja ya kutoa taarifa kwamba ninarudi.” Akasema james
“ nafurahi kusikia umerudi James.”
“ Emmy uko wapi mida hii?
“ Niko nyumbani kwangu,wewe uko wapi?
“ Nimefikia hotelini.Ninakuomba ujiandae leo jioni nina hitaji kuonana nawe.Ni siku nyingi sijakuona mpenzi wangu nina hamu sana na wewe.Nahitaji kuupitisha usiku wa leo nikiwa nawe malkia wangu” Akasema James.uso wa Emmy ukachanua kwa tabasamu
“ usijali darling nitakuja.Hata mimi nina hamu mno na wewe.Umefikia hoteli gani? Nina hamu kubwa ya kukuona mpenzi wang ni siku nyingi sana hatujaonana.”
James akamuelekeza hoteli aliyofikia na kukata simu
“ Ouh jamani ! James amerudi. Kwa nini amefikia hotelini? Hoteli aliyofikia ni hoteli ya gharama kubwa sana hapa Arusha na ninafikiri atakuwa ana pesa za kutosha.Ngoja nijiandae nikamuone.Hata kama nina vidonda usoni nitamuona hivyo hivyo.James ananipenda na chochote nitakachomwambia lazima atanisikiliza.Nina hakika hana taarifa zozote kuhusiana na Baraka kwani yeye ndiye baba yake mzazi.” Akawaza emmy huku akiinukana kwenda kujitazama majeraha yake katika kioo
‘ siyo majeraha makubwa sana.Akiniuliza nitamwambia kwamba nilipata ajali ndogo ya gari ndiyo maana nikachubuka namna hii.Yule mshenzi alitaka kuniua jana.kama si Chris kutokea angenifanyia kitu kibaya sana.Sitaki tena madawa ya yule mganga kwani jana hazikuweza kunisaidia.Aibu niliyoipata jana ni kubwa sana kwani lile pembe la ng’ombe alilonipa nitembee nalo mkobani wakati wa kwenda kumuona Wayne lilianguka na watu wote wakaliona.Nadhani hata wayne aliliona pia.Ilikuwa ni aibu kubwa mno.Kwa nini yule mganga asababishe niaibike kiasi kile? Kila aliyekuwepo pale anatambua kwamba mimi ni mshirikina.Ninaogopa hata kutembea mtaani kwa aibu niliyoipata.Kwa sasa nitalazimika kutafuta namna nyingine ya kumpata Wayne lakini si kwa kutumia waganga wa kienyeji.Nimegundua kwamba waganga hawa ni walaghai na hawana msaada wowote.Kama dawa zao zingekuwa za kweli basi jana nisingeaibishwa na Wayne kiasi kile..Mganga yule alinihakikishia kwamba mara tu Wayne atakaponiona atastuka na kujenga tabasamu usoni mwake na atataka nirudiane naye lakini haikuwa hivyo.” Akawaza Emmy na mara picha ya tukio la jana ikamjia kichwani
“ Gosh ! niliiona sura yake alikuwa amekasirika sana.Sijawahi kumuona Wayne akiwa katika hali ile. Ninafikiria kuacha kumfuatilia na kumuacha aendelee na maisha yake lakini siwezi kuishi bila ya yeye.Lazima nipambane nimrudishe wayne kwangu.” Akawaza Emmy

TUKUTANE SEHEMU IJAYO............
 
BEYOND PAIN

SEHEMU YA 33

MTUNZI :pATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kwa nini yule mganga asababishe niaibike kiasi kile? Kila aliyekuwepo pale anatambua kwamba mimi ni mshirikina.Ninaogopa hata kutembea mtaani kwa aibu niliyoipata.Kwa sasa nitalazimika kutafuta namna nyingine ya kumpata Wayne lakini si kwa kutumia waganga wa kienyeji.Nimegundua kwamba waganga hawa ni walaghai na hawana msaada wowote.Kama dawa zao zingekuwa za kweli basi jana nisingeaibishwa na Wayne kiasi kile..Mganga yule alinihakikishia kwamba mara tu Wayne atakaponiona atastuka na kujenga tabasamu usoni mwake na atataka nirudiane naye lakini haikuwa hivyo.” Akawaza Emmy na mara picha ya tukio la jana ikamjia kichwani
“ Gosh ! niliiona sura yake alikuwa amekasirika sana.Sijawahi kumuona Wayne akiwa katika hali ile. Ninafikiria kuacha kumfuatilia na kumuacha aendelee na maisha yake lakini siwezi kuishi bila ya yeye.Lazima nipambane nimrudishe wayne kwangu.” Akawaza Emmy

ENDELEA…………………….

Saa moja za jioni ilimkuta Emmy tayari amekwisha ifka katika hoteli hii kubwa ya kitalii.Alikuwa amependeza vilivyo.Alitaka kuonekana mrembo mbele ya james mtu ambaye alikuwa ni mpenzi wake wa siku nyingi .Taarifa zake tayari zilikuwapo mapokezi,akapokelewa na kupelekwa hadi katika chumba cha james.Nje ya chumba kile kulikuwa na walinzi wawili waliokuwa wanalinda.Emmy akakaribishwa kwa heshima kubwa sana.Mlango wa chumba cha james ukafunguliwa akaingia ndani.Alishangazwa na uzuri wa chumba kile.Ameingia hoteli nyingi sana na hakuwahi kuoa hoteli iliyokuwa nzuri kama hii
“ james !!! akasema Emmy kwa mshangao
“ Emmy “ akasema James
Emmy akamkimbilia na kumkumbatia
“ Ouh my love….” Akasema Emmy
“ nashukuru umerudi mpenzi wangu.Nilikuwa nakuota usiku na mchana lini utarudi.Nashukuru Mungu umerudi salama” akasema Emmy akiwa bado amemkubamtia james
“ I’m back now my love..” akasema James na kumbusu Emmy mdomoni na ndipo alipoona vidonda usoni
“What happened?Mbona una vidonda usoni? Akauliza James
“Nilipatwa na ajali ndogo ya gari nashukuru Mungu sikuumia sana.Nilipatwa na mikwaruzo kidogo.”
“ Pole sana mpenzi wangu” akasema James na kumbusu tena mdomoni kisha akamshika mkono na kumuongoza hadi sofani.
“ Nimefurahi nimekuona tena Emmy.Bado unawaka kama zamani.Ninakupenda sana malaika wangu” maneno yale yakaufanya uso wa Emmy uchanue kwa tabasamu .
“ Hata mimi nimefurahi mno kukuona tena mpenzi wangu.James umebadilika sana.Ilibaki kidogo nikupotee kama ni wewe kweli.Umenenepa sana James” akasema Emmy
“ Emmy kabla hatujaendelea mbele na maongezi yetu kuna kitu ambacho unatakiwa ukifahamu.Kwa sasa ninafahamika kama Nabii James.Unaponiita jina langu unatakiwa kuanza na neno nabii”
“ nabii James? Emmy akashangaa
“ Ndiyo Emmy.Kwa hivi sasa mimi ni mpakwa mafuta wa bwana.Ninamtumikia bwana.Mbona umestuka sana kusikia mimi ni Nabii?akauliza James
“ Nimestuka kwa sababu siktegemea hata siku moja kama ungeweza ukafanya kazi kama hiyo.Ninafahamu ulisomea utaalamu mwingine kabisa na si uchungaji.”
“ Ndiyo emmy.Nilisomea mambo mengine kabisa lakini bwana alikuwa na kusudi na mimi na aliinita ili anitumie katika kazi zake na mimi nimeitika na kwa sasa ninamtumikia yeye pekee” akasema James
“ Nimefurahi sana kwa mabadiliko haya makubwa uliyoyafanya james.”
‘ Ahsante sana Emmy.Ninaweza kusema kwamba bwana amenibariki na hivi sasa maisha yangu ni mazuri mno.Nina fedha za kutosha na nina uwezo wa kufanya lolote hapa duniani.Mambo yote haya ni kwa ajili yetu sisi wawili.Mimi na wewe” akasemaJames na Emmy akainuka pale alipokuwa amekaa na kwenda kumkumbatia huku akimwagia mabusu kemkem.
“Kwa sasa ninaishi Ulaya.Nina majumba katika nchi nyingi za ulaya na ninafanya kazi zangu za kinabii huko na kama mambo yatakwenda vizuri basi hata wewe utahamia Ulaya na tutaishi huko kwa amani kwa raha mustarehe” akasema James na kuzidi kumchanganya emmy
Waliongea mambo mengi na baadae wakaenda kupata chakula cha usiku halafu wakaelekea chumbani.Emmy alianza mautundu yake ili kumuhamasisha James kingono lakini kila alipojaribu hakukuwa na muitikio wowote toka kwa James .Emmy akashangazwa na hali ile
“ james what happened? Nina hamu na wewe sana.Ni miaka mingi sijakuona.Nina hamu na penzi lako” akalalama Emmy kwa sauti nyembamba huku akiwa tayari mtupu kabisa.
James akamvuta kwake na kumbusu kisha akasema
“ Emmy kabla ya kufanya mambo haya tuna mambo mengi ambayo nataka tuyaongee.Mimi na wewe ni wapenzi wa muda mrefu sana toka tukiwa shuleni.Ninakupenda na katika maisha yangu sijawahihata mara moja kukusaliti kwa kutembea na mwanamke mwingine yeyote..Kokote niendako nimekuwa nikijua kwamba nina mpenzi wangu ambaye ananisubiri.Sikuwa na safari ya kuja Tanzania hivi karibuni lakini nilionyeshwa katika maono kwamba nije Tanzania kuna mwanamke wa maisha yangu ambaye ni wewe Emmy.Kwa hiyo usiwe na haraka na mambo haya.Nimekuja hapa kwa sababu yako” akasema James. Halafu akambusu Emmy na kuendelea
“Emmy nina malengo makubwa na wewe.Ninataka tukaishi sote Ulaya .Nataka nikufanye malkia wa himaya yangu lakini kabla ya kufanya hivyo nataka kusikia toka kwako je unanipenda kwa moyo wako wote kama ninavyokupenda mimi?
Emmy akamuangalia James na kusema
‘ My love hilo sio swali la kuniuliza wakati unafahamu fika upendo wangu kwako hauna kipimo.Ninakupenda kuliko kitu chochote.Sijawahi kumpenda mwanaume kama ninavyokupenda James.Hata ulipopotea nimekaa mwenyewe siku zote hizi nikijua kwamba siku moja lazima utarudi tu ili tuje tuendeleze mapenzi yetu. James nakupenda sana,zaidi ya unavyofikiri” akasema Emmy
“ nafurahi kusikia hivyo Emmy.Nakumbuka wakati ninaondoka nilikuhakikishia kwamba nitarudi siku moja kwa ajili yako.Ni muda mrefu umepita toka wakati huo na leo nimetimiza ahadi yangu.I’m back for you.Naomba unihakikishie Emmy kwamba kwa muda huu wote haujawahi kuwa na mahusiano na mwanaume yeyote yule.Kama umewahi kuwa katika mahusiano naomba unieleze na nitakuelewa kwani sisi ni wanadamu na wakati mwingine huwa tunashindwa kuvumilia na kuanguka.”
“ James my love,sijawahi kuwa na mpenzi chini ya jua zaidi yako wewe.Ni wewe pekee ambaye ninakufamu kama mpenzi wangu na ndiyo maana siku hizi zote nimekuwa nikijitunza ili nisijiinginze katika mahusiano nikijua kwamba siku moja utarejea tu” akasema Emmy .James akatabasamu na kumbhusu.
“ nashukuru kwa kunitunzia penzi langu Emmy.Ninakupenda sana.”
“hata mimni nakupenda sana James.Ninashukuru Mungu umerudi .Nilikuwa mpweke sana” akasema Emmy huku akimkumbata zaidi James.Kimya kifupi kikapita halafu James akasema
“ Emmy wewe ni mpenzi wangu na ninaomba nikueleze ukweli kuhusu maisha yangu.Ninakueleza ukweli kwa sababau ninakupenda na kukuamini na ninakuomba nitakayokueleza hapa usimwambie mtu yeyote”
“ Niamini mpenzi wangu.Siwezi kumweleza mtu yeyote yule “ akasema Emmy
James akafikiri kidogo na kusema
“ Emmy kwa sasa sina tena nguvu za kiume na siwezi kufanya mapenzi tena”
Emmy aliyekuwa amemkumbatia james akastuka na kuinuka akamuangalia James kwa macho makali ya mshangao
“ Sijakuelewa James unamaanisha nini unaposema kwamba huna tena nguvu za kiume?
“ Sikiliza Emmy.Najua unataka tufanye mapenzi sasa hivi lakini naomba niwe wazi kwako kwamba kwa sasa siwezi kufanya hivyo.Siwezi kufanya mapenzi.Sina uwezo huo.Sina tena nguvu.Jogoo wangu hawiki tena”
“How did that happen James? Ulikuwa kidume wa shoka.Imekuaje tena? Nini kimetokea? Tafadhali naomba uniambie” akasema Emmy.James akamtazama kwa tabasamu na kusema
“ Nitakwambia Emmy kwa sababu ninakuamini.”
“Tafadhali niambie James.Uliumwa? Nini kimepelekea upoteze nguvu zako?
“ Ni hadithi ndefu sana lakini kwa ufupi ni kwamba nilikubali kutolewa nguvu zangu za kiume na wala sikuumwa wala kuwa na matatizo yoyote” akasema James Emmy akazidi kuchanganyikiwa
“ James unazidi kunichanganya.Nani alikumaliza hizo nguvu?
“ Emmy naomba ufahamu kwamba mimi si nabii wa kweli.Ninatumia nguvu za giza katika unabii wangu na ndiyo maana nimekuwa ni nabii ninayesifika kwa kuwa na nguvu za ajabu sana”
Kauli ile ya James ikamtetemesha Emmy.Jasho likaanza kumchuruzika usoni
“ Ouh my gosh ! James”
“ Mbona unashangaa Emmy.Hili si jambo la ajabu hata kidogo.Watu wengi siku hizi wanajifanya manabii wengine wanajiita mitume lakini wengi wao si wakweli na wanatumia nguvu za giza katika kutenda miujiza na kuwalaghai watu”
“ J…ja..j.James.. imetokeaje hadi ukaingia katika mambo hayo? Akauliza Emmy huku sauti yake ikitetemeka
“Nilishawishiwa kuingia huko na rafiki yangu mmoja anayetoka nchini Nigeria na yeye pia ni nabii kama mimi.Nilipokubali nilipelekwa nchini Nigeria na huko nilipewa machaguo matatu ya kuchagua ili niweze kupata nguvu na uwezo wa kutenda miujiza.Kwangu mimi chaguo rahisi lilikuwa ni kuondoa nguvu zangu za kiume yaani kuharibu uwezo wangu wa kufanya tendo la ndoa na hivyo siwezi kabisa kupata mtoto wala mke.Baada ya hapo nimekuwa ni mtu mwenye nguvu kubwa ya kutenda miujiza mikubwa ,kutabiri mambo yakawa kweli na nimekuwa ni tajiri mkubwa.Nina pesa lukuki na sioni furaha ya maisha bila ya kuwa na mke na mtoto.Emmy kuna kitu ninataka nikuulize”
“ Uliza James” akasema Emmy kwa wasi wasi.
“ Siku moja nikiwa katika maombi niliona maono kwamba mimi na wewe tulibahatika kupata mtoto.Naomba unihakikishie je maono haya ni ya kweli:? Mimi na wewe tuliwahi kuwa na mtoto? Ninahitaji sana mtoto kwa sasa ambaye atakuwa mrithi wa mali zangu nyingi nilizonazo”
Emmy alistuka sana kwa kusikia maneno yale toka kwa James.Alihisi baridi kali mwilini mwake.Alikosa neno la kusema
“ emmy naomba unijibu.Ni kweli kuhusu jambo hii? Akauliza james baada ya kuona Emmy amekaa kimya
“ James jambo hili halina ukweli wowote.Mimi na wewe hatujawahi kuwa na mtoto kamwe.Nilitegemea ukirudi tutafute walau mtoto mmoja lakini kwa sasa haiwezekani tena” Akasema Emmy
“ Nafurahi kusikia uthibitisho huo toka kwako.Inawezekana maono yangu hayakuwa ya kweli.Hata hivyo kwa kuwa tayari umeijua siri yangu kuna kitu ambacho ni lazima unywe.” Akasema James huku akiinuka.Emmy alikuwa anatetemeka kwa woga.Baada ya dakika mbili james akarejea akiwa na chupa mkononi akampatia Emmy
“ Kunywa hii” akasema James.
“ Emmy akaishika chupa ile yenye rangi ya kahawia akaifungua kifuniko na huku mkono wake ukitetemeka akaiweka mdomoni.Kilikuwa ni kinywaji kitamu na chenye harufu nzuri.Wakati akinywa James akamuwekea mkono kichwani na kuanza kuongea maneno ambayo Emmy hakuyafahamu.Ghafla kinywaji kile alichokuwa anakunywa Emmy kikageuka damu.Emmy akataka kutema James akamuangalia kwa jicho kali akalazimika kunywa damu ile na kuimaliza.Ghafla akaanza kuona mwili wake unabadilika na kuwa wa moto sana.
“ James nimeanza kujisikia vibaya sana.Mwili umekuwa wa moto.Umenipa nini hiki? Akasema emmy kwa wasi wasi.James akachukua mafuta toka katika kichupa kidogo akampaka mikononi na lile joto alilokuwa analisikia Emmy likatoweka.
“ Emmy naomba unisikilize vizuri.Tayari ninafahamu kila kitu kuhusu wewe.Ninafahamu uongo wako wote uliokuwa unanidanganya.Ulinidanganya kwamba hauna mwanaume kumbe tayari ulikwisha olewa,kibaya zaidi ulinidanganya kwamba hatukuwahi kuwa na mtoto kumbe wakati ninaondoka nilikuacha ukiwa na mimba changa na ukazaa mtoto wa kiume anaitwa Baraka.Bwana aliyekuoa aligundua kwamba Baraka hakuwa mwanae ukatokea mtafaruku mkaachana,ukaenda kwa mganga na kumtoa kafara mtoto wangu wa pekee kabisa.Emmy nimeumia sana kwa mambo uliyonifanyia.Huu ni ukatili mkubwa sana ambao hauvumiliki.Ulidhani kwamba sintafahamu unyama ulioufanya kwa mtoto wangu wa pekee? Ingekuwa ni kwa kunidanganya mimi nisingekuwa na matatizo lakini kwa kumuua mtoto wangu kwa sababu zako binafsi imeniumiza mno.”
Emmy alistuka sana na mwili wake ukawa unatetemeka kwa woga
“ James..” akasema Emmy lakini James akamzuia.
“ Emmy sitaki uongee chochote,umenisikitisha sana na hapa nilipo moyo wangu unawaka kwa hasira .Naomba nikufahamishe kwamba leo hii ni siku yako ya kulipia uovu wako.” Akasema James huku uso wake ukianza kubadilika.Mwili wake ulionekana kama vile unaanza kujaa.
“ Ouh Mungu wangu niokoe na balaa hili” akasema Emmy baada ya kuona namna James alivyoanza kubadilika na kuwa na umbo la ajabu.Mwili ulikuwa unamtetemeka kwa uoga .
“ Emmy sitaki kupoteza wakati.Ni wakati wako wa kulipa sasa uovu wote ulioufanya na hasa kitendo cha kumtoa mwanangu kafara kwa sababu ya mwanaume..Nitakupa adhabu ambayo itakuwa funzo kwa wengine pia.Baraka alikuwa ni mwanangu wa pekee kabisa na kwa sasa ambapo sina tena uwezo wa kupata mtoto Baraka angekuwa ndiye mrithi wa utajiri wangu wote.Mali zote nilizonazo,utajiri wote nilionao hauna maana bila ya kuwa na mtoto au mke.Hakuna mwanamke ambaye anaweza kukubali kuishi na mwanaume ambaye hawezi kumtimizia haja zake za mwili.Kwa maana hiyo maisha yangu hapa duniani hayana thamani tena na yote hii ni kwa sababu yako Emmy kwa sababu ya tamaa zako.” Akasema James huku mwili wake ukitetemeka kwa hasira
“James naomba unisamehe..nimekosa sana na ninaomba msamaha wako..ninakupenda James na niko tayari kuishi nawe hata kama hauna nguvu za kiume.Nitavumilia yote lakini naomba usinipe adhabu yoyote James.Ni kweli nilimtoa kafara Baraka kwa mizimu nikitegemea kwamba Wayne atarudi kwangu lakini haikuwa hivyo.James niko chini ya miguu yako na niko tayari kufanya chochote unachokitaka” akalia Emmy
“ machozi yako ya kinafiki hayawezi kunifanya nikageuza mawazo yangu.Lazima leo nikupe adabu kali sana.” Akasema James halafu aka chukua kichupa kidogo cha mafuta akamrushia Emmy matone na mara tu matone yale yalipomgusa Emmy mwili ukaanza kumuwasha sana.Akaanza kujikuna.Kadiri alivyokuwa anakuna ndivyo mwili ulivyozidi kumuwasha .Ghafla vikaanza kujitokeza vitu kama unga unga kila alipojikuna na taratibu ngozi ya mikono ikaanza kuwa ngumu.Mwili ukaendelea kumuwasha sana na joto likaongezeka.Wakati akijikuna James alikuwa amenyoosha mkono akiongea maneno ambayo Emmy hakuyafahamu.Emmy akaanza kuhisi joto kali mno kana kwamba alikuwa karibu na moto mkali.
“James ..james..james..!!!! ninaungua..james ninaunguaaaa..!!! akapiga kelele Emmy baada ya kuanza kuhisi alikuwa anaungua.James hakumjali akaendelea kuongea yale maneno yake aliyoyafahamu mwenyewe akiwa amefumba macho na mkono wake wa kulia akiwa ameuelekeza kwa Emmy.Ghafla Emmy akaanza kuona kizungu zungu na aliona kana kwamba kila kitu kilikuwa kinazunguka kwa kasi akaendelea kupiga kelele.Alihisi kuungua mwili mzima kwa moto mkali sana na taratibu akaanza kuhisi mabadiliko katika mwili wake.Ngozi yake ilianza kuwa ngumu.Lilikuwa ni tukio la kutisha sana.Moshi mwingi ukajaa mle chumbani na baada ya dakika kama tano hivi moshi ule ukatoweka na hapo ndipo kilitokea kitu cha ajabu mno.Emmy alikuwa ameguka nyoka lakini kichwa kilibaki kuwa cha binadamu.Lilikuwa ni joka kubwa la kutisha.James akalisogelea joka lile akalimwagia mafuta kichwani na ghafla Emmy akazinduka na kupiga ukelele mkubwa sana baada ya kujikuta katika umbo lile.
“ James….James naomba unisamehe…Nimekukosea sana na usinifanye hivi’ akalia kwa nguvu Emmy ambaye bado mwili wake ulikuwa unatoa mvuke.
“Huo ndio mshahara wa uovu wako.Ulimkatili mwanangu na haya ndiyo malipo yake.Hii ni adhabu yako na utaishi hivyo kwa siku zote za maisha yako.Nataka dunia yote wafahamu uovu ulioufanya na ili liwe fundisho kwa wengine.Kazi iliyonileta imekamilika na hautaniona tena katika maisha yako Emmy na wala usihangaike kunitafuta kwani mimi si binadamu wa kawaida tena.I’m a half devil.Nakutakia kila la heri katika maisha yako mapya” akasema James halafu akafungua mlango na kuwaita wale walinzi wake wawili.Wakasimama kati kati ya chumba huku wameshikana mikono halafu James akawashika vichwani akaongea maneno yake aliyoyajua mwenyewe na kitu kama wingu kikatokea mle chumbani na katika wingu lile James na vijana wake wakapotea.Wingu lile lilipotoweka James na watu wake hawakuwapo wala kila kitu chao.Emmy akapiga kelele kubwa sana.
Kelele alizopiga Emmy zikawafikia wahudumu ambao walifika mara moja katika chumba kile ili kujua kama kuna tatizo lolote.Mlango haukuwa umefungwa wakaingia ndani na ndipo walipokutana na kitu cha kutisha sana.Kulikuwa na joka kubwa mno lenye kichwa cha binadamu.Muhudumu mmoja akaanguka na kuzimia kwa uoga.Mwingine akakimbia na kwenda kutoa taarifa kuhusiana na tukio lile.Kwa haraka wakataarifiwa polisi ambao walifika pale haraka sana na kuelekea chumbani.Waliingia chumbani mle wakiwa na silaha zao tayari kwa lolote linaloweza kutokea na wao kama wengine wote walistushwa mno na tukio lile la ajabu.Hakuna aliyewahi kuliona tukio kama lile la nyoka mwenye kichwa cha binadamu.Emmy alikuwa analia kwa nguvu.
Taarif za kuonekana nyoka mwenye kichwa cha binadamu zilianza kusambaa kwa kasi usiku ule na ndani ya muda mfupi watu wakaanza kufika pale hotelini hususan waandishi wa habari walotaka kufahamu ukweli wa tukio hilo.Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha naye aliwasili katika hoteli ile na akathibitisha kutokea tukio lile kwa vyombo vya habari vilivyokuwapo pale hotelini.
Upelelezi wa chanzo cha tukio lile ukaanza mara moja.Wahudumu walihojiwa na wakatoa maelezo yao kwamba chumba kile kilipangwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la James ambaye alijisajili hotelini hapo kama mfanya biashara wa kimataifa.Kitu cha ajabu ambacho kiliwashangaza wengi ni pale ambapo picha ya james haikuonekana katika kamera yoyote ya usalama pale hotelini.Yalikuwa ni mambo ya kushangaza sana.Kwa kupitia simu iliyokutwa katika mkoba wa Emmy wakafanikiwa kuzipata namba za baba yake wakampigia.Akiwa amelala chumbani kake akitafakari mara simu yake ikaita.Aliitazama simu ile ikiita akasita kuipokea.
“Baada ya aibu yote hii aliyotutia Emmy anadiriki kunipigia simu? Anataka nini? Akajiuliza baba yake Emmy lakini mwishowe akaamua kuipokea simu ile.
“hallo” akasema
“ Hallo ndugu samahani naomba kukuuliza unamfahamu mwenye namba hii ya simu? Ikauliza sauti ya upande wa pili
“ Ndiyo ninamfahamu”
“ Mna mahusiano gani naye?
“ Ni mwanangu” akajibu baba yake Emmy kwa wasi wasi
“ Mbona unaniuliza hivyo nini kimetokea? Wewe ni nani? Akauliza baba yake Emmy
“Unaongea na afisa wa polisi hapa .Kuna tukio limetokea hapa Meru view hotel usiku huu linalomuhusisha mwanao.Tunakuomba ufike hapa mara moja”
“ Afande nini kimetokea? Nini kimemtokea mwanangu? Akauliza baba yake Emmy kwa mstuko
“ Sintaweza kukwambia kwa simu lakini ninakuomba ufike hapa hotelini mara moja ili u weze kushuhudia wewe mwenyewe.” Akasema afisa Yule wa polisi na kukata simu.Baba yake Emmy jasho lilikuwa linamtiririka.
“ baba Emmy nini kimetokea? Akauliza mke wake ambaye naye alistushwa na mabadiliko yale ya ghafa ya mume wake
“ Kuna afisa wa polisi amenipigia simu na kunitaarifu kwamba kuna tatizo limemtokea Emmy.”
“ Emmy !!! mama yake naye akastuka
“ Ndiyo..lakini hajasema ni tatizo gani”
“ Ouh Emmy amefanya nini tena ? akajibu mama yake huku akilia
“ Nyamaza usilie.Nataka nielekee huko nikaone nini kimetokea” akasema baba yake Emmy
“ Tunakwenda sote”
“ Hapana ,wewe utabaki hapa hapa.Vipi kama kuna tatizo kubwa?
“ hapana baba Emmy.Lazima na mimi niende nikashuhudie kilichompata mwanangu. Akasema mama Emmy na wote wakainuka na kuanza kujiandaa.

*********************

Ni muda wa kwenda kulala sasa.Tayari tulikwisha fanya maombi ya usiku yaliyoongozwa na Chris.Nikiwa najiandaa kupanda kitandani mara simu yangu ikaita.Alikuwa ni baba mkwe.
“Hallo baba “ nikasema baada ya kupokea simu ile
“ Wayne kuna tatizo limetokea” akasema baba mkwe
“ tatizo !! ………nikastuka
“ndiyo kuna tatizo limetokea.Nimepigiwa simu na afisa wa polisi usiku huu akinitaarifu kwamba kuna tataizo limemtokea Emmy katika hoteli ya Meru view na amenitaka nifike huo mara moja”
“ Umesema Meru View hotel? nikauliza
“ Ndiyo”
“ Huyo afisa wa polisi amesema ni tatizo gani limempata Emmy?
“Hajaniambia ni tatizo gani lakini amenitaka nifike mara moja”
“baba naomba unisubiri ninakupitia hapo nyumbani sasa hivi ili twende wote.Tafadhali usiende peke yako” nikasema na kukata simu.Nikavuta pumzi ndefu
“ Emmy kafanya nini tena safari hii? Nini kimetokea katika hoteli hiyo? Nakumbuka hoteli hiyo ndiyo alifikia mtu anayeitwa james ambaye ni baba mzazi wa Baraka.Nini kimetokea hapo hotelini?Lazima kutakuwa na tukio kubwa ngoja niende nikashuhudie” nikawaza huku nikivaa nguo halafu nikatoka na kwenda kumgongea Chris nikampa taarifa zile na kwa haraka wote tukaondoka kuelekea kwa baba mkwe
“ Kwa mujibu wa Sheila hoteli hiyo aliyoitamka baba mkwe ndiyo alifikia mtu anayeitwa James baba mzazi wa Baraka.Unadhani nini kinaweza kuwa kimetokea? Nikamuuliza Chris
“Sifahamu Wayne.Ngoja tukajionee wenyewe nini kimetokea” akasema Chris.Hatukuongea tena hadi tulipofika kwa baba mkwe.Tulimkuta akiwa katika hali ya wasi wasi mwingi
“Baba nini kimetokea? Nikamuuliza
“ hata mimi sijui chochote wayne.Nimepigiwa simu usiku huu na afisa wa polisi akinitaka nifike hapo hotelini mara moja.Tusipoteze wakati twendeni haraka.” Akasema baba mkwe na wote tukaingia garini tukaelekea eneo la tukio
“Emmy atakuwa amefanya nini tena safari hii? Kama ni tukio linalowahusisha hadi polisi basi lazima litakuwa ni tukio kubwa ..Naomba Mungu asiwe amejeruhi mtu.” Akasema baba mkwe.hakuna aliyemjibu kila mmoja alikuwa anawaza lake.Nilianza kupata picha kwamba huyo mtu anayeitwa james lazima kuna kitu alitaka kufahamu kuhusiana na Emmy na ndiyo maana akamtaka Sheila wakaonane hotelini kabla hata hajaonana na Emmy.Sheila na Emmy walikuwa katika ugomvi mkubwa nina hakika lazima Sheila atataka kuitumia nafasi hiyo kumchafua Emmy kwa huyo bwana wake na kama atakuwa amemueleza ukweli kuhusiana na Baraka lazima kutakuwa na tukio kubwa limetokea hapo hotelini” nikawaza.
Tulifika hotelini na kukuta idadi kubwa ya askari wakilinda eneo hilo .Watu walikuwa wengi pia.Nilianza kutetemeka mwili baada ya kuuona umati ule mkubwa wa watu pamoja na askari wengi.
Baba mkwe akajitambulisha kwa askari,tukachukuliwa na kupelekwa kwa kamanda wa polisi wa mkoa ambaye alikuwapo pale hotelini,
“Lazima kutakuwa na tukio kubwa kiasi cha kuwakusanya watu wote hawa wa ngazi za juu mahala hapa.” Nikawaza baada ya kumuona pia na mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa pembeni ya kamanda wa polisi wa mkoa.Miguu ilikuwa inanitetemeka.Tulisalimiana na mkuu wa mkoa na kamanda wa polisi wa mkoa halafu kamanda wa polia akatuvuta pembeni mimi ,baba mkwe na Chris kwa maongezi .Hakutaka mama mkwe asikie kile alichotaka kutuambia.
“ Jamani kwanza nawaomba samahani kwa kwuasumbua usiku huu lakini kutokana na uzito wa tukio lililotokea imetulazimu kuwaiteni hapa .Emmy ni mwanao wa kumzaa mwenyewe?
“Ndiyo .Emmy ni mwanangu kabisa” akajibu baba mkwe
“ Unaishi naye nyumba moja au yeye ana makazi yake mengine?
“ Kwa sasa Emmy amekwisha olewa na ana kwake na huyu hapa ni mume wake ingawa kumetokea kutokouelewa baina yao na wakatengana” akasema baba mkwe
“ Sasa baba kuna tukio limetokea usiku huu hapa hotelini.Kwa mujibu wa wahudumu wa hoteli hii walisikia kelele za mwanamke akiomba msaada na walipokimbia kwa ajili ya kwenda kumsaidia mwanao mle chumbani walikuta kitu cha ajabu sana”
“ Afande naomba unieleze ukweli,mwanangu amefariki dunia? Akauliza baba mkwe
“ Habana hajafariki dunia.”
“ sasa nini kimemtokea? Akauliza baba mkwe huku akivunta pumzi kwa nguvu
“ Ninyi ni wanaume na ninawaomba muwe na mioyo migumu lakini ukweli ni kwamba Emmy amegeuka nyoka”
Nilihisi mwili wangu wote umekufa ganzi kwa taarifa ile.Miguu haikuwa na nguvu ikanilazimu kumuegemea Chris ambaye naye alikuwa anatetemeka.Baba mkwe midomo ilikuwa inamcheza na hakuweza kuongea.Michirizi ya machozi ikaonekana machoni pake.Akaanguka chini.Haraka haraka askari wakafika na kumbeba wakamkimbiza katika gari la wagonjwa ambalo lilikuwapo pale hotelini kwa ajili ya kutoa msaada kwani ilitegemewa watu wengi wangepatwa na mstuko kwa tukio lile
“ Afande naomba mnieleze ni nini hasa kilichotokea? Imewezekanaje Emmy ageuke nyoka? Nikamuuliza kamanda wa polisi wa mkoa .Kabla hajatujibu nikawaona maaskari wakiwa wamembeba mama mkwel katika machela wakimuwahisha katika gari la wagonjwa.Nadhani alikuwa amezidiwa kwani huwa ana matatizo ya shiniko la damu kwa hiyo alipomuona mume wake ameanguka ghafla naye akazidiwa..
“ Wayne ni vigumu kusimuilia kuhusu mkasa huu kwani kila kitu kinaonekana kama muujiza fulani lakini tunaendelea kufanya uchunguzi na tutabaini nini chanzo cha tukio hili.Ninalihusisha tukio hili na imani za kishirikina kwani katika hali ya kawaida haiwezekani binadamu akabadilika na kuwa nyoka.” Akasema kamanda wa polisi.Chris akaondokana kwenda kufuatili hali ya baba na mama mkwe nikabaki nimesimama na wale askari.
“ Afande ninaweza kuruhusiwa kwenda kumuona Emmy huko chumbani”
“ Hapana Wayne.Kwa sasa haturuhusu mtu yeyote aingie mle chumbani hadi uchunguzi utakapokamilika.Tunataka pia kuhakikisha kwamba kunakuwa na usalama wa kutosha kwani hatuna uhakika kama kiumbe kile hakiwezi kuwa na madhara kwa biandamu na ndiyo maana unaona tumewatoa hata wageni wote waliokuwa vyumbani kwa ajili ya usalama wao” Akasema kamanda wa polisi.
“ Afande Emmy amekutwa na nani chumbani? nikauliza
“ hakukuwa na mtu yeyote chumbani zaidi ya Emmy peke yake.Chumba hicho alichokutwa na tukio hilo kilikuwa cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la James na ambaye haijulikani yuko wapi hadi mida hii.Tunahisi pengine yeye ndiye aliyetenda tukio hili na kisha akakimbia.” Akasema kamanda wa polisi.Nikainama na kufikiri halafu nikasema
“Afande kuna kitu naomba nikiseme ambacho naona kinaweza kusaidia katika uchunguzi kuhusiana na tukio hili.Kuna mwanamke mmoja anaitwa Sheila nina hakika atakuwa anafahamu kitu kuhusiana na jambo hili” nikasema na kumstua kamanda wa polisi wa mkoa
“ Sheila ni nani? Akauliza
“ Sheila ni rafiki mkubwa wa Emmy “
“ Kwa nini unasema hivyo Wayne? Akauliza kamanda wa polisi
“ Jana nilikuwa safarini na Sheila tukitokea Mombo Tanga na tukiwa njiani alipigiwa simu na mtu mmoja aitwaye james na kumtaka waonane hapa hapa hotelini usiku.Nadhani atakuwa anafahamu kitu kuhusiana na kilichotokea.Endapo atakamatwa na kuhojiwa anaweza akatusaida kujua mahala aliko huyo James” nikasema
‘ Wayne unamfahamu huyo mtu anayeitwa James?
“ hapana afande simfahamu na sijawahi kumuona .Nimemsikia jana kwa mara ya kwanza toka kwa Sheila lakini yeye ndiye chanzo cha mimi kutenganana mke wangu kwani aliwahi kuzaa mtoto na mke wangu tukiwa ndani ya ndoa kwa hiyo naweza kusema kwamba ni watu waliokuwa wana mahusiano ya kimapenzi ” nikasema.
Kamanda wa polisi akawaita maafisa watatu wa polisi akaongea nao halafu akanifuata.
“ Wayne unafahamu mahala anakoishi huyo Sheila” akauliza
“ Ndiyo afande.” Nikajibu
“ Basi utaongozana na hawa maafisa wa polisi na kwenda kumchukua Sheila kwa ajili ya mahojiano.”
Tuliingia katika gari la polisi na kuondoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwa Sheila.Kwa kuwa ilikuwa ni usiku ilinilazimu nimpigie kwanza simu ili kumfahamisha kwamba ninahitaji kuonana naye.Alistuka sana kwa nini ninataka kuonana naye usiku ule.Haraka haraka akafungua mlango na kupigwa na butwaa baada ya kugundua nilikuwa nimeongozana na maaskari .
“ Karibui ndani.” Akasema kwa sauti ya kutetemeka.aliogopa sana
“ Wayne kuna nini? Mbona usiku huu tena ukiwa na askari? Kuna tatizo gani? Akauliza Sheila kwa wasi wasi.
“Shela kuna tatizo limetokea usiku wa leo”
“ tatizo gani?
“ Emmy amepatwa na matatizo “
“ matatizo?
“ Ndiyo amepatwa na matatizo.”
“ Matatizo gani” akauliza kwa wasi wasi
“ Alikuwa amekwenda kuonana na James na hatujui kilichotokea kati yao lakini naomba ufahamu kwamba Emmy amegeuka nyoka”
Pale pale Sheila akaanguka chini na kupoteza fahamu.Damu ikaanza kumtoka mdomoni Ikatulazimu kumpakia garini na kumkimbiza hospitali.Tulipomfikisha hospitali madaktari wakasema kwamba Sheila alikwisha fariki kitambo. Nilichanganyikiwa.
Tulirejea tena hotelini nikiwa sina nguvu kabisa.mambo yale yaliyotokea yalinimaliza kabisa nguvu.Nilitafuta sehemu nikaa kwani sikuweza tena kusimama.Mambo yaliyokuwa yanatokea yalikuwa ni kama filamu.Niliwasiliana na Chris akaniambia kwamba alikuwa ameongozana na baba na mama mkwe ambao walikimbizwa hospitali kutokana na mstuko walioupata.Nilimtaarifu kuhusianana kifo cha Sheila akastuka sana

*********************

Kulipambazuka tukiwa bado pale pale hotelini.Wageni wote waliondolewa na kupelekwa katika hoteli nyingine .Asubuhi hii kulikuwa na heka heka kubwa hapa hotelini.Tayari taarifa zilikwisha samba kila kona ya dunia kwamba kuna mwanamke amebadilika na kuwa nyoka .waandishji wa habari wa vyombo mbalimbali walifika asubuhi hii ili kuweza kuipata habari hiyo.Watu wote walizuiliwa nje ya hoteli na hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kuingia ndani.
Nikiwa nimekaa sofani nikiwa na rafiki yangu Beka aliyefika usiku baada ya kumpigia simu akanifuata afisa mmoja wa polisi na kuniambia kwamba kamanda wa polisi wa mkoa anahitaji kuniona.Nikaongozana na Beka na yule afisa wa polisi hadi katika mlango mmoja wa chumba kilichokuwa na idadi kubwa ya askari wamesimama nje.Nilijua hapo ndipo kwenye tukio
“ wayne,kuna mambo ambayo naomba uyafahamu kuhusiana na kinachoendelea hapa..Ni kwamba kwa sasa Emmy ametulia halii tena kama jana na anaweza kuongea.Ameongea nami na amesema kwamba anahitaji kuongea nawe.Je uko tayari kuingia na kuongea naye?
‘ Niko tayari afande “ nikasema
‘ Vizuri .sasa tunataka uongee naye na ufahamu nini kilichotokea nani alifanya tukio hilo? Huyu James yuko wapi na tunawezaje kumkamata?
“ sawa afande” nikajibu lakini uso wangu ukionyesha uoga
‘ Usiogope Wayne tutakuwa karibu na hakuna kitu chocote kitakachokutokea” akanipa moyo kamanda wa polisi nikafunguliwa mlango na kungia ndani.Hakuruhusiwa mpiga picha yeyote yule kuingia mle chumbani.Nilikuwa peke yangu na askari wawili waliokuwa na silaha.Mwili wangu ukanisisimka baada ya kuliona joka lile kubwa la kutisha likiwa na kichwa cha Emmy.Toka nimezaliwa sijawahi kuona joka la namna ile.Nilikuwa natetemeka mwili mzima kwa hofu.Niliogopa sana.Sikutaka hata kusogea karibu zaidi.
‘Wayne usiogope,siwezi kukudhuru.Tafadhali sogea karibu ,kuna mambo ninayotaka kuongea nawe.” Akasema Emmy.Hakuwa amebadilika kitu kichwani.Nywele zake ndefu ,uso wake wa kung’aa,nyusi zake zilizochongwa vizuri ,kope zake za bandia kila kitu kilikuwa vile vile.Kuanzia shingoni kushuka chini alikuwa na mwili wa joka la kutisha sana
“ Sogea karibu Wayne” akasema Emmy
“ Nikapiga hatua kumsogela lakini kwa tahadhari kubwa sana.Wale askari wawili waliokuwa mle ndani waliziweka tayari silaha zao endapo kungetokea jambo lolote baya.Nilikuwa ninatetemeka wakati nikimsogelea karibu
“ Wayne naomba usiniogope mimi ni yule yule Emmy mke wako lakini kwa sasa nina mwili wa nyoka.Wayne nimekuita hapa ili niuungame kwako na kukuomba msamaha kwa mambo yote niliyowahi kukufanyia.Nimekufanyia mambo mengi mabaya sana na ambayo hayavumiliki hata kidogo.Hukupaswa kufanyiwa mambo yale niliyokufanyia,Ulinipa kila nilichokihitaji lakini sikuridhika na kutaka kupata zaidi.Ulijitahidi kunipa kila raha ya dunia lakini sikutosheka nikataka kupata raha zaidi.Kupenda starehe na anasa vimeniponza na haya ndiyo malipo yake” akasema Emmy.Macho yangu yalikuwa yanatoa machozi
“Wayne wewe ni mwanaume wa pekee kabisa katika hii dunia.Pamoja na kukufanyia mambo mengi,vitimbi vya kila aina lakini bado uliendelea kunipenda na kunijali na hukuwahi hata siku moja kunitolea lugha ya matusi na kashfa licha ya mimi kukutukana kila mara.Naomba nikiri kwako kwamba baada ya kuamua tuachane ndipo nilipouona umuhimu wako katika maisha yangu.Nilijiona kama nimekosa kitu fulani muhimu na ndipo nilipoanza jtihada za kuyarejesha mapenzi yetu tena.Nilienda kwa mganga Tanga ambaye alinidanganya kwamba atanisaidia ili uweze kurejea kwangu.Nilikubali kumtoa kafara mwanangu Baraka kwa ajili ya kurudiana nawe.Wayne naomba unisamehe kwa kosa hili kubwa nililolifanya.Sikuishia hapo niliendelea na uovu wangu na mwishowe nikamroga Clara akaanguka na kupooza mwili.Najua nilikuumiza sana kwa mambo haya yote.Katika dakika zangu hizi za mwisho naomba unisamehe kwa yale yote niliyokukosea.Nahitaji unisamehe wayne kabla sijafa” akasema Emmy .Nilishindwa niseme nini ni machozi tu yaliyokuwa yananitoka
“ wayne naomba ufahamu kwamba sikuwa mwaminifu katika ndoa yetu hata kidogo.Nilitembea na wanaume wengi nje ya ndoa na mmoja wao ni James ambaye ndiye baba mzazi wa Baraka.James ndiye aliyenifanya hivi baada ya kugundua kwamba nilikuwa nimemtoa mwanae kafara.James ana nguvu za kishetani na aliumia sana aliposikia kwamba nilifanya kitendo kile kwa mwanae wa pekee kabisa kwani kwa sasa yeye hana tena nguvu za kiume.Amefanya hvi kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa jambo hilo.Siwezi kumlaumu kwa jambo hili alilolifanya kwani ninastahili.Ninastahili adhabu hii kwa kosa hili na makosa yote niliyoyafanya.” Nilishindwa kujizuia nikaanza kulia kwa kwikwi
“ wayne naomba usilie mpenzi wangu.Usinililie mimi.Ninastahiili adhabu hii.Nimefanya mambo mengi mabaya ,nimewakosea watu wengi na haya ndiyo malipo yake.”
“ Emmy kwa nini lakini yakukute haya? Kwa nini alifanya hivi James? Nikasema kwa uchungu
“ wayne usisikitike kabisa.Kama nilivyosema ninastahili adhabu hii.Nimelia usiku kucha na baada ya kutafakari nimegundua kwamba ninastahili adhabu .”
“ Niambie tutampata wapi james? Nikauliza
“ James hamtaweza kumpata kamwe.Yule ana nguvu za kishetani na hata mimi sifahamu ameelekea wapi kwani aliyeyuka hapa kama upepo yeye na walinzi wake na sijui wako wapi.Msisumbuke kumtafuta kwani hamtaweza kumpata na alinihakikishia hilo kwamba hakuna atakayeweza kumpata.”
“ lazima tumpate james ili aweze kukurudisha katika umbo lako la ubinadamu.” Nikasema huku nikifuta machozi.Sikuwa na uoga tena wa kukaa karibu na Emmy.
“ Wayne msipoteze muda huo.Yaliyotokea yamekwisha tokea na tuyaache yaende.Kupitia mimi watu wengi watajifunza kwamba atendaye kwa ubaya hulipwa kwa ubaya.Muda unakwenda sana Wayne naomba uniitie baba na mama niwaombe msamaha.Nimewakosea sana” akasema Emmy
“ baba na mama wote wako hospitali baada ya kupatwa na mstuko “ nikamwambia.Akafumba macho .nahisi alisikia uchungu mkubwa
“Wayne kama sintaonana nao naomba uniombee msamaha .Waambie kwamba nimetubu makosa yangu yote niliyowakosea na ninawaomba waniombee sana” akasema Emmy
“ Vile vile naomba uniombee msamaha kwa rafiki yangu Sheila .Nilkorofishana naye siku chache zilizopita nikamtolea maneno machafu.mwambie anisamehe”
“ Emmy Sheila amefariki dunia jana usiku baada ya kuzipata taarifa hizi” nikamwambia Emmy ambaye alifumba tena macho
“ Wayne kuna mambo mawili ambayo nataka kukuomba.Kwanza nataka uniletee padre ili niungame dhambi zangu na pili naomba ufahamu kwamba hakuna njia nyingine yoyote ya kufanya kunirejesha katika ubinadamu na siwezi kuendelea kuishi katika hali hii.Mwenye uwezo wa kunirejeshea ubinadamu ni James lakini naye ametoweka kimiujiza na si rahisi kumpata tena.kwa hiyo ninaomba baada tu ya kuungama makosa yangu kwa padre nitaomba nipigwe risasi nife.Nikisha kufa tu Clara atakuwa mzima tena.Ninaomba usimuache Clara.Yeye pekee ndiye mwanamke anayekufaa na nina hakika hata wewe unampenda pia.Fanya kila utakaloweza umuoe Clara na uanzishe familia..”
“ Emmy tafadhali usiseme hivyo.Sintakubali ufe.Tutamtafuta James kila kona ya dunia na tutampata” nikasema
“ Wayne naomba unisikie.hakuna atakayeweza kumpata James.Ana nguvu za kishetani na anauwezo wa kuyeyuka kama upepo kwa hiyo hataweza kukamatwa.Nenda kafanye hayo niliyokwambia Wayne.Nahitaji padre haraka sana” akasema Emmy
“ Emmy hapana sintaweza kufanya hivyo hata kidogo.Siko tayari ufe..Jeshi la polisi likisaidiana na polisi wa kimataifa watamtafuta James kila kona ya dunia na atakuja kukurejesha katika ubinadamu’ nikasema kwa uchungu
“ Wayne hapa nilipo nina maumivu makali sana.Ninahisi kama ninaogelea kwenye tanuru la moto.Niondolee mateso haya kama unanipenda Wayne.Niitie padre niungame dhambi zangu na baada ya hapo nipigwe risasi nife niondokane na mteso haya makali.Fahamu vile vile kwamba kifo changu ndiyo uzima wa Clara.Nahitaji uwe na maisha mazuri na mwanamke unayempenda naye akakupenda kwa moyo wake wote na haya yatawezekana pale tu nitakapofariki kwani Clara atapona.” Akasema Emmy
“ Nenda Wayne…nenda haraka” akasisitiza
Nilitoka ndani ya kile chumba nikilia machozi.
“ Wayne nini kimetokea? Emmy amesemaje? Akaniuliza kamanda wa polisi
Niliwaleleza wale maafisa wa polisi kuhusiana na kille nilichoongea na Emmy .kamanda wa polisi mkoa aliniomba niende nikamchukue padre kama alivyotaka Emmy yeye akiambatana na maafisa wengine wa polisi na viongozi wa mkoa waliitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili suala lile lililogubikwa na utata mkubwa.
Niliongozana na askari wawili kulekea kanisani kwa ajili ya kumchukua padre.Tukiwa njiani niliwasiliana na Chris aliyekuwa hospitali akanitaarifu kwamba baba mkwe hali yake ilikuwa inaendelea vizuri ila mama mkwe bado hali yake haikuwa nzuri.Nilimweleza kila kitu nilichoongea na Emmy hata naye alipatwa na mstuko.Nilifika kanisani na kumpata padre.Nilimueleza kila kitu bila kumficha na bila kupoteza wakati tukaingia garini na kurejea hospitali.Tulipofika hotelini tulikuta kuna vurugu kubwa kati ya askari polisi na kundi la watu waliokuwa wamevunja uzio wa hoteli wakitaka kuingia ndani kumuona mwanamke aliyegeuka nyoka.Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.Kwa kuwa tulikuwa na gari la polisi hatukupata matatizo tukapita na kuingia ndani.Nikaingia katika chumba kile ambacho hakutakiwa kuingia mtu yeyote asiyehusika.Bado Emmy akiwa na mwili wa nyoka alikuwa amekaa pale pale.
“ Wayne umerudi? Umekuja na padre? Akauliza Emmy baada ya kuniona nimeingia mle chumbani.Aliongea kwa sauti yake ile nzuri na nyororo kana kwamba hakuwa na mwili wa nyoka.Yalikuwa ni maajabu makubwa kuwahi kuyashuhudia
“Ndiyo Emmy.Nimekuja naye” nikasema na kumuita padre akaingia mle ndani
“ Wayne naomba unipishe .Nataka niwe peke yangu na padre” akasema Emmy
Wale askari wawili waliokuwa na silaha walikataa kutoka kwa kuhofia labda pengine Emmy angeweza kumdhuru padre .Niliwahakaikishia kwamba Emmy hakuwa na madhara yoyote kwani bado ni binadamu halisi.Wakuu wao wakawaomba watoke mle ndani ya chumba na kuwaacha padre na yule mtu nyoka mle chumbani.hata hivyo walikuwa makini sana katika kusikiliza endapo kungetoka sauti yoyote ile
Wakati padre akiendelea kuongea faragha na Emmy mle chumbani niliomba msaada wa polisi ili nielekee hospitali kuonana na baba mkwe.Nilipanda gari la polisi tukaelekea hospitali.Tulipofika tukaonana na Chris akatupeleka moja kwa moja katika chumba alicholazwa baba mkwe.Alikuwa amekaa kitandani akionekana mwenye mawazo mengi sana
“ Wayne” akasema baba mkwe baada ya kuniona
“ baba unaendeleaje ? nikauliza
“ Ninaendelea vizuri japokuwa hawataki kunipa ruhusa nikashughulikie tatizo la mwanangu.Kuna taarifa gani huko? Nini kinaendelea? Tukio lile limetokeaje? Akauliza baba mkwe.Ilinilazimu kumueleza kila kitu namna tukio lile lilivyotokea hadi hatua iliyopo hivi sasa.Nilimueleza pia maongezi yetu yote tuliyoongea na Emmy na mwisho nikamwambia kuhusu ombi la Emmy.Aliinama akafikiri na kusema
“ wayne Emmy yuko sahihi.Hakuna namna tunayoweza kufanya ili kumrejesha katika ubinadamu.Hapo alipo anapata mateso makali sana na ili kumuepushia mateso hayo ninakubali maombi yake yatekelezwe.” Akasema baba mkwe huku akivaa shati lake
“ Wayne tunakwenda wote hospitali .Nataka nikalimalize suala hili.” Akasema baba mkwe na kumuaga muuguzi aliyekuwa ameleta dawa kwamba atarejea baada ya muda mfupi.Tuliingia garini na kuondoka kurejea hotelini.Tayari padre alikwisha maliza kuongea na Emmy na alikuwa anazungumza na maafisa usalama.Baba mkwe akaingia mle chumbani kwa Emmy na tukamuacha mwenyewe ili aongee na binti yake.Baada ya kama dakika ishirini hivi baba mkwe akatoka mle chumbani.macho yake yalikuwa mekundu.
“Yuko wapi kamanda wa polisi? Akauliza baba mkwe.bahati nzuri wakati anamuulizia naye akatokea akiwa na maafisa wengine.Walimaliza mkutano wao wa dharura uliofanyika pale pale hotelini
“baba pole sana.Unaendeleaje? akasema kamanda wa polisi huku akimpa mkono baba mkwe kumsalimia
“ Ninamshuku Mungu ninaendela vizuri sana.Poleni na nyie”
“ ahsante sana baba tumeshapoa.”
Baba mkwe akamuomba wasogee pembeni kidogo waongee,nami pia nikajiunga nao
“Afande nimetoka kuongea na Emmy.Hali yake inasikitisha sana.Mmefikia wapi katika kumkamata mtu aliyetenda kitendo hiki? Akauliza baba mkwe
“ Kwa kweli mpaka sasa bado suala hili linautata mkubwa.Bado hatujafanikiwa kumpata huyo James na haijulikani yuko wapi.Taarifa tuliyoipokea toka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro haionyeshi jina la mtu ambaye ndiye anayesemwa kuhusika na tukio hili.Kamera za ulinzi za hapa hotelini hazimuonyeshi kabisa huyo mtu kwa hiyo tumeshindwa kuipata sura yake.Mzee tukio hili limetawaliwa na nguvu za giza kwa kiasi kikubwa sana lakini tunafanya kila tuwezalo ili kumfahamu huyo James ni nani na tutampata tu” akasema kamanda wa polisi
“ Kamanda ninaafikiana na mawazo ya Emmy kwamba tulimalize suala hili na tumundolee maumivu aliyonayo kwa sasa.Tufanye kama anavyotaka.Nimeongea naye na nimeyaona mateso makali aliyonayo.Huyo James inaonekana haitakuwa rahisi kumpata kutokana na mazingira yake kwani kwa mujibu wa Emmy alitoweka tu kama upepo ” akasema baba mkwe
“ Mzee unamaanisha tumpige risasi mwanao?
“ Ndiyo afande.Niko tayari mwanangu apigwe risasi ili aondokane na mateso haya makubwa aliyonayo.” Akasema baba mkwe
“ Suala hilo ni gumu na tayari limezua mjadala mkubwa kwani sheria hazituelekezi hivyo.”
“ Nalifahamu hilo lakini hakuna namna nyingine ya kuweza kumrudisha mwanangu katika ubinadamu.Hebu fanyeni maamuzi haraka haraka ili tuweze kumuondolea mwanangu maumivu makali aliyonayo.” Akasema baba mkwe.

************************

Sulala la Emmy lilizidi kuchukua sura mpya kila dakika.Eneo la kuzunguka hoteliile lilifurika watu waliotaka kumuona nyoka mtu.Hatimaye baada ya mjadala mrefu ukihusisha makundi mbali mbali ya wanaharakati wa haki za binadamu iliamriwa kwamba Emmy apigwe risasi kwani alianza tena kulia kwa mateso makali aliyokuwa anayapata.Japokuwa hata mimi niliona kwamba ni uamuzi wenye busara kwa ajili ya kumuondolea Emmy mateso aliyokuwa anayapata lakini niliumia mno.Emmy alikuwa ni mke wangu wa ndoa na japokuwa tulikuwa tumetengana na akanifanyia vitimbi vingi sana lakini nilimsamehe na niliumizwa sana na tukio lile.Hata wewe ndugu msomaji lazima ungeumia sana kwa mtu ambaye mmeishi naye kwa miaka mingi atokewe na tukio kama lile.Ilikuwa ni saa kumi na mbili za jioni maamuzi hayo yalipotolewa.Hakutakiwa mtu mwingine yeyote aingie mle chumbani kwa Emmy kwani alikuwa akipiga kelele kubwa kwamba anaumia.Saa moja za jioni askari watatu waliokuwa na bunduki zenye viwambo vya kuzuia sauti wakaingia katika chumba cha Emmy.Wengine wote tukakaa kimya kila mmoja akisali kufuatana na kitendo kinachoenda kutokea mle ndani.Sauti ya Emmy akipiga kelele za maumivu makali zilisikika.Niliumia sana.Baada ya kama dakika kumi hivi askari wale wakatoka.Tayari walimaliza kazi.Machozi yalinitoka.Tayari Emmy alikuwa amepigwa risasi.Huo ukawa mwisho wake haapa duniani.Niliumia mno.

**********************

Hatimaye siku ya siku ikafika.Ni siku ambayo safari ya mwisho ya Emmy hapa duniani ilihitimishwa.Ni siku ya mazishi ya mtu aliyewahi kuwa mke wangu wa ndoa,mwanamke niliyempenda sana licha ya vitimbi na vituko vya kila aina alivyonifanyia.Sikutegemea kama mwisho wa Emmy ungekuwa namna hii.Ulikuwa ni mwisho wa uchungu na wa masikitiko makubwa.
Tulikabidhiwa mwili na jeshi la polisi kwa ajili ya maziko ,mwili ambao ulikuwa ni kichwa tu .Ile sehemu ya chini iliyokuwa ni nyoka ilichukuliwa na kwenda kuteketezwa mbali na mji.Jeneza lenye kichwa cha Emmy halikufunguliwa hata wakati wa kutoa heshima za mwisho .
Watu walikuwa ni wengi sana makaburini.Wengi waliguswa na kifo kile cha Emmy na hasa mazingira yake .Wapo waliomuonea huruma na wapo waliokuwa wakimkejeli na kumbeza kwa vitendo vyake alivyokuwa akivifanya ili mradi kila mmoja alisema lake.Baada ya padre kufanya ibada fupi ya makaburini hatimaye jeneza lenye kichwa cha Emmy likaingizwa kaburini.Wa kwanza kutupia udongo alikuwa ni baba mkwe.Mama mkwe bado alikuwa hospitali .Wa pili kutupia udongo nilikuwa mimi.Baada yangu wakafuata ndugu jamaa na marafiki halafu zoezi la kufukia likaanza.Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu .Niliumia sana kila niliposikia kishindo cha udongo ukitupiwa kaburini.
“ Kwa heri Emmy.Pumzika kwa amani huko uendako.Siku zote nitakuombea ili uwe na mapumziko mema.Nina imani Mungu wetu mwenye upendo na huruma amekusameme dhambi zako zote kwani ulitubu kabla ya umauti.Siku zote nitazikumbuka na kuzienzi zile nyakati zote za furaha tulizokuwa nazo mimi wewe na Baraka .Utaendelea kuwa sehemu muhimu ya maisha yangu.Katika maisha yangu niliyoishi nawe nimejifunza mambo mengi sana,nimejifunza upendo wa kweli,uvumilivu na kumtegemea Mungu kwa kila jambo.Nitaviendeleza vitu hivi katika siku zote za uhai wangu zilizobaki hapa duniani.Kwa heri Emmy” nilikuwa nikiwaza wakati kaburi la Emmy likifukiwa.Baada ya zoezi lile kukamilika tukaweka shada za maua halafu tukarejea nyumbani.Nawashukuru sana rafiki zangu Chris na Beka waliokuwa nami kwa kipindi hiki chote cha matatizo na kunifariji .namshukur pia mama yangu alikuja kuungana name katika wakati huu mgumu.Mwili wangu ulikuwa umechoka sana nikaomba nipatiwe sehemu nipumzike.Nilitafutiwa sehemu nzuri chini ya mti nikawekewa godoro na kujilaza hapo
Picha yote ya maisha yangu na Emmy toka tulipokutana ikanijia kichwani.Nilishindwa kujizuia kutokwa na machozi.Niliyakumbuka maongezi yangu ya mwisho na Emmy kule hotelini akiniomba msamaha.
“Huyu James ni nani ambaye alimtenda Emmy vile? Nashindwa kuelewa ni binadamu mwenye roho ya namna gani anayeweza kumgeuza mwenzake nyoka.Hata kama alimkosea hakupaswa kumtenda mwenzake namna ile.Mpaka leo kitendawili cha James ni nani hakijateguliwa.Mtu pekee ambaye alikuwa akimfahamu James viuri ni Sheila lakini naye kwa sasa ni marehemu.Hakuna tena mtumwingine atakayetusaidia kuweza kumpata .Nakumbuka Emmy alisema kwamba tusisumbuke kumtafuta James kwanio hatutaweza kumpata.Kwa mujibu wa Emmy James alitoweka ghafla yeye na walinzi wake.Ama kweli duniani humu kuna maajabu makubwa sana.” Nikawaza na Kutokana na uchovu mwingi taratibu nikajikuta nikipitiwa na usingizi.
Sikumbuki nililala kwa muda gani lakini nilistuliwa na mtu aliyekuwa akinitingisha .Alikuwa ni Chris
“ hey Chris “ Nikasema kwa uchovu huku nikiyafikicha macho
“ Wayne samahani kwa kukuamsha.Kuna wageni wamekuja kukupa pole”
“ Ni akina nani?
“ Itakuwa vizuri kama ukiinuka na kwenda kuonana nao.Ni watu wako wa muhimu” akasema Chris
Nikainuka kwa uchovu na kuongozana na Chris kuelekea waliko wageni wangu waliokuja kunipa pole.Tuliiacha nyumba ya wazazi wa Emmy na kuingia katika nyumba ya jirani.Nilimfuata Chris tukaingia sebuleni na ghafla nikakutana na kitu cha ajabu kilichonistua mno.Mwili wangu wote ukanisisimka..Nilibaki nimepigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa nisiamini nilichokiona.
Mbele yangu alikuwa amesimama Clara akiwa na uso uliojaa machozi.Pembeni yake walikuwepo wazazi wake pamoja na baba mkwe.
“ Clara !!! nikasema kwa mshangao
“Wayne “ akaita Clara halafu akapiga hatua kunfuata tukakumbatiana.Sikuamini nilihisi kama vile bado niko ndotoni.
“ Ouh Wayne my love” akasema Clara na kunikumbatia kwa nguvu zaidi
“ Clara is that you? Nikasema huku nikimuangalia nisiamini nilichokiona.Mtu ambaye siku mbili zilizopita alikuwa kitandani na hakuweza kufanya kitu chochote leo hii ni mzima wa afya na huwezi kuamini kama alikuwa mgonjwa hajiwezi.
“ Its me Wayne..I’m ok now” akajibu Clara kisha tukakumbatiana tena.Ulikuwa ni kama muujiza kumuona Clara akiwa mzima namna ile.Niliachana na Clara na kwenda kuwasalimia wazazi wake
“Pole sana Wayne kwa kilichotokea na samahani kwa kuchelewa mazishi tulikosa usafiri wa haraka wa kutuwahisha huku Arusha” akasema Clara
“ nashukuru sana kukuona tena Clara.Bado siamini kama ni wewe kweli”
“ Ni mimi Wayne.” Akajibu Clara
“Imetokeaje hadi ukapona ghafla namna hii?
“ Hata mimi sifahamu imetokeaje Wayne lakini nilishangaa tu nimekuwa mzima ghafla kana kwamba sikuwa ninaumwa chochote .Sielewi haya yametokeaje” akasema Clara.Mara moja nikakumbuka maneno ya Emmy alisema kwamba pindi atakapofariki tu basi Clara atapona.Ni kweli Clara amepona.Nilimshukur sana Mungu kwa kumjalia mwanamke yule ninayempenda kupona na kuwa mzima tena
“ Wayne “ akaita baba yake Clara
“ naam baba “ nikaitika
“ Tumekuja sisi sote pamoja na Clara kukupa pole kwa matatizo yote yaliyotokea na kuungana nawe katika kipindi hiki kigumu ulichonacho.Kama ilivyo kwako hata sisi tumeumia sana na ndiyo maana tuko hapa” akasema baba Clara
“ Baba nashukuru sana kwa kufika kwenu .,Nimefarikjilka sana kuwaoneni hapa mkiwa na Clara.Nimefarjika mno” nikasema
“Tulisikia kupitia vyombo vya habari kuhusiana na jambo lililotokea,tulistushwa sana lakini hatukufahamu kama aliyepatwa na tatizo lile alikuwa nimtu aliyewahi kuwa mke wako.Baada ya kupona ghafla Clara ndiye aliyetustua baada ya kuiona picha ya Emmy katika gazeti.Wayne poleni sana.Tukio lile lililotokea ni tukio kubwa na la kustusha.Clara alisisitiza kwamba lazima aje ahudhurie mazishi na kukupa pole .Wayne napenda kuchukua nafasi hii kukuomba samahani kwa maneno niliyokutamkia mimi mwenyewe wakati tulipokuja kumchukua Clara kumpeleka Dar es salaam kwa matibabu.Nilikutamkia maneno mabaya na ambayo yalikuudhi sana.Naomba tusameheane na tufungue ukurasa mpya kati yetu.Yaliyopita yamekwisha pita, tutazame ya mbele.Clara ametueleza mengi sana na tumemuelewa.Sisi kama wazazi wake hatutakuwa na kipingamizi chochote kwake kuhusiana na hatima ya maishayake na yeye mwenyewe ndiye atakayemchagua nani anataka kuwa naye maishani mwake.Kwa kuwa kwa sasa bado tuko katika majonzi,tutaongea zaidi kesho ” akasema baba yake Clara.Pamoja na kwamba nilikuwa katika majonzi lakini nilifurahi sana moyoni kwa kauli ile ya baba Clara.
“ baba nawashukuru sana kwa kufika kwenu.Kwa ufupi niI kwamba mimi sikuwa na tatizo lolote nawe.maneno yale uliyoyasema wakati ule yaliniumiza sana lakini nilikwisha yasahau yote.Yamekwisha pita.” Nikasema na kisha tukaendelea na maongezi .
Saa nne za asubuhi siku iliyofuata tuliwasindikiza wazazi wa Clara uwanja wa ndege kwa ajili ya kurejea Dar es salaam.Clara alibaki Arusha.Alitaka aendele kukaa nami na kunifariji.Baada y a kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro tulielekea makaburini ambako tuliwasha mishumaa katika kaburi la Emmy
“ Pumzika kwa amani Emmy.” Nikasema huku nikiweka shada la maua halafu nikampisha Clara
“ Emmy najua mimi na wewe hatukuwa tukielewana.Mambo mengi yalitokea kati yetu katika kulipigania penzi la Wayne.Nilikwisha kusamehe muda mrefu sana Emmy na nitakuombea upumzike kwa amani huko uliko.Ninakushukur u kwa sababu bila wewe nisingeonana na Wayne.Pumzika kwa amani Emmy” akasema Emmy na kuweka shada la maua.Tukiwa garini nilimsimulia Clara kila kitu kilichotokea na kila alichokifanya Emmy.Clara alilia sana .
“Wayne pole saana kwa mateso yote uliyoyapata ,wewe ni mwanaume wa pekee kabisa hapa duniani.Watu kama wewe ni nadra sana kuonekana zama hizi.Niliyaona machoz I yako wakati nikiumwa nikiwa sijiwezi kitandani ,nilikuona namna ulivyoumia.Machozi yale yamenidhihirishia ni namna gani unavyonipenda..Wayne ninakupenda na ni wewe pekee nitakayekupa moyo wangu.Wazazi wangu hawakutaka kabisa nirejee Arusha lakini niliwaeleza ukweli kuhusu mimi na wewe na wakanielewa.Wayne we’re free now.Its our time to enjoy life” akasema Clara
“Ni kwelihayo unayoyasema Clara.Ni wakati wetu sasa wa kuyafurahia maisha .Lakini sintaweza kuyasahau mateso na maumivu yote niliyoyapitia katika kipindi hiki chote nilichokaa na Emmy.Ilikuwa ni zaidi ya mateso,zaidi ya maumivu.It was BEYOND PAIN” Nikasema
“ Usijali wayne.I’m here now.Nitakusaidia kusahau yote yaliyotokea.Kwa pamoja tutasahau kila mateso tuliypoyapitia hapa duniani na kutengeza dunai yetu peke yetu,dunia iliyojaa furaha amani na upendo.” Akasema Clara
“ I love you Clara” nikasema
“ I love you too Wayne”
Wiki mbili baada ya kumalizika kwa msiba wa Emmy , mimi na Clara tukaruka kwa ndege tukaeleka katika visiwa vya Zanzibar kwa ajili ya mapumziko.Tulikuwa huru sasa na hatukuhgofia chochote kwani hakukuwa na yeyote atakaye tubughudhi.Mwanzo mpya wa maisha yangu na Clara.

TAMATI ASANTENI KWA KUTIMIA MDAA WENU KUFATILA SIMULIZI HII
 
Asante kawawa kwa kutuletea story nzr ila mwandishi kaonyesha mapungufu yafuatayo

1) Mwandishi hakutuonyesha pesa za kifisadi zilizofisadiwa na wayne zilirudishwaje kwenye jamii

2) Mwandishi kaonyesha kuzipa nguvu kubwa nguvu za giza kwa kitendo kile emmy kugeuka nyoka nilitegemea baada ya padri kufika tungeona nguvu ya kimungu ikishinda nguvu za giza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom