Sehemu ya 35
“Mtatumia muda gani?” aliuliza Maggie.
“Kesho jioni kaa mbele ya televisheni yako,” alisema Joker.
Maggie akaondoka mahali hapo, aliliamini kundi hilo ni lazima kile alichohitaji kifanyike kingefanyika kwa haraka sana.
Alipofika nyumbani aliendelea kuwasiliana na Andrea na kumwambia alitakiwa kupunguza kiasi cha pesa ili amlipe lakini mwanaume huyo alikataa katakata.
Siku iliyofuata, kama kawaida akakaa mbele ya televisheni yake, alitaka kuona kile alichoambiwa kikitokea. Akiwa hapo, huku akiangalia CNN ndipo akakutana na habari ambayo alikuwa akiisubiri kwa hamu kubwa.
Maiti ya mwanaume mmoja, Andrea ilikutwa ufukweni ikiwa imetupwa huku imechomwa visu mara kadhaa tumboni na shingoni mwake.
Maggie alipoiona habari hiyo, haraka sana akampigia simu Joker na kumshukuru, hakuishia hapo, kwa kuwa kazi yake ilifanyika kikamilifu, akamtumia kiasi cha dola elfu kumi kama shukrani kwa kulifanya jambo hilo kwa umakini na kwa haraka kama alivyotaka.
“Usijali! Siku yoyote ukitaka tukufanyie kazi kama hizi, tuambie, hata kama ni nje ya nchi, tutasafiri,” alisikika Joker huku kwa jinsi sauti yake ilivyokuwa ilikuwa ni rahisi kuigundua furaha aliyokuwanayo moyoni mwake.
“Haina shida!” aliitikia Maggie na kukata simu.
.
.
Je, nini kitaendelea?