Simulizi toka mahabusu na Samson Mwigamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simulizi toka mahabusu na Samson Mwigamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, Dec 16, 2011.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  "Makamanda nimetoka gereza la Keko jana Alhamisi Desemba 15, 2011 kwa dhamana ya wadhamini wawili waliosaini bond ya shilingi milioni 5 na mdhamini mmoja kuweka rehani hati ya nyumba yake yenye thamani ya shilingi 42 milioni. Kwa sasa naomba tu niseme: "Wameniweka kizuini kwa zaidi ya wiki moja lakini mawazo yangu hawakuyazuia hata kwa dakika moja, wamenilaza kwenye mazingira magumu ya mateso lakini ubongo wangu hawakuugusa, wamedhoofisha mwili wangu kwa kiasi fulani lakini roho yangu ya ujasiri imeimarika maradufu" Samson Mwigamba, Desemba 16, 2011."

  " Keko nilipokelewa kishujaa sana. Bahati nzuri niliingia na kombat kama ya kamanda wa anga. JIna langu kule lilikuwa "mwanaharakati". Nilipewa heshima kubwa na naweza kuwahakikishia kwamba nilikula ugali wa magereza siku mbili kwa maana ya siku ya Jumatano nikiwa rumande ya kituo kikuu cha polisi Dar na Alhamisi nilipoingia kwa mara ya kwanza gereza la Keko. Na siku hiyo ndo nililala 'mchongoma'. Kuanzia kesho yake Ijumaa ndo makamanda wengi zaidi wakagundua kwamba niko mle. KLewanza ambaye sitamsahau ni rafiki yake Nanyaro ambaye walifanya na Nanyaro kazi pale Leopard tours anaitwa Wilson William ambaye amekaa ndani ya gereza hilo akiwa mahabusu tangu mwaka 2008 hadi leo na nimemwacha na kesi haijaanza kusikilizwa. Yeye ndiye alinifanyia mpango kwa kijana ambaye ni kiongozi wa cell moja na ambaye alikuwa akigombea udiwani huko Ukonga wenzake wa CCM walipoona atashinda wakampa kesi ya wizi wa kutumia silaha. Yuko humo tokea Julai mwaka jana na kesi haijaanza kusikilizwa. Huyo kijana akanipangia mahali pa kulala kwa unafuu kidogo ambapo alinipa kigodoro changu peke yangu cha kama futi mbili hivi. Kuanzia hiyo Ijumaa nilikuwa nikiitwa na makundi mbalimbali kula kwao tokea chai hadi lunch ambapo tulikuwa tunakula wali wanaoletewa na ndugu zao. Ingawa gerezani ratiba ni kula mara moja kwa siku kwenye saa 9 mchana na uchi kiduchu asubuhi saa moja, lakini mimi nilikuwa nakula milo mitatu. Maana walikuwa wakitunza chakula na usiku tukiwa ndani ya cell wananiita nakula nao. Mengi zaidi nitayasimulia kupitia makala zangu. Msikose."

  My TAKE:
  Najua yupo humu mzee wa CHADEMA Ukonga, Embu fuatilieni hii kitu huyu mtu anaonekana kuwa potential candidate huko ukonga!
   
 2. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Pole sana SAM.
   
 3. PATOXIC

  PATOXIC Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Pamoja sn sam wewe hutishwi ukitishwa ukaogopa utakuwa msaliti tunasubiri siku ifike ili tuoneshe kuwa kumbe sio wewe peke yako tuko wengi. na wakidhubutu kukufifisha waambie wataibuka wengine kwa maelfu.
   
 4. M

  Masscom Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  pole sn mdau. km ulivyosema watakudhoofisha mwili lakin nia na ushujaa utakuwa pale pale. wajasiri km wewe wachache sn
   
 5. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,313
  Trophy Points: 280
  Unakomaa sasa!! Wamekujenga kwa gharama zao wenyewe.Holaaaaaaaaaaaaa
   
 6. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndo gharama za uanaharakati. Aluta continua
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Honmgera saaaaaaana shujaa kaza buti muda wa ukombozi umefika mwanaharakati
   
 8. R

  Rugemeleza Verified User

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pole sana na mapambano yanaendelea
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hongera sana Kamanda! Harakati kila mahali
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Bado mpaka sasa sijaelewa mfumo wa sheria wa Tanzania ukoje! labda wenye ufahamu naomba mnijulishe, hivi kwa kesi hii ya Mwigamba haikutosha Mahakama kumuambia ajidhamini mwenyewe kwa sababu ni mtu anaejulikana kwenye jamii na ni kiongozi wa chama cha siasa?
  Hivi ni fasheni kwenda kujaza watu magerezani bila sababu za msingi? au kuna mfumo wa wIzi ambao sisi hatujaugunduwa mpaka leo hii huenda serikalini bajeti ya mfungwa/mahabusu mmoja kwa siku ni shilling10,000=?
  Maana mimi hainiingi akilinii, sidhani kama kila kesi ni lazima udhaminiwe na watu.
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Vipi hawajakufanyia ule mchezo wao!..
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [FONT=&amp]Prison inmates are no lesser persons and deserve access to dignified lives, access to decent accommodation, rehabilitation, education, skills, spiritual and physical nourishment to prepare them for re-integration in society, Sijui ni kwa nini huu mfumo wetu wa kimagereza hauotoi haki kwa kwa wafungwa wetu. Wakati umefika kwa wanaharakati kutumia fursa wanayoipata kuingia gerezani, kuwaamsha wafungwa juu ya haki zao, kwani kifungo pekee hakiziki haki zako zote na UTU wako[/FONT][FONT=&amp]. At the end of the day wafungwa wenyewe wataanza kupropose radical changes that could transform the face of correctional facilities kwa kupitia TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA.[/FONT]

  [FONT=&amp]Our Government should recognize that prisoners do have certain rights, althought they do have fewer rights than free citizens because the restriction of some of their rights is necessary to maintain security in prisons. [/FONT][FONT=&amp]Even The 1977 constitution of United Republic of Tanzania, guarantees prisoners these rights despite their conviction and sentence to imprisonment.

  Mbali na hayo pole mkuu kwa misukosuko uliyopitia, na hongera kwa kumaliza vitisho (jela) wanavyotuwekea
  [/FONT]
   
 13. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Pole mkuu lakini pamoja na hayo yote bado makala yako itabaki kuwa kumbukumbu isiyofutika, tunakutakia kila la heri
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Wewe kama umezoea kutiwa vijitii vya nyuma usidhani hii thread kuna wapuuzi wenzako, navalue kutofautiana lakini coment za kishoga hazikubaliki hapa, Tafuta forum ya mashoga wenzako upeleke huu upuuzi wako, hapa waache Great Thinkers wajadili issues.
  Mijitu mingine akili zao ni shake well before use!!
   
 15. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,810
  Trophy Points: 280
  mlango mmoja ukifungwa, saba zaidi inafunguliwa.
  Tanzania na demakrasia tunayoitaka.
   
 16. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Pole na maswaibu. Ila angalia usihadithie mengi ya humo ndani mpaka yale ambayo mahabusu huyafanya kwa siri ili kurahisisha maisha, usije ukawasababishia jela ikawa chungu kwao..!
   
 17. R CHUGGA

  R CHUGGA Senior Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  usihofu mwanaharakati tupo pamoja nawe katika matatizo hayo,ila kumbuka kuwa uhuru hauji hivi hivi bila vikwazo na hivyo ndivyo vikwazo vyenyewe!mapambano bado yanaendelea.,
   
 18. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pole na yaliyokusibu usife moyo mapambano bado yanaendelea kamanda ipo siku haki itapatikana na haya manyanyaso hayatakuwepo
   
 19. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  acha hasira mkuu utapasuka. Sijakuuliza wewe unaanza kuropoka.
   
 20. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Pole sana kamanda,ila mpaka kieleweke tu.PeeeeeePoweeeeer
   
Loading...