SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

Endeleeni mimi niko napitia comment hapa. Kumbe zenyewe nitamu kama tembele. Ila maina mkaidi kweli unatumwa na mwenyekiti unamgomea.
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA THEMANINI NA TISA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA NANE : Sekunde chache mbele akasikia ngurumo ya gari likisimama nje ya geti, kisha akasikia geti likifunguliwa, kisha gari likaingia ndani na geti kufungwa tena, “mh! nani huyo usiku huu, ina maana anko alitoka?” alijiuliza Talib huku akijaribu kujiinua ili akachungulie, lakini akashindwa kutokana na uchovu wa pombe, akaamua kuachana na mpango wa kuinuka, na kujilaza vizuri, lakini muda huo huo akasikia vishindo vinataembea kuja kwenye ile nyumba yake na kuishia kwenye mlango wake, ikifuatiwa na mlango kugongwa hodi…………. ENDELEA………..
Hapo Tarib akajuwa lazima tukio limesha fanyika sasa anakuja kujulishwa au kuuliza jambo kuhusu tukio hilo, hivyo alichofanya ni kujikausha kama vile hajasikia hodi ile licha ya mgongaji ambae ni bwana Mahamud kugonga mara kadhaa huku akiita, lakini bado Talib aliuchuna na kujifanya amelala fofofo pale juu ya kochi, “mh! huyu atakuwepo humu ndani kweli,” Talib akasikia mgongaji ambae ni mjomba wake akiuliza huku akijaribu kunyonga kitasa, hapo Talib akajuwa kuwa hakuwa na ujanja zaidi ya kuamka ili akafungue mlango maana lazima angetiliwa mashaka kuhusu tukio ambalo mpaka sasa hakuwa anajuwa kama limefanyika na mafanikio yapoje.
Naam ilikuwa ni bahati ya Talib, maana wakati anaingia hakukumbuka kuufunga ule mlango, ile bwana Mahamud kujaribu tu kitasa na mlango ukafunguka akaingia ndani na kukutana na harufu nzito ya sigara, akatazama juu ya kochi na kumuona Talib amelala hajitambui, “dah! afadhari kumbe umelala, mana nilijuwa wamesha kushambulia hawa washenzi” alisema Mahamud huku ana toka mule ndani ambako alishindwa kukaa muda mrefu kutokana na harufu nzito ya moshi wa sigara, akaondoka zake kulekea nyumba kubwa pasipo kujuwa kuwa Talib alikuwa ana msikilizia tu! “lakini huyu mtu kumbe ni kweli bado anavuta haya madudu yake, nilidhani ange kuwa msaada katika familia yangu na yake huko kijijini” aliwaza Mahamud, huku anaendelea kutembea, “lakini sio mbaya, yupo Higgno ni kijana mwema na ni msaada tosha kabisa” aliendela kuwaza Mahamud, ambae alimkuta mke wake anamsubiri sebuleni.
Talib, baada ya kutoka mjomba wake, alifumbua macho huku anatabasamu, lilikuwa ni tabasamu la matumaini na ushindi, akijuwa kuwa tayari watu wake wamesha fanikisha mpango mzima, hakika alitamani atoke usiku ule ule kwenda kugawana fedha, ambazo aliamini yeye ndie mwenye mgao mkubwa, na ndio mwanzo wa kuishi maisha ya kifahari, “nitawachek kesho mapema sana” alijisemea Talib huku akijigeuza ubavu wa pili na kuendelea kuuchapa usingizi.*******
Yap!, baada ya kufanikiwa kuwa kimbia polisi na Higgno, huku akipita mbele ya gari la kina Soraya, Idd alikimbia mpaka nyumbani kwao na kuingia ndani, baada ya kufunguliwa mlango na mama yake akaenda kulala kimya kimya, akiugulia maumivu ya kutolewa jino kwa ngumi, alishindwa kueleza gari ameliacha wapi, huku wazazi wake wakijuwa kuwa ameliegesha nje ya nyumba yao, Idd alijilaza kitandani huku akiwaza ataikwepaje ile kesi, “au nimuambie baba kuwa gari ameazima Talib” aliwaza Idd, ambae kiukweli hakuwa na uwezo wa kukimbia kwenda popote, kwasababu hakuwa hata na senti moja, maana hata zile elfu orobain alizopewa na baba yake alisha zimaliza kwenye pombe, “ninge kuwa hata na shilingi elfu kumi ninge kimbilia gado” aliwaza Idd, ambae usingizi ulimgomea kabisa, “au niseme kuna watu waliomba lift walisema wanaenda kwa Talib, ndio nikawaleta pale na wakati nataka kuondoka nikashangaa tunavamiwa na yule mpuuzi” aliwaza Idd, ambae kila wazo alilolipata aliona kuwa halimfai, "maana wataniuliza niliwabebaje watu nisio wajuwa”.
Idd aliwaza na kuwazuwa mpaka alipo pata majibu mawili, “hapa ni kuwa kataa hawa wajinga, nitasema kuwa nilikuwa napita zangu ndio nikawaona watu pale kwa mzee Mahamud, niliposimama kuwauliza wana fuata nini pale tena usiku ndio nikashangaa tuna vamiwa na kuanza kupigwa” hilo ndilo wazo la kwanza, na la pilli ni kwamba, “yeye alikuwa anakuywa pombe mtini Pub, akaja Talib na rafiki zake wakanywa pombe mpaka usiku, “wale rafiki wa Talib, wakaazima gari wakidai wanakuja nalo mara moja, nilipo wakabidhi hawakurudi mpaka nilipoamua kwenda nyumbani” ilo ndilo jibu la pili alilo lipata Idd, akiamini moja kati yake litamtoa kwenye kesi ile.
Lakini kwa upande mwingine Idd alikuwa anajaribu kuamini kuwa wale walioingia ndani wanaweza kuwa walifanikiwa kuiba fedha, hivyo akimpata Talib mapema anaweza kupata mgao wake na kuondoka zake akimuachia baba yake msala wa gari lake kukutwa eneo la tukio.*******
Naam, usiku wa leo ulikuwa ni usiku wa kipekee kwa familia tatu, yaani ya bwana Mahamud, ambao walijivunia kwa kupata kijana ambae amekuwa msaada mkubwa sana katika familia yao, na kuwasaidia kuokoa mamilioni ya fedha, na pia kuokoa uhai wa bwana Mahamud kwa kitendo cha kumuwahi yule jamaa aliekuwa anataka kuiokota bunduki, ambayo mwisho wake ungekuwa ni kumtwanga nayo yeye mwenyewe.
Kilicho wafurahisha zaidi ni kuwa kijana huyo ndie mkwe wao mtarajiwa, “lakini mke wangu hebu tujiulize wale jamaa funguo wameitoa wapi, na wamepajuwaje pale ukutani” aliuliza Mahamud kwa sauti iliyojaa mashaka makubwa, “lazima tujiulize pia Soraya alijuwaje kuwa kuna tukio kama hili, halafu kumbuka siku ile funguo ilipotea mara tu baada ya Soraya kuondoka” alisema mama Soraya kwa sauti fulani ambayo Mahamud hakuipenda, “kama uliwahi kuwaza upuuzi juu ya Soraya basi ni huo, kwanza wale wezi wamezijuwa mpaka namba za siri za lile kabati, namba ambazo Soraya hazijuwi kabisa, halafu swala la kupotea funguo sio kwamba ilipotea muda ule, sema tuligundua muda ule” alisema Mahamud akionyesha wazi kuto kupendezwa na kauli ya mke wake, “ni sawa mume wangu naomba unisamehe, japo sikuwa na maana mbaya, ila inabidi tukae na Soraya ili atuambie alijuwaje kama kuna mpango wa uvamizi” alisema mama Soraya, “ni kweli inabidi tuongee nae, maana Talib yeye hajuwi lolote, nimemkuta amelala fofofo ndani mwake, tena amesahau hata kufunga mlango” alisema Mahamud.*******
Familia ya bwana Frank nayo sikuile hawakuweza kupata usingizi, walikesha wakiongelea swala la Higgno kuopoa mschana mrembo na mzuri Soraya, ambae ni mtoto wa tajiri mkubwa sana, pia waliongelea kuhusu bahati iliyowaangukia ya kupata gari huku wakiahidiwa kujengewa nyumba nyingine na kuongezewa biashara, “ila hili swala la dini ndio limekaa vibaya” alisema mzee Frank, “yaani hata mimi nimeona hapo ndipo pagumu, bora wangekuwa ni wa Swahili wenzetu tunge washawishi binti yao abadili dini, lakini ni waarabu sijui unaanzia wapi” alisema mama Higgno, “lakini mke wangu kwani tatizo lipo wapi, mwenye kuyatafuta ndie mwenye kuyamaliza, cha msingi tuyapokee maamuzi yake, kikubwa ni kwamba dini zote zinafahamika na zina muabudu mungu mmoja” alisema mzee Frank na mama Higgno akaunga mkono, “ni kweli kabisa, istoshe yeye ni mkubwa sasa, muda wowote anaenda kuwa na familia yake, lazima tumuachie awe na maamuzi yake” alisema mama Higgno, nao wakendelea kuongea hili na lile huku wakikumbuka matukio kadhaa ya kimapenzi yaliyo mkuta kijana wao hasa kuhusu Hilda na yule mschana Joan, walicheka sana na kuambizana kuwa, “kweli kila jambo lina sababu zake, hebu ona alivyompata mschana mzuri” alisema mama Higgy, ambae alikuwa anaona harufu ya kuwa tajiri ikiwanukia kwa nguvu na kasi ya ajabu.*******
Upande wa Higgno na Soraya ilikuwa ni Hatari zaidi, maana ile kufika tu walioga na kuingia ndani kulala, ungesema Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana basi wangepitiwa na usingizi haraka, lakini haikuwa hivyo, kila mmoja kiungo cha uzazi kilimtamani mwenzie, hata walipoamua kupeana dudu baada ya muda mfupi walitamaniana tena, halafu zaidi ni kwamba leo walikuwa wamezidisha baadhi ya mitindo na vijiutundu vya kupeana utamu, vijiutundu vilivyo zidisha hamu ya kuendelea kupeana, jogoo wa kwanza alipowika lilimkutia Soraya akiwa juu ya Higgno anakuna nazi, muda waliopitiwa na usingizi hakuna aliekumbuka ilikuwa ni saa ngapi, ila walishtuka saa tatu asubuhi, ni baada ya simu ya Soraya kuita na alipoitazama mpigaji alikuwa ni Laylah, ambae alimueleza Soraya kuwa yeye baada ya kuona wamechelewa kumpitia akaamua kwenda mwenyewe nyumbani kwa kina Soraya, ambako alichukuwa gari la mzee Frank na kuelekea Luhila kwaajili ya kuwafundisha, hivyo wakapanga kuwa Soraya na Higgno waende Luhila kwa kina Higgno halafu ataondoka pamoja kwenda kwakina Soraya.*******
Naam Saa nne kasoro ndio mida ambayo Talib aliamka akiwa na akili yake timamu, ni baada ya pombe kuisha kichwani mwake, sasa ndio alikumbuka ule mpango wake wa wizi wa fedha za mjomba wake, alichungulia upande geti akamuona mtu mwingine kabisa, ambae sie babu Ndolite, hiyo ilikuwa ni dalili ya kwanza ya kuwa tukio la jana lilifanyika, “yes mambo ndio hayo sasa” alijisemea Talib huku anachukuwa simu yake na kuitafuta namba ya Zido, alipoipata na kutaka kuipiga akakumbuka kuwa simu ile ilishapoteaga, hivyo akatafuta namba ya Vitus na kupiga, akashangaa kusikia kuwa simu ilikuwa haipatikani, “dah! wasije kuwa wamenizimia simu makusudi ili wanizime mkwanja wangu, maana Idd anajifanya mjanja mjanja sana” alisema Talib, huku anasogea dirisha la upande wa nyumba kubwa na kuchungulia, akaliona gari la mjomba wake likiwa pale nje, ilionyesga kuwa hakuwa ameenda ofisini kwake, hivyo ni dalili ya pili ya kuwa jana tukio lilifanyika, “hawawezi kunizidi akili hawa, tena kabla sijaondoka nitahakikisha naenda nyumba kubwa kuchunguza kama tukio lilifanyika na wameondoka na kiasi gani” aliwaza Talib huku ana anza kusokota bangi yake ambayo angeivuta kabla hajaingia bafuni kuoga.*********
Hilda aliamshwa na shangazi yake, ambae alikuwa anahitaji kuwasha jiko kwaajili ya kumipikia mgonjwa, yaani kaka yake mzee Komba, ambae ndie baba yake Hilda, “nipishe we Tembele mi nataka niwashe moto” alisema shangazi huku anatupa kuni chini, karibu kabisa na alipolala Hilda, ambae aliinuka kwa kukurupuka, hivyo ndivyo Hilda alivyo amshwa na kukimbilia ndani huku akidondosha nguo yake ya ndani yenye mchanganyiko wa uchafu, aliyo kuwa ameifungia kwenye nguo yake baada ya kuitumia kama kitambaa cha kujifutia walipomaliza kufanya yao jana usiku pale kichani, “we mpuuzi unataka huu uchafu wako auone nani? Hebu njoo uchukuwe” alisema shangazi na Hilda akarudi mbio mbio na kuokota nguo yake, “sijui walikufanya nini masikini, maana huo uchafu sio wa kwenye kum*.. si mav.. hayo?” alisema shangazi kwa sauti ya masikitiko, lakini Hilda hakujibu lolote zaidi ya kukimbilia ndani, ambako hakukaa muda mrefu akatoka na kuelekea bafuni kuoga, na alipo toka huko alivaa nguo zake na kutoka pale nyumbani, akipitia mlango wa nyuma na kutokomea mtaani akijuwa fika kuwa pale nyumbani ange simangwa kutwa nzima na shangazi yake.
Lakini kule mtaani mambo yalikuwa mabaya kwake, kwasababu ile anatokea tu barabara kubwa, akashangaa kuona watu kadhaa wakiwa wamesimama pembezoni mwa barabara, ungesema wanasubiri mgeni fulani wa kitaifa ambae angepita muda huo, na yeye akiwa amekosa pa kwenda muda ule, pasipo kujuwa mama yake yupo wapi akaamua kusimama pale barabarani ili aone kile wenzake wanacho subiri kukiona.
Naam dakika chache baadae Hilda akayaona magari mawili yanakuja taratibu, ikionyesha wazi kama sio kuna mgeni maalumu alikuwa ndani yake basi kuna watu walikuwa wanajifundisha kuendesha magari yale, ni kweli hata magari yale yalipo wafikia Hilda aliweza kuona kuna watu walikuwa wanajifundisha kuendesha magari yale, Hilda alijikuta akitoa macho kwa mshangao, akiwatazama watu wanao jifundisha kuendesha magari yale, alikuwa ni mama na baba Higgno, huku walimu wao wakiwa ni waschana warembo kweli kweli, kila mmoja na mwanafunzi wake ndani ya gari lake.
Ukweli ni kama mwili wa Hilda ulikuwa umeshikwa na ganzi, alisimama kwa dakika kadhaa akiendelea kushangaa magari yale yakiyoyoma taratibu kuelekea upande wa nyumbani kwa kina Higgno, na hata baada ya magari yale kutoweka, Hilda alitumia dakika kadhaa kusimama pale, akiwa na watu wengine huku akikumbuka matukio kadhaa ya siku na miaka mingi iliyopita aliyofanyiwa na Higgno, alikumbuka upendo mkubwa alioonyeshwa na Higgno, ambae alihakikisha yeye Hilda hakosi vitu alivyo hitaji na kumfanya na yeye aonekane kama mtoto wa mtu mwenye uwezo pale kijijini, hata kule shuleni alikokuwa anasoma kabla ya kudanganywa na Talib,.
Hilda alitafuta baya alilofanyiwa na Higgno, pengine kinge kuwa ndio chanzo cha kumchukia na kuyapuuzia yale anayo yaona kwa kina Higgno, lakini hakupata hata moja la bahati mbaya, zaidi ya yeye kuwa chanzo cha ukorofi na vurugu kwa Higgno, “mh! ningekuwa nipo na Higgno na mimi ninge fundishwa kuendesha gari” aliwaza Hilda huku anaanza kutembea kuelekea upande wa barabara kuu iendayo kusini mwa tanzania, huku akikumbuka jinsi alivyopewa matunzo na Higgno, wakati anaishi kwake, tena alimhudumia yeye na mwanae, kitu ambacho baba wa mtoto yaani Talib hakuwahi kufanya, “ngoja nikamuombe msamaha, nadhani atanisameheme tu” aliwaza Hilda huku akiendelea kuwaza na kupanga mambo yake.
Naam baada ya kutembea kwa mwendo fulani, mrefu kidogo, akiwa anakaribia kuingia madukani, yaani kule barabarani, akasikia ngurumo ya magari ikija kutoka nyuma yake, na alipogeuka kuyatazama safari hii aligundua kuwa yalikuwa yanaendeshwa na watu wanao juwa kuendesha, maana yalikuwa speed, hivyo akapisha pembeni na kutazama na alichokiona ndani ya gari la nyuma wakati linampita kilimfanya ashindwe kuamini macho yake, maana aliweza kumuona Higgno akiwa amekaa pembeni ya dereva, ambae ni mschana mrembo wa kiarabu mmoja wa wale walimu, huku wakiongea na kucheka kwa furaha, ikionyesha wazi kuwa wawili wale ni wapenzi, hakika moyo ulimlipuka vibaya sana Hilda, ambae alikosa hata nguvu ya kusimama na kujikuta anakaa chini, huku watu wakimshangaa kwa tukio lile, walioijuwa historia yao, hawakumshangaa.*******
Naam sasa turudi kwa mzee Mahamud, ambako Mahamud na mke wake walikuwa sebuleni wanajiandaa kwa mipango mingine na mzee Frank, huku wakisubiri jibu la kuhusu dini, ambayo wawili hawa yaani Soraya na Higgno wataifuata, na ndio wakati Talib alipoingia sebuleni pale, “shikamoo anko” alisalimia Talib huku anapitiliza kwenda kwenye ukumbi wa chakula, “marahaba Talib, naona jana ulilala fofofo, hata ukusikia mambo yaliyotokea usiku” alisema Mahamud, ikiwa ndiyo simulizi ambayo Talib alikuwa anaihitaji, “kimetokea nini tena anko?” aliuliza Talib akijifanya kushtuka kweli kweli, “bangi na pombe hizo, yaani kama tunge uwawa humu ndani wewe usinge juwa chochote mpaka polisi wanakuja wewe umelala tu, hivi bangi utaacha lini wewe” alisema mama Soraya kwa sauti ya ukali, “tatizo shangazi unamsikiliza Soraya, mambo hayo nimeacha toka mwaka jana” alisema Talib kwa sauti iliyopooza, huku akitafakari neno polisi walikuja, “we haya bwana, tutaona mwisho wa hizo bangi zako” alisema mama Soraya, na hapo Mahamud akamsimulia Talib kilichotokea usiku na jinsi Higgno alivyo waokoa.
Baada ya simulizi ndefu ambayo ilimpa ganzi Talib na kuzidi kumchukia Higgno na mwenzie Soraya, “lakini anko, wakina Higgno jana si walikuja hapa nyumbani?” aliuliza Talib kwa sauti tulivu, “ndio walikuja tena ulikosa mambo” alijibu Mahamud, “si unakumbuka niliwahi kukuambia nini kuhusu Higgno na baba yake?” aliuliza tena Talib, huku shangazi na mjomba wake wakimsikiliza, “kwahiyo unataka kusema nini Talib?” aliuliza shangazi yake, yaani mama Soraya, “we shangazi tatizo lako hupendi kusikiza ninacho mueleza, yaani hata hushtuki kuwa wamekuja wao na funguo imepotea” alisema Talib, na hapo Mahamud na mke wake wakatazamana kwa mshangao, “lakini funguo imepotea juzi sio jana” alisema Mahamud, “juzi?” aliuliza Talib kwa mshangao, huku akitazama chini akitafuta jibu jingine, akamsikia shangazi yake akicheka, “yaani Talib, hivi kwanini unawachukia wakina Higgno kiasi cha kuwasingizia maovu kama hayo?” aliuliza shangazi, kwa sauti ya kusuta, “ni wachukie nini wakati nawafahamu vizuri wale matapeli, we huoni wamekuja wao tu! na usiku wake linatokea tukio kama hili?” aliuliza Talib, na hapo Mahamud na mke wake wakatazamana tena, safari hii sio kwa kumshangaa Talib, ila ikionyesha kuwa imewaingia, na Talib alipogundua hilo akaongezea la kwake, “nilishakuambia kuwa wale ni wazee mishe mishe, na kinacho fuatia hapo ni kukufirisi kila kitu na wakiweza wanakuuwa kabisa” alisema Talib, na hapo ungeweza kuona mshtuko mkubwa usoni kwa Mahamud na mke wake.
Naam ni kweli swala hili liliwashtua vibaya sana, Mahamud na mke wake, na kuanza kujutia kile walicho kifanya kwa haraka haraka bila kuchunguza na kabla hawaja juwa wafanye nini wakasikia ngurumo ya gari nje ya nyumba yao, hapo wakatazamana kwa macho ya mshangao na wasi wasi, maan wao walishajuwa kuwa wakina Soraya wanakuja na wazazi wazi wa Higgno na Higgno mwenyewe….. ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom