SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SABINI NA NANE
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SABINI NA SABA: Naam geti lilifunguliwa na mlinzi baada ya kuwaona waliogonga aka shusha pumzi, “hallow nyie munataka nini kwenye majumba ya watu na mizigo yenu?” aliuliza mlinzi akijitahidi kutoa sauti ya vitisho, akionyesha kuwa anaamini wanafamilia hawa hawakustahili kuingia pale, akichukulia hata uvaaji wao ulikuwa tofauti na wale wenyeji wa mule ndani, yaani magauni marefu na shungi kwa kina mama, japo wanaume sio tofauti sana, wakati mama Higgno alitupia gauni lake la kitenge na kilemba cha kikongo………. ENDELEA……..
Wote watatu wakatazamana kwa mshangao, huku mzee Frank akimtathimini mzee mwenzie ambae amepewa dhamana ya ulinzi wa nyumba hii kubwa ya kifahari yenye mali nyingi sana, “samahani mzee mwenzangu, kwanza huwa tuna anza na salamu, kisha tunaulizana nia na dhumuni” alisema mzee Frank kwa sauti ya upole na iliyojaa busara, huku mkewe na mwanae Higgno wakitazama ndani ya uwigo ule, ambako sasa waliweza kuona watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni wanawake waliokuwa wanaendelea na pilika zao za upishi na nyingine kadha wa kadha, “salamu za nini wakati nyie wenyewe mumeshindwa kujielewa, hebu jiangalieni kwanza, halafu fananisheni na watu waliokuwepo ndani, kisha mujiulize nyie mumekuja hapa kama nani” alisema yule mlinzi kwa sauti ambayo ilizidiwa na umri wake, yaani aliongea kama kijana muhuni, wote watatu wakajitazama nguo zao, kisha kila mmoja akamtazama mwenzie na kujiona walikuwa sawa kabisa, kisha wakamtazama mzee yule alievalia sale za askari wa jeshi la akiba, yaani mgambo mwenye kushikilia rungu kubwa mkononi mwake, “samahani bwana mgambo, sisi ni wagen……?” aliongea mama Higgno, akitaka kumuelekeza babu juu ya ujio wao, lakini babu akamdaka juu kwa juu, “mama umeanza dharau, nani mgambo sasa?” aliuliza babu kwa hasira kari akionekana kuwa ameona kama vile amedharauliwa kwa kuitwa mgambo.
Mpaka hapo mzee Frank na mke wake pamoja na kijana wao, wakaona kuwa mzee huyu hakuwa na dalili ya kuwaelewa, pia walishaanza kukereka na maneno ya mlinzi yule, hapo ni busara tu! ndizo zilizo tumika kuweza kuwafanya mpaka sasa wapo pale mlangoni, vinginevyo wange kuwa wamesha ondoka zao, “samahani kwa hilo mwanajeshi, tuna omba tujieleze sisi ni wakina nani, na shida yetu ni nini?” alisema mzee Frank kwa sauti ya busara ya kulazimisha, maana hata yeye hakupendezwa na dharau za mlinzi huyu, “hakuna cha kujieleza bwana, humu ndani leo haingii mtu wa ovyo ovyo, kuna ugeni maalumu unatarajiwa, tena mutoke haraka maana karibu magari ya wageni yataanza kuingia” alisema mlinzi na kuanza kufunga gate akiwafungia wakina Higgno kwa nje, “mh! jamani, inawezekana kweli leo kuna watu maalumu wanakuja hapa, ndio maana kama kuna sherehe” alisema mama Higgno wakiwa wamesimama nje ya geti hili la nyumba ya Mahamud, “hapana mama Higgno, basi asinge niambia tuje leo” alisema bwana Frank, ambae tayari hasira zilisha mkaba, “au hukumsikiliza vizuri, pengine hakukuambia uje leo” alisema Higgno, ambae hakuonyesha dalili zozote za kukasirika, “mh! jamani, kwani kesho ndio lini?” aliuliza bwana Frank, ambae alichoshwa na maswali ya familia yake, ambayo yalizidi kumpandisha hasira, “kama alikuambia kesho basi ndio kesho, twendeni, nyumbani kesho mutakuja wenyewe” alisema mama Higgno, ambae alionekana kutopendezewa na kile kilicho watokea, safari hii mzee Frank na Higgno wakacheka kidogo, “sio kesho ya leo, hii ni kesho ya jana, na kesho ya jana ni leo, hivi munashindwa kuelewa nyie?” aliuliza mzee Frank, ambae hakuelewa kwanini yametokea mambo kama yale, “hooo! nimekumbuka kuwa mzungu ametuletea kilongambali” alisema mzee Frank, huku anajipapasa mfukoni na kutoa simu yake kisha akapiga kwa Soraya.
Naam simu haikuita sana ikapokelewa, “asalaam alaykum” sauti tulivu nyororo iliyojaa nidhamu na heshima ilipenya masikioni kwa mzee Frank, kiasi cha kumfanya mzee huyu atoe simu sikioni na kuitazama kwanza kama vile alitumia simu ambayo sio ya kwake, alipohakikisha kuwa ya kwake akaiweka tena sikioni, “waalaykum salaam, ni mimi mzee Frank, nimesha kuja kama ulivyo niambia tupo hapa nje” aliongea zee Frank, huku akijitambulisha, akidhania kuwa pengine Soraya hakuwa amemtambua, ndio maana aliongea kwa heshima kubwa na unyenyekevu, “hooo! kwahiyo mupo nje au ndani?” aliuliza Soraya kwa sauti ya unyenyekevu, lakini iliyojawa na furaha, “tupo nje ya geti, naona mlinzi ameshindwa kutuelewa sijui huku mueleza kama tutakuja” alisema mzee Frank, ambae sasa hasira zilishaanza kumpungua, “sawa! nyie subirini hapo hapo wanakuja kuwa pokea” alisema Soraya na kukata simu, hapo Frank akawa geukia wakina Higgno huku anatabasamu, “haya sasa kesho imeshafika tunakuja kupokelewa” alisema mzee Frank, huku akiwa anamsimananga kimafumbo mke wake, ambae hapo mwanzo alitoa neno la kashfa kwake kuwa kesho bado haijafika.******
Tuende kidogo Luhuila, ambako baada ya Nurse kumkabidhi mgonjwa yaani mzee Komba kwa Nurse wa zahanati ya Luhuila, akaondoka zake, na kumuachia kazi nurse yule ambae hata asubuhi alienda kwa mzee Komba kuijulisha familia yake kuwa mgonjwa wao ameshaletwa pale zahanati, wakikubaliana kuwa waje pale mida ya saa sita mchana, lakini sasa lilishapita lisaa lizima toka mgonjwa afike pale zahanati na zilisha pita dakika thelathini toka itimie saa sita, hivyo nurse yule akaamua kwenda tena kuwa julisha ili waweze kupeleka chakula kwa mgonjwa.
Dakika kumi baadae Nurse alikuwa ameshafika nyumbani kwa mzee Komba ambako saa hii alimkuta Hilda peke yake, tayari mama yake alipotelea mtaani toka ameenda kupeleka ujumbe kwa Ngonyani ili apelekewe wifi yake, yaani dada yake Komba na wakati anarudi nyumbani ndipo alipokutana na Njogopa anatoka kugema ulanzi, hivyo wakashauriana watafute sehemu wakae ili wanywe ulanzi.
Ni kweli walitafuta sehemu nzuri kwenye kichaka fulani na kuanza kunywa ulanzi wao taratibu, mama Hilda japo hakuwa na uwezo wa kutaa kupewa dudu kwa malipo ya ulanzi, lakini mpaka muda huo hakuwa anajuwa kuwa mzee Njogopa ambae ni rafiki mkubwa wa Komba, ambae alikuwa na mke na watoto wanne, na alikuwa anajuwa fika kuwa rafiki yake huyu alikuwa anaumwa, moyoni mwake alishapanga kuonja kitumbua cha mke wa rafiki yake, tena pale pale porini.
Nurse akiwa nyumbani kwa mzee Komba na Hilda alimueleza Hilda lengo la kuja kwake pale nyumbani likiwa ni kuwajulisha kuwa wanahitajika kupeleka chakula kwa mgonjwa, maana tayari alishafika pale zahanati, “basi naandaa chakula nakuja sasa hivi” alisema Hilda ambae moyoni mwake alikuwa anajuwa fika kuwa hakuwa na chochote cha kupika, nyumba ilijaa harufu ya njaa tupu, “sawa msichelewe maana mgonjwa anatakiwa ale ili anywe dawa” alisisitiza nurse, kabla hajaondoka na kumuacha Hilda akimsindikiza kwa macho mpaka alipotoweka, “sasa mimi chakula nitakitoa wapi, mngojeni dada yake aje ampikie” alisema Hilda akimaliza na msonyo mkali huku akiingia ndani kwenda kujiandaa kuelekea kwenye ulanzi ambao alikuwa ameumissi kwa siku mbili nzima.*******
Naam mida hii ndiyo mida ambayo Kijana Idd Mahadhi Salum alichukuwa gari la baba yake na kuelekea mtaani, safari yake akiipanga kuhitimisha mtini pub,iliyopo mtaa wa pili toka kwa kina Soraya, sehemu ambayo kwa kijana au mpenda starehe na totoz wa hapa songea lazima angependa kwenda, Idd akiwa na elfu alobaini yake mfukoni aliendesha gari taratibu, akikatiza mitaa ya songea mjini kueleka kati kati ya mji, huku kichwani mwake akiwaza namna ambayo ata pata fedha ya kuondoka hapa mjini, kabla Mahamud hajasanuka kuwa yeye na baba yake ndio waliosambaza sms ya kashfa dhidi yake, kwa maana hiyo Idd alikuwa ana muachia baba yake msala.
Naam sasa basi wakati Idd anakatiza eneo la kina Soraya ili akapite barabara ya nyuma ili akaingie na kulificha gari upande wa uwani wa mtini pub, mara akaanza kusikia sauti kubwa za qaswida toka kwenye nyumba ya mzee Mahamud, ambae sasa alikuwa anamuogopa kama ukoma, sambamba na harufu nzuri za vyakula, “mh! wananikumbusha ile jumapili, sijui leo kuna nini, au ndio huyo mchumba wa soraya analeta barua” aliwaza Idd kwa machungu makubwa huku anakatiza kwenye eneo la nyumba hii kubwa iliyo zungukwa na ukuta mkubwa.
Na wakati ana karibia usawa wa geti, Idd akawaona watu watatu, yaani mama mmoja mtu mzima, na wanaume wawili mmoja akiwa ni kijana na mwingine ni mtu mzima, ambae alimkumbuka kuwa ni yule aliemsukuma siku ile na gari akasaidiwa na Soraya, ambae sasa alimuona anaongea na simu, (ni wakati ule mzee Frank anaongea na Soraya, Idd akapunguza mwendo na kufanikiwa kuyanasa maongezi yale, ambayo aliyaona kuwa haya kuwa na msingi kwake, lakini baada ya kufika mbele kidogo akajikuta anavutika kufuatilia kulikuwa na jambo gani pale kwa Mahamud, hivyo akatafuta sehemu ya kuegesha gari na kusimama, halafu akalizima na kushuka toka kwenye gari akatafuta grocer moja ya jirani akanunua pombe kali, ambayo kipindi kile ilikuwa inauzwa mia tisa chupa ndogo, iliyobatizwa jina kuwa kischana au kiimoro kutokana na udogo wake, kisha akarudi kwenye gari lake na kuanza kuinywa huku macho na masiko akiyaelekeza kwenye geti la nyumba ya Mahamud.*****
Mahamud baada kumkaribisha Jamal, akamuomba mke wake waingie chumbani kidogo, ambako alimuuliza kisa cha kunyongea ghafla, “sio siri baba Soraya, yaani natamani hata nikuambie tughairi hili jambo, yaani sijui kwanini moyo wangu umesinyaa ghafla, naona kama siku ya leo sio nzuri” alisema mama Soraya ambae sijui kama alikuwa anakijuwa anacho sema, “wasi wasi wako tu mke wangu, nimekuja na Jamal, ili aweze kuwa tambua hao wageni, si unajuwa yule ni mjanja mjanja, lazima kama ni wezi au matapeli atakuwa anawafahamu” alisema Mahamud na hapo kidogo mama Soraya akatuliza nafsi yake, nao wakatoka kuendela na shughuli zao.
Mzee Mahamud akiwa sebuleni na watu wawili watatu wa kiume wanapata vinywaji na vitafunwa, kama kalimati, kababu na vireja, huku wanaendelea na maongezi ya hapa na pale, mara wakamuona Laylah anakatiza kutoka chumbani kwa Soraya na kuelekea upande wa mlango wa nyuma, ambako kulikuwa na wakina mama wanaendelea na kazi zao, mahamud akaendelea na maongezi na wale wenzie, “sijamuona Talib, au nae anaendelea na maandali ya kumpokea shemeji yake?” aliuliza Jamal, na hapo Mahamud, akawatazama wale wageni wengine akawaona wapo makini kusikiliza jibu, “si unakumbuka ile kazi niliyo kuambia nime mtuma, nadhani atakuwa ameenda huko” alijibu Mahamud bila kufafanua, “lakini boss ni muhimu akiwepo hapa, ili tuweze kuoanisha matukio” alisema Jamal, ambae anamfahamu vyema Talib.
Kwa maneno yale ya Jamal ni kama mahamud alihisi kuwa Jamal anatia shaka kwa Talib, “huyo wala usiwe na wasi wasi nae, maana ndie chanzo cha habari” alisema Mahamud, akimtoa wasi wasi Jamal, “hata kama boss, lakini ujuwe kuwa siku zote ili nyeusi iwe safi lazima nyeupe itiwe tope” alisema Jamal akijichekesha ili kufanya kama anaongea utani, hapo Mahamud akatuliza kichwa kidogo na kuyatafakari maneno ya Jamal, lakini kabla haja ya patia jibu sahihi, mara akatokea mama Soraya, “baba Soraya, tayari wageni wameshafika ndio tunaenda kuwapokea getini, nyie tusubiri hapa hapa tutawaletea wageni wenu” alisema mama Soraya, akimaanisha kuwa, wageni wa kiume watawaleta kule ndani, na mgeni wa kike watakuwa nae wao wenyewe wakina mama, “sawa cha msingi wasisitize wahudumu wachangamke kuhudumia huku ndani” alisisitiza Mahamud.
Baada ya hapo mama Soraya akatoka kuelea nje akiongozana na wakina mama kadhaa kueleka getini wakiimba nyimbo za shangwe, huku mlinzi akiwatazama kwa mshangao maana hakuona dalili ya wageni ambao yeye alikuwa anawawazia kichwani mwake,
Huku wakina Higgno na wazazi wake wakiwa nje ya geti wakisubiri kama Soraya alivyo waambia, mara wakaanza kusikia kelele na shangwe, zina kuja upande wa geti na baada ya shangwe zile kufika getini, upande wa ndani, Frank na familia yake licha ya kuendelea kusikia kelele za shangwe pia wakasikia sauti ya ukali ya mwanamke mtu mzima akimkemea milinzi, “babu unaniuzi, safari hii nitakuchoka, unawezaje kuwazuia wageni wetu, ikiisha hii shughuli utaipata dawa yako” alimaliza kuongea huyo mwanamke ambae walitambua kuwa ni mama mwenye nyumba, kisha likafunguliwa geti kubwa.
Naam mzee Frank na familia yake walishangaa kuona kundi la wakina mama likitoka huku linaimba kwa shangwe, na kwenda kuwapokea jamanda lililo bebwa na mama Higgno, mpokeaji akiwa ni mama mmoja ambae licha ya umama wake lakini bado alikuwa anapendeza, yani wa moto, kwa mzee Frank na mke wake kila walie muona alikuwa ni mgeni kwao, hata yule mama aliewapokea jamanda pia alikuwa ni mgeni kwao, japo walitambua kuwa ni mama mwenye nyumba, kwasababu ni utamaduni wa kupokelewa na mwenyeji, tofauti na Higgno ambae alihisi kuwahi kuiona sura ya mama yule sehemu, lakini hakukumbuka ni wapi alipowahi kumuona, ila hakujali maana kwa watu mashuhuli kama hawa ni kawaida kuwaona.
Naam pia katika mapokezi hayo kuna jambo lilitokea na kuwashangaza wakina Frank, na familia yake, ni tukio la mama yule ambae sisi tuna mfahamu kama mama Soraya kusogea karibu na Higgno na kupiga nusu goti, “mwanangu kuanzia leo wewe na wazazi wako munakaribushwa katika nyumba hii” alisema mama Soraya, na Higgno akaitikia kwa sauti yake tulivu na ya upole, “asante sana mama” hapo zikalipuka shangwe na vigeregere, kisha akainuka na kuwaongoza wageni kuingia ndani, pasipo Higgno kujuwa kuwa hiyo ni moja ya taratibu za rafiki au mchumba wa kiume anapotembelea kwa mara ya kwanza kwa wazazi wa kikeni, hakika tukio hili liliwashangaza sana baba na mama Higgno, wakianza kushangaa wasijuwe kinacho endelea, maana hata walipo mtazama Higgno walimuona na yeye anawatazama kwa mshangao, akionyesha fika kuwa hajui lolote.******
Talib ambae hapo mwanzo hakuweza kuwaona wageni walio zuiliwa kuingia ndani, akaelekea ndani kwake na kujisokotea bangi yake, huku mawazo yake yakiwa ni kuhusu tukio litakalo tokea usiku wa siku ile, tukio ambalo litamfanya auage umasikini, tukio la mamilioni ya fedha, mara akaanza kusikia kelele za shangwe toka kwa kina mama zikitoka ndani kuelekea getini, hapo akiwa na bangi yake mkononi akajivuta dirishani na kuchungulia na kuona kundi la wakina mama likitoka nje na dakika chache baadae akawaona wanaingia ndani wakiwa wameongozana na watu watatu, ambao ni wageni, Talib alipowatazama wale wageni alijikuta anapatwa na mshtuko wa ajabu, “yule mzee si ananifahamu yule” alijisema Talib, ambae alishtuka sana baada ya kumuona mzee Frank, ambae kwa maelezo ya Soraya ni kwamba alishaenda polisi, na endapo angemuona kijana alie toa vitisho dukani kwake angeenda kumtolea taarifa polisi ili akamatwe………… ITAENDELEA
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SABINI NA TISA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SABINI NA NANE: hapo akiwa na bangi yake mkononi akajivuta dirishani na kuchungulia na kuona kundi la wakina mama likitoka nje na dakika chache baadae akawaona wanaingia ndani wakiwa wameongozana na watu watatu, ambao ni wageni, Talib alipowatazama wale wageni alijikuta anapatwa na mshtuko wa ajabu, “yule mzee si ananifahamu yule” alijisema Talib, ambae alishtuka sana baada ya kumuona mzee Frank, ambae kwa maelezo ya Soraya ni kwamba alishaenda polisi, na endapo angemuona kijana alie toa vitisho dukani kwake angeenda kumtolea taarifa polisi ili akamatwe……… ENDELEA……..
Hapo Talib akaona kuwa huu ni msala kwake, hivyo akizubaa atakamatwa kabla hajatekeleza mpango wake, “inabidi nitoke nikazuge kitaa mpaka waondoke ndio nirudi” aliwaza Talib huku anavaa viatu vyake haraka kwaajili ya kuondoka pale nyumbani, hakuwaza kuhusu fedha ya kula wala njaa aliyokuwa nayo muda ule, “Soraya nae yaani ujanja wote ule anakuja kubebwa na mafala kama hawa” aliongea Talib kwa kulalamika na kulaumu, huku akiendelea kuvaa viatu vyake na kuvuta bangi yake.
Wakati huo Mahamud alikuwa sebuleni na watu wawili watatu, mmoja wao akiwa ni mjomba wa Soraya, ambae alishafahamishwa juu ya ugeni ule ,wakiwasubiri wageni ambao waliambiwa kuwa tayari wameshafika pale nyumbani, sasa mahamud akasogeza mdomo wake karibu na sikio la Jamal na kumnong’oneza jambo, “Jamal naamini utakuwa una wafahamu watu hao, naomba uwe makini kuwa soma nakusikiliza majibu yao,mana nitawauliza maswali fulani fulani nawe pia una ruhusiwa kuuli maswali” alisema Mahamud, na wakati huo huo wakasikia sauti tulivu iliyojaa nidhamu ya asili ya mngoni halisi toka upande wa mlangoni, “hodi jamani” huku watu wote wanageuza macho kutazama mlangoni.
Naam Jamal ambae alitazama kwa makini sana, ili kuona kama anaweza kuwa tambua wageni wale walioingia pale sebuleni, aliweza kuwaona watu wawili ambao ni wazi kuwa ni mtu na kijana wake, kwa jinsi walivyo tofautiana kwa umri, na pia ukizingatia tayari alishajuwa kuwa wanao kuja ni baba mama na kijana wao, ukweli kabisa Jamal alitegemea kumuona kijana ambae atakuwa anamfahamu, maana kuwa na Soraya sijambo dogo, lakini ilikuwa tofauti kabisa, alikuwa ni mgeni kabisa machoni mwake.
Hapo Jamal akamtazama mzee Mahamud, ambae pia aliamini kuwa atakuwa anamuona kijana huyu kwa mara ya kwanza, lakini akashangaa kumuona Mahamud akitoa macho kwa mshangao, huku ameachama kwa furaha, “hooooo! kijana umekuja siku nzuri sana, tena wakati muafaka, karibu sana” alisema Mahamud kwa sauti iliyojaa furaha, huku anasimama na wakina jamali wakasimama pia kuwa karibisha wakina Higgno, “asante sana mzee Shikamoo” alisalimia Higgno, huku anapokea mkono wa mzee Mahamud, wakionyesha kufahamiana kwa karibu, “marahaba, karibuni sana” alisema Mahamud huku anamshika mkono mzee Frank, “asante sana” aliitikia mzee Frank, ambae alifurahi kuona kijana wake anafahamiana vizuri na mzee huyu tajiri mkubwa hapa songea na Tanzania nzima pia.
Naam walitumia dakika kadhaa kusalimiana, kisha wakaonyeshwa sehemu za kukaa, nao wakakaa, “karibu kijana, umekuja siku ambayo kiukweli ni nzuri, maana yule binti yangu nilie kueleza jana, anakuja kutuonyesha mchumba wake, kwa hiyo ameshapata mchumba” alisema Mahamud, mwenye kuonekana kuwa na furaha kubwa sana, huku anamtazama Higgno ambae alionyesha kumfahamu na kwamba hakutegemea kumuona mahali hapa, ukweli waliokuwepo mule ndani walishangaa kidogo, maana walidhania kuwa Higgno ndie mchumba mwenyewe wa Soraya aliekuwa anasubiriwa “imekuwa vizuri sana, na pengine tunge kuwa tumeingilia na kuvuruga mipango mingine” alisema Higgno, kwa sauti ya upole, huku anacheka kidogo, hapo Mahamud na mzee Frank wakacheka kidogo, maana walijuwa Higgno alikuwa anamaanisha nini, “ni kweli bwana, tena sijui kama tungeeleweka” alisema mzee Frank, huku anaendelea kucheka.
Naam wakiwa wanaongea kwa furaha, huku wanaendelea kuwasubiri wageni wao pasipo kujuwa kuwa wageni wenyewe ndio hawa waliokuwa nao hapa sebuleni, ambao pia hawakuwa wana jijuwa kuwa wao ndio wageni waliokuwa wanasubiriwa, mara wakaanza kusikia kelele na shwangwe za wakina mama zikihamia ndani, zikifuatiwa na kundi dogo la wanawake kuingia ndani na kukaa kwenye makochi, na kwenye jamvi (carpet) yani zuria la manyoya lililo lala juu ya sakafu ya sebule ya jumba hili la kifahari, ambalo ukiingia lazima utavua viatu kabla ya kuuliza au kuambiwa.
Mke wa Mahamud alienda moja kwa moja, mpaka mume wake na kumnong’oneza jambo, “tunaweza kuanza ili tumalize mapema, watu wale waende makwao” alisema mama Soraya, kisha akaenda kumueleza vivyo hivyo kaka yake ambae ndie msemaji kama ilivyo kawaida, baada ya hapo akaenda kukaa karibu na mama Higgno, ambae kiukweli yeye ndie alikuwa anashangaa kuliko maelezo, maana alikuwa anaona mapicha picha tu!, kwasababu kwa jinsi alivyo pokelewa kule nje na wakina mama na kupewa hongera nyingi nyingi, na kuona dalilizote za kuwa ile sherehe ni kwaajili yao, hivyo akashangazwa sana na jambo lile maana alicho juwa yeye ni kwamba wanafika pale wanapata chakula cha mchana kisha wanaondoka kurudi zao nyumbani, lakini kila alipomtazama mume wake yaani mzee Frank, hakuona dalili yoyote ya kushangaa wala kushikwa na butwaa kama ilivyokuwa kwa Higgno.*******
Naam ndani ya kichaka chini ya mwembe, mita kama ishirini toka barabarani mama Hilda na bwana Njogopa rafiki mkubwa wa mume wake, tayari walisha kunywa makopo kadhaa ya ulanzi, ambao ndio kwanza ulikuwa unatoka mianzini haujatiwa hata maji, tayari pombe ilishapanda kichwani kuharibu akili zao kwa kiasi cha kati, na kubakiwa na akili ya kuanza kupapasana sehemu nyeti huku wakipeana mate.
Naam ni kama walikuwa bichi moja nzuri sana yenye upepo mwanana, maana ilifikia wakati hata wakaacha wazi sehemu zao nyeti ili kila mmoja aweze kuchezea ya mwenzie, wakati mama Hilda akichezea dudu ya Njogopa huku yeye akichezewa kikunde chake na kujisikia raha kweli kweli haikuchukuwa muda akatandika kanga yake chini, “tufanye mara moja halafu tuendelee na pombe”, alishauri mama Hilda huku anapandisha gauni lake mpaka kiunino ukweli hakuvaa chupi, kisha akapiga magoti kubinua kiuno chake kwa juu na kuacha vyombo hewani, hapo Njogopa akakenua meno kwa tabasamu la uchu, na kusogelea nyuma ya mama Hilda, kisha akazamisha dudu ndani na kazi ikaanza, wakapeana dudu kwa raha zote kama wapo chumbani, hawakujuwa kuwa mita chache toka pale walipo kuna mwanamke mmoja aliekuwa anatoka madimbeni (mshamba ya kondeni/mtoni) alikuwa anawatazama, huyu alikuwa ni mschana tu, mschana huyu alikuwa anaitwa alikai kwa jina la utani, jina ambalo alipewa kwasababu ya kwamba hakuwa na utaratibu wa kukaa na jambo moyoni mwake, kwa kifupi alikuwa ni cha umbeya, ambae hakukaa sana akatoka mbio kueleka kijijini akiwa na lengo la kwenda nyumbani kwa Njogopa kumueleza mke wa Njogopa kile kilicho kuwa kinaendelea kule maporini.*******
Mlinzi aliishiwa pose baada ya kuambiwa na boss wake kuwa atapata adhabu yake kwa kile kilicho kifanya, yaani kuwazuia wale wageni, “dah! sijui kwanini nilijifanya mkali wakati watu wenyewe walikuwa wanaongea kwa upole” aliwaza Mlinzi ambae kama ulikuwa humjui kwa jina basi alikuwa anaitwa Ndolite au babu Ndolite, japo wenyewe walipenda kumuita babu, “dah! kumbe nilimzuia mchumba wa Soraya” hakika babu alikuwa ameshushuka kweli kweli, “lakini mbona watu wenyewe ni masikin…” kabla babu haja maliza kujiuliza, mata akamuona Talib anakuja pale getini akitokea kwenye nyumba anayo kaa, akitembea kwa mwendo wa tahadhari kubwa, “babu mtu yoyote akiniulizia mwambie sijarudi kabisa, alisema Talib kisha bila kuchelewa akatoka nje pasipo kujali njaa wala ukapa wa fedha alionao, hakujali wala kuwaza atakula wapi na wala ataenda kukaa wapi mpaka muda ambao shughuri hii itakapo kwisha.********
Mzee komba aliekuwa amelala juu ya kitanda cha Hospital njaa inamuuma kweli kweli, maana toka alipokunywa uji asubuhi kule Hospital ya mjini hakuwa amekula tena hata muda wa kunywa dawa ulishapita, tayari maumivu ya kichwa yalishaanza kumchamanda, “yaani mke wangu na binti yangu wanaweza kunifanyia hivi?” aliwaza kwa machungu mzee Komba, ambae sasa alijutia tabia yake ya kuamua kumchukia Frank, ambae hakuwahi kumtendea ubaya hata siku moja, zaidi ni kwamba Frank na familia yake walikuwa wanamtendea yaliyo mema mara zote, na yeye kuamua kulipiza ubaya, ambao matokeo yake ni hayo ya mganga kutembea na mke wake na binti yake, huku yeye akiambulia mshtuko na kuanguka huku akiishia kupooza mguu.
Wakati Komba akiendelea kijiwazia na kujinung’unisha mara akatokea yule nurse akiwa amebeba sahani ya chakula mkononi, “mzee nashindwa kuielewa familia yako kwanini wanakufanyia hivi” alisema nurse huku anavuta meza akiisogeza karibu na kitanda alicholalia Komba, na kisha akaweka chakula juu yake, “yaani toka asubuhi tuna waeleza kuwa utakuwepo hapa zahanati, nimeenda tena kuwaeleza umeshafika na unahitaji chakula, lakini wapi, hawana hata dalili ya kuleta chakula” alisema nurse kwa sauti ya masikitiko makubwa, “mama kwa kweli nimepatikana, sikutegemea kama watanifanyia hivi” alisema mzee Komba, kwa sauti iliyojaa huzuni na masikitiko, “lakini kwa kuwa tupo hapa kijijini, nadhani hakuna yatakayo haribika” alisema nurse huku anatoka na kwenda kuchukuwa chupa ya uji na kikombe, ambapo hakutumia muda mrefu alirudi akiwa amebaba chupa ya uji na kikombe.
Naam ukiachilia taaluma ya unurse pia ongezea na uwana kijiji walionao, nurse alihakikisha anamsaidia mzee Komba ambae ni mwana kijiji mwenzie, ambae alimuinua kitandani na kumnawisha, halafu mzee Komba akaanza kula taratibu, “ndizi na utumbo” tena aliletewa na uji wa ulezi, siku hizi wanaita uji wa lishe, tena chakula ambacho bila kuumwa pengine asinge pata nafasi ya kukila siku za hivi karibuni.
Naam wakati anaendelea kula mara akaingia mama mmoja mtu mzima, japo hakumfikia mzee Komba kwa umri, lakini aliekuwa amevalia mavazi masafi ya kike gauni la kawaida tu, huku juu yake akiwa amevalia vitenge juu yake, “jamani kaka nini kime kupata, yaani toka juzi unaumwa unashindwa kuwa tuma wakina Hilda kuja kutujulisha” alisema yule mwanamke kwa sauti iliyojaa lawama” ukweli Komba hakuwa na jibu juu ya hilo swali, zaidi alianza kutoa machozi, machoni mwake na kumshangaza huyu mwanamke aliemuita kaka, “samahani wewe ni ndugu yake?” aliuliza Nurse akimtazama yule mwanamke, “ndiyo mimi ni ndugu yake watatu kuzaliwa toka kwake, yaani baba mmoja mama mmoja” alijibu yule mwanamke, ambae kumbe ndie yule dada yake wa makemba, ambae alipelekewa ujumbe na Ngonyani kuwa aje haraka Luhila kaka yake anaumwa.
Naam yule Nurse akamsimulia yule mama, kuanzia usiku wa juzi pale mzee Komba alipo pelekwa pale zahanati akiwa amepoteza fahamu, na kukimbiwa na wenzake lilipokuja swala la kumpeleka mjini, na jinsi mke wa bwana Komba na binti yake walivyo mtelekeza, “wacha niende nikamtafute wifi nijuwe ni kwanini anafanya hivi” alisema dada yake Komba pasipo kujuwa kuwa wifi yake alikuwa katika lindi la burundani ya pombe na mapenzi.*******
Turudi mjini, nyumbani kwa Mahamud, ambako watu wote walikuwa ndani wakisubiri tukio la kutambulishwa kwa mchumba wa Soraya, mama Soraya alikuwa makini sana kumtazama Higgno, ambae alitegemea kumuona akijishauwa shauwa, kwa kufanikiwa lengo lake la kumshawishi na kumlaghai Soraya na kufanikiwa kuwa nae, lakini cha kushangaza hakumuona kuwa na hali yoyote ya kufurahia au kutataikia jambo lile, yaani alikuwa ametulia kama mtazamaji mwingine tu, mara mjomba akasimama, “asalaam alaykum mabibi na mabwana, wacha nimkaribishe bwana Mahamud atueleze sababu ya kutuita hapa siku hii ya leo” alisema mjomba, huku watu wote wakiwa kimya kabisa, hasa mama Higgno ambae alikuwa ametulia anasubiri kusikia kinachoendelea na ondoa maswali ya kichwani mwake na wakati huo akaonekana Soraya.
Alisimama mzee Mahamud ambae kama ilivyo kwa mjomba wa Soraya na wakina Jamal na wakina Higgno na baba yake, kuwa kuna wageni walikuwa wanasubiriwa na pengine wapo nje wanasubiri waingie kwa mpangilio maalumu ambao pengine mama Soraya ameupanga, “asalamu alaykum”alisalimia Mahamud ambae alionyesha tabasamu la hali ya juu, tabasamu ambalo lilimshangaza hata mke wake, ambae alitegemea kumuona mume wake akimtazama Higgno kwa jicho la mshaka, “waalaykum salaam” waliitikia watu wote waliokuwepo mule ndani, “kwanza kabisa kabla sijajuwa kama wageni wetu wataingiaje na utaratibu gani umepangwa, mimi nina jambo moja nahitaji kuliongea” alisema Mahamud, na watu wakamtazama, hasa wale wa upande wa kike, ni kama walikuwa wanashangaana, “ina maana hajamtambua mkwe wake mwenyewe, wakati wamekaa wote humu ndani muda wote huu?”alijiuliza mama Soraya kwa mshangao, na wakati huo huo Soraya akaletwa pale sebuleni, akiwa amevalia gauni lake refu nzuri, amepambwa akapambika, pia kichwani kwake alivalishwa niqab, ambayo iliziba uso wake wote na kubakiza macho pekee, “anaonekana mzuri, lakini mwili wake unafanana na Soraya” aliwaza Higgno, akimtazama mwanamke huyu pasipo kujuwa kuwa ni Soraya wake, ambae alienda kukaa sehemu aliyo andaliwa huku akisindikizwa na macho ya watu wote waliokuwepo hapa, huku mzee Mahamud akiwa amesimamisha maongezi yake.
Naam baada ya Soraya kukaa, ndipo Mahamud akaendelea, “nime sema nina jambo la kuongea kwasababu ni muhimu sana kwangu, japo kwenu linaweza lisiwe muhimu, naliongea hapa kwasababu ya heshima kwa kijana huyu, hakika mpaka sasa sikuwahi kulifahamu jina lake, kijana ambae naweza kusema ni tofauti kidogo na vijana wengine niliowahi kuwaona na pengine kuwasikia katika dunia hii ya sasa hivi” alisema Mahamud akionekana mwenye furaha usoni mwake, huku watu wote wakimsikiliza kwa umakini, wakati huo mama Soraya alikuwa anamtazama mwanae kwa umakini sana, akamuona anaangaza macho kushoto na kulia akigeuzagueza shingo yake mpaka alipo mtazama Higgno, ambae hakuwa na mpango wowote wa kumtazama Soraya hata kwa bahati mbaya, kitendo kile kilimshangaza mama Soraya, kuliko Soraya mwenyewe, ambae aliejisemea moyoni, “atakuwa hajanitambua” alisema Soraya, huku baba yake akiendelea kuongea, “ikiwa ni siku muhimu kwangu na familia yangu ambapo tunaenda kumtambua na kumkaribisha kijana ambae ataelekea kuwa mchumba wa binti yetu wapekee, nimeona pia nimkaribishe kijana ambae mwaka mmoja uliopita niliwahi kusema kuwa endapo ninge mfahamu ninge muoza binti yangu, ikiwa pamoja na kuwaandalia kila kitu kizuri kinachohitajika katika maisha, kama vile nyumba gari fedha na biashara pia” mzee Mahamud alieleza kwa mapana simulizi yake inayo muhusu yeye na kijana mpole na mwenye nidhamu ya hali ya juu, tayari Soraya alishajuwa kuwa anae zungumziwa ni Higgno, kasoro mama yake ambae sasa alikuwa anatazama wanaume waliokuwepo mule ndani kuona kama atamuona huyo kijana ambae mume wake alikuwa anamzungumzia, lakini hakumuona mtu mwinge zaidi ya Higgno na baba yake, zaidi ya hapo ni wale aliokuwa anawafahamu.
Mahamud alisimulia mkasa mzima, kuanzia kusaidiwa siku ile ambayo alivamiwana wale vibaka kule msamala, pia alivyokutana nae jana pale mjini alipodondosha wallet yake na yeye kuiokota akimpelekea kama ilivyo, na rundo la fedha ndani yake, hapo kila mmoja akaanza kutazama kumtafuta kijana mwenyewe kama alivyofanya mama Soraya dakika chache zilizopita, wapo waliomtazama Higgno na wapo ambao walidhania kuwa bado hajaingia pale sebuleni, “kweli sikuweza kuvumilia, niliamini kijana huyu ni zawadi kubwa sana katika maisha ya binti yangu, hivyo nilimuomba amchumbie binti yangu, lakini bahati njema kwake, kuwa tayari alikuwa anamchumba na anapanga kupeleka barua, malengo yake yakitimia, ila la kufurahisha mimi nitakuwa mshenga wa kijana huyu, na nitamfanyia mambo mengi ambayo yatakuwa kama msaada katika maisha yake na mke wake” hapo kila mmoja mule ndani akapiga makofi, huku mama Soraya akitamani kumuona kijana huyo mwenye moyo wa ajabu, na sio Higgno ambae licha ya muonekano wake mzuri na wa upole lakini ni tapeli, “bahati mbaya kijana huyu, sijamjuwa jina lake, atajitamburisha mwenyewe, na kuanzia sasa ninamkaribisha hapa nyumbani, na ninaomba kila aliepo hapa amchukulia kama ndugu kwake” alisema Mahamud na kila mmoja akashangilia huku wakistaajabu kwa moyo wa kijana huyu, “kijana hebu simama ujitambulishe mbele ya wageni waliopo hapa pamoja na mama yako yule pale na dada yako huyu hapa ambae leo atatuonyesha mchumba wake” alisema Mahamud na hapo Higgno akasimama na hapo mama Soraya aliekaa karibu kabisa na mama Hoggno aliekuwa anatokwa na mchozi kwa sifa alizopewa mwanae, mama Soraya akatoa macho ya mshangao, na kujikuta amesha nongo’ona, “mungu wangu, kumbe ni huyu Higgno, hakika mungu huwajalia mema wale walio wema, mwenyezi mungu ni samehe” alisema mama Soraya na kumfanya mama Higgno, amtazame kwa mshangao…… ITAENDELEA MUWE NA USIKU MWEMA
 
Nomasana 🔥🔥
𝐖𝐞𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐬𝐞𝐦𝐚 𝐰𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢 𝐚𝐧𝐚𝐫𝐮𝐝𝐢 𝐊𝐮𝐭𝐨𝐤𝐚 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐦𝐰𝐞𝐧𝐠𝐞 𝐀𝐥𝐢𝐤𝐮𝐭𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐇𝐢𝐠𝐠𝐧𝐨 𝐒𝐢 𝐮𝐧𝐚𝐣𝐮𝐚 𝐭𝐞𝐚𝐦 𝐢𝐝𝐝 𝐧𝐚 𝐦𝐢𝐛𝐚𝐧𝐠𝐢 𝐲𝐚𝐨 𝐚𝐦𝐞𝐜𝐡𝐞𝐳𝐞𝐚 𝐤𝐢𝐜𝐡𝐚𝐩𝐨 𝐤𝐢𝐧𝐨𝐦𝐚 𝐲𝐚𝐚𝐧𝐢.
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA THEMANINI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SABINI NA TISA: alisema Mahamud na hapo Higgno akasimama na hapo mama Soraya aliekaa karibu kabisa na mama Hoggno aliekuwa anatokwa na mchozi kwa sifa alizopewa mwanae, mama Soraya akatoa macho ya mshangao, na kujikuta amesha nongo’ona, “mungu wangu, kumbe ni huyu Higgno, hakika mungu huwajalia mema wale walio wema, mwenyezi mungu ni samehe” alisema mama Soraya na kumfanya mama Higgno, amtazame kwa mshangao…… ENDELEA……..
Lakini akamuona mama huyu ambae anaweza kuwa ndie mke wa tajiri mkubwa kuliko mwanamke yeyote hapa mkoani Ruvuma, akamuona ametoa macho ya mshangao kumtazama Higgno ambae alikuwa amesha simama huku tabasamu likishamiri katika uso wake wa upole, “asalaam alaykum” alisalimia Higgno kwa sauti tulivu ya upole huku tabasamu likiwa limeendelea kushamili usoni mwake, “waalaykum salam” waliitikia watu wote waliokuwepo mule ndani, sura zao zikichanua kwa matabasamu ambayo yalionyesha kupendezwa na sifa ambazo kijana huyu alipewa na Mahamud mwenyewe, na kilicho wavutia wengi ni kitendo cha kukataa kumchumbia binti wa mzee huyu tajiri licha ya kuahidiwa maisha mazuri, mama Soraya akamtazama binti yake akamuona anamtazama Higgno kwa macho fulani ya kipekee, japo ilikuwa vigumu kwa wengine kulifahamu hilo, kwasababu alikuwa amevaa niqab, na akiwa bado anamtazama binti yake mama Soraya akamuona Soraya anaondoa macho yake kwa Higgno ambae hakuwa anamtazama na kumtazama yeye, na macho yao yalipokutana akatazama chini kwa aibu ya kike, “napenda kutoa shukrani zangu kwa mzee Mahamud na familia yake, ambayo kiukweli naweza kusema sijajutia kuifahamu na siwezi kujilaumu kumsaidia mzee Mahamud kupambana na wale jamaa siku ile” alisema Higgno kwa sauti yake ile ile ya upole, ambayo ilimvutia kila mmoja mule ndani huku wakimsiliza kwa umakini, “nasema hivyo kwasababu nilipoamua kumsaidia mzee Mahamud toka kwa wanyang’anyi, siku tegemea kama nitapewa heshima kama hii katika sehemu kama hii, hivyo siwezi kulinganisha na msaada nilioutoa kwa mzee Mahamud, ambao umekuwa mdogo sana ukilinganisha na heshima aliyonipa mbele ya watu wake katika siku muhimu ya binti yake” hapo kila mmoja akakubali kwa kuitikia kwa kichwa, huku baadhi wakipiga makofi ya kumpongeza kijana huyu, “ina maana ni kweli hajui kuwa mwanamke mwenyewe ni Soraya, na mchumba wake ni yeye” aliwaza mama Soraya safari hii kimoyo moyo, japo uso wake ulionyesha mshangao wa wazi, “kitu nadhani hata mzee Mahamud na familia yake hawajatambua pia na wao wametoa msaada mkubwa sana katika familia yangu, ni juzi tu baba ameunguliwa na duka lake na mumemsaidia kulirudisha duka lake, hii ni tosha kuwa hata ningepoteza maisha yangu wakati nakusaidia mzee wangu, damu yangu ingekuwa imeenda mahali pazuri” alisema Higgno, na hapo kila mmoja akaonekana kusisimkwa kwa maneno ya Higgno, hata wazazi wake walishangazwa na busara za hali ya juu alizo zionyesha Higgno, ambae alimaliza maongezi yake na kukaa chini akiwa amesahau kujitambulisha jina lake.
Naam hapo ndipo mjomba akasimama, “sasa nimeelewa kwanini shemeji yangu alipenda huyu kijana awe mkwe wake, hakika wazazi wa kijana huyu wamebahatika kupata zawadi kubwa sana, ya kuwa na kijana kama huyu” alisema mjomba na kila mmoja akaunga mkono maneno yale huku wengine wakikosoa kuwa haikuwa vyema kusema maneno ya kuwa alitamani kijana huyu ndie angekuwa mkwe wake, maana yangemvunja moyo mwanaume ambae anakuja kutambulishwa kuwa mchumba wa binti yao, “sasa nadhani tunaenda kuanza ratiba yetu, wageni waruhusiwe kuingia” alisema mjomba akiamini kuwa wageni bado wapo nje wanasubiri utaratibu wa kuingia ndani, naomba wageni wetu wakiingia tuwapokee kwa kusimama kidogo, maana ndio wakwe zetu watarajiwa” alimaliza mjomba kisha akamtazama mzee Mahamud ikiwa ni kumjulisha kuwa wageni wajulishwe waanze kuingia ndani.*******
Naam dada yake mzee Komba yaani shangazi yake Hilda alifika nyumbani kwa kaka yake, na kukuta hapakuwa na mtu yoyote, akaenda nyumba ya jirani kuuliza napo akaambiwa kuwa mara ya mwisho alionekana Hilda akitoka na kuelekea upande wa barabarani, ni lisaa limoja limeshapita, “atakuwa ameenda kwenye ulanzi, kule vilabuni, lakini mama yake sijamuona kabisa” lilikuwa jibu baya sana kwa dada yake mzee Komba, ambae alielekea huko barabarani kwenye vilabu vya pombe lengo kumpata Hilda ili amueleze mambo mawili ni jambo gani lilimshtua mzee Komba na kuanguka ghafla, pili ni sababu zipi zinazowafanya wamtelekeze namna ile mzee Komba.
Dakika kumi baadae akafanikiwa kufika barabarani, sehemu ambayo kulikuwa na vilabu kadhaa vya ulanzi, ambavyo mida hii ya saa saba mchana tayari pilika zilishaanza, music mkubwa ulianza kusikika, watu walishaanza kuingia mahali pale ambapo palikuwa pametawaliwa na harufu ya nyama za kuchoma, nyama ambazo watu hununua bila kuuliza ni nyama ya nini.
Shangazi yake Hilda alianza kuingia club moja baada ya nyingine, akimsaka mtoto wa kaka yake, ambae katika miaka ishirini na nne ya kuzaliwa tayari binti huyu alikuwa mlevi mbwa wa ulanzi, “samahani Hilda alikuja hapa leo?” aliuliza shangazi, kila alipoingia, “Hilda ni yupi huyo?” lazima angeulizwa swali hilo na yeye angefafanua, “yule binti wa mzee Komba” hapo shangazi ange pewa jibu ambalo lingempa picha ya maisha ya kaka yake na familia yake, ambayo kiukweli sio kwamba hakuwai kuyasikia, ila hakuwahi kuyashuhudia tu, lakini alisha yasikia na kupata habari zake, “hooo kumbe unamaanisha #Tembele, alikuja mida fulani akazuga zuga kisha akatoka mtazame hapo mbele” jina TEMBELE lilimshangaza shangazi, maana hakuwa na habari au kumbukumbu ya kwamba mtoto wa kaka yake alikuwa anajina lingine la tembele, “kwanini anaitwa tembele?” aliuliza shangazi, ili kutoa utata wa jina hilo, hata mjibuji wake akacheka kidogo, “ni TEMBELE LA UWANI si unajuwa ile tabia yake ya kuwasaidia vijana kukata kiu zao” alifafanua mtoa majibu, na hapo shangazi akatoka kwa unyonge kuelekea kule alikoelekezwa.
Lakini ile shangazi anatoka nje akakutana na kundi la watu wakike kwa wakiume, likiwa linapita barabarani kuelekea upande wa kule alikotoka yeye, yaani Luhila seko mtaani anakoishi kaka yake, “kimenuka leo, mshenzi sana huyu mwanamke, yaani mume wake anaumwa yupo Hospital yeye anaenda kuinamishwa maporini na waume wa watu” alisikika mmoja wa watu waliokuwepo kwenye kundi lile, “nasena hivi nikimfuma nitamtembeza uchi Luhila yote” alisema mwanamke mmoja ambae alikuwa ametangulia mbele kabisa sambamba na wanawake wawili, wote wakionyesha wana hasira kali sana.
Shangazi hakujiuliza mara mbili, akaachana na ratiba ya kumsaka Hilda ambae anaitwa TEMBELE na kuanza kulifuata lile kundi, maana kwa maelezo yale alijuwa fika kuwa anae zungumziwa ni mama Hilda ambae ni wifi yake, na dalili zote zilionyesha kuwa anaenda kufumaniwa.******
Idd, akiwa amekaa ndani ya gari, huku anakunywa pombe yake kali alisha yaona yale mapokezi na mtindo wa upokeaji wa wagaeni wale ulimshangaza sana Idd, na mpokeaji akiwa ni mama Soraya mwenyewe, “sijaelewa ina maana gani?” alijiuliza Idd, ambae bado macho yake yalikua ameyaelekeza kwenye geti la Mahamud, ambapo dakika chache mbele akiwa bado anajiuliza akamuona Talib anatoka kwa mwendo wa tahadhari kubwa sana, “huyu fala kumbe yupo” alijisemea Idd, ambae aliona kwamba Talib ndie anaweza kumpa habari kamili ya kinachoendelea kwa kina Soraya, huyu boya atanipa report kamili” alisema Idd, huku anaifunga chupa ya pombe na kuiweka kwenye seat ya pembeni ya gari lile na kisha akaliwasha gari akaweka gia namba moja na kuachia clachi gari likaaza kuondoka taratibu kuingia barabarani kwa lengo la kumfuata Talib, ambae bahati nzuri na yeye alipoingia barabarani akaelekea upande wa kulia wa barabara ambako yeye Idd alikuwepo, hapo Idd, akasimamisha gari na kushusha kioo, “oya mchizi mambo vipi?” alisalimia Idd kwa lugha ya kihuni (kwa kipindi hicho) hapo Talib akashtuka na kumtazama msalimiaji, ambae alikuwa ndani ya gari, akamuona Idd, “dah! afadhari nimekuona Idd, mambo vipi?” alisalimia Talib huku akilisogelea gari, “poa tu! vipi mbona unasema afadhari umeniona?” aliluza Idd kwa sauti fulani ya pose na majivuno, “dah! mwenzio nina ubao mkali sana, halafu huko ndani kuna fala amaengia siwezi hata kuonana nae uso kwa uso” alisema Talib, pasipo kufafanua huku anatupia macho kwenye seat ya pembeni na dereva, pale ilipolala chupa ndgo ya pombe kali, ambayo yeye alikuwa ameimisi kwa muda mrefu maana mara ya mwisho ni siku kama nne zilizopita, tena alikuwa amekunywa ulanzi, “kwahiyo unataka nikupe hela ukale?” aliuliza Idd kwa majingambo na nyodo, “hiyo moja wapo, lakini kuna inshu nyingine nataka tuongee” alisema Talib, ambae alionakuwa akimtia nyembe Idd itakuwa rahisi kumsaidia gari kwaajili ya tukio lake la usiku, “unataka kuongea nini Talib, we sema tu nikuachie hata buku ukale kwa mama ntilie” alisema Idd, huku anazama mfukoni kutoa noti kadhaa, ambazo alichomoa buku na nyingine akazieka kwenye mkebe wa dash board, “Tatizo lako Idd unajifanya mjanja, ndio maana hata Soraya umemkosa, ungenishirikisha mimi tayari ungekuwa umesha jibebea mzigo, ona sasa kuna boya mmoja anamchukuwa mazima” alisema Talib, ambae tayari alisha tamani ile chupa ya kischana, ambayo alikuwa anaitazama kwa uchu, “weeee! ina maana ni kweli Soraya anachumbiwa, anachumbiwa na jamaa gani?” aliuliza Idd kwa sauti iliyojawa na mshangao, “kuna fala mmoja hivi, mjinga mjinga, sijui kama mitishamba haijausika” alisema Talib kwa sauti ya dharau, “dah! huyo fala ana zari kweli kweli” alisema Idd,kwa sauti ya kujilaumu na kukata tamaa, “acha ujinga Idd, hiyo sio inshu, kutegemea demu ili upate mali, wewe si mzee wa inshu, sasa mimi nataka nikupe mpango wa hela” alisema Talib, ambae alijuwa fika kuwa Idd toka amerudi msumbiji hakuwa na fedha yoyote, zaidi ya kumtegemea baba yake, “poa twenzetu mtini pub tupige pombe huku unanipa huo mpngo wako” alishauri Idd, ambae alihamasika kwa kusikia mpangp wa hela, Talib akaingia kwenye gari huku akiiokota chupa ya pombe na kuifungua kisha kuanza kuinywa wakati gari linasogea taratibu mtini pub.********
Naam baada ya mjomba kumuachia ukumbi Mahamud, ambae hakuwa anaelewa utaratibu uliopangwa akamtazama mke wake ikiwa ni ishara ya kumueleza kuwa wageni wanaweza kuingia, hapo mama Soraya akiwa mwenye uso ulioonyesha hali fulani ya fahadhaa, alimtazama mume wake ambae alishangaa kidogo kwa muonekano wa mke wake huyu, “assalam aleykum” alisalimia mama Soraya, kwa sauti ya upole ambayo ilijibiwa kwa sauti kubwa ya shangwe, “waalaykum salaam” Mahamud alimtazama mke wake ambae alionyesha wazi kuwa amenyongea kidogo, akampa ishara ya kuchangamka kidogo, kisha Mahamud akamnongo’oneza Jamal, “kuwa makini sasa, akiingia tu nadhani utamfahamu, maana wewe ni mtoto wa mjini” alisema Mahamud, kisha akamtazama mke wake kama wengine mule ndani walivyofanya, wakiwa wanahamu ya kumuona kijana ambae amebahatika kumchumbia Soraya, “kwanza kabisa niseme kuwa hakika mwenye kutenda mema, basi mwenyezi mungu humjalia yaliyo ya kheri, na wote wenye mioyo safi njia yao ni moja” alisema mama Soraya huku watu wote mule ndani kasoro Soraya na Laylah, ambae sasa aliingia na kukaa nyuma kabisa ikiwa ni sehemu ya mpango wao na Soraya, wao pekee walijuwa mama Soraya anamaanisha nini, wengine wote walidhania kuwa mama Soraya anaunga mkono maneno ya mume wake juu ya kijana Higgno, “ukweli nimefurahi sana kuona binti yangu anapata mume bora, mwenye sifa zote za kuwa mume, na mimi ninampokea kwa mikono miwili kuwa mchumba wa binti yetu, naomba yeye na wazazi wake wafanye utaratibu wa kuleta barua ili tufanye utaratibu wa ndoa” sio Higgno na mzee Mahamud peke yao walioshangazwa na maneno yale ila ni watu wote mule ndani mpaka mzee Frank na mke wake walishangazwa na jambo lile, kasoro mama Soraya Laylah na Soraya mwenyewe, ndio pekee waliojuwa kuwa yule ni Higgno mchumba wa Soraya, watu wote wakamtazama Higgno ambae pia alionyesha kushangazwa na jambo lile, huku akimtazama baba yake kama vile anamuuliza nini kinaendelea, maana yeye aliambiwa kuwa wazazi wake wamealikwa kwa chakula cha mchana, wakaambiwa waende na kijana wao sasa haya mengine yanatokea wapi.
Hapo mjomba baada ya kuona hata huyo kijana mwenyewe yupo kwenye mshangao, akamtazama Mahamud ambae pia alionyesha wazi kuwa katika mshangao mkubwa, mjomba akasimama, “mpaka hapo mumetuacha njia panda, munamaanisha huyo mchumba ndie huyu, kijana ambae alimsaidia mzee Mahamud?” aliuliza mjomba, safari hii sio kama msemaji, aliulizia kama mshangaaji anaehitaji uthibitisho, huku watu wote wakimtazama Higgno ambae bado alikuwa katika mshangao na wasi wasi mkubwa, ukweli hakuna mmoja alie toa jibu, mjomba akamtazama Soraya, mjomba tunaomba ututhibitishie kama kweli huyu ndie kijana mwenyewe au laa, isije kuwa kama siku ile” alisema tena mjomba huku pamoja na watu wote wakitazama pale alipokaa Soraya, ambae alikuwa amevalia niqab yake na kubakiza macho tu! “Soraya akaitikia kwa kichwa kukubali kuwa Higgno ndie mchumba wake, hapo zikalipuka kelele za shangwe na vifijo na vigelegele, huku wakimtazama Higgno kwa macho ya hongera, mzee Mahamud, akionekana mwenye tabasamu la furaha na kushindwa kuelewa ile mipango ilikuwa imewekwa vipi, au walipanga kumshtukiza.
Lakakini basi wakati furaha na shangwe zinaendelea mara ghafla sauti ya mjomba ikasikika, “jamani tulieni kidogo, naona mkwe wetu anataka kuongea jambo” hapo watu wote mule ndani wakatulia kimya, huku wanageuza shingo zao kutazama upande ule aliokuwa amekaa Higgno, wakamuona amesimama uso wake ukiwa katika hali ya mshangao na simanzi, “samahani sana watu muliomo humu ndani, samahani wazazi wa huyu mschana, yaani mzee Mahamud na mke wako, samahani wazazi wangu pia samahani sana wewe mschana mwema” hapo watu wakashikwa na mshangao mkubwa na kuanza kunong’onezana, wakiulizana kuwa “huyu kijana anataka kusema nini?” “halafu mbona kama amekosa amani ghafla?” hayo ndiyo maswali yaliyozagaa pale ukumbini, “ukweli ninatanguliza samahani kwa watu wote humu ndani, kwasababu najuwa nitakacho kiongea hata nyinyi hamtanielewa kama mimi nisivyoelewa kinachoendelea hapa, kwa kifupi mimi sio mchumba wa huyu mschana, pengine amenifananisha, Kwa sababu sijawahi kumuona mschana, naimani hata yeye hajawahi kuniona” alisema Higgno na hapo watu wote wakaacha midomo wazi kwa mshangao na kumtazama Soraya, ambae alikuwa ameinamisha kichwa chini na kabla mtu yoyote hajaongea lolote Higgno akaendelea, “mimi nipo hapa kwasababu nime wasindikiza wazazi wangu, ambao wamealikwa mahali hapa, pia isitoshe nina mchumba wangu, ambae natarajia kumchumbia hivi karibuni, naomba mniwie radhi, nadhani hata binti yenu, ataishi na mimi kwa wasi wasi endapo atagunduwa kuwa nimemuacha mschana mwingine kwaajili yake, hivyo nisameheni na pole ni kwa usumbufu” alimaliza Higgno na kukaa chini……… ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom