Anaweka kidogo sanaWe jamaa we jamaa
Unatupa raha kidogo tu halafu unasepa:
Tena bila chumviAnaweka kidogo sana
ngoja tumuite aje hapa asitufanyie hiviTena bila chumvi
Sure ni Kama Kisonge sijui kasongo yeye mutu ya Kongo(drc) mbele ya Deus.Dereva tax hana bahat
Nakuja nakuja
Tupia mambo veveNakuja nakuja
TunasubiriNakuja nakuja
Njoo uwaeleze namna tulivomchapa derevaNakuja nakuja
Naukubali sana uandishi wako mkuu, kazi nzuri saana,Hongera sana🙏🙏🙏🙏🙏🔥🔥🔥🔥🔥TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHILINI NA TISA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NANE: Pale barabara ya chini ya NPF, kwenye miti ya wakoloni, dereva wa Taxi alipomuona Higgno anashuka akajuwa sasa amesha fanikiwa kujiopolea binti mrembo wa kiarabu, japo hakuwa amemuona sura, kwasababu ya ile niqab, fanya haraka wewe” alisema dereva wa Taxi, huku ana mshika mkono Higgno, ambae wakati huo huo wakaona simu inaanza kuita, ile Higgno anataka kupokea yule jamaa akamzuia “wewe usipokee hiyo simu, hebu toka haraka” alisema dereva wa taxi aliekuwa amemshika Higgno mkono na kumvuta kwa nguvu kwa lengo la kumsukumia pembeni……… ENDELEA NAYO
lilikuwa kosa kubwa sana kwake, maana alishangaa kuona kuwa licha ya kutumia nguvu nyingi sana kumfuta Higgno, lakini yeye ndie alie yumba na kupepesuka kidogo, na hapo akagundua kuwa mkono wa kijana yule ulikuwa umeshupaa kwa mazoezi, ile dereva wa taxi anapata ufahamu kuwa Higgno hakuwa mtu wa kawaida, tayari alishadakwa mkono na nyang’anywa upanga, ile anataka ajitete ili kujiepusha toka kwenye kifinyo ambacho alikiona wazi kinamjia kutokana na upumbavu wake, akashtuka mvua za ngumi nyingi sana zikishuka usoni kwake, tena ni ngumi mfululizo ambazo zilituwa kiufasaha sehemu ya mashavu pua machoni na mdomoni, mpaka alipoanza kuona nyota za kila rangi zikitawala usoni kwake, huku pumzi ikishindwa kutoka vizuri puani na kutumia mdomo pekee akiachama kama samaki kwenye maji ya moto, alihisi jasho la joto likichirizika usoni mwake, machoni na mdomoni alihisi miwasho na chumvi nyingi, halikuwa jasho ni damu, kila alipojaribu kujiinua alikutana na ngumi zilizo mrudisha chini, ghafla akajihisi mwili unakosa nguvu na kupoteza fahamu, Hapo Higgno alipo jihakikishia kuwa dereva wa Taxi yupo chini na hakuwa na uwezo wakufanya lolote, akaitazama ile simu, ambayo bado ilikuwa inaita, akaona jina la mpigaji ni mama, akaipokea na kuiweka sikioni, “hallow shikamoo” alisalimia Higgno kwa sauti yake tulivu na ya upole huku ameshika panga kwa mkono wa kushoto, na hapo Higgno akakutana na maswali kama matatu, mfululizo, “hallow baba, upo salama mwanangu, vipi mwanangu yupo salama, kwan mupo wapi sasa” ni maswali ambayo alifanikiwa kulijibu lile la mwisho.******
Mzee Mahamud akiwa njiani anaelekea nyumbani kwake bado kuna kitu kilikuwa kina msonga kichwani kwake, ni kitendo cha gari la mzee Mahadhi kuonekana kwenye bar, tena bar yenywe inasifa moja kubwa ya matendo ya uzinzi, “kama gari alikuwa nalo yule kijana, kwahiyo Idd ndie aliekuwepo hapo bar” aliwaza mzee Mahamud huku anaendesha gari lake kueleka nyumbani kwake, “mungu wangu ina maana huyu kijana huko south afrika amejifunza ulevi, kwanini sikuwahi kuliwaza swala hili?” aliwaza mzee Mahamud ambae alipania kumueleza mke wake, ili aongee na binti yao juu ya kukaa mbali na Idd, kuwa sio kijana mwema hata kidogo, “sijui watakuwa wamefikia wapi katika urafiki wao, ni bora kumsikiliza mwenyewe Soraya katika uchaguzi wake wa mwanaume atakae mfaa” aliwaza bwana Mahamud ambae aliumia zaidi pale alipo waza kuwa mwanae amejitahidi kujitunza kwa miaka mingi halafu aje kujitoa kwa kijana mwenye kushinda bar, “bora iwe kuwa alienda kuongea na mtu mara moja, lakini sio kunywa pombe na kufuata wanawake” aliwaza bwana Mahamud, huku anaingia nyumbani kwake, pasipo kujua kuwa dakika chache zilizo pita mke wake amtoka hapo hapo nyumbani.*****
Naam dakika chache zilizopita mama Soraya baada ya kuona simu imepokelewa na yule kijana mpole na kumsalimia hakukumbuka hata kuitikia salamu ile, “hallow baba, upo salama mwanangu, vipi mwanangu yupo salama, kwan mupo wapi sasa?” aliuliza mama huyu kwa sauti iliyojaa pupa na wasi wasi, “tupo NPF kwenye miembe ya wakoloni, naomba uje umchukuwe mtoto wako amelewa sana”, mama Soraya alimsikia kijana yule mwenye sauti ya upole akisema kwa kunyeyekea na kusihi, na mpaka anamaliza kuongea tayari alikuwa amesha ingia ndani ya gari na kuliwasha, kisha akaanza kuondoa gari akielekea langoni na honi mfululizo akizilindimisha, babu mlinzi akafungua gate haraka na mama Soraya akatoka nje na gari kwa mwendo wa kasi ya ajabu.
Mama Soraya aliendesha gari huku akiomba amkute mwanae akiwa salama, huku akimshukuru sana kijana yule kwa kutumia juhudi na uvumilivu mkubwa kuhakikisha Soraya anakuwa salama, katika hiyo hali ya ulevi aliyokuwa nayo, na kingine alicho kiwanza ndani ya dakika tano alizotumia kutoka kwake mpaka kufika kwenye kona ya NPF, ni imekuwaje kitokee kitu kama hicho, wakati Soraya aliondoka jioni hiyo akiwa na Idd kijana wa mzee Mahadhi, kijana ambae wamemuona anafaa kuwa mchumba wa binti yao.
Mama Soraya alikata kona ya NPF akifuata barabara iendayo hospital na magereza, lakini alipotembea kidogo akaweza kumulika gari dogo jeupe aina ya Toyota la kukodishwa yaani Taxi, likiwa lime simama pembeni ya barabara huku kijana mmoja amesimama pembeni ya gari hilo akiwa ameshika panga mkononi, kwanza moyo mama Soraya ulilipuka kwa mshtuko, “mungu wangu, ameshika upanga” alinong’ona mama Soraya huku ana jilazimisha kupunguza mwendo na kusogeza gari pembeni akiliegesha nyuma ya lile gari dogo la kukodishwa yaani Taxi, na alipotazama vizuri akaona kuna mtu amelala chini huku amechafuka damu uso mzima, “shikamoo mama” alishtuka mama Soraya baada ya kusikia sauti ile ya upole toka kwa yule kijana ambae alisogea kwenye gari lake, “marhaba baba, sijui…..sijui wewe ndie ulienipigia simu?” aliuliza mama Soraya kwa sauti iliyojaa wasiwasi, huku akitazama lile panga mkononi kwa Higgno, kijana mwenye sura na umbo zuri la kiume.
Ni kama Higgno aliona wasiwasi wa mama yule, akatupa panga karibu na yule dereva wa Taxi, “ndio mama, nimekutana na huyu dada kule bomba mbili ni kama alikuwa anamkimbia mtu au anakimbia kitu fulani, akaniomba nimsaidie kumfikisha nyumbani, kwasababu yeye mwenyewe alionekana amelewa lakini hanuki pombe yoyote, naomba nimpakize kwenye gari lako” alisema yule kijana mpole yaani Higgno, “sawa mwanangu naomba unisaidie kumpakiza” alisema mama Soraya, huku akishuka toka kwenye gari na kumfuata nyuma Higgno aliekuwa anaelekea kwenye lile Taxi, ambalo bado mlango ulikuwa wazi, mama Soraya akachungulia ndani na kumuona mwanae akiwa amelala kwenye kiti cha gari lile kiti cha nyuma, akiwa amevalia nguo zake vizuri na ile niqab yake ikiwa usoni kwake, na kimfuko kidogo kizuri cha zawadi kile ambacho tuna kifahamu kuwa ni cha Higgno kikiwa pembeni ya Soraya, mama Soraya akamtazama Higgno usoni, akaiona sura yake tulivu ya upole ikimtazama Soraya, “amelala mara tu tulipoingia kwenye gari” alisema Higgno kwa sauti tulivu ya upole, nikama mama Soraya hakufuatilia maneno ya Higgno, zaidi ilimjia kumbu kumbu ya maneno ya Higgno alipokuwa anabishana na dereva wa Taxi, “kama yeye mwenyewe amejiziba uso kwa maadili yake kwanini mimi nimfunue?” ukweli mama Soraya alimtazama Higgno kwa macho ya kipekee kabisa, kuwa ni kati ya vijana ambao hajawahi kuwaona toka amezaliwa na yeye akiwa mwenyeji wa mkoa huu, ambao ni bora kijana wakiume umpatie fedha au kitu chochote cha thamani akipeleke kokote kuliko kumpatia mwanamke, hata kama hana matatizo ya akili, lazima atakula kitumbua, (ni zana ya kufikirika sio kweli) “naomba unisaidie kumnyayua naona amelewa sana” alisema mama Soraya, huku akipisha pale mlangoni, lakini Higgno akaonekaa kusita kidogo, “samahani mama, huyu ni mwanamke, nina ruhusiwa kumbeba?” aliuliza Higgno nadhani alihofia baada ya kugundua kuwa ni familia yenye maadili na matajiri, hasa baada ya kuona usafiri wa mama huyu ambae hakuwa mweupe kama mwanae, ila uvaaji wake ni kama wa yule mschana, “usijali baba, nime kuruhusu umbebe niwekee kwenye gari, kwani mwenzie yupo wapi?” aliuliza mama Soraya huku akijaribu kutazama kwenye gari la kukodi kama kutakuwa na Idd nae kalewa, nilimkuta peke yake anasema nimsadie kufika nyumbani, ni kama alikuwa anamkimbia mtu fulani” alisema Higgno ambae alisogelea kwenye seat ya gari, akamnyanyua Soraya toka kwenye gari kwa ungalifu mkubwa pasipo kumfunua sehemu yoyote, huku mama Soraya akitazama jinsi kijana mpole alivyombeba Soraya kama mtoto mdogo.
Lakini wakati Higgno anamnyanyua Soraya wote wakashangaa kuona Soraya ana jitikisa, “kwani tumeshafika nyumbani” aliuliza Soraya kwa sauti ya kichovu, huku anazungusha mikono yake shingoni kwa Higgno na kuwa kama ana mkumbatia fulani, “mama yako amekuja kukuchukuwa” alisema Higgno, huku mama Soraya anachukua kile kijifuko cha zawadi kwenye gari la kukodi na kuwahi kwenye mlango wa kati kati wa lile gari la kifahari yani Toyota Land Cruzer, “mama…. mama we! mama…” aliita kivivu Soraya, “abee mwanangu, nini kimekukuta mwanangu?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya huzuni na masikitiko, “mama… usisahau zawadi yangu… toka kwa kijana mpole” alisema Soraya “nime kuchukulia mwanangu” alisema mama Soraya huku anafunga mlango wa gari lake, “haya mwanangu ingia twende” alisema mama Soraya baada ya kuingia kwenye gari, “hapana mama ninakaa mbali wacha tu niwahi” alisema Higgno ambae hakujuwa anaongea na mama tajiri mke wa bwana Mahamud, yule aliemsaidia asikabwe na majambazi, “jamani mwanangu, nitakupatia dereva akupeleke mpaka nyumbani” alisema mama Soraya kwa kubembeleza na kusihi,
Hii ni bonas tu mzigo kamili utaendelea usiku hapa hapa jamii forums... ITAENDELEA
Pamoja kiongozNaukubali sana uandishi wako mkuu, kazi nzuri saana,Hongera sana🙏🙏🙏🙏🙏🔥🔥🔥🔥🔥
Umetisha mkuuTEMBELE LA UWANI

Sasa hapa ndyo tunaanza,Pamoja kiongoz