Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 2,117
- 5,240
- Thread starter
- #181
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO: lakini hakuona mtu yoyote ambae angeushtua hata mshipa mmoja wa aibu zaidi ya mzee mmoja aliekuwa amesimama huku ameshikilia baiskeli yake japo alionekana kumtazama kwa mshangao lakini Joan hakumjali, akapiga pafu la pili la sigara yake huku anatembea kuelekea ndani ya bar, na wakati huo huo Joan akasikia mlio wa pikipiki alipogeuka na kutazama nyuma akaiona pikipiki inasimama na akashuka Higgno, “hooo! Higgno, za masiku” alisema Joan kwa sauti ya kuchangamka huku moshi wa sigara ukimtoka mdomoni mwake, akimsogelea Higgno na kumfanya yule mzee mwenye baiskeli mpya ashangae ENDELEA SASA...
Nakumtazama Higgno kwa macho yale yale ya mshangao, akamuona Higgno akiwa anamtazama yule mwanamke kwa macho ya tahadhari, kama vile hakupendezewa kuitwa na yule mwanamke, kitu ambacho hata yule mwanamke alikiona na kupooza kidogo, “jamani higgno umekuwa handsome” alisema Joan kwa sauti ya kujibebisha huku akijisogea karibu karibu kabisa na Higgno na kusimama mbele yake, huku mzee mwenye baiskeli mpya akiwa amesimama, anawatazama kwa mshangao, “mbona kawaida tu!” alijibu Higgno, akijaribu kumkwepa yule dada na kumfuata yule mzee mwenye baiskeli, “kumbe huyu mdingi alikuwa anakusubiri wewe, mwenzio natambulishwa kwa mchumba leo, nitakualika kwenye harusi yangu” alisema Joan, huku anapeleka sigara yake mdomoni na kupiga funda moja nakupuliza moshi kwa nguvu huku Higgno na baba yake wakimshangaa Joan, “ndiyo ni baba yangu nitakaribia kwenye harusi” alijibu Higgno alieshikilia kijifuko kizuri cha zawadi mkononi mwake, “ok! kumbe mdingi wako, sasa wacha mimi niingie mara moja hapa ni shtue …. (alitaja pombe kali ile ya mtunisha misuri) nikate hangover maana jana nilikuwa tungi kweli kweli” alisema Joan kisha akaondoka na kuingia kwenye ile bar iliyopo jirani na pale waliposimama, huku Higgno na baba yake wakimtazama mschana huyu alie elekea moja kwa moja counter na kuagiza pombe aliyohitaji, “unafahamu vipi huyu mwanamke” aliuliza baba yake Higgno yaani mzee Frank, “nilisoma nae huyu ndie alikuwa rafiki yake Hilda” alisema Higgno huku anashika vizuri kile kijifuko cha zawadi ambayo mpaka sasa hata mimi sijui alikuwa ameweka nini, nakupokea baiskeli ya baba yake wakianza kutembea kuelekea mbele huku Higgno akikokota ile baiskeli, wakimuona yule mschana akipewa chupa ndogo ya pombe hiyo, “mh! kazi kweli kweli, yaani mschana mzuri kabisa anafanya mambo ya ajabu” alisema mzee Frank, huku safari ikiendelea, huku kwa macho yao wakimuona yule mschana akiifungua na kugugumia mafunda kadhaa huku akikunja sura kwa uchungu wa pombe ile.
Higgno na baba yake walifika kwa shangazi yake Higgno, ambako waliwakuta shangazi na mama mmoja ambae walitambulishwa kama vile ni mama wa mschana mwema ambae anatarajiwa kuwa mchumba wa Higgno, ambao walikuwa wanasaidiana na waschana wengine wawili waliotambulishwa kama majirani wa pale kwa shangazi, waliosaidia na kupika chakula kilicho kuwepo mezani, wakati huo kina subiri kuliwa na wageni wawili hao, huku mzee Frank na Higgno wakipepesa macho wakitarajia kumuona mchumba mtarajiwa, lakini hawakuona hata dalili, wakaamini kuwa muda ukifika watamuona.******
Upande wa Soraya bado taswira ya kijana yule ambayo japo aliiona miaka mingi iliyopita, lakini hakuweza kuisahau ilimjia kama ilivyo japo mwili wake ndio ulikuwa umebadilika, ukiachilia urefu ulioongezeka kidogo, pia amekuwa mpana kidogo na misuri iliyoimarika hasa sehemu za mikono akionekana anafanya mazoezi ya nguvu, alitulia kimya kama vile akili yake ilikuwa imehama kidogo, akikumbuka siku ambayo alimsaidia pale kichakani alipokuwa amezingirwa na vijana wanne wa songea boys, wakihitaji kumuingilia kimwili, hakika kosa yule kijana mpole alietokea kama muokozi wake na kuokoa bikira yake ambayo alikuwa anaipoteza kwa aibu, “ni yeye yule kaka kwanini hakuniona” aliwaza Soraya, akisahau kama alikuwa amevaa kizuia uso, yaani niqab.
Hata walipo simama nje ya lile jengo la walilo simama juzi walipo fika hapa bombambili, na kama ilivyokuwa juzi na leo pia Idd alishuka kwenye gari na kuingia ndani ya ile nyumba, akimuacha Soraya akiwa katika lindi la mawazo, “kama ni yeye basi nitamuona tu” alijisemea Soraya, ambae bado alikuwa amejiziba uso kwa ile niqab yake.
Idd hakutumia muda mrefu mule ndani, alitoka na kuingia kwenye gari, “vipi Soraya, naona kama umepooza ghafla?” aliuliza Idd huku anaondoa gari kuelekea mtaa wa kojani, “wala ni kama nimepata mshtuko tu” alisema Soraya, huku akijaribu kujichangamsha kwa tabasamu, “ok! sasa naona muda umeenda sana, kama vipi pale Kojani tununue tu vitu tukalie pale kwenye juice ya mabungo” alisema Idd na Soraya akiunga mkono na wakakubaliana iwe hivyo, hakujuwa kuwa mwenzie Idd alikuwa anawaza anayo yawaza kichwani mwake.*******
Naam ilipita nusu saa pasipo mzee Frank na Higgno kumuona mchumba mtarajiwa, zaidi waliona pilika nyingi za kupigiana simu na samahani za hapa na pale, “samahani kaka mchumba tume mtuma dukani mara moja anakuja sasa hivi” alisema shangazi kila alipokatisha sebuleni, nusu saa la pili likiwa lina elekea mwishoni, huku Higgno akiwa na mcheche wa kukiona kifaa alicho kibebea zawadi, kifaa ambacho angefanya nacho uzinduzi wa kukila kitumbua kule magetoni aliko kufanyia usafi wa kina, ambako leo hii angewahi kwenda kupitia mitego yake ili kutazama kama amenasa kitoweo, ambavyo aliamini kuwa vinge mfanya mchumba asirudi kwao, mara wakashtuka mlango wa sebuleni umefunguliwa kwa ghafla na pupa, kama vile kuna mtu alikuwa anafukuzwa na mwizi, ile kushtuka kamuona Joan akiingia kwa haraka ndani na kujikuta akiwa kati kati ya sebule akiwatumbulia macho Higgno na baba yake, ambao aliwakumbuka mara moja kuwa ametoka kuonana nao lisaa lililopita,
Ni kama Joan alishtuka sana kuwaona wakina Higgno wakiwa pale maana alitoa macho ya mshangao kama amedondosha kanga mbele ya baba mkwe, huku Higgno na baba yake wakishangaa na maneno fulani ya Joan yakipita vichwani mwao “mwenzio natambulishwa kwa mchumba leo, nitakualika kwenye harusi yangu” huku wana mtazama yule mschana aliewaambia hivyo lisaa limoja lililopita, ambae hakuweza kusimama tena pale mbele yao, akakimbilia upande wa vyumbani, kisha Higgno akamtazama baba yake ambae pia alikuwa anamtazama, wakatazamana kwa macho ya mshangao, wakati huo huo wakamuona shangazi anapita mbio mbio kutokea jikoni, “afadhari ameshafika nadhani tutafanya haraka muwahi kabla jioni haija ingia” alisema shangazi na kuzidi kuwashangaza baba na mwanae.
Mpaka hapo mzee Frank akajuwa kuwa Higgno asinge kubaliana na jambo lile, hivyo akainamisha kichwa chini kwa masikitiko huku akijizuia kuangua kicheko, hata alipomuona Higgno anainuka hakushangaa, “sasa baba utaniagia kwa shangazi, nadhani unalo la kumueleza” alisema Higgno kisha akaelekea mlangoni akaufungua na kutoka zake nje akiwa na kijifuko chake cha zawadi.
Mzee Frank hakuweza kumzuia mwanae kwasababu hata yeye asingekubali mwanae amchumbie Joan, hivyo akatulia mpaka alipomuona dada yake anakuja kutoka chumbani huku uso wake umefadhaika, “kaka Higgno mwenyewe yupo wapi?” aliuliza shangazi mara baada ya kutokumuona Higgno, “amesha ondoka” alijibu mzee Frank kwa sauti iliyo poa, “kwani kimetokea nini huyu binti alipoingia hapa ndani” aliuliza shangazi, “kwani yeye amekuambia nini?” mzee Frank nae akauliza, “hajasema kitu zaidi amelala kifudi fudi hataki hata kuongea” alisema shangazi na hapo mzee Frank akatabasamu, “dada wala usisumbuke, nikwamba Higgno anamfahamu vizuri huyu mschana, na isitoshe tumekutana nae hapo sokoine wakati tunakuja” alisema mzee Frank na kuanza kusimulia kilicho tokea, “hivyo basi, yeye mschana anajua kilichotokea ndio maana amekuwa hivyo” alisema mzee Frank, shangazi akashusha pumzi ndefu, ya uchovu, “Joan amesha vuruga” alisema shangazi kwa sauti ya kichovu ya kunong'ona.******
Huku kwa wakina Idd na Soraya mambo yalikuwa mwanana, tayari walishanunua vitafunwa vyao na kueleka Kuchile ambapo waliingia na kutafuta sehemu moja nzuri iliyojificha, sehemu ambayo ilimshawishi Soraya kukubali kukaa, maana alishaanza kuleta mgomo wa kuingia sehemu kama hii ya bar na guest house, kutokana na maadili na malezi yake hakuwahi kukaa sehemu kama hii, lakini alikubali kukaa kwa makubaliano ya hali mbili, moja ikiwa ni kutokutoa niqab usoni mwake, mbili kwa kuwa ilikuwa ni sehemu iliyojificha na kuzungukwa na mauwa yaliyotengeneza uzio mkubwa na mzuri wa eneo hili, hakujua kuwa haki hizo mbili zote zilikuwa ni faida kwa Idd, ambae alishapania kutekeleza ubakaji wake, kwa maana ya kwamba, ile niqab ilisadia Soraya asinge fahamika kwa mtu yoyote na kutoa taarifa kwa mzee Mahamud wakati anampeleka chumbani akishirikiana na yule muhudumu wa kike, pili ile sehemu iliyojificha ilikuwa nzuri kwake, maana hakuna ambae angeona wakati Soraya anaanza kuzidiwa na kilevi.
Ile wanakaa tu akatokea yule muhudumu wa kike na kama ilivyo pangwa, ikaangizwa juice na maji ambayo ni kama yalisha andaliwa, mara moja vitu walivyo agiza vikaletwa pamoja na glass mbili, “mimi nitakunywa kwenye chupa haina haja ya glass” alisema Idd, huku anafungua ile chupa ya maji na kuiweka mdomoni, kisha akapiga funda moja la maji yale na kuifunga ile chupa kisha akaiweka tena mezani huku anamtazama Soraya ambae alifungua ile chupa iliyowekewa juice na kuimiminia kwenye Glass, “nimekunywa muda mrefu hii juice” alisema Soraya huku anatabasamu na kushika kile kitambaa cha niqab usoni mwake na kukitupia kichwani, halafu akaipeleka glass mdomoni na kupiga funda dogo kama vile la kuonja, akakubali kwa kichwa na kuongeza funda jingine kubwa halafu akaweka mezani na kumtazama yule dada aliekuwa anamtazama muda wote, “juice yenu nzuri utaniandalia nyingine niondoke nayo” alisema Soraya, na hapo Idd akatabasamu kwa ushindi, “usiwe na wasi wasi dada yangu, ngoja nikakuwekee oda” alisema yule dada muhudumu na kuondoka zake, “hapa ni pazuri bila shaka umepapenda sana” alisema Idd huku anainua tena ile chupa ya maji na kuipiga funda moja zito, halafu akaifunga tena ile chupa ambayo Soraya alidhania kuwa ilikuwa ni maji kwa weupe wake na kuiweka mezani, akisikilizia jinsi pombe kali ambayo haikuzimuliwa na kitu chochote ikishuka kwenye koo lake na kwenda kuunguza maini mwilini mwake, “yah! ni pazuri sana, tena inafaa ukifunga ndoa unakuja kupumzika hapa hata siku mbili” alisema Soraya na wote wakacheka kidogo, “lakini panafaa kuja na mwanamke mzuri kama wewe sio” alisema Idd kwa uchokozi, “umenza kaka Idd, kwani mimi nina uzuri gani?” alisema Soraya akijifanya kujinunisha, lakini alishindwa na kujikuta anatabasamu, “inamaana wewe hujijui kama ni mzuri Soraya?” aliuliza Idd, ambae alikuwa ana hesabu tu funda za juice alizokuwa anakunywa Soraya, ambazo ndani ya dakika kumi alisha kunywa robo tatu ya glass, ambayo kwa kiwango cha dawa ilitosha kabisa kuanza kumlewesha mtu ambae hatumii kilevi chochote,”wana….” alisema Soraya na kusita kidogo, baada ya kuona mdomo wake unaanza kuwa mzito, akaitazama glass ambayo ilikuwa na Juice kidogo sana, hapo Idd akajua kuwa tayari mzigo umelewa, “wanasema mimi ni mzuri, hivi ni kweli eeh?” alisema Soraya kwa sauti fulani ya kilevi, huku anainua macho kumtazama Idd, hakumuona Idd mbele yake zaidi aliona kiti kitupu na chupa ya maji, na hapo Soraya akagundua ukweli kuwa alikuwa amewekewa kitu kwenye ile juice, akapata wazo la kuzimua dawa kwa kunywa maji mengi na maji pekee ni yale aliyokuwa anakunywa Idd…..…. ITAENDELEA
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA: kuanza kumlewesha mtu ambae hatumii kilevi chochote,”wana….” alisema Soraya na kusita kidogo, baada ya kuona mdomo wake unaanza kuwa mzito, akaitazama glass ambayo ilikuwa na Juice kidogo sana, hapo Idd akajua kuwa tayari mzigo umelewa, “wanasema mimi ni mzuri, hivi ni kweli eeh?” alisema Soraya kwa sauti fulani ya kilevi, huku anainua macho kumtazama Idd, hakumuona Idd mbele yake, zaidi aliona kiti kitupu na chupa ya maji, na hapo Soraya akagundua ukweli kuwa alikuwa amewekewa kitu kwenye ile juice, akapata wazo la kuzimua dawa kwa kunywa maji mengi, na maji pekee ni yale aliyokuwa anakunywa Idd... ENDELEA NAYO
Soraya bila kujua kama yale yaliyokuwa ndani ya chupa sio maji akanyoosha mkono wake na kuchukuwa yale maji huku akianza kuona hata macho yake yanakuwa mazito, akaikamata ile chupa ya maji na kuifungua kisha akasongeza mdomo, lakini kabla hajafikisha ile chupa mdomoni akakutana na harufi kali ya pombe na kuirudisha mezani mara moja, “mungu wangu nisaidie, kumbe huyu Idd anakunywa pombe basi hata humu kwenye juice yeye ndie alieniwekea pombe ili nilewe halafu anifanye anachotaka kunifanya” aliwaza Soraya, huku anachukuwa simu yake mezani, hakuwa na kitu kingine chochote hata mkoba wenye fedha na vitu vingine vilikuwa kwenye gari, “lazima nijitahidi nitoke hapa, nikiweza nichukuwe tax nitalipia nyumbani” alijisema Soraya ambae alizidi kuona hatari ya kuingiliwa kimwili ikimsogelea kwa kasi kubwa sana, kwasababu mwili alijihisi wazi kuwa ameshalewa, “ina maana baba ana yajua haya anayotaka kunifanyia Idd” aliwaza Soraya kwa machungu makubwa sana, huku anajikongoja na simu yake mkononi akieleka kule walikotokea yaani kwenye lango la kutokea hapa Kuchile bar, alijitahidi kujikaza ili asitokee mtu akagunduwa kama amelewa, Soraya akusahau kujiziba uso na ile niqab yake, alipoanza kutembea, “sijui leo nitaokolewa na nani mimi” aliwaza Soraya huku akikumbuka miaka ile alipookolewa na kijana mpole, ambae leo pia alimuona lakini hakufanikiwa kukutana nae.******
Wakati haya yana tokea mida hii ya saa kumi na mbili za jioni, mzee Mahamud yeye alikuwa anamalizia kukusanya mapato yake ya siku na kuelekea msikiti wa mkoa ambako angekutana na bwana Mahadhi Salum, njia nzima alikuwa ana waza jinsi mwanae atakavyoolewa na kijana toka kwenye familia ya kiucha mungu, na yeye jinsi atavyo mfanikishia mwanae mipango ya kimaisha ikiwa pamoja na nyumba nzuri miradi binafsi na usimamizi wa miradi yake, pia kumnunulia gari zuri la kutembealea, “haidhuru akiwa nayo mawili” alijisemea mzee huyu, wakati anashuka na kuingia msikitini, akipishana na bwana Mahadhi aliekuwa amesha maliza kuswali.
Ni kweli mara baada ya swala ya magharib Mahamud alitoka na kumuona bwana Mahadhi aliesimama pale nje anasalimiana na watu wengine waliokuwepo eneo lile, waliokuja kuswali Magharib, “assalaam alaykum” alisalimia bwana Mahamud mara baada ya kuwafikia Mahadhi na wenzake, “hoo! Waalaykum salaam bwana Mahamud” walisamiana wote kwa pamoja huku wakionyesha kumfurahia bwana Mahamud, ambae ndie tajiri pekee pale mjini alie changamana na watu wa kawaida,
Kikawaida bwana Mahamud hakuweza kukatiza maongezi aliyoyakuta, hivyo ilibidi awe msikilizaji wa muda kabla hajasogea pembeni na bwana Mahadhi kuongea mawili matatu kuhusu vijana wao, “halafu mzee Mahadhi, kuna kitu nilisahau jana kukuuliza, hivi gari lako umeliuza, aliuliza mmoja kati ya watu waliokuwa wanaongea na bwana Mahadhi Salum, “hapana kwanini niuze wakati sina uwezo wa kununua gari jingine, au kwasababu hujaniona nalo siku mbili hizi?” aliuliza Mahadhi kwa uchangamfu pasipo kujuwa kama mwenzie alikuwa na maana nyingine kabisa, “hapana bwana Mahadhi sema nililona gari lako sehemu ambayo ilinishtu kidogo, nikasema mbona shekhe ameghafilika” alisema yule mtu na wenzake wakacheka kidogo wakichukulia kama ni swala la utani, “hapana bwana Mabrouk ni mambo ya vijana hayo, siku mbili hizi analitumia yule kijana wangu Idd” alisema Mahadhi, “hooo! hapo saawa maana nililiona pale mtini pub limefichwa kidogo, mh! nikasema shekhe kulikoni tena” alisema Maborouk na wote wakacheka tena, lakini mzee Mahamud akashtuka kidogo, huku Mahadhi akishtuka zaidi maana hakutegemea kama mwanae angefanya jambo la kijinga kama hilo, maana licha ya kujuwa kuwa mwanae ni mnywaji mzuri wa pombe toka amefika songea akitokea south afrika, lakini alimsihi asionyeshe tabia hiyo hadharani, “unajuwa hawa vijana nchi za wenzetu zina wavuruga sana, lakini sina shaka na shekhe atakaa chini na kijana wake, maana tukiwaacha tukosa maimamu wa baadae” alisema mwingine, na stori zikaendelea kabla hawajaagana na kuondoka zao eneo lile, huku bwana Mahamud akikosa la kuongea na Mahadhi na kuondoka zake, japo hakumuonyesha kuwa hakupendezwa na tabia ya kijana Idd, “sasa nime amini kuwa Soraya ni mtoto mwenye akili nyingi sana” alisema Mahamud akiwa njiani anaelekea kwake.******
Naam ilisha timia saa kumi na mbili na nusu, Higgno alikosa amani moyoni mwake baada ya kugundua kuwa mschana alieletewa na shangazi yake ni Joan, ukweli alikata tamaa ya kuwa na mwanamke mzuri, maana aliamini kuwa yeye kama yeye asingeweza kupata mschana mzuri mwenye hadhi yake, kwasababu hakuwa na fedha ya kutosha, kama mschana wa kiwango cha chini kabisa Hilda aliweza kukataa na kumfuata Talib sasa mschana gani angeweza kumpata, “hata kama ni masikini lakini siwezi kuwa na mwanamke kama Joan” aliwaza Higgno huku anatembea taratibu na kijimfuko chake mkononi, akikatiza shule ya msingi sokoine ambayo sasa palikuwa kimya na kuifuata barabara ya kuchile na sio ya kwa sanga one, ile aliyokuja nayo, lengo lake akapandie dala dala kituo cha kilimani, lakini nikipata kazi kwa yule mzee mwarabu nitakuwa na hela nyingi na kupata mschana mzuri nitaishi nae” aliwaza Higgno akiendelea kutembea taratibu.
Naam Higgno akiwa mwenye mawazo mengi alitembea taratibu pembezoni mwa uzio wa bar moja kubwa sana, ambayo hata watu wanao ingia ni wenye fedha nyingi, na alipokaribia lango la kuingilia mara akamuona mschana mmoja alievalia gauni refu zuri lililo ashiria kuwa mschana au mwanamke yule mwenye umbo na kimo cha kupendeza mwenye rangi ya kiarabu mikononi mwake kuwa ni mschana toka kwenye familia tajiri kama sio yeye mwenyewe ni tajiri, akitoka mule bar, “mh! jamani watu wanafaidi, basi na mimi hata nimpate kwenye ndoto tu” aliwaza Higgno ambae aliingiwa na pepo la kutamani kuiona japo sura ya mwanamke yule ambae aliamini kuwa anatoka kupewa dudu ndani ya bar ile yenye guest house, lakini wakati anamkaribia mschana yule ambae alikuwa anatembea kueleka kule alikokuwa anaeleka yeye, akagundua kuwa mschana yule alikuwa amelewa sana, maana hata kutembea kwake kulikuwa ni kwa shida kidogo, kwasababu alianza kuyumba yumba na kusimama akiacha kutembea, akamuona anageuka kama vile kuna kitu anatazama, ndipo alipogundua kuwa mschana yule alikuwa amevaa niqab, “khaaa kumbe amevaa ninja” aliwaza Higgno akijilaumu huku anapunguza mwendo kwa ghafla, lakini alimuona yule mwanamke bado amesimama akimkodolea macho kama vile anamfahamu, nae akapeleka kumbukumbu zake kwa schana mdogo wa kiarabu aliemuokoa siku ile kule TTC matogoro, ““daima… mungu amekuongoza kuniokoa katika matatizo makubwa” Higgno alisikia sauti tamu nyororo toka kwa mwanamke yule aliejiziba uso wake kwa niqab, ambae yeye alichkulia kama mlevi ambae amemfananisha, maana aliongea kama vile wanafahamiana.*******
Unadhani muda huo Idd alikuwa wapi, ukweli ni kwamba Idd alipoona dalili zote za kwamba Soraya ameshaanza kulewa, akaona ni wakati wakuhakikisha chumba kipo tayari na kumshtua yule mwanamke muhudumu wajekumsomba Soraya akajilie kitumbua kipya, ndipo alipoinuka na kuelekea ndani akijuwa kuwa Soraya hatokuwa na uwezo wowote wakutoka pale, kwasababu muda mfupi ujao atakuwa amelewa vibaya sana, na pengine kutokujitambua kabisa, kwasababu mambo kama yale alikuwa ana yafahamu vizuri sana, alishayafanya kwa waschana kadhaa akiwa msumbiji hata afrika ya kusini, na hata akitoka pia asingefika mbali kwasababu licha ya kulewa Soraya asinge kuwa na fedha yoyote ya kumfisha nyumbani kwasababu mkoba wake wenye fedha yeye Idd alikuwa ameufungia ndani ya gari.
Idd alikutana na yule mhudumu wakike ambae alienda kumuonyesha chumba nae akaenda kufanya taratibu za malipo, akitumia kama dakika kumi na tano hivi, kisha akamtuma yule mudumu akamchukuwe Soraya na yeye akatangulia chumbani, “usisahau na chupa yangu, nije niongezee stimu mpaka ajuwe kwanini ina majina mengi kuliko ya kwake” alisema Idd akaimini kuwa Muhudumu atamkuta Soraya na kumletea mule chumbani ajilie kitumbua, yeye akavua viatu na tisht lake kisha akapanda kitandani na kutulia kisubiri kufanya uzinduzi, “nitamuingiza mpaka mdomoni mshenzi huyu” alisema Idd akionyesha kupania kweli kweli.
lakini dakika tano baadae muhudumu yule alirudi na kumueleza Idd kuwa Soraya hayupo pale nje, Idd aliekuwa amesha vua viatu na tisht yake, akavaa haraka na kutoka nje akiwa haamini alichokisikia, “au kuna mtu ameniwahi baada ya kuona amelewa” aliwaza Idd huku anaelekea kwenye gari, maana alijuwa kwa akili ya haraka lazima Soraya angeenda kwenye gari, ili akapumzike baada ya kuona amelewa, lakini alipofika kwenya maegesho ya magari hakuona dalili ya uwepo wa Soraya, uliza kwa watu waliokuwa wamekaa maeneo yale, “oya kuna demu amevaa gauni refu halafu…” hata kabla hajamalizia yule aliemuuliza akadakia, “demu mmoja mkali kinyama, halafu amevalia uninja ametoka kama dakika ishirini zilizopita” mpaka anamaliza kuongea yule jamaa tayari Idd alisha kimbilia nje, akifuatiwa na mhudumu wake, nako hawakuona dalili ya uwepo wa Soraya, “kum.. make kwanini nilimuacha peke yake huyu Malaya” alipiga kelele Idd, huku anakimbia kufuata barabara, huku yule mhudumu ambae ukimuona ungeshindwa kutafsiri umri wake kuwa ni kibibi au kimama, maana kilikomaa sura na mwili, akimtazama kijana huyu aliekimbia kwa mita kama mia na kusimama akitazama mbele pengine angemuona Soraya, lakini inaonyesha hakumuona, maana alirudi tena mpaka pale langoni, “anabahati huyu Malaya, leo angekiona cha mtema kuni, aliongea Idd kwa hasira, huku anaingia ndani ya lango na kueleka pale alipokuwa amekaa akiongozana na yule mwanamke muuza bia
Idd alipofika pale kwenye meza na kukaa kwenye kiti chake, ndipo alipogundua kuwa chupa yake ilikuwa imefunguliwa, na kwamba kama sio kuonjwa basi Soraya aliyanusa yale maji yake na kubaini kuwa ilikuwa ni pombe, maana yalikuwa upande wa kiti cha Soraya ambacho sasa kilikuwa kimekaliwa na yule mwanamke muuza bar, yakiwa yamefunguliwa kizipo chake kwa hasira Idd alichukuwa chupa ile ya maji na kuiweka mdomoni, kisha akagugumia mafunda matatu kwa mkupuo mmoja na kukunja sura kwa maumivu ya uchungu wa ile pombe, “sasa best na mimi niondoke zangu” alisema yule mschana kama vile anamtega Idd, maana alijuwa lazima kijana huyu aliekuwa amepania kula kitumbua, atakitafuta chochote ilimradi asilale bila kula kitumbua, kwanza Idd hakujibu kitu, alichukuwa tena ile chupa na kugugumia tena ile pombe kama alivyofanya mwanzo, kisha akaiweka mezani ikiwa imebakia kidogo sana, akainua uso na kumtazama yule mwanamke ambe rangi ya ngozi yale ilimpendeza na kumvutia, macho na midomo yake ya kusinzia, yaani iliyo legea navyo vilimfanya ajikute anampenda yule dada, “unawahi wapi bwana, kaa hapa unipe kampani” alisema Idd na yule mwana dada akatabasamu, “nikae hivi hivi bila kinywaji?” aliuliza yule mwanamke kwa sauti fulani ya kukwaruza iliyo haribiwa na pombe, sauti iliyompendeza Idd na kumfanya ahisimsisimko mpaka kwenye eneo la chini ya kitofu chake na kuishtua dudu yake, “wewe sasa hivi ni mteja ita muhudumu atuhudumie” alisema Idd huku anachukuwa lile kopo lake la maji na kujimimi nia maji yaliyobakia na kutupa kile chupa chini na yule mwana dada akaita muhudumu.*******
Shangazi alishikwa na fadhaha baada ya kusikia toka kwa kaka yake kisa cha Joan kule maeneo ya Sokoine shule ya msingi, “sasa dada pole kwa usumbufu, wacha nimuwahi huyu kijana kabla hajafika mbali” alisema baba Higgno na kuinuka tayari kuondoka zake, “kwa kweli kaka naomba unisamehe bure tu! maana sikujuwa kama huyu mtoto amebadilika hivi jamani sijui amepatwa na nini” alisema Shangazi kwa sauti ya masikitiko, akijifanya kutokuijua tabia ya Joan, “sio amebadilika huyu ndivyo alivyo toka zamani, hata Higgno anamfahamu vizuri tu! si alisoma nae Luhuwiko” alisema mzee Frank huku anaeleka mlangoni na kufungua mlango kisha akatoka na kuondoka zake, hapo Shangazi akaelekea jikoni, alikowaacha wakina mama Joani, “vipi mwali wako ameingia?” aliuliza mama Joan kwa sauti ya kunong’ona, “amekuja na amesha maliza mchezo” alisema shangazi kwa sauti ya juu, na kumshangaza mama Joan ambae alidhania kuwa bado wakina baba Higgno wapo sebuleni, “watakusikia hebu ongea taratibu, amemalizaje mchezo?” aliuliza mama joan kwa sauti ile ile ya kunong’ona, “watasikia wakina nani, wakati nakuambia wamesha malizana na wameshaondoka” alisema shangazi kwa sauti ya ghadhab na chuki, “sijakuelewa ujue, kimetokea nini kwani?” aliuliza mama Joan kwa sauti ya taharuki, “hakuna cha kuuliza bwana wee!, mwanao amekutana na wegeni anakunywa konyagi huko mtaani na sigara juu anavuta” alisema shangazi kilichobakia tule tunywe tuselebuke” alisema shangazi, na hapo mama Joan akajishika kichwani “mayo neneee Joan, ilikuwaje ukanywa mipombe hadharani mwanangu, ona sasa umekosa mchumba” alipiga kelele mama Joan, wakati huo akamuona Joan anatoka ndani akiwa amevalia suruali yake ya kubana na kijishati kifupi, “sasa mama tutaonana kesho nyumbani” alisema Joan na kuondoka zake, huku mkoba wake ameuning’iniza kwapani, watu wote walimtazama kwa macho ya mshangao na kumsidikiza kwa macho hayo hayo, wakimshuhudia akiondoka zake na kutokomea mtaani, “utakalia hivyo hivyo mshenzi wewe” alisema mama Joan kwa hasira.*****
Ilikuwa hivi dakika saba zilizopita, Soraya akiwa amesha jikongoja kutoka pale langoni, akaanza kuona miguu inakosa nguvu na macho yanazidi kulegea, akajihisi kichwa kina kuwa kizito kama vile anashindwa kukibeba, hata alipopiga hatua kadhaa akaona anapepesuka kidogo, akajiwahi na kusimama “mungu wangu leo nini kinanitokea akinikuta hapa lazima atatimiza unyama wake” aliwaza Soraya huku anatazama kama anaweza kuona gari au pikipiki aikodi, japo hakuwa na uwezo wa kukaa kwenye pikipiki mpaka nyumbani kwao, sehemu pekee anayoweza kufanya malipo, hata akikodi gari alihofia kubakwa na dereva wa gari hilo kwasababu anajuwa wanaume wengi walikuwa wanamtamani.
Hakukuwa na gari wala pikipiki zaidi aliweza kumuona kijana mmoja akija kwa kasi mbele yake, na alipomtazama yule kijana ni kama alipunguza mwendo kwa ghafla, Soraya akatabasamu, “mh! macho yangu au ndio huu ulevi alioniwekea” aliwaza Soraya, sio kwamba kwasababu alimuona yule kijana ila alimuona kijana yule yule aliekuwa anatamani kukutana nae kwa miaka mingi sana, “daima… mungu amekuongoza.. kuniokoa katika matatizo makubwa” alisema Soraya kwa sauti ya kilevi huku ananyoosha mkono kumpatia kijana yule ambae alionekana kusita kumshika mkono kwa maana ya kumpa msaada, akionyesha kutokumtambua wala kumjuwa, Soraya akajiona kuwa alikuwa bado kwenye matatizo makubwa, alitamani kumkumbusha kijana lakini akashindwa maana ndio kwanza alizidi kukosa nguvu na kuyumba akianza kuanguka, hapo kwa umahili wa hali ya juu, yule kijana akamdaka, Soraya alijaa kifuani kwa kijana yule, japo alikuwa amelewa lakini Soraya alihisi msisimko wa ajabu na raha isiyo na kifani kuegemea kifuani kwa mwanaume ambae amekuwa akiomba kukutana nae, “kijana… kijana mpole naomba unisaidie unipeleke nyumbani” alisema Soraya kwa sauti ya kilevi na kufanya kijana yule ambae sisi tunamtambua kuwa ndie Higgno kutoa macho ya mshangao, akiwa kama hamuelewi mschana huyu mwenye sauti nzuri mwenye kunukia marashi, anasema ampeleke nyumbani kwao wapi, na atakujuwaje kwao ikiwa hata yeye mwenyewe hamjuwi, “tuondoke….. tuondoke…. atakuja sasa…. sasa hivi” alisema Soraya kwa sauti ya kilevi, huku nusu ya mwili wake umeegemea kwa Higgno alieshika kijifuko cha zawadi, Higgno akaamua kupiga moyo konde na kuanza kutembea akimsadia yule mwanamke ambae pia alijitahidi kujivuta akionyesha kuwa alihitaji kuondoka mahali pale haraka sana, “halafu… mwenzio baba amesema hiviiii…. amesema niniiiii, henheee amesema hivi, ukiniowa ata tupa nyumba… halafu atatupaaaa… na gari… halafu nanini vileeeee”, aliongea Soraya maneno ambayo Higgno aliyachukulia kama ni maneno ya kilevi.
Kilicho mshangaza Higgno ni aina ya ulevi aliotumia mschana yule mzuri wa mwili alievaa uninja, mwenye kunukia marashi na ngozi ya kiarabu, maana licha ya kulewa kule lakini hakuwa na dalili ya harufu ya pombe, “ndio umeniletea zawadi yangu, aliongea Soraya wakati wana karibia barabara kuu, huku akishika kile kijifuko cha zawadi kwa mkono wake ambao haukuwa na nguvu, Higgno akabakia anamshangaa yule mwanamke ambae kiukweli alikuwa amelewa, “sasa watu si watasema ni Demu wangu” aliwaza Higgno, ambae licha ya usumbufu huu, lakini alijikuta anapenda kutoa msaada ule, “sina kuuliza… we…. wewe kijana mpole, umeniletea zawadi….yangu” aliuliza tena Soraya, na kumfanya Higgno ashindwe kutofautisha ile sauti ni ya ulevi au uchovu au mgonjwa, “hebu! sasa tusubiri gari” alisema Higgno wakiwa wamesimama pembeni ya barabara, sehemu ambayo wakati mwingine hutumika kama kituo cha daladala, “kwani unaitwa nani…..halafu mbo…. mbona hukuja kunitafuta nyumbani……. umekaa siku zote hizo, au umeowa tayari?” japo swali hilo Higgno alilichukulia kama ni la kilevi, kwasababu kuoa kwake au kutokuowa hakumuhusu kitu wala kumsaidia yule mschana wa daraja la juu, lakini Higgno alijikuta amejibu, “bado sijaoa” alisema huku ana tazama kushoto na kulia na kuliona gari moja dogo linakuja na kusimama pembeni yao, “Taxi hii mnaenda” aliuliza dereva wa gari lile, “ndiyo tunataka lift, unafanya shilingi ngapi?” aliuliza Higgno ambae kiukweli hakuwahi kukodi usafiri huu, na leo ndiyo mara ya kwanza, unaenda wapi” aliuliza dereva wa taxi “eti we dada unaenda wapi?” aliuliza Higgno akimtazama Soraya aliekuwa amejiegemeza kifuani kwake, akionyesha mwenye uchovu mwingi sana, “hukujui kwetu……we kijana mpole…..si mjini bwana … hebu acha utani wako” alisema Soraya ambae sijui kwanini aliamini kuwa Higgno alimfuata yeye na alikuwa anamfahamu vizuri! “ingieni, kwa mjini utanipa elfu mbili” alisema Dereva wa taxi huku anashuka na kuwafungulia mlango wa seat za nyuma, Higgno ambae katika safari yake, ilikuwa ni lazima apite mjini ili achukue daladala za matogoro, ndipo aende mahilo kule shambani kwake, alimlipa dereva wa taxi ile elfu mbili kisha nae akaingia pamoja na Soraya, ambapo mwanzo alitaka kukaa seat ya mbele huku Soraya akikaa seat ya nyuma, lakini mlevi Soraya akawa mkali, “kwanini….unakimbia bwana…… njoo tukae wote huku” alisema Soraya kwa sauti ya ukali wakilevi, yenye kudeka ndani yake, “kaka mtoto huyu, umempa nini anaonekana amekoloea kishenzi” alitania dereva wa Taxi, “kaka unadhani hata namfahamu basi mimi nina msaidia tu!” alisema Higgno huku anaingia seat ya nyuma na kukaa pembeni ya Soraya, “basi kama vipi niachie mimi” alisema dereva wa taxi, ambae alijua kuwa Soraya amelewa kiasi cha kushindwa kujitambua…..…. Hatimae soraya na Higgno wamekutana tena, hali ya kuwa soraya yupo matatizoni je nini kitaendeleaaaa? Vip kuhusu Idd kule bar? Endelea Kufuatilia mkasa hapa hapa jamii forums moneytalk