Simulizi: Sumaya fate of love

Janie_Kelvin

Member
Jun 5, 2022
33
51
Ni simulizi inayohusu familia, mapenzi, kazi na safari ya maisha kwa ujumla.
Ungana na mimi katika simulizi hii…..

SEHEMU YA KWANZA

TANZANIA

1995

“Pushhhhhh!!!!!”

“Mrs Hernad jitahidi sukuma mtoto yupo karibu kutoka jitahidi yaani bado kidogo tu.. sukuma!!!”

“Nurse I can’t.. do it anymore… Siwezi nahisi nguvu zinaniishia kabisa “
“Hapana Mrs jitahidi unajua bado…..”kabla hajamalizia hali ya Mrs Hernad ilibadilika ghafla

“Nesi nashindwa…. Aaaaah siwezi..siwe…aaah msaidie mwanangu tafadhali msaid…. Mwana…….”Ghafla akakata moto.Ilikuwa ni taharuki ndani ya chumba hiko cha kina mama kinachojulikana kama labour ward.

Huku nje alionekana mwanaume akiwa amesimama huku kama amevurugwa hata kiti hakikaliki ni kama mwendawazimu alienda mbele na kurudi nyuma akikuna kichwa chake, tai yake ilining’inia shingoni haikueleweka ni staili gani aliifunga kifupi tu alikuwa rafu sana kama mtu aliyechanganyikiwa na pembeni yake aliketi mama ambaye umri wake umeenda yaani ni mtu mzima tayari naye japo alikaa lakini hakuonekana kutulia.Ghafla aliona kitanda cha wagonjwa kikitoka ndani ya labour ward na aliyekuwa akiburuzwa ni mke wake Mrs Hernad ambaye alikuwa akihema kwa mbali tena kwa shida sana, kwa haraka alimfuata daktari mmoja ili aongee nae na daktari huyo alimpa taarifa kuwa haikuwa rahisi kwa mke kujifungua kwa njia ya kawaida hivyo alitakiwa kufanyiwa upasuaji ili mtoto aokolewe kingine alimtoa wasiwasi kuwa wote wawili yaani mama na mtoto wangekuwa salama.Baada ya kusema hayo daktari alimuacha hapo Mr Hernad na kuelekea chumba cha upasuaji naye Mr Hernad alipiga magoti na kusali huku akilitaja jina la Sumaya alimgeukia mama yule ambaye ni mama yake huku naye akimtuliza ili asiwe na papara.Ni katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam pirika pirika za kila siku katika hospitali hiyo kubwa ziliendelea kama kawaida kwani hakukuwa na muda wa kula bata ukiwa hospitalini hapo hakuna daktari wala nesi aliyoenekana kuzembea kwa muda huo.

Huku chumba cha upasuaji kilichojulikana kama thieta, madaktari walizidi kushauriana huku kila daktari akionekana kutoa mchango wake.Huku Mrs Hernad akifanyiwa matayarisho kwaajili ya operation.

“Ni sahihi lakini hii ni win to loose situation, ni lazima tukubali matokeo yatakayo tokea na pia tusikubali kupoteza vyote hapa kuna uwezekano mdogo sana wa kumuokoa mama ni kama asilimia ishirini tu za makadirio ila kuna uwezekano mkubwa wa kumuokoa mtoto ni kama asilimia tisini.So let’s do it”Wote walikubaliana na mawazo ya Dokta Luis ambaye ndiye aliyekuwa akizungumza na Mr Hernad wakati wakitoka labour ward ni daktari bingwa wa mambo yote yanayohusiana na uzazi na saikolojia hakuwa mzembe hata kidogo. Kwa haraka Mrs Hernad alifanyiwa upasuaji ili kuweza kumuokoa mtoto kwa sababu uwezekano wa mama kupona haukuwepo.

Shughuli ilikuwa pevu siku hiyo ni karibia saa nne zilitumika kwenye zoezi hilo, ndipo daktari mmoja mmoja alionekana kutoka ndani ya thieta lakini hakuna aliyethubutu kuzungumza na Mr Hernad kazi hiyo ilikuwa chini ya Dokta Luis, hivyo Dokta Luis alimfuata Mr Hernad na kuongozana mpaka ofisini kwake.Waliketi huku Dokta Luis hakuonesha wasiwasi lakini alionesha sura ya furaha hali iliyompa matumaini Mr Hernad.

“Well… Mr Hernad my super hero hongera sana Mungu amekujalia hatimaye umempata Princess wa Kasri lako, tena mrembo haswa kama mama yake”Alizidi kuonesha sura ya furaha

“Dokta Sijui niseme nini nina furaha sana hatimaye ndoto yangu ya kuitwa baba imetimia.. am… vipi kuhusu Sumaya wangu Dokta anaendeleaje? Naweza kwenda kumuona?”

“Ooh worry out Mr Hernad, unajua ni kipindi kirefu sana umehangaika juu ya jambo hili la kupata mtoto na leo ndoto zako zimetimia amini kuwa Sumaya alikuja kwako kama malaika mkombozi, kukutoa kwenye huzuni uliyokuwa nayo kwa muda mrefu sana lakini ni furaha iliyoleta huzuni pia”

“Ni kweli Dokta sijui nimpe nini kama zawadi yangu kwake Sumaya wangu, Mungu ni mkubwa sana”

“And you know Mr Hernad wanaume siku zote tumeumbiwa moyo wa ujasiri sana tofauti na wenzetu kina mama japo nao ni majasiri sana kwa upande mwingine, am… Mr Hernad I’m very very sorry ilikuwa ni vigumu mkeo kujifungua kwa njia ya kawaida licha ya hayo alipoteza damu nyingi sana lakini ni jambo ambalo hatukuweza kuforce kwani tungewapoteza wote wawili, ukweli mkeo hatupo naye tena Mr Hernad”

Lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa Mr Hernad alikuwa kama mtu aliyemwagiwa maji ya baridi kwenye baridi kali alisimama ghafla kuanza kupiga mikono yake kwenye ukuta kama mwendawazimu naye Dokta Luis kama mtaalamu alimfuata na kuanza kumtuliza ili angalau hasira zake zishuke ili waangalie utaratibu unaofuata.Jambo hilo lilimchanganya sana kwani hakulitegemea kwa wakati huo, licha ya hayo Sumaya alikuwa ni binti mdogo kabisa wa miaka ishirini na mitano tu.

Wakati akitoka katika ofisi ya Dokta Luis ndipo alipomuona mwanadada ambaye alijitanda vizuri mtandio wake kama kujisitiri akija upande wake alimtambua vyema kabisa mwanadada huyo ndipo walisalimiana kisha yule dada alianza kuuliza maswali Mr Hernad mfululizo kutokana na wasiwasi kwa hali aliyoiona kwa Mr Hernad.

“Shemeji kuna nini? Dada ameshajifungua? Vipi mtoto na dada wanaendeleaje? Aah samahani nimechelewa kuja na chakula shemeji nilishindwa kuja mapema kwasababu ya mitihani”

“Aah Usijali Zuleya… hata hivyo chakula hakina umuhimu kwa sasa”

“Kwanini au mmeshamnunulia chakula? Shemeji ongea na mimi”

“Zuleya dada yako hatupo naye tena Zuleya ila mtoto yupo salama kabisa” Aliongea Mr Hernad kwa huzuni na kumfanya Zuleya aangushe kapu ambalo alihifadhia chakula kwaajili ya dada yake ambaye kwa sasa ni marehemu.

“Aaaahhhhhhhhhhh!!!!!!!!”Alipiga ukunga wa maumivu Zuleya kwani ni kama amechomwa na msumari wa moto kwenye moyo wake katika familia yao walibahatika kuzaliwa wawili tu yeye na dada yake ambaye waliishi maisha magumu sana baada ya kufariki wazazi wao kwa mtego kwani ajali ya gari waliyopata haikuwa ya kawaida na ndugu kuwanyang’anya mali zote za wazazi wao na kuwatenga na Sumaya ndiye alikuwa mlezi mkuu wa Zuleya angalau hata mjomba wao alikuwa upande wao kuwasomesha japo hakuwa na kipato kikubwa naye hakuchukua muda alifariki kutokana na maradhi tofauti yaliyomsumbua ndipo Sumaya aliacha chuo akiwa anakaribia kuingia Mwaka wa tatu na kuanza kumuhangaikia mdogo kwake ili asome ndipo alipoonana na Mr Hernad na kufunga ndoa ya serikali, na hapo Mr Hernad alimalizia kumsomesha Sumaya mwaka mmoja uliobaki na kumsomesha Zuleya huku akiwanunulia nyumba nzuri ya kuishi na kumuajiri msaidizi wa kazi ambayo aliishi Zuleya na ndipo maisha yao yalipobadilika na kuwa mazuri tofauti na mwanzo.

Zuleya alimtizama shemeji yake huku uso wake ukiwa umeiva na kuwa mwekundu kutokana na kilio. Machozi tayari yalishalowanisha sehemu kubwa ya mwili wake.

Kwakuwa Sumaya alikuwa ni muislamu hivyo kama ulivyo taratibu zao maandalizi ya mazishi yalianza kufanyika mapema sana na siku iliyofuata Sumaya alizikwa, ilikuwa ni huzuni kubwa sana ni kama kitoto kichanga kilikuwa kinaelewa nini kimetokea kililia mfulilizo huku kikionesha huzuni ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Mr Hernad na wasaidizi wa kazi kumtuliza mtoto huyo ambaye Mr Hernad aliamua kukuaita Sumaya kwani kalifanana sana na mama yake kwa kila kitu hata watu wa nyumbani hapo walishangaa sana jambo hilo.

Mr Gedione Hernad alikuwa ni mfanyabiaahara mkubwa sana ndani na nje ya nchi, masomo yake alisomea nchini Australia katika chuo cha mambo ya siasa Deakin University pia alisoma vilevile masuala ya masoko (marketing) na huko ndipo alipokutana na Dokta Luis ambaye alikuwa akisoma chuo cha udaktari La Trobe University, wawili hao walikutana katika mashindano ya vyuo vikuu nchini Australia katika mambo mbalimbali ya elimu, vipaji na michezo tofauti ndipo walipoonana na kujenga urafiki wao wa kudumu japo Mr Hernad alimzidi Dokta Luis kwa miaka na elimu kwani Dokta Luis muda huo ndio alikuwa akianza masomo yake nchini Australia.Vilevile alikuwa ni kiongozi mwenye madaraka serikalini naam alikuwa ni Waziri wa mambo ya nje lakini kabla ya kushika wadhifa huo alipitia nafasi mbalimbali za uongozi na mwisho kuwa Waziri wa mambo ya nje.Pia alimuoa mwanamke na kuishi naye.Hakuna ambaye alikuwa hamfahamu Mr Hernad kwa sifa zake upendo ustaarabu na moyo wa huruma na kutoa lakini miaka mitano ya ndoa yake mke wake alifariki bila kuwa na mtoto, aliishi maisha hayo kwa miaka karibia mitatu alipata mwanamke mwingine na kumuoa naye alikuwa na matatizo ya uzazi hivyo hawakubahatika kupata mtoto katika miaka mitatu ya ndoa yao. Suala la mtoto lilimsumbua sana akili Mr Hernad huku familia yake ikihangaika huku na huko kumuombea Mr Hernad japo apate mtoto na ndipo mke wake alipomruhusu atatute mwanamke ambaye angeweza kumpa watoto kuliko kuendelea kusononeka jambo hilo hata familia yake ililiafiki na ndipo alipokutana na Sumaya na kufunga nae ndoa ya serikali kwa wakati huo Mr Hernad alishafikia umri wa miaka arobaini huku mwaka mmoja kupita kwenye ndoa yao alipata ujauzito, ni kama neema iliingia katika familia ya Mr Hernad naye hakuruhusu mke wake huyo Kufanya chochote hata kujikuna yaani alikuwa akimlea kama yai Sumaya aliishi kama malikia huku daktari wake alikuwa alimfuata nyumbani kwa vipimo vyote na mazoezi alifanyia hapo hapo nyumbani kwani kulikuwa na kila kitu.Mapenzi ya Mr Hernad kwa Sumaya yaliongezeka mara dufu mpaka alifunga CCTV Camera chumbani kwake ili muda wote amuone mke wake kipenzi.

Hayo Ndio maisha ya Mr Hernad aliyepitia changamoto kadhaa kwenye maisha yake licha ya kuwa na pesa za kutosha na kugundua kuwa pesa haiwezi kununua furaha katika maisha bali furaha unaipata kutoka kwa watu wa karibu na kutoka kwako mwenyewe na aina ya maisha unayoishi uwe na masikini au tajiri unaweza kutengeneza furaha yako mwenyewe unaweza ukawa na kila kitu katika maisha ukawa tajiri na ukakosa furaha lakini masikini ambaye hawezi hata kupata milo mitatu kwa siku akawa na furaha kwenye maisha yake.


2000

Ilipita miaka mitano na tayari Sumaya alikua na alishaanza shule, mtoto huyo alipendwa sana na Mr Hernad Kwani halikuwa jambo rahisi kupata mtoto kwake hivyo alimlea kwa mapenzi yote Princess wake huyo mmoja na wa pekee kwenye maisha yake.Hakuwahi kumjua mama yake ila mke wa Mr Hernad Bi Rahel ndiye alikuwa akimlea kama mama yake na yeye alijua kuwa huyo Ndio mama yake mzazi licha ya kuwa hawakufanana hata chembe.

Mr Hernad aliongea na mama yake pamoja na mke wake na kuwaambia lengo lake na kutaka kumpeleka Sumaya Jamaica ili akasome huko lakini alipendelea aende na mama yake mdogo Zuleya japo walijaribu kupinga hilo lakini alishikilia msimamo wake Ila hakuna aliyetambua kuwa licha ya Mr Hernad kuamua hivyo moyoni aliumia sana kuwa mbali na Princess wake Sumaya wake wa pekee aliyebaki katika huu ulimwengu uliojaa mambo tofauti ya kila aina.

Mwezi mmoja ulitosha kwaajili ya maandalizi ya Visa ya Zuleya na Sumaya pamoja na kila kitu muhimu kilichohitajika kwenye safari hiyo na hatimaye Zuleya na Sumaya waliiacha nchi ya Tanzania na kwenda Jamaica.

Mr Hernad alibaki na huzuni kubwa sana baada ya Sumaya kuondoka kwani uwepo wake kwenye maisha yake ni kama faraja kubwa sana ambayo aliikosa kwa muda mrefu sana.

“Mwanangu hivi unaona maamuzi uliyofanya ni sahihi?”

“Mama hayo ni maamuzi niliyoamua mwenyewe kutoka moyoni”

“Hata kama Gedione ni maamuzi yako Ndio sasa kama yametoka moyoni mbona unaumia sana?”

“Hapana mama nipo sawaa”

“Gedione mimi ni mama yako na nakujua vizuri sana kuliko mtu yeyote hata marehemu baba yako hakukujua kama mimi hivi”

“Mama najua hilo Ila nimeona ndo njia pekee ambayo itamsaidia pia Sumaya maana hata wewe unafahamu magumu niliyoyapitia mama japo huko nje naonekana kuwa na furaha.Sina amani mama tokea Sumaya binti mdogo kabisa kuniacha mwenyewe”

“Najua Ged usiwaze sana najua ulimpenda sana Sumaya kuliko kitu chochote ni kama Sumaya alikuwa zawadi ya kwako lakini zawadi ambayo haikudumu”

“Ni kweli mama na mimi ndiye nilikuwa mwanaume wa kwanza kwa Sumaya lakini nimesababisha haya yo…”

“Shii!!! Gedione tema mate chini mwanangu futa kabisa hiyo kauli kichwani kwako kuwa mwanaume wa kwanza kwa Sumaya sio sababu ya hayo yote kutokea.Ila tambua mimi Nakupenda sana mwanangu hata Rahel anakupenda sana na anaumia kukuona katika hali kama hiyo na kushindwa kukuzalia”

Yalikuwa na maongezi marefu sana lakini yaliyotengeneza taswira mpya ndani ya akili ya Mr Hernad angalau alipata ahueni na kuwa mchangamfu.

Kila siku iliyoitwa leo Mr Hernad aliwasiliana na binti yake wa pekee huku mali zote alizonazo aliandika jina la binti yake Sumaya Gedione Hernad kuwa mrithi wake.

Maradhi ya uzee yalianza kumsumbua mama yake Gedione hivyo kupelekea kuwa tu kitandani huku akiwa hajiwezi na mtu pekee aliyetoa msaada wa hali na mali ni Bi Rahel kwani ndiye mkwe wake, lakini naye Mr Hernad hakuwa nyuma kumsaidia mama yake kwani ndiye mtu pekee aliyemlea sana kuliko hata baba yake aliyekuwa akuhangaika na maisha kutwa kucha na asiijali familia yake hata pale umauti ulivyomkuta.Mama Gedione hakubahatika kupata mtoto mwingine zaidi ya huyo mmoja kwani maisha yao ya zamani hayakueleweka hata mume wake hakuwa akijali hilo muda mwingi alikuwa mbali na familia yake mara chache sana alirudi na kuchungulia kisha angeondoka na kwenda kula bata alikokuwa akikujua yeye maisha yake yalikuwa ya starehe sana kuliko kutulia na familia yake hata kusoma kwa Gedione kulikuwa kwa shida sana na ndo maana Gedione alipambana kwa hali na mali ili familia yake isije kuteseka kama walivyoteseka na mama yake.

Lakini mwisho wa siku hakuna kitakachodumu milele, mama yake Gedione alifariki ni kama Mr Hernad alizidi kupoteza watu wa muhimu sana kwenye maisha yake ambao Ndio faraja kwake siku zote.Hata Sumaya na Zuleya walikuwepo pia kwenye msiba huo wa mtu muhimu sana kwenye maisha yao.



JAMAICA


2005

“Mama where you? I’m here….. Mama Zuleya niko hapa?”Ilikuwa ni sauti nzuri ya binti mrembo Sumaya Hernad

“Aah toto you are here… I’m so happy”Akimkumbatia kwa upendo, “ My only daughter Sumaya you remind me about something past, I only have Sumaya who gave me happy but now I also have only one Sumaya who give me happy.I love you “

“Binti yangu wa pekee Sumaya unanikumbusha kitu nyuma nilikuwa na Sumaya mmoja ambaye alinipa furaha lakini sasa pia nina Sumaya mmoja ambaye ananipa furaha.Nakupenda”

“Mmh Mama penda pia”

Sumaya msichana mrembo ambaye urembo wake ulijidhihirisha akiwa bado mdogo alikuwa ni mrefu wa wastani mwenye mwili wa kawaida si mwembamba sana wala mnene, macho makubwa ya wastani na mdomo uliojichora vizuri sana huku shavuni akipambwa na vishimo ambavyo viliongeza uzuri wake maradufu.

Walikuwa wakiishi wawili tu kwenye nyumba na wao hawakuacha kuzungumza kiswahili mara chache hiyo iliwafanya wazungumze Kiswahili muda mwingine japo hakikuwa kizuri sana hasa upande wa Sumaya ambaye aliondoka Tanzania akiwa bado mdogo sana lakini pia muda mwingine walizungumza lugha ya asili ya kijamaica ni kama krioli kwa wajamaica iliyojulikana kama Patois kwa namna fulani waliuzoea sana utamaduni wa Jamaica hasa Sumaya ambaye alikulia huko.

Maneno aliyoyaongea Zuleya kwa upande fulani yaliwasha taa ya njano kwa mtoto Sumaya na kuwaza Mama yake huyo alikuwa na maana gani mpaka kumwambia maneno hayo.Katika nchi ya Jamaica ndani ya jiji maarufu Kingston na ndio mji mkuu wa Jamaica ndipo Zuleya aliishi na mwanaye Sumaya na kupatiwa nyumba ya kuishi na rafiki mkubwa wa Mr Hernad ambaye walikuwa wakiishi wote Australia, Sumaya alisoma shule maarufu na iliyojulikana sana ndani na nje ya Jamaica Allman Town Primary School.Alikuwa ni mwanafunzi mwenye akili na bidii sana darasani hata walimu na wanafunzi wenzake walishangazwa sana na uwezo mkubwa alionao Sumaya mara nyingi alipokea tuzo mbalimbali kama mwanafunzi bora.Alikuwa pia na rafiki yake aliyeitwa Lukas naye ni mtanzania na huyo ndiye aliyekuwa rafiki wa pekee kwake waliambiana mambo mengi ambayo walikuwa wakiambiana kila mmoja wao akipata tatizo.Siku iloyofuata Sumaya hakutoka ndani wakati wa mapumziko lakini Lukas alijua tu kuwa rafiki yake huyo ana shida alimfuata iliongee nae.

“Lukas!!!”

“Yow!! Wadup?”Aliuliza Lukas kwa lugha ya Patois akimaanisha “Hey What’s up” yaani anaendeleaje lakini Sumaya alionekana mnyonge sana

“I know you Sumaya it’s like we shared the same blood uko vipi?”

“Lukas it’s true niko na problem.It’s about family issues”

“If possible you can let me know and look a possible solution that can be helpful you are my friend best friend”

“Unajua Lukas in my family me and my mom Zuleya are only Islamic even my dad and my mom are christians also I wonder I’m not familiar with my dad and mom but I look familiar with mom Zuleya, why?”

“Mmmmmh”Alivuta pumzi kijana Lukas akiwa amemuelewa kabisa Sumaya “But Sumaya mmh I guess there is something wrong about this issues what if mom Zuleya is your biological mother?”

“How this can be possible Lukas and if this is true why they are not make me aware about this?”

Akili yake sasa ilizidi kuchangamka kutokana na maneno aliyoambiwa na Lukas naye aliapa kutoliacha hilo lipite hivi hivi, aliona atafute muda mzuri ambao yeye na mama yake mdogo watakuwa free kuongea kwasababu muda mwingi Zuleya alikuwa busy na kazi zake hospitalini naye Sumaya busy na shule hivyo sio rahisi sana kupata muda wa kukaa pamoja labda mwisho wa wiki lakini napo sio siku zote, mtoto huyo wa miaka kumi alionekana kuwa na akili ya kuchumbua mambo zaidi na kuyafikiria sana kuliko hata umri wake jambo ambalo hata mtu mzima hawezi kutambua hilo.Lakini alijitahidi asioneshe hilo kwa Mama yake lakini damu ni nzito kuliko maji Zuleya aliitambua vema hali aliyonayo Sumaya nae alificha hilo mpaka atakapo pata nafasi ya kuzungumza nae kwa uzuri zaidi na hata hivyo tabia za Sumaya hazikuwa tofauti sana kama marehemu mama yake na hiyo ilikuwa rahisi sana Zuleya kutambua kwa haraka tatizo lolote alilonalo Sumaya.

ITAENDELEA………
 
SUMAYA FATE OF LOVE

SEHEMU YA PILI


Lakini alijitahidi asioneshe hilo kwa Mama yake lakini damu ni nzito kuliko maji Zuleya aliitambua vema hali aliyonayo Sumaya nae alificha hilo mpaka atakapo pata nafasi ya kuzungumza nae kwa uzuri zaidi na hata hivyo tabia za Sumaya hazikuwa tofauti sana kama marehemu mama yake na hiyo ilikuwa rahisi sana Zuleya kutambua kwa haraka tatizo lolote alilonalo Sumaya………..


ENDELEA…………..



Ni jumapili tulivu wakiwa katika mandhari yaliyovutia sana katika fukwe ya bahari Zuleya na Sumaya huku wakiwa wameshikana mikono kila aliyewaona hakusita kusema kuwa walikuwa ni mama na mtoto kutokana na kufanana kwao mikononi walishika ice cream.Walitembea kwa hatua kadhaa ndipo walipopata sehemu nzuri na kuketi, baada ya kumaliza ice cream zao ndipo Zuleya alipoanzisha mazungumzo.

“It’s been a long time since we came here for refreshment my dearest daughter Sumaya”

(Ni kipindi kitefu tokea tuje hapa kwa kujiliwaza binti yangu mpenzi Sumaya)

Alitabasamu Zuleya huku akimtizama Sumaya kwa upendezi wa hali ya juu na kumfanya Sumaya aone aibu za kitoto kwa mama yake huyo

“Mama I have…….” (Mama nina….)

Kabla hajamaliza kuongea Zuleya alimziba mdomo na kumkumbatia

“Najua kama haupo okay Sumaya, tell me what’s your problem?”

“Mom…..why don’t I look familiar with my mom and dad?? But I look familiar with you? It’s true that you are my biological mother? And if not who are you what do you mean to me?.Why me and you are Islamic and others are Christian? Tell me why mom Zuleya” (Mama.. kwanini sifanani na mama na baba yangu?? Lakini nafanana na wewe? Ni kweli kwamba wewe ni mama yangu mzazi? Na kama sio wewe una maana gani kwangu?.Kwanini mimi na wewe ni waislamu na wengine ni wakristo? Niambie Kwanini mama Zuleya)

Swali hilo lilimshitua sana Zuleya hakutegemea kuulizwa swali kama hilo kutoka kwa mtoto huyo

“Oooh well Sumaya Mr Hernad and Mrs Hernad are your biological parents.I’m not your biological mother Sumaya but I’m your aunt as you calling me”
(Ooh vizuri Sumaya Mr Hernad na Mrs Hernad ni wazazi wako.Mimi sio mama yako mzazi Sumaya lakini ni mama yako mdogo kama unavyoniita)

“But mom Zuleya……” (Lakini mama Zuleya…..)

“Shiii!!!!!! Sumaya wachana na hayo mawazo”Alimkumbatia kwa upendo.

Baada ya kukaa kwa muda waliona ni wakati mzuri wa kurejea nyumbani, walielekea kwenye gari na kuondoka.Lakini kitu cha kushangaza baada ya kufika nyumbani walikuta mgeni nje na wote walimfahamu vizuri sana mgeni huyo, baada tu ya kushuka kwenye gari yule mgeni alimfuata Zuleya kwa hasira na kumshika mkono huku akitaka kumfokea lakini Zuleya alimtuliza na kumwambia asubiri afungue mlango waende chumbani kuliongea hilo hata hivyo kulikuwa na mtoto, ilimbidi awe mvumilivu na ndipo walipoingia chumbani lakini haukupita muda mrefu zilisikika kelele za Zuleya akilia na baada ya Sumaya kusogea jirani na mlango wa mama yake mdogo alisikia pia kelele za mtu akifoka kumfokea Zuleya.

“Where have you been Zuleya? And you didn’t pick up my phone, you just think am I crazy Zuleya?”

(ulikuwa wapi Zuleya? Na hautaki kupokea simu zangu, unadhani mimi ni kichaa Zuleya?)

“But Dajuan I didn’t do anything bad….”

(lakini Dajuan sijafanya kitu chochote kibaya..)

“Shut up Zuleya, you didn’t care about it now a days you just doing at your own……you cared much your own things”

(kelele Zuleya siku hizi haujali kuhusu hiki unafanya vitu upande wako tu….unajali sana vya vitu vyako)

“Dajuan I didn’t mean that….. I just want to spend a day with my daughter because most of the time I didn’t get a chance to be with her like today”

(Dajuan sijamaanisha hivyo…. Nilitaka kutumia siku hii na binti yangu kwa sababu mara nyingi sipati nafasi ya ya kuwa na yeye kama leo)

“Liar!!!!!!!!”(Muongo!!!!)

Alianza kumpiga Zuleya, Zuleya alilia kilio cha maumivu hata Sumaya alisikia uvumilivu ulimshinda Sumaya alianza kugonga mlango kwa hasira na hatimaye ulifunguliwa na Dajuan ndiye alitoka ndani kwa hasira Na kuelekea sebuleni kwa nia ya kutaka kuondoka lakini Sumaya alimuita kwa nyuma.

“Yow bro!!!…..” Dajuan aligeuka nyuma na kumtizama Sumaya

“How dare are you”(unathubutu vipi?)

“Simama hapo hapo.Mwanaume huna haya wewe huwa nakuangalia tu kila siku ukija hapa na unampiga na kumfokea Mama kila siku unakuja kwa shari.Sikupendi nakuchukia, nampenda sana mama Zuleya na namthamini sana kama wewe hujui thamani yake naomba umuache.Upo kwaajili ya pesa tu unachukua pesa zake na bado una mpiga”Aliongea Kipatois huku akiwa anamaanisha kile ambacho alikuwa akikisema.Hata Zuleya chumbani alisikia na kujiuliza Sumaya amepata wapi ujasiri wa kuzungumza na Dajuan hivyo wakati yeye hakuthubutu hata kutia neno alitoka chumbani na kumfuata Sumaya

“Wah gwaan Sumaya?” “Nini kinaendelea Sumaya” “please stop…….Enough!!!!”

(Tafadhali acha….. inatosha!!!!)Aliongea Zuleya akionekana mwenye wasiwasi sana kutokana na hali aliyoikuta sebuleni

“Mom please leave me, I hate this guy mom i wish i could be stronger and fight him but I don’t have such power”

(mama tafadhali niache, namchukia huyu mtu natamani ningekuwa mwenye nguvu nipigane nae lakini sina hizo nguvu)

“But he is your da….”(lakini ni ba..)

“He is not mom…. Never he can’t be my dad”

(sio mama…… kamwe hawezi kuwa baba yangu)Aliongea kwa ujasiri mpaka kila mtu alishangaa ujasiri wa Sumaya kuongea hivyo na bado alimgeukia tena Dajuan

“Dajuan siwezi kuwa na baba ambaye kila siku ana mnyanyasa mama yangu ondoka nyumbani kwetu”

“Zuleya hivi ndo umeamua si ndio Kwahiyo umemtuma mwanao anidhalilishe tena mbele yako ukishuhudia”Aliongea kwa lugha ya Patois

“Mama mwambie ukweli kuwa humtaki huyu mwanaume hakupendi anatumia pesa zako tu mwambie”naye Sumaya alimgeukia mama yake na kuongea kipatois

“Enough Sumaya!!!!!!!!! Dajuan leave my house please, right now”

( Inatosha Sumaya!!!!!! Dajuan ondoka nyumbani kwangu tafadhali, sasa hivi)

“Zuleya…..”

“I said leave Dajuan..!!”

(nimesema ondoka Dajuan)

Sumaya alielekea mlangoni na kumfungulia mlango Dajuan ambaye alitoka huku akiwaangalia kwa hasira wawili hao.

Dajuan alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu sana wa Zuleya kwa karibia miaka minne tokea wafike nchini Jamaica ni mzawa wa Jamaica lakini alikuwa akimnyanyasa sana Zuleya kwa kumpiga na kumfokea kila alipoenda nyumbani kwa Zuleya, hakuwa na kazi ya kueleweka hivyo muda mwingi aliutumia kuvuta bangi na kunywa pombe wakati huo pesa alizokuwa akizitumia alizichukua kutoka kwa Zuleya mara nyingi alikuwa akimlazimisha ampe pesa hata nusu yote ya mshahara wa Zuleya alichukua na kwenda kufanyia starehe zake.Lakini Zuleya alimpenda sana mwanaume huyo licha ya kuchoka na manyanyasiko aliyokuwa akiyapata japo kadri muda ulivyozidi kwenda upendo kwa Dajuan ulipungua lakini bado alimpenda kwa kiasi hiko hiko ila shida ilikuwa upande wa Sumaya aliyekuwa akishuhudia manyanyaso aliyokuwa akipewa mama yake na kuamua kufanya jambo ili kumsaidia mama yake na hiyo ndio aliona njia ya pekee ya kumsaidia kwani hakuwa na nguvu za kupambana na Dajuan hata hivyo alimjengea mama yake wakati mgumu sana juu ya alichokifanya mbele yake na yeye akidhani ana saidia.

“Sumaya what have you done??”

(Sumaya umefanya nini)

“I’m tired…. Mom I’m tired and I’m not scared about him anymore.He is bullying you mama every day”(nimechoka… mama nimechoka na simuogopi tena.Anakuonea mama kila siku”

“But he didn’t deserve it Sumaya, you are young and can’t understand it just leave it as it is”( lakini hakustahili hiki Sumaya, wewe ni mdogo na huwezi kulewa hiki kiache kama kilivyo)

“He deserve it mom…. Weh yuh ah deal wid?” (Anastahili hiki mama…. Utafanya nini na hili?)

Aliongea kwa hasira na kumuacha mama yake hapo kisha naye akaenda chumbani kwake na kujitupa kitandani huku akilia.Zuleya alitambua ni kiasi gani Sumaya aliumia kutokana na jambo lililotokea muda mfupi uliopita alijifikiria na kumfuata chumbani kwake japo aongee naye labda wanaweza kuelewana.Alipofika mlangoni alikuta mlango upo wazi hivyo alichungulia na kumuona Sumaya akiwa amelala huku akilia alitaka kuingia lakini alisita kutokana na hali aliyokuwa nayo Sumaya kwa wakati huo, aliona amuache kwanza mpaka atakapo tulia na kupata chakula cha jioni ndipo waongee jambo hilo.

Hata Zuleya alipoandaa chakula Sumaya hakuthubutu kushuka chini kwaajili ya kwenda kula hata kwa upande wa Zuleya hakuweza kula bila ya kujumuika na mtoto wake hamu ya chakula iliisha kabisa na ndipo akapanda juu kuelekea chumbani kwa Sumaya na sasa alimkuta ametulia kidogo hata kuongea anaweza alisogea taratibu mpaka kitandani na kuketi pembeni ya Sumaya, aliishia kumtizama tu asipate ujasiri wa kuongea neno lolote.

“Mom…”Aliita Sumaya “I’m so……”

“Shii!!!…. Sumaya I know what have you been through, hata mimi nina huzuni sana my dear”

“Nilikuwa na hasira sana.. it’s just a temper, kutokana na kilichotokea na vyote ambavyo vinatokea.Nakupenda mama siwezi vumilia kwa yote unayopitia mama aah najua…..”

“Inatosha Sumaya najua umeumia sana mwanangu nakuahidi haitatokea tena, sipendi kukuweka katika situation kama hii”Alimkumbatia na kumfuta machozi yaliyokuwa yakitiririka katika mashavu yake.

“Pramise … mom?”

( unaniahidi mama?)

“Mi pramise yuh my daughter”

( nakuahidi binti yangu)

Walishuka chini na kujumuika pamoja kupata chakula huku Sumaya akikisifia chakula kilichopikwa na mama yake kuwa kilikuwa kitamu sana pia utani wa kawaida uliendelea wakati wakipata chakula ilikuwa ni nyumba yenye watu wawili tu lakini kulikuwa na furaha muda mwingi.

Nchi ya Jamaica ilisifika sana kwa uzuri wake wa mandhari ya kijiogragfia kama bahari na fukwe zinazovutia, milima, misitu ya kiasili, maporomoko ya maji na sehemu mbalimbali zinazovutia kwa starehe na kufurahi hivyo kuifanya Jamaica kupendeza zaidi na kujulikana kama taifa la kisiwa cha Caribbean(Caribbean island nation) kutokana na kuzungukwa na bahari ya Caribbean,Ni nchi inayojitegemea iliyopo bara la America, America ya kaskazini huku ikiwa imezungukwa na bahari ya Caribbean.Kitu kingine kikubwa kinachotambulisha Jamaica ni nchi ambayo muziki maarufu wa rege ulizaliwa na msanii maarufu aliyejulikana dunia nzima kwa kuimba muziki huo wa rege, Bob Marley alizaliwa hapo.Na pia hata mavazi ya asili ya Jamaica yalikuwa ni ya kuvutia sana hasa kwa wanawake hata hivyo walikuwa na tamaduni zao husika kama ilivyo kwa kila nchi kuwa na tamaduni kama ilivyo nchini Tanzania Kwahiyo ni kawaida kwa kila nchi kuwa na tamaduni, mila na desturi pamoja na miiko.


* * *
Nchini Tanzania ni kipindi ambacho Mr Hernad alishastafu na alikuwa na nguvu angalau za kuendesha biashara zake bila shida, ni muda ambao alikaa kwenye bustani yake ya maua akisoma kitabu cha siasa ya dunia ambacho kiliandikwa kwa lugha ya Kiingereza taratibu akishushia na kahawa yake aliyoipenda hasa Sumaya alipokuwa hai alikuwa akimtengenezea kila siku, alipenda sana maua na pia kuna kumbukumbu fulani za maisha ya nyuma kila akaapo kwenye hiyo bustani kubwa zaidi ni binti mrembo Sumaya aliyemuheshimisha na hatimaye kuitwa baba, mwanzoni wakati anaijenga nyumba yake bustani yake ilikuwa ya kawaida sana na maua machache kwani hakuwa mtu wa kupenda sana maua lakini alipomuoa Sumaya bustani ilianza kupendeza kwa kuongezwa maua mbalimbali yaliyovutia zaidi na ndipo Mr Hernad alianza kupenda maua na kuanza kuitunza bustani hiyo.

“Ni miaka kumi imepita tokea uniache Sumaya wangu, still Nakupenda sana siwezi kukusahau, siwezi kusahau huba lako Sumaya ulinifanya nijivunie kuwa mwanaume na nikaitwa baba, baba Sumaya……”Wakati akiendelea kutafakari hayo alimuona mtu akija kwake alionesha tabasamu baada ya kumuona mtu huyo na kusimama kwaajili ya kumkaribisha.

“Mr Hernad I’m so happy to meet you”

(Mr Hernad nina furaha sana kukutana na wewe)

“Aah Mr Khaleed Karibu sana” Akimkaribisha kiti ili akae

“Asante sana” Akiketi “Habari za siku rafiki yangu”

“Salama tu za hapa nyumbani, Vipi wote wazima lakini”

“Tunashukuru Mungu anasaidia Khaleed”

Mr Hernad alimuagiza mtu alete kinywaji kwaajili ya mgeni huyo wa muhimu sana, na baada ya muda mfupi kinywaji kililetwa huku kikiambatana na biskuti.Mr Khaleed alikaribishwa na kisha mjadala uliomleta ulianza.

“Kuna kitu muhimu sana Mr Hernad cha kuzungumza mimi na wewe tu na ni lazima kiwe siri”

“Mmmh kitu gani tena?”

“Hivi Gedione unaweza kuamini kuwa kuna mtu anakufuatilia na pia anataka kufuatilia nyaraka zako za muhimu sana?”

“Khaleed inawezekana vipi hiko kitu?”

“Amini usiamini ila ukweli ndio huo na inaonekana anayekufuatilia hatoki mbali na ni moja ya familia yako na pia sidhani kama yupo pekeyake kuna mtu nyuma yake”

“Hili ni jipya kabisa kwangu”

“Unajua una biashara nyingi sana na pia nyumba magari na mali nyingine za thamani, kuna yeyote umemdokeza kuhusu kuandikisha mali zote kwa mtoto wako?”

“Hapana hata Rahel sijamwambia mtu pekee ambaye nilimwambia ni mama na tayari ameshafariki lakini Rahel nimeshampa umiliki wa hii nyumba pamoja na magari mawili ila nyumba zote tatu zilizobaki na magari yote pamoja na biashara ni kwaajili ya binti yangu”

“Vizuri hilo Ndio msaada kwako usimwambie yeyote mpaka wakati sahihi utakapowadia.Unajua mimi ni mwanasheria wako na nimekuhudumu kwa muda sasa naelewa vingi Gedione”

“Lakini ni lazima tuanze kufuatilia mapema ili tujue ni nani”

“Ni kweli lakini halihitaji papara jambo hili, hata hivyo sio rahisi kufanikisha hili na hata hivyo tumeshashtukia mchezo ila hata baadhi ya mienendo na safari zako hawatakiwi kujua sana maana italeta matatizo”

“Sawa tutazidi kuwasiliana”

“Lakini Mr Hernad why Jamaica? Na sio nchi nyingine? Mbona kuna nchi ambazo wanatoa elimu kwa kiwango cha juu sana kama Marekani, Australia, Ufaransa na nchi nyingi tu”

“Aaah Khaleed unajua nimeona ni kawaida tu halafu naipenda sana Jamaica mandhari, tamaduni zao and all about that Country I don’t know why?”

“But it’s good sio mbaya kama umepapenda”

Waliagana na Mr Khaleed aliondoka lakini alimuachia mawazo sana Mr Hernad juu ya jambo hilo zito alilomueleza hata hamu ya kuendelea kukaa bustanini iliisha alichukua vitu vyako vya muhimu na kuelekea chumbani huko alimkuta mke wake ambaye alionekana akimdadisi sana na kumuuliza

“Upo Sawa kweli mume wangu? Halafu ni kama nimemuona Mr Khaleed?”

“Nipo Sawa mke wangu, ni kweli nilikuwa na Mr Khaleed kule bustanini ila ameondoka”

“Mmh mlikuwa mnaongea nini bustanini na ukashindwa hata kumkaribisha ndani mgeni mume wangu?” Aliongea huku akionekana kutopendezwa na hilo, alifikiria kwa muda na kukumbuka onyo alilopewa na Khaleed kuwa iwe siri yao na asimwambie mtu yeyote

“Aah Hakutaka kuingia ndani hata hivyo alihitaji fresh air, usiwe na wasiwasi tulikuwa tunaongea kuhusu biashara”

Alimsogelea mke wake na kumbusu kisha akajitupa kitandani mke wake alimuangalia kwa muda na kuendelea na mambo yake.

Zilipita siku chache na Mr Hernad hakuonesha wasiwasi wowote huku akiwasiliana na Mr Khaleed na kupanga mipango yao kimya kimya.Ni siku ambayo hakuweza kwenda kwenye biashara zake na kupumzika nyumbani kama kawaida akiwa kwenye bustani yake aliyoipenda sana ghafla simu yake ilianza kuita na kuangalia mpigaji kisha akaipokea na kuweka vyema sikioni.

“Hamna shida nakuja sasa hivi nipe dakika 30”

Simu ilikata na aliinuka na kuelekea chumbani ili ajiandae, mke wake alishangaa kwa sababu asubuhi alimwambia kuwa haendi kazini lakini muda huo anajiandaa ili aondoke lakini alimjibu tu kifupi kuwa kulikuwa na dharura na alihitajika haraka.

Kama alivyoomba baada ya dakika 30 alikuwa ameshawasili eneo husika ni katika Hospitali ya Aga Khan moja kwa moja alielekea katika ofisi ya Dokta Luis, baada ya salamu maongezi rasmi yalianza huku Dokta Luis akianza na samahani kwa Mr Hernad kwa kumuharibia muda wake na pia kwa atakachomwambia kwa wakati huo naye Mr Hernad aliipokea kwa moyo wote asijue ni kipi Dokta Luis alikuwa akimaanisha.

“Unajua wewe ni kaka yangu tokea tupo Australia ile siku tuliyokutana kwenye mashindano nilipopoteza wallet yangu yenye nauli na wewe pekee ukanijali na kunipatia nauli, uliacha alama kubwa sana moyoni mwangu Mr Hernad najuta kwa kushindwa kurejesha fadhila hizo”

“Unazungumzia nini Dokta Luis hayo mambo yameshapita wewe ni ndugu yangu tumeshare vitu vingi sana”

“Ni kweli Mr Hernad ila lazima nikuambie hili, miaka kumi imepita nilishindwa kumsaidia shemeji yangu wakati akiwa anajifungua na kupelekea kupoteza maisha na wakati nilikuwa nikitambua ni kiasi gani ulimpenda ni kiasi kikubwa sana kisichokuwa na mfano”

“Luis huu Sio muda wa kujilaumu ulikuwa ni mpango wa Mungu ni kweli nilimpenda sana na nitaendelea kumpenda”

“Kaka, siku ambayo Sumaya alikuja hapa kwaajili ya kujifungua haikuwa nzuri kwa upande wake”

“Una maanisha nini Dokta? Sijakuelewa vizuri”

“Ni dhahiri kuwa mkeo kuna dawa au niseme sumu kwa lugha nyingine alipewa na aliyempa alidhamiria kuwaondoa wote wawili yaani mama na mtoto wakati wa kujifungua na ndio maana aliwahi zaidi kupata uchungu kabla ya muda”

“Whaaaaaat!!!!!!!!” Alishituka

“Yeah! Lakini japo kuwa tulishindwa kuwaokoa wote ila angalau tulifanikiwa kumuokoa mtoto kuliko tungewakosa wote”

“Luis una..una…una uhakika na hili jambo?”

“Kaka I’m professional na naelewa vizuri na mimi ndiye nilishughulika na Sumaya”

“Why Luis?!! Why?!! Kwanini hukuniambia mapema kuhusu hili suala kwanini unajua ni kiasi gani nimeumia kumpoteza Sumaya? na mpaka nilianza kijihukumu mwenyewe”

“Kaka na ndio maana nimeanza na samahani najua kama nilifanya makosa miaka iliyopita lakini nataka kufuta kosa nililofanya na pia nilikuwa naangalia mbali kuhusu usalama wa mtoto unadhani kama mpango ungeenda vibaya si tungempoteza na mtoto Mr Hernad lakini pia wacha nikupongeze kwa kuchukua hatua ya kumpeleka Sumaya nje ni kama umesave maisha yake”

“Una maanisha nini Dokta Luis?”

“Hivi unadhani kama mtu yule aliweza Kufanya jaribio la kuwaondoa mama na mtoto kabla hajajifungua angeshindwa sasa kumuondoa mtoto?”

“Ni kweli kabisa Luis lakini unataka kuniambia kuwa mtu huyo atakuwa ni miongoni mwa familia yangu?”

“Wake up brother unadhani kuwa ni mtu wa nje ndiye afanye huo upuuzi?”

“Lakini mbona hakuna hata mtu aliyekuwa akionekana kuwa na chuki dhidi ya Sumaya? Hata mtoto alipozaliwa hakuna aliyeonesha chuki?”

“Kaka wake up from a nightmare sisi binadamu ni viumbe vya ajabu sana na ni hatari kuliko unavyofikiria, unajua ni kwanini mke wako mkubwa hakuja siku ambayo mke wako alikuwa akijifungua na ilikuwa muhimu afike yeye kama mwanamke?”

“Kwahiyo Unataka kusema kuwa mke wangu anahusika kwa haya yote?”

“Hapana sijamaanisha kuwa mke wako ndo ana husika lakini tumia akili brother, mimi yangu Ndio hayo nadhani sasa naweza kwenda kwenye majukumu yangu”



Mr Hernad alianza safari ya kurejea nyumbani huku akuonekana kuwa mnyonge sana na hapo akapokea taarifa kuwa mmoja Kati ya watumishi wake amefiwa na kaka yake aliyempa taarifa ni mtumishi wake ambaye alimteua kuwa kiongozi wa hiyo biashara yake.Hakuweza kuijibu kwa muda huo kwani alikuwa akiendesha gari hata hivyo hakuwa kwenye hali nzuri kutokana na taarifa alizopewa na Dokta juu ya kifo cha Sumaya kilichotokea miaka kumi iliyopita, moja kwa moja alimuwazia msaidizi wa kazi ambaye alikuwa akimuhudumia Sumaya kipindi chote cha ujauzito na hata kumlea Sumaya baada ya mama yake kufariki alimfikiria sana lakini hakuamini kama msaidizi huyo angeweza kutenda unyama kama huo, lakini hakuacha kumfikiria mkewe lakini napo akili ilikataa kabisa kuwa naye Rahel angeweza kumuua Sumaya.Aliporudi nyumbani baada ya kuulizwa na mke wake hakumwambia chochote walichozungumza na Dokta Luis badala yake alimwambia kuhusu msiba uliotokea.



ITAENDELEA………
 
SUMAYA FATE OF LOVE

SEHEMU YA TATU


Aliporudi nyumbani baada ya kuulizwa na mke wake hakumwambia chochote walichozungumza na Dokta Luis badala yake alimwambia kuhusu msiba uliotokea……….

ENDELEA……….


Ilipita miaka kadhaa huku ndani ya nchi ya Jamaica maisha upande wa Sumaya na Zuleya yakiendelea kama kawaida na tayari alikuwa ameshaanza masomo yake ya sekondari Meadowbrook High School na hata mwezi haukupita alikuwa amehamia shuleni hapo kutoka shule ya wasichana ya Wolmers Girls High School.Siku hiyo Lukas akiwa amekaa anamsubiri Sumaya ghafla kuna mtu alimfikia na kumuita.

“Lukas please come with me”

(Lukas tafadhali ambatana na mimi)

“But Amoy……”

(Lakini Amoy…..”

“Shii!! Lukas please”

(Shii!! Lukas tafadhali “

Lukas alikubali kumfuata mtu yule huku akionekana mwenye wasiwasi na kugeuka nyuma kila wakati.

“Lukas umenitenga sana kipindi hiki” Aliongea kipatois

“Hapana Amoy siwezi kukutenga unajua ni kiasi gani Nakupe….”

“Shut up!! unajua ni Kwanini Lukas napata aibu kutoka kwa rafiki zangu umeanza mahusiano na na huyu msichana ambaye amehamia hapa hivi karibuni ndio maana huna haja na mimi tena Lukas”

“Sasa hayo yanatoka wapi Amoy? Ni bora ungeniuliza kwanza ili nikupe majibu kuliko kunihukumu bure”

Muda huo Sumaya alikuwa akimtafuta Lukas ili waondoke wakati akizunguka kumtafuta huku akimuita ndipo alipowaona Lukas na msichana Amoy wakibishana alipata mshangao usio wa kawaida kwani hakutegemea na ndipo wote walipogeuka na kumtizama Sumaya lakini Lukas alionesha wasiwasi kwenye uso wake huku Amoy akionesha dhahiri kuwa alikuwa na chuki dhidi ya Sumaya, taratibu alimsogelea na kuanza kumtizama juu mpaka chini naye Sumaya alimtizama bila kupepesa macho yake.

“Nakuona umemfata Lukas si ndio? Huna hata chembe ya aibu muiba wanaume wa watu eeeeh”

“Unaongea kuhusu nini dada sikuelewi”

“Hunielewi nisikilize kwa makini wewe hapa umehamia huna hata mwezi lakini kila kitu kimebadilika hapa darasani wanaume wote wana kuangalia wewe et mrembo hahah!! Sasa umeanza kuingia kwenye himaya yangu Sumaya, Lukas ni wangu na atabaki kuwa wangu”

“Amoy unavuka mipaka Amoy nisikilize, nitakupiga na sitajali chochote Sumaya hana kosa”

“Kwahiyo Lukas unataka kunipiga kisa huyu malaya?”

“Lukas kipi kinaendelea hapa please naomba niondoke” Akigeuka na kutaka kuondoka

“Su…. Sumaya wait” Lukas alimgeukia Amoy na kumpa onyo na kisha kumkimbilia Sumaya ambaye hata hakumjali, Amoy alizidi kupata hasira huku moyoni akiwaza ni kwa namna gani atafanya ili amfundishe adabu Sumaya.

Amoy ni msichana wa Kijamaica ambaye alikuwa wakisoma darasa moja na Lukas na Sumaya lakini pia alikuwa kwenye mahusiano na Lukas na mahusiano yao yalidumu kwa kipindi cha miezi saba kabla ya Sumaya kuhamia shuleni hapo lakini baada ya kuhamia hapo kama kawaida Sumaya alikuwa karibu sana na Lukas kwani walikuwa ni marafiki wa muda mrefu walioshibana sana kwa zaidi ya miaka kumi hata wanafunzi wote wa darasani walidhani Lukas na Sumaya walikuwa na mahusiano hata baadhi ya wavulana wenzake walijenga chuki dhidi yake kwa sababu kuna waliofahamu kuwa Lukas alikuwa na mahusiano na Amoy.Kwa jinsi Sumaya alivyokuwa mrembo hakuna mwanaume hata mmoja aliyemlinganisha na msichana mwingine darasani humo na wengine walithubutu hata kusema shule nzima.Alikuwa na bidii sana darasani alipendwa na walimu tofauti kutokana na bidii zake.

Sumaya aliwahi usafiri na kupanda kwani sio siku zote ambazo Zuleya alimfuata shule na gari Kwani kuna siku alikuwa bize na kazi zake, alichukua taxi kuliko kukaa na kusubiri basi huku akimuacha nyuma Lukas akiwa na huzuni kwa kilichotokea shuleni.

Hata alipofika nyumbani hakuonesha uchangamfu wowote na hata Zuleya alihisi hilo baada ya chakula cha jioni Sumaya aliingia chumbani kwake na kushika simu yake alishangaa kukuta missed call zaidi ya thelathini na jumbe kumi zote kutoka kwa Lukas akimtaka msamaha kwa kilichotokea, hakuonesha kujali kabisa alizima simu na kuiweka pembeni.

Zuleya alifungua mlango taratibu na kuingia chumbani kwa Sumaya alimkuta akilia lakini Sumaya alipomuona mama yake alifuta machozi na kujiweka sawa ili asijulikane kama alikuwa akilia.

“Sumaya unalia? Kwanini?”

“Hapana mama I’m not crying” Akigeukia pembeni asimtizame mama yake

“Umesahau nani anakulea Sumaya tokea nimerudi hapa unaonekana haupo sawa na sasa unalia ni lazima kuna tatizo niambie”

“Mama sina tatizo Nipo Sawa”

“Sawa kama huna tatizo” Akitaka kuinuka lakini Sumaya alimshika mkono

“Mama……. Ni kweli nina tatizo”

“Niambie Sumaya mimi ni mama yako na kila kitu kwako usinifiche tatizo langu ni lako na pia lako ni langu”, Sumaya alimuelezea mama yake kila kitu kilichotokea shuleni na kwa jinsi alivyokuwa akijisikia vibaya juu ya jambo hilo.

“Ni dhahiri kuwa Sumaya unampenda Lukas?” Aliuliza Zuleya kwa udadisi

“Hapana sijamaanisha kuwa nampenda Lukas mama ila kwanini hakuniambia kuliko kusababisha haya yote”Huku akitizama chini

“Sumaya mimi ni mama yako na ni mkubwa kwako naelewa hili ficha tu ila lisemwalo lipo kama halipo basi laja”

“Mama…..”

“Sumaya usiwaze Sawa haya ni mambo ya kawaida lakini pia hao wasichana wenzako ishi nao kwa akili sana, pole sana mwanangu”

“Nitaishi hivi mpaka lini? Wananichukia wote nakosa hata ujasiri wa kwenda shule natamani hata nirudi Wolmers”

“Lakini si ulitaka mwenyewe kuhamia Meadowbrook? Na bila shaka ni kwa sababu ya Lukas, lala sasa binti yangu uwe na usiku mwema Nakupenda”Akimbusu kwenye paji la uso

“Asante mama na kwako pia, Nakupenda”

Aliinuka na kuondoka akimuacha Sumaya na maswali mengi alikuwa akimtizama mpaka alipofunga mlango wake, alijilaza kitandani na kuwaza jambo na kuzidiwa na usingizi.Asubuhi saa yake ya mezani ilikuwa ikipiga kelele kumuamsha naye hakuwa na hiyana aliamka na kwenda bafuni kujiandaa na kisha alielekea mezani kupata kifungua kinywa tayari alimkuta mama yake yupo mezani alimsalimu na kuendelea kupata kifungua kinywa pamoja, baada ya hapo waliongozana wote mpaka kwenye gari Zuleya alimfikisha Sumaya mpaka kwenye geti la shule na kumuacha hapo ndipo Sumaya alipoingia getini akasalimiana na walinzi na kuelekea darasani.Muda ulienda sana hata Sumaya alipotupa jicho kwenye meza ya Lukas hakuweza kumuona aliumia sana moyo na kujilaumu kutompa nafasi ya kumsikiliza.Muda wa masomo ulipokaribia kuisha aliingia mwalimu ambaye alihusika na mambo yote ya safari za shule na mwalimu wao wa darasa, safari ikiwemo utalii na safari nyingine za kimasomo, alitumia nusu saa kuelezea juu ya safari aliyopangwa kwaajili ya kwenda katika fukwe za Morant ( Morant Bay) na safari hiyo ikitarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huo na zilibaki wiki mbili tu hivyo wanafunzi walitakiwa kujiandaa vyema kwaajili ya nguo na pesa za matumizi kama chakula na vitu vingine vidogovidogo kwani pesa ya usafiri huwa inaambatanishwa na ada kwa wakati huo hawakutakiwa kutoa pesa kwaajili ya usafiri na magari ya shule ndio yanatumika.

Wanafunzi wote walitawanyika kuelekea nyumbani lakini Sumaya alikuwa na wasiwasi sana alichukua taxi kuelekea nyumbani kwa Lukas ambaye alikuwa akiishi na mjomba wake lakini mjomba wake alikuwa ni mtu wa kazi sana mara nyingi aliondoka asubuhi sana na kurudi usiku kutokana na kazi zake na nyumbani alibaki msaidizi wa kazi wakati ambao hata Lukas alikuwa akienda shule.

Alifika na kubisha hodi alipokelewa na msaidizi wa kazi baada ya salamu alimuilizia Lukas na kuambiwa yupo chumbani kwake alioneshwa chumba cha Lukas kilipo na alielekea chumbani taratibu na kuufungua mlango na kuingia alipigwa na bumbuwazi alipomuona Lukas akiwa amesimama huku akiwa amevaa bukta iliyomfika juu ya magoti na juu hakuvaa chochote kifua chote kilikuwa wazi na kilijengeka kwa mazoezi, aliziba macho yake kwa aibu kwani hakuwahi kumuona Lukas akiwa hivyo naye Lukas kwa haraka alichukua t- shet yake na kuvaa kisha akamkaribisha Sumaya ambaye aliketi kitandani akiwa mwenye aibu bado.Lukas alimsogelea Sumaya na kumshika kwenye mabega huku akimtizama naye Sumaya alijitoa taratibu na kuvunja ukimya.

“Kwanini hukuja shuleni leo?”

“Majibu yote unayo Sumaya bado una kinyongo na mimi?” Swali hilo lilimfanya Sumaya kukosa majibu kabisa na akabaki kumtizama Lukas

“Sumaya naomba nisamehe kwa kilichotokea jana najua nilipaswa kukuweka wazi juu ya hili ukweli Amoy nina mahusiano naye kwa muda sasa lakini….” Kabla hajamaliza kuongea Sumaya alimkatisha maneno ya Lukas yalikuwa kama msumari wa moto kwa Sumaya kwani ni siku nyingi sana alikuwa akimpenda sana Lukas lakini kutokana na mazoea waliyokuwa nayo hakuweza kumwambia na kingine ni aibu zake za kike ila alitegemea siku moja Lukas aje kumwambia kuwa anampenda lakini mambo yamekuwa kinyume chake Lukas alimchukulia Sumaya kama rafiki yake wa karibu na kama ndugu yake hivyo alikuwa na mahusiano na mtu mwingine bila yeye kufahamu.

“Luka mimi sina shida nimekuelewa ila nisamehe kwa kukuchunia jana ni hasira tu kutokana na maneno ya Amoy, nimesababisha usiende shule leo Lukas”

“Hupaswi kujilaumu Sumaya sio kosa lako pia asante kwa kunijali na kuja kuniona”

Lukas alimsogeza Sumaya karibu yake na kumkumbatia hakujua hali hiyo ilizidi kuibua hisia nyingi za mapenzi kwa Sumaya kumuelekea, Sumaya alimng’ang’ania Lukas asitake kumuachia naye Lukas hakuhisi kitu chochote kutoka kwa Sumaya aliona ni upendo tu walionao siku zote.

Baada ya kuongea kwa muda na kumwambia kuhusu safari ya utalii waliyoambiwa shuleni. Sumaya alimuaga Lukas na kuondoka, alichukua usafiri wa pikipiki ili awahi zaidi kurudi nyumbani maana muda ulikuwa umesogea kidogo.Alipofika nyumbani alimkuta mama yake tayari ameshawasili alimsalimia kisha kuingia chumbani kwake alijitupa kitandani akionekana mwenye furaha sana muda wote alilikumbuka kumbatio la Lukas alicheka kwa sauti mpaka akijishtukia lakini alishindwa kabisa kuzuia furaha yake na huo ndio udhaifu mkubwa wa Sumaya hakuweza kuficha hisia zake za huzuni wala furaha.

“Lukas leo sio mara yako ya kwanza kunikumbatia lakini kumbatio hili limejaa huba zito la kiutu uzima kuliko kumbatio lolote ulilowahi kunipa.Sijui kwanini kadri siku zinavyozidi kwenda hisia zangu kwako zinazidi viwango, nitawezaje kuendelea kuficha ukweli huo na ili hali una mpenzi Lukas? Nakupenda”

Alijisemea mwenyewe akiwa ameshika simu yake na kuitazama picha ya Lukas ambayo alikuwa ameisave kwenye kioo cha simu yake yaani ‘Wallpaper’ na karibia kila sehemu ya simu yake aliisave picha ya Lukas ni huba zito alilonalo Sumaya kwa Lukas.Mlango wake ulifunguliwa na mama yake ndio aliingia na kumkuta akiwa amejilaza na mwenye furaha sana alimfahamu sana Sumaya kuliko mtu yeyote alivyomfahamu kwa sababu ya damu moja na pia ni mtu pekee ambaye ameishi naye kwa muda mrefu.

“Sumaya?”

“Mama”

“You….. are looking so happy right?”

(Unaonekana una furaha sio?)

“Mom!!!! Hapana”

“Sumaya let me tell you something, katika watu ambao huwezi kuwaficha ni mimi nakujua kuliko mtu yeyote yule huwezi kunificha chochote”

“Mama Niko tu nafuraha leo”

“It’s about Lukas right?”

(Ni kuhusu Lukas sio)

“Umejuaje?”

“Kama nilivyokuambia mwanzoni i know you Sumaya so usinifiche kuwa huru kwangu”

“Ni kweli mama leo hakuenda shule nilipokuwa narudi nilipita kwake kumjulia hali, akaniomba msamaha lakini aliniweka wazi juu ya uhusiano wake na Amoy lakini mmmh mama”

“Vipi binti yangu?”

“I can’t imagine!!!! Alinikumbatiaaa”

Zuleya alichukua mto na kumrushia usoni Sumaya naye Sumaya alimrushia mama yake walizoeana sana kiasi cha kuishi kama marafiki lakini heshima waliyonayo ilibaki palepale hakuna aliyevunja heshima yao.

“Lakini Sumaya chunga sana hiki kitu usije ukavunjika moyo” Alipomwambia hayo aliondoka naye Sumaya hakuacha kumtizama mama yake mpaka anapotelea mlangoni, Zuleya alitamani sana angemtoa mwanaye huko alipo lakini hakuweza kwa muda huo kwani siku zote wanasema moyo wa mtu ni kichaka.

Siku iliyofuta kama kawaida Sumaya aliwasili shuleni lakini alishangazwa kukuta kundi lililojita The Queens ambalo liliongozwa na Amoy likimsubiri kwenye meza yake, hakuogopa kabisa aliwafuata na kutaka kufahamu walikuwa wana hitaji nini kutoka kwake aliwafikia na kusimama mbele yao kabla hata hajaongea Amoy alimrukia Sumaya lakini Sumaya hakuwa mzembe hata kidogo japo ni mrembo ila pambano alilijua vizuri alimkwepa na kumpiga kofi la uso kisha akamgeukia kabla Amoy hayafanya chochote alimkamata na kumbana.

“Huyu si ndio kiongozi wenu? Sasa ambaye hajitaki aje asogee hapa nimfundishe nini maana ya adabu ili siku nyingine msije kuvamia meza za watu hovyo” Aliongea Sumaya kwa lugha ya kiingereza

“Ladies njoeni mniokoe Ina maana nyie wote mnamuogopa huyu?”

“Et The Queens, Queens gani are you mad or something?”

Wakati mchezo huo ukiendelea watu wengi wa darasa hilo walikuwa wakiangalia ikiwepo wanaume na asilimia kubwa walikuwa upande wa Sumaya na wakifurahi amuadabishe Amoy kwani tabia za Amoy zilichukiwa sana na wengi darasani humo ikiwemo kujisikia na kujiona ana mamlaka kuliko yeyote na yote hayo ni kwa sababu baba yake alikuwa tajiri.

Siku hiyo Amoy moto wa Sumaya aliuona na alipewa adabu haswa yeye na kundi lake, waliishia kupita kila meza na kusafisha viatu vya wote waliokuwa darasani ni aibu kubwa kwao kwa sababu walikuwa wakiheshimika na kuogopwa na wanafunzi wengi darasani lakini leo mtu mmoja tu alitosha kuwapa adabu.

Lukas aliingia darasani na kukuta darasa limetulia sio kawaida hata kundi lote la Amoy lilitulia alipoketi tu Amoy aliinuka na kumfuata huku darasa zima likicheka

“Asante sana Lukas Kwahiyo ukaamua umtume Sumaya aje kuniaibisha darasani? Unamtuma…”

“Amoy jaribu kutulia sijamtuma mtu kwani nini kimetokea?”

“Wamefundishwa adabu hao leo jeuri yote kwishaaaa!!!!! Hahahahahah!!”Aliropoka mmoja Kati ya wanafunzi walioshuhudia mtanange wa Sumaya.

“Amoy please nisamehe mimi mpenzi nitalishughulikia hili”

“Niache hii ndio furaha yako Lukas” Amoy alirudi kwenye meza yake na Lukas alimfuata ili amuombe msamaha lakini Amoy alimfukuza.

Wakati wakirejea nyumbani Lukas alimfuata tena Amoy lakini Amoy hakutaka kumsikiliza kabisa aliona amuache atulize hasira kwanza, Lukas alimpenda sana Amoy na hakuwa tayari kumpoteza na ndio maana muda mwingi alijishusha mbele ya Amoy japo kuwa Amoy muda mwingi alikuwa mkorofi, mbabe, mwenye hasira lakini alimvumilia na kumpenda.

Aliamua kumfuata Sumaya na kumuuliza juu ya yote yaliyotokea naye Sumaya alimwambia kila kitu.

“Kweli Amoy ni mkorofi” Aliongea Lukas

“Lukas hakuna kitu ambacho sikipendi kwenye maisha yangu kama uonevu”

“Lakini nikuambie kitu Sumaya unajua yule ndio kila kitu kwangu nampenda ninachokuomba mvumilie tu mtaelewana vizuri si unajua yule ndo wifi yako”

Maneno ya Lukas yalimkera sana Sumaya kiasi cha kushindwa kujizuia na akamuacha hapo Lukas na yeye akaondoka, Lukas alishangaa sana kitendo hiko lakini hakuweza kugundua chochote kilichopo kwa rafiki yake huyo.

Lukas alifika nyumbani na kuingia chumbani kwake alichokiwaza muda huo ni Amoy pekee hivyo aliichukua simu yake na kumpigia simu badala yake iliita bila mafanikio yoyote alituma jumbe lakini hazikujibiwa, alianza kukata tamaa lakini aliona apige labda Amoy alikuwa akijisomea hakuweza kupokea simu awamu hii simu ilipokelewa lakini kwa njia tofauti

“Unataka nini wewe malaya wa kiume?”

“Amoy jitahidi kupunguza ukali wa maneno mpenzi wangu najua kilichotokea lakini nisamehe mimi”

“Mbona unakuwa king’ang’anizi Lukas nimeshasema sitaki na kuanzia leo mimi na wewe basi hakuna tena mahusiano sikupendi Lukas endelea na huyo Sumaya wako”

“Tafadhali nisikilize Amoy…… Amoy….. Amoy….. Hallo…Hail up… Amoy”

Simu ilishakatwa na Amoy hakutaka kumsikiliza Lukas, Alikata tamaa Lukas na kuizima simu yake.Aliwaza mengi juu ya mahusiano yake na Amoy na pia juu ya urafiki wake na Sumaya, alilia kiume kijana Lukas.

Huku upande wa Sumaya hakuweza kulala mpaka awasiliane na Lukas lakini alipiga simu yake mara kadhaa na jibu alilopewa ni kuwa simu haipatikani, alipata wasiwasi sana Sumaya usiku kwake ulikuwa mrefu bila kujua ni kipi ambacho rafiki yake alikuwa akikipitia kwa muda huo ambao hata na yeye alikuwa akihangaika.

Asubuhi alijiandaa na siku hiyo hakumsubiri mama yake ampeleke kwa gari aliondoka na usafiri wa kawaida mpaka shuleni, baada ya kuingia darasani aliketi akimsubiri Lukas afike lakini kabla ya Lukas aliingia Amoy akiwa ameambatana na mwanaume ambaye walisoma wote darasa moja kimuonekano ukiwaangalia ni wazi kuwa wana mahusiano tena sio ya siku chache ni muda mrefu hakutaka kuwafatilia aliwaacha wakakae, siku hii Lukas alichelewa sana darasani alipoingia tu alitupa macho kwenye meza ya Amoy hakuweza kumuona ndipo alipoangalia mwisho na kumuona Amoy akiwa bize na mwanaume aliyeingia naye walikuwa wakicheka na kufurahi huku wakikumbatiana Lukas aliumia sana kiasi cha kushindwa kuvumilia aliwafuata mpaka walipokaa.

“Amoy what kind of rubbish you are doing??”

(Amoy ni aina gani ya uchafu unafanya??)

“Hey bro tafadhali usiniinglie, mimi nilidhani tumeshamalizana jana kwenye simu au uliona kuwa ni utani basi nikuambie face to face kuwa sikupendi Lukas”

“Amoy please usinipe adhabu kama hii mpenzi wangu nakuomba Amoy just look at me kumbuka ni mangapi tumefanya mimi na wewe”

“Lukas sitaki kusikiliza ngonjera zako, ondokaaa!!!”

Lukas alishindwa kuvumilia zaidi alitoka ndani ya darasa na kuondoka naye Sumaya hakuwa nyuma alimfuata Lukas ili waondoke wote alitambua kuwa Lukas alikuwa kwenye maumivu makali sana.

Walichukua usafiri wa haraka wa kuwafikisha nyumbani na walipofika moja kwa moja waliingia chumbani, kwa mara ya kwanza Sumaya alilishuhudia chozi la Lukas na hapo taswira ya msichana Amoy ilimjia alijikuta akimchukia sana Amoy kwa kitendo alichokifanya kwa Lukas.

Alimgeukia Lukas alianza kumbembeleza taratibu akimfuta machozi.

“Sumaya kwani mimi nina shida gani mbona ni kama sina bahati ya kupendwa?”

“Luka usiseme hivyo huwezi jua ni wangapi wanakutazama kwa upendo ni wangapi leo hii wanatamani kukufuata na kukuambia kuwa wanakupenda”

“Lakini Kwanini haya yote Kwanini?”

“Kila kitu kina sababu Lukas yawezekana Amoy hakuwa wa chaguo lako na chaguo lako linakuja”

Taratibu alikishusha kichwa cha Lukas mpaka kifuani kwake naye Lukas alitulia kwenye kifua cha mtoto mzuri, huku moyoni Sumaya alifurahi sana kuwa karibu na Lukas alimkumbatia kwa upendo.

“Sumaya asante kwa kuwa na mimi wakati huu mgumu hakika wewe ni rafiki wa kweli wa shida na raha”

“Ni wajibu wangu Lukas usijali”

Baada ya muda angalau Lukas alitulia na wakaanza kucheza michezo tofauti kama gemu, walikimbizana chumbani na michezo mingi ya kufurahisha.

Muda ulienda sana na ndipo wakashituka kuwa ilikuwa ni saa moja kasoro kwa haraka Sumaya alijiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani naye Lukas aliona sio vizuri kumuacha aende mwenyewe muda huo hivyo walichukua usafiri pamoja mpaka nyumbani, walipofika nje ya geti walishuka wote na kutizamana huku moyoni Sumaya akitamani hata amkumbatie Lukas na kumbusu lakini aliona aibu sana kufanya hivyo bila kutegemea Lukas alimsogelea zaidi Sumaya na kumkumbatia kwa upendo na kisha kumbusu kwenye paji la uso.

“Asante sana Sumaya kwa kampani yako kipenzi sikuwaza kama leo nitakuwa mchangamfu tena kwaajili yako Sumaya”

Kisha akaaga na kuondoka na usafiri waliokuja nao hapo, Sumaya alibaki aneganda kama barafu pale pale asiamini kitendo alichikifanya Lukas, maneno yake yalikuwa kama maua yaliyovutia na kuchipuka kwenye bustani nzuri ya mapenzi alihisi kama anaelea angani Kumbe yupo chini amekanyaga ardhi ndipo akili ikamrudia na kugundua kuwa alikuwa nje hivyo kwa haraka aliingia ndani, wakati hayo yote yakifanyika kuna mtu alikuwa makini sana kufatilia kila hatua hakuwa mwingine ni Zuleya ambaye aliketi kwenye kibaraza cha kupumzikia katika ghorofa ya nyumba hiyo, nyumba yao ilikuwa ni ya ghorofa moja.

“Well my daughter” Alishituka Sumaya “Kwanini hujamkaribisha mgeni ndani?”

“Aaah…… aaah… mama alikuwa na haraka hata nyumbani hajaaga alinisindikiza tu”

“Bila shaka mmetoka kwake?”

“Ni kweli mama Zuleya”

“Okay…… ka change hizo nguo uje unisaidie kitu hapa”

“Sawa mama”

Baada ya kubadilisha nguo alielekea jikoni ili amsaidie mama yake.Zuleya aliamua kumweleza Sumaya juu ya kutaka kumkaribisha Lukas siku ya jumamosi nyumbani kwaajili ya chakula cha mchana na jioni, jambo hilo liliibua furaha sana kwa Sumaya hakutegemea kabisa alimwambia mama yake kuwa angefanya hivyo.

ITAENDELEA…………
 
SUMAYA FATE OF LOVE


SEHEMU YA NNE


Baada ya kubadilisha nguo alielekea jikoni ili amsaidie mama yake.Zuleya aliamua kumweleza Sumaya juu ya kutaka kumkaribisha Lukas siku ya jumamosi nyumbani kwaajili ya chakula cha mchana na jioni, jambo hilo liliibua furaha sana kwa Sumaya hakutegemea kabisa alimwambia mama yake kuwa angefanya hivyo………..


ENDELEA…………


Sumaya alionekana kushuka kwenye gari na kuingia ndani ya shule, aliketi kwenye meza yake kama ilivyo kawaida kwake alikuwa akimsubiri Lukas aingie lakini haikuwa kama alivyotegemea wanafunzi wote walishawasili kasoro Lukas tu.

Kwa hasira Sumaya alimfuata Amoy mpaka alipokaa na kumpiga kibao cha shavuni, wanafunzi wote waliwageukia wao.

“Umefurahi sio?…… nakuuliza Amoy umefurahi? Chochote kibaya kikimkuta Lukas nita deal sambamba na wewe Amoy ulichomfanyia Lukas hakustahili hata mimi sijakipenda hata kidogo”

“Sumaya…….”

“Shiii!!!!…… Lukas ana thamani kubwa sana kwangu kuliko hata unavyofikiria Amoy, cheza na vyote ila sio na Lukas”

Alilifuata begi lake na kuondoka, alielekea nyumbani kwa Lukas kwa bahati nzuri alimkuta akinywa chai alimsogelea na kumuuliza kuhusu kutoonekana shuleni naye Lukas alimueleza kuwa hakujisikia vizuri na ndio maana hakuweza kwenda shule.Walipomaliza kunywa chai waliongozana mpaka chumbani na kuanza kujisomea.

Ilikuwa siku ya jumamosi, Sumaya akiwa ameketi sebuleni akiangalia tamthiliya ya kifilipino iliyojulikana kama ‘My iternal’ ni tamthiliya nzuri ya mapenzi iliwavutia watu wengi kuitazama kutokana na kuigizwa kwa ufundi wa hali ya juu sana kwenye sekta mbalimbali hasa sekta ya mapenzi.

Lakini kengere ya mlangoni ilitoa kelele kuashiria kuna mtu mlangoni, aliinuka na kwenda kufungua hakuamini moyo wake ulilipuka kwa furaha baada ya kumuona Lukas akiwa amesimama mbele yake bila kijielewa Sumaya alijikuta akimrukia na kumkumbatia Lukas naye alimkumbatia Sumaya kisha alimkaribisha ndani na kuketi sebuleni.

“Kumbe na wewe unaipenda hii tamthiliya?” Aliuliza Lukas

“Sana na huwa sichoki kuiangalia”

“Basi tuiangalie wote, Aunt Zuleya yuko wapi?”

“Aaah alielekea sokoni maana kuna vitu vilipungua hapa ndani”

“Aah sawaaaa” Alimtizama Sumaya na kumkonyeza kwa njia ya kawaida lakini Sumaya alilipokea kwa njia tofauti huku moyoni akiwa na furaha isiyo ya kawaida. Waliendelea kuangalia tamthiliya hiyo huku kila mmoja alijikuta akiweka umakini zaidi sehemu ambayo ilikuwa ikioneshwa kwa muda huo.

“Naipenda sana hii scene”

Aliropoka Sumaya na wakati akishangaa Lukas aliinuka na kuketi alipokuwa Sumaya alimkumbatia na kuanza kumbusu taratibu mdomoni huku akimpapasa sehemu tofauti, Sumaya naye alimkumbatia Lukas huku hisia nyingi zikimjaa, waliendelea kupeana busu wakiwa kwenye sofa.

“Sumaya!!!!!!!” Ni sauti ambayo ilimshitua Sumaya na kumfanya akurupuke

“Lukas……” Alihema kwa nguvu

“Bila shaka Aunt Zuleya atakuwa amefika nimesikia kengere”

Aliinuka Sumaya na kwenda mlangoni kumbe yale yote yalikuwa ni mawazo yake tu hakuna chochote kilichotokea Kati yake na Lukas kwa muda huo.

Alimfungulia geti mama yake na aliingiza gari ndani, baada ya kupaki alisogea kwenye gari na kufungua buti ya gari akitoa mizigo ambayo ilikuwa humo wakisaidiana na mama yake naye Sumaya alimtaarifu kuwa Lukas alishafika nyumbani Zuleya alionesha tabasamu usoni alipopewa taarifa hiyo.

Walibeba kila kitu na kuingia ndani, Zuleya alipomuona Lukas alizidi kutabasamu.

“Mkwe wangu huyo!!!!!” Aliongea Zuleya ili kuona Lukas angefanyaje lakini Lukas alicheka tu huku akimtizama Zuleya kwa upande wake aliona ni utani tu kwakuwa alikuwa karibu na Sumaya kwa upande wa Sumaya alibaki na swali Kwanini mama yake amwambie Lukas hivyo ila kwa Zuleya alikuwa na maana yake mpaka akamwambia Lukas hivyo.

“Shikamoo Aunt Zuleya”

“Marahaba Lukas za nyumbani”

“Safi Aunt”

“Howdeedo?” ( unaendeleje?”

“I’m very fine Aunt”

“Okay karibu sana”

Sumaya na mama yake walielekea jikoni kwaajili ya kuandaa chakula cha mchana huku Lukas akiwa sebuleni akiendelea kuangalia tamthiliya.

Saa saba chakula kilikuwa tayari kimeshapikwa na kuandaliwa mezani, wote kama familia walijumuika mezani na kula chakula pamoja.

Sumaya alifurahi sana kuwa na Lukas mwanaume aliyempenda sana tokea utoto wake.

Baada ya chakula waliketi sebuleni na kuanza kupiga soga mbalimbali na kufurahi mpaka jioni ilipofika na kuandaa chakula cha kisha wakala na ndipo Lukas aliaga na kuondoka.

Siku ya safari ya utalii kuelekea Morant Bay iliwadia na wanafunzi wote walikuwa wameshawasili shuleni kwaajili ya safari hiyo magari yalikuwa yameshaandaliwa, Sumaya alimfuata Lukas.

“Hey Lukas!!”

“Sumaya”

“Umebeba chochote?”

“Hapana, umesahau jana uliniambia nisibebe chakula chochote?”

“Nakumbuka nilikuwa tu nakuuliza” Alifungua begi lake na kutoa chocolate mbili na akampatia Lukas moja

“Nilinunua muda sana kama wiki imepita kila nikitaka kukupa mambo yanakuwa mengi ila leo nimekumbuka”

“Thank you, Sumaya you remaind me that time when we are young” Alimkonyeza Sumaya

(Asante, Sumaya unanikumbusha wakati ule tukiwa wadogo)

Safari ilianza na Sumaya aliketi siti ya jirani ya Lukas walikuwa wakipiga stori na kusikiliza muziki wa rege pamoja, safari yao ilikuwa ya furaha sana.

Ilikuwa ni safari ndefu kidogo na iliwachukua muda kufika maana jioni waliwasili, walipatiwa sehemu ya kulala na wasichana wote walipewa chumba kimoja na kwa upande wa wanaume ni hivyo hivyo.

Lukas aliketi na Sumaya naye Sumaya alitoa chakula maalumu alichikiandaa ilikuwa ni vitafunwa vya aina tofauti ambavyo iliviandaa mwenyewe kisha Lukas alikwenda kununua juisi ili washushie, wakati waliendelea kula alipita Amoy akiwa na yule mwanaume wake aliwakata jicho kali na bila hata kusalimia aliwapita Lukas alijisikia vibaya sana hata Sumaya alitambua hilo lakini aliweza kumtuliza na kuwa kawaida.

Baada ya kula na kuongea kwa muda sasa waliruhusiwa kwenda kulala, Sumaya alimuwazia Lukas muda wote alipokuwa kitandani mambo mengi ya nyuma na ya sasa aliyakumbuka sana.

“Lukas nakupenda sijui ni Kwanini sijauruhusu moyo wangu kumpenda mwingine zaidi yako, nitakulinda kwa gharama yoyote ile ili uwe wangu Lukas” Alijisemea mwenyewe na ndipo usingizi ukamchukua na kumpeleka kwenye ndoto ya bustani nzuri ya mapenzi, na katika bustani hiyo walikuwa wawili tu yeye na Lukas wakiimba na kucheza pamoja michezo mbalimbali ikiwemo kukimbizana, kujificha, kutupiana maua na kumwagana maji yaliyokuwa kwenye chemichem.Wakati wakiendelea kucheza huku wamekumbatiana Lukas aliteleza na kuwafanya wote wawili kuanguka kwenye shimo ndogo lililojaa maua, Lukas aliusogeza mdomo wake kwenye mdomo wa Sumaya kisha akampiga busu la mahaba naye Sumaya alizidi kumbana Lukas huku wakipeana busu, Alilivua taratibu gauni jepesi alilovaa mrembo Sumaya na kulitupa kando naye alitoa shati lake na kulitupia pembeni huku kifua chake kilichojengeka kwa mazoezi kikiwa nje aliusogeza mdomo wa Sumaya kwake na kuendelea kumpiga busu, na kila mmoja akiwa na shauku kubwa ya kuwa na mwenzie ndipo Lukas aliitoa nguo ya ndani ya msichana Sumaya.

Sumaya alishituka kwenye ndoto hiyo na muda huo alamu ilikuwa ikiwaamsha na tayari ilikuwa saa kumi na moja na nusu alfajiri, alihisi unyevu unyevu kama maji kwenye nguo yake ya ndani alipojigusa ni kweli alilowesha nguo yake.

Hakuwa na muda wa kupoteza aliamka na kwenda bafuni alioga vizuri na kurejea chumbani alijitayarisha vizuri kisha akaketi kitandani na kuchukua simu yake alituma ujumbe kwa Lukas na muda huo huo ujumbe ulijibiwa alijihakikishia kuwa Lukas alikuwa ameshaamka ni muda ambao pia wanafunzi wenzake walikuwa wakijiandaa, ilipohitimu saa kumi na mbili na nusu walikusanyika sehemu moja baada ya kupatiwa maelekezo walianza safari yao kama kawaida Sumaya alikuwa na Lukas, walifika Sehemu kuketi huku msimamizi mkuu akiwaongoza na kuwapa taarifa mbalimbali.

Hatua ya mwisho walifika beach na kuketi wengi wao waliketi wawili wawili ikiwemo Sumaya na Lukas, minong’ono ilisambaa kuwahusu kila mmoja akiongea chake.

“Hey guys it seems that they are longer friends but they look perfectly they match so wow!!!!!”

(Jamani inaonekana kwamba ni marafiki wa muda mrefu lakini wanaonekana bomba wanaendana sana waoo!!)

Aliongea mmoja Kati ya marafiki wakubwa wa Amoy akiwasifia Sumaya na Lukas.Wakati wakiendelea kula alifika Amoy na kuelekea kwa mpenzi wake aitwaye Bartt lakini alishangazwa kumkuta Bartt akilishana na mtu mwingine kabisa.

“Bartt unafanya nini?” Aliuliza Amoy kwa hasira

“Nisikilize Amoy kama uliweza kumuacha Lukas bila sababu yoyote vipi kuhusu mimi? Na nikuambie tu kitu usichokijua kuwa huyu ndio mpenzi wangu na nampenda sikuwahi kukupenda Amoy na wewe ndiye ulilazimisha mapenzi kwangu”

“Amoy mpenzi wangu hakuwahi kukupenda na sisi tuna muda mrefu kwenye mahusiano hilo ni fundisho tu kwa watu kama wewe Amoy”

“Please Bartt usinifanyie hivyo nakuomba”

“Amoy ondoka na usimsumbue mpenzi wangu hakupendi mbona unalazimisha, ulichomfanyia Lukas hakustahili kabisa” Aliongea msichana aliyeitwa Alvita “Alvita, Bartt sikutegemea hili” Aliinuka huku akifuta machozi na wanafunzi wenzake wakimcheka kwa ujinga wake, alifika mpaka alipokaa Sumaya na Lukas alipiga magoti huku akilia kwa kwikwi.

“Sumaya, Lukas naomba mnisamehe, Lukas najua nimekukosea sana kukudhania vibaya kama una mahusiano na Sumaya”

“Amoy ondoka hapa haraka” Lukas alijawa na hasira

“No Lukas yupo hapa kuomba msamaha usimfukuze”

“Sumaya naomba nisamehe niombee msamaha kwa Lukas nimemkosea sana”

“Mimi nimekusamehe Amoy nina imani hata Lukas amekusamehe”

“Amoy nilikupenda kuliko nilivyojipenda mwenyewe, siku zote nilijishusha kwako na wewe ukawa juu lakini bado uliniona mjinga.Nimekusamehe ila siwezi kuwa na wewe tena sio kama nakuchukia hapana still nakupenda Amoy ila acha ibaki kama historia mimi na wewe”

“Lukas please……… Sumaya nisaidie”

Sumaya alihisi maumivu sana alishindwa kukaa pale aliinuka na kwenda kukaa mbali akiwa pekeyake alimpenda sana Lukas hakuwa tayari kushuhudia tukio hilo, ghafla alimuona Lukas akija upande wake huku amebeba vitu vyote alifuta machozi haraka na kutulia naye Lukas aliketi pembeni yake”

“Mbona uliniacha?”

“No… Lukas….. nilishindwa kuvumilia kumuona Amoy kuwa kwenye hali ile, umemuacha wapi?” Ilimbidi adanganye ili kuficha ukweli

“Nimemuacha kule Sumaya sitaki tena kuwa na yeye japo nilimpenda na bado nampe…….”

“Lukas….. tule unajua muda umeisha tunaondoka soon” Alimkatisha Lukas na wote waliendelea kula.

Walirejea tena walipoweka kambi yao na kuendelea na matayarisho ya kurudi siku iliyofuata.

Asubuhi na mapema safari ilianza kurejea Kingston, wanafunzi wote walikuwa na furaha isipokuwa Amoy alikuwa na huzuni iliyopitiliza alijuta kwenda safari hiyo iliyojaa huzuni kwake.Waliwasili Kingston salama na kila mwanafunzi alirejea nyumbani.

Sumaya alipofika nyumbani alipokelewa na mama yake kwa upendo.

“Mwanangu nilikumiss jamani nilibaki mpweke sana.Vipi tour ilikuwaje?”

“It was great!!!” Huku akizunguka na kuinyoosha mikono yake juu

“Ni kwa sababu ya Lukas sio?”

“Mamaaaa”

“Najua umepata nafasi nzuri sana kufurahi na Lukas au mimi muongo Sumaya”

“You are right mom, nimefurahi saana”

“Furaha yako ni yangu, nenda kabadilishe nguo halafu uje kuna kitu special nimeandaa kwaajili yako”

Kwa haraka zaidi Sumaya alikimbilia chumbani kwake na kubadilisha nguo kisha akamfuata mama yake sebuleni, alikuta amemuandalia chakula kizuri sana cha asili ya Kijamaica ambacho Sumaya alikipenda sana ni chakula maarufu Jamaica kilichojulikana kama Brown stew chicken kilikuwa ni chakula cha kiasili nchini Jamaica, aliruka na kumkumbatia mama yake akifurahi sana na kumshukuru kwa kumuandalia chakula hiko.


* * *

“Mume wangu unajua umri unaenda sasa itabidi umtafute mtu ambaye atasimamia vizuri biashara zako badala yako”

“Ni kweli mke wangu ila bado sijampata……..”

“Una maanisha nini kusema kuwa hujampata?”

“Rahel usimamizi wa biashara unahitaji mtu ambaye ni mtaalamu wa mambo haya sio kila mtu tu”

“Natamani hata ningekuwa na mtoto wa kukusaidia mume wangu” Alitoa machozi Rahel na kumfanya Mr Hernad ajisikie vibaya

“Usiseme hivyo mke wangu yote ni mipango ya Mungu usilie” Alimsogeza kwenye kifua chake na kumkumbatia huku akimpapasa mngongoni kumbembeleza.

Kuna muda Rahel alionekana ni mwenye huzuni na mpweke sana kwa kukosa mtoto katika maisha yake na Sumaya alikuwa kama kiliwazo pekee kwake japo hakuwa mtoto wa kumzaa lakini alimchukulia kama mwanaye aliyemzaa.

Asubuhi kama kawaida Mr Hernad aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kwenye biashara zake, alimuaga mkewe na kuondoka baada ya kupata kifungua kinywa.

Wakati akiwa kazini simu yake iliita na alipotazama mpigaji aliachia tabasamu pana usoni na kuipokea ilikuwa ni simu ya video kutoka kwa mwanaye mpenzi Sumaya aliipokea kwa furaha.

“Daddy how are you?”

“I’m fine my Princess”

“Nimekumiss baba natamani nije Tanzania”

Alijikuta akiropoka vitu ambavyo Sumaya hakutakiwa kuvisikia

“Mimi pia ila sio sehemu salama kwa sasa”

“Una maanisha nini baba?”

“Ahh namaanisha kuwa bado hujamaliza masomo yako so sio vizuri ukija huku kipenzi”

“Uh….. baba sio mbaya niombee tu maana next week tunaanza mitihani ya mwisho baba”

“My little genius najua wewe una akili sana kama alivyokuwa mama yako”

“Alivyokuwa? Baba mbona sikuelewi”

“Sumaya yaani mama yako alivyokuwa wakati bado yupo msichana mdogo kama wewe alikuwa genius sana”

“Ooh nimerithi kutoka kwake”

Waliongea kwa muda na Mr Hernad alimuomba binti yake amuache afanye kazi zake kwanza.

Alipokata simu alibaki na mawazo sana kwa kuongea vile na Sumaya alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa ukweli alichanganywa na vitu vingi sana alivuta shuka lake na kulala kwani kwa Jamaica ilikuwa ni usiku.

Mr Hernad alianza kufanya uchunguzi wake kimya kimya ili ajue ni nani alimpa sumu mke wake kipenzi Sumaya, aliona aanze na anayehusika na chai jikoni alimfuata na kumuuliza maswali ya mitego ili asifahamu Mr Hernad alikuwa akitaka nini lakini hakuweza kupata majibu kwani siku hiyo huyo msaidizi haikuwa zamu yake kuwepo jikoni na hakufamu ni nani siku hiyo alikuwa akihusika.

Aliona asiwe na haraka juu ya hilo ni vyema afuatilie taratibu na kwa umakini zaidi maana hilo jambo halihitaji haraka wala pupa.

Ilimbidi akutane na Mr Khaleed amweleze jambo hilo pengine angemsaidia kwa mawazo au kwa namna yoyote atakayoweza kumsaidia, alimuomba waonane sehemu tofauti kabisa na nyumbani maana nyumbani ingeweza kuwa hatari ni lazima kuchukua tahadhari mapema.

Mr Hernad aliwasili kwenye mgahawa na kuketi huku akimsubiri Mr Khaleed punde Mr Khaleed aliingia na kuelekea moja kwa moja kwenye meza aliyoketi Mr Hernad, walisalimiana na ndipo Mr Hernad alipomueleza Mr Khaleed kila kitu alichoelezwa na Dokta Luis hata Mr Khaleed alishangazwa na jambo hilo kuwa lingewezekana vipi.

“Kwanini hakusema mapema jambo hilo?”

“Hata mimi nilimuuliza na akasema aliangalia kwanza usalama wa mtoto, nimeghafirika sana Khaleed”

“Ina maana anaye msuspect ni Mkeo Bi Rahel? Inawezekana vipi hili jambo?”

“Khaleed sielewi hajasema moja kwa moja kuwa ni Rahel ila akasema tu niwe makini na nifuatilie jambo hili na ndio maana niakona nikuambie pengine utanipa msaada wowote hata wa mawazo”

“Lazima tufanye uchunguzi ila ulichoanza kukifanya kipo sahihi ila kifanye kwa akili sana bila pupa”

“Ni kweli hili jambo nitahakikisha namfahamu ni nani aliyemuwekea sumu Sumaya.”

Walipata kahawa na kisha waliagana kila mmoja alirejea nyumbani, Mr Khaleed alishangazwa na jambo hilo kwa sababu hakutegemea kutokea kwenye nyumba ya Mr Hernad akiwa njiani aliwaza ni kwa jinsi gani atamsaidia Mr Hernad kujua ukweli kuhusu hilo.

Alifika nyumbani na mke wake alikuwa akiandaa chakula na msaidizi wa kazi jikoni, aliingia chumbani ili aoge na ndipo aende sebuleni.

Maisha yaliendelea kama kawaida hakuna kitu kilichobadilika kwa upande wa Mr Hernad alizidi kuchapa kazi kukuza zaidi biashara zake, alimkumbuka sana Sumaya aliona ni vyema ampigie simu japo walishazungumza kabla hajaenda kazini licha ya kuwa majira na nyakati ni tofauti kabisa Kati ya Tanzania na Jamaica ni nchi tofauti zilizopo kwenye mabara tofauti.

“Baba shikamoo vipi nyumbani mnaendeleaje mama hajambo?”

“Sisi wazima mwanangu nimekukumbuka sana Princess Sumaya” Aliongea kwa hisia

“Mimi pia baba, tumeshaanza mitihani natumaini unaniombea sana”

“Zaidi ya unavyofikiri mwanangu lakini nikuombe kitu binti yangu”

“Kitu gani baba?”

“Mwanangu najua ndoto zako sikuzote ni kuja kuwa mwana mitindo mkubwa duniani lakini please soma usimamizi wa biashara”

“Daddy why??”

“Please Sumaya do it for me, biashara zangu zinahitaji msimamizi mbobezi na wewe unaweza binti yangu”

“But daddy that is not my hobby not my choice”

“Sumaya don’t let me down please i will be so upset”

“Daddy” Alikata simu Sumaya na baba yake alijisikia vibaya sana alihitaji msimamizi wa biashara zake na hakuwa na mwingine wa kumtegemea zaidi ya Sumaya kwa sababu ni mtoto wake wa pekee na pia aliamini Sumaya aliweza kwa asimia mia moja.

Wakati anaweka simu mezani ujumbe uliingia kwenye simu yake aliichukua simu na kuufungua ujumbe huo, alishituka baada ya kuuona ujumbe huo uliosomeka kwa maandishi makubwa, ‘RUDI NYUMBANI HARAKA’ namba iliyoonekana kutuma ujumbe huo hakuifahamu kabisa kwani ilikuwa ngeni, alihisi nyumbani kuna hatari alikusanya kila cha muhimu na kuondoka kurudi nyumbani kwa haraka alikuwa mwenye wasiwasi sana.

Alifika nyumbani mlinzi alimfungulia geti aliingiza gari ndani mkukumkuku alilipaki kisha akashuka haraka kuingia ndani, nyumba ilitulia sana hata taa hazikuwashwa alizidi kupata wasiwasi alisogea sebuleni na kutafuta swichi ilipo na alifanikiwa kuwasha taa alichikiona alipigwa na bumbuwazi.

“Mke wangu kumbe wewe ndio umepanga haya yote?

Aliuliza huku asiamini kabisa kilichotokea.


ITAENDELEA……….
 
SUMAYA FATE OF LOVE


SEHEMU YA TANO


Alifika nyumbani mlinzi alimfungulia geti aliingiza gari ndani mkukumkuku alilipaki kisha akashuka haraka kuingia ndani, nyumba ilitulia sana hata taa hazikuwashwa alizidi kupata wasiwasi alisogea sebuleni na kutafuta swichi ilipo na alifanikiwa kuwasha taa alichikiona alipigwa na bumbuwazi.

“Mke wangu kumbe wewe ndio umepanga haya yote?

Aliuliza huku asiamini kabisa kilichotokea.


ENDELEA……..


“Surpiseeee!!!!!”

Zilisikika kelele na watu wengi walikuwepo hata Mr Khaleed na Dokta Luis.

“Happy birthday to you!!! Happy birthday to you!!!Happy birthday Mr Hernad…. Happy birthday to you!!!”

Walipiga makofi na kushangilia pamoja.

“Ni mimi mume wangu unajua una mambo mengi sana na umri pia unachangia umekuwa msahaulifu sana nikaona nikufanyie tafrija ndogo.Nisamehe kwa kukufanya uwe na wasiwasi”

Bila kuongea chochote Mr Hernad alimsogelea mke wake na kumkumbatia kwa upendo

“Asante sana mke wangu kwa upendo wako nilishasahau kabisa japo mliniwish asubuhi pia hata binti yangu aliniwish”

Basi keki ilikatwa watu wakala wakanywa na kufurahi pamoja na kusahau shida zote wakati huo, Mr Hernad alifurahi na kuona kuwa watu wote wapo upande wake na pia walimsapoti sana alipata nguvu mpya na fikra mpya kwenye kichwa chake.

Tafrija hiyo ndogo iliisha na watu wote walitawanyika kwenda nyumbani kwao naye Mr Hernad alimtumia binti yake picha za tafrija na kumweleza ni kiasi gani amefurahia tukio hilo ambalo hakulitegemea kabisa, kilikuwa ni kitu kikubwa sana kwake kufanyiwa hivyo tena na watu aliowapenda sana ikiwemo mke wake Bi Rahel.


* * *

“Sumaya, wakati unahamia hapa sikujua kuwa wewe mstaarabu na mwenye roho nzuri, unajua ni vile ulipohamia hapa kila mtu alikuwa anaongea chake wanaume wote darasani walikuwa wanakuangalia wewe basi wengi tulikuwa tunakuchukulia kwa namna tofauti”

“Uuh….. Alvita usiongee yote hayo hata mimi nilikuwa napitia wakati mgumu sana na mtu pekee aliyekuwa upande wangu ni Lukas, unajua Lukas ndiye rafiki yangu mkubwa tokea tupo wadogo na anajua kipi ambacho huwa nakupitia na ni zaidi ya rafiki kwangu”

“Tokea tulivyoenda tour nilikuwa natamani sana kuzungumza na wewe, nisamehe kwa kukuchukulia vibaya na pia japo sipaswi kuwasemea ila kwa niaba ya wanafunzi wengine tusamehe Sumaya”

“Usijali Alvita mimi sina shida juu ya hilo”

“Tanzanian girls are very kind”

(Wasichana wa kitanzania ni wakarimu sana)

Sumaya alimnong’oneza kitu Alivita naye Alvita alipiga kelele huku akimtaja Sumaya

“Shii!!!! Alvita mbona hivyo mimi nimekuambia wewe kwakuwa ni rafiki yangu mkubwa sasa”

“Lakini Kwanini unapenda kuishi kwa mateso hivyo Sumaya?”

“Kwanini”

“Mwambie ukweli kuliko kuendelea kuteseka”

“Nilitamani na natamani sana kumwambia lakini nina aibu kupitiliza halafu kwa jinsi tulivyokua mimi na Lukas na kuchukuliana inakuwa vigumu”

“Sikia Sumaya kwa upande mwingine wanaume ni dhaifu sana na ndio maana huwezi ukakuta mwanaume akitongozwa na mwanamke anakataa sijui labda iweje kama umeshindwa kwa maneno hata vitendo vitumike tena tunamaliza shule utakuwa na muda mwingi Sumaya do it today because tomorrow is not a promise”

“Alvita…….. umeniambia vingi nitajitahidi”

“Au mimi nikamwambie?”

“No!!!! Usimwambieee”

Kwa mbali walimuona Lukas akiwa bize kutembea, Alvita alimuita Lukas kwa kutishia kuwa anataka kumwambia ukweli.

Lukas alisogea mpaka walipo Alvita na Sumaya aliwasalimia na kuketi.

“Lukas kuna shida hapa” Sumaya alimuangalia Alvita huku akiwa na wasiwasi sana

“Shida gani?”

“Naomba nielekeze hiki kitu kabla hatujaingia kwenye mtihani” Alimtizama Sumaya

“Upo na genius hapa unashindwa kumuomba” Alitania Lukas na wote wakacheka

“Unajua kingine Sumaya amekumiss sana hata alipokuona alifurahi akashindwa hata kukuita”

“Mimi pia nimemmiss unajua mitihani hii tunaonana mara chache sana, Sumaya usijali ngoja tumalize mitihani tutaenjoy pamoja”

Sumaya alitabasamu tu kidogo lakini moyoni alikuwa na furaha isiyoelezeka alimtizama Lukas wakati akumuelekeza Alvita ambaye hata alikuwa hamsikilizi kwani hakuwa na shida ya kuelekezwa ilikuwa ni mbinu tu ya kuwakutanisha alijifanya anamsikiliza Lukas kwa makini sana.

Alipomaliza aliaga huku akimkonyeza Sumaya kisha akaondoka, Sumaya aliishia kumtizama mpaka anapotea kwenye macho yake na ndipo akamgeukia Alvita akiwa na furaha sana wote walitizamana na kucheka tu.

Kilikuwa ni kipindi ambacho mitihani ilimalizika na Sumaya alikuwa tu nyumbani na mama yake japo mama yake hakuwa wa kushinda nyumbani kutokana na kazi zake hivyo muda mwingi alikuwa nyumbani mwenyewe tu.

Akiwa mpweke ametulia chumbani kwake majira ya saa kumi na mbili simu yake iliita na mpigaji alikuwa ni Lukas aliipokea haraka na kuweka sikioni, alikata simu akiwa mwenye furaha sana aliinuka na kwenda kwenye kabati lake la nguo alilifungua na kuanza kuchambua nguo ili aone ni ipi itamfaa, macho yake yalitua kwenye nguo moja aliitoa kwenye henga na kuijaribisha mwilini mwake kama itamfiti vizuri ilikuwa ni nguo ambayo hakuwahi kuivaa kabisa ilikuwa ni gauni fupi kiasi lilifika juu ya magoti la rangi ya maroon, aliitupia kitandani.

“That one wil fit me”

Alikimbilia bafuni na kuoga haraka kisha akaenda kuketi kwenye meza yake ya kuvalia alipaka makeup taratibu akijiangalia kwenye kioo na kupaka lipstick nyekundu mdomoni alipo hakikisha amemaliza kujiremba aliliendea gauni lake na kulivaa, alisogea mpaka kilipo kioo cha kabati la nguo na kujiangalia juu mpaka chini huku nywele zake alizosuka kwa mtindo wa rasta akiziachia na kuzivuta zote ambazo zilikuwa mbele kupitia kwenye bega na kumfanya azidi kuwa mrembo sana aligeuka geuka ili aone kama gauni limemkaa vizuri.Gauni lilimpendeza sana kwani lilibana vyema mwili wake na kufanya umbo lake lionekane dhahiri huku likiacha mabega yake wazi kwa kuwa na mikanda midogo iliyopita chini ya mabega (off shoulder) na pia kuacha nusu ya mgongo wake wazi, aliisogelea ranki ya viatu na kuchagua viatu vya rangi ya maroon sawa na gauni lake kisha alifungua tena kabati na kuchukua pochi yake akaweka pesa kidogo na tishu pamoja na vitu vidogovidogo.

Alipohakikisha kuwa alikuwa tayari aliufungua mlango wa chumba chake na kuzishuka ngazi taratibu aliuendea mlango wa sebuleni na kuufungua, uso kwa uso alikutana na Lukas ambaye ni kama alikuwa akimsubiri tu atoke nje.

“Ya mon?” Aliuliza Lukas akimaanisha kuwa’hakuna tatizo?’

“Ya mon” Naye Sumaya alijibu

Waliongozana mpaka kwenye geti na kutoka tayari Lukas alikuja na usafiri hivyo waliingia ndani ya taxi na kuondoka.

Wakati wakiwa kwenye taxi Sumaya aliichukua simu yake na kumtumia ujumbe mama yake kuwa ametoka na angechelewa kurudi na mama yake alimkubalia.Sumaya alimtizama Lukas naye Lukas alimtizama Sumaya.

“Umependeza!!!” Walijikuta wakiongea pamoja na kuanza kucheka hakuna aliyethubutu tena kutoa neno lolote kwa wakati huo mpaka wanafika kwenye hotel maarufu hapo Kingston.Lukas alitoa dola kumi ya Kijamaica na kumpatia dereva taxi kisha wakashuka na kuingia hotelini.

Waliketi na kuagiza chakula na kuanza kula, Sumaya alikuwa akila huku akimtizama Lukas kwa kuibia ibia.

“Utatumia kinywaji gani Sumaya?” Aliuliza Lukas

“Maybe wine lakini nitakunywa kidogo sana”

Lukas alimuita muhudumu wa hotel na kumuagiza kinywaji, punde waini ililetwa pamoja na glasi mbili.Sumaya alianza kunywa waini kidogo kidogo lakini kadri alivyokunywa ndio alizidi kuongeza kiwango na hata hivyo hakuwa mzoefu sana mwisho alijikuta akilewa zaidi kuliko Lukas.

“Sumaya inatosha sasa umelewa sana”

“No.. no Lukas mimi sijalewa, hivi mimi na wewe nani kulewa” Aliongea sauti ya kilevi

“Inatosha usinywe” Lakini Sumaya alikuwa mbishi aliendelea kunywa.

“Lukas hahahah unajua wewe ni handsome” Aliendelea kunywa “I love you Lukas please usinikatae nitaumia sana, Nakupenda” Japo alilewa lakini aliongea kwa hisia sana mpaka machozi yalimtoka.

“Sumaya, unalia nini?”

“Lukas hujaelewa nini nimekuambia nakupenda niambie basi hata nakupenda pia”

Lukas alijua labda ni kulewa tu alitaka kumnyanyua ili waondoke lakini Sumaya alikataa kuondoka, Aliwaza Lukas atafanya nini kwa wakati huo kurudi mpaka nyumbani kwa hali hiyo aliona sio vizuri alimuacha Sumaya hapo na kwenda mapokezi na kulipia chumba alikabidhiwa funguo.

Alimfuata Sumaya na kumwambia kuwa amelipia chumba, alimsaidia Sumaya kutembea mpaka chumbani na kumkalisha kitandani Sumaya Alimtizama Lukas na kutaka kumbusu lakini Lukas alimkwepa.

“Please usinifanyie hivyo Lukas” Alijitupa kitandani na kulala hapo hapo.

Lukas alimvua viatu na kumlaza vizuri kisha akamfunika shuka, aliketi akiyatafakari maneno ya Sumaya alisogea mpaka alipolala na kuanza kumuangalia kwa uzuri alishusha macho yake mpaka kwenye kifua cha Sumaya kilichojaa vizuri kutokana na nguo aliyovaa ilifanya kionekane kidogo kwa juu.

“Ni mrembo sana, Kwanini sikuweza kugundua siku zote hizi?”

Alijiuliza Lukas akizidi kumtizama Sumaya aliyelala

“Aah…. Lukas hebu acha hayo mawazo” Alijikuta akijikataza mwenyewe na kuona yale maneno yalitokana na pombe alizokunywa ila aliwaza wakati Sumaya akiongea ni dhahiri kuwa aliongea kwa hisia sana.

Asubuhi Sumaya alishituka na kuketi kitandani huku pombe alizokunywa zikiwa bado hazijaisha kichwani, aliangaza kila kona ya chumba lakini hakumuona Lukas alianza kupata wasiwasi na kuhisi kuwa Lukas alimuacha pekeyake.

Aliinuka ili aende bafuni na mlango haukufungwa aliingia moja kwa moja na kubaki akiacha mdomo wake wazi.

“Aaaahhhh” Alipiga kelele na kugeuka nyuma naye Lukas alishituka na kuchukua taulo kujifunga, alijisahau kabisa kufunga mlango hivyo Sumaya alimkuta akiwa hajavaa nguo yoyote ile.

“Samahani Lukas sikujua kama upo bafuni”

Alifungua mlango na kutoka bafuni, aliketi kitandani huku akifikiria jambo lililotokea bafuni muda mfupi uliopita.

Lukas alitoka bafuni akiwa hana wasiwasi naye Sumaya alipomuona alifunika uso wake kwa aibu aliinuka na kukimbilia bafuni akimuacha Lukas chumbani ambaye alikuwa amefunga taulo tu.

Baada ya muda alitoka akiwa ameoga na kumkuta Lukas tayari ameshavaa nguo zake, Lukas alijua kuwa Sumaya ni mwenye aibu sana hakutaka kumsumbua alitoka ndani ya chumba ili ampishe avae naye angemkuta nje.

Alivaa haraka na kumfuata Lukas nje walichukua usafiri kuondoka lakini njiani Sumaya hakuwa hata na ujasiri kwa kumtizama Lukas kwa aibu alizonazo.

Alimfikisha Sumaya mpaka nyumbani na taxi iligeuza kuelekea nyumbani kwa Lukas.

Ilipita wiki moja na wawili hao hawakuonana kabisa zaidi ya kuwasiliana kwenye simu tu tena kwa mara chache sana, Sumaya alijikuta akimkumbuka sana Lukas alijiandaa vizuri na kufunga safari mpaka kwa Lukas.

Alipofika alikaribishwa vizuri na msaidizi alimsalimu na kuingia chumbani kwa Lukas, alipoingia alimuona Lukas amesimama pembeni ya kitanda na alionesha kuwa alitoka kuoga na alifunga tu taulo lakini safari hii Sumaya hakuonesha aibu yoyote badala yake alisogea mpaka alipo Lukas na kumkumbatia bila kujali maji yaliyokuwa mwilini mwa Lukas.

“Lukas na… nakupe..nda , unajua…. ni kipindi kirefu nimeishi kwa maumivu ya hisia tokea tupo wadogo ulijenga hisia za mapenzi kwenye moyo wangu tumekuwa mbali kwa wiki tu lakini kwangu ni muda mrefu sana nimeshindwa kuendelea kuvumilia Lukas nimekukumbuka mno”

“Lakini……Sum…….” Kabla hajamaliza kuongea Sumaya alimkatisha na kuupeleka mdomo wake kwenye mdomo wa Lukas uvumilivu ulimshinda kabisa Sumaya na kwa muda huo hakujali lolote zaidi ya hisia zake zilivyokuwa zikimpeleka.

“I can’t hold it anymore Lukas…… siwezi tena kuzuia hisia zangu kwako” Aliongea kwa hisia na kumbusu tena Lukas.

Lukas naye alishusha mikono yake ambayo ilikuwa ikitetemeka asijue nini afanye amkumbatie au amtoe hakutegemea kabisa jambo hilo lingetokea kati yake na Sumaya kutokana na maisha waliyoishi na kuheshimiana tokea wakiwa wadogo.

“Nooo!!!! Sumaya” Alimsukuma Sumaya na kurudi nyuma

“Lukas nakuomba usinitese please, nimeteseka sana kwa kipindi kirefu Kwahiyo upo tayari kuniona nikiendelea kuteseka kwaajili yako?”

“Sikufanya yote yale kwa kuwa nilikuwa na hisia za mapenzi na wewe Sumaya lakini wewe ni mtu wa karibu sana kwangu na ulistahili yale yote”

“Kama ni hivyo kwanini ulinifanyia yote yale Lukas? Kwanini?” Akitoa machozi

“Sidhani kama ni sahihi kwetu Sumaya”

“Lakini nakupenda Lukas!!!!”

“Look Su…….” Akimshika mkono

“Niacheeeee!!!!”

Aliutoa mkono wake na kugeuka akitaka kuondoka lakini kabla hajafika mlangoni Lukas alimuwahi na kumkumbatia, alijikuta akiingiwana hisia za huruma na mapenzi kwa Sumaya kwani hata na yeye pia alihitaji sana faraja kwa wakati huo, hapo alimgeuza kwake huku wakiangaliana usoni taratibu Lukas alimbana Sumaya kwake na kuusogeza mdomo wake kwa Sumaya na kumpiga busu laini alishusha mikono yake mpaka kwenye kiuno cha Sumaya akimpapasa kwa mahaba, naye Sumaya alimkumbatia Lukas wakiwa wanapeana busu.

Alimsogeza kitandani kisha akaizungusha mikono yake mgongoni kwa Sumaya na kuifungua zipu ya gauni akalishusha nalo likadondoka chini.

“Feeling so shy” Aliongea Sumaya kwa hisia akiwa amembana Lukas.Alijiona ni kama yupo nje kabisa.

“Don’t worry about it” Lukas alimtoa wasiwasi Sumaya.

Alimlaza kitandani huku kila mmoja akiwa na shauku kubwa na mwenzie, taratibu aliitoa nguo ya ndani ya mrembo Sumaya, waliingia kwenye sayari nyingine ya mapenzi.

********

*******

*****

“Uh!!!!!” Alipiga kelele Sumaya

“Sumaya, Kwanini hakuniambia mapema?” Aliuliza Lukas na kumfanya Sumaya ahisi aibu sana kwani hakuwahi kukutana na mwanaume yeyote kimwili mpaka umri huo aliofikia aliyafumba macho yake ili asimtizame Lukas kisha akajibu

“Kwa sababu nakupenda na nakuhitaji sana sikuwa na namna Lukas”

“Umeumia sana?” Aliuliza kwa hisia za kujali sana

“Ha.. hapana sio sana ki… dogo tu”

“Polee” Alimvuta kwake na kumbusu,

Ilikuwa ni siku ambayo Sumaya alikuwa akiisubiri kwa hamu kubwa kuliko siku zote.

******

******

******

*******

**

“Mmmmmh” Alishusha pumzi ndefu Lukas “Sumaya, asante sana umenipa zawadi ya kipekee sana, la.. la…lakini sijakuumiza?”

“Lukas usijali yaani hata ungenivunja mguu nisingejali kwakuwa tu nipo na wewe”

“Unataka unipe kesi kwa Aunt Zuleya” Alitania Lukas na wote wakacheka “Inuka taratibu twende bafuni mama” Alimshika mkono na kumuongoza mpaka bafuni.

Walirejea kitandani na kulala kutokana na uchovu waliokuwa nao.

Lukas ndiye alikuwa wa kwanza kuamka alimtizama Sumaya kwa uzuri na kwa karibu zaidi alijikuta anatabasamu, alijivuta na kutaka kutoka kwenye kitanda lakini alishituka Sumaya alimshika mkono wake na kuongea kwa hisia.

“Usiondoke mpenzi” Akifumbua macho yake na kumuangalia kwa ulegevu.

“Siondoki nipo hapa kwaajili yako” Lukas alisogea kitandani alipolala Sumaya na kumkumbatia kisha akamzungusha na kuweka juu yake aliibusu midomo ya Sumaya na kumpiga denda, wote walijawa na hisia na hamu kubwa.

Alimzungusha tena na kuwa juu ya Sumaya wakipeana busu.

*****

******

*****

Dakika tisini za mpira uwanjani kila mmoja alionekana kuchoka huku Sumaya akiwa juu ya kifua cha Lukas wakihema kwa uchovu, waliishia kutizamana bila kuongea chochote ila macho yao na hisia zao ziliongea.

Jioni Sumaya alirejea nyumbani na Lukas alihakikisha amemfikisha Sumaya mpaka getini na yeye alirudi kwake, mama yake hakumkuta kuashiria kuwa alikuwa hajarudi alionekana ni mwenye furaha sana, aliingia jikoni na kuanza kuandaa chakula kizuri alichokipenda sana alipika huku akiimba imba nyimbo nzuri za mapenzi.

Aliandaa chakula mezani na muda huo mama yake alikuwa akirudi kutoka kazini, alishangazwa na hali aliyoikuta ndani kwani meza ilisheheni vya kila vya kila aina vya Kijamaica na Kitanzania hakuongea kitu baada ya kusalimiana aliingia chumbani na punde alirejea sebuleni akimtizama mwanaye ambaye alikuwa akimaliza kuandaa vitu mezani.

Alipomaliza alimkaribisha mama yake na yeye aliketi pembeni ya Zuleya.

“Kipi kinaendelea Sumaya?” Aliuliza kwa udadisi

“Mama hebu kula kwanza tutaongea vizuri haya mambo usijali”

“Mmmh sijawahi kabisa kuexperience kitu kama hiki kutoka kwako nina imani kutakuwa na jambo zuri sana”

“Punguza presha mama angu”Alimtoa wasiwasi na kuendelea kula lakini Zuleya hakuacha kumuangalia Sumaya wakati wakiendelea kula.

Baada ya kumaliza kula Sumaya aliondoa vyombo vichafu mezani na kupeleka jikoni na kuanza kuviosha taratibu, mama yake alimfuata jikoni akiwa haelewi kinachoendelea.

“Sumaya kuna nini?”

“Mama bwana mimi nimepika tu chakula kizuri leo basi kwani kuna nini?”

“I know you little girl it’s Lukas?”

“Uh…come one mom!!!”

“Niambie ni kweli si ndio?”

“Yah.. It’s him” Aligeukia upande mwingine akiona aibu

“Haya leo kuna mpya gani?”

“Finally I got him……Lukas ni wangu sasa” Uso wake ilizidi kuchanua kwa tabasamu

“Sumaya…….”

“Mom believe me Lukas now is mine”

“I see you my dear una furaha sana mpenzi, Nafurahi zaidi ukiwa na hali hiyo” Alimkumbatia mwanaye

“Lakini Sumaya chunga sana kitu hiki mwanangu nakuomba uwe makini sana”

“Mom……”

“Shii!!!! Hakuna tatizo my little babe”

Aliosha vyombo haraka na kuingia chumbani alijitupa kitandani na kuchukua simu yake alikuta missed call mbili kutoka kwa Lukas pamoja na meseji.

“Hey babe what’s up?” Aliifungua meseji iliyotoka kwa mpenzi wake mpya

“I’m good babe” Aliijibu huku akiwa na furaha sana moyoni muda huo huo alimpigia Lukas simu.

“Honey..!” Sauti laini ya msichana Sumaya ilisikika katika masikio ya Lukas na kufanya nywele zake kusisimka

“Sumaya, una sauti nzuri jamani yaani mpaka goosebumps”

“Hahahah Lukas, umeifanya siku yangu iwe ya tofauti kabisa leo”

“Sumaya mimi natakiwa kukushukuru kwa zawadi yako ya leo unajua i can’t imagine nilivyofurahi sikujua kama una nithamini na kuniamini kiasi hiki”

“Lukas ukweli nilikuwa na hisia na wewe tokea muda mrefu sana since we are young, nilishindwa nitakuface vipi lakini finally I’m with you”

“Nakupenda”

“Eeh Lukas unasemaje?”

“I love you Sumaya”

“Lukas unajua siamini kama umenitamkia maneno hayo leo, kwa mara ya kwanza Lukas umenifanya nijione wa kipekee sana”

“Huu ndio mwanzo mpenzi nitakuwa nakuambia kila siku na kila wakati ninapoamka na kulala”

Waliongea kwa muda mrefu sana huku kila mmoja akiwa na shauku ya kuongea na mwenzie bila kuacha hakuna aliyetamani kukata simu, mpaka Sumuya alizidiwa na usingizi huku akimuacha Lukas bila kukata simu naye Lukas alikata simu na kulala lakini alikuwa ni mwenye furaha sana kupita maelezo.

“Yes!” “Najua lakini nitamleta huko kwaajili yenu ahh mnajua nimemlea kwaajili hiyo hamna shida” Baada ya kusikiliza sauti ya upande wa pili aliaga na kukata simu.

Hakuwa mwingine bali ni Mr Ludovick mjomba wake Lukas, aliichukua simu yake na kumpigia Lukas Lakini haikupokelewa alijaribu mara kadhaa bado hakukuwa na majibu aliamua apige simu ya mezani na ndipo ilipokelewa na msaidizi wa kazi alimuulizia Lukas na kuambiwa kuwa alitoka muda mrefu hakuwa na cha kuendelea kuhoji alikata simu huku akiwaza pengine Lukas alikuwa hajaona kama amepigiwa na akiona atapiga

“He will call me back” Alijisemea mwenyewe na kuendelea na kazi.


* * *

“Hey Anitha changamka bwana wageni wanakuja muda sio mrefu”

“Madam kila kitu kipo Sawaa, labda vinywaji tu”

“Changamka sasa kwani una subiri nini?”

Aliitoa simu yake na kutafuta namba kisha akipiga na kuweka sikioni

“Hallow my honey.. umeshajiandaa?…… Okay stay calm mpaka nitakapo kuambia then make sure utoke bomba yaani mpaka wakusahau” Alikata simu huku akiwaka usoni kwa tabasamu huku akiwaza siku hiyo itakuwa ni ya kipekee sana kuwahi kutokea nyumbani hapo.

“Hey Anitha..?”


ITAENDELEA………..
 
SUMAYA FATE OF LOVE


SEHEMU YA SITA



“Hallow my honey.. umeshajiandaa?…… Okay stay calm mpaka nitakapo kuambia then make sure utoke bomba yaani mpaka wakusahau” Alikata simu huku akiwaka usoni kwa tabasamu huku akiwaza siku hiyo itakuwa ni ya kipekee sana kuwahi kutokea nyumbani hapo.


“Hey Anitha..?”


ENDELEA………..


“Madam nilimfuata Halima ili akaanze kuwapokea wageni ili mimi nimalizie vitu vichache hapa maana wameshaanza kuja”

“Amejiandaa vizuri?”

“Hapana…”

“So what?? Wewe nenda kapokee wageni halafu Halima aje huku chap chap”

“Sawa madam”

Alianza kuizunguka bustani na kukagua kama ipo Sawa kila sehemu na hakuna upungufu wowote.

Alimfuata mlinzi na kumpa maagizo kisha akamfuata Halima na kumtaka amalizie vitu vichache ambavyo viliachwa na Anitha, Halima na Anitha walikuwa ni wasaidizi wa kazi kwenye jumba kubwa na la kifahari la Mrs Costanzo ambaye alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa sana Tanzania alimiliki kampuni za mafuta ya ngozi na vipodozi vya asili iliyojulikana kama ‘COS CORPORATIONS’ kwa kifupi ni ‘COS CORP’ ambayo aliachiwa na marehemu mume wake aliyefariki miaka mitatu iliyopita ambaye alikuwa na asili ya Marekani ila ni Mmarekani mweusi (Black American) ilikuwa na matawi manne jijini Dar es salaam.

Siku hiyo aliandaa tafrija kubwa sana nyumbani kwake ya kumuaga mwanaye mpenzi Alvin Costanzo kwenda nje ya nchi kwaajili ya masomo yake ya chuo kikuu alikuwa akienda kusomea usimamizi wa biashara ili aje kuendesha kampuni za wazazi wake.

Katika maisha yao ya ndoa walijaliwa kupata watoto wawili tu Alvin na Nicole, Alvin akiwa amehitimu kidato cha sita na Nicole akiwa shule ya msingi darasa la sita katika shule ya gharama sana ya kulipia ambayo ni ya kimataifa (International school).

Wageni mbalimbali walizidi kumiminika kutoka sehemu mbalimbali kwaajili ya tafrija hiyo hata Mr Hernad na mke wake kwani Mr Hernad alikuwa na urafiki na familia hiyo.

Wageni wote walikusanyika katika sehemu yao maalumu na walikuwa wakimsubiri muhusika ambaye sio mwingine ila ni Alvin, Mrs Costanzo alimfuata Anitha kumwambia kuwa amfuate Alvin ili aongozane na mdogo wake wa kike aliyeitwa Nicole wawe kama surprise kwa wageni.

Anitha alielekea mpaka gorofani kilipo chumba cha Alvin hakuwa na haja ya kugonga mlango aliufungua na kumkuta Ivan ameketi kitandani akimalizia kuongea na mama yake kwenye simu.

“Nimekumiss mpenzi unajua tokea nimeamka sijakuona” Aliongea Anitha alipomkaribia Alvin

“Anitha……”

“Alvin ina maana mapenzi yetu ni ya maneno tu? Hapana bwana sio vizuri et”

“Anitha nahitaji kuondoka sasa hivi kwani mama kanisisitizia sana nimchukue na Nicole”

“Please japo kiss tu mpenzi wangu”

Walisogeleana na kupigana busu la mahaba na kisha waliachiana na Alvin alielekea kilipo chumba cha mdogo wake, aligonga mlango na Nicole alitoka akiwa amependeza sana.

“Wow!!! What the beautiful Princess!!!” Alisifu Alvin kwa muonekano wa mdogo wake ni kama mtoto wa kike wa mfalme

“And you are the handsome Prince” Alitabasamu Nicole na kumfanya Alvin afurahi, walishikana mikono na kuanza kutoka ndani kuelekea kwenye bustani.

“Yes!!!” Aliongea Anitha huku akijishika mdomoni alikuwa na furaha isiyoelezeka kwani tokea Alvin ametoka shule alikuwa akivutiwa nae sana kiasi cha kushindwa kuficha hisia zake na kuamua kumueleza ukweli japo mwanzoni ilikuwa ni ngumu kwa upande wa Alvin kwa kupitia mambo mengi ya kukatisha tamaa kwenye mahusiano lakini kutokana na kuzidiwa na msichana huyo aliamua kumkubalia tu na hawakuwahi kufanya chochote zaidi ya kuongea tu na hiyo ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kupeana busu.

Aliwafuata Alvin na Nicole nyuma taratibu ili asiwakaribie sana kuwapa nafasi ya kwenda bustanini wakiwa wenyewe tu.

“Wooooooooow!!!!!!!!!” Zilikuwa ni shangwe za wageni waliokuwepo hapo kuwasubiri wawili hao kwa hamu kubwa hakuna ambaye hakufurahi kwa kuwaona wawili hao kwa taratibu wakienda kukaa sehemu yao maalumu iliyoandaliwa kwaajili yao.

Utambulisho mfupi ulifanyika na ndipo mambo mengine yaliendelea huku Anitha macho yote yakiwa kwa Alvin mwanaume aliyempenda sana hata baadhi ya wasichana rika la Alvin waliokuwepo hapo walimkodolea macho kwani hakuwa haba Alvin alikuwa ni kijana mtanashati sana kila mwanamke aliyemuona hakuacha kuvutiwa nae.

Mrs Costanzo alitoka na kuelekea maliwato baada ya kumuona mtu aliyemfahamu akienda huko pia, Alipiga hatua za haraka ili amuwahi mtu huyo, aliweza kumsubiri mpaka alipotoka na kisha kumshika mkono.

“Gedione?”

“Nisha unahitaji nini muda huu?”

“Well….. usijifanye leo hii wewe ni mgeni kwangu Gedione” Huku akiishika shika tai ya Mr Hernad

“Hivi unajua nimemuacha mke wangu garden?”

“Inaonekana unampenda sana na kumuamini mkeo?

You real trust her but Gedione you don’t know how animal she is….”

“Una maanisha nini Nisha? Najua huo ni wivu wako kimapenzi nakuomba usimuingize kabisa Rahel kwenye hili”

Kwa umakini wa hali ya juu na jambo la haraka Mrs Costanzo alimvuta Mr Hernad na kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo kisha akafunga mlango.

“We Nicole una uhakika umemuona madam kaja huku?”

“Ndio dada Halima nina uhakika kabisa”

“Hebu twende bwana” Alimvuta mkono na kuondoka ndipo Mrs Costanzo na Mr Hernad walipovuta pumzi ya ahueni.

“Gedione hivi unajua nilikuwa nakupenda kiasi gani hata kutaka kuhatarisha maisha yangu? Lakini mwisho wa siku ulinigeuka na kumuoa Anna ukaniacha nikitapatapa kama mfa maji”

“Nisha hayo mambo hayana umuhimu wowote kwa sasa”

“Kwa sababu Anna amefariki sio? Au kwa sababu alishindwa kukuzalia mtoto?”

“Shut up Nisha!!!!”

“I won’t Gedione, una kumbuka kuwa nilikuwa tayari kukuzalia idadi yoyote ya watoto uliowahitaji kutoka kwangu Mr Hernad as they calling you… hahah…. Lakini ulinitenda vibaya kwa kuitoa mimba uliyonipa mwenyewe bila hata kujali and at the end ulinitelekeza ukaenda kuoa”

“Mrs Costanzo…”

“Gedione licha ya yote yale ukaoa wake zaidi ya wawili ili tu upate mtoto na ukasahau ulichokifanya nyuma, hata mimi pia niliolewa na nimepata watoto wawili sasa lakini ukweli usiopingika bado nakupenda sana Gedione upo moyoni mwangu”

“Nisha ya kale yamepita I’m not thinking of you anymore”

Nisha alimrukia Mr Hernad na kumpiga busu la haja akitaka kumuaminisha kuwa bado alimpenda sana lakini Mr Hernad alijitoa haraka na kuondoka akimuacha Mrs Costanzo.

Mawazo yalimrudisha nyuma Mrs Costanzo alikumbuka wakati aliopoanzisha mahusiano na Mr Hernad wakiwa shule.

“Nisha”

“Niambie mpenzi wangu” Alimtizama huku akitabasamu

“Nakupenda na unajua hilo ila ninachokuomba kuwa makini si unajua huu ni mwaka wangu wa mwisho namaliza na wewe nakuacha hapa”

“Gedione ondoa wasiwasi mimi ni wako bwana kwani utaenda kusoma mbali?”

“Ndio..”

“Gedione…”

“Hapana sitaenda mbali bwana sitaki kuwa mbali na wewe Nisha”

Wakati huo walikuwa wakitoka shule na kurejea nyumbani, Gedione alikuwa akikaribia kuhitimu masomo yake ya kidato cha nne na Nisha alikuwa kidato cha kwanza.

Walikuwa ni watu waliopendana sana muda huo asubuhi waliongozana wote kwenda shule na jioni walirudi nyumbani pamoja na waliishi mtaa mmoja.

Gedione baada ya kuhitimu aliendelea kusoma na Sasa alikuwa akisoma shule nyingine kabisa kidato cha tano na cha sita, miaka ilisonga na hatimaye alihitimu masomo yake lakini baada ya kuhitimu alipata ufadhili wa kwenda nje kusoma.Hakukuwa na namna ya Kufanya ilibidi maandalizi yaanze ili aondoke.

“Kama ingekuwa amri yangu nisingeruhusu uondoke Gedione”

“Usijali Nisha hata mimi natamani nibaki hapa na wewe ila kikubwa jitahidi usome si unajua huu mwaka wako wa mwisho?”

“Hamna shida mpenzi “

Nisha alikuwa kidato cha nne wakati ambao Gedione alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Australia kwaajili ya masomo kila mmoja alijisikia vibaya sana kumuaga mwenzie.

Ilipita miaka mitano na ndipo Gedione aliporejea tena nyumbani kutoka nchini Australia, kwa mara nyingine tena alionana na mpenzi wake Nisha ilikuwa ni furaha mpya ndani ya mioyo yao na tayari Nisha alikuwa akisoma elimu ya juu yaani chuo kikuu alikuwa akisomea Sheria ya biashara mwaka wa pili.

Waliendelea kuwa kwenye mahusiano mpaka mwaka ukaisha lakini baada ya siku chache Nisha alihisi mabadiliko mwilini mwake hivyo alikwenda hospitali kupima na kukutwa na ujauzito kwa upande wake alilifurahia jambo hilo akijua kuwa litazidi kuimarisha mahusiano yao na akiamini hata Gedione atafurahi sana.

Siku hiyo alitoka kwaajili ya matembezi na Gedione kisha wakachukua chumba kwenye hotel wakiwa na furaha sana ndipo Nisha aliamua kumweleza Gedione ukweli.

“Gedione nina bonge la surprise guess what?”

“Mmmh niambie tu mpenzi”

“Okay, can you imagine kuwa nina ujauzito Gedione”

Aliongea huku akiwa na furaha sana lakini Gedione ghafla furaha yote aliyokuwa nayo iliisha alibaki akitoa macho kana kwamba hajasikia vizuri na kumuomba Nisha arudie tena naye alimwambia tena jambo hilo.


“You can’t be serious Nisha huwezi kuwa na ujauzito”

“Gedione mimi nikajua utalifurahia hili huoni kama ni baraka kwetu mimi nipo tayari kuacha hata chuo niishi tu na wewe nikuzalie tu watoto”

“Noo… Nisha hiyo mimba ni lazima utoe utake usitake”

“Gedione..”

“Nimeshasema”

Alibeba vitu vyake vyote na kuondoka akimuacha Nisha akilia na asiamini kilichosemwa na Gedione, baada ya Gedione kuona inakuwa vigumu kumshawishi Nisha aliamua kutumia njia nyingine ya kumshawishi kwa kumpenda na kumjali kisha akampeleka hospitali bila Nisha kujua lengo la Gedione na huko daktari alishafanya mipango yote na Gedione.

Nisha hakuwa na chakufanya baada ya Gedione Kufanya alichokiona kuwa ni sahihi kwake kwani alikuwa akiamini wataendelea kuwa pamoja kwenye mahusiano lakini huo ulikuwa mwisho wa mahusiano yao na Gedione aliamua kuoa mwanamke mwingine kabisa.

Alishindwa kuendelea kuwaza sehemu iliyoumiza sana moyo wake siku ambayo Gedione alimtamkia wazi kuwa hamtaki na kwenda kufunga ndoa na mtu mwingine, alifuta machozi Mrs Costanzo.

“Ulinirubuni kuwa unanipenda Gedione na mwisho uliutesa moyo wangu lakini nilijaliwa kumpata mwanaume tajiri na akanioa alinipa kila kitu nilichotaka lakini bado sikuwa na furaha ya moyo yote uliondoka nayo Gedione.Zawadi pekee kwa mume wangu niliona nimzalie watoto tu.Gedione ulikuwa mwanaume wangu wa kwanza kukupenda tokea nilipotambua nini maana ya mapenzi na niliamua kutokuwa na mwingine zaidi yako lakini ulinitelekeza Mr Hernad….”

Alikumbuka kuwa anahitajika bustanini haraka alijiweka sawa na kwenda kwenye tafrija.Shamrashamra ziliendelea na ukafika muda wa kupeana salamu na kutakiana heri kwa kugonganisha glasi ya kinywaji kila mmoja akiwa na kinywaji chake mkononi alitembea kwa kila mtu na kufanya kama vile alivyosema muongozaji wa sherehe (MC).

Alvin alifika aliposimama Anitha na kumsalimu, Anitha alionesha tabasamu akifurahia uwepo wa Alvin.

“Alvin umependeza mpaka naona wivu” Alisema Anitha kivivu

“Wivu wa nini sasa?”

“We huoni vile wadada wanavyokuangalia? Nisije nikampiga mtoto wa mtu hapa”

“Hahahah Anitha sasa umpige kwanini et?”

“Wanamuangalia sana handsome wangu”

Waliogopa wasije kuhisiwa vibaya hivyo Alvin aliendelea kuwasalimia watu, jioni tafrija ilimalizika na kila mtu alirejea kwake sasa lakini Mrs Costanzo hakuwa sawa kabisa tokea ule muda alipoongea na Mr Hernad alijitahidi kuwa sawa mbele ya watoto wake.

Usiku Anitha hakuweza kupata usingizi kabisa kila alipojitahidi kujigeuza, aliamka akiwa amevaa tu kinguo laini cha kulalia (night dress) kilichoacha sehemu ya mapaja kidogo nje na kufanya mguu wake wa bia na mweupe kuonekana huku umbo lake likiwa dhahiri limejichonga kwenye kigauni hicho.

Taratibu kwa kunyata alizipanda ngazi kwani chumba chake kilikuwa chini na pia chumba cha Halima kilikuwa chini kila mtu alilala kwenye chumba chake alifika kwenye mlango wa chumba cha Alvin aliogopa kugonga kwani angesikika hivyo alinyonga kitasa taratibu kwa bahati nzuri Alvin hakuwa amelala kwani mlango haukufungwa aliingia na kumkuta Alvin akiwa amevaa boksa tu huku amejilaza kitandani akiperuzi kwenye simu yake alishituka kumuona Anitha, aliiweka simu pembeni na kumtizama Anitha kuanzia juu mpaka chini na jinsi alivyovaa hakuwahi kabisa kumuona Anitha akiwa hivyo alishangaa kiasi.

Anitha hakuogopa alizidi kusogea mpaka alipo Alvin bila kuogopa Alvin alikosa cha kufanya zaidi ya kumtizama tu Anitha mpaka alipomkaribia na kumkumbatia.

“A….An…Anitha umekuja kufanya nini huogopi?”

“Nimeshindwa kulala kabisa Alvin nakuwaza wewe tu mpenzi”

“Unadhani wakitukuta humu itakuwaje?”

“Alvin hilo sio tatizo nani atatukuta muda huu…. Halafu unajua unakaribia kuondoka nahitaji muda hata wa kufurahi na wewe”

“Mmh una ujasiri sana ku…..” Aliacha kuongea na kumvuta Anitha kisha akampeleka bafuni kwa haraka na kuchukua taulo akajifunga na akaenda mlangoni kufungua mlango.

“Naam mama..”

“Alvin hujalala mpaka muda huu? Na nimesikia kama ulikuwa unaongea?” Akiingia chumbani kwa Alvin huku akiangaza huku na huko

“Ndio nilikuwa naongea na simu mama marafiki zangu wananitafuta mpaka muda huu kunipa pongezi”

“Aaah sawaa nilitoka kuchukua maji maana naona kwenye friji langu maji yameisha na sikumwambia Anitha aniwekee maji na leo mambo yalikuwa mengi kweli lakini mwanangu…..”

“Mama it’s too late unatakiwa upumzike sasa maana siku ilikuwa ndefu mimi bado nipo na tutazidi kuongea usijali mama”

Alvin aliona mama yake anampotezea muda maana na Anitha alikuwepo humo, Mrs Costanzo hakuwa na kipingamizi aliondoka na huku akimuacha Alvin akisikilizia mlangoni kuhakikisha kama mama yake aliondokana kuingia chumbani kwake baada ya kuhakikisha mlango wa mama yake ukifungwa alienda bafuni na kumtoa Anitha ambaye alihema kwa kushukuru maana kama bosi wake angemkuta humo tena na hivyo alivyovaa ingekuwa ni hatari.

Alimsogelea Alvin na kumkumbatia kwa mahaba bila kujali chochote hata naye Alvin alijibu kwa kurudisha kumbatio hilo kwa Anitha.

“Usiku wote huu nitakuwa na wewe Alvin kuwa huru na mimi”

“Lakini Anitha……”

“Shiii…. Usiongee chochote”

Alvin alikuwa anajitahidi kutofanya chochote na Anitha lakini anajikuta anazidiwa na kushindwa kujizuia hata baada ya kuutizama mwili wa Anitha aliyevaa kinguo laini na chepesi kilichouchora mwili wake.

Aliusogeza mdomo wake mpaka kwa Alvin na kumpa denda laini na kuzidi kumpagawisha Alvin, alirudisha shambulizi kwa Anitha na kuanza kupapasa kila sehemu ya mwili wake naye Anitha uvumilivu ulimshinda kwa kuzidiwa na hisia kumuelekea Alvin alikitoa kigauni chake na kukidondosha chini, Alvin alizidi kushangaa kwa jinsi Anitha alivyoumbika na kuwa na mwili laini.

Walijikuta wanashindwa kustahimili zaidi na kuangukia kwenye huba zito.

*******
******
*******
****
**


“You can’t be serious Nisha huwezi kuwa na ujauzito”

“Gedione mimi nikajua utalifurahia hili huoni kama ni baraka kwetu mimi nipo tayari kuacha hata chuo niishi tu na wewe nikuzalie tu watoto”

“Noo… Nisha hiyo mimba ni lazima utoe utake usitake”

“Gedione..”

“Nimeshasema”

Mr Hernad aliyakumbuka maneno hayo alishindwa kabisa kupata usingizi alijutia kitendo alichokifanya kwa Nisha aliwaza mengi sana mpaka kukumbuka alipomrubuni Nisha na kutoa ujauzito

“Mpenzi, nisamehe kwa yaliyotokea sikuwa tu vizuri muda ule ila nahitaji twende hospitali tukapate angalau ushauri tu wa daktari si unajua sio jambo la kukurupuka”

“Asante Gedione mimi sina shida nimekusamehe mpenzi, nisubiri kidogo nibadilishe nguo”

Baada ya muda mfupi Nisha alitoka na kuongozana na Mr Hernad mpaka hospitali walionana na daktari akawapa ushauri kidogo kisha akamuita Nisha na kuingia naye katika chumba ambacho kilikuwa na kitanda na Nisha alipewa agizo kuwa alale kitandani ili amfanyie uchunguzi bila kujua nia ya daktari huyo alitii agizo na kufanya kama alivyoambiwa, alimchoma sindano ya usingizi na ya kuzuia maumivu yaani sindano ya ganzi.

Baada ya nusu saa zoezi lilimalizika lakini Nisha hakuwa ameamka kutokana na sindano, alipoamka alihoji juu ya kilichotokea lakini alielezwa kitabibu zaidi hivyo alielewa.

Waliongozana pamoja ma kurejea nyumbani lakini Nisha alihisi hali tofauti kabisa mwilini maumivu kidogo tofauti na ilivyokuwa mwanzo kabla hajaenda hospitali na kuamua kumuuliza mwenzie.

“I’m sorry Nisha kwa nilichofanya lakini sikuwa na namna ilibidi tu uabort!”

Maneno ya Mr Hernad yalikuwa kama kisu cha moto kilochouchoma moyo wa Nisha nguvu zilimuishia na kujikuta akikaa chini machozi yakimtoka na mwili wake kuwa baridi ghafla.

“Why Gedione why are you doing this to me? Nimekukosea nini mwanangu amekukosea nini hata ukaamua kumkatili kiasi hiki? Niambie Gedione..!”

“Nisha nisamehe”

“Msamaha wako una msaada gani kwa sasa Ged? Umenikatili sana”

“Nimefanya hayo yote kwasababu nakupenda Nisha sikuwa na cha kufanya”

Baada ya siku chache hali ilikuwa shwari Nisha alimsamehe Mr Hernad na kuacha hilo lipite lakini baada ya muda alimfuata Nisha na kumuweka wazi jambo ambalo lilikuwa ni tata sana na alijua kuwa ni gumu kwa upande wa Nisha.

“Nisha samahani sana kwa hili lakini lazima nikuambie”

“Niambie”

“Nisha mimi nimepata mchumba na next week napeleka posa”

“What!!!!!!… hivi Gedione unachukulia hili jambo ni rahisi kiasi hiki?”

“Sina cha kukuficha zaidi Nisha maana mficha maradhi kifo humuumbua”

“Huu mwaka umeniamulia Kwanini unaniumiza hivi Gedione? Nimekosea wapi mimi Kwahiyo sina thamani tena kwako please nakuomba usinifanyie hivi kama kuna kitu nimekukosea nisamehe”

Alipiga magoti kuomba msamaha ili tu Mr Hernad asimuache lakini hilo halikufua dafu kwani Mr Hernad alishafanya maamuzi yake

“Please kuanzia leo usinitafute kabisa Nisha start your own life” Alimuaga na kuondoka akimuacha Nisha akiangua kilio kama mtoto bila msaada wowote.

Mr Hernad alishindwa kujizuia chozi lilimtoka akijilaumu kwa alichokifanya kwa Mrs Costanzo miaka ya nyuma.

“Ni kweli nilikukosea sana Nisha please nisamehe sana, i was wrong by that time but nilijiona nipo sahihi….. Nisha.. aaah” Alifuta machozi

Alikumbuka mengi sana aliyofanya na Nisha wakati ule wapo kwenye mahusiano lakini.

Wakati akiendelea kuwaza mke wake alishituka na kumkuta mumewe akiwa ameketi na kuegamia kitanda akiwa mbali kimawazo.

“Mume wangu….. mume wangu?” Aliita Rahel kwa sauti ya chini iliyojaa usingizi.

Mr Hernad hakuwa na habari kama mke wake ameshaamka na anamuita mpaka pale alipomgusa bagani ndipo alishituka na kumtizama mke wake asijue atamwambia nini.

“Kwani tatizo nini mbona hujalala mpaka muda huu mume wangu?”

Alimuuliza huku naye akijiinua kwenye kitanda lakini Mr Hernad hakumjibu chochote badala yake alivuta shuka na kugeukia upande mwingine akijifanya kulala alimuacha mke wake njia panda hata hivyo naye aliona alale tu na kusubiria kesho ili aongee naye kinaganaga pale pale simu ya Mr Hernad ilianza kuita na jina lilisomeka kwenye kioo cha simu ‘COS CORP’ na hivyo ndivyo alimsave Mr Costanzo kwenye simu yake aligeuka kidogo na kumtizama mke wake ambaye naye alikaza macho yake kumtizama mume wake bila kusita Mr Hernad aliipokea simu hiyo na kuweka sikioni ilisikika sauti ambayo haikuwa ngeni kwake na alikuwa akiisikia sana siku za nyuma sauti nzuri ya Mr Costanzo ambaye japo umri ulisogea lakini alizidi kuwa mzuri kama binti wa miaka ishirini na tano na sauti yake haikubadilika ilizidi tu kuwa nzuri na laini.

“Gedione nimeshindwa kulala mwenzio kuonana na wewe leo kumezidi kuibua hisia nyingi za mapenzi juu yako nakuomba kesho tuonane Gedione utachagua wewe ni wapi mimi nitakuja……talk to me please Ged…. I will be so upset if you let me down”

“O….Okay….. tutawasiliana ke… kesho tafadhali” Alibabaika na kushindwa kuongea kuongea vizuri huku mke wake akizidi kumuangalia kwa mashaka alikata simu na kuweka pembeni kisha akaendelea kulala bila kumsemesha mke wake.

Hali ya Mr Costanzo haikuwa nzuri hata baada ya kuongea kwenye simu kidogo na Mr Hernad hakuridhika alihitaji kuonana nae.

“I’m so silly…… ina maana nimeshindwa kuvumilia mpaka asubuhi nimpigie sijui kimetokea nini muda huu yupo na mke wake si nitamuweka kwenye hali ngumu Gedione…… Nisha you are so stupid”

Alizidi kujilaumu na kujitukana mwenyewe kwa kumpigia simu Me Hernad usiku kama huo na ili hali alijua kabisa amelala na mke wake mara ghafla ujumbe uliingia kwenye simu yake alipoangalia aliyetuma jina lilisomeka ‘GEDIONE’ aliifungua haraka ili ajue ni kipi kimeandikwa.



ITAENDELEA……….
 
SUMAYA FATE OF LOVE


SEHEMU YA SABA



“I’m so silly…… ina maana nimeshindwa kuvumilia mpaka asubuhi nimpigie sijui kimetokea nini muda huu yupo na mke wake si nitamuweka kwenye hali ngumu Gedione…… Nisha you are so stupid”

Alizidi kujilaumu na kujitukana mwenyewe kwa kumpigia simu Me Hernad usiku kama huo na ili hali alijua kabisa amelala na mke wake mara ghafla ujumbe uliingia kwenye simu yake alipoangalia aliyetuma jina lilisomeka ‘GEDIONE’ aliifungua haraka ili ajue ni kipi kimeandikwa.


ENDELEA……….



“Nisha ni kweli nimekukosea sana kipindi cha nyuma nilijiona sahihi sana but i was wrong, nisamehe sana ila sijapenda ulivyonipigia simu usiku huu na unajua kabisa kuwa nipo na mke wangu hivi unafikiri amejisikiaje nimeona kutopokea ningesababisha shida kwa mke wangu na ndio maana nikaona nipokee tu so please naomba usinipigie simu Nisha.Good night.”

Meseji ya Mr Hernad ilisomeka hivyo kwa namna nyingine ilimuumiza sana Nisha ila hakuwa na la Kufanya zaidi aliiweka simu pembeni na kujilaza kitandani akiwa mwenye huzuni sana.


* * *

“Aah uncle Carlos!!!!! How are you?”

“I’m great fine Sumaya” wakikumbatiana kama ishara ya kukumbukana maana wameonana muda mrefu sana kisha Sumaya alimnong’oneza kitu Carlos

“Kutana na Mama yangu Zuleya….. Mom Zuleya huyu ni uncle wangu wa kitambo sana anaitwa Carlos”

“I’m glad to meet you Carlos” Walishikana mikono na kusalimiana.

Waliendelea kuzunguka supermarket kutafuta vitu mbalimbali, na baada ya muda Sumaya alitoka kidogo kuwapisha maana yeye ndiye aliweka mtego na kuwakutanisha wawili hao mpango ulikuwa wake na Carlos.

“Wewe ni mama yake mzazi kabisa wa Sumaya?” Lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa Carlos na kuuvunja ukimya mrefu uliotawala baina yao baada ya Sumaya kuwaacha

“Hapana ni mtoto wa dada yangu mimi ni mama yake mdogo”

“Ooh mmefanana sana aisee”

Yalikuwa ni maongezi marefu sana kati ya Carlos na Zuleya yote hayo ilikuwa ni kufahamiana zaidi na kujenga urafiki, walibadilishana namba za simu kwaajili ya mawasiliano.

Muda ulipita na Sumaya alirejea huku akiwa kama hafahamu chochote kile alimfuata mama yake.

“Mama samahani kwa kukuacha hapa bila kuaga”

“Ulienda wapi maana nilishindwa hata kukuuliza uliondoka ghafla sana?”

“Lukas aliniita mara moja nami nikaona nisiwasumbue”

“Lakini alikuwa mgeni wako huyu ukaamua kumuacha hapa Sumaya”

“Samahani mama” Sumaya alitabasamu chini chini akiufurahia mpango wake, baada ya muda waliagana na kisha Sumaya na mama yake waliingia kwenye gari na kuondoka wakiwa njiani hakuna aliyethubutu kuongea chochote kwa mwenzie na badala yake Sumaya alikuwa bize na simu yake huku mama yake akiwa bize na usukani.

“We Sumaya hebu niambie huyo uncle wako mmefahamiana vipi?” Aliuliza Zuleya akionekana kutaka kufahamu vitu fulani kuhusu Carlos

“Shuleni, ni mpishi mzuri sana kwani hajakuambia?”

“Kuhusu kuniambia hivyo havikuhusu nataka tu kujua mmefahamiana Vipi”

“Aaaah alikuwa anakuja shuleni mara kwa mara kukiwa na events mbalimbali kama sherehe na yeye ndiye anapewa tenda ya kuleta chakula kutoka kwenye mgahawa wake kwahiyo mara kadhaa huwa ananisalimia tukazoeana tu hivyo”

“Ina maana wanafunzi wote shuleni kwenu alikuzoea wewe tu?”

“Hapana ni wengi ila mimi ndiye nilikuwa rafiki yake mkubwa sana”

“Oooh sawaa, He is so kind” Alijikuta akiropoka mbele ya Sumaya

“Ni kweli mama he deserve to be my father…” Naye Sumaya aliongea kwa mtego

“Shut up!!!!!!”

Ukimya ulitawala mpaka wanafika nyumbani na kuanza kutoa mizigo yote kwenye gari na kuingiza ndani baada ya kufanya hivyo kila kitu kiliwekwa mahali pake na kisha kila mmoja aliingia chumbani kwake kama kawaida kwa upande wa Sumaya ilikuwa na kuongea na Lukas lakini leo kwa upande wa Zuleya mambo yalikuwa ni tofauti kabisa na siku zote alikuwa ni mwenye furaha sana huku akizungumza na Carlos kwa muda mfupi tu walizoeana na kuwa marafiki.

Carlos Williams kijana mtanashati na mstaarabu asiyekuwa na makuu na mtu yeyote, alikuwa ni mzaliwa wa Kenya na aliishi huko na familia yake, katika maisha yake alipenda sana mambo ya upishi kwa sababu mama yake alikuwa akipika vyakula vizuri ambavyo yeye alikuwa akivipenda sana na alimzoesha kwenda kwenye mgahawa wake mdogo alipokuwa akipika kama mama ntilie wakati bado akiwa kijana mdogo sana hivyo suala la upishi lilitawala akili ya Carlos na kupenda sana kupika.Hata alipohamia nchini Jamaica alifanya kazi kwenye migahawa tofauti na baadae alipopata mtaji alifungua mgahawa wake uliokua siku hadi siku na kupata umaarufu mkubwa katika maeneo mengi ya mji wa Kingston hata kuanza kupata tenda sehemu tofauti tofauti kwenye mikutano, sherehe na matukio mbalimbali kwa sababu alipika chakula kwa usafi na ustadi wa hali ya juu.

“Lukas kama tulivyoongea muda ndio huu mimi nifanye maandalizi uende chuo”

“Lakini mjomba mimi naona tu nisome hapa hapa hamna shida na pia vyuo vipo vinavyofundisha carrier yangu”

“Hilo sio la muhimu Lukas kikubwa uende huko na mimi nimeshapigiwa simu kwahiyo naanza maandalizi”

“Sawa mjomba” Muda huo Lukas akili yake yote ilikuwa ikimuwaza Sumaya ambaye itabidi amuache hapo na ndio kwanza penzi lao lilikuwa likianza kukita mizizi na kuchanua, alipata mawazo sana.

Aliingia chumbani kwake na kupiga simu baada ya kuongea kwa muda mrefu alikata simu na kuanza kujiandaa kisha aliondoka zake.

Jioni Sumaya alionekana akiwa kwenye kioo chake kwenye meza ya kuvalia nguo akijiremba, alichukua kitana kikubwa cha nywele na kuzichana nywele zake ndefu zilizofikia usawa wa chini ya mabega kuelekea mgongoni kisha akakata mstari katikati kutenganisha nywele pande mbili halafu akachukua jelly ya nywele na kuipaka pembeni ya nywele alizivuta kwa nyuma usawa wa shingo na kuzibana kila fungu kwa upande wake kisha akachukua mafuta mengine kwenye kopo jeusi na kupaka kwenye mikia ya nywele na kisha kuzichana hapo zikawa na mawimbi madogomadogo na kujaa kama kaweka vibanio alimalizia kwa kupaka makeup na lipstick nyekundu mdomoni aliliendea kabati na kutoa kigauni cha rangi ya blue na kukivaa kilikuwa kimefunika shingo yake huku nyuma ikiacha nusu ya mgongo wazi, ilimfika usawa wa magoti na kumkaa vema kabisa mwilini mwake.

Alipomaliza alichukua hereni za rangi ya dhahabu kubwa mfano wa duara kama bangili na kuzivaa kisha akachukua viatu vyeusi na kuvaa akabeba na pochi yake nyeusi.

Alimfuata mama yake ambaye alikuwa sebuleni akiangalia tamthiliya aliketi jirani na kumtizama bila Kuongea chochote.

“Why are you looking me like a beggar?”

( Kwanini unaniangalia kama omba omba?) Aliuliza Zuleya baada ya kugeuka na kumuona Sumaya akimtizama

“Hahahah!!!!” Alicheka Sumaya bila kujibu

“Wewe mtoto utakuwa chizi wewe”

“Sorry mom I have a date today”

Hapo Zuleya alimuangalia kwa kumkazia kisha akacheka na kumwambia Sumaya.

“Sikuwa hata na hilo wazo kwanza sikukuangalia et you look so amazing ni Lukas huyo, haya unaenda wapi leo?”

“Hata sijui ila naweza nisirudi leo mama……”

“We hebu ishia hapo hapo, sasa hivi ni saa 12 na nusu by saa nne nataka uwe hapa”

“Mom huoni kama muda hautoshi sasa si bora nisiende tu?”

“Nimeshasema na sirudii…….” Alishituka baada ya kuona ujumbe kwenye simu aliachia tabasamu na kuinuka akielekea chumbani juu

“Mama inakuwaje sasa?”

“Nenda.. nenda”

“Na muda wa kurudi Vipi?”

“Nenda tu nenda”

Sumaya hakutaka tena kuuliza alijua ni ofa amepewa hivyo alichukua simu yake na kutuma ujumbe kisha akaingia chumbani kwake na kujiweka Sawa punde ujumbe uliingia kwenye simu yake na kuusoma alilipuka kwa furaha na kuanza kuelekea ulipo mlango aliufungua na kutoka ndani haraka, alifika hadi nje ya geti na kulikuta gari jeusi na punde alishuka Lukas akiwa kwenye mavazi nadhifu sana alimkumbatia Sumaya na kumsalimu kisha akamfungulia mlango na baada ya Sumaya kuingia naye aliingia na dareva aliliondoa gari.

Huku nyumbani Zuleya naye alikuwa akijiandaa kwaajili ya kutoka kwenda dinner na Carlos alikuwa ni mwenye furaha sana kwani ni muda mrefu sana hakuwahi kutoka kwaajili ya dinner wala date tokea wanaanza mahusiano na Dajuan wakati penzi lao linaanza kuchipuka, machozi yalianza kumtoka lakini aliyazuia haraka na kuyafuta kisha aliichukua tena makeup na kupaka usoni alipomaliza aliketi kitandani na kuichukua simu yake alikuta ujumbe kutoka kwa Carlos.

“I’m on my way to your house, usijali nakumbuka ulivyonielekeza pia natumia map”

Alitabasamu na kumjibu kuwa alikuwa akimsubiri tayari ameshamaliza kujiandaa.

Zilipita dakika ishirini na tano honi ya gari ilisikika nje na Zuleya alitambua kuwa hakuwa mwingine ni Carlos alitoka ndani na kuelekea getini alipofungua aliliona gari aina ya BMW nyeusi na tayari Carlos alitoka ndani ya gari na kuegemea gari hiyo, Carlos alimsalimu Zuleya kisha akamfungulia mlango na yeye akazunguka upande wa pili wa gari n kuingia muda huo huo alipiga moto gari na kuondoka hapo.


‘R HOTEL KINGSTON’ maandishi makubwa yalisomeka juu ya jengo kubwa la hotel hiyo ya kifahari sana yenye hadhi ya nyota tano iliyopo New Kingston katika jiji la Kingston.

Sumaya aligeuza shingo yake na kumtizama Lukas kana kwamba anamshangaa naye Lukas alijua ni kwanini Sumaya anamshangaa hivyo.

“Look Sumaya ni vitu vya kawaida sana hivi usiwaze sawa”

“Lukas this place is too expensive how could you do that?”

“Because i love you Sumaya and i want you to enjoy our date”

“This is not our first date Lukas”

“I know but najali sana furaha yako”

“But Lukas……”

Lukas alimziba mdomo Sumaya akimtaka asiendelee kuongea naye akatoa dola ishirini za kijamaica kwenye wallet yake na kumpatia dereva kisha wakashuka na kuelekea ndani ya hotel hiyo, walifika mapokezi Lukas alimuonesha Sumaya sehemu ya kukaa kisha yeye akaelekea kwa muhudumu wa hotel hiyo aliyekuwa mapokezi ambaye alivalia sare za kazi na kuongea naye baada ya muda alitoa funguo na kumpatia Lukas, Lukas alimsogelea Sumaya na kumpa ishara kuwa waondoke naye Sumaya alimfuata Lukas na kuongozana wote mpaka kwenye lift ambayo iliwafikisha ghorofa ya tatu walishuka ndani ya lift na kuanza kutembea kuelekea upande wa kulia na hapo walitazamana na mlango ulioandikwa kwa juu ‘NO 205’ aliichukua kadi yake na kuingiza mlangoni na mlango ulifunguka kisha Lukas alimziba macho Sumaya na kuingia naye ndani ya chumba.Ilikuwa ni hotel ya hadhi sana na wakati huo gharama ya usiku mmoja tu ilikuwa inakaribia shilingi laki tatu za kitanzania.

“Surprise!!!!!!!” Yalikuwa maneno ya Lukas alipomuachia Sumaya, uvumilivu ulimshinda Sumaya akajikuta anapiga kelele na kumkumbatia Lukas kwa furaha.Chumba kilivutia sana huku mezani zikijaa zawadi mbalimbali zilizofungwa zote ni kwaajili ya Sumaya nyingine zikiwa kwenye box na nyingine kwenye vifungashio maalumu vya rangi ya pink na nyekundu kwaajili ya zawadi.

“Asante sana mpenzi lakini umetumia gharama nyingi sana Lukas”

“Sumaya kwako sioni hasara yoyote hata nikitumia pesa kiasi gani kuwa huru na mimi kingine nilitaka leo iwe siku special sana kwetu halafu umependeza sana kipenzi unajua kujiremba mtoto wa kike lakini na uzuri wako pia unazidi kukufanya uonekane the best”

“Love…”

Alimsogelea Sumaya na kuanza kumpa busu laini huku Sumaya naye akimkumbatia Lukas kwa nguvu, waliendelea kupeana busu la mahaba na ghafla mlango uligongwa na kuwashitua wawili hao na Lukas ndiye alielekea mlangoni kisha alimkaribisha muhudumu ambaye alibeba chakula kwaajili yao baada ya kuviweka mezani aliwakirimu na kuondoka.

Lukas alimshika kiuno Sumaya na kumvutia kwake tena na kuanza kupeana busu la mahaba, waliendelea kuzungushana hapo naye Lukas aliivua t sheti lake na kuliweka kando kisha taratibu alilivuta gauni la Sumaya na kufanikiwa kulivua kwenye mwili wake na kulitupa pembeni, kila mmoja alijawa na hisia nyingi juu ya mwenzie alimlaza kitandani kwa taratibu na kuingia kwenye sayari ya mahaba.

*************
*********
********
******
****
**


Walionekana Zuleya na Carlos wakiingia ndani ya R HOTEL bila kujua kuwa Sumaya na Lukas walikuwepo hapo pia, walichangua meza ambayo ingewafaa wao wawili tu na kwenda kuketi punde muhudumu aliwafuata na kuwapa list ya vyakula kwaajili ya kuchagua ni kipi kitawafaa ili awaletee, baada ya kuchagua muhudumu aliondoka na kuwaacha hapo.


“Ahh kuna kitu nilisahau kabisa hivi uncle yuko wapi?”

“Uncle?”

“Ooh sorry i mean your daughter Sumaya ina maana umemuacha nyumbani pekeyake?”

“Aah Sumaya” Alitabasamu kidogo na kusema “She is out for her date today”

“Oh okay” Alijibu Carlos akimtizama Zuleya ambaye aliinana chini kwa aibu kidogo

“Look Zuleya haya ni mambo ya kawaida halafu Sumaya sio mtoto mdogo anajua jema na baya kwahiyo usihisi vibaya kuwa nimelipokeaje Sawa dear?”

Zuleya aliinua kichwa chake na kumtizama Carlos ambaye alikuwa akitabasamu huku naye akimtizama pia alilipokea tabasamu la Carlos kwa kutabasamu na muda huo chakula kilietwa na muhudumu aliwakirimu kisha akaondoka.Walianza kula huku kila mmoja akimtizama mwenzie bila kuzungumza chochote ila macho yao yaliongea zaidi.


“Ooh babe you are so amazing”

Ni maneno ya Lukas akimwambia Sumaya kisha akampiga busu laini.

Waliendelea kukumbatiana kwa muda kisha wakainuka na kuelekea bafuni ili waoge kisha wale chakula.

Wakiwa bafuni hawakuacha kucheza cheza kumahaba huku wakimwagiana maji na sasa wote walijikuta wakipandwa na hisia tena na kumaliza kila kitu huko huko bafuni, walipomaliza na kuhakikisha kila mmoja ametosheka walioga na kwenda kuketi kitandani ili wapate chakula kwani muda huo njaa ilianza kuwashika kutokana na shughuli pevu iliyofanyika.

Lukas alitoa kibox kidogo chekundu alikifungua na kutoa mkufu wa dhahabu uliovutia sana kwa nakshi zake na kung’aa ulikuwa na maandishi madogo yaliyoandikwa kwa herufi kubwa yaliyosomeka ‘SUMAYA’ na kidani chake kilikuwa kikifunguka na kwa ndani kiliandikwa kwa herufi kubwa pia yaliyosomeka ‘LUKAS’

Alimvalisha Sumaya shingoni huku Sumaya naye akiendelea kukiangalia na kuonesha kuwa kimemvutia sana.

“Lukas nakupenda, Asante kwa zawadi yako nimeipenda sana” Alimkumbatia na kumpiga busu

“Usijali”

“But why this today Lukas Kwanini unafanya haya yote leo?”

“Mpenzi usiwaze hebu tule najua una njaa sana maana ule mtanange sio wa kitoto” Aliongea Lukas na kumfanya Sumaya acheke.

Walikula chakula na walipomaliza walijilaza kitandani na kuanza kupiga stori mbalimbali za kuchangamsha huku kila mmoja akiwa na furaha sana ndipo kwa utulivu Lukas alimsogelea zaidi Sumaya huku akimtizama usoni naye Sumaya alielewa hilo na kujiweka tayari kusikia kile ambacho Lukas alitaka kumwambia.

“Why this today?……. Am Sumaya upo sahihi kuuliza hivyo mpenzi”

“Una maanisha nini Babe?”

“Ukweli……. Aahh but I’m sorry Sumaya nina safari ya kwenda chuo nje ya Jamaica”

“What!!!!!!!” Sumaya alipata mshituko kidogo aliposikia hivyo

“Ndio Sumaya naweza kwenda Marekani au Mexico na sio kama nimeamua mimi ila mjomba ndio amepanga haya yote siwezi kupinga” Aliongea Lukas kwa huzuni hata Sumaya alitambua hilo alimkumbatia akijaribu kumfariji

“Lakini Lukas inakuwaje kuhusu mimi na wewe?”

“Huu sio mwisho Su mawasiliano yapo unajua wewe ndio kila kitu kwangu”

Walikumbatiana hapo mpaka wakazidiwa na usingizi wote.

Carlos na Zuleya walipomaliza kula na kuridhika Carlos alimrudisha Zuleya nyumbani kwani muda ulienda sana alihakikisha Zuleya ameingia ndani na kisha yeye alielekea nyumbani kwake, Carlos alijipiga kifuani na kujiona amepiga hatua kubwa sana kwa Zuleya mpaka kufikia hapo njiani aliweka nyimbo tofauti za mapenzi zilizomvutia kwa wakati huo kutokana na furaha aliyonayo.

Alifika nyumbani kwake ambapo aliishi mwenyewe tu, alipaki gari yake na kuingia ndani akaelekea chumbani kwake kabla hajafanya chochote simu yake iliita na Zuleya ndiye alikuwa mpigaji aliipokea na kuweka sikioni.

“Hallo Carlos! Umefika nyumbani?”

“Mmmh Zuleya hiyo sauti mbona kama upo kitandani, yes ni kama ulikuwa ukinifuatilia nimeingia chumbani sasa hivi”

“Aah tayari nimejilaza tu kitandani and i have nothing to do actually nilitaka kuuliza kama umefika salama maana usiku ni mnene”

“Usijali dear mimi nimefika salama”

“Okay usiku mwema Carlos”

“Na kwako pia Zuleya”

Zuleya alikata simu na kuiweka pembeni alikuwa na furaha sana na hakujua ni kwanini hali hiyo inampata.

“Sijui kwanini nikiwa na Carlos nakuwa mwenye furaha sana hata nikiongea naye i guess i’m in love, yes nampenda Carlos” Alijishika upande wa moyo huku akiyasikilizia mapigo yake ya moyo yanavyoenda haraka.

Asubuhi wakiwa bado hotelini Sumaya ndiye alikuwa wa kwanza kuamka, alimtizama Lukas alipolala bila kumuamsha kisha akampiga busu mdomoni naye Lukas alishituka na kumtizama Sumaya waliamka na kwenda bafuni kuoga kisha wakajiandaa kwaajili ya safari ya kurudi nyumbani.

Mlango ulifunguliwa na Sumaya aliingia ndani akiwa amebeba mabox na vimifuko vya zawadi alielekea moja kwa moja mpaka chumbani kwake na kuweka mizigo kitandani nyumba ilikuwa kimya sana alihisi huenda mama yake aliondoka ila aliona akamuangalie chumbani kwake, Alifungua mlango wa chumba cha Zuleya na kumkuta akiwa amelala hakutaka kumsumbua hivyo alitaka kutoka lakini kabla hajafanya hivyo alisikia akiitwa aligeuka na kumtizama mama yake.

“Yaani Ndio unarudi muda huu jana nilikuambia nini?”

“Mama…..”

“Umejisahaulisha sio? Anyway za unakotoka?”

“Safi…. Nilidhani umeondoka maana nyumba ipo kimya sana”

“Leo weekend mapumziko yangu, ulikuwa wapi jana?”

“Uuuh….. R Hotel mama”

“R Hotel?”

“Ndio kwani vipi?”

“Nothing…”

“But I’m sorry kwa kukuacha jana mpweke”

“Usijali hata hivyo nilitoka pia”

Sumaya alimuangalia mama yake kama vile alitaka kumuuliza ila akamuaga na kwenda chumbani kwake, alimpigia simu Lukas kuhakikisha kama ameshafika nyumbani na baada ya hapo alielekea jikoni ili kuandaa chai.

Wakati akiendelea kuandaa chai alisikia alarm ya mlangoni ikipiga kelele kuashiria kuwa kulikuwa mtu mlangoni, aliacha Kufanya alichokuwa akikifanya na kwenda mlangoni kuufungua mlango alipofungua ghafla alipigwa na butwaa asiamini alichokiona mlangoni pale.

“You again?”


ITAENDELEA………..
 
SUMAYA FATE OF LOVE


SEHEMU YA NANE



Wakati akiendelea kuandaa chai alisikia alarm ya mlangoni ikipiga kelele kuashiria kuwa kulikuwa mtu mlangoni, aliacha Kufanya alichokuwa akikifanya na kwenda mlangoni kuufungua mlango alipofungua ghafla alipigwa na butwaa asiamini alichokiona mlangoni pale.


“You again?”


ENDELEA…….



“Sipo hapa kuulizwa maswali yako kama mama yako yupo muite nina shida naye”

“Siwezi Kufanya huo upuuzi ondoka hapa kwanza mama hayupo”

“Sumaya hivi unajua huwa sina mchezo tena haswa kwa watoto kama wewe”

“Ondoka kabla sijakuitia watu hapa unataka nini kwetu?”

Zuleya alisikia sauti za watu wakibishana sebuleni hivyo alivaa haraka na kwenda kuangalia ni nani anabishana na Sumaya alishuka haraka mpaka sebuleni naye hakuamini alichokiona.

“Dajuan…..?”

“Zuleya”

Ni muda mrefu umepita huku Zuleya na Dajuan wakiwa hawana mawasiliano ya aina yoyoten wala kuonana Sumaya hakutaka kuingilia maongezi yao aliingia jikoni kuendelea kuandaa chai.

“Kuna kitu chochote ambacho ulikisahau hapa wakati ule ulipoondoka?” Aliuliza Zuleya akionesha kabisa hakufurahishwa na uwepo wa Dajuan nyumbani kwake

“Uuh… Zuleya… look..” Alipiga magoti Dajuan “Zuleya I’m sorry najua nilikufanyia mambo mabaya sana wakati ule nimegundua kuwa wewe ni mwanamke wa pekee sana kwangu”

“Kwahiyo leo ndio umegundua kuwa mimi ni mwanamke wa pekee kwako?”

“Zuleya……”

“Shut up Dajuan siwezi tena kuwa na wewe na isitoshe nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine kwa sasa”

“Zuleya…….”

“Yes Dajuan I’m in love.Nilikupenda na kukuvuilia bila kujali yote uliyokuwa ukinifanyia na ukaniona mpuuzi, et leo unakuja turudiane are you okay?”

“Zuleya nilikamatwa na kwa kipindi chote nilichokuwa kimya nilikuwa gerezani sio kama nilikuwa sikupendi mpenzi”

“I don’t care…….. Dajuan sijali ulikuwa wapi ila siwezi kurudia ya nyuma ambayo yaliumiza moyo wangu na maisha yangu”

Muda huo huo Carlos alikuwa aliingia ndani na kukuta hali hiyo kwa haraka Zuleya alipomuona Carlos alimfuata na kumkumbatia huku akilia.

“Kuna nini Zuleya?”

“Carlos…….” Alishindwa kuzungumza chochote badala yake alizidi kulia,

Kwa hasira na wivu Dajuan aliinuka na kutaka kumvamia Carlos ili amfundishe adabu.

“Dajuaaan!!!! get out of here now!!!” Alipaza sauti Zuleya huku akiwa amebadilika kabisa na kuwa mwekundu usoni kwa hasira na kilio, Dajuan alisitisha alichokuwa akitaka kukifanya na kumtizama Zuleya na asiamini maana hakuwahi kumuona Zuleya akiwa hivyo, Huku akimtizama Carlos kwa jicho kali aliufungua na mlango na kuufunga kwa hasira.

Kilio kilizidi kwa Zuleya na ilimbidi aongozane na Carlos mpaka chumbani kwake, walipoingia Carlos alimkalisha kitandani Zuleya ambaye kwa muda huo alikuwa akilia kilio cha kwikwi.

“Samahani kwa kukuingilia kwenye maisha yako Zuleya”

Zuleya kilio cha kwikwi kilikatika ghafla na akawa anamtizama Carlos kwa maswali

“Kwanini?”

“Yule mwanaume ni mpenzi wako?”

“He is not, alikuwa na ni muda mrefu umepita sasa leo amekuja from no where and by the way mwanangu hajamkubali kabisa”

“Lakini anaonekana anakupenda sana Sumaya sio shida kwani si unafanya kitu ambacho moyo wako unapenda”

“Carlos hujui chochote kumuhusu Dajuan, ni mwanaume wangu wa kwanza kuwa naye tokea nije hapa Jamaica nilimpenda ila most of the time he used to bullying me, aaah alikuwa akinipiga yaani aah he used my money for his own interest…….” Na hapo kilio kilianza tena kwa Zuleya

“Basi inatosha Zuleya usilie sasa upo na mimi” Alimkumbatia Zuleya na kuanza kumbembeleza taratibu huku akimfuta machozi.

Zuleya alitulia kwenye kifua cha Carlos huku akisikilizia mapigo ya moyo ya Carlos yakienda mbio sana.

Aliinua uso wake na kumtizama Carlos kisha alimkumbatia vizuri, Carlos naye alizielewa hisia za Zuleya japo na yeye hakuwa akitegemea kwa wakati huo aliushusha mkono wake mpaka kwenye kiuno cha Zuleya na kuanza kukitomasa taratibu Zuleya alishituka na kumtizama Carlos usoni aliusogeza mdomo na kumpiga busu la haja lililoamsha hisia nyingi za Zuleya kwani ni kipindi kirefu sana aliikosa huduma hiyo, waliendelea kupeana busu na mwishoni walizama penzini.

**********

*********

*******

Nyumbani kwa Mrs Costanzo Anitha akiwa na Alvin pamoja na Halima jikoni muda huo Nicole hakuwa amerudi kutoka shuleni, Alvin alionekana mchangamfu sana kuliko siku zote na Anitha ndiye aliyekuwa akiongoza maongezi hayo kwa kiasi kikubwa.


“Kuja hapa ni bahati kubwa sana” Aliongea Anitha akichambua mchele

“Kwanini?”

“Alvin nyie hamuwezi kujua yaani maisha yenu ni mazuri tokea mnazaliwa”

“Ila kweli Anitha umeongea kitu cha ukweli” Alichangia Halima ambaye alikuwa akihangaika kukaanga nyama

“Mimi hii sio sehemu ya kwanza kufanya kazi, kuna sehemu nilifanya kazi yaani huyo bosi hata kuwagusa watoto wake hataki wala salamu kwanza kula mnakaa jikoni hakuna kusogea mezani wakati wao wanakula mnaitwa tu wakimaliza mkatoe vyombo vichafu”

“Mhh uliwezaje kuishi hapo Anitha?” Aliuliza Alvin

“Mwanzoni nilivumilia kwani nilikuwa bado sijazoea sana ila baadae nilizoeana na mlinzi na muda mwingine tunapanga dili natoka nje, nilimpata huyo mmama aliniambia kuna sehemu wana tafuta mtu nikatoroka”

“We Anitha Kumbe jasiri hivyo? Mimi sina huo ujasiri na hii ndio sehemu ya kwanza Kufanya kazi”

“Una bahati madam hapa hana shida na watoto wake hawana shida, kwanza hata sikuamini kama nitakuja sehemu kama hii”

Waliendelea kupiga stori mpaka Alvin alipotoka na kuingia chumbani kwake baada ya simu yake kuita na mama yake ndiye aliyekuwa akimpigia huku akimtaka achukue gari na amfuate sehemu.

Alijiandaa kisha alielekea sehemu ya parking ambapo kulikuwa na jumla ya magari matatu alichagua gari moja Toyota Crown kwani ndio gari alilolipenda nyumbani hapo, mlinzi alimfungulia geti kisha akaliondoa gari.

“Yes mom nimeshatoka nyumbani”

“Okay si unapakumbuka Leyla fashion wear?”

“Hapana mama”

“Hebu acha utoto Alvin umesahau nguo zile za sherehe tulinunua wapi?”

“Aah nakuja mama”

Aliongeza spidi na kuingia barabara kuu ndani ya dakika arobaini tu alikuwa ameshafika posta kwenye duka la mwanadada maarufu sana jijini Dar es salaam kwa kuuza nguo mbalimbali na pia alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa Mrs Costanzo, alielekea eneo la parking na aliliona gari la mama yake ambalo analipenda sana kulitumia aliingia ndani na kumkuta mama yake akipiga stori na mwanamke mnene wa wastani mwenye rangi nyeusi ya kung’aa aliyevalia vazi lake kama mlimbwende.

“Leyla huyu ndiye mwanangu wa kwanza yule niliyemfanyia tafrija wiki iliyopita”

“Aah Alvin karibu Ile siku mlipofika sikuwa nchini hongera sana mwanangu hapa ndio dukani kwangu ukisikia Leyla Fashion ndio hapa”

“Asante aunt” Alijibu kifupi sana kwani hakuwa ni mtu wa stori sana na pia aliangalia na aina ya mtu mwenyewe hakuwa na stori na kina mama wala kuwachangamkia tofauti na mdogo wake na kingine alikuwa ni mwanaume hivyo ilikuwa vigumu kwa upande wake.

“Sasa fanya hivi nyoosha mbele hapo halafu kata kushoto utaona pameandikwa MEN FASHION WEAR kaanze kuchagua nadhani wewe sio mgeni hapa tena Alvin”

“Sawa aunt Leyla”

Alielekea alipoelekezwa na kuwaacha hapo wakiendelea na stori zao kwani hata hivyo ni muda mrefu umepita hawajaonana.

Mrs Costanzo alimfuata mwanaye alipo na kumkuta akiwa yupo bize na simu.

“Alvin umesahau ulichoambiwa?”

“Mama kuna haja gani ya kununua nguo nyingi Mbona nyumbani zipo nitaenda kununua huko huko”

“Sikia Alvin wewe shida yako nini kwanza hela si natoa mimi chagua chache hapo sawa nyingine utanunua huko, nataka niwanunulie na hao waliobaki na wewe ndio utarudi nazo ila hakikisha hauzitoi mpaka nitakaporudi”

“Ina maana haturudi wote nyumbani muda huu?”

“Kwani umesahau kama Nicole hajarudi haya nenda wewe umfuate mimi nirudi”

Alvin hakumjibu chochote mama yake zaidi ya kuishia kumuangalia tu kisha akaanza kuchagua nguo zake.

Walimaliza kuchagua nguo na Kufanya malipo yote ndipo Leyla alitoa raba nzuri za kiume na kumpa Alvin kama zawadi, Alvin alishukuru na kutoka ndani na ile mizigo aliipakia kwenye siti za nyuma ya gari kisha aliliondoa gari hapo.

“Mmh shoga yangu una mtoto handsome”

“Nawe aaah”

“Kweli nina binti nyumbani atamfaa Alvin haha”

“Nani…….. Zulfa?

“Eeh si unajua mimi nimebarikiwa kupata warembo tu sina dume, kwanza nimekumbuka Nisha vipi kuhusu Gedione?”

“Ndio hilo lililonibakiza hapa nishauri sijui nifanye nini kuhusu yule mwanaume”


Alipewa ushauri na rafiki yake ndipo alipoondoka na kumfuata Nicole shuleni kwani muda ulibaki mchache tu waruhusiwe kutoka shuleni hapo lakini ujumbe uliingia kwenye simu yake alijitahidi ausome kwa muda huo kwani alidhani bila shaka huo ujumbe utakuwa wa muhimu.

“Meeting at RED INN” Alijikuta Akitabasamu kisha akaujibu ujumbe huo

“Keep watching.Good job”

Aliendelea kushikilia vema usukani wake huku akiwa na tabasamu mwanana usoni.
*

Katika ofisi ya Mrs Costanzo aliingia Mr Hernad baada ya kupewa ruhusa, aliketi kwenye moja ya viti vya kifahari vilivyopo ofisini humo kisha ikafuatia na salamu muda wote macho ya Mrs Costanzo hayakukatika kwa Mr Hernad.

“Hatimaye leo umefika Gedione!!!”

“Na sina muda mrefu wa kukaa hapa sikutaka kukufanya ujisikie vibaya siku zote hizi ulikuwa ukinitaka tuonane na sikuweza kuja”

“Hilo kwangu halina shida kikubwa tu umefika nimekuona”

“Sitarajii Kama utaupoteza muda wangu Nisha”

“Come on Ged…. Unadhani nilikuwa nakuita ili nikupotezee muda?…… well….”

Alisimama alipoketi kwenye kiti chake na kusogea mpaka sehemu yenye meza kubwa kisha akachezea kompyuta iliyopo mezani na kuzima camera aliyokuwa ofisini kwake halafu alienda mlangoni aliufunga mlango vizuri na kumfuata Mr Hernad ambaye alikuwa amesimama baada ya mlango kufungwa.

“Kwanini umefu…….” Kabla Mr Hernad hajamalizia sentensi yake Mrs Costanzo alimziba mdomo

“Nahitaji privacy……. Ni mimi na wewe tu Gedione”

“Nisha huoni kama hii ni ofisi…..”

“Lakini ni ofisi yangu Ged huwezi kunipangia” Alianza kufungua vifungo vya shati alilokuwa amelivaa na alilivua kisha akaliweka juu ya meza huku akibaki na sidiria pekee, Mr Hernad alishindwa kuelewa afanye nini na tayari Nisha alishaanza kuvua nguo zake.

Nisha aliujua vizuri udhaifu wa Mr Hernad kwake hivyo hakuwa na wasiwasi alijua tu ni lazima aingie kwenye mtego, alivua nguo zote na kubakiwa na nguo za ndani pekee kisha alimsogelea zaidi Mr Hernad na kumkumbatia.

“Najua Ged kitu ambacho huwezi kunidanganya hujawahi kumpata mwanamke kama mimi na nina udhaifu wako mkubwa Gedione na una hitaji hiki kitu kutoka kwangu”

Mr Hernad alikosa cha kujibu zaidi ya kumtizama tu Mrs Costanzo na muda huo tayari koti lake lilishawekwa pembeni na vifungo vya shati lake vikifunguliwa alikuwa kama mtu asiye jielewa hakuweza kumkatalia Nisha kwani ni mwanamke aliyekuwa ndiye udhaifu wake na alikuwa akijua ni nini Mr Hernad alikitaka.

Walisogea mpaka lilipo sofa kubwa la ofisi huku miili yao ikichemka hasa Nisha ambaye alikuwa akimhitaji zaidi Mr Hernad, walijitupa kwenye sofa na mechi ilianza kuchezwa kikamilifu.

*************
***********
********
******

“Nisha kilichotokea leo naomba kisijirudie tena tafadhali nina mke najisikia vibaya juu ya hili nililofanya”

Nisha hakujibu chochote alimtizama tu Mr Hernad ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka baada ya kuoga kwenye bafu iliyo ndani ya ofisi ya Mrs Costanzo

“Kingine nisije kusikia kuhusu hizi habari tena”

“Gedione I’m not an idiot…. Ningetaka kufanya hivyo ningefanya maana humu ndani kuna camera lakini niliizima, unajisikia vibaya juu ya hili ni kwamba umemsaliti mkeo sio kwani mimi hukuwahi kunisaliti Kwahiyo leo ndio mara yako ya kwanza Kufanya usaliti?”

“Sijamaanisha hivyo Nisha…”

“Ila umemaanisha nini?”

Nisha aliinuka kutoka kwenye kiti alichokaa na kumsogelea Mr Hernad kisha akamkumbatia kwa mahaba

“Umenipa furaha ambayo niliikosa kwa muda mrefu natamani usiondoke Gedione ubaki tu na mimi siku nzima”

“Nisha hata mimi nina majukumu yangu wacha niende”

Kabla hajaondoka Nisha alimpiga busu kama kumuaga ndipo akamuachia aondoke, alikuwa ni mwenye furaha sana kwa upande wake hakuona tatizo lolote japo alijua kuwa Mr Hernad alikuwa na familia yake.
*

“Sijafurahishwa kabisa huo ni uzembe wa hali ya juu kabisa naona mnataka kurudia yale ya nyuma ya Sumaya kumbukeni hili jambo ni la hatari na linahitaji umakini”

“Tumekuelewa Boss ila madam ndio mtu pekee tunaye mtegemea kutoa muongozo”

“Victor kuweni makini hili jambo haliwezi kuisha hapa tumelipambania kwa muda mrefu sana kiasi cha kutoa uhai wa mtu na Hata kama ikitokea kunahitajika kufanya hivyo tutafanya tena”

“Sawa mkuu”

“Ongea na Abdul na Bakari mpange mipango mizuri kuhusu jambo hili” Alitoa simu yake na kutafuta jina kisha akapiga na ilisikika sauti ya kike.


“Hallo mkuu..”

“Naona umeanza kulala sio mapenzi yamekunogea kipindi hiki unasahau kazi yako”

“Hapana hili jambo sio dogo lina hitaji umakini”

“Sawa ila kumbuka kutorudia makosa kama yale ya Sumaya”

“Hamna shida mkuu”

Simu ilikatwa na mwanaume yule aliiweka mfukoni kisha akatoka ndani na kuingia kwenye gari lake muda huo ilikuwa ni saa moja na nusu na giza lilikuwa limeshatawala kwenye anga la jiji hili, safari yake ilimfikisha kwenye kumbi moja ya starehe maeneo ya Mwenge na hiyo ndio alikuwa kumbi yake aliyoizoea kwani alipoingia tu alilakiwa na wanawake wengi walioonesha kumfahamu vyema mtu huyo alichagua sehemu na kuketi huku pembeni yake wakiwa wanawake wawili.

Aliagiza kinywaji chake alichokipenda siku zote Red wine na kuanza kunywa taratibu akiwa bado amezungukwa na wanawake hao, watu walikuwa wakitoka na kuingia huku wengine wakiwa bize kunywa na kucheza.

Alipomaliza kunywa kinywaji chake na wale wanawake alilipia kisha akachagua mwanamke mmoja ambaye aliongozana naye mpaka kwenye mlango mwingine tofauti na ule wakuingilia na kulikuwa na walinzi pia ambao walimfahamu vyema mtu huyo walimpisha na alitokea sehemu ya mapokezi alilipia gharama ya chumba kwa usiku mmoja kisha alipewa funguo na kuondoka na yule mwanamke, ilikuwa ni kawaida yake kwa bwana huyo kununua wanawake wawili au mmoja kila alipoenda hapo na hapo alionekana akiingia kwenye chumba na mwanamke huyo.



Asubuhi Mrs Costanzo akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi zake ujumbe uliingia kwenye simu yake kwa haraka aliifungua ili aone ni ujumbe gani, alionekana kutabasamu baada ya kuona ujumbe huo na haikufahamika ni ujumbe gani aliiweka pembeni simu yake na kuendelea na kazi.

Punde aliingia Sekretari wake na kumpatia faili kisha akamkumbusha juu ya kikao cha wazabuni kilichotakiwa kufanyika siku hiyo na tayari wahusika walishaanza kuwasili kwaajili ya kikao hiko na baada ya Sekretari kuondoka Mrs Costanzo alianza kuandaa nyaraka muhimu ili aende kuonana na wazabuni hao.
Wafanyakazi wa ngazi za juu na chini walikusanyika kwenye ukumbi maalumu wa mikutano ya ofisi na mambo mengine yaliyohusisha ofisi kwa ujumla.


Ilikuwa ni siku ambayo Lukas alihitajika kwaajili ya safari yake ya kwenda nchini Marekani na Kisha kuingia Mexico haikujulikana kama anakwenda kwaajili ya masomo au Vipi mambo hayo yote aliyajua mjomba wake Mr Ludovick na watu wake kwani wao ndio wapangaji wa hiyo safari.

Mr Ludovick hakuwa na muda wa kumpeleka Lukas uwanja wa ndege kutokana na ubize wa kazi hivyo alimuagiza tu dereva amfikishe Lukas na muda huo Sumaya na mama yake walikuwa njiani kuelekea huko kwaajili ya kumuaga Lukas, Sumaya hakuonekana na furaha kabisa aliwaza ndio kwanza ameanza kuyafurahia mapenzi yake na Lukas na kipindi hiko hiko Lukas anaondoka japo hakuwa akienda mbali sana lakini aliumia kupita maelezo.

Waliwasili katika uwanja wa ndege wa Kingston na kuwasiliana na Lukas ambaye kwa muda huo alikuwa akimsubiri Sumaya.

Kwa mbali Sumaya alimuona Lukas amesimama, alimkimbilia na kumkumbatia kwa huzuni huku machozi yakimtoka.

“Usilie Sumaya siendi nchi ya mbali kusema kuwa hatutaonana na Hata kama ningeenda mbali tungeonana tu”

“Lukas wewe huumii kama mimi ninavyoumia kuwa mbali na wewe”

“Sio kama siumii Sumaya ila mimi ni mwanaume lazima nijikaze ninaumia sana tu, unajua huu ni muda ambao tulianza kulifurahia penzi letu”

“Nashindwa kujizuia kulia Lukas inauma”

“Usilie kipenzi”

Zuleya naye alikuwa akisogea hapo huku akiwatizama kwa huzuni kubwa.

“Lukas uwe na safari njema baba ila usisahau kuwa kuna mtu umemuacha huku”

“Sawa mama sitasahau namheshimu sana Sumaya hata na wewe mama siwezi kufanya hivyo”

“Sawa Sumaya Usilie mwanangu utaumwa hiyo ni safari tu atarudi”

Haukupita muda Lukas aliondoka na kuelekea kwenye ndege kwaajili ya safari huku nyuma Sumaya hakuacha kumtizama mpaka anapotea kwenye macho yake, aligeuka na kuambatana na mama yake kurudi nyumbani.



ITAENDELEA……….
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom