bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
IMEANDIKWA NA : ATUGANILE
MWAKALILE
*********************************
*********************************
***************
Simulizi : Sitasahau Tanga
Sehemu Ya Kwanza (1)
Nikiwa kwenye mishe zangu za
research kwenye mji wa Tanga,
ilikuwa ni research ya siku kumi
na nne. Jioni ya siku ya pili
nikakatisha sehemu flani hivi
mjini hapo kuangalia na
kutembea tembea, lahaula
nikakutana na binti mmoja wa
kuvutia sana kwakweli nikajikuta
nikivutiwa naye alikuwa mweupe
sana na nywele ndefu na umbo
kama la mamiss hivi dah nikaona
hapa ndio penyewe yani kwani
alikuwa na ugonjwa wangu
mkubwa unaonivutia kwa
wadada nao ni rangi nyeupe.
Sikutaka kupoteza wakati mtoto
wa kiume ikanibidi nimsogelee ili
niweze kumsabahi, tukasalimiana
pale na kujuana majina na
tukabadilishana namba. Basi
ikawa kila jioni nakutana na yule
binti, pesa yote namalizia kwake.
Kwakweli nikampenda kwani
alikuwa ni binti mzuri sana kama
malaika aliyeshushwa hata demu
wangu niliyemwacha Dar
nikamsahau kabisa kwani
hakuwa na mvuto kama huyu
dada wa kitanga.
Baada Ya kumaliza ile research ya
siku kumi na nne sikutamani
kurudi Dar ila ilinibidi nirudi ili
nikakabidhi kazi ya watu na
nikasake mavumba ya ziada ya
kunifaa kumchumbia yule binti
wa kitanga.
Niliporudi Dar sasa ndio nilielewa
ule wimbo wa "Tanga kunani
pale".
Siku hiyo nikiwa kwenye chumba
changu nimetoka kuoga mara
simu ikaita kuichek ni yule binti
wa kitanga.
MIMI: Hallow mpenzi
BINTI: Ndio mpenzi, mbona
hujajisugua vizuri umeacha povu
sikioni?
MIMI: (Nikachukua kidole na
kugusa sikioni kukitoa kikatoka
na povu), haa umejuaje mpenzi?
BINTI: Nimekuona hapo mpenzi
wangu.
MIMI: (Nikiangalia kushoto na
kulia), umenionaje?
BINTI: Usijari mpenzi, chukulia
kawaida tu.
Baada ya simu kukatika, Dah
nilikaa nikawaza na kuwazua
nikaamua kupotezea tu. Nikavaa
fastafasta, halafu nikaenda
kununua msosi nikachukua na
kilimanjaro moja nikashushia ili
nilale vizuri. Mara simu ikaita,
BINTI: Mpenzi si nilikukataza
wewe kunywa pombe?
MIMI: (Nikiwaza kichwani,
majanga haya) mbona mi
sijanywa pombe!
BINTI: Nimekuona mpenzi
umekunywa bia moja.
MIMI: (Nikashtuka na kuangalia
kushoto na kulia), aaah sijui eeeh
kwani umejuaje?
BINTI: Fanya yote ila tambua
hakuna utalofanya nisijue.
Halafu akakata simu, nikaanza
kuwaza tena amejuaje kama
nimekunywa? Au kasikia harufu
ya pombe kwenye simu. Mara
sms ikaingia kwenye simu yangu,
kuangalia ni yule binti, sms
iliandikwa "usiwaze sana mpenzi"
Nikiwa chumbani nimejiinamia
mara demu wangu wa Dar
akanipigia simu na kuniambia
kuwa nimempotezea siku hizi
kwani tangu nimerudi sijaonana
nae, sikutaka kuongea mengi ila
nikamwambia asijari nitaonana
nae tu. Wakati najiandaa kulala
binti wa Kitanga naye akanipigia,
BINTI: Mpenzi ulikuwa unaongea
na nani kwenye simu?
MIMI: Ni rafiki yangu wa kawaida
tu mpenzi.
BINTI: Niambie ukweli tafadhari.
MIMI: Huo ndio ukweli mpenzi.
BINTI: Sawa ila nitakachofanya
usinilaumu badae.
MIMI: Jamani mpenzi unataka
kufanya nini tena?
BINTI: Si nilikukataza kuongea na
wanawake wewe, na kwanini
unanidanganya?
MIMI: Aaah samahani mpenzi,
sitarudia.
Akakata simu, nikawaza sana bila
ya kupata jibu nikaamua kulala
tu.
Asubuhi nikashtushwa na simu
yake,http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
BINTI: Mbona hukushusha
chandarua usiku?
MIMI: Umejuaje mpenzi?
Nilisahau bhana.
BINTI: Usijari mpenzi.
Basi nikaamka na kwenda zangu
kuoga, nikarudi na kuvaa ili
nijiandae kwenda kwenye mishe
zangu. Mara simu ikaita.
BINTI: Mpenzi hiyo tisheti
uliyovaa siipendi.
MIMI: (Nikiangalia ile tishirt
yangu), umejuaje kama nimevaa
tishirt usiyoipenda?
BINTI: Nimejua tu mpenzi,
unajua mi nakupenda kwahiyo
mambo mengi unayofanya
yanakuja kwangu kwa hisia.
MIMI: Asante kwa upendo wako
mpenzi basi nitaibadili usijari.
Nikakata simu na kwenda
kwenye mishe zangu. Ila
nikawaza sana kama yale mambo
ni upendo kweli au kuna vitu vya
ziada katikati hapa, nikaamua
kupotezea na kufanya mambo
mengine.
Nikarudi home nikiwa
nimejichokea hata nikaona uvivu
kwenda kutafuta msosi.
Nilipofika nikajilaza kitandani na
kujikuta nikipitiwa na usingizi
hapo hapo.
Nikaanza kuota nipo sehemu
nzuri sana na mchumba angu
huyo wa kitanga, tukienjoy na
kula raha tu.
Kulivyokucha nikaamka na
kwenda kuoga kama kawaida,
nakumbuka jana jioni nilikuwa
na elfu themanini kwenye wallet,
nikaichukua na kuicheki ile pesa
nakuta imebaki elfu thelathini
nikaanza kujiuliza elfu hamsini
imekwenda wapi. Mara yule binti
akawa anapiga simu,
BINTI: Mpenzi jana tulienjoy
eeh!!
MIMI: Aaaah, eeeh wapi tena?
BINTI: Si ndotoni mpenzi!!
MIMI: Kivipi mpenzi?
BINTI: Yani ndoto uliyoota wewe
usiku na mimi nimeota hivyo
hivyo.
Akakata simu bado nikawa
najiuliza juu ya upotevu wa pesa
yangu. Mara akanitumia sms
"usijari mpenzi, hiyo pesa
tumeitumia ndotoni"
Nikawaza sana juu ya upotevu wa
pesa yangu, nikajiuliza inakuwaje
mtu ufanye matumizi ya pesa
ndotoni? Likanijia wazo kuwa
yule binti si mtu wa kawaida.
Nikajishauri kwenda kupata
ushauri kwa rafiki yangu wa
karibu. Wakati natoka kwenye
chumba changu kuna sms
ikaingia kwenye simu yangu ila
nikaipotezea sikuisoma wala nini.
Nikaenda kwenye shughuli
zangu, badae nikaenda kwa
mshikaji wangu kumweleza kama
nilivyowaza. Nikamkuta na
tukapiga story mbili tatu badae
nikamweleza mambo yote.
MIMI: Ndio hivyo bhana.
RAFIKI: Aaah pole sana mshikaji
wangu ila nilikwambia kuwa
makini na Tanga, hata hivy
usipende kuwatongoza mademu
hovyohovyo sehemu yoyote ile.
MIMI: Sasa nishauri ndugu cha
kufanya.
RAFIKI: Cha msingi tumtafute
mtaalam twende, haya mambo ya
kishirikina kaka.
MIMI: Dah umenitisha kaka hata
kurudi kwangu naogopa.
RAFIKI: Usiogope wangu, wee
nenda tu ukiogopa atakushtukia
mapema.
MIMI: Dah sijui kama nitalala leo
kaka.
RAFIKI: Usijari kaka, cha msingi
potezea kama hujui kitu vile
halafu kesho twende kwa
mtaalam kaka.
MIMI: Poa kaka nashukuru
maana nishapagawa hapa.
Tukaagana pale halafu nikarudi
kwangu.
Nikiwa chumbani nikachukua
simu yangu kuikaguakagua
nikakuta missed call kibao na
sms moja nikashangaa hata
ilikuwaje sikusikia wakati inaita,
kumchek aliyekuwa anapiga ni
demu wangu wa Dar na ile sms
ni kutoka kwa binti wa kitanga,
iliandikwa "usijaribu kumweleza
yoyote juu ya habari zangu"
nikashtuka sana, ni hii sms
niliyoipotezea wakati naondoka
asubuhi. Mara simu ikaanza
kuita, kuangalia ni dada yangu
anapiga
MIMI: Hallow dada,http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
DADA: Mbona umekuwa na akili
fupi sana wewe? Unajua matatizo
aliyoyapata mchumba ako huku?
MIMI: Kwani kafanyeje tena
dada?
DADA: Muda wote amekupigia
simu hupokei, mwenzio yupo hoi
huku ule ujauzito umetoka.
MIMI: (Hata nilisahau kama
demu wangu wa Dar alikuwa na
mimba yangu) nini dada mbona
sikuelewi?
DADA: Huwezi kunielewa kwa
simu, kama unaweza njoo
hospitali au njoo nyumbani.
MIMI: Poa dada ngoja nijiandae.
Nikakata simu, nikaenda kuoga
na kuvaa fastafasta niondoke,
wakati nataka kutoka simu yangu
ikaanza kuita, kuitoa na
kuiangalia ni yule binti wa
kitanga.
BINTI: Unataka kwenda wapi?
MIMI: Aaah hapana siendi
popote.
BINTI: (Akacheka kidogo),
unataka kwenda wapi?
MIMI: Eeeh aaah nataka kwenda
kutafuta chakula.
BINTI: Haya rudi kakae, chakula
nitakuletea leo.
MIMI: (Huku nikiwa na hofu
moyoni), utaniletea kivipi?
BINTI: Kwani shida yako ni
chakula au ni nini? Kama ni
chakula sasa mashaka ya nini si
nimekwambia nitakuletea au?
MIMI: (nikaamua kujigeresha
kidogo), aaah Acha utani bhana
mpenzi wangu, unajua wazi upo
mbali sasa chakula utakiletaje?
BINTI: Nitakileta kwa hisia na
utashiba kabisa kwahiyo usitoke.
Akakata simu, nikaanza kuwaza
itakuwaje sasa na vipi kuhusu
kwenda hospitali nikawaza cha
kufanya, au niende halafu akipiga
nimwambie sijaenda? Bado
nikawa na utata moyoni.
Nikainuka pale nilipokaa na
kujipa moyo kuwa naenda tu hata
iweje. Nikaenda mpaka mlangoni
ile nataka kufungua mlango tu
sms ikaingia kwenye simu yangu,
kuangalia ni demu wa kitanga
"nimekwambia usitoke"
http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikakosa raha kabisa, nikarudi na
kukaa kitandani nikaamua
kujilaza nikitafakari, mara sms
ikaingia kwenye simu yangu
kuangalia ni yule binti wa
kitanga "angalia mezani
nimekuletea chakula"
Loh nikainuka kama nimepigwa
shoti vile, kuangalia naona juisi
ya Azam mango na biskuti,
nikawaza kuwa ameletaje vitu
vile nikaanza kupata mashaka,
mara sms nyingine ikaingia
"usiogope mpenzi, kula tu"
Nilikosa amani kwakweli,
nikasogelea ile juisi na kuiangalia
kama ni juisi kweli ndio ilikuwa
Azam mango kabisa na ndio juisi
niipendayo, mmh nikaziangalia
na zile biskuti zilikuwa biskuti za
ukweli kabisa zile zenye
mchanganyiko wa chokleti,
kutokana na njaa yangu nikaanza
kuvifakamia huku bado niliwaza
ameletajeletaje.
Nilipomaliza tu, akapiga simu.
BINTI: Vipi mpenzi umeshiba?
MIMI: Ndio nimeshiba, kwani
umeviletaje?
BINTI: Hata kushukuru hujui?
MIMI: Samahani mpenzi
nilijisahau.
Akakata simu, nikakaa na
mawazo pale kitandani. Mara
simu ikaita kuangalia ni dada
anapiga tena.
DADA: Vipi wewe yani huna hata
hofu na mwenzio?
MIMI: Aaah dada samahani.
DADA: Kwahiyo unakuja au huji?
MIMI: Aaah sijui dada.
DADA: Hujui nini? Nipe jibu
moja, unakuja au huji?
MIMI: Sitaweza kuja kwa leo
dada, nitakuja kesho.
DADA: Nilijua tu, mxyuuuu
(akanisonya na kukata simu).
Nikawa pale kitandani
nimejiinamia tu huku kichwani
mawazo mengi yamenitawala,
mara sms ikaingia kwenye simu
yangu
"si ulale mpenzi wangu jamani"
Nikaamua kujilaza huku nikijiona
bonge la boya maana nipo kama
vile mtu anayeongozwa na
rimote.
Mara usingizi ukanipitia pale
kitandani, nililala hadi
nikajisahau nikaja kushtushwa na
mlio wa simu.
RAFIKI: Vipi kaka mbona leo
hujatokea maeneo?
MIMI: Kivipi ndugu wakati ndo
kumekucha!
RAFIKI: (huku akinicheka),
kumekucha wakati saa kumi na
moja jioni hii?
MIMI: (nikafungua pazia na
kuchungulia dirishani, kumbe
kijua cha jioni ndio kipo
ukingoni), acha masikhara bhana
saa mbili hii (huku nikiangalia
saa yangu ya ukutani).
RAFIKI: (Akinicheka tena), wee
boya saa kumi na moja hii labda
kama leo una kazi ya ulinzi ndio
mida ya kujiandaa hii (akinicheka
tena).
MIMI: (Nikiangalia vizuri ile saa
ya ukutani, iliyoonyesha mshale
mdogo kwenye tano na mkubwa
kwenye nane), daah
nilichanganya mida kaka.
Nikakata simu na kuanza kuwaza
imekuwaje nimelala hadi
kujisahau vile, ni usingizi wa
namna gani ulinipata dah!! Mara
rafiki yangu akaanza kupiga tena.
RAFIKI: Kaka, vipi ule mpango
wa kwenda kwa mtaalam au
umepotezea?
MIMI: Hapana sijapotezea kaka,
nataka sana unipeleke itakuwaje
sasa?
RAFIKI: Wewe tu, nilitaka
nikupeleke leo au unaona yale
majanga yako ya kawaida kaka?
Kabla sijamjibu simu ikakatika,
na kuanza kuita tena kuangalia ni
binti wa kitanga.
BINTI: Ulikuwa unaongea na
nani?
MIMI: Rafiki tu mpenzi
wangu.http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
BINTI: Ulikuwa unaongea nae
kuhusu nini?
MIMI: Hamna kitu ni salamu tu.
BINTI: Unanificha sio?
MIMI: Hapana sijakuficha huo
ndio ukweli.
BINTI: Wee ni muongo eeh!! Haya
njia ya muongo fupi na mi naijua.
Akakata simu, nikabaki kwenye
maswali na viulizo vya kila aina.
Kwanza nikawaza juu ya usingizi
niliolala hadi kusahau kuamka
kwenda popote pia kusahau kula.
Nikajiuliza inamaana sijala
chochote tangu nilipokula juisi na
biskuti usiku. Mara sms ikaingia,
"usijari mpenzi kula na kuoga na
vyote vya muhimu umefanya
ndotoni"
Aaah majanga haya!!
ITAENDELEA
MWAKALILE
*********************************
*********************************
***************
Simulizi : Sitasahau Tanga
Sehemu Ya Kwanza (1)
Nikiwa kwenye mishe zangu za
research kwenye mji wa Tanga,
ilikuwa ni research ya siku kumi
na nne. Jioni ya siku ya pili
nikakatisha sehemu flani hivi
mjini hapo kuangalia na
kutembea tembea, lahaula
nikakutana na binti mmoja wa
kuvutia sana kwakweli nikajikuta
nikivutiwa naye alikuwa mweupe
sana na nywele ndefu na umbo
kama la mamiss hivi dah nikaona
hapa ndio penyewe yani kwani
alikuwa na ugonjwa wangu
mkubwa unaonivutia kwa
wadada nao ni rangi nyeupe.
Sikutaka kupoteza wakati mtoto
wa kiume ikanibidi nimsogelee ili
niweze kumsabahi, tukasalimiana
pale na kujuana majina na
tukabadilishana namba. Basi
ikawa kila jioni nakutana na yule
binti, pesa yote namalizia kwake.
Kwakweli nikampenda kwani
alikuwa ni binti mzuri sana kama
malaika aliyeshushwa hata demu
wangu niliyemwacha Dar
nikamsahau kabisa kwani
hakuwa na mvuto kama huyu
dada wa kitanga.
Baada Ya kumaliza ile research ya
siku kumi na nne sikutamani
kurudi Dar ila ilinibidi nirudi ili
nikakabidhi kazi ya watu na
nikasake mavumba ya ziada ya
kunifaa kumchumbia yule binti
wa kitanga.
Niliporudi Dar sasa ndio nilielewa
ule wimbo wa "Tanga kunani
pale".
Siku hiyo nikiwa kwenye chumba
changu nimetoka kuoga mara
simu ikaita kuichek ni yule binti
wa kitanga.
MIMI: Hallow mpenzi
BINTI: Ndio mpenzi, mbona
hujajisugua vizuri umeacha povu
sikioni?
MIMI: (Nikachukua kidole na
kugusa sikioni kukitoa kikatoka
na povu), haa umejuaje mpenzi?
BINTI: Nimekuona hapo mpenzi
wangu.
MIMI: (Nikiangalia kushoto na
kulia), umenionaje?
BINTI: Usijari mpenzi, chukulia
kawaida tu.
Baada ya simu kukatika, Dah
nilikaa nikawaza na kuwazua
nikaamua kupotezea tu. Nikavaa
fastafasta, halafu nikaenda
kununua msosi nikachukua na
kilimanjaro moja nikashushia ili
nilale vizuri. Mara simu ikaita,
BINTI: Mpenzi si nilikukataza
wewe kunywa pombe?
MIMI: (Nikiwaza kichwani,
majanga haya) mbona mi
sijanywa pombe!
BINTI: Nimekuona mpenzi
umekunywa bia moja.
MIMI: (Nikashtuka na kuangalia
kushoto na kulia), aaah sijui eeeh
kwani umejuaje?
BINTI: Fanya yote ila tambua
hakuna utalofanya nisijue.
Halafu akakata simu, nikaanza
kuwaza tena amejuaje kama
nimekunywa? Au kasikia harufu
ya pombe kwenye simu. Mara
sms ikaingia kwenye simu yangu,
kuangalia ni yule binti, sms
iliandikwa "usiwaze sana mpenzi"
Nikiwa chumbani nimejiinamia
mara demu wangu wa Dar
akanipigia simu na kuniambia
kuwa nimempotezea siku hizi
kwani tangu nimerudi sijaonana
nae, sikutaka kuongea mengi ila
nikamwambia asijari nitaonana
nae tu. Wakati najiandaa kulala
binti wa Kitanga naye akanipigia,
BINTI: Mpenzi ulikuwa unaongea
na nani kwenye simu?
MIMI: Ni rafiki yangu wa kawaida
tu mpenzi.
BINTI: Niambie ukweli tafadhari.
MIMI: Huo ndio ukweli mpenzi.
BINTI: Sawa ila nitakachofanya
usinilaumu badae.
MIMI: Jamani mpenzi unataka
kufanya nini tena?
BINTI: Si nilikukataza kuongea na
wanawake wewe, na kwanini
unanidanganya?
MIMI: Aaah samahani mpenzi,
sitarudia.
Akakata simu, nikawaza sana bila
ya kupata jibu nikaamua kulala
tu.
Asubuhi nikashtushwa na simu
yake,http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
BINTI: Mbona hukushusha
chandarua usiku?
MIMI: Umejuaje mpenzi?
Nilisahau bhana.
BINTI: Usijari mpenzi.
Basi nikaamka na kwenda zangu
kuoga, nikarudi na kuvaa ili
nijiandae kwenda kwenye mishe
zangu. Mara simu ikaita.
BINTI: Mpenzi hiyo tisheti
uliyovaa siipendi.
MIMI: (Nikiangalia ile tishirt
yangu), umejuaje kama nimevaa
tishirt usiyoipenda?
BINTI: Nimejua tu mpenzi,
unajua mi nakupenda kwahiyo
mambo mengi unayofanya
yanakuja kwangu kwa hisia.
MIMI: Asante kwa upendo wako
mpenzi basi nitaibadili usijari.
Nikakata simu na kwenda
kwenye mishe zangu. Ila
nikawaza sana kama yale mambo
ni upendo kweli au kuna vitu vya
ziada katikati hapa, nikaamua
kupotezea na kufanya mambo
mengine.
Nikarudi home nikiwa
nimejichokea hata nikaona uvivu
kwenda kutafuta msosi.
Nilipofika nikajilaza kitandani na
kujikuta nikipitiwa na usingizi
hapo hapo.
Nikaanza kuota nipo sehemu
nzuri sana na mchumba angu
huyo wa kitanga, tukienjoy na
kula raha tu.
Kulivyokucha nikaamka na
kwenda kuoga kama kawaida,
nakumbuka jana jioni nilikuwa
na elfu themanini kwenye wallet,
nikaichukua na kuicheki ile pesa
nakuta imebaki elfu thelathini
nikaanza kujiuliza elfu hamsini
imekwenda wapi. Mara yule binti
akawa anapiga simu,
BINTI: Mpenzi jana tulienjoy
eeh!!
MIMI: Aaaah, eeeh wapi tena?
BINTI: Si ndotoni mpenzi!!
MIMI: Kivipi mpenzi?
BINTI: Yani ndoto uliyoota wewe
usiku na mimi nimeota hivyo
hivyo.
Akakata simu bado nikawa
najiuliza juu ya upotevu wa pesa
yangu. Mara akanitumia sms
"usijari mpenzi, hiyo pesa
tumeitumia ndotoni"
Nikawaza sana juu ya upotevu wa
pesa yangu, nikajiuliza inakuwaje
mtu ufanye matumizi ya pesa
ndotoni? Likanijia wazo kuwa
yule binti si mtu wa kawaida.
Nikajishauri kwenda kupata
ushauri kwa rafiki yangu wa
karibu. Wakati natoka kwenye
chumba changu kuna sms
ikaingia kwenye simu yangu ila
nikaipotezea sikuisoma wala nini.
Nikaenda kwenye shughuli
zangu, badae nikaenda kwa
mshikaji wangu kumweleza kama
nilivyowaza. Nikamkuta na
tukapiga story mbili tatu badae
nikamweleza mambo yote.
MIMI: Ndio hivyo bhana.
RAFIKI: Aaah pole sana mshikaji
wangu ila nilikwambia kuwa
makini na Tanga, hata hivy
usipende kuwatongoza mademu
hovyohovyo sehemu yoyote ile.
MIMI: Sasa nishauri ndugu cha
kufanya.
RAFIKI: Cha msingi tumtafute
mtaalam twende, haya mambo ya
kishirikina kaka.
MIMI: Dah umenitisha kaka hata
kurudi kwangu naogopa.
RAFIKI: Usiogope wangu, wee
nenda tu ukiogopa atakushtukia
mapema.
MIMI: Dah sijui kama nitalala leo
kaka.
RAFIKI: Usijari kaka, cha msingi
potezea kama hujui kitu vile
halafu kesho twende kwa
mtaalam kaka.
MIMI: Poa kaka nashukuru
maana nishapagawa hapa.
Tukaagana pale halafu nikarudi
kwangu.
Nikiwa chumbani nikachukua
simu yangu kuikaguakagua
nikakuta missed call kibao na
sms moja nikashangaa hata
ilikuwaje sikusikia wakati inaita,
kumchek aliyekuwa anapiga ni
demu wangu wa Dar na ile sms
ni kutoka kwa binti wa kitanga,
iliandikwa "usijaribu kumweleza
yoyote juu ya habari zangu"
nikashtuka sana, ni hii sms
niliyoipotezea wakati naondoka
asubuhi. Mara simu ikaanza
kuita, kuangalia ni dada yangu
anapiga
MIMI: Hallow dada,http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
DADA: Mbona umekuwa na akili
fupi sana wewe? Unajua matatizo
aliyoyapata mchumba ako huku?
MIMI: Kwani kafanyeje tena
dada?
DADA: Muda wote amekupigia
simu hupokei, mwenzio yupo hoi
huku ule ujauzito umetoka.
MIMI: (Hata nilisahau kama
demu wangu wa Dar alikuwa na
mimba yangu) nini dada mbona
sikuelewi?
DADA: Huwezi kunielewa kwa
simu, kama unaweza njoo
hospitali au njoo nyumbani.
MIMI: Poa dada ngoja nijiandae.
Nikakata simu, nikaenda kuoga
na kuvaa fastafasta niondoke,
wakati nataka kutoka simu yangu
ikaanza kuita, kuitoa na
kuiangalia ni yule binti wa
kitanga.
BINTI: Unataka kwenda wapi?
MIMI: Aaah hapana siendi
popote.
BINTI: (Akacheka kidogo),
unataka kwenda wapi?
MIMI: Eeeh aaah nataka kwenda
kutafuta chakula.
BINTI: Haya rudi kakae, chakula
nitakuletea leo.
MIMI: (Huku nikiwa na hofu
moyoni), utaniletea kivipi?
BINTI: Kwani shida yako ni
chakula au ni nini? Kama ni
chakula sasa mashaka ya nini si
nimekwambia nitakuletea au?
MIMI: (nikaamua kujigeresha
kidogo), aaah Acha utani bhana
mpenzi wangu, unajua wazi upo
mbali sasa chakula utakiletaje?
BINTI: Nitakileta kwa hisia na
utashiba kabisa kwahiyo usitoke.
Akakata simu, nikaanza kuwaza
itakuwaje sasa na vipi kuhusu
kwenda hospitali nikawaza cha
kufanya, au niende halafu akipiga
nimwambie sijaenda? Bado
nikawa na utata moyoni.
Nikainuka pale nilipokaa na
kujipa moyo kuwa naenda tu hata
iweje. Nikaenda mpaka mlangoni
ile nataka kufungua mlango tu
sms ikaingia kwenye simu yangu,
kuangalia ni demu wa kitanga
"nimekwambia usitoke"
http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikakosa raha kabisa, nikarudi na
kukaa kitandani nikaamua
kujilaza nikitafakari, mara sms
ikaingia kwenye simu yangu
kuangalia ni yule binti wa
kitanga "angalia mezani
nimekuletea chakula"
Loh nikainuka kama nimepigwa
shoti vile, kuangalia naona juisi
ya Azam mango na biskuti,
nikawaza kuwa ameletaje vitu
vile nikaanza kupata mashaka,
mara sms nyingine ikaingia
"usiogope mpenzi, kula tu"
Nilikosa amani kwakweli,
nikasogelea ile juisi na kuiangalia
kama ni juisi kweli ndio ilikuwa
Azam mango kabisa na ndio juisi
niipendayo, mmh nikaziangalia
na zile biskuti zilikuwa biskuti za
ukweli kabisa zile zenye
mchanganyiko wa chokleti,
kutokana na njaa yangu nikaanza
kuvifakamia huku bado niliwaza
ameletajeletaje.
Nilipomaliza tu, akapiga simu.
BINTI: Vipi mpenzi umeshiba?
MIMI: Ndio nimeshiba, kwani
umeviletaje?
BINTI: Hata kushukuru hujui?
MIMI: Samahani mpenzi
nilijisahau.
Akakata simu, nikakaa na
mawazo pale kitandani. Mara
simu ikaita kuangalia ni dada
anapiga tena.
DADA: Vipi wewe yani huna hata
hofu na mwenzio?
MIMI: Aaah dada samahani.
DADA: Kwahiyo unakuja au huji?
MIMI: Aaah sijui dada.
DADA: Hujui nini? Nipe jibu
moja, unakuja au huji?
MIMI: Sitaweza kuja kwa leo
dada, nitakuja kesho.
DADA: Nilijua tu, mxyuuuu
(akanisonya na kukata simu).
Nikawa pale kitandani
nimejiinamia tu huku kichwani
mawazo mengi yamenitawala,
mara sms ikaingia kwenye simu
yangu
"si ulale mpenzi wangu jamani"
Nikaamua kujilaza huku nikijiona
bonge la boya maana nipo kama
vile mtu anayeongozwa na
rimote.
Mara usingizi ukanipitia pale
kitandani, nililala hadi
nikajisahau nikaja kushtushwa na
mlio wa simu.
RAFIKI: Vipi kaka mbona leo
hujatokea maeneo?
MIMI: Kivipi ndugu wakati ndo
kumekucha!
RAFIKI: (huku akinicheka),
kumekucha wakati saa kumi na
moja jioni hii?
MIMI: (nikafungua pazia na
kuchungulia dirishani, kumbe
kijua cha jioni ndio kipo
ukingoni), acha masikhara bhana
saa mbili hii (huku nikiangalia
saa yangu ya ukutani).
RAFIKI: (Akinicheka tena), wee
boya saa kumi na moja hii labda
kama leo una kazi ya ulinzi ndio
mida ya kujiandaa hii (akinicheka
tena).
MIMI: (Nikiangalia vizuri ile saa
ya ukutani, iliyoonyesha mshale
mdogo kwenye tano na mkubwa
kwenye nane), daah
nilichanganya mida kaka.
Nikakata simu na kuanza kuwaza
imekuwaje nimelala hadi
kujisahau vile, ni usingizi wa
namna gani ulinipata dah!! Mara
rafiki yangu akaanza kupiga tena.
RAFIKI: Kaka, vipi ule mpango
wa kwenda kwa mtaalam au
umepotezea?
MIMI: Hapana sijapotezea kaka,
nataka sana unipeleke itakuwaje
sasa?
RAFIKI: Wewe tu, nilitaka
nikupeleke leo au unaona yale
majanga yako ya kawaida kaka?
Kabla sijamjibu simu ikakatika,
na kuanza kuita tena kuangalia ni
binti wa kitanga.
BINTI: Ulikuwa unaongea na
nani?
MIMI: Rafiki tu mpenzi
wangu.http://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
BINTI: Ulikuwa unaongea nae
kuhusu nini?
MIMI: Hamna kitu ni salamu tu.
BINTI: Unanificha sio?
MIMI: Hapana sijakuficha huo
ndio ukweli.
BINTI: Wee ni muongo eeh!! Haya
njia ya muongo fupi na mi naijua.
Akakata simu, nikabaki kwenye
maswali na viulizo vya kila aina.
Kwanza nikawaza juu ya usingizi
niliolala hadi kusahau kuamka
kwenda popote pia kusahau kula.
Nikajiuliza inamaana sijala
chochote tangu nilipokula juisi na
biskuti usiku. Mara sms ikaingia,
"usijari mpenzi kula na kuoga na
vyote vya muhimu umefanya
ndotoni"
Aaah majanga haya!!
ITAENDELEA