Simulizi: Sehemu isiyo na jina

Simulizi: Sehemu isiyo na jina

ILIPOISHIA.
"pole sana Fiona, naamini unaangaika sana huko
uliko"
Nilijikuta nasema maana maneno aliyokuwa Fiona
anauasema kwangu, viapo vile vya nguvu, hasa
aliponambia kuwa Mimi ni sawa na pumzi
aliyokuwa anaivuta. Kiukweli niliumia sana sana.
SONGA NAYO.
"Unayajua Mapenzi?
Nilimuuliza Sofia.
"Sitaki hata niyajue Jumanne maana kwa jinsi nilivyo
haswa ni mtihani sana kwetu kujihusisha na
mapenzi"
"Sawa"
Nilisema kisha nikatulia.
"Kwanini umeniuliza Hivyo Jumanne?"
"Kwasababu sina hakika kabisa na kile ambacho
umekifanya kama ni sahihi, ni bora ungemuua kuliko
kumwacha anaishi maana naamini ndio umemtesa
kabisa zaidi ya mateso yaani anaweza hata kufa
kabisa"
Nilisema.
"Jumanne kweli unacho kizungumza?"
"Sahihi kabisa, Mimi ndiye namjua Fiona, Nimekaa
naye sana"
Nilisema tena.
"Naomba usitoke humu; nitarudi muda si mrefu"
Sofia alisema. Kisha akapotea pale pale.
Nilibaki mule ndani peke yangu, nilikuwa najiamini
sana kwasababu nilikuwa nimewazoea, kawaida
yangu nilikuwa nikibaki ndani ya majumba Yale
peke yangu, nilikuwa napenda kuagiza karanga
mbichi kwa ajili ya kutafuna, maana wale viumbe
walikuwa si wa mchezo katika swala zima la
kujamiana. Nilihofia pia Sofia naye anaweza
akageuka nae akataka tufanye mapenzi. Niliendelea
kukaa kumsubili Sofia arudi huku nikitafuna karanga
zangu. Haikupita Robo saa Sofia akawa amerudi.
Alionekana mwenye hasira sana.
Alinifuata akanizoa kwenye kiti nilichokuwa nimekaa
na kunitupa nikajipigiza kwenye ukuta na kutua
Chini.
Sofia alianza kubadilika macho yakawa meusi kama
ya joka.
"Tafadhali Sofia naomba usiniue!"
Nilisema hivyo. Muda huo tayari nilikuwa nishajua
kabisa ni wakati wangu wa kufa.
"Jumanne! Napenda nikuue lakini ngoja nikuache
kwanza nione nini kitaendelea........ila hupaswi tena
kuwa Mfalme katika Koo ile kwasababu Mdogo
wangu kaisha Athirika kabisa"
Sofia alisema. Muda huo machozi yalikuwa
yanamtoka hata hasira zilimpungua.
"Alinilazimisha yeye kufanya Mapenzi"
Nilisema, kulikuwa hakuna namna ya kujitetea zaidi
ya kuzungumza hivyo.
"Simama uje ukae hapa tuzungumze vizuri"
Sofia alisema.
Nilisimama nikasogea aliponiambia niende kukaa.
Nilifika nikakaa kwenye kiti Jirani na alipokuwa
amesimama tayari hali yake ilikuwa amerudi katika
usawa.
"Jumanne naomba unifundishe mapenzi, nataka
namimi nijue jinsi hayo mapenzi yalivyo, ili
nihakikishe kama kweli hali niliyomkuta nayo Fiona
niyakweli!"
Sofia alisema. Kauli yake Mimi ilinishitua sana.
"Sofia hupaswi kufanya mapenzi maana ni hatari,
utamuua mdogo wako ukifanya mapenzi na Mimi?"
Nilisema. Lengo langu ili kuilinda heshima na
huruma iliyokuwepo baina ya Sofia na Fiona, viumbe
ambao walikuwa ni Mtu na mdogo wake.
"Utaki?"
Sofia alisema kwa ukari huku akiniangalia Usoni.
Niliogopa nikajua ndio mwisho wangu wa kuishi
endapo nitagoma kufanya naye.
"Sawa nitafanya lakini naomba tukimaliza kufanya
mapenzi unisaidie kurudi nilikotoka!"
Nilisema hivyo makusudi maana nilijua kabisa
nikisha Fanya mapenzi na Sofia naye lazima
anogewe kwahio ambacho kingefuata huko ni
uwadui na kuuana.
"Kama ni hivyo naomba unifundishe jinsi ya kufanya
mapenzi"
Sofia alisema tena. Nilisimama nikamwambia
aondoe vazi lake. Bila kusita naye alifanya hivyo
hivyo, kisha nikamwambia ajilaze kwenye kiti
ambacho kilikuwa kama kochi la futi tatu, naye
akafanya hivyo hivyo, alikuwa aogopi kabisa.
Alipojilaza Mimi nilimsogelea kisha nikaanza
kumchezea ili kumwandaa. Nilimshika shika
kiufasaha kabisa nikamuona akaanza kuguna
miguno ya kafara, sauti zao za mahaba ndizo
zilikuwa zinanitisha Mimi, Sauti zile zilikuwa si za
kawaida kabisa nazani hazikuwa hata za Binadamu
maana kila alipokuwa anazidi kulia kwa madeko
ndio nami nilizidi kupandisha mizuka.
Nilimtoa nyoka pangoni kisha nikamzamisha
shimoni, shimo ambalo nyoka mwenyewe alikuwa
anaenda kulifungulia kwa mala ya kwanza ili
kurekebisha kipimo kabisa. Nilimpa Sofia kile
ambacho alikuwa anakitaka. Baada ya kumaliza
yeye mwenyewe alipoa kisha nikamwambia tukaoge
kwanza halafu mambo mengine yaendelee. Kweli
naye alitii na kwenda kuoga,.... nilioga naye
tukamaliza tukarudi ndani. Sielewi wale viumbe
wakoje, hata dakika kumi hazikuisha Sofia alitoka
na kukimbia mbio kuelekea sehemu ambayo alijua
yeye.
Kama ilivyokuwa kwa Fiona ndivyo hivyo hivyo kwa
Sofia. Wakati huu sikushituka kabisa kwasababu
nilikuwa nishawaozea jinsi walivyo. Afadhali hata
kwa Sofia yeye aliwahi kurudi. Yeye alirudi nyakati
za saa moja hivi. Hata kurudi kwake kulikuwa
tofauti na Fiona huyu alikuwa kawaida.
"Naomba unisamehe Jumanne mpenzi wangu"
Sofia alisema. Hapo tu ndipo Mimi walikuwa
wananiuzi, tayari Sofia naye ailianza kuniita mpenzi,
jambo ambalo Mimi nilikuwa silitaki.
"Mapenzi ni mazuri Sana kuna raha sana. Kwahio
kesho tutarudia"
Vile vile kama alivyosema mdogo wake.
"Hapana Sophia kesho hatutakiwi kufanya tena,
tukifanya unakuwa kama Fiona"
Nilisema. Nilivyosema hivyo akapoa.
"Jumanne kwahio unataka nikurudishe kwa Fiona.
"Hapana, naomba unisaidie kutoka katika inchi hii
nirudi nyumbani"
"Ni kweli Jumanne maana kwa Jinsi nilivyomuona
mdogo wangu, sina hakika kama wewe unaweza
kuwa mfalme maana watagundua tu kuwa
alijihusisha kimapenzi iwe isiwe, ni bora Mimi
ambaye sijaathirika sana nibaki niwe naenda
kumliwaza"
Sofia alisema. Hapo kidogo alinipa matumaini ya
kurudi nyumbani habari za Ufalme watajua wao.
"Utanisaidia Sofia kutoka huku?"
Niliuliza.
"Usijali nitafanya kila mbinu kesho nikuondoe,
hakuna anaye Jua kuwa wewe uko na Mimi ila
wanajua uko kwa Fiona. Na hata siku ikitokea
wanakuhitaji ukawe mfalme nitamwambia Fiona
awadanganye kuwa ulimtoroka yeye akiwa vitani na
haikujulikana ulienda wapi"
Sofia alisema.
"Hilo litakuwa wazo zuri lakini ningeomba msisubiri
wao wajue bora umwambie Fiona ndiye aende
akariport kabla ili iwe rahisi kwao kumtafuta mtu
mwingine"
Nilisema, hapo niliongezea ushauri.
"Hilo ni wazo zuri Jumanne"
Sofia alisema.
"Haya, Sofia hawatojua kuwa Mimi nimerudi katika
ulimwengu wangu?"
Nilimuuliza.
"Hawatokufuatilia hata usijali"
Sofia alinijibu jawabu zuri ambalo lilinipa matumaini
zaidi. Tuliongea mengi sana siku hio nikampa
ushauri kuusu mapenzi yalivyo endapo akizama
sana na kuyazoea. Kiujumla aliupenda ushari wangu
akaridhika nao sana.
Usiku sikulala naye kama nilivyo lala na Fiona siku
ya kwanza, nililala kwenye godoro zuri tu halafu
chumba kingine tofauti na alichoingia yeye, maisha
ya pale yalikuwa tofauti kidogo na ya nyumbani kwa
Fiona. Kweli asubuhi mapema kabisa kama
tulivyokuwa tumepanga Sofia aliniamsha na
kunichukua kisha akanambia nifumbe macho kama
ilivyokuwa Imepangwa, kweli nilijikuta ndani ya poli
inje kidogo ya ziwa Ngozi.
"Jumanne naomba uondoke ila nitalikumbuka sana
penzi lako umenitamanisha kuendelea kufanya
mapenzi, siku moja usishangae naweza hata
kutoroka na kuja huku kwa ajili yako, nitajua jinsi ya
kukupata. Nimeamua kukutoa kule kwasababu ya
kuilinda heshima yangu na Mdogo wangu. Nenda!"
Sofia alisema. Kisha akapotea huwezi amini muda
ambao Sofia alitoweka sauti ya Fiona alisikika
Masikioni mwangu akiniita huku akisema.
"Jumanne umeamua kuniacha nife?"
Sauti hiyo ilinishitua sana. Lakini nilishindwa kuijibu
ikanibidi nitafute namna ya kurudi nyumbani.
Niliianza safari ya kulikatiza pori lile ambalo
limelizunguka Ziwa Ngozi kuelekea nyumbani. Kwa
bahati nzuri nilikutana na watu wakiwa mashambani
huko nikawaomba msaada wa kurudi nyumbani.
Sauti ya Fiona iliendelea kunisindikiza lakini
sikuthubutu kuijibu. Jioni kabisa ndio nilifika
nyumbani lakini njiani huko nilikuwa nishakumbana
visanga kibao kutoka kwa watu, kila mmoja alikuwa
akidai kwamba, nilishafariki na kuzikwa. Kauli hizo
sikuzijali kwasababu nilikuwa najua watu
watanikimbia na kunisema hivyo, ni kweli watu
walinikimbia wengine wakawa wananifuata ili
kuhakiki kama kweli au ni mzimu wangu.
Hata nilipofika nyumbani Mama alizimia, ndugu
zangu wengine walikimbia.
Nilijitahidi sana kuwashawishi mpaka kuamini,
niliwasimulia mengi niliyokutana nayo kipindi niko
huko. Walipokuja kuamini ni pale nilipowasimulia
Habari za kuzaliwa kwangu ndipo waliamini kabisa
kuwa Mimi nilichukuliwa na mizimu ya ziwa Ngozi.
Hicho ndicho kisa cha maisha yangu. Sijatunga Bali
ni chakweli.
ILIPOISHIA.
Walipokuja kuamini ni pale nilipowasimulia Habari
za kuzaliwa kwangu ndipo waliamini kabisa kuwa
Mimi nilichukuliwa na mizimu ya ziwa Ngozi.
Hicho ndicho kisa cha maisha yangu. Sijatunga Bali
ni chakweli.
SONGA NAYO.
Baada ya kutoka katika maisha hayo Jumanne
aliishi kwa mawazo sana, ndugu zake walipokuwa
wanajaribu kumuuliza ni kitu gani ambacho alikuwa
anakiwaza yeye alikuwa akiwajibu kuwa; anawaza
kwasababu ya kuwaacha wasichana wawili Raulati
na Jamila katika mazingira Yale, jumanne alikuwa
akiwapenda sana Raulati na Jamila, mabinti ambao
walikuwa ni Mapacha. Ndugu zake walijitahidi sana
kumuweka sawa kwa kumshauli asahau habari za
Jamila na Raulati kwani wale walikuwa ni mabinti
Mapacha, ndugu wawili waliozaliwa pamoja kwahio
hata kama wangetoka naye, bado ingemlazimu
awaowe wote wawili jambo ambalo lingekuwa
gumu sana. Na hata kama angemchagua mmoja
angemchagua nani ambaye angekubali aolewe peke
yake na mwenzake abaki au nani angekubali abaki
halafu mwenzake aolewe. Kwahio ilikuwa ngumu
sana katika swala hilo. Baada yakupokea ushauri
mwingi ndipo walipomshauli asimulie Kisa cha
maisha yaliyomkuta huko. Kisa hicho ambacho
umemaliza kukisoma. Mwanzo ilikuwa ngumu sana
kwa Jumanne kukubali kukisimulia kisa hicho cha
ajabu katika maisha yake, alikuwa anadai kuwa kuna
vitu ambayo hakupaswa kabisa kuviweka bayana
kwasababu alipewa Onyo kubwa sana na kiumbe
aliyemsaidia kutoka kule kuwa endapo tu atathubutu
kuuzungumza baadhi ya vitu ambavyo alimkataza
basi angerudi katika maisha Yale Yale ya uko
alikokuwa. Kwa maana hiyo kutokana na kisa chake
Sofia alimkataza Jumanne asitamke baadhi ya vitu
ambavyo alikumbana navyo huko. Hapo hawali
Jumanne alisimulia kisa chake lakini baadhi ya
vipengere alikuwa avisemi kabisa, lakini kila
alipokuwa anazidi kukaa mawazo yalizidi kumtuma
auseme ukweli wa kila jambo ambalo alikutana nalo
huko, jambo zito sana ambalo alikatazwa ni kuusu
kufanya mapenzi na wale Binadamu wa Ajabu yaani
Sofia na mdogo wake Fiona, halafu jambo lingine
alikuwa amekatazwa ni kwamba hakupaswa kabisa
kuijibu sauti ya Fiona ambayo ilizidi kumfuata hata
pale alipofika nyumbani na kuishi, Sauti ile
ilimshinda Jumanne akajikuta anaijibu sauti ile
kuwa; amwache asimfuatilie. Siku ambayo Jumanne
alitamka hivyo alilia siku mzima kwasababu ya
maagano ambayo waliwekeana na Sofia. Maagano
hayo Jumanne aliyasema kwa ndugu zake kuwa
aliambiwa kuwa akithubutu kuusema ukweli ule na
kuijibu sauti ya Fiona lazima arudi kule na adhabu
yake ni kuishi kwa mateso mpaka pale Ambako
angefariki. Baada ya ndugu zake kujua hivyo
walijaribu kumtembeza Jumanne kwa waganga
mbali mbali ili waifunge mizimu isiendelee
kimfuatilia. lakini kila mganga alishindwa na
alikuwa anakumbana na vipigo vya kuumiza sana.
Baada ya kushindwa kwa waganga walimfanyia
maombi ya Dini wakaamini kabisa kuwa hatopata
matatizo tena, toka hapo jumanne hakusikia wala
kupata dalili zozote kuusu mizimu kumwandama.
Miezi miwili tangu kuombewa ndipo alipoanza
kuongea kwa uhuru katika vyombo vya Habari Vitu
ambavyo alikutana navyo huko alikokuwa. Mwisho
alishauliwa kukitoa kitabu ili kibaki kama
kumbukumbu kwa wasikilizaji na watanzania wote
wajue kuusu swala la Mizimu. Ushauri huo Jumanne
aliufanyia kazi ndipo alikaa chini na kuiandika
hadithi yake kamili. kitu cha pekee alichokiacha ni
kuusu Sauti ya Fiona aliyoijibu, baadaye kitabu
chake kiliingia sokoni watu wakakiona na kukisoma.
Ingawa kilikuwa na page chache lakini kilivutia sana
kwa wasomaji.
Kwakuwa alikuwa ni Mwanafunzi katika Chuo kikuu
cha Sayansi cha mbeya Jumanne alianza kufanya
taratibu za kurudi chuo kwa ajili ya kuendelea na
masomo yake. Siku moja kabla ya kwenda chuo,
kulipokucha Jumanne hakuwepo ndani, ndugu zake
walitafuta sana sana lakini hawakufanikiwa kumpata,
baaye waliamini Jumanne alirudi tena alikokuwa
kwa maana hiyo alichukuliwa tena na mizimu ya
ziwa Ngozi, baada ya kujua hivyo walienda kufanya
tambiko katika mizimu yao lakini hawakufanikiwa
ndipo walipoamua kumsahau Jumanne kwa namna
hiyo.
Mwisho wa hadithi hii ya kuvutia.
Imetungwa na Hemed Mayugu.
Kama ikitokea Jumanne akirudi msimu wa Pili wa
Hadithi hii utakuijia hapa hapa, nazani atatwambia
vingi vingi vya mambo ambayo yanaendelea
kumkuta. Tumuombee na Tuombe Jumanne apate
kurudi ili Hadithi yetu nzuri iendelee. Asanteni sana
kwa Ushirikiano wenu katika kuifuatilia Hadithi hii ya
kusisimua.

-MWISHO-

Simulizi nzuri sana... Inahuzunisha pia...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Sehemu ya (05),
WhatsApp 0755577488.
ILIPOISHIA.
Sisi hatukuamini kabisa kama ni kweli maana hata
kumbukumbu ya ndoto ilianza kujirudia vichwani
mwetu.
Tulianza kujadiliana sisi kwa sisi kuwa hatutaudhulia
katika mchezo huo, tena tulipanga hata siku hiyo ya
Ijumaa tusiende shule kwasababu tuliogopa
tuliamini kabisa kuwa ndoto ile huwenda ikatimia
kwasababu hatukuwahi kuota ndoto ya
kufanana..........
SONGA NAYO.
Basi tuliendelea kukaa mpaka siku hiyo ya Ijumaa,
lakini cha kushangaza tulipata hamasa ya kwenda
shule, na tulisoma vizuri kabisa. ulipofika wakati wa
kwenda msikitini hatukwenda kabisa, hatukwenda
msikitini, na hiyo ndiyo ilikuwa mala yetu ya kwanza
kutoenda msikitini siku ya Ijumaa. Kilichokuwa
vichwani mwetu tulikuwa tunawaza muda wa
michezo ufike twenda kushangilia, ndani ya muda
mfupi tulijikuta tunasahau kabisa ndoto ambayo
tuliiota wiki iliyopita siku ya alhamisi.
Hatimaye wakati wa michezo ulifika siku hiyo ya
ijumaa, wanafunzi wote tulikusanyika kwenye uwanja
wa michezo. Saa nane na nusu mpila ulianza
kuchezwa lakini mpila ulipoanza tu hivi mapigo yetu
ya moyo yakaenda mbio, wasiwasi ukazidi
kututawala, tukajishauri tuondoke, maana sasa
tunakoelekea ni kutukuta kilichotukuta kwenye
ndoto. Bado tukiwa tunaangalina na kushauliana
mala wanafunzi wa upande wetu walishangilia, kwa
maana hiyo timu yetu ya shule ilikuwa ishapata gori.
Aaaa! Nasi tukajiunga kushangalia tukasahau kabisa
kuwa lazima ile ndoto ilikuwa na maana yake, basi
tulipomaliza kushangalia tulitulia mpila ukaendelea
lakini dakika mbili tu, kilitokea kimbuka kama kile
kile cha kwenye ndoto, hapo sasa ndipo tulishikwa
Bumbuwazi.
"Tuondoke haraka lazima ni lazima"
Tulijikuta tunasema, lakini tulipogeuka nyuma
ulizuka tena upepo mkari kutokea nyuma yetu,
upepo huo ulichanganyikana na vumbi zito,
tukageuka tena upande wa uwanjani napo hatukuona
kitu vumbi ndilo lilikuwa limeisha tawala sehemu
yote. Hatukua na ujanja tulijisemea tu ngoja litimie
ambalo lilikuwa linakusudiwa kwenye ile ndoto.
Lakini sasa hali ile hatukuweza kuivumilia, tulianza
kukimbia hovyo huku tumeshikana mikono, harafu
sasa cha ajabu tulikuwa hatugongani na Mwanafunzi
yeyote, ilikuwa kama tupo njiani peke yetu.
Tulikimbilia tusikokujua ghafra tuliona pango Dogo
kwenye lile vumbi tukatamani kuingia humo kungoja
upepo utulie ndiyo tuchukue hatua nyingine.
Tukiwa mule ndani ya pango hilo dogo tulisikia
kelele nyingi azieleweki watu si watu mbwa si
mbwa tena Kama vile zinatufuata. Tuliamua kutoka
tukimbie lakini atukuweza. Badala yake lile pango
lilikua kubwa, pana halafu ndani ikawa Kama kuna
vitu vya kung'aa.
Tuliogopa sana ila atukujua tutokee wapi. Tukiwa
wenye hofu, ghafra walitokea watu wawili wazee;
Mwanamke na mwanamume wakatwambia
"Karibuni katika makao yenu mapya".
"Makao yetu mapya!? Tuliuliza Kwa mshangao sana,
swali letu halikujibiwa. Badala yake wale wazee
walipotea.
Baada ya wazee wale kupotea hatukujua ni nini
kiliendelea Bali nasi tulijikuta humu humu ndani ya
Jumba la A place with no name. Hatukuwahi kutoka
inje ya jumba hili na tunaishi kama kawaida, kama
ndiyo Dunia nyingine basi tushafika inatubidi
kukubali. kwanza toka tufike hapa hatukuwahi
kuuona mlango wa kutokea inje ya Jumba hili, lakini
Tunashukuru kwakuwa kila kitu tunapata"
Raulati alizungumza hivyo. Kisa chao kweli hata
Mimi kilinishangaza sana, lakini sikukiamini kabisa.
Nilijiuliza kirahisi tu hivyo, haiwezekani kimbunga
kivume harafu kiwapoteze watu kwa njia kama ya
kwao, japo kuwa kweli walianza kwa kuota ndoto
kama Mimi nilivoota ndoto, lakini ndoto yangu
ilikuwa kama ukweli kwasababu sikupewa nafasi ya
kuitafakari nikiwa nyumbani, Bali nilijikuta nimo
ndani ya Jengo lile la ajabu.
"Jumanne bado utuamini sisi?"
Jamila aliniuliza.
"Nawamini"
Niliwajibu kwa upole.
"Basi amka ukaoge na kupiga mswaki kama
uogopi"
Jamila alinambia tena, nilikuwa nashindwa hata
kusimama, lakini nilishangaa tu Raulati anasimama
na kunishika mkono huku akiniangalia usoni. Macho
yangu na yake yalikuwa yamepishana kama futi
moja tu, hakika yule Binti alikuwa Mzuri kabisa
alikuwa mzuri. Macho yangu yenyewe yalijikuta
yanamuogopa hata kumwangalia kwa Aibu.
"Twende ukaoge, siku tatu ujaoga tangu ufike hapa"
Raulati alisema.
Sikuwa na ujanja baada ya kushikwa na Binti yule
nilijikuta nasimama mwenyewe kisha wakaniongoza
njia ya kuelekea bafu lilipo.
Walinionesha halafu Mimi nikaingia bafuni kuoga,
kiunoni bado nilikuwa na tauro langu. Bafuni nilipo
ingia nilikuta bafu ni lingine kabisa tofauti na la
mwanzo. Palikuwa ni pasafi tu wala hakukuwa na
vitu kama nilivyovikuta mwanzo. Bafuni kulikuwa na
kila kitu kizuri unachokijua katika vyumba hivyo,
muonekano wake ulikuwa wa Kibillionare, kwakweli
mazingira ya mule yalipendeza sana, chumba kile
kilikuwa ni kikubwa tu na kilikuwa kimejitosheleza
kila kitu, kama ni maisha yalikuwa ni maisha
yanayoitajika kabisa, Bafu lile nashindwa hata
kulielezea labda kwasababu mazingira yangu
niliyokuwa nimeyazoea hayakukaribia kabisa.
Nilioga nikamaliza nikajifuta vizuri na taulo lingine
kabisa ambalo lilikuwa ndani ya Bafu lile
nimendaliwa, baada ya kumaliza nililivaa koti
ambalo Jamila alinipa kwa ajili ya kulivaa baada ya
kuoga. Taulo la gunia niliacha huko huko.
Nilitokea bafuni mule nikawakuta mabinti wale wote
wamesimama huku wakiniangalia kwa matamanio
kweli, Tabasamu ndilo lilikuwa limetawala ndani ya
nyuso zao.
"Tunakupenda Jumanne wetu"
Sauti nzuri ya mahaba iliwatoka mabinti wale. Kwa
Jinsi nilivyokuwa na mashaka Juu yao sikutaka
kabisa kuwajibu ila niliwaoneshea Tabasamu tu
basi.
"Chumba chako unakikumbuka?"
Jamila aliniuliza.
"Hapana"
"Kile pale nenda kila kitu kipo safi"
Nilioneshwa baada ya kukataa kuwa sikikumbuki.
Nilisogea kwenye Chumba nilichooneshwa,
nikaushika mlango na kuufungua, nilisitaajabu sana
baada ya kukuta chumba si kile cha hawali na
kilipendeza sana kile Chumba hakiamungu
nilipendezwa sana na maadhari ya Chumba kile,
nilijikuta natamani kuingia haraka. Lakini Kabla
sijaingia ndani niligeuka Nyuma na kuangalia kama
Raulati na Jamila wananiangalia, lakini sikuwaona
pale walipokuwa wamesimama, kidogo wasiwasi
ulianza kuniingia tena. Basi niliingia ndani ya
Chumba hicho, nilipoingia kabisa ndani nilikuta nguo
safi zimekunjwa vizuri ziko juu ya kitanda,
nilizichukua na kuzivaa. zilikuwa ni nguo za kawaida
tu lakini zilinipendeza sana.
Baada ya kumaliza kuvaa nguo zile nilishitukia
mlango unagongwa, Sauti ilikuwa ya wale Mabinti
ikiliita jina langu.
"Hawa wamejuaje kama nimeisha maliza kuvaa"
Nilijisemea mwenyewe, maana wale mabint Mimi
nilikuwa siwaamini kabisa, nilijua wale ni majini tu,
kwa mazingira yale kwakweli Mimi walinitisha sana,
Fikra zangu zoote ziliamini kuwa lazima watakuwa
ni majini tu, lazima. Kwasababu hata mazingira Yale
sikuyaona kama ni ya kawaida, halafu kipindi hicho
nilikuwa nishasoma hadithi nyingi kuusu maisha ya
majini kutoka kwa watunzi tofauti kama akina
Mavugo, Rais wa Iramba zilizokuwa zinahusu majini
majini, hadithi zote zilionesha kuwa maisha ya
majini huwa yapo vizuri na ya kifahari, uthamani wa
Vitu vyao huwa mala nyingi vya dhahabu tu. Kingine
kilichonitisha ni ndoto nilio iota, kwani ndoto ile
nilikuwa kwenye ziwa Ngozi, ziwa ambalo historia
yake huwa inaogopesha, kwahio moja kwa moja
mabinti wale Mimi sikuwaamini kabisa lazima
walikuwa ni majini. Hilo tu ndilo lilikuwa wazo langu
kuu Juu yao, hata kisa chao walichonisimulia
niliamini si cha kweli Bali cha kutunga tu kama
hadithi zingine ambazo nilikuwa nishazisoma.
Nilitoka Chumbani mule kwa unyonge sana.
"Jumanne mbona ujiamini wewe.........Ebu jiamini
basi utaishi je kwa mashaka muda wote huu,
mbona sisi tushazoea wala hatuwazi kiasi hicho"
Mabinti wale walisema. Kweli walijitahidi sana kwa
nguvu zao kunishawishi lakini kwangu walikuwa
hawana mafanikio kabisa.
Nilitoka nao tukarudi sehemu ya kukaa tukaendelea
kuongea mambo mengine. Nilijaribu hata
kuwadadisi walizaliwa mwaka gani wakanambia
kuwa wao walizaliwa mwaka 1990 inamaana kwa
muda huo walikuwa na umri wa miaka kumi na
saba tu, walikuwa ni mabinti wabichi hasa.
Tukiwa tushaongea mengi mwisho nilianza kuhisi
njaa, nilipoiangalia saa nilikuta ni kama saa nane na
nusu, basi nikajikuta nasema kuwa"Nahisi njaa"
Ndivyo nilivyosema tu hivyo wale Mabinti wote
walisimama na kunifuata kisha wakanisogelea na
kunishika kwa pamoja.
"Jumanne mpenzi wetu twende tukale"
"Mh!"
Niliguna tu, nilishindwa hata kuuliza maana sikujua
chakula hicho kiliandaliwa muda gani. Nami
nilinyanyuka nilipokuwa nimekaa nikaongozana nao.
Jumba lile lilikuwa limekamilia na Dyaning
ilikuwepo, huwezi amini nilipofika Dyning sikuamini
kabisa sijui walikuwa wanatembea na mawazo
yangu, nilikuta mezani kuna ugari na hotpot ya
nyama ya kuku tena alikuwa kuku mzima kabisaa
aliyekuwa kakatwakatwa vipandevipande kama
tulivyozoea, kabisa sikumbuki kama kulikuwa na
kipande kilichokuwa kimesalia katika yule mnyama
tena alikuwa Jogoo ambaye kwa kipimo alikuwa na
kilo zaidi ya tano.
"Jumanne utapasuka ukicheza na maisha ya huku,
yani huku ni television tu ndiyo hatuna, lakini vingine
vyote Burudani sana"
Wale mabinti walisema.
"Kwa maana hiyo hata Disko lipo?"
Nilijikuta nauliza swali hilo.
"Subili kama unalitaka wewe mwenyewe utafurahi tu,
lakini mpaka ukubali kuwa mpenzi wetu, ndiyo
vingine ivijue"
Nilijibiwa hivyo, Nilijikuta nacheka kwanza kwenye
ile meza ya chakula.
Tulizungumza vingi sana pindi tunakula, nao
walipata fursa ya kuniuliza jinsi nilivyifika pale, ni
nini kilinikuta Mpaka kufika pale? Bila kusita
niliwasimulia. Mchana wa siku hiyo uliisha kwa
kuongea tu na mabinti wale.
Baada ya stori zote za mchana hatimaye usiku
uliingia tukala tena chakula cha nguvu, wakati huu
tulikula wali na maharage pamoja na mboga za
majani. Baada ya zoezi la kula usiku kuisha,
niliagana na Mabinti wale nikaelekea chumbani
kwangu, nao pia wakaelekea Chumbani kwao.
Chumba cha mabinti wale sikujua kilikuwa upende
upi katika Jumba lile ambalo nilikuwa siijui hata
ramani yake.
Baada ya kuingia Chumbani nilikaa tu kitandani
huku nikuwaza. Nilijiuliza maswali mengi sana, vipi
nilifika pale, nilifanya kosa gani mpaka kufika pale?
Jumba hilo liko wapi Duniani hapa?"
Madirisha ya Jumba lile yalikuwa juu kabisa, yani
huwezo wa kulifikia ili kuchungulia inje ilikuwa si
rahisi kuyafikia na kuchungulia. Japokuwa ilikuwa ni
siku ya nne ndani ya Jumba lile, lakini niliona Kama
ndio siku ya kwanza kwangu, kwani siku tatu
nilizitumia kwenye usingizi mzito wa bila
kujitambua. niliwaza mengi sana, hata mabinti wale
nao nilianza kuwajaji mwenyewe, Yaani Jamila na
Raulati ambao walikuwa na mvuto wa ajabu, katika
kutafakari sana kuusu mabinti hawo, kidogo
niilijikuta nikifarijika moyoni. Nilijiona Kama vile
kwenye Jumba lile panaweza kuwa pahara sahihi
kabisa kwani nitaishi dunia ya peke yangu iliyojaa
furaha ya mapenzi kutoka Kwa mapacha wawili
wenye mvuto wa pekee. Mvuto wa wale watoto
wakike kwakweli sikuwahi kuona mwanamke wa
kuwafananisha nao toka kuzaliwa kwangu. Baada ya
kutafakari mambo mengi, sikujua usingizi ulinipitia
vipi ila nilishituka baada ya kusikia nagongewa
mlango. Tena mgongaji alikuwa akigonga kwa
nguvu sana.
"Nani anayegonga hivyo mlango wakati Mimi
nimelala"
Nilisema Kwa sauti ya uchovu.
"AMKA HARAKA HATUNA MUDA WA KUPOTEZA."
Ilisikiska sauti nzito ya mwanaume ikisema, sauti
hiyo ilitokea mlangoni, kwamaan hiyo kulikuwa na
Mwanaume ndiye kasimama mlangoni. Sauti hiyo
ilinifanya niogope na kujawa na wasiwasi mwingi.
"FANYA HARAKA TUONDOKE"
Bado nikiwa hata sijafikilia cha kufanya sauti ile
ilisikika tena ikisema. .........................
SaAfi
 
Story Kali sana nimeipenda. Lakini kuna kitu nataka kujua, hivi hii simulizi ni kazi ya kubuniwa au ni ya kweli? Maana daah!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom